content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
JESHI la Polisi Tanzania, Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), limewasilisha mifumo miwili ya teknolojia katika mkutano wa Mawaziri wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na limesema lipo tayari kuipeleka katika nchi zote za jumuiya hiyo zisizo na teknolojia hiyo. Mifumo hiyo iliyobuniwa na wataalamu wa Tehama wa jeshi hilo nchini, ni wa Usimamizi wa Makosa ya Usalama Barabarani na kupata Taarifa ya Upotevu ya Polisi kwa njia ya mtandao bila kulazimika kwenda kituo cha Polisi. Jeshi hilo, Kitengo cha Tehama, Makao Makuu, limeifikisha mifumo hiyo katika mkutano huo unaoendelea jijini Dar es Salaam, unaowahusu mawaziri wa sekta ya Tehama, Habari, Mawasiliano, Uchukuzi (Usafirishaji) na Hali ya Hewa kutoa elimu na kueleza utayari wao kuzisaidia nchi nyingine za SADC. Akizungumza na gazeti hili juzi katika eneo la mkutano huo; Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) walikoweka Banda lao la Jeshi la Polisi, Msimamizi wa Kitengo cha Tehama, makao makuu ya Polisi, Dar es Salaam, Gabriel Mukungu, alisema jeshi hilo lipo tayari kuifikisha mifumo hiyo katika nchi za jumuiya hiyo. “Tuko hapa kuoneshauwezo wa kiteknolojia wa Jeshi la Polisi. Mifumo hii miwili tuliyoileta hapa imebuniwa na vijana wa jeshi wenyewe, hatujanunua kutoka nje. Hatua hii imesaidia pia kupunguza gharama kwa Jeshi la Polisi na kwa wananchi,” alisema Mukungu. Akifafanua kuhusu mifu- mo hiyo, akianza na Mfumo wa Usimamizi wa Makosa ya Usalama Barabarani, Mukungu alisema miaka ya zamani wakosaji wa sheria za usalama barabarani wali- andikiwa faini kwa karatasi (vitabu vya notification) vilivyokuwa vinatengenezwa kwa gharama na kulazimika kusafirishwa mikoa yote kwa magari. Alisema baada ya kuanza kwa mfumo huo Aprili 2017 katika Mkoa wa Pwani na Julai kusambazwa nchi nzima, mabilioni ya Serikali yaliokuwa yakipokea sasa hakuna tena wizi huo kwa kuwa fedha zinapelekwa moja kwa moja serikalini na adhabu imeainisha kosa la dereva na mwenye gari tofuati na awali. “Sasa hivi mtu akikosa, ana nafasi ya kulipa faini ya kosa lake katika kipindi cha siku saba na kwa wanaokiuka utaratibu huo wanageuka kuwa wadaiwa sugu na hukamatwa kwa kamera maalum zinazowekwa barabarani na kuwabana kulipa faini hizo mara mbili ya faini ya awali (penalty),” alisema Mukungu. Kuhusu Taarifa ya Upotevu ya Polisi (Police Loss Report), Mukungu alisema umeanza Julai Mosi mwaka huu na unafanya kazi nchi nzima. Alisema mtu aliyepoteza kitu anaingia moja kwa moja kwenye mtandao wa intaneti kwa tovuti ya https://lormis.tpf. go.tz kusajili taarifa zake za upotevu. “Masharti hapa ni lazima mtu awe na kitambulisho cha taifa. Tumefanya hivi ili kuhimiza kila mwananchi apate kitambulisho hiki kuonesha umuhimu wake. Kwa hiyo kama umepo- telewa na nyaraka kama vyeti, laini ya simu na kadi za benki, hana ulazima wa kwenda Kituo cha Polisi, anaweza kuipata ‘loss re- port’ mtandaoni,” alisema. Akieleza zaidi, Mukungu alisema gharama ya kuipata ni Sh 500 kiasi ambacho watu wengi wanaweza kukipata kwa njia ya simu ya mkononi. Hata hivyo, alisema mtu hatopata taarifa ya upotevu kwa vitu kama kadi ya gari, gari lenyewe na vyombo vya moto, hati za nyumba, mashamba, kampuni, silaha, kifo na mtu kupotea kwa kuepuka hatari ya mwizi wa vitu husika, hawajaziweka mtandaoni kuepuka matumizi mabaya na watu kujihalalishia vitu hivyo. “Kwa aina hii ya upotevu, mtu atalazimika kwenda kituo cha polisi”. Alisema hivi sasa wanaunganisha mifumo hiyo na kampuni za simu ili kurahisisha taarifa kuwafikia kampuni hizo mara moja kama zinavyowafikia Polisi.
kitaifa
Na Malima Lubasha-Musoma MAHAKAMA Kuu Kanda ya Musoma, imewahukumu kunyongwa hadi kufa watu watatu kwa kosa la kumuua Tabu Makanya (58) kwa kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili. Waliohukumiwa kunyongwa hadi kufa ni Musiba Maregeba, Abeid Casimil na Ndaro Sumuni wote wakazi Kijiji cha Kwibara Kata ya Mugango Wilaya ya Musoma vijijini mkoani Mara, huku Wandwi Mugulu diwani wa Kata ya Mugango, akiachiwa huru. Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Girson Mdeme wa hiyo baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani na upande wa Jamuhuri.  Jaji Mdeme, alisema ametoa adhabu hiyo ya kunyongwa hadi kufa kwa washtakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi saba pamoja na vielelezo vilivyotolewa mahakamani na upande wa mashtaka.  Awali washtakiwa hao walihukumiwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza katika kesi namba 189/2013 ambayo hukumu yake ilitolewa Julai 14,2015. Jaji Mdeme alisema, wakati washtakiwa wakisubiri kunyongwa baada ya hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, walikata rufaa ambayo ilisikilizwa na na Mahakama Kuu Kanda ya Musoma  Agosti 16. Washtakiwa hao walikuwa wakituhumiwa kumuua Tabu Makanya (58) mkazi wa Kijiji cha Kwibara Kata Mugango, ambapo Februali 21 mwaka 2013 majira ya saa 5.00 usiku walivamia nyumba ya mwanamke huyo kwa kubomoa mlango kwa jiwe kubwa marufu fatuma. Ilidaiwa wakiwa na mapanga na tochi, baada ya kuingia ndani walitoa onyo kwa watoto wa Tabu na kuwata kukaa kimya bila kupiga kelele. Baada ya kuwatisha watoto, walimvamia mwanamke huyo kisha kumchinja na kutenganisha kichwa na kiwiliwili na kukiweka ndani ya mfuko wa sandarusi na kuondoka nacho.  Ilidaiwa wakati watuhumiwa hao wakiwa katika harakati za kutoka eneo la tukio, wananchi walifanikiwa kumkamata mtuhuniwa mmoja akiwa na kichwa hicho. Kuhusu diwani aliyekuwa amejumuishwa kwenye kesi hiyo, inadaiwa alikamata baada ya uchunguzi wa awali kuonesha kwamba yeye ndiye aliwatuma watu hao kumtafutia kichwa cha binadamu kwa makubaliano ya kuwapatia fedha.  Ilidaiwa kuwa, diwani huyo alitaka kichwa hicho ili kukitumia kishirikina kwenye masuala ya uvuvi wa samaki lakini baada ya jalada lake kupelekwa kwa Mwanasheria wa Serikali, aliondolewa kwenye kesi hiyo.
kitaifa
NA MWAMVITA MTANDA-KIGALI KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amefichua kuwa alifanya jitihada za kumshawishi aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Emmanuel Okwi ili asalie Msimbazi, lakini nyota huyo wa kimataifa wa Uganda aligoma katakata. Okwi mwenye umri wa miaka 27, ameachana na Simba, baada ya mkataba wake kumalizika msimu msimu uliopita wa Ligi Kuu Tanzania Bara, huku kukiwa na taarifa kuwa anakaribia kujiunga na Fujairah FC inayoshiriki Ligi Kuu ya Falme za Kiarabu (UAE). Mshambuliaji huyo, amekuwa na mchango mkubwa katika kikosi cha Simba, tangu alipojiunga nayo mwaka 2009, akitokea klabu ya SC Villa ya nyumbani kwako Uganda. Akiichezea Simba, Okwi amefanikiwa kutwaa mataji matatu ya Ligi Kuu Tanzania Bara huku pia akiiwezesha timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika katika mashindano yaliyopita. Katika fainali za mataifa ya Afrika(Afcon)zilizomalizika hivi karibuni na Algeria kutwaa ubingwa, Okwi aliisaidia Uganda kutinga hatua ya 16 bora, huku akifunga mabao mawili. Akizungumza na MTANZANIA kwa njia ya mtandao, Aussems alisema mshambuliaji huyo ambaye msimu uliopita wa Ligi Kuu alifunga mabao 14, ameacha pengo katika kikosi chake. “Nilizungumza na Okwi akiwa Misri na timu yake ya Taifa iliyokuwa inashiriki michuano ya mataifa ya Afrika(Afcon), nilimwambia bao nataka kufanya naye kazi. “Aliniambia anataka kubadilisha mazingira kwani amekaa sana Tanzania na ametumikia timu kubwa za Simba na Yanga hivyo anataka kumaliza muda wake wa soka nchi zingine,”alisema Mbelgiji huyo na kuongeza. “Pia niliongea na mabosi wa Simba wamuongeze dau maana nilifikiri labda tatizo lilikuwa fedha lakini bado hakuwa tayari.” Wakati huo huo, Aussem alizungumzia fununu za mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na klabu ya Difaa El Jadida ya Morocco, Simon Msuva kuwa yu mbioni kujiunga na Simba kwa kusema hakuwahi kuuomba uongozi wake umsajili, lakini akakiri ni mchezaji mzuri na anatamani kufanya naye kazi. “Namfahamu Msuva, ni mchezaji mzuri na ningependa kufanya naye kazi Simba,”alisema Aussems. Katika hatua nyingine, Klabu ya Simba imetangaza ratiba ya michezo minne ya kirafiki ya kikosi chake ambacho kwa sasa kimepiga nchini Afrika Kusini, kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika. Ratiba hiyo inaonyesha Julai 23, kikosi hicho kitashuka dimbani kujipima na Orbret TVET, Julai 24 itapepetana na Platinum Stars, Julai 27 kitavaana na Township Rollers na kukamilisha kwa mchezo dhidi ya miamba ya Afrika Kusini, timu ya Orlando Pires kwa kumenyana nayo Julai 30.
michezo
WASHINGTON, MAREKANI  WAGOMBEA urais wa chama cha Democrat nchini Marekani wamemlaumu Rais Donald Trump baada ya kutokea visa viwili vya mashambulizi ya bunduki vilivyosababisha vifo vya watu 29 Texas na Ohio. Wagombea hao wanasema matamshi ya Trump ya kibaguzi dhidi ya walio wachache nchini humo yanachochea mgawanyiko na machafuko. Katika mikutano ya umma na hata kwenye televisheni wagombea kadhaa wamezungumzia haja ya kuwepo kwa sheria kali za udhibiti wa bunduki.  Pamoja na hayo wanasiasa hao wameelekeza kiasi kikubwa cha lawama zao kwa Trump wakisema mashambulizi hayo ya Dayton na El Paso yana uhusiano na matamshi yake ambayo amekuwa akiyatoa kwa miezi sasa dhidi ya wahamiaji na watu watu wasio wazungu. Seneta Bernie Sanders amesema “Namwambia Rais Trump, tafadhali achana na matamshi ya kibaguzi dhidi ya wahamiaji, wachana na chuki inayoshuhudia nchi hii ikitumbukia katika machafuko tunayoyaona.” Rais Trump mwenyewe amelaani mashambulizi yote mawili.  “Ninachotaka kusema ni kwamba hizi ni sehemu mbili nzuri na tunawapenda watu wake. Chuki haina nafasi katika nchi yetu na tutalishughulikia suala hilo,” alisema Trump. Alipoulizwa kuhusiana na hatua atakazochukua baada ya tukio hilo la mauaji, Trump alisema; “Tumefanya mengi zaidi kuliko tawala zilizopita na jambo hilo halizungumziwi sana, lakini tumefanya mengi kusema kweli. Lakini labda mengi zaidi yanastahili kufanyika.” Watu 20 waliuwawa katika duka la jumla la Walmat mjini El Paso huko Texas na polisi wanasema kisa hicho kitachukuliwa kama ugaidi wa ndani ya nchi wakati ambapo wanachunguza madai ya shambulizi lililotokana na chuki.  Mshukiwa wa tukio hilo, Connor Betts e huenda akahukumiwa kifo iwapo atapatikana na hatia.  Polisi pia inasema haijui bunduki hiyo iliponunuliwa ingawa inasema pia kuwa sheria za Texas zinakubali kubeba bunduki kubwa katika sehemu ya umma. Wakati hayo yakijiri wanafunzi waliokuwa darasa moja na Connor Betts huko Ohio wanasema kuna wakati alifukuzwa shule baada ya kuandika orodha ya watu anaotaka kuwauwa na orodha nyingine ya wasichana anaonuia kuwabaka.
kimataifa
Na NORA DAMIAN, MWANAFUNZI Cynthia Mchechu, ambaye ameshika nafasi ya pili kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne uliofanyika Novemba mwaka jana, amesema Rais Mstaafu wa Marekani, Barack Obama, amechangia mafanikio yake. Cynthia aliyekuwa akisoma Shule ya Sekondari ya Wasichana ya St. Francis Mbeya, alisema ndoto yake ya baadaye ni kuja kuwa mwanasheria. “Wakati Rais Obama anaapishwa mwaka 2009 (yeye alikuwa darasa la nne) nilifuatilia historia yake nikajikuta nimevutiwa nayo na kuamua kuongeza juhudi katika masomo.  “Kumwamini Mungu pia ni siri kubwa ya mafanikio yangu, uhusiano mzuri kati ya wazazi na walimu wangu na kusoma kwa bidii,” alisema. Akielezea ratiba yake ya kila siku mwanafunzi huyo alisema huamka saa 12:00 asubuhi kisha hufanya usafi wa mwili na wa shule. Ikifika saa 12:45 huenda kunywa chai hadi saa 1:15 wanapokwenda mstarini. Alisema kuanzia saa 1:30 huingia darasani hadi saa 10:20 jioni ambapo hutoka na kwenda kuoga kisha kwenda kupata chakula kuanzia saa 11:30 hadi saa 12:15 jioni ambapo huingia tena darasani kwa ajili ya kusali rozali. Alisema husali rozali hadi saa 1:00 usiku kisha kuingia kujisomea hadi saa 5:30 usiku na kwenda kulala. “Kidato cha kwanza hadi cha pili walikuwa wanalala saa 3:30 usiku lakini kidato cha tatu na cha nne tukawa tunalala sasa 4, lakini baadaye sisi wa kidato cha nne tulibadilishiwa ratiba tukawa tunalala saa 5:30 usiku,” alisema. ATAMANI KUWA MWANASHERIA Mwanafunzi huyo alisema matarajio yake ni kuja kuwa mwanasheria kwa sababu anapenda kutetea watu na anapenda kuona haki ikitendeka kila mahali. “Kuna gazeti lilimuandika Rais Obama kuwa ni mwanasheria, baada ya kulisoma ndoto yangu ikaanzia hapo…na nitaendelea kusoma kwa bidii nataka nije kusoma Chuo Kikuu cha Havard Marekani…nataka niwe mwanasheria tena jaji na ikiwezekana zaidi niwe jaji mkuu,” alisema. Aliwashauri wanafunzi kuwa na imani katika kile wanachokifanya na kuzingatia muda na kwenda mbele zaidi ya yale wanayofundishwa na walimu wao. Alisema pia anajivunia wakati alipokuwa kiongozi shuleni kwani aliweza kujifunza mambo mengi. “Nilikuwa dada mkuu msaidizi, kuna mambo mengi mazuri na ya kujifunza unakuwa mtu wa kati ya mwalimu na mwanafunzi kwahiyo unapata uchungu na utamu wa pande zote, kwakweli nilijifunza mambo mengi sana,” alisema. Mwanafunzi huyo alisema anapenda sana kusoma vitabu, kuandika mashairi na kusafiri. WAZAZI Cynthia ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto wanne na msichana pekee katika familia ya Nehemia Mchechu na Mercy Mchechu. Mama mzazi wa Cynthia, Mercy alisema alikuwa akitegemea matokeo ya mwanawe kuwa mazuri kutokana historia yake katika madarasa ya nyuma. “Kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu na ni ndoto ya kila mzazi kuona mwanawe anafanya vizuri katika mitihani. Cynthia alikuwa akipenda sana mambo ya shule na amekuwa akisoma zaidi ya vitu ambavyo hupewa darasani. “Tuliposikia habari hizi kwamba ameongoza kitaifa tumefurahi sana tunaendelea kumwombea kwa sababu safari yake bado inaendelea,” alisema Mchechu.
kitaifa
Shirika la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF) limeandaa kongamano la kitaifa kujadili masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa shirika hilo Koshuma Mtengeti amesema, lengo la kongamano hilo ni kutafuta namna ya kutokomeza ukatili kwenye jamii.Kongamano hilo litakalofunguliwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa litafanyika Machi 21-22, katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu (DUCE) litahudhuriwa na wajumbe 600.Kati ya mada zitakazojadiliwa ni pamoja na ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto, ukatili wa kimtandao, hali ya ukatili kwenye familia na mashuleni, rushwa ya ngono vyuoni na nyinginezo.“Nchi yetu ina sera nzuri zinazopinga ukatili wa aina zote lakini matukio ya ukatili yanaendelea, hivyo mijadala kama hii itasaidia sana kuendelea kuongeza uelewa wa masuala haya, na kuhimiza vitendo hivi kuendelea kuripotiwa, “amesema Mtengeti.Utafiti wa kidemografia wa afya 2015/16 unaonyesha kuwa 40% ya wanawake wenye umri kati ya miaka 15-49 nchini wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kimwili tangu wakiwa na umri wa miaka 15.
kitaifa
Msanii wa Bongo fleva Diamond Platinumz ameamua kufanyia kufuru msanii wake aliyemsajili hivi karibuni ‘Zuchu’. Zuchu ambaye ni mtoto wa msanii Hadija Koppa alisajiliwa na lebo ya Wasafi Classic Baby (WCB) Aprili 8. Tangu kusajiliwa mwamadada huyo katika lebo hiyo kubwa ya muziki nchini Nyota wa Bongo Fleva Diamondi amekuwa akimposti katika ukurasa wake wa Instagram mfululizo. Pengine ni mkakati wa Diamond kumpromoti msanii wake huyo mpya ambaye tayari ameachia nyimbo kadhaa ndani ya muda mfupi miongoni mwa nyimbo hizo ni ‘Wana’. Tangu Aprili 7, 2020 Diamond ashamposti Zuchu takribani mara 50, ikiwa ni wastani wa posti 5 kwa siku tofauti na kawaida yake. Welcome to @wcb_wasafi Family @officialzuchu …. Subscribe, ADD and Follow Zuchu on Her Official Social Media pages so that you can be the first one to get her First Release…. YOUTUBE: ZUCHU TWITTER: OfficialZuchu FACEBOOK: OfficialZuchu TIKTOK: OfficialZuchu SNAPCHAT: OfficialZuchu TRILLER: OfficialZuchu #WCB4Life @wcb_wasafi @boomplaymusic_tz A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on Apr 8, 2020 at 11:36am PDT imagine jus Within 7 Days of her introduction to the Music industry…… @officialzuchu is Now Living to the Max with #PepsiMaxTz ….This Proves the Power of Women in the World🌍 Yani Ndani ya Siku 7 Tu!….Hakika Wanawake Wakiwezeshwa wanaweza…. Jamani Hii PEPSI MAX nyie Wenzangu Mshaionja??? Hebu Fanya Kuifata kwa Mangi Hapo Dukani Half utajua ni namna gani hawa PEPSI Wana balaa Zito!!👌🏼#PepsiBabaLao #PepsiMaxTz @pepsi_tz #IAmZuchu A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on Apr 16, 2020 at 2:22am PDT Jeje, wewe Unaishije Mpaka Max? ISHI MPAKA MAX na PEPSI MAX…. @pepsi_tz #IshiMpakaMax #LiveToTheMax A post shared by SIMBA..!🦁 (@diamondplatnumz) on Apr 17, 2020 at 9:36am PDT
burudani
MKUU wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti ameagiza kukamatwa mara moja kwa mawakala wawili wa kampuni binafsi  wanaopita vijijini wilayani Karagwe na Kyerwa kwa tuhuma za kuwapotosha na kuwalaghai wakulima wa kahawa wasikubaliane na mfumo wa serikali.RC Gaguti alitoa maelekezo hayo katika mkutano wa viongozi wa vyama vya msingi, watendaji wa kata na viongozi wa Chama Kikuu cha Ushirika mkoani KDCU Limited, wilayani Karagwe mara baada ya kukagua viwanda vitatu vya kukoboa kahawa vya Karim Amri, ASU Company Limited na KDCU Limited.“Nimeona nije kujionea msimu unaendeleaje na kama kuna changamoto yoyote tuitatue kwa pamoja na si kusubiri…... pia nina taarifa kuwa kuna mawakala wawili wa Kampuni binafsi wamekuwa wakipita vijijini kupotosha wakulima wasifuate mfumo wa Serikali ili baadae waje wanunue kahawa yao kwa bei ndogo tu namuagiza Kamanda Polisi Mkoa….wawakala hao wakamatwe mara moja.” aliagiza Mkuu wa Mkoa.Alisema kuwa maelekezo ya Serikali yapo wazi kuwa kama kuna mfanyabiashara yeyote anataka kununua kahawa, awasiliane na ofisi yake lakini awe na bei inayomnufaisha mkulima huku akidai kuwa mpaka sasa hakuna mfanyabishara aliyekidhi vigezo vya kununua zao hilo.Hadi sasa vyama vikuu vya ushirika mkoani Kagera; KCU 1990 LTD na KDCU LTD vimekusanya jumla ya kilogramu milioni 8.5 sawa na asilimia 20% ya malengo ndani ya msimu huu wa 2019/20.Taarifa zinabainisha zaidi kuwa Shilingi bilioni 6.2 zimelipwa kwa wakulima.
kitaifa
Na AGATHA CHARLES – Dar es Salaam MBUNGE wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete, amesema hatamani kuwa rais bali anataka siku moja awe Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM). Kauli hiyo aliitoa Dar es Salaam jana alipohojiwa katika kipindi cha Clouds 360 kinachorushwa na Televisheni ya Clouds. Jibu hilo la Ridhiwani lilitokana na swali aliloulizwa na watangazaji wa kipindi hicho kama ana ndoto za kuwa rais wa nchi. “Sijawahi kutamani kuwa rais ila muda ukifika natamani kuwa Katibu Mkuu wa CCM,” alisema. Ridhiwani alisema mafaniko yake hadi hapo alipofikia ni kutokana na mchango wa baba yake ambaye ni Rais mstaafu Jakaya Kikwete. “Malezi yangu, kuzaliwa na kiongozi kumenisaidia kufika hapa, nisingezaliwa huko labda ningekuwa mtu tofauti na nilivyo, mzee wangu ana mchango mkubwa hata jimboni, ananipa changamoto, ananielekeza, ana nafasi ya kunishauri,” alisema. Pia alisema katika kutekeleza sera ya Tanzania ya viwanda, tayari Mkoa wa Pwani una viwanda 164 vikiwamo vinavyojengwa na vilivyokamilika, huku 84 vikiwa ni vikubwa. Alisema uwekezaji wa viwanda hivyo umegawanyika katika sehemu mbili, chini ya Sh bilioni tano na ule ulio juu zaidi. “Sehemu kubwa ni viwanda vya kuchakata malighafi, kuna vya matunda, marumaru, nondo, korosho, mabati, saruji na malighafi ya nyumba na vinavyofanya kazi nikivitaja ni zaidi ya 40,” alisema. Ridhiwani alisema jimbo lake na mkoa wote wa Pwani, unafanya jitihada kuhakikisha bidhaa zilizokuwa zikipatikana China ziweze kupatikana Chalinze ili kuepuka gharama za usafirishaji. Alisema uwekezaji wa kiwanda cha Twyford Tanzania Ceramics kilichotembelewa wiki hii na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, uligharimu Dola za Marekani milioni 158. Ridhiwani alisema kiwanda hicho kinachotarajia kukamilika katika kipindi cha Julai hadi Agosti, kitakuwa na uwezo wa kutoa kontena 28 hadi 30 kwa siku. Alisema kupitia kiwanda hicho, wananchi watapata faida kwa kufanya biashara na kuongezeka kwa ajira. “Kitakuwa na ajira zaidi ya 2,000 zilizo rasmi, huku zisizo rasmi zikiwa ni zaidi ya 4,000. Hata hivyo, bado nasisitiza ajira izingatie wazawa kwa sababu wananchi tayari wanalalamikia upendeleo katika kupeana ajira, walioajiriwa pale wengi si wakazi wa Chalinze, hata Waziri Mwijage nilimwambia,” alisema. Pamoja na jitihada hizo, alisema utekelezaji wa sera ya Tanzania ya viwanda unaweza ukakwamishwa kutokana na uwezo wa kutafsiri neno na nia nzuri ya Rais Dk. John Magufuli. “Rais hawezi kujenga viwanda peke yake, wasaidizi tutoe tafsiri sahihi ya nia yake nzuri, tutekeleze. Sitokubali kumdhalilisha rais, akisimama mwaka 2020 akiulizwa kuwa viwanda viko wapi aseme viko Pwani, atoe mfano Chalinze,” alisema.
kitaifa
MANILA, PHILIPPINES RAIS wa Philippine, Rodrigo Duterte, ametishia kuwarusha viongozi mafisadi kutoka katika ndege angani, akisema ameshawahi kufanya hivyo kitambo. Duterte aliyasema hayo Jumanne wiki hii wakati akiwahutubia waathirika wa kimbunga katikati ya Philippines. “Kama wewe ni fisadi, nitakubeba kwa kutumia helikopta hadi Manila na kukurusha nje,” alisema Duterte, ambaye ameanzisha vita dhidi ya ufisadi na mihadarati. Alitishia kutoa adhabu hiyo kwa yeyote atakayeiba fedha za msaada alizoahidi kuzitoa. “Nimefanya hivi kitambo, kwanini nisiweze kufanya tena?” alisema huku akishangiliwa na watu hao. Haya ni madai mapya ya rais huyo ambaye amekiri kutekeleza mauaji ya kiholela. Hata hivyo, msemaji wake amepinga madai hayo. Mapema mwezi huu, msemaji mwingine, Martin Andanar, alisema kauli za mwajiri wake zipokewe kwa makini, lakini zisipewe uzito baada ya kusema kuwa aliwaua watu watatu alipokuwa Meya wa Davao nchini humo. Wakati kauli hiyo mpya akiitoa Jumanne wiki hii, jana Rais Duterte alionekana kujiweka kando na kauli zake za awali. “Helikopta, nimtupe mtu? Na iwapo ni kweli, sitakiri,” alisema wakati wa mahojiano na shirika la habari la ABS-CBN. Rais huyo ana historia ya kuyakana maneno yake. Watu 6,000 wanasemekana kuuawa na polisi, wanamgambo na wauaji wa kukodi nchini hapa tangu Duterte azindue vita dhidi ya mihadarati baada ya kuchaguliwa kuwa rais Mei, mwaka huu. Wanasiasa wa upinzani na makundi ya haki za binadamu wamekuwa wakitaka aondolewe madarakani, lakini amebakia maarufu miongoni mwa wapigakura wanaotaka aisafishe nchi hiyo.
kimataifa
MASHIRIKISHO ya sanaa nchini yanatarajia kutoa tuzo ya heshima kwa viongozi mbalimbali akiwemo hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia hiyo.Pia yamepanga kumpa tuzo Rais John Magufuli na Rais wa Zanzibar, Dk Mohammed Shein kutokana na michango yao ya kufuata nyayo za Mwalimu Nyerere katika uongozi wao.Tuzo hizo zinatarajiwa kukabidhiwa keshokutwa katika tamasha lililoandaliwa na mashirikisho hayo manne ya sanaa za maonesho, ufundi, muziki na filamu. Katika tamasha hilo, litakaloanza kwa kongamano la wasanii, Rais Magufuli atafungua pamoja na kukutana na wasanii.Hayo yalisemwa jana nyumbani kwa Mwalimu Nyerere, Mikocheni Dar es Salaam baada ya viongozi wa shirikisho hizo kwenda kushukuru familia ya Mwalimu kutokana na mchango aliouonesha wakati wa uhai wake.Akizungumza jana, Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifamba alisema lengo la tamasha hilo lililoandaliwa na wasanii ni kutambua mchango wa mwalimu lakini pia kutangaza aliyoyafanya ili wale walio na umri wa miaka 20 kwa sasa ambao hawakumfahamu wamfahamu.“Hatutaki historia ife, wapo wasiomjua mwalimu na ni wale ambao wenye miaka 20 kwa sasa, hivyo tutatumia sikuhiyo kumzunguzia mwalimu kama kiongozi mashuhuri kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla,” alisema Mwakifamba.Alisema katika tamasha hilo litaambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo burudani, mashairi, nyimbo na hata video ili kizazi cha sasa kiendelee kumtambua mwalimu kwa kazi mbalimbali alizofanya.Akiwapokea wasanii nyumbani kwa Mwalimu Mikocheni, mtoto wa Mwalimu, Makongoro Nyerere alitumia muda mwingi kueleza ratiba ya mwalimu wakati wa uhai wake kuanzia asubuhi hadi jioni na kuwashukuru kwa kukumbuka mchango uliotolewa na Mwalimu.Alisema Mwalimu Nyerere pamoja na waasisi wenzake waliwatumia wasanii katika harakati mbalimbali, na kuwapongeza kwa kutambua suala hilo. Makongoro aliyekuwa akiwafurahisha wasanii kwa muda mrefu kutokana na maelezo yake, alisema kwa sasa amerudi CCM na ni mjumbe wa Halmashauri Kuu.
michezo
UKITAZAMA kwa jicho la tatu, mwenendo wa mbio za marathon za kuwania ubingwa kwenye Ligi Kuu ya England (EPL) kati ya Manchester City na Liverpool, ilikuwa patashika ya nguo kuchanika, kwani City ilifanikiwa kubeba ubingwa huo kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya mpinzani wake Liverpool.Mfano huo unaweza kuuleta Tanzania na ‘ku-paste’ kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara (TPL), kwani vigogo wa ligi hiyo, Simba na Yanga walikuwa wanafukuzana kama farasi jangwani kuwania taji hilo.Mpaka ligi inakaribia ukingoni bado kulikuwa na kitendawili juu ya nani ataibuka bingwa kutokana na hesabu zilivyokuwa zikiibeba Simba, lakini uhalisia wa soka ulikuwa umeegemea upande wa Yanga.MABINGWA SIMBA Lakini mwisho wa siku mashabiki wa soka waliishuhudia Simba ikifanikiwa kutetea taji hilo kwa shida na kulinyakua kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufikisha pointi 91, ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote huku ikiwa na michezo miwili mkononi. Hiyo ni baada ya kumuacha mpinzani wake Yanga ambaye ana hazina ya pointi 86, ambaye wakati huo alikuwa amebakiwa na mchezo mmoja tu kabla ya kuhitimisha ligi hiyo iliyofikia kileleni Mei 28.Simba tunaweza kusema kilichombeba ni kuwa na viporo vingi, ambavyo pia alijitahidi kuvila vizuri kwa kuondoka na pointi tatu kila alipocheza ukiondoa sare chache na kufungwa mara chache tofauti na Yanga.Pamoja na Simba kufanikiwa kutetea taji lake, lakini vita kubwa ilikuwa kwa timu za kushuka daraja, ambazo zilipambana kufa au kupona huku zingine kama Kagera Sugar ikicheza play-off. Mwandishi wa gazeti hili anachambua mwenendo mzima wa ligi hiyo na ushindano ulivyokuwa hadi Simba kufanikiwa kutwaa taji hilo kwa mara ya pili mfululizo.AZAM ILIPEWA NAFASIKabla ya ligi hiyo kuanza timu zilizokuwa zinapewa nafasi kubwa ya kuweza kuleta ushindani mkubwa mbele ya Simba kulingana na maandalizi iliyoyafanya ni Azam pekee. Kila mmoja anafahamu fika Azam ilikuwa miongoni mwa timu zilizowekeza vya kutosha kwa kufanya usajili mzuri wa wachezaji ambao ulitegemewa kuleta ushindani mkubwa mbele ya Simba iliyojizatiti vya kutosha chini ya bilionea Mohamed Dewji ‘Mo’. Licha ya Yanga kubebwa na jina lake kulingana na historia yake ya kutwaa taji hilo mara nyingi kuliko timu yoyote kwenye ligi hiyo, lakini hakuna aliyekuwa akitarajia kuona Yanga ikileta ushindani kutokana na timu hiyo kutokuwa na mfadhili wala fedha za usajili.UPINZANI WA YANGALicha ya mabingwa hao wa kihistoria kupitia kwenye kipindi kigumu ikiwemo kukosa viongozi na kushindwa kulipa stahiki za wachezaji kwa wakati, lakini walifanikiwa kuleta upinzani dhidi ya Simba na kuongoza ligi hiyo kwa muda mrefu zaidi kuliko timu nyingine 19 zilizoshiriki ligi hiyo.Ni wazi shukurani kubwa zinapaswa kupelekwa kwa benchi la ufundi linaloongozwa na Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mwinyi Zahera aliyesimama bila kujali kipindi hicho cha mpito na kuwajenga kisaikolojia kuweza kupambana bila kuchoka na kufanikiwa kuleta ushindani kwa Simba, ambao walikuwa wamefanya maandalizi makubwa kwa kupanga bajeti kubwa na kusajili wachezaji wa maana.Haikuwa rahisi kuona wachezaji wa timu kama Yanga wakidai mishahara ya mpaka miezi mitatu, lakini walionesha kucheza kwa moyo na kujitolea. Hata walipofikia kukata tamaa kabisa bado Zahera alionekana kuyeyusha huzuni na kuibua furaha katikati ya mioyo yao.Mwisho ikaonekana inawezekana, Yanga ikawa tishio bila ‘meno’ na ukisogea vibaya unapigwa nyingi. Yanga haikuwa na wachezaji wengi wa hadhi yao, lakini kwa pamoja ilionesha wao ni nani na muhimu kwao ilikuwa mabao, mengine yanafuata. Kimasihara ikauweka ubingwa wa Simba rehani na kubadili mawazo ya wengi kuwa mwisho wa msimu watarajie lolote, tofauti na ilivyotarajiwa, kwamba Simba itatetea ubingwa kirahisi baada ya Azam nayo kuyumba ilipofika katikati baada ya kucheza muda mrefu bila ya kupoteza mchezo.Muvi imeisha na Yanga imemaliza kwenye nafasi ya pili ikiacha historia kwa ilichokifanya kwa Simba waliokuwa wanapewa nafasi kubwa ya kufanikiwa kutetea ubingwa huo, kutokana na usajili wa wachezaji walioufanya na kuweka bajeti ya maana iliyokuwa inasababisha wachezaji wa kikosi hicho kucheza kwa kujiamini muda wote uwanjani. Simba walipewa kila kitu.Mshahara kwa wakati, ‘bonus’ za kutosha na waliishi katika mazingira ya juu ya kama timu kweli inayohitaji kufanya mapinduzi Afrika lakini spidi ya Yanga ilibaki kidogo iyeyushe matumaini yao ya ubingwa na kushika chati za juu kwenye msimamo. Ilifika wakati ilikuwa inaonekana ngumu kwao kuikimbiza Yanga, huku wakiwa na mtihani wa michuano ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika.Wapinzani wao Yanga walijikuta wakitawala usukani wa ligi hiyo hadi wanafikia utofauti wa pointi 21. Hakika Yanga inastahili pongezi kwa ushindani walioonesha licha ya kuonekana ni timu dhaifu mbele ya Simba msimu huu.AZAM HAIKUWA MBALIUkiachilia mbali Simba, Azam ni timu ya pili iliyokuwa inapewa nafasi ya kuleta ushindani kutokana na usajili walioufanya kujiandaa katika ligi hiyo. Lakini walijikuta kikosi hicho kilishindwa kufikia malengo ya timu na kujikuta wakipoteza michezo kadhaa na kulazimisha sare zilizosababisha kukata tamaa ya ubingwa na kupelekea uongozi wa timu hiyo kuvunja benchi la ufundi lililokuwa likiongozwa na Mholanzi Hans Van Der Pluijm na kikosi hicho kukabidhiwa kwa makocha wa mpito, Abdul Mingange na msaidizi wake Iddi Cheche.Pamoja na mabadiliko hayo, walishindwa kuleta ushindani na kujikuta wakizorota kwenye zoezi la kutwaa ubingwa huo na kuishia kupigania nafasi za juu kwenye msimamo wa ligi hiyo ili kulinda heshima yao ambapo wamekalia nafasi ya tatu. Tumezoea kuona Mtibwa Sugar ni miongoni mwa timu zinazofanya vyema ukiachilia Yanga, Simba na Azam ambapo nayo inafuatia lakini wameshindwa kuonesha umwamba wao na kujikuta wakipoteza michezo mingi tofauti na hadhi yao.KMC ni timu ngeni kwenye ligi hiyo lakini imeleta ushindani mkubwa hadi imefanikiwa kushika nafasi ya nne na kujitoa kwenye hadhi ya ‘underdog’ na kuzizidi timu nyingine tano zilizopanda pamoja msimu huu. Timu hiyo sasa itashiriki michuano ya Kombe la Shirikisho la Afrika baada ya Tanzania kupewa nafasi nne, mbili Ligi ya Mabingwa wa Afrika na idadi kama hiyo, Kombe la Shirikisho.Biashara United na JKT Tanzania zilipanda pamoja na KMC mwishoni mwa msimu uliopita, lakini zenyewe zilikuwa zinapambana na hali yao kwa muda mrefu zikigombea kutoshuka daraja. Wengine waliopanda ligi hiyo na KMC ni Coastal Union na Alliance ambao michezo yao ya mwisho ndio iliyozihakikishia timu hizo kutoshuka daraja na sasa wana uhakika wa kuendelea kuwepo katika ligi hiyo msimu ujao.Ya mwisho iliyopanda sambamba na KMC au Kino Boys ni African Lyon ambayo yenyewe ilikuwa ya kwanza kabisa kushuka daraja na sasa inajiandaa na michezo ya Ligi Daraja la Kwanza na maisha yao mengine mapya waliyoyaacha kwa takriban miezi nane tu iliyopita na sasa wanarejea tena huko walikotoka.
michezo
RAMADHAN HASSAN -DODOMA MFUMUKO wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020, umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Kaimu Mkurugenzi wa Takwimu na Sensa ya Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Ruth Minja alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari. Alisema mfumuko wa bei wa taifa kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umebaki kuwa asilimia 3.2 kama ilivyokuwa kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Minja alisema hali hiyo inamaanisha kuwa kasi ya mabadiliko ya bei za bidhaa za vyakula na bidhaa kwa mwaka ulioishia Juni 2020 umebaki kuwa sawa na kasi iliyokuwepo kwa mwaka ulioishia Mei 2020. Alisema kuwa sawa kwa mfumuko huo kumechangiwa na kuongezeka na kupungua kwa baadhi ya bei za bidhaa za vyakula na zisizo za vyakula kwa kipindi kilichoishia Juni 2020 zikilinganishwa na bei za Juni 2019. Minja alisema baadhi ya bei za vyakula zilizopungua ni pamoja na unga wa mahindi kwa asilimia 1.6, matunda asilimia 2.1, viazi mviringo asilimia 5.0 na mihogo asilimia 13.3. Alisema baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula zilizoongezeka bei ni pamoja na mavazi kwa asilimia 2.7, gesi ya kupikia asilimia 7.8, mkaa kwa asilimia 11.2, samani asilimia 2.7 na vitabu vya shule asilimia 1.5. Kaimu Mkurugenzi huyo alisema mfumuko wa bei wa bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa mwezi ulioishia Juni mwaka 2020 umepungua hadi asilimia 3.8 kutoka asilimia 4.4 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Alisema kwa upande wa Afrika Mashariki, nchini Kenya mumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umepungua hadi kufikia asilimia asilimia 4.59 kutoka asilimia 5.33 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020. Kwa upande wa Uganda, alisema mfumuko wa bei kwa mwaka ulioishia mwezi Juni 2020 umeongezeka hadi asilimia 4.1 kutoka asilimia 2.8 kwa mwaka ulioishia mwezi Mei 2020.
uchumi
KINSHASA, DRC Shirika la afya la kimataifa WHO, limetangaza kuwa hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa Ebola kuzidi kusambaa na kiwango chake kiko juu zaidi miongoni mwa wananchi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. WHO limeeleza kuwa vyanzo vya maambuziko ya ugonjwa wa Ebola vimeongezeka na sasa njia za usafiri na shughuli za umma ni hatari kwa wananchi kuambukizana huku tathimini ya kusambaa kimataifa imebaki hatari ndogo. Taarifa ya WHO imesema kuwa kitaifa na majimboni nchini humo hatari ya kuambukizana iko juu na kushauri majimbo jirani na mataifa kuimarisha tahadhari dhidi ya maradhi hayo. Aidha WHO wamesisitiza kuendelea kushirikiana na mataifa jirani na washirika kuhakikisha mamlaka za afya zinachukua tahadhari na zinakuwa tayari kuchukua hatua.Jumanne iliyopita Naibu mkurugenzi wa WHO Peter Salama alionya taifa jirani la Uganda kuchukua tahadhari kufuatia tishio la maambukizi mpakani jirani na ziwa Albert.Kwa mujibu wa takwimu wa shirika la WHO mlipuko wa Ebola umesababisha vifo vya watu 101 tangu ulipolipuka mnamo mwezi Agosti mwaka huu. Huu unakuwa mlipuko wa mara ya kumi kutokea nchini DRC tangu mwaka 1976, ambapo hali ya hatari iko juu sana katika jimbo la kaskazini mashariki ambako kunavikundi kadha avinavyomiliki silaha jirani na mpaka wa Uganda Rwanda na Sudani kusini.
kimataifa
WATU wawili wanaodaiwa kuwa majambazi wamefariki dunia kwa kupigwa risasi na wenzao, baada ya kutaka kuwatoroka askari wakati wa operesheni ya kuwasaka majambazi mkoani Shinyanga.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Saimon Haule alithibitisha hayo jana alipozungumza na waandishi wa habari. Alieleza kuwa mauaji hayo yalitokea juzi saa 3:00 usiku katika vichaka vya Mtaa wa Buhangija Kata ya Ibinzamata Manispaa ya Shinyanga. Kamanda aliwataja waliouawa ni Geoffrey Ntabazi (29) na Ramadhani Masoud (33), ambao walikuwa wahusika kwenye matukio ya unyang'anyi na uvunjaji ya Januari 28 na 30, mwaka huu.Kamanda Haule alisema watu hao wanaodaiwa kuwa ni majambazi, walikufa kwa kupigwa risasi na majambazi wenzao, baada ya kutaka kuwatoroka wakati wa operesheni ya kuwasaka majambazi waliotajwa na marehemu hao kuhusika kwenye matukio ya unyang'anyi na uvunjaji.Alisema majambazi hao walitaja silaha ambayo huitumia pamoja na wenzao, waliokuwa wamejificha kwenye vichaka eneo la Buhangija. Baada ya kufika hapo, ghafla majambazi hao waliokuwa wamejificha, walianza kuwashambulia askari na kumpata jambazi mmoja na mwingine aliyekuwa ameongozana na askari.
kitaifa
Na MWANDIHI WETU, DAR ES SALAAM WAKAZI wa Kata za Kivule na Msongola wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam waliovunjiwa nyumba zao wamemwomba Rais Dk. John Magufuli kuwatembelea kwenye makazi yao ili wamweleze unyama waliofanyiwa na kikundi kinachojiita Umoja wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA). Wakazi hao zaidi ya 2000 ni miongoni mwa wamiliki wa nyumba 500 zinazodaiwa kuvunjwa kimakosa kwa amri ya Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke. Wakizungumza na MTANZANIA mwishoni mwa wiki, baadhi ya wakazi hao walisema mtu pekee ambaye wanaona anaweza kuwasaidia ni Rais Dk. Magufuli kwani wanao uhakika kwamba waliowafanyia unyama huo wana mkono wa mtu mzito aliyeko serikalini. “Kama rais wetu (Dk John Magufuli ) anatusikia tunamwomba aje hapa katika ziara zake za kushtukiza ili tumweleze ukweli wa jambo hili, kuna wateule wake wachache wameamua kututesa na kutufanyia hila, hawa wana mkono wao humu. Hii si mara ya kwanza, kila wakijisikia wanakuja kutubomolea nyumba bila haki yoyote” alisema mmoja wa wananchi hao Aneth Athuman. Naye Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema) aliiomba Serikali kukifanyia uchunguzi kikundi cha Uvikiuta kwani huenda kimetumika kubeba ajenda za watu wengine. Mwita ambaye alikwenda kutoa misaada ya kibinadamu kwa wananchi waliobomolewa nyumba zao alisema kuna baadhi ya wateule wa rais wapo nyuma ya kikundi hicho ambacho kimejificha kwenye mgongo wa dini kuhodhi eneo kubwa la ardhi kinyume cha taratibu. “Ukitaka kujua kwamba huu unyama una mkono wa baadhi ya wateule wa Rais, angalia namna viongozi hao walivyokaa kimya hadi sasa bila kuchukua hatua, leo hii hatumwoni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akija hapa kusikiliza kero za wananchi kama alivyofanya maeneo mengine. “Kama RC Makonda alifanya ziara maeneo mbalimbali ya Dar es salaam na baadhi ya mikutano yake ikaripotiwa ‘live’ na vyombo vya habari kwa nini asije hapa akawasikiliza wananchi ambao wamebomolewa nyumba zao bila hatia, kama hakuna ajenda ndani yake ni nini?,” alihoji Waitara. Wiki iliyopita Polisi wilayani Temeke kwa kushirikiana na dalali wa mahakama walibomoa nyumba 500 za wakazi wa Kivule na Msongola kwa madai kuwa Uvikiuta wameshinda kesi ya ardhi namba 73 ya mwaka 2014 ambapo iliamriwa nyumba hizo zibomolewe. Hata hivyo wananchi wanadai kuwa hati iliyotolewa na mahakama hiyo inahusu nyumba tano tu na si vinginevyo. Washtakiwa katika kesi hiyo walitajwa kuwa ni Elia Mharage, Astria Charles, Daud Zebedayo na Chacha Marwa.
kitaifa
MADRID, HISPANIA KOCHA wa klabu ya mabingwa watetezi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya, Real Madrid, Zinedine Zidane, ameweka wazi kuwa nyota wake, Cristiano Ronaldo na nahodha Sergio Ramos, wamemaliza tofauti zao. Uongozi wa klabu hiyo uliwakutanisha wachezaji hao juzi, kabla ya kuelekea katika mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid kwenye Ligi Kuu nchini Hispania. Sababu za wawili hao kuwa kwenye mgogoro ni baada ya Real Madrid kukubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Tottenham kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, Novemba 1, kwenye Uwanja wa Wembley, hivyo Ronaldo akatupia lawama kwa uongozi wa klabu hiyo kwa kudai kwamba, walifanya makosa makubwa kuwauza wachezaji wao, James Rodriguez na Alvaro Morata. Kauli hiyo ya Ronaldo ilionekana kumchukiza sana Ramos na ndipo nahodha huyo alisema kuwa, Ronaldo ni mchezaji mbinafsi sana na hakupaswa kuongea kauli kama hiyo na alitakiwa kushirikiana na wenzake ili kuisaidia timu. Hata hivyo, baada ya mgogoro huo kuwa mkubwa, Ronaldo aliweka wazi kuwa, hana mpango tena wa kuendelea kuwa na timu hiyo mara baada ya kumaliza mkataba wake. “Ni wazi kwamba Sergio Ramos ni miongoni mwa wachezaji wenye akili sana ndani na nje ya uwanja, anaweza kumwambia kitu mchezaji yeyote hata kama ni Cristiano Ronaldo, isitoshe wachezaji hao wamekuwa pamoja kwa muda mrefu na wamezoeana. “Mchezaji huyo alistahili kumwambia hivyo Ronaldo kutokana na kauli yake, lakini ukweli ni kwamba kila kitu kipo sawa kwa sasa, uongozi wa klabu uliamua kukaa pamoja na wachezaji hao kwa ajili ya kumaliza tofauti zao na kila kitu kinakwenda sawa sasa. “Kwa pamoja naweza kusema nina wachezaji wawili kwenye kikosi ambao wanatengeneza historia ndani ya timu hii, wamekubali kumaliza tofauti zao ili kuweza kuipigania timu yao katika michezo inayofuata,” alisema Zidane. Wababe hao wa soka barani Ulaya, msimu huu wanaonekana kuwa wameuanza vibaya kutokana na kiwango chao na ushindi wanaoupata, huku baadhi ya mshabiki wakidai kuwa, mshambuliaji wao huyo ambaye ana tuzo nne za Ballon d’Or, amekuwa kwenye kiwango cha chini.
michezo
WAZAZI wa wanafunzi wanaosoma Shule ya Sekondari ya Dodoma kwa kushirikiana na Bodi ya shule wamekubaliana kuchangishana Sh milioni 264.3 kujenga uzio kuzunguka shule.Uamuzi huo wa kujenga uzio, ulifikiwa katika kikao hicho, baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais- Tamisemi, Selemani Jafo kuagiza bodi hiyo wakati wa mahafali ya kidato cha nje mwaka jana kujenga ukuta kuzunguka shule.Akizungumza na wazazi wa wanafunzi wa shule hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Sekondari ya Dodoma, Philbert Bagenda alisema, serikali imetoa agizo la elimu bure na kuwataka walimu au bodi kutochangisha wazazi katika michango, lakini haijazuia kuchangia elimu kwa hiari. “Serikali imekataza kutoza michango, lakini bado haijazuia wazazi au wadau wa elimu wenye nia njema kuchangia elimu kwa hiari yao kwa manufaa ya jamii kwa ujumla,” alisema.Mwenyekiti huo alisema pamoja na serikali kutoa Sh bilioni 1.44 kukarabati majengo ya shule na mabweni ya wananfunzi, inakabiliwa na tatizo la uzio, jambo ambalo linasababisha wanafunzi kukosa utulivu wawapo shuleni hapo. Alisema pamoja na kupata kiasi hicho kwa ajili ya ukarabati ya shule hiyo na ujenzi mabweni, shule ni kongwe lakini haina uzio miaka mingi.Bagenda alisema walianza kuweka mipango kwa kutafuta na kuweka mipaka ya shule kwa usahihi, kufuatilia michoro ya uzio na kutafuta thamani halisi ya ujenzi wa uzio na hayo yote yalifuata utaratibu kupitia Halmashauri ya Jiji. “Mipango hiyo imekamilika na kupata kibali cha kuanza ujenzi na wataalamu wa Jiji ndiyo waliotupatia thamani halisi ya Sh milioni 264.3 hadi ujenzi wa uzio unakamilika,” alisema.Bagenda alisema kutokana na kumaliza taratibu hizo, bodi iliona ni jambo jema kuwashirikisha wadau wa maendeleo ya elimu kabla ya yote ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha wazazi ili kuchanga kwa hiari bila kushurutishwa. Mzazi Nasoni Manyere alisema licha ya serikali kukataza michango, si jambo baya wazazi kukubaliana kufanya shughuli za kimaendeleo.
kitaifa
Simba na Singano wamekuwa kwenye mgogoro kwa takriban wiki ya pili sasa, ambapo mchezaji huyo anadai kutaka kuondoka kwa vile amemaliza mkataba wake wa miaka miwili huku uongozi wa klabu yake ukisema bado mchezaji wake halali kwani alisaini mkataba wa miaka mitatu unaotarajiwa kumalizika mwakani.Taarifa ya TFF kwa vyombo vya habari jana ilisema imepokea kwa masikitiko taarifa za mgogoro wa kimkataba kati ya Singano na Simba.“TFF imeagiza mwakilishi wa klabu ya Simba pamoja na mchezaji wa Simba wafike ofisi za TFF siku ya Jumanne tarehe 09/06/2015 kwa mazungumzo,” ilisomeka taarifa hiyo.Aidha taarifa hiyo ilisema kila upande unatakiwa kufika na vielelezo vyake.“Katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye mazungumzo, TFF inaziasa pande zote mbili zijiepushe na kutoa matamko yanayoweza kuchochea hali ya kutoelewana na kuamsha hisia mbaya katika familia ya mpira wa Miguu Tanzania,” ilisomeka taraifa hiyo.Mwanzoni mwa wiki hii Simba ilitishia kumshitaki mchezaji huyo, kwa madai ameidhalilisha klabu kwa kitendo chake cha kudai hajasaini mkataba wa miaka mitatu na kumtaka apeleke mkataba wake wa miaka miwili anaodai alisaini.Katika moja ya malalamiko yake, Singano ambaye anahusishwa na kutaka kujiunga na Azam anasema uwepo wake Simba haujamnufaisha kwani licha ya kufanya vizuri lakini hana pakuishi mpaka sasa.
michezo
TIMU ya Taifa ya Tanzania Bara U20 imefuzu nusu fainali ya mashindano ya CECAFA yanayochezwa nchini Uganda baada ya kuwafunga wenyeji Uganda, Hippos, kwa mabao 4-2 katika mchezo uwa robo fainali kwenye Uwanja wa Pece, Gulu. Tanzania Bara U20 inayonolewa na kocha Zuberi Katwila ilianza kuzifumania nyavu za wapinzani wao dakika ya 25 bao likifungwa na Andrew Simchimba likadumu hadi mapumziko. Dakika ya 46 Uganda walisawazisha bao lililofungwa na Abdul Kayondo na dakika ya 60, Andrew Simchimba aliifungia bao la pili Tanzania Bara, lakini Uganda walifanikiwa kusawazisha dakika ya 60. Baada ya mabao kuwa 2-2 kila timu ilijitahidi kumsoma mpinzani wake na kujaribu kutumia makosa yake, lakini Tanzania Bara kupitia kwa Kelvin John ilifanikiwa kuzifumania nyavu za Uganda katika dakika ya 88 na 90 na kuzima ndoto za ufalme wa Uganda kwa timu za Tanzania. Tanzania Bara ambayo ilitinga robo fainali baada ya kumaliza ikiwa na pointi saba kinara wa Kundi B baada ya kushinda michezo miwili na kutoka sare mchezo mmoja, sasa itacheza nusu fainali ya mashindano hayo.Katika mchezo mwingine wawakilishi wa Zanzibar, walifungwa na Eritrea kwa mabao 5-0, na Kenya ikamfunga Burundi kwa mabao 2-1.
michezo
['Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa, watoto wanne kati ya watano wenye umri wa miaka 11-17 duniani hawafanyi mazoezi ya viungo ya kutosha.', 'Shirika la afya duniani (WHO) limesema kuwa afya za watoto zinaharibiwa kutokana na ukosefu wa mazoezi hivyo kuathiri ukuaji wa ubongo na shughuli zao za ujuzi kupungua uwezo.', 'Utafiti huo umesema kwamba chanzo ni kutokufanya mazoezi, inashauriwa kuwa ni vyema mtoto kufanya mazoezi walau kwa saa moja kwa siku.', 'Tatizo hili limekuwa kubwa duniani kote katika mataifa maskini na tajiri.', 'Watoto wa kiume wanaoneka kujishughulisha zaidi katika kufanya mazoezi kuliko watoto wa kike katika nchi 4 kati ya 146 zilizofanyiwa utafiti.', 'Mazoezi gani wanapaswa kuyafanya?', 'Mazoezi yoyote yanayofanya mapigo ya moyo yaende kwa haraka na mapafu kupumua kwa nguvu, kama vile;', '-Kukimbia', '-Kuendesha baiskeli', '-Kuogelea', '-Kucheza mpira ', '-Kuruka kwa mguu mmoja', '-Kuruka Kamba', '-Sarakasi', 'Daktari kutoka shirika la afya dunia, Dkt Fiona Bull amesema kuwa hadhani kwamba ni lengo kubwa sana la kujiwekea lakini ni vyema kuzingatia afya.', "''Ni vizuri kujijengea afya nzuri na maendeleo ya mwili.''", 'Tofauti kati ya mazoezi ya wastani na yale ya kutumia nguvu ni kwamba mazoezi ya wastani unakuwa unaweza kuzungumza lakini ya mazoezi ya nguvu hayakuruhusu kuzungumza, kwa sababu unakuwa hauna pumzi ya kutosha.', 'Kwanini ni muhimu kujali?', 'Sababu kubwa ni afya ya sasa hivi na ya baadae. ', 'Kwa muda huu mfupi, kuwa mchamgamfu kunamaanisha:', '-Moyo na mapafu yanakuwa na afya', '-Mifupa na misuli imara', '-Afya ya akili ya mwili inakuwa nzuri', '-Uzito mdogo', "''Vijana wachangamfu wana uwezekano wa kuwa watu wazima wachangamfu,'' Anaeleza Daktari kutoka shirika la afya duniani.", 'Na vilevile muda unavyozidi kwenda basi unapunguza hatari ya kupata magonjwa kama mshtuko wa moyo, kiharusi, na aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari.', 'Ukosefu wa mazoezi unamuweka mtu mmoja kati ya watu wazima wanne hatarini.', 'Lakini uchunguzi unasema kuwa kuna ushahidi wa kutosha unaoonesha kujishughulisha ni kitu kizuri kwa ukuaji wa ubongo.', "''Wanakuwa na uwezo wa kutambua, kujifunza kwa urahisi, na tabia nzuri ya kujichanganya na wengi.'' Amesema Dkt Guthold.", 'Je kwa kawaida watoto ni wavivu tu?', 'Je, utafiti huu unatuambia nini kuhusu misingi ya watoto?', "Dkt Bull amesema kuwa ''Watoto sio wavivu''", "''Hii inatueleza kuhusu kitu kikubwa zaidi lakini sio kuhusu watoto peke yake. "]
michezo
NA ZAINAB IDDY UONGOZI wa Simba umetangaza kamati maalumu ambayo imepewa jukumu la kutafuta mwekezaji atakayenunua asilimia 50 ya hisa ili kukamilisha azma ya klabu hiyo kujiendesha kisasa. Hatua hiyo inatokana na klabu hiyo kubadili mfumo wake wa uendeshaji kutoka ule wa wanachama uliodumu kwa miaka mingi hadi kuwa wa hisa. Kamati hiyo inaundwa na watu watano ambao ni Wakili Damas Ndumbaro, Mbunge wa Ilala, Musa Hassani ‘Zungu’. Pia yumo Abdallah Lazak Badru, Yusuph Majib na  Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jaji  Thomas Mihayo. Mfanyabiashara maarufu na mwanachama wa klabu hiyo, Mohamed Dewji, anapewa nafasi kubwa ya kupewa fursa hiyo, baada ya kuweka wazi kuwa yuko tayari kununua hisa zenye thamani ya Sh bilioni 20. Wanachama wengi wa Simba wanamuunga mkono bilionea huyo kukabidhiwa timu yao kutokana na mchango wake uliowezesha kusajiliwa kwa  wachezaji kadhaa wapya wenye ubora msimu huu wa Ligi Kuu Tanzania Bara, akiwemo aliyekuwa kiungo wa Yanga Haruna Niyonzima. Akizungumza wakati akitangaza kamati hiyo Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Simba, Dk. Arnold Kashembe, alisema kamati hiyo itafanya kazi yake katika kipindi cha siku 45 kabla ya kuwasilisha jina la mshindi katika kamati ya utendaji. “Tumeunda kamati hiyo ambayo itakuwa huru kufanya kazi zake kwa mujibu wa sheria za nchi na baada ya kuona wote hao ni wazuri katika masuala ya kisheria pamoja na kifedha kwa maana ya uuzaji na ununuzi wa hisa. “Kamati hiyo inatarajia kukutana kwa mara ya kwanza kati ya Jumatano na Alhamis, baada ya hapo wataweka mikakati yao juu ya vipi wataanza majukumu yao ya kumpata mwekezaji mkubwa, lengo likiwa ni kuifanya timu yetu iendeshwe kisasa zaidi,” alisema. “Baada ya kamati hiyo kumpata mwekezaji kwa asilimia 50, itapeleka jina lake kwenye kamati ya utendaji kabla ya kuitishwa mkutano wa wanachama ambao ndio utakaoidhinisha iwapo kama apewe hisa hizo au la. “Kama wanachama watapitisha jina la mwekezaji huyo aliyepatikana, hapo ndipo mfumo rasmi wa uendeshaji wa klabu utakapoanza, kati ya asilimia 50 zitakazobaki zitatolewa asilimia 10 na kupewa wanachama wote hai, huku zile asilimia 40 zitauzwa kwa wanachama kulingana na uwezo wa mhusika, lakini yule mwekezaji mkubwa kwenye hisa hataruhusiwa kuja kuchukua katika zile 40% za wanachama,” alisema Kashembe.
michezo
Kiungo wa zamani wa Yanga Salvatory Edward ameingilia kati suala la kipa timu yake hiyo ya zamani Claus Kindoki.Kindoki aliyeletwa Yanga na kocha wa timu hiyo Mwinyi Zahera amekuwa akishutumiwa na mashabiki wa timu hiyo kutokana na kiwango kibovu anachoonyesha tangu alipojiunga na timu hiyo akitoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).Kipa huyo alisajiliwa kama chaguo la kwanza baada ya klabu hiyo kuachana na Youthe Rostand ambae aliachwa kwa kwa kuwa aliruhusu mabao mengi ya kizembe.Kindoki amejikuta akifungwa mabao rahisi kwenye ligi na mechi za kirafiki na hadi sasa ameruhusu mabao 10.Hata hivyo Salvatory Edward aliyewahi kutamba na Yanga na Taifa Stars katikati ya miaka ya 1990 mpaka katikati ya miaka ya 2000, ameibuka na kuisihi klabu yake hiyo kuwa nyuma ya kipa huyo kwani tayari wameshamsajili.“Kindoki sio kipa mbaya ingawa sio wa kiwango cha kuitwa wa kulipwa; lakini tayari Yanga imeshamsajili , hivyo wanachotakiwa ni kumuunga mkono tu kwa sasa, kumlaumu watamuondolea kabisa hali ya kujiamini na wao sasa hivi wamebakiwa na makipa wawili tu, kwani Beno Kokalonya wanasema amegoma.“Binafsi sipendi na lawama wanazompa hata kama ni kipa wa kawaida lakini ndio tayari wako nae, wanapaswa kumuunga mkono tu na sio vinginevyo,”alisema Edward aliyetamba kwa jina la Dokta wakati akimudu vyema nafasi ya kiungo.
michezo
WATU watatu wamekufa na wawili wamejeruhiwa na kulazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru, baada ya kufukiwa na kifusi kwenye machimbo ya moramu.Machimbo hayo yanayotumika kwa ajili ya shughuli za ujenzi, yapo eneo la Moivaro katika Kata ya Moshono jijini hapa.Tukio hilo limetokea umbali wa kilometa nane kutoka katikati ya Jiji la Arusha, baada ya mabonge makubwa ya moramu kuporomoka, wakati watu hao wakiwa kwenye shughuli ya uchimbaji.Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Jonathan Shana alisema tukio hilo ni la Aprili 23, mwaka huu saa 2:00 asubuhi.Kamanda Shana alisema tangu kutokea ajali hiyo vikosi vya uokoaji kutoka mamlaka za ulinzi na usalama, vilikusanyika eneo la tukio na kuendelea kufukua udongo, kuwatafuta watu waliofukiwa. “Lakini pia vifaa mbalimbali vya uokoaji viliwasili mara moja ili kufanikisha ufukuaji kifusi linaenda kwa haraka na vizuri,” alisema Kamanda Shana.Alisema watu watatu waliofariki, walikuwa wamefunikwa na ngema iliyobomoka kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa kuamkia siku hiyo na wawili walijeruhiwa na kukimbizwa hospitalini. Alishukuru Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ), mgambo, viongozi mbali mbali na jeshi lake kwa kufanya kazi hiyo kuwa rahisi. Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro alisema hiyo ni mara ya pili kwa machimbo hayo kuporomoka na kusababisha maafa.Kwamba mwaka 2013 hali kama hiyo ilijitokeza na kuua watu 13 na wengine kadhaa kujeruhiwa. “Lakini katika tukio hili watu watatu waliofariki baada ya kufukiwa na gema lililobomoka kutokana na mvua zilizonyesha usiku wa jana na wawili walijeruhiwa na gema tu na tumewakimbiza hospitalini,” alisema. Shuhuda wa ajali hiyo, Ruben Jacob ambaye ni mchimbaji wa moramu Moivaro, alisema aliona gari linapakia moramu chini ya machimbo hayo, ila ghafla alisikia kishindo kikubwa cha kuanguka kwa gema na kufunika watu.“Viongozi mbali mbali walipofika niliona miili mitatu imetolewa chini ya kifusi na watu wawili walikimbizwa hospitalini kwa matibabu,” alisema Jacob. Meya wa Halmashauri ya Jiji la Arusha, Calist Lazaro alisema taarifa ya kufukiwa kwa watu hao, aliipata asubuhi na alijaribu kusambaza taarifa kwa viongozi wenzake, ambao walitoa mashine za kuchimba kifusi ili kuokoa watu hao. “Wizara ya Madini kama imetoa leseni ya uchimbaji sisi jiji tutachukua ushuru, ila sina hakika sababu machimbo haya yalifungiwa, lakini nitafuatilia baada ya shughuli hizi kuisha,” alisema.
kitaifa
Na ZAINAB IDDY-DAR ES SALAAM TIMU ya taifa ya vijana walio chini ya miaka 17, Serengeti Boys, leo inarusha karata yake muhimu dhidi ya Niger katika mchezo wa Kombe la Afrika kwa vijana nchini Gabon. Mchezo huo utafanyika katika Uwanja wa Port Gentil mjini Port Gentil, ambapo kikosi hicho kikiwa kimevuna poibnti nne katika michezo yake miwili ya awali, ikianza kupata suluhu dhidi ya Mali Mei 15, mwaka huu kabla ya kuifunga Angola mabao 2-1. Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema kuwa mchezo huo ni muhimu kupata matokeo ili kujiweka katika nafasi ya kucheza hatua inayofuata. “Tumejiandaa vema kuwania nafasi ya angalau kuingia nusu fainali,” alisema Shime. Naye Nahodha wa timu hiyo, Dickson Job aliwatoa shaka Watanzania akisema vijana wote wako vema kwa ajili ya mchezo huo kwani mpira wa miguu kwao ni ajira kwa manufaa ya yao binafsi, familia na taifa ambalo limewatua Gabon kutafuta Kombe la Mataifa ya Afrika. Serengeti Boys inahitaji sare ya aina yoyote ili iweze kuvuka huku Niger ambayo ina pointi moja ikiburuza mkia katika Kundi B.
michezo
Katika mechi hiyo Simba ililazimika kusawazisha dakika 10 kabla ya kumalizika mchezo kupitia kwa Brian Majwega baada ya Mwadui kuongoza kwa karibu muda wote wa mchezo kwa bao lililofungwa na Nizar Khalfan.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya mtandao jana, Kerr alisema anajua mashabiki wa timu hiyo wanatamani kushinda hivyo wanajipanga kupata ushindi katika mechi zijazo.“Najua Simba wanahitaji ushindi, lakini matokeo ya sare ni moja ya matokeo kwenye mchezo, wachezaji wangu jana (juzi) walicheza kwa jitihada wawezavyo lakini mchezo wa soka ndivyo ulivyo,” alisema.Alisema anaendelea kurekebisha makosa yaliyojitokeza katika mechi zilizopita ili Januari Mosi wapate ushindi kwenye uwanja wa Ngwanda Sijaona dhidi ya Ndanda ya Mtwara. Baada ya mechi hiyo Simba itacheza na Mtibwa Sugar Januari 16 baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Mapinduzi Zanzibar.Simba ina pointi 24 ikiwa nyuma ya Yanga kwa pointi tisa, Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 33 ikifuatiwa na Azam yenye pointi 32 na Mtibwa Sugar ikiwa nafasi ya tatu kwa pointi 27.
michezo
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM KITUO cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimesema haki ya uhuru wa kujieleza na kukusanyika iko shakani, kutokana na kuwapo kwa udhaifu katika sheria mbalimbali. Hapa nchini uhuru wa kujieleza unalindwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 18 na mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo taifa limeridhia. Akizungumza jana wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Kulinda Uhuru wa Kujieleza na Kukusanyika, Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa LHRC, Ana Henga, alisema uhuru wa kujieleza ni muhimu kwani unaweza kulitoa taifa kutoka hapa lilipo na kuliwezesha kusonga mbele. Kampeni hiyo imeandaliwa na kituo hicho kupitia mradi wa uhakiki kwa kushirikiana na wadau washirika ambao ni Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Baraza la Habari (MCT), Policy Forum, Twaweza, Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo Afrika (WiLDAF) na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. “Watu wengi wanaogopa kujieleza, vyombo vya habari vinafungiwa kwa ujumla hali si nzuri, uhuru wa kujieleza na kukusanyika uko katika hatihati. “Baada ya Serikali kukataza mikutano ya kisiasa mpaka mwaka 2020 utaratibu wa kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi kabla ya kukusanyika umegeuzwa na kuwa si taarifa tena bali ni kuomba idhini au kibali jambo ambalo linapingana na katiba ya nchi,” alisema Henga. Alisema wameamua kuendesha kampeni hiyo baada ya kubaini changamoto kadhaa zinazofifisha uhuru wa kukusanyika nchini ambazo ni uzuiaji holela wa mikusanyiko. Nyingine ni mkanganyiko wa sheria, matumizi holela ya nguvu katika kutawanya mikusanyiko, kukosekana kwa utaratibu maalumu katika matumizi ya maeneo ya wazi na kukataliwa kukusanyika. Naye Mwakilishi kutoka MCT, Paul Malimbo, alizitaja sheria kinzani kuwa ni Sheria ya Takwimu ya mwaka 2015, Sheria ya Huduma za Vyombo vya Habari ya mwaka 2016 na Sheria ya Makosa ya Mtandaoni ya mwaka 2015 na kupendekeza zifanyiwe marekebisho kuendana na Katiba na mikataba ya kimataifa na kikanda ambayo taifa limeridhia. Kwa mujibu wa Malimbo, sheria ya takwimu inazuia mjadala juu ya usahihi wa takwimu, inazuia watu na taasisi kuchapisha taarifa zao wenyewe na kuyumbisha uhuru wa kujieleza kwa kuwaisha watu adhabu ya kifungo na kulipa faini. Naye Mwenyekiti wa TEF, Theophil Makunga, alisema uhuru wa kujieleza na kukusanyika ni muhimu hasa kwa waandishi wa habari kwani huwarahishia kupata habari. “Tunashiriki kwenye kampeni hii ili kuwafanya watu wajieleze tupate habari na kuandika, vyombo vya habari tunatakiwa tupate habari kwa serikali na watu wote sasa wasipozungumza tutakosa cha kuandika na matokeo yake tutashindwa kufanya kazi. “Mfumo wa vyama vingi tumeukubali wenyewe kama jamii hivyo, haiwezekani baada ya miaka 25 tafiti zionyeshe serikali inabinya upinzani, si sifa nzuri kwa nchi ni lazima tuuruhusu uzungumze,” alisema Makunga. Kampeni hiyo iliyobeba kaulimbiu ya ‘Bila uhuru wa kujieleza na kukusanyika hatuwezi kuendelea’ni ya nchi nzima na inatarajiwa kuhitimishwa Novemba mwaka huu.
kitaifa
 MWANDISHI WETU WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amepokea hundi ya Sh bilioni 1.1 kutoka Kampuni ya Uchimbaji Madini Geita (GGML) ili kukabiliana na mapambano dhidi ya maambukizi ya corona. Akipokea hundi hiyo, Ummy alitoa wito kwa viwanda vya ndani kuchangamkia fursa za uzalishaji wa vifaa tiba na kinga dhidi ya ugonjwa wa Covid-19 kutokana na fedha zinazochangwa na kampuni mbalimbali nchini.  Ummy alisema hayo jana Dar es Salaam wakati akipokea hundi hiyo kutoka GGML ambayo mbali na kutoa fedha hizo pia imeandaa mikakati kadhaa kudhibiti corona nchini. Alisema Serikali inaendelea kuthamini msaada mkubwa unaotolewa na wadau hao katika kuonyesha jitihada za kuwalinda watumishi wa afya walio mstari wa mbele kudhibiti maambukizi. “Niwaombe wadau wanaotoa misaada kutoka nje ya nchi kuzingatia mwongozo wa upokeaji wa dawa na vifaa tiba kwa kuhakiki ubora. Tutaendelea kuelekeza TMDA, kuhakikisha wanaongeza umakini uhakiki na usalama, kumekuwa na wimbi la uingizaji wa vifaa tiba, lazima kuhakikisha ni salama na vina vigezo vinavyohitajika. “Pia natoa wito kwa viwanda vya ndani kwamba tunahitaji sana barakoa, PPE, sanitizer, hela hii ielekezwe kununua vifaa vinavyozalishwa ndani ya nchi, mfano barakoa za ndani ya nchi, kuna kiwanda Pugu, uwezo bado mdogo,” alisema Ummy. Akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi hiyo, Makamu Rais, Maendeleo Endelevu GGML, Simon Shayo alisema kampuni yao pia imezindua mikakati kadhaa ya kupambana na janga hili ambalo lilibisha hodi hapa nchini Machi 16, mwaka huu na kuathiri zaidi ya watu 400 hadi kufikia sasa. Alisema mikakati hiyo inalenga kushirikiana na Serikali pamoja na wataalamu wa afya kuelimisha jamii kuhusu virusi vya corona ikiwa ni pamoja na kugawa vifaa kwa jamii inayozunguka mgodi na wafanyakazi wa GGML kujikinga dhidi ya ugonjwa huo. “Kwanza tumekabidhi hundi hii ya Sh bilioni 1.1, ni sehemu ya Sh bilioni 1.6 fedha ambazo GGML imetoa katika kutekeleza mikakati mbalimbali ya kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini. “Fedha hizi Sh bilioni 1.1 zitaelekezwa kwenye ngazi ya kitaifa kupitia mfuko maalumu wa mapambano dhidi ya Covid–19 ambao unasimamiwa na ofisi ya Waziri Mkuu. “Hata hivyo, fedha nyingine kiasi cha Sh milioni 500 zinatumika kwa ajili ya kusaidia juhudi zinazofanywa katika ngazi ya mkoa na jamii, zitakazojumuisha ununuzi wa vifaa-tiba muhimu na vitendea kazi kama vile vifaa vya kujikinga, barakoa, mashine za kusaidia upumuaji,” alisema Shayo. Pia alisema GGML ilikabidhi matanki 10 yenye ujazo wa lita 1,000 kila moja yaliyowekwa kwenye sehemu za wazi za mji wa Geita ili kuwawezesha wananchi kunawa mikono.  “GGML pia imetoa kimiminika cha klorini ambacho kinatumika kutakasa mikono badala ya sabuni. “Mradi huo pia unawezeshwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira ya Mjini Geita (Geuwasa) ambayo itatoa maji kila mara ili kuhakikisha kuwa huduma hiyo inapatikana kwa umma wakati wote.  “Matanki hayo ambayo ni sehemu ya usambazaji wa msaada huo yamewekwa katika maeneo yafuatayo: Kituo cha mabasi (2), Kituo cha Mwatulole (1), Kituo cha Shilabela (1), Kituo cha Nyankumbuko (1), Soko la Nyankumbuko (1), Hospitali ya Geita (1), Soko la Dhahabu (2) na kituo cha Moyo Watoto Yatima cha Huruma (1),” alisema Shayo. Aidha, aliongeza kuwa katika kujenga uelewa kuhusu janga hili kwa jamii zinazozunguka mgodi, GGML imekuwa ikigawa vipeperushi vyenye taarifa za virusi vya corona ndani na nje ya mgodi.
afya
KIBALI cha kukariri kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora, kimeleta kizaazaa na kusababisha wanafunzi 11 wa kidato cha nne kutolewa chumba cha mitihani na kuingizwa katika karandinga na kupelekwa kituo cha polisi.Tukio hilo lilitokea Ijumaa saa 2.15 asubuhi katika shule hiyo ambayo wanafunzi walichukuliwa kupelekwa kituoni, na saa 5 asubuhi walitolewa kupelekwa kwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa (RCO) na waliachiliwa saa 2 usiku walipoitwa wazazi wao na kuambiwa hatima yao wataipata kupitia shuleni.Mkurugenzi Mwendeshaji wa shule hiyo, Richard Magessa alithibitisha kizaazaa hicho na kudai kilichofanyika kwa wanafunzi wao kilikuwa sio sahihi kwani hao ni halali na taarifa zao zipo ofisini na wana sifa za kufanya mitihani. Aliwataja wanafunzi walizuiliwa kufanya mitihani kuwa ni Simon Kaugila, Said Mabuyu, Jasmin Ally, John Benjamin, Abdulmaliki Said, Ramadhani Majuto, Yona Yuda, Regina Kasanga, Said Nuru, Juma Hassan na Ramadhani Nasibu.Alibainisha kuwa vibali hivyo hutolewa na Kitengo cha Elimu Mkoa na Usajili kwa kawaida unaanza Januari kila mwaka na baada ya kusajili Baraza la Mitihani la Taifa hufika mikoani kwa ajili ya kupata taarifa za watoto.Mkurugenzi huyo alisema Necta walifika Aprili katika Ofisi ya Elimu Mkoa na walikabidhiwa nyaraka mbalimbali zinazowahusu watoto na kama kuna makosa huwa wanatakiwa kuorodheshewa taarifa kama sio sahihi.Alisema changamoto hizo ni namba halisi za matokeo kidato cha pili, orodha ya masomo yanayotakiwa kufanya kwa kila mtahiniwa na vibali vya kukariri kwa watahiniwa waliokariri kidato cha tatu, lakini wanafunzi hao waliondolewa pasipo na maelekezo yoyote.Kwa upande wao, wazazi na wananchi waliokuwepo katika maeneo hayo, walidai wamesikitishwa kwa Ofisa Elimu Sekondari Manispaa ya Tabora, Chatta Luleka, kuchukua maamuzi hayo ya kufika shuleni hapo akiongozana na gari la polisi na kuwatoa wanafunzi kwenye chumba cha mtihani na kuwalazimisha kuingia kwenye gari hilo.Walidai ofisa huyo alitakiwa kutoa maelekezo mapema ili uongozi wa shule waufanyie kazi na sio kukurupuka kuwatoa wanafunzi kwenye vyumba vya madarasa kama watuhumiwa, hivyo kuwatia wasiwasi.Wazazi hao ambao hawakutaka kutaja majina yao kwenye vyombo vya habari, walidai wamedhalilishwa watoto wao kwa sababu shule hiyo kwa sasa inafanya vizuri na walipata tuzo na kikombe cha ushindi na walimu watatu walipewa pongezi katika mwaka 2015, 2016 hadi 2017.
kitaifa
EVANS MAGEGE N LEONARD MANG’OHA-DAR ES SALAAM KANISA Katoliki nchini limewaelekeza waumini wake kufunga, kufanya hija, mikesha na maombi maalumu kwa lengo la kuombea mvua. Pamoja na hilo, kanisa hilo limewaelekeza viongozi wake kuadhimisha misa kwa lengo hilo hilo. Maelekezo hayo yametolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa kanisa hilo (TEC), Askofu Tarcsius Ngalalekumtwa, kupitia barua yenye kumbukumbu namba ya TEC/PR/ 1/2017 iliyoandikwa Januari 13, mwaka huu kwenda kwa maaskofu wote wa kanisa hilo. “Ni kipindi cha mvua za kilimo katika maeneo yetu mengi lakini hali ya hewa siyo ile tuliyoizoea. Mvua hazifiki kuruhusu shughuli zetu za kilimo kuendelea na baadhi ya maeneo tayari yana uhaba mkubwa wa chakula. “Ninaomba kasi ya sala iwepo pote nchini. Mungu aliyewatunza wana wa Israeli walipokuwa safarini kuelekea nchi ya ahadi kwa kipindi cha miaka 40, atuangalie kwa wema, huruma na upole. Tuombe baraka juu ya kazi zetu za kilimo, tukayapate mazao ya nchi tuweze kumtumikia Mungu kwa mioyo yenye utulivu na shukrani,” inasomeka barua hiyo. Katika barua hiyo yenye kichwa cha habari ‘Ukame nchini’ ambayo pia ina saini ya Askofu Ngalalekumtwa inawaelekeza viongozi wake kuadhimisha misa za kuomba mvua, kuwepo kwa hija, mfungo, mikesha na maombi maalum kwa lengo hilo huku ikisisitiza kuwa; aombaye hupewa. Katika hatua nyingine baadhi ya waumini wa Kanisa Katoliki kupitia Jumuiya zao jana asubuhi walieleza kujulishwa juu ya jambo hilo. Mmoja wa waumini aliyezungumza na gazeti hili alisema wamejulishwa kufanya ibada za kuombea mvua lakini pia nchi na viongozi wake. Gazeti hili lilimtafuta Askofu Ngalalekumtwa kwa njia ya simu ili kuthibitisha kama tamko hilo ameliandika yeye ambapo alisema: “Mimi nimewaandikia maaskofu basi ndio kazi yangu”. Askofu Ngalalekumtwa ambaye yupo mkoani Iringa alipoulizwa kama kuna msukumo wowote wa kuandika barua hiyo kwa sasa alijibu kwa kumhoji mwandishi wa habari hizi akisema: “Ulichokisoma ni kweli au si kweli? Kuna mvua au hakuna?” Wakati Kanisa Katoliki likija na uamuzi huo, Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini (TMA), imesema maeneo mengi yamepata mvua za vuli chini ya wastani na kwa kuchelewa hivyo kuathiri mfumo wa kawaida wa mvua hasa katika maeneo ambayo yamekuwa yakipata mvua mara mbili kwa mwaka. Kutokana na hilo, Mtaalamu wa kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, amewataka wakulima kuacha kulima mahindi na badala yake wajielekeze kwenye mazao yanayostahimili ukame. Akizungumza na MTANZANIA Jumapili, Meneja Ofisi Kuu ya Utabiri, Samwel Mbuya, alisema kuchelewa kwa mvua hizo ambazo zilitarajiwa kuanza kati ya Septemba na Oktoba mwaka jana katika baadhi ya mikoa nchini, zilisababisha mikoa hiyo kukabiliwa na vipindi virefu vya kiangazi tofauti na ilivyozoeleka. Aliitaja baadhi ya mikoa iliyokumbwa na ukosefu mkubwa wa mvua uliokwamisha kufanyika kwa shughuli za kilimo ni pamoja na Dar es Salaam, Morogoro na mikoa yote ya Kanda ya Ziwa. Alisema pia mvua zilizokuwa zikitarajiwa katika baadhi ya maeneo ambayo hupata mvua za vuli kuanzia Novemba zimenyesha kwa kiwango cha chini na kwa kuchelewa. “Lakini kuanzia Januari hii na Februari tunatarajia mvua za msimu zitaanza hasa katika maeneo ambayo hupata mvua mara moja kwa mwaka lakini zitakuwa za wastani, ambapo kwa mikoa ya Dodoma na Singida kutakuwa na mvua za chini ya wastani hali inayotegemewa pia katika mikoa ya Ruvuma na Mtwara,” alisema Mbuya. Mbuya alisema maeneo mengi ambayo muda wa mvua za vuli umepita wasitegemee kupata mvua za uhakika na kuwataka wananchi kuendelea kufuatilia taarifa na maangalizo yanayotolewa na TMA ili kufahamu hali ya mwelekeo wa mvua katika siku zijazo. Aliitaja baadhi ya mikoa inayotarajiwa kupata mvua hizo zinazotarajiwa kunyesha kati ya mwezi huu na ujao kuwa ni pamoja na Tabora, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Iringa. Katika taarifa aliyoitoa kwa gazeti hili ilionyesha kuwa mvua za kati ya Oktoba na Desemba mwaka jana zilinyesha chini ya wastani katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kaskazini Mashariki ikijumuisha mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara. “Mvua za chini ya wastani zimenyesha pia katika maeneo ya ukanda wa Pwani ya Kaskazini mikoa ya Pwani, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, visiwa vya Pemba na Unguja,” ilieleza taarifa hiyo. Alipotafutwa Mtaalamu wa Kilimo kutoka Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Lilian Mpinga, kuelezea hali hiyo ya mvua na mwelekeo wake katika masuala ya kilimo, aliwataka wananchi kujielekeza kulima mazao yanayostahimili ukame. “Mazao yanayopaswa kulimwa ni yale yanayostahimili ukame ambayo ni mihogo, viazi vitamu, uwele, mbaazi lakini mazao kama mahindi hayafai kulimwa wakati huu kutokana na kuhitaji kiasi kikubwa cha mvua,” alisema Mpinga. Awali, Meneja huyo wa TMA akizungumzia hali ya upepo uliokuwa ukivuma baharini kiasi cha kusababisha ajali ya jahazi lililokuwa likitoka Tanga kuelekea Pemba na kukatisha maisha ya zaidi ya watu 12 mwanzoni mwa wiki hii, alisema kwa sasa hali imerejea kawaida. “Ni kweli kulikuwa na upepo mkali uliosababisha kuwapo kwa mawimbi makubwa na baada ya kuona hali hiyo tulitoa angalizo siku mbili kabla ya siku ya tukio lile ambapo kulikuwa na viashiria vilivyoonyesha kuwapo upepo mkali kati ya Januari 10 na 12. “Lakini hali imerejea kawaida kama kutakuwa na mabadiliko na kukawa na kuimarika kwa mfumo wa upepo ambao mwanzo ulionekana kuimarika na upepo kuvuma kutoka Kaskazini mwa Bahari ya Hindi tutatoa taarifa,” alisema.
kitaifa
ENDAPO ningembiwa kitu gani nikibadilishe kwenye tasnia ya muziki nchini basi ningebadilisha upepo wa Bongo Fleva uende sawa na muziki wa Dansi, muziki mama uliozaa aina zote za miziki unazozisikililiza. Miaka ya 80 wakati haijulikana kama kuna muziki utazaliwa unaoitwa Bongo Fleva, muziki wa Dansi ulikamata sehemu kubwa ya jamii, vijana wa zamani mpaka wazee wa wakati huo waliuhusudu muziki huu. Hakukuwa na lugha chafu zinazoweza kuvuruga maadili ya jamii yetu, hakukua na video zinazoonyesha sehemu kubwa ya miili ya wanawake ikiwa wazi ndiyo maana jumbe zilizosokotwa kwenye nyimbo zile zilifika mubashara kwa watu wote. Sasa leo hii Bongo Fleva imetawala, muziki wa Dansi umeminywa na vyombo vya habari vimeutenga muziki huu, nauliza hivi ikitokea Dansi ikafa kabisa mamilioni ya mashabiki wake mtawapeleka wapi? Ni kweli Dansi ya zamani na ya sasa imekuwa tofauti, wanamuziki wa zamani waliimba kulingana na mazingira ya wakati ule hata hawa wanamuziki wa sasa wanapiga muziki kulingana na mazingira ya sasa lakini hawapati nafasi ya kusikika sababu Bongo Fleva imepewa kipaombele. Nafurahi kuona Sikinde Ngoma ya Ukae wanajaribu kukimbizana na wakati. Akina Mjusi Shemboza wanakung’uta gitaa kwa uhodari ili kukishawishi kizazi hiki cha dotcom kielewe muziki ni nini. Maisha ya msanii wa Bongo Fleva na mwanamuziki wa Dansi yana utofauti mkubwa. Bongo Feva imewekwa kibiashara hivyo ni lazima vijana hawa watengeneze fedha ila upande wa muziki wa Dansi ni tofauti. Dansi ni muziki wenye mashabiki wengi ila tatizo bado wadau hawajauweka katika levo za kibiashara ndiyo maana wanamuziki wake hawanufaiki kama wale wana Bongo Fleva. Hivi sasa wasanii wa Bongo Fleva wanauza kazi zao kimtandao na kupata diliza matangazo kwenye kampuni mbalimbali lakini wanamuziki wa Dansi hutegemea maonyesho pekee. Kuna ulazima madereva wanao iendesha Bongo Fleva wakaushika pia usukani wa muziki wa Dansi ili mambo yawe sawa kwa wanamuziki wote
burudani
HISTORIA ya aina yake imeandikwa katika sherehe za miaka 58 ya Uhuru wa Tanzania Bara na miaka 57 ya Jamhuri, zilizofanyika kwa mara ya kwanza katika Kanda ya Ziwa, na mkoani Mwanza.Kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza jana, uwanja huo na maeneo ya jirani vikiwamo Viwanja vya Furahisha, kuliandikwa historia kutokana na kufana kwa sherehe hizo, zilizohanikizwa na burudani mbalimbali za kwaya, muziki wa kizazi kipya, wa jadi (Sungusungu), gwaride, halaiki na maonesho ya ndege vita.Historia hiyo inatokana na ukweli kwamba katika sherehe za jana, mambo ya msingi ya kitaifa yalipewa kipaumbele cha pekee na Rais John Magufuli na viongozi wengine wa kitaifa.Mbali ya Rais Magufuli, sherehe hizo zilihudhuriwa na Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hasssan, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, maspika Job Ndugai (Bunge la Tanzania), Zubeir Ali Maulid (Baraza la Wawakilishi Zanzibar).Pia walikuwapo majaji wakuu, Profesa Hamis Juma (Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na Othman Makungu (Zanzibar) pamoja na marais wastaafu Benjamin Mkapa na Ali Hassan Mwinyi, mawaziri wakuu wastaafu Mizengo Pinda, John Malecela, Edward Lowassa na Frederick Sumaye.Lakini pia walikuwapo viongozi wa vyama vya upinzani akiwamo Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, ambaye hii ni mara yake ya kwanza kuhudhuria sherehe za kitaifa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani 2015.Mbowe alifuatana na viongozi wake mbalimbali wakiwamo wabunge John Mnyika (Kibamba), John Heche (Tarime Vijijini), Godbless Lema (Arusha Mjini) na aliyekuwa Mbunge wa Ilemela, Ezekiel Wenje na aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu. Viongozi wengine wa upinzani walikuwa ni John Cheyo (UDP), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF), John Shibuda (ADA-TADEA), Mwenyekiti wa Chama cha Wakulima (AFFP), Said Soud Said na Hamad Rashid Mohammed (ADC).Mambo yaliyofanya sherehe hizo kuwa za kihistoria ni pamoja na uamuzi wa Rais Magufuli, kuwasamehe wafungwa 5,533, idadi ambayo ni kubwa na haijawahi kutokea katika historia ya nchi hii.Wafungwa hao waliosamehewa ni wale walioko magerezani kwa kufungwa kuanzia siku moja hadi mwaka mmoja, waliofungwa miaka mingi kuanzia miaka mitano hadi 30 waliobakiza mwaka mmoja kumaliza vifungo vyao. Rais Magufuli alisema ametoa msamaha huo kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 45(1)(a-b) na Sheria ya Magereza Kifungu cha 49 Sura ya 58.Uamuzi huo wa kihistoria wa Rais kusamehe idadi kubwa ya wafungwa, pia unatokana ziara yake ya hivi karibuni kwenye Gereza Kuu la Butimba mkoani Mwanza ambako alishuhudia msongamano mkubwa wa wafungwa na mahabusu, lakini pia hali hiyo iko katika magereza yote nchini. Alisema kwa mujibu wa takwimu alizo nazo, kuna jumla ya wafungwa 17,547 na mahabusu 18,256 nchini, hivyo kufanya jumla yao wote kuwa 35,803.“Pia Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) na Waziri wa Katiba na Sheria wamefanya kazi kubwa na kuwasamehe mahabusu 345 na waliokuwa wanakabiliwa kesi mbalimbali na 256 wa kesi za uhujumu uchumi, kwa hiyo watu 601 wameachiwa huru,” alieleza Rais Magufuli.Aliwataka wanufaika wa msamaha huo, kujutia makosa yao na wasirudie makosa au kusiwepo na mtu mwingine yeyote, kufanya makosa akidhani atapa msamaha.Idadi ya waliosamehewa kila mkoa Aliitaja mikoa na idadi ya wafungwa na mahabusu waliosamehewa kwenye mabano kuwa ni Kagera (713), Dodoma (385), Morogoro (365), Mara (260), Mbeya (259), Kigoma (252), Tanga (245), Geita (230), Rukwa (214), Arusha (208) na Manyara 207.Mikoa mingine ni Tabora (207), Mwanza (190), Ruvuma (181), Singida (139), Simiyu (136), Lindi (299), Pwani (128), Iringa (110), Songwe (96), Katavi (74), Shinyanga (74) na Njombe 70.Alisema wanufaika wa msamaha huo, wataanza kutoka magerezani leo. Rais alimkabidhi Kamishna Jenerali wa Magereza, Phaustine Kasike orodha ya wafungwa wote watakaonufaika na msamaha huo.Alimkabidhi orodha hiyo papo hapo mbele ya umati. Viongozi watoa kauli Jambo jingine la kihistoria kwenye sherehe hizo jana ni uamuzi wa Rais Magufuli kuwapa nafasi ya kuzungumza viongozi mbalimbali, wakiwamo wastaafu na viongozi wastaafu.Sherehe za Uhuru zilizoeleka kuwa ni za gwaride tu na shughuli nyingine chache bila ya kuwapo kwa hotuba, lakini katika miaka ya karibu, kiongozi wa nchi amekuwa akitumia kutoa hotuba, lakini jana akaenda mbali zaidi na kuwapa nafasi wastaafu, wapinzani na viongozi wengine kusalimia wananchi. Miongoni mwa walioongumza ni marais wastaafu Mkapa na Mwinyi, lakini pia Rais wa Zanzibar, Dk Shein, mawaziri wakuu wastaafu Pinda, Lowassa, Malecela na Sumaye, pamoja na viongozi kadhaa wa upinzani.Viongozi hao kwa sehemu kubwa walisisitiza umuhimu wa kudumisha amani, umoja, mshikamano na kufanya kazi ili taifa liondokane na utegemezi.“Mimi nawahimiza Watanzania wote tuendelee kudumisha umoja, amani na tufanye kazi kwa bidii,” alisema Mkapa aliyewasalimu wananchi kwa salamu yake iliyokuwa maarufu wakati wa utawala wake, akisema “Mambo.”Kwa upande wake, Mzee Mwinyi aliyekuwa maarufu kwa jina la “Ruksa” wakati wa utawala wake kati ya mwaka 1985 hadi 1995, alianza kwa kuonesha umahiri wake katika lugha ya Kiswahili, akionesha utofauti wa matumizi ya maneno ya “Nawapongezeni na “Nawapongeza.”Lakini ujumbe wake, ulikuwa ni kukubali kazi kubwa na nzuri inayofanywa na Rais Magufuli, akimpongeza. Aliwataka Watanzania kumwombea dua Rais ili jicho la wabaya lisimdhuru, lakini pia alisisitiza umuhimu wa kuendelea kutunza amani, umoja na usalama wa nchi.Naye Lowassa ambaye mwaka 2015 alipambana na Dk Magufuli kuwania urais akiwa na Chadema kabla ya kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM) hivi karibuni, aliwataka Watanzania wamuunge mkono Rais Magufuli kwani mtindo wake wa uongozi, utaletea taifa maendeleo makubwa katika kipindi chake cha miaka 10.Sumaye ambaye kama Lowassa alikimbilia Chadema mwaka 2015, kabla ya kujitoa wiki iliyopita, akidai kufanyiwa ‘figisu’ katika kuwania Uenyekiti wa Kanda ya Pwani na ule wa Taifa wa Chadema, alisema kama taifa bado kuna kazi kubwa ya kufanya ya kupata uhuru wa kiuchumi ili kuondokana na utegemezi.Cheyo wa UDP na Profesa Lipumba wote walipongeza kazi kubwa, inayofanywa na Rais Magufuli, na kuwataka kuendelea kuwaunga mkono. Hamad Rashid ambaye ni Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, alizungumzia suala la kulinda amani na Muungano wa pande mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia viongozi hao wa vyama vya upinzani, wakiongozwa na Mbowe, walitaka sherehe hizo zisaidie kuwepo na maridhiano ya kisiasa na utengamano wa kisiasa na kuimarisha demokrasia.“Miaka 58 ya Uhuru ni uthibitisho kwamba kuna haja ya kuwepo kwa maridhiano, mshikamano na upendo kati yetu, siku ya leo ifungue milango ya kupendana, maridhiano yatakayotusaidia katika kujenga taifa letu,” alisema Mbowe ambaye pia ni Mbunge wa Hai mkoani Kilimanjaro.Mbowe alisema Rais Magufuli ana nafasi ya pekee ya kujenga maridhiano na utengamano nchini.Sherehe Kanda ya ZiwaKatika kuvunja mazoea, serikali iliamua sherehe hizo kufanyika Kanda ya Ziwa katika Mkoa wa Mwanza. Hiyo ni historia kubwa iliyobebwa na sherehe za miaka 58 ya Uhuru, kwani mara nyingi sherehe hizo hufanyika Dar es Salaam na Dodoma. Rais Magufuli aliwasifu wananchi wa Kanda ya Ziwa, kwa kujitokeza kwa wingi ndani na nje ya Uwanja wa CCM Kirumba katika sherehe hizo. Alisema haijapata kutokea.“Ikumbukwe kuwa hatukufanya sherehe hizi kwa miaka miwili, mwaka 2015 na mwaka 2018 na badala yake fedha zake zilifanya kazi za maendeleo,” alisema Rais Magufuli.“Hivyo hivyo ndio sababu tukaamua tufanye sherehe hizi mkoani Mwanza tofauti na ilivyozoeleka, hii ni kwa sababu ya kubadili mazoea.”Alisema sherehe hizo huambatana na fursa mbalimbali, kuchochea maendeleo ya mkoa huo. Jambo jingine la kihistoria lililopamba sherehe hizo jana ni kundi la wananchi wa kabila la Wasukuma 1,200 walioingia uwanjani, wakiwa wamevalia mavazi ya asili.Wasukuma hao ni walinzi wa jadi maarufu Sungusungu. Wakiwa uwanjani hapo walicheza na kuimba na kuzunguka uwanja, hali iliyonogesha zaidi sherehe hizo.Watanzania wapongezwaKatika hatua nyingine, Rais Magufuli amewapongeza Watanzania kwa maendeleo waliyoyapata katika miaka 58. Alisema mafanikio hayo ni matokeo ya kazi nzuri, inayofanywa na Watanzania wenyewe. Katika hilo, aliwataka Watanzania wote kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili matunda ya kuwa huru kisiasa, yatoe mbegu bora ya kuwa huru kiuchumi.Aliyataja baadhi ya mambo makubwa ya kimaendeleo, yaliyofanyika katika kipindi cha miaka 58 ya Uhuru ni ujenzi wa kilometa 12, 679.55 za barabara za lami kutoka kilometa 360 za lami wakati nchi inapata Uhuru, kilometa zingine zaidi ya 2,400 zinajengwa na zingine 7,087 zipo katika hatua mbalimbali za kuanza kujengwa.Kuhusu sekta ya afya, alisema vituo vya kutolea huduma ya afya, alisema vimeongezeka kutoka 1,095 wakati tunapata Uhuru hadi kufikia 7,293 kwa sasa, lakini pia wataalam katika sekta mbalimbali nao wameongezeka.Nafasi ya Tanzania kimataifa Kwa mujibu wa Rais Magufuli, katika kusherehekea miaka 58 ya uhuru, Tanzania inajivunia kwa mchango ilioutoa kimataifa ikiwemo ukombozi wa Bara la Afrika, kutafuta amani na kujenga mtangamano, kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Pia alisema katika miaka 58 ya Uhuru, Tanzania imekuwa na mahusiano mazuri na mataifa mbalimbali duniani.
kitaifa
Na NORA DAMIAN – DAR ES SALAAM WAKATI mchakato wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuwapata wagombea watakaopeperusha bendera ya chama hicho kwenye uchaguzi mkuu wa Oktoba ukitarajiwa kuanza kesho, joto linaonekana kuanza kupanda. Katika uchaguzi wa mwaka huu, mchuano mkali unatarajiwa kuwa ndani ya chama haswa kwenye nafasi ya Urais wa Zanzibar, ubunge, uwakilishi na udiwani. Ratiba iliyotangazwa juzi na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, imegeuzwa kuwa ajenda katika mitandao ya kijamii huku wengi wakihoji iwapo wataibuka wanachama watakaotaka kupambana na Rais Dk. John Magufuli ambaye anatarajiwa kuomba tena ridhaa ya chama chake kuwania ngwe ya pili. Hata hivyo hali hiyo haitarajiwi sana kwasababu CCM ina utaratibu wa kumpitisha rais anayemaliza muhula wake wa kwanza kugombea tena miaka mitano bila kupingwa. Kwa upande wa Zanzibar kumekuwa na mjadala nani atapewa kijiti cha kumrithi Rais wa sasa, Dk. Ali Mohamed Shein, anayemaliza kipindi chake cha pili hasa baada ya kuwapo wanasiasa mbalimbali wanaotajwa kutaka kuwania nafasi hiyo. Katika dakika za lala salama wanaotajwa kugombea wamekuwa wakipigana vikumbo huku baadhi yao wakitumia upepo wa shughuli mbalimbali kujinadi kiaina na wengine wakionekana kufanya harakati za kimya kimya ili kujitengenezea mtaji wa kura katika vikao vya ndani ya chama. Kiongozi mmoja mwandamizi wa CCM aliliambia MTANZANIA Jumapili kuwa, “huku Bara hakuna shida kazi imeshaisha, gumzo liko Zanzibar subirini.” Rekodi zinaonyesha mbali ya Dk. Shein marais wengine waliowahi kuiongoza Zanzibar ni Sheikh Abeid Amani Karume (1964-1972),  Sheikh Mwinyi Aboud Jumbe (1972-1984), Ali Hassani Mwinyi (1984-1985), Idris Abdul Wakili (1985-1990), Salmin Amour (1990-2000) na Amani Abeid Karume (2000-2010). Rais wa kwanza wa Zanzibar, Abeid Amani Karume,  alipata wadhifa huo baada ya kutokea mapinduzi yaliyosababisha kupinduliwa kwa Sultani wa mwisho wa Sultan Jamshid bin Abdullah Januari 1964. Miezi mitatu baadaye, Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilianzishwa na Karume akawa makamu wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku Mwalimu Julius Nyerere akiwa Rais. Jina la Karume lilirejea tena baada ya Amani Abeid (mtoto wa Karume) kuchaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na kuingia madarakani Novemba 2000 hadi Novemba 2010. WANAOTAJWA ZANZIBAR Miongoni mwa wanaotajwa kuwania urais Zanzibar ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, Balozi Ali Karume, Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Masauni na Waziri wa Viwanda upande wa Zanzibar, Balozi Amina Ali ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 alijitokeza kuwania nafasi ya kuteuliwa kugombea urais wa Jumuhuri ya Muungano wa Tanzania. Katika orodha hiyo yumo pia aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Zanzibar, Dk. Khalid Salum Mohamed, ambaye aliondolewa kwenye wadhifa huo Machi 3 mwaka huu baada ya kile kilichoelezwa kukaidi agizo la chama chake la kutoanza kampeni kabla ya wakati. Mbali na hao, pia wanatajwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Abood, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Issa Haji Ussi Gavu na Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan. Hata hivyo Agosti 26, mwaka huu, Samia alisema hana nia ya kuwania urais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. urais Zanzibar. UBUNGE, UDIWANI UWAKILISHI Kulingana na ratiba iliyotolewa juzi wanaotaka kugombea ubunge, uwakilishi, udiwani na viti maalumu watachukua na kurejesha fomu Julai 14 hadi 17 mwaka huu. Wanachofanya makada wengi hivi sasa hasa wale wanaotajwa kutaka kugombea nafasi hizo ni kutafuta ushawishi au ‘kiki’ ya kuwafanya waonekane ili kujitengenezea mtaji wakati wa vikao vya ndani na nje ya CCM.  Wengine wamekuwa wakiitumia kwa kasi mitandao ya kijamii kujipambanua kwa kueleza yale waliyotekeleza wakati wakiomba kura mwaka 2015. Wamo pia baadhi ya wabunge wa kuteuliwa na wale wa Viti Maalumu ambao pia ni mawaziri wameonyesha dalili ya kutaka kugombea majimbo mbalimbali. Mapema wiki hii wakati akihitimisha hotuba ya Makadirio ya Mapato ya Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2020/21, Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango, ambaye ni mbunge wa kuteuliwa alisema; “Watanzania msisahau kumpatia rais wetu wabunge na madiwani wanaomudu maadili na mwendo wa Hapa Kazi Tu…na kama itawapendeza wananchi wenzangu wa Buhingwe na chama chetu (CCM) basi iwe pamoja na mimi mtumishi wenu. Jimbo la Buhingwe kwa sasa linaongozwa na Albert Obama. Katika kile kinachoonekana ni kumjibu Dk Mpango,  Obama, wakati akichangia bajeti hiyo alisema wananchi wa Buhingwe wanajua alipowatoa na atakapowapeleka na ana imani atapitishwa tena na CCM kugombea jimbo hilo. “Ukija kwenye orodha ya majina yangu bungeni utaambiwa Obama anaitwa nani, utaambiwa ni mashine ya jimbo, mashine ya kusaga na kukoboa, jina la nne utakaloambiwa kwangu ni simba wa yuda la mwisho ni katapila. “Naomba hayo majina yawe katika ‘hansard’ ya Bunge, Buhingwe wanajua tulikotoka, tuliko na tunakoelekea. Niseme 2020 Magufuli hapa, Obama hapa,” alisema Obama. Wachambuzi wa kisiasa wanasema uamuzi wa baadhi ya wabunge wa kuteuliwa na wale wa viti maalumu kuamua kuingia ‘mzima mzima’ katika kinyang’anyiro hicho unachochewa pia na rekodi zao za kiutendaji. RATIBA ILIVYO Kwa mujibu wa Polepole, kwa upande wa Tanzania Bara tukio la kwanza litakuwa ni uchukuaji fomu kwa nafasi ya kiti cha urais, litakaloanza Juni 15 hadi 30 mwaka huu. Alisema tukio la pili ambalo litakwenda sambamba na muda huo wa siku 15 ni utafutaji wa wadhamini mikoani. Alisema tukio la tatu litakuwa ni vikao vya uchujaji, ambapo Julai 6 hadi 7 mwaka huu, kitaketi kikao cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, kitakachoanzisha mchakato wa uchujaji, kisha Julai 8 mwaka huu kitaketi kikao cha Kamati ya Usalama na Madili ya Taifa chama hicho. “Julai 9 mwaka huu, kitaketi Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, ambacho kitatoa mapendekezo yake kwa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM juu ya majina ya wanachama wasiozidi watano, wanaoomba kugombea nafasi hiyo ya urais,”alisema Polepole. Vilevile Polepole alisema Julai 10 mwaka huu, Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kitapendekeza kwa Mkutano Mkuu wa CCM, majina yasiyozidi matatu ya wanachama wa chama hicho, wanaoomba kugombea urais. Katibu huyo wa itikadi na uenezi wa CCM, alisema Julai 11 hadi 12 mwaka huu, Mkutano Mkuu wa CCM Taifa utachagua jina moja la mgombea wa urais wa Tanzania. ZANZIBAR Kwa upande wa Zanzibar, Polepole alisema Juni 15 hadi 30 mwaka huu itakuwa ni tukio la uchukuaji fomu na kurejesha. “Juni 15 hadi 30 mwaka huu, kutafuta wadhamini mikoani, baada ya hapo vitafuata vikao vya uchujaji, Julai 1 hadi 2 mwaka huu, itaketi Sekretarieti ya Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya Taifa Zanzibar, Julai 3 kitaketi kikao cha Kamati ya Usalama na Maadili Zanzibar,”alisema Polepole. Polepole alisema Kikao cha Kamati Maalumu ya Halmashauri Kuu ya CCM kitakuwa Julai 4 mwaka huu kwa ajili ya kutoa mapendekezo juu ya wanachama waliojitokeza kuomba kugombea urais wa Zanzibar. “Kikao hicho kitafuatiwa na Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri ya Taifa kitakachoketi Julai 9 kwa ajili ya kupendekeza majina matatu ya wanachama wanaoomba kugombea kiti hicho. Kisha, Julai 10 mwaka huu, Halmshauri Kuu ya Taifa ya CCM kitachagua jina moja la mgombea. Aidha alisema Julai 11 hadi 12, Mkutano Mkuu wa CCM taifa utaketi kwa ajili ya kuthibitisha jina la mwanachama atakayesimama katika uchaguzi wa
kitaifa
 Na ASHA BANI – Dar es Salaam WACHIMBAJI, wauzaji na wasafirishaji wadogo wa madini, wamemwomba Rais Dk. John Magufuli kuondoa zuio la kusafirisha mchanga wenye madini alilolitoa wiki iliyopita, baada ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam. Pia wachimbaji hao wamesikitishwa na hatua ya watendaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini, kumpotosha Rais kuwa makontena yaliyozuiwa bandarini yana mchanga wa dhahabu, badala ya mchanga wenye madini mengine, ikiwa ni pamoja na shaba, chuma, salfa, mercury na nickel. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, kiongozi wa wachimbaji wa madini ya nickel kutoka Dodoma, Thobias Rweyemamu, alisema tangu Machi 2, mwaka huu walizuiwa kusafirisha mchanga na mawe jambo ambalo limewasababishia hasara kubwa. Alisema hata shughuli za uzalishaji katika maeneo ya machimbo zimesimama na kusababisha hasara ya Sh milioni 4 kila siku. “Tunapata hasara kubwa tangu Machi 2, tunapoteza Sh milioni 4 kila siku, wachimbaji waliokuwa wanaendelea na shughuli zao wamesimama, hali imekuwa ngumu, tutashindwa kuendesha maisha, familia zetu zinatutegemea na kundi kubwa la vijana migodini… hali hii ikiendelea tutawafanyaje?” alihoji Rweyemamu. Alisema hadi sasa wachimbaji wadogo zaidi ya 110 wamezuiliwa, huku mchanga wenye nickel zaidi ya makontena 60 na copper makontena saba yakiwa na mchanganyiko wa madini yamezuiliwa. Rweyemamu alisema kutokana na hali hiyo, bado wanaingia hasara ya kulipia ushuru wa Dola za Marekani 20 kila siku ambazo ni  sawa na Dola 12,000 kwa mwezi jambo linalowatia gharama kubwa. Alisema wamekuwa wakifanya biashara hiyo kwa miaka mingi, baada ya kupata vibali halali kutoka Wizara ya Nishati na Madini na wapo kihalali si kama ilivyoelezwa. Mchimbaji mwingine, Paul Kaliyemba, alisema Rais Magufuli alipotoa agizo hilo, hawakupaswa kuchanganywa na maelezo ya wataalamu wa wizara. Kaliyemba alisema wanafanya biashara hiyo kihalali, hata wizara inatambua kwa sababu leseni zilitolewa na Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) na  walifanya ukaguzi na kujiridhisha. Alisema kutokana na hali hiyo, wamemwandikia barua Rais Magufuli kupitia Wizara ya Nishati na Waziri Mkuu kupitia upya uamuzi wao na wachimbaji wadogo waruhusiwe kuendelea na biashara yao. Kuibuka kwa wachimbaji hao, kumetokana na Rais Magufuli kupiga marufuku usafirishaji wa mchanga wenye madini ya dhahabu kwenda nje ya nchi. Kutokana na agizo hilo, Rais Magufuli aliagiza Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) kuzuia makontena 262 yenye mchanga unaodaiwa kuwa na madini usisafirishwe kwenda nje ya nchi. Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Deusdedit Kakoko, alisema baada ya Rais kushuhudia makontena hayo, Alhamisi iliyopita walianzisha operesheni maalumu na kubaini makontena 262 yaliyokuwa na mchanga wa dhahabu tayari kwa kusafirishwa nje. Alisema makontena hayo ni mali ya mgodi wa Buzwagi, unaomilikiwa na Kampuni ya Acacia yaliyokuwa yamehifadhiwa bandari kavu ya Mofed iliyopo Kurasini, Temeke. Hata hivyo, Meneja Uhusiano wa Acacia, Asa Mwaipopo, alisema makontena hayo ni ya mchanga wa madini ya shaba na yalifikishwa bandarini kabla ya zuio la Rais Magufuli. 
kitaifa
MANCHESTER, ENGLAND STAA wa mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Manchester City, Leroy Sane, ameweka wazi kuwa hana tatizo na kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Low, baada ya kumwacha kwenye michuano ya Kombe la Dunia. Mshambuliaji huyo wa pembeni alitikisa vyombo vya habari siku chache kabla ya kuanza kwa Kombe la Dunia nchini Urusi, huku jina lake likiachwa kati ya wachezaji 23 wa timu taifa ambao walikwenda kwenye michuano hiyo, wakati huo Sane aliweza kuipa ubingwa Manchester City na kutwaa uchezaji bora chipukizi na alitoa pasi 15 za mabao na mwenyewe akifunga mabao 10. Hata hivyo, Ujerumani hawakuweza kufanya vizuri na kujikuta wakitolewa katika hatua ya makundi, lakini mchezaji huyo ameweka wazi kuwa hana tatizo na kocha huyo kutokana na kumwacha na tayari alifanya mazungumzo naye. “Nilifanya mazungumzo na Joachim Low, bila shaka nilikubaliana na maamuzi yake, alinipa sababu sahihi za kuniacha na ndio maana kila kitu kipo sawa na wala sina tatizo naye. “Nilijisikia vibaya baada ya kuona wanatolewa kwenye hatua ya makundi, najua ni jambo ambalo liliwaumiza wengi,” alisema Sane.
michezo
ABDUCADO EMMANUEL NA MITANDAO DIMBA la White Hart Lane linatarajia kuwaka moto kesho saa 9.00 alasiri kwa mchezo wa watani wa jadi wa jiji la London ‘London Derby’, wakati wenyeji Tottenham Hotspur watakapoikaribisha Chelsea katika Ligi Kuu England. Kuelekea mchezo huo, Kocha wa Tottenham, Mauricio Pochettino, ameanza kuuona mgumu kufuatia timu yake kutopata muda mwingi wa kujiandaa ukilinganisha na Chelsea. “Tunakabiliana na timu ngumu, katika hali hii Chelsea ambayo inazo siku tatu zaidi za kujiandaa kuliko sisi ambao tunayo moja. Hii inawapa faida wapinzani wetu. Tunatakiwa kukubali kanuni za mchezo, lakini tunahitaji kusema nini ni kweli kuhusu sisi,” alisema Pochettino. Hiyo inatokana na timu zote hizo kucheza katikati ya wiki hii, Spurs ikicheza juzi dhidi ya Qarabag na kuifunga bao 1-0 kwenye Kombe la Ligi ya Europa na Chelsea ikakipiga na Maccabi Tel Aviv Jumanne iliyopita na kuichapa mabao 4-0 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya. Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho, yeye kwa upande wake ameendelea kupatwa na kicheko kufuatia mwenendo mzuri wa timu yake hivi sasa. “Ni jambo la muhimu na tunafurahia kushinda mechi zetu mbili zilizopita (Norwich City na Maccabi Tel Aviv). Naamini itatuongezea hali ya kujiamini. Ni jambo la muhimu kwa sababu tulicheza mechi nyingi bila ushindi mfululizo. Kufanya hivyo ni jambo zuri.” Hata hivyo, Chelsea inaweza kuwa kwenye wakati mgumu dhidi ya Spurs kutokana na rekodi bora waliyonayo kwa sasa wakiwa hawajapoteza mechi yoyote ya ligi, toka walipofungwa na Manchester United katika mchezo wa ufunguzi (1-0). Vile vile Spurs imeimarika hivi sasa baada ya straika wake tegemeo, Harry Kane, kuanza kuonyesha makeke yake ya msimu uliopita kufuatia kuanza vibaya msimu huu mpaka sasa amefunga mabao tisa ndani ya mechi sita zilizopita. Kane, 22, ana rekodi nzuri dhidi ya Chelsea ikiwa ni baada ya kufunga mabao mawili wakati Spurs ikiwalaza matajiri hao mabao 5-3 msimu uliopita kwenye siku ya Mwaka Mpya. Kwa upande mwingine, Chelsea imeanza msimu huu vibaya baada ya kufungwa michezo saba kati ya 13 waliyocheza mpaka sasa, matokeo ambayo yamemweka kwenye presha kubwa Mourinho ya kutimuliwa ndani ya kikosi hicho. Msimu uliopita kwenye mechi zao mbili baina yao zilitengeneza jumla ya mabao 11, hiyo inaonyesha kuwa safu ya ulinzi ilikuwa katika wakati mgumu sana na kutokana na vipaji vya washambuliaji wa pande zote mbili, mabao yanatabiriwa kufungwa leo. Winga wa Chelsea, Eden Hazard, amefunga mabao kwenye mechi tatu za mwisho dhidi ya Spurs, huku Kane naye akifunga mawili katika mchezo wa mwisho waliokutana. Uwepo wa wakali Kane, Christian Eriksen, Mousa Dembele na Mkorea Son Heung-min kwenye eneo la ushambuliaji la Spurs, unatarajia kuwaweka kwenye wakati mgumu mabeki wa Chelsea hasa rekodi yao ikionyesha kuwa wameruhusu mabao 23 ndani ya mechi 13 za ligi msimu huu. TAARIFA ZA KLABU Spurs itamkosa kiungo wake Dele Alli, ambaye atakuwa akitumikia adhabu ya kukosa mchezo mmoja baada ya kukusanya kadi tano za njano huku pia ikitarajia kuwakosa Erik Lamela, Nabil Bentaleb, Nacer Chadli na Alex Pritchard walio majeruhi. Chelsea itamkosa nahodha wake, John Terry, aliyeumia kwenye mchezo uliopita dhidi Maccabi Tel Aviv ya Israel. REKODI ZAO Chelsea imefungwa mechi tano na kushinda mmoja kwenye michezo saba iliyopita ya ligi waliyocheza ugenini, pia imeshinda mmoja tu kati ya tisa iliyopita katika Uwanja wa White Hart Lane. Mshambuliaji wa Spurs, Kane, amefunga mabao saba katika mechi nne zilizopita za ligi, pia imepiga mashuti mengi yaliyolenga lango msimu huu kuliko timu nyingine yoyote ya ligi hiyo. Spurs imepoteza mechi mbili tu kati ya 20 zilizopita walizocheza kwenye uwanja wa nyumbani. Huku Chelsea ikifunga mabao matatu tu katika mechi zake nne zilizopita za ligi. Kiungo wa Chelsea, Cesc Fabregas, ametengeneza mabao 11 dhidi ya Spurs, matano zaidi ya timu nyingine yoyote kwenye ligi hiyo. Mechi nyingine kali kesho, Liverpool iliyokuwa kwenye makali tokea ianze kunolewa na Mjerumani, Jurgen Klopp, itawaalika Swansea ndani ya Uwanja wa Anfield huku Arsenal ikisafiri kuwafuata Norwich, zote zikichezwa saa 1.15 usiku.   LEICESTER V MAN UNITED Wakati shughuli hiyo ikiwa pevu kesho, leo saa 2.00 usiku kutakuwa na mtanange mwingine mkali kwa vinara wa ligi, Leicester City kuwakaribisha Manchester United walio nafasi ya pili kwenye Uwanja wa King Power. Kocha wa Leicester City, Muitaliano Claudio Ranieri, atakuwa akiangalia tena namna wachezaji wake watakavyopambana na vigogo hao, akichagizwa na kasi nzuri ya nyota wake, Jamie Vardy na Riyad Mahrez. Vardy ambaye ni mshambuliaji anaamini ya kuwa leo atavunja rekodi ya nyota wa zamani wa Man United, Ruud van Nistelrooy, kwa kufunga bao la 11 mfululizo baada ya kuifikia rekodi ya Mholanzi huyo ya kufunga mabao 10. Akiwa na mabao 13 mpaka sasa kileleni kwenye ufungaji bora ndani ya mechi 13, Mwingereza huyo amekuwa na msimu mzuri sana akiisaidia Leicester kuongoza ligi kwa pointi 28 huku United wakiwa nazo 27. MAN CITY V SOUTHAMPTON Shughuli nyingine pevu itakuwa kwenye Uwanja wa Etihad kwa Manchester City kuwakaribisha Southampton, zote zikitoka kupoteza mechi zao zilizopita, Saints ikifungwa na Stoke City bao 1-0 huku Man City ikipigwa na Liverpool mabao 4-1.   Saints chini ya kocha Ronald Koeman, ina rekodi nzuri msimu huu, ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja ugenini ikishinda miwili na sare nne, ikiwemo ule walioichapa Sunderland kwenye mchezo wake wa mwisho wa ugenini.   City yenyewe ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 26 sawa na Arsenal, imeshinda mchezo mmoja kati ya minne iliyopita ya ligi, pia imepoteza mechi iliyopita ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa kufungwa na Juventus bao 1-0 jijini Turin, Italia.   Msimu uliopita, Saints ilifungwa na City mabao 3-0 nyumbani, lakini vijana wa Manuel Pellegrini wakapoteza mchezo Etihad kwa kupigwa na Southampton 2-0.   Nyota wa Saints, Jay Rodriguez, ataukosa mchezo huo baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake mwanzoni mwa wiki hii, itamkosa pia staa wake, Graziano Pelle, anayetumikia adhabu, huku Fraser Forster na Florin Gardos nao wakiendelea kukosekana.   City itamkosa kipa wake tegemeo Joe Hart, nahodha Vincent Kompany, walio majeruhi huku mabeki Pablo Zabaleta na Eliaquim Mangala wakiwa kwenye hati hati ya kucheza, lakini itawapokea kiungo wake nyota David Silva na mshambuliaji Wilfried Bony, watakaorejea dimbani.  
michezo
  Na Eliya Mboneya, Arusha Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu(AfCHPR), imesema Mahakama za ndani Tanzania katika kesi ya kubaka na kulawiti iliyokuwa inamkabili mwanamuziki Nguza Viking (Babu Seya) na mwanawe Johnson Nguza (Papii Kocha) zilitenda haki kwa kiwango kikubwa na kwa upande mwingine zilikiukwa. Aidha, kutokana na kukiukwa kwa baadhi ya haki zao hizo, mahakama hiyo imewaruhusu kuwasilisha hoja na kuainisha ni namna wanaweza kuomba fidia kulingana na haki zao ziliokiukwa ndani ya siku 30 huku upande wa Jamhuri ukitakiwa kujibu hoja hizo ndani ya siku 30. Akitoa hukumu hiyo katika mahakama hiyo leo Ijumaa Machi 23, Kiongozi wa majaji nane waliokuwa wakisilikiza shauri hilo, Gerald Niyungeko mbele ya Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Sylvain Ore, amesema baadhi ya haki zilizotendwa ni pamoja na kuwaachia watuhumiwa watatu kwenye kesi hiyo pamoja na kubakiza mashitaka manne kati ya 21 yaliyokuwa yakiwakabili. “Haki zao hazikukiukwa kulingana na uamuzi uliotolewa na mahakama za ndani za Tanzania kwa kuwaachia washtakiwa wengine na kupunguza mashtaka 21 hadi manne, lakini kwa upande mwingine zilikiukwa, kwa mfano wakiwa Mahakama ya Halimu Mkazi Kisuti walikaaa mahabusu kwa siku nne bila kufahamishwa makosa yao lakini pia hawakuwa na wakili wa kuwatetea. “Aidha, waleta maombi pia waliomba kupimwa mkojo na damu ili kuthibitishwa kama waliwaingilia wale watoto ambao upande wa jamhuri ulidai waliambukizwa magonjwa ya zinaa lakini walikataliwa. “Kwa upande mwingine, Nguza aliomba kupimwa kama ana uwezo wa kufanya tendo la ndoa au lakini pia alikataliwa,” amesema Jaji Niyungeko. Hata hivyo, kuhusu kupinga kifungo cha maisha, Jaji Niyungeko amesema mahakama haikujielekeza katika shauri hilo kwa sababu waleta maombi wako huru kwa msamaha wa rais hivyo haikuona sababu ya kushughulikia hilo kwani wako nje kwa mujibu wa sheria. Babu Seya na Papii Kocha waliachiwa kwa msamaha wa rais Desemba 9, mwaka jana kutokana na kifungo cha maisha jela walichohukumiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Juni mwaka 2004 baada ya kumkuta na hatia ya kunajisi na kulawiti watoto 10 ambapo walikata rufaa Mahakama za juu na kugonga mwamba na hivyo kulazimika kukimbilia AfCHPR wakidai haki zao zilivunjwa.
kitaifa
Na Florence Sanawa, Mtwara Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mtwara Mjini (MTUWASA), imeanzisha utaratibu mpya ya kulipia madeni yake kwa njia ya elektroniki kupitia mtandao wa simu za mkononi (NMB Mobile) ili kurahisisha ukusanyaji madeni katika Manispaa ya Mtwara Mikindani. Akizungumza na na waandishi wa habari Ofisa Biashara wa MTUWASA, Judith Namwereni amesema ukusanyaji huo kwa njia ya kielektroniki utaongeza hamasa kwa watu wengi kutumia huduma hiyo. “Wateja wetu ni wengi ndiyo maana tumefanya mazungumzo na benki hii ili kurahisisha ukusanyaji wa mapato hata ukiangalia watumiaji wa benki kwa sasa ni wengi kwa hiyo ili kuwapunguzia safari ya kuja kulipa ofisini sasa wanaweza kulipia kupitia simu zao za kiganjani huduma hii inaenda na wakati na iko kidigitali zaidi. “Wako watu wanatumia maji hadi miezi sita bila kulipa huenda ikawa umbali sasa tumerahisisha ili kupunguza mlundikano wa madeni uliokuwepo waone umuhimu wa kulipia huduma ya maji wanayopata kupitia mamlaka hii,” amesema. Kwa upande wake Meneja Uhusiano wa Benki ya NMB, Kanda ya Kusini, Haji Msingwa amesema kutokana na idadi kubwa ya Watanzania kutumia simu za mkononi itaongeza hamasa kwa wateja wa mamlaka hiyo kulipia maji kupitia NMB mobile. “Tumejipanga kuhakikisha kila kijiji na kata anakuwapo Wakala wa NMB Mobile ili kurahisisha watumiaji wa huduma hiyo kufanya malipo na mihamala mbalimbali ili twende kidijitali zaidi na kuacha njia za zamani ambazo zimekuwa zikipoteza muda kwa wateja wetu,” amesema Msingwa
kitaifa
KLABU ya Yanga imewatuliza mashabiki wake kufuatia kutolewa katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika ikisema kazi haijaisha wanajipanga upya kwa ajili ya Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho Afrika. Yanga imetolewa na Zesco United ya Zambia kwa jumla ya mabao 3-2, wakitoka sare nyumbani ya bao 1-1 na kufungwa ugenini mabao 2-1 na hivyo kuangukia Kombe la Shirikisho. Akizungumzia mipango yao jana, Ofisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli (pichani) aliwaomba mashabiki kusahau yaliyopita na kuungana kuiunga mkono timu kuelekea katika michezo ijayo. “Tumepokea matokeo kwasababu ni sehemu ya mchezo, bado tuna kazi kubwa naamini umoja wetu upo, tuendelee kuisapoti timu kwa hali yoyote kwa kuangalia na michuano iliyoko mbele yetu,”alisema. Kikosi hicho tayari kimewasili Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Polisi Tanzania utakaochezwa kesho.Bumbuli alisema hawatakuwa na muda wa kumpumzika timu itafanya maandalizi ya mchezo huo na mwingine dhidi ya Coastal Union ili kupata matokeo mazuri.Yanga ilianza vibaya ligi msimu huu baada ya kupoteza mchezo wake wa kwanza dhidi ya Ruvu Shooting kwa bao 1-0 huku ikielezwa sababu huenda wana kikosi kipya kisichokuwa na muunganiko mzuri.
michezo
KOCHA wa AFC Leopards Casa Mbungo ameondoka klabuni hapo baada ya kusitisha mkataba wake. Kocha huyo mnyarwanda jana alikwenda mazoezini na kuwaaga wachezaji na wafanyakazi wenzake.“Nitawakumbuka, nitaikumbuka Kenya. Tafadhali endeleeni kufanya kazi kwa bidii, hamuwezi kujua kitakachokuja mbele,” Mbungo aliwaambia wachezaji wake.Mbungo ameondoka kwenye klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Kenya kutokana na kukumbwa na ukata. Amelazimika kusitisha mkataba wake baada ya kutolipwa mshahara wake kwa miezi mitano na huku akidaiwa kudai malimbikizo ya mshahara wake zaidi ya sh milioni mbili za Kenya.Ametoa siku 15 kwa klabu hiyo kumlipa fedha zake vinginevyo atawashitaki kwa Shirikisho la soka la kimataifa, Fifa. AFC Leopards kwa siku za karibuni imekumbwa na ukata na haijalipa wafanyakazi wake tangu SportPesa ilipositisha mkataba nao tangu Agosti mwaka huu.“Inasikitisha safari hii kuisha hivi, tumejifunza mengi kutoka kwako, yatabaki kwenye fikra zetu, Mungu akuvariki kocha Andre Casa Mbungo,” alisema nahodha wa timu hiyo Robinson Kamura.Kocha msaidizi Anthony Kimani anatarajiwa kuiongoza Leopards katika mechi ya mwishoni mwa wiki dhidi ya Zoo Kericho mjini Kakamega
michezo
Mwenyekiti wa Shiwata, Cassim Taalib alisema jana kuwa kikao cha Kamati Utendaji ya Mtandao huo kilichoketi juzi kilifikia uamuzi huo baada ya kufuatilia kwa karibu mafanikio ya Samatta akiwa na timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu yake ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na kufanya vizuri katika mashindano ya Afrika hadi kuchaguliwa kuwa mchezaji bora.Alisema Shiwata inatoa kiwanja hicho kama zawadi kwa mchezaji huyo kutokana na uwezo wake wa kulitangaza taifa katika medani ya kimataifa katika mchezo wa soka ambako wengine watafuata nyayo zake.Taalib alisema taratibu za makabidhiano zinafanywa kwa mawasiliano na baba yake mzazi, Ali Samatta na atakabidhiwa eneo hilo mara baada ya kurudi kutoka Ubelgiji ambako anaenda kusaini mkataba na timu ya KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji.Shiwata yenye wanachama zaidi ya 8,000 inamiliki ekari 300 za kujenga makazi, kumbi za starehe, viwanja vya michezo na nyumba za kuishi katika kijiji cha Mwanzega wilayani Mkuranga na ekari 500 eneo la Ngarambe kwa ajili ya kilimo.
michezo
MKUU wa Wilaya ya Chemba, Saimon Odunga amesema kesho watazindua utaratibu wa ugawaji wa vitambulisho vya wajasiriamali baada ya kupitisha vigezo ambavyo wanaona wanaweza kupata wajasiriamali.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu, Odunga alisema sifa ambazo zimewekwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekuwa ngumu kupata mjasiriamali, ambaye anastahili kupewa kitambulisho. “Leo (jana) tumekutana na kuangalia utekelezaji wa ugawaji wa vitambulisho kwa kutumia sifa za TRA, tumeona hazina uhalisia na hatutaweza kumpata mjasiriamali hata mmoja wa kupata kitambulisho, hivyo tunaweka vya kwetu.“Tumeona wajasiriamali wa maduka na migahawa na biashara zinazofanana na hizo, tuwaondoe katika orodha ya watu watakaonufaika na tuwalenge hasa wale wanaopanga biashara barabarani,” alisema Odunga. Wakati wakuu wa wilaya wakikabidhiwa vitambulisho na Mkuu wa mkoa, Dk Binilith Mahenge, Meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma, Kabula Mweneri alisema wajasiriamali wanaostahili kupata vitambulisho hivyo ni wale wenye mapato ghafi yasiyozidi Sh milioni nne kwa mwaka.Pia asiwe amewahi kupata Kitambulisho cha Mlipa Kodi (TIN) ya biashara na kutakiwa kujaza fomu maalumu. Odunga alisema baada ya kupitia vigezo vyao, ambavyo ambavyo ni kwa yule anayepanga bidhaa zake chini, watawatumia watendaji wa mitaa kuwabaini wafanyabaishara wa aina yiyo. “Hata wangesema anayepata faida, pia tusingeweza si mama ntilie au machinga, hivyo sheria ya kuwa na mapato ghafi milioni nne imekuwa ngumu, hivyo sisi tumepanga kuwapa wale wanaopanga biadhaa zao chini.Alisema ili utaratibu huo ufanikiwe, leo wanaendesha semina kwa watendaji wa mitaa na vijiji, ili kuwapa mafunzo ya vigezo hivyo ili kesho wazindue rasimu ugawaji wa vitambulisho. Hivi karibuni, Rais John Magufuli alizindua vitambulisho vya wajasiriamali na kuwakabidhi wakuu wa mikoa kwa ajili ya kwenda kuvigawa kwa wajasiriamali wadogo. Mkoa wa Dodoma ulipokea 25,000 na viligawiwa kwa uwiano wa idadi ya watu ambapo Halmashauri ya Jiji imepatiwa vitambulisho 5,000, Chamwino 4,000, Kongwa 3,750, Mpwapwa 3,500 na Bahi vitambulisho 2,750. Pia Halmashauri ya Chemba walipatiwa vitambulisho 2,750, Kondoa Mji 2,500 na Halmashauri ya Kondoa Vijijini ilipata mgawo wa vitambulisho 750.
kitaifa
Na BADI MCHOMOLO UKIWA unakumbwa na msongo wa mawazo mara kwa mara unaweza kufanya mambo ambayo utakuja kuyajutia katika maisha yao kama utashindwa kuwa makini na kufanya maamuzi sahihi juu ya mawazo ambayo yanakusumbua. Wadau wengi wa muziki duniani waliguswa na kifo cha staa wa muziki wa Pop nchini Marekani, Michael Jackson, ambacho kilitokea Juni 25, 2009. Wapo ambao walipoteza fahamu baada ya kupata taarifa ya kifo cha msanii huyo. Msanii huyo aliacha watoto watatu ambao ni Michael Joseph Jackson Jr mwenye umri wa miaka 20, Paris Jackson mwenye umri wa miaka 18 na Prince Michael Jackson II mwenye miaka 15. Kila mmoja kati ya wote hao waliguswa sana na kifo hicho cha baba yao, lakini ilikuwa tofauti kwa Paris ambaye alionekana kama anataka kuchanganyikiwa. Kipindi Jackson anapoteza maisha Paris alikuwa na umri wa miaka 11, alikimbizwa hospitalini baada ya kupata taarifa ya kifo hicho cha baba yake, lakini baada ya muda alirudi katika hali ya kawaida, ila kila mara alikuwa anaonekana akiwa na mawazo, hivyo alikuwa anasimamiwa na wataalamu wa kuondoa mawazo ili aweze kuwa sawa. Tangu hapo alianza kufikiria kuvuta Sigara huku akiwa na lengo la kutaka kupunguza mawazo ya baba yake na kuna wakati alikuwa anafikiria kunywa pombe ili alewe sana na apate usingizi akiwa na lengo la kupoteza ndoto za mara kwa mara juu ya baba yake. Alishindwa kunywa pombe kwa kipindi hicho, lakini aliweza kuvuta sigara kwa kujificha sana, uvutaji wa kujificha mara kwa mara ulimfanya aizoee sigara, lakini baada ya kufikisha miaka 17 alianza kuonekana wazi kuwa anavuta sigara. Majimbo mbalimbali nchini Marekani yamekuwa yakipiga marufuku uvutaji wa sigara kwa vijana wenye umri chini ya miaka 18, hata hapa Tanzania, lakini kwa Paris akiwa na miaka hiyo 17 alikuwa anavuta mitaani na kukumbana na misukosuko ya kila mara na polisi. Alikuwa na furaha sana baada ya Aprili mwaka jana kutimiza miaka 18, hivyo aliamua hatoweza kujificha tena katika uvutaji wa sigara, ni wazi alikuwa anavuta kila kona jambo lililomfanya kuathirika na uvutaji wa sigara. Familia yake ilijaribu kukaa naye pamoja na kumshauri kuachana na uvutaji wa sigara lakini aliwajibu kuwa anatamani kuachana na uvutaji lakini anashindwa kabisa na alianza kuvuta kutokana na kutaka kupunguza mawazo ya baba yake, lakini kwa sasa anashindwa kuacha. “Mawazo yanaweza kukuweka katika mazingira magumu ndani ya maisha yako, wakati nina umri wa kuanzia miaka 11 nilikuwa katika wakati mgumu baada ya kumpoteza baba yangu kipenzi, nilifikiria kufanya mambo mengi ambayo ni mabaya katika maisha yangu kama vile kunywa pombe, kuvuta sigara na mambo mengine. “Lakini kikubwa ambacho nilikifikiria na nikakifanya ni kuvuta sigara, jambo ambalo lilikuwa baya zaidi kwa kuwa nilikuwa na umri mdogo, hivyo limeniharibu na hadi sasa najaribu kutaka kuacha lakini ninashindwa. “Nikikaa muda mrefu bila kuvuta sigara najisikia vibaya, lakini ninaamini kama ningeweza kuzuia hisia zangu katika kipindi cha kifo cha baba yangu basi nisingekuwa kwenye hali nilionayo kwa sasa na sipendi kuwaona vijana wadogo wakifikiria kuvuta sigara,” alisema Paris. Uvutaji wa sigara ni hatari kwa afya, mbali na Paris kujitaja kuwa anashindwa kuachana na uvutaji wapo wengi ambao wameathirika na uvutaji wa sigara na wanashindwa kuacha, hilo ni tatizo.
burudani
MKUU wa Mkoa wa Dodoma, Dk Binilith Mahenge amewaagiza wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo ifi kapo Juni 30, mwaka huu, wawe wamekamilisha ununuzi wa mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato.Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC), Dk Mahenge alisema halmashauri zote saba zinatakiwa kukamilisha ununuaji wa mashine za kukusanyia mapato (POS) na akazipongeza ambazo tayari zimekamilisha ununuzi huo.Amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Muduka Kessy kufuatilia kwa karibu na kuhakikisha halmashauri za Kondoa Mjini, Vijijini, Chemba, Bahi, Jiji, Kongwa, Chamwino na Mpwapwa zinakamilisha ununuzi wa mashine hizo.Dk Mahenge ameipongeza Halmashauri ya Kondoa Vijijini ambayo imenunua mashine 59 na hivyo hakuna kituo cha kukusanya mapato ambacho hakina mashine hiyo.Ameipongeza pia halmashauri ya Kondoa Mjini kwa kuweka lengo la kununua mashine 56 na kuvuka lengo kwa kuongeza mashine tatu zaidi kwa ajili ya kukusanya mapato.Akaziomba zote zilizobaki kuhakikisha kwamba zinakamilisha ununuzi huo, ambapo takwimu zinaonesha kwamba Halmashauri ya Kongwa haijakamilisha mashine 77, kati ya 150 zinazotakiwa, hivyo inatakiwa kutumia fedha za ndani au kukopa ili kupata mashine hizo.Pia takwimu zinaonesha kwamba, Halmashauri ya Chemba bado mashine 65, kati ya mahitaji ya mashine 130, hivyo mikakati madhubuti inahitajika ili kununua mashine zilizobaki.Halmashauri ya Bahi bado mashine 20, kati ya 80 zinazotakiwa kuwapo katika maeneo mbalimbali ya kukusanya mapato katika wilaya hiyo na kuachana na mtindo wa kutumia risiti.Pia aliitaka, Halmashauri ya Chamwino ambayo bado mashine 50, kati ya 120 zinazotakiwa kuwapo katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo, kuhakikisha nayo inakamilisha.“Halmashauri ya Mpwapwa imenunua mashine 110 kati ya mashine 113 na hivyo bado mashine tatu, hivyo inatakiwa kukamilisha idadi ya mahitaji yake kupitia mkakati wa kukamilisha katika robo ya nne ya mwaka (Aprili-Juni),” alisema.Akisoma takwimu katika halmashauri ya Jiji, mkurugenzi wake, Godwin Kunambi alisema ina mashine 339 za kukusanyia mapato ambazo ni zaidi ya malengo ya mashine 336.Alisema mashine zilizoongezeka zimewekwa katika maeneo yaliyobuniwa ya makusanyo ya mapato na mkakati ni kupeleka katika shule ili kuhakikisha kila mapato yanayoingia yanaingizwa kwenye mashine hizo.Alizitaka halmashauri nyingine zilizobaki kuhakikisha zinakamilisha ifikapo Juni 30, mwaka huu, ambao ni mwisho kutokuwa na mashine hiyo, ili kuondoa mwanya wa kupotea mapato ya mkoa.Mkuu wa Mkoa, Dk Mahenge aliwataka viongozi wa halmashauri hasa wakurugenzi kuhakikisha wanatekeleza maazimio yanayofikiwa katika vikao, kwani tayari jambo la kila halmashauri kuwa na mashine hizo lilijadiliwa na kuwekewa maazimio katika vikao vilivyotangulia.
uchumi
MWAMVITA MTANDA-DAR ES SALAAM BAADA ya Simba kupata ushindi wa mabao 2-1 katika mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika ambao umewapa nafasi ya kutinga hatua ya robo fainali, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Patrick Aussems, amesema atapambana kuhakikisha kikosi chake kinachukua ubingwa wa Afrika. Simba ilitinga hatua hiyo baada kupata ushindi katika mchezo huo uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ushindi huo uliifanya Simba kufikisha pointi tisa na kumaliza kwenye nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi hilo nyuma ya Al alhly ya Misri iliyomaliza na pointi 10, JS Soaura iliyomaliza nafasi ya tatu ikiwa na pointi nane, wakati AS Vita ikimaliza mkiani na pointi zake saba. Akizungumza na MTANZANIA jana, Aussems alisema mipango yake kwa sasa ni kuhakikisha wanafanikiwa kuchukua ubingwa wa michuano hiyo. Alisema awali walikuwa na malengo ya kufikia hatua ya makundi ya michuano hiyo, lakini baada ya kufanikiwa alipata morali iliyopelekea asonge mbele zaidi. “Nitapambana kwa hali na mali kuhakikisha kuwa Simba inafanikiwa kuchukua ubingwa, hakuna sababu  ya kuhofia timu yoyote ambayo tutakutana nayo, nina imani timu yangu inaweza na ndio maana mpaka hapa tumefanikiwa kwa kiasi kubwa sana,” alisema Aussems.  “Nataka Simba iweke historia mwaka huu ipate ubingwa wa Afrika na pia ishinde tena michuano ya Ligi Kuu, hata kama nitaondoka basi nitakuwa nimeacha historia nzuri,” alisema Aussems.  Aussems alimmwagia sifa kiungo wake, Haruna Niyonzima, kwa kiwango alichokionesha katika mchezo huo.
michezo
Lulu Ringo, Dar es Salaam Kocha Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema msimu huu wa 2018/2019 ukimalizika ataachana na timu hiyo kutokana na washabiki, wanachama wa klabu hiyo kushindwa kujitolea kuisaidia timu yao. Zahera ameiambia Mtanzania Digital kwamba anashangaa kuona Yanga ikijiita timu ya wananchi na yenye matajiri wengi lakini inashindwa kujisaidia yenyewe. “Mimi nasema hivi ukijisaidia na Mungu anakusaidia, sasa mimi Kocha Zahera nimeamua Ligi hii ikimalizika naweza kuondoka Yanga sababu nimefanya mambo mengi sana kuisaidia timu lakini naona wanayanga wenyewe hawapendi kujisaidia. “Kama nawaambia washabiki na wanachama tuijenge timu yetu sisi wenyewe na hakuna chochote kinachofanyika sitaweza kuendelea hivi,” amesema Zahera. Mwanzoni mwa Februari mwaka huu Kocha Zahera alianzisha kampeni ya kuchangia klabu ya Yanga ambapo amesema pesa itakayopatika itatumika kununua wachezaji na kujenga uwanja wa mazoezi kwa msimu ujao. Mratibu wa klabu ya Yanga, Hafidh Salehe Jana Februari 21, alitanga zaidi ya shilingi milioni 21 ndizo zilizopatika tangu kampeni hiyo kuanzishwa, kiasi kilichoonekana kutomridhisha Kocha Zahera kutokana na mipango mikubwa aliyo nayo baada ya msimu huu kuisha. Zahera amesema anashangaa kuona wanachama na washabiki wa Yanga kuchangia kiasi hicho kwa takribani wiki nne toka kampeni hiyo ilipoanza. “Hao matajiri wengi walioko Yanga kama kila wiki wanachangia Yanga pamoja na wanachama, mashabiki tunauwezo wa kupata fedha nyingi na mwezi wa tano tukanunua wachezaji wazuri na tukajenga uwanja wa mazoezi,” amesema Zahera. “Kinachonishangaza zaidi mashabiki na wanachama wao wanalalamika tu timu inapofungwa, sasa nawaomba wajipange ni jinsi gani watayaepuka maumivu kila mara timu ikicheza wapende kujisaidia wenyewe. “Basi nadhani Mungu hawezi kunilaumu kwa maamuzi ntakayochukua kwa kuamua kuachana na timu ya Yanga maana itakua vigumu sana kuendelea kujitolea wakati watu wao wenyewe hawapendi kujitolea,” amesema Kocha Zahera.
michezo
MANCHESTER, ENGLAND NAHODHA wa klabu ya Manchester United, Wayne Rooney, amedai kwamba wachezaji wanapaswa kulaumiwa na sio kocha wao, Van Gaal. Mshambuliaji huyo amesisitiza kwamba, wachezaji hawachezi kulingana na majukumu yao hivyo lawama anatupiwa kocha badala yao ambao wanatakiwa kuonesha uwezo wao kwa lengo la kuitetea klabu. Mwishoni mwa wiki iliyopita timu hiyo ilishuka dimbani katika mchezo wa Kombe la FA na kufanikiwa kushinda mabao 3-1 dhidi ya wapinzani wao Derby County. Kutokana na ushindi huo, Rooney anaamini kuwa wachezaji wanatakiwa kuwajibika kama timu ina shida au kufungwa na sio kocha wa kutupiwa lawama. “Sio vizuri lawama kutupiwa kocha pale timu inapopoteza mchezo wake, sisi wachezaji tunakuwa uwanjani hivyo tunatakiwa kuonesha majukumu yetu ili kuweza kuibeba timu. “Najua kila mchezaji anaingia uwanjani kwa ajili ya kutafuta ushindi, lakini kama hachezi kufuatana na majukumu yake basi timu haiwezi kushinda kisha kosa linakuja kuwa la kocha badala ya wachezaji,” alisema Rooney. Hata hivyo, kocha wa klabu hiyo, Van Gaal, anaamini kuwa watafanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano hiyo ya Kombe la FA msimu huu.
michezo
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MWANASIASA Mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa, John Shibuda amewataka waliopokea fedha za mgao wa Escrow kuzirejesha. Vilevile alimwomba Rais Dk.John  Magufuli awasamehe. Shibuda ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Maswa Magharibi na  kwa sasa ni Katibu Mkuu wa Chama cha Ada Tadea, alisema dini zote zinasema asamehewe yule ambaye anatubu na kukubali. Alisema   anaona  Ngeleja anatakiwa asamehewe kwa vile  amefanya kitendo cha kishujaa, kukiri  na kuamua kuzirejesha fedha hizo Shibuda ametoa kauli hiyo siku chache baada ya Mbunge wa   Sengerema, William Ngeleja (CCM) kurejesha Sh milioni 40.4 alizopewa na mfanyabiashara, James Rugemalira. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Shibuda alisema kitendo kilifanywa na Ngeleja ni cha kishujaa na anapaswa kusamehewa kwa kuwa ametambua kosa lake mbele ya umma. ‘’Kwa kitendo chake Ngeleja kutubu, tukubali tusiwe na inda na choyo ila wale wengine nao wakubali kuzirejesha fedha na Mheshimiwa Rais awasamehe kama dini zetu zinavyosema, mtu akitubu asamehewe,’’alisema. Wakati huohuo,  Shibuda amewashambulia wapinzani kwa akidai   wanatakiwa kuwa  na ajenda mpya kwa vile  zilizopo, Rais wa sasa Dk. John Magufuli amekwisha kuzitatua kwa kiwango kikubwa. Alisema Serikali ya awamu ya tano imo katika dunia ya mabadiliko ya mila, jadi na utamaduni na kokomesha uzembe. Alisema ajenda ya vyama vya upinzani kama rushwa, ufisadi  imenyauka na kuvitaka kutafuta sehemu ya kutokea. “Vyama vya upinzani kwa sasa ajenda yao ni nini? Ni zile zile za wakati ule Mwalimu   Nyerere aliporuhusu vyama vingi. “Wanasayansi walianza na dawa ya Panadol  lakini leo kuna dawa zaidi ya tatu basi na wapinzani wawe na vikosi kazi vya kubuni tiba mbadala ya kutengua utumishi uliotukuka wa Rais Magufuli,’’ alisema. Shibuda alisema serikali ya awamu ya tano inafanya vizuri huku akidai Taifa limepata Rais mwenye utumishi wachangamfu na kugusa hisia za jamii.
kitaifa
Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amerusha kijembe kwa watani wao jadi Simba kufuatia usajili wa beki Kennedy Wilson Juma kutoka Singida United. Jana kupitia akaunti yao rasmi, klabu ya Simba ilitangaza umsajili beki huyo ambaye ana sifa ya matumizi makubwa ya nguvu awapo uwanjani kutokana na ukubwa wa umbo lake. “Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili. Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi,” taarifa kutoka Simba imeeleza. Kutokana na taarifa hiyo, Dismas Ten hakuwa nyuma kurusha kijembe kama ilivyojadi ya utani wao pindi moja ya timu zinapofanya usajili au tukio lolote lazima upande mwingine uponde.     Jamani fanyeni mumpe hati yule Mnyaturu.. Msije shangaa mnaletewa Sholo Mwamba hapo 😂😂😂😂😂 . . Kutoka kugombania wachezaji na TP Mazembe,Al ahly ,As Vita mpaka Singida United?😂😂😂 Toeni hati jamani..!😂😂😂 . Tunapitia comment Kisha tuta Press Play A post shared by Dismas Ten Sylvester (@dismasten) on Jun 18, 2019 at 4:29am PDT “Jamani fanyeni mumpe hati yule Mnyaturu.. Msije shangaa mnaletewa Sholo Mwamba hapo. Kutoka kugombania wachezaji na TP Mazembe,Al ahly ,As Vita mpaka Singida United? Toeni hati jamani! Tunapitia comment Kisha tuta Press Play,” Ten ameandika Kennedy amesaini mkataba wa miaka miwili na ataitumikia Simba mpaka mwaka 2021.     Ingizo jipya kwenye kikosi cha Mabingwa, beki wa kati Kennedy Wilson Juma amesaini mkataba wa miaka miwili. Uwepo wa Kennedy kwenye kikosi kwa kushirikiana na mabeki wengine tulionao ni hakika safu yetu ya ulinzi itakuwa imara zaidi. #NguvuMoja A post shared by Simba Sports Club (@simbasctanzania) on Jun 18, 2019 at 3:00am PDT
michezo
WAKATI kocha wa Yanga SC, Charles Mkwasa, akiendelea kutupa vijembe vya kuwafunga wapinzani wao Simba SC kwenye mchezo wao wa mwishoni mwa wiki hii, kikosi hicho leo kimetamba kuendeleza makali yake dhidi ya Biashara United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara utakaochezwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.Yanga wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na hasira ya kuendeleza dozi ya kichapo lengo likiwa ni kuongeza idadi ya pointi kutoka 21 na kufikisha 24 na kuishusha Kagera Sugar.Yanga wanaoshika nafasi ya tano wanaingia kwenye mchezo huo wa 11 wakiwa na ari ya ushindi baada ya kuifunga Tanzania Prisons kwa bao 1-0 na kuvunja rekodi iliyowekwa na timu hiyo kushindwa kupoteza mchezo toka walipoanza msimu, wanakutana na Biashara ambayo ina morali ya kuibuka na ushindi kwenye michezo miwili iliyopita licha ya kushika nafasi ya 15 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 15.Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwani toka Biashara imepanda ligi hiyo msimu uliopita ni miongoni mwa timu inayoleta ushindani mkali kila inapokutana na Yanga. Aidha rekodi zinaonesha kwa msimu uliopita timu hizo zilipokutana kwenye michezo ya ligi hiyo Yanga ilishinda mara moja kwa mabao 2-1 Uwanja wa Taifa na mchezo wa mzunguko wa pili Biashara ilishinda kwa bao 1-0 kwenye uwanja wa Karume Mara .Kocha Mkwasa alisema ushindi walioupata kwenye mchezo wa juzi umewapa nguvu na huo ni mwanzo wa kuvuna matokeo mapya kuchagiza mbio zao za ubingwa.
michezo
MKUU wa Jeshi la Polis Nchini (IGP), Simon Sirro amewang’oa rasmi wakuu wa Polisi wa mikoa watatu (RPC), walioachishwa kushika nyadhifa zao na Waziri wa Mambo ya Ndani na Nchi, Kangi Lugola.Hivi karibuni Lugola alitangaza kuwa wakuu hao wa Polisi, wanatakiwa kuachia wadhifa wao kutokana na sababu tatu kuu, ambazo alisema kuwa walishindwa kutokomeza rushwa na kuwalinda wauzaji wa dawa za kulevya na biashara ya magendo. Waliotakiwa kuachia wadhifa wao ni aliyekuwa RPC wa Mkoa wa Kipolisi Ilala, Salum Hamdun, RPC wa Mkoa wa Kipolisi Temeke, Emmanuel Lakula na Mkuu wa Polisi Mkoa wa Arusha, Ramadhan Nganzi.Kwenye uamuzi wake huo wa kuwaachisha wadhifa huo, Lugola aliingia kiundani kwa kusema kuwa kati ya hao, makamanda wawili wametenguliwa kutokana na kukaidi maagizo aliyoyatoa ya kufyeka vichaka vya rushwa katika mikoa yao, huku mmoja anajihusisha na kuwalinda wauzaji wa dawa za kulevya na kusindikiza wafanyabiashara wa magendo. Agizo hilo la Lugola lilionekana kusababisha taharuki hasa ya kisheria, ambapo alikosolewa na wadau mbalimbali wa sheria kuwa hana mamlaka ya kuwatoa kwenye madaraka askari hao.Taharuki iliongezeka zaidi, baada ya askari hao kuonekana wakiendelea na majukumu yao kwa takribani wiki moja tangu waziri huyo alipotaka waachie nyadhifa zao hizo. Wakili Jebra Kambole alizungumza na gazeti hili, ambapo alibainisha kuwa Sheria ya Jeshi la Polisi Sura Namba 322 kama alivyorejewa Mwaka 2002, ndiyo inatoa mamlaka ya Waziri na Mkuu wa Jeshi la Polisi, ambapo Kifungu cha 7(1) cha sheria hiyo kinampa waziri uwezo wa kumpa IGP maelekezo na miongozo mbalimbali. Alisema Kifungu cha 7(2) Cha sheria hiyo, kinampa mamlaka IGP uwezo wa kupanga vikosi vyake na kiwemo kuwapandisha na kuwashusha vyeo.Japo sheria pia inampa uwezo waziri kutoa maelekezo kwa IGP juu ya utendaji kazi huo na kifungu hicho cha sheria kimetumia neno “May” na kwa mujibu wa Sheria ya Tafsiri Tanzania Kifungu cha 53 Sura Namba 1 ya Sheria za Tanzania Kama ilivyorejewa 2002, May lina maana sio sharti la lazima.Alisema waziri hana mamlaka ya kuwaondoa kwenye nafasi zao, bali kumpa maelekezo mwenye mamlaka afanye hivyo, ambaye ni IGP ambaye naye sio lazima atende, kama alivyoambiwa anatumia akili yake na mamlaka yake kuamua hafanyi kama kasuku. Lakini, jana IGP Sirro aliamua kuwango’a rasmi RPC hao wote watatu na kusema kuwa kwa sasa wamerejeshwa makao makuu ya Polisi, kupisha uchunguzi dhidi yao. Uamuzi huo wa IGP Sirro, umemaliza taharuki hiyo, kwa kuwa kwa sasa wanakuwa nje ya wadhifa wao, kama alivyoagiza Waziri Lugola.
kitaifa
Na UPENDO MOSHA, MOSHI BARAZA la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, limepitisha sheria mbili za kudhibiti utumiaji wa mifuko ya plastiki pamoja na kudhibiti ufungaji wa mazao kwa mtindo wa lumbesa. Akizungumza katika kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika jana mjini Moshi wakati wa mjadala wa kupitisha sheria hizo, Meya wa Manispaa hiyo, Raymondy Mboya, alisema sheria  ya kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ina lengo la kulinda mazingira na afya za Wananchi, wakati sheria ya lumbesa inalenga kuwasaidia wakulima kiuchumi. “Halmashauri yetu tumepiga hatua kubwa  kwa kupitisha sheria hii ya kudhibiti matumizi ya mifuko ya plastiki ambayo ina lengo kubwa la kutunza mazingira na afya za wananchi wetu pamoja na sheria ya ufungaji wa mazao kwa mtindo wa lumbesa. “Sheria hii ya Lumbesa itawasaidia wakulima kuuza mazao yao vizuri na kupata faida, tofauti na ilivyo sasa ambapo wafanyabiashara wamekuwa wakiwanyonya wakulima kwa njia hiyo. “Hiyo Sheria ya Lumbesa imepitishwa bila kipingamizi na wajumbe wote wa baraza, wakati sheria ya matumizi ya mifuko ya plasiti imepitishwa kwa kupigiwa kura na madiwani 28 wakiwamo 16 walioikubali na 10 walioikataa. “Matumizi ya mifuko ya plasitii ni hatari kwa afya za wananchi kwani kwa mujibu wa taarifa za wataalamu wa afya, mifuko hiyo imekuwa ikisababisha magonjwa mbalimbali ikiwamo kansa na ugumba. “Kwa hiyo, huu ni wakati wa wananchi kujiandaa kuachana na matumizi ya mifuko hiyo kwa sababu sasa sheria ya kuizuia imepitishwa,” alisema Mboya. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa hiyo, Michael Mwandezi, alisema sheria hizo zitaanza kutumika baada ya mamlaka husika kuzisaini.
kitaifa
NA MOHAMED KASSARA-DAR ES SALAAM MWENYEKITI wa Kamati ya Usajili Simba, Zakaria Hanspope, amesema kwa sasa hayupo tayari kukaimu nafasi ya raisi wa klabu hiyo, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi. Aveva na Makamu wake Kaburu, Juni 28, mwaka huu walipandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka matano ikiwamo kutakatisha fedha, huku wakiwekwa ndani hadi Julai 13, mwaka huu kutokana na makosa hayo kutokuwa na dhamana. Kutokana na tuhuma hizo kuwabili viongozi wa juu wa klabu hiyo waliokuwa wakisimamia shughuli mbalimbali za klabu, baadhi ya mashabiki wametaka jina la  Hanspope kukaimu moja ya nafasi hizo kutokana na kukaa muda mrefu  kwa mujibu wa  Katiba ya Simba. Hanspope ameibuka na kutoa kauli hiyo saa chache baada ya kikao cha Kamati ya Utendaji ya Simba kukutana kwa ajili ya kujadiliana masuala mbalimbali, ikiwemo uendeshaji wa klabu hasa katika kipindi hiki wanachokabiliwa na maandalizi ya msimu ujao. Inaelezwa kuwa idadi kubwa ya mashabiki wanaunga mkono kati ya Hanspope au msaidizi katika Kamati ya Usajili, Kassim Dewji, mmoja kuchukua mikoba ya kuiongoza klabu hiyo hadi pale mambo yatakapokaa vizuri. Akizungumza na MTANZANIA jana, Hanspope aliwataka wanachama wa klabu hiyo kutafuta mtu mwingine sahihi atakayeweza kuingoza Simba kwa kipindi hiki ambacho viongozi wao wamepatwa na matatizo. “Siko tayari kukaimu moja ya nafasi za juu za kuiongoza Simba kutokana na kukabiliwa na shughuli nyingi binafsi ambazo zinanifanya kusafiri mara kwa mara, hivyo muda mwingi sitakuwa karibu na timu. “Wanachama wanatakiwa kuchagua mtu sahihi ambaye ataiongoza Simba kwenye kipindi hiki kigumu cha mpito, hasa ukizingatia sasa hivi tupo katika mchakato wa kujenga kikosi imara kwa ajili ya msimu ujao pamoja na michuano ya kimataifa,” alisema Hanspope.
michezo
MOSCOW, URUSI UFARANSA wamefanikiwa kuingia hatua ya fainali kwenye michuano ya Kombe la Dunia nchini Urusi, baada ya juzi kushinda bao 1-0 dhidi ya Ubelgiji. Ushindani ulikuwa wa hali ya juu katika mchezo huo kutokana na ubora wa kila timu, lakini Ufaransa imeweza kuwazidi wapinzani kutokana na vitu vifuatavyo. Mlinda mlango Hadi kufikia mchezo wa juzi, Ufaransa imeruhusu jumla ya mabao manne tangu kuanza kwa michuano hiyo huku wakiwa wamecheza jumla ya michezo sita. Walikuwa na mlinda mlango ambaye alikuwa kwenye kiwango cha hali ya juu, Hugo Lloris, anayekipiga katika klabu ya Tottenham. Safu ya ulinzi Tangu kuanza kwa michuano hiyo, Ufaransa haijapoteza hata mchezo mmoja kati ya sita waliocheza, walitoka suluhu dhidi ya Denmark katika hatua ya makundi, lakini michezo mingine yote mitano waliibuka na ushindi. Ubora wa safu ya ulinzi ulikuwa unaundwa na beki wa kati, Samuel Umtiti (Barcelona), Raphael Varane (Real Madrid), Benjamin Pavard (Stuttgart), Lucas Hernandez (Atletico Madrid) na wengine. Hao waliweza kumuweka sehemu salama mlinda mlango wao, Lloris, ili asiwe kwenye wakati mgumu. Viungo Wachezaji ambao walikuwa wanaunda safu ya kiungo walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha washambuliaji wake wanalishambulia lango la wapinzani. Katika safu hiyo kulikuwa na N’Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (Juventus), Paul Pogba (Man United) na Corentin Tolisso (Bayern Munich). Wachezaji hao walikuwa kwenye kiwango bora kuhakikisha wanaleta mawasiliano kati ya safu ya ulinzi na ushambuliaji. Kila mchezaji alionekana kuvaa jezi kwa ajili ya kulipigania taifa hilo na kutaka kuandika historia mpya baada ya mwaka 1998 kufanya hivyo. Pogba alikuwa anahakikisha anapiga mipira mirefu ili kuwafikia washambuliaji, kazi hiyo ilikuwa inafanywa na mchezaji mwingine Kante. Washambuliaji Uwepo wa Kylian Mbappe mwenye umri wa miaka 19, akitokea klabu ya PSG, Antoine Griezmann wa Atletico Madrid, kulileta changamoto kubwa kwa safu ya ulinzi ya wapinzani wao katika kila mchezo. Wachezaji hao hadi sasa kila mmoja ana jumla ya mabao matatu. Mbappe alionekana kuwa tishio tangu kwenye mchezo dhidi ya Argentina katika hatua ya 16 bora ambapo Ufaransa ilishinda mabao 4-3, huku mchezaji huyo akifunga mabao mawili na kutoa pasi ya mwisho. Kwa hali ya kawaida Ufaransa imeonekana kuwa na kikosi chenye wachezaji wengi vijana wakiwa na kasi kubwa na hadi sasa wamefunga jumla ya mabao 10. Hata hivyo, kocha wa timu hiyo, Didier Deschamps, amekuwa na lengo la kutaka kuandika historia mpya katika timu hiyo kuwa wa kwanza kutwaa taji hilo mara mbili akiwa mchezaji na kocha. Alikuwa nahodha mwaka 1998 wakati timu hiyo inatwaa ubingwa kwenye ardhi ya nyumbani na sasa ana ndoto ya kufanya hivyo akiwa kocha. Timu inayokutana na Ufaransa katika fainali Jumapili lazima iwe makini katika kuwazuia wapinzani wao katika safu ya ushambuliaji na viungo.
michezo
TRIPOLI, LIBYA MAELFU ya wananchi nchini Libya wamefanya maandamano katika mji mkuu wa nchi hiyo wa Tripoli wakiwa wamevalia vizibao vya njano kama wanavyofanya washiriki wa maandamano ya vizibao vya njano kupinga siasa za kiuchumi za serikali ya Ufaransa, ambapo nao wamelaani mienendo hasi ya Serikali ya Rais Emmanuel Macron dhidi ya nchi yao. Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari nchini humo, washiriki wa maandamano hayo wamelaani vikali operesheni za Jenerali Khalifa Haftar, kiongozi wa kundi linalojiita ‘Jeshi la Kitaifa la Libya’ pamoja na uungaji mkono wa kijeshi wa Ufaransa dhidi ya nchi yao.  “Sisi wazawa wa Tripoli kama walivyo wakazi wa miji mingine ya Libya, tumekuja hapa kuonyesha upinzani wetu kwa utawala wa mtutu wa bunduki wa Haftar na mashambulizi yake,” amesema mmoja wa waandamanaji. Siku chache zilizopita, Shirika la Habari la Al Jazeera liliripoti kwamba, meli ndogo ya kivita mali ya Ufaransa ilituma silaha na zana za kijeshi kwa wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar nchini Libya. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, boti ndogo za mwendo kasi zilitumika kupakua shehena ya silaha kutoka kwenye meli hiyo ya kivita ya Ufaransa.  Aidha wiki iliyopita, Waziri wa Ulinzi wa Tunisia, Abdelkrim Zbidi alinukuliwa akisema kuwa maofisa wa usalama wa nchi hiyo waliwatia mbaroni watu 13 wakiwa na pasi za kusafiria za Ufaransa kwenye kivuko cha Ra’s Ajdir katika mpaka wa Libya.  Wiki iliyopita, Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa nchini Libya ilitangaza kukata ushirikiano wake wa kiusalama na serikali ya Ufaransa kutokana na hatua ya nchi hiyo kuliunga mkono kundi la wapiganaji wa Jenerali Khalifa Haftar.  Wapiganaji wa kundi hilo walianzisha mashambulizi makali Aprili 4 mwaka huu, dhidi ya mji wa Tripoli sambamba na kushambulia makao makuu ya Serikali ya Maridhiano ya Kitaifa mjini humo. Hujuma hizo hadi sasa zimepelekea karibu watu 270 kuuawa na wengine 1300 kujeruhiwa, sambamba na watu 35,000 kuwa wakimbizi.
kimataifa
CHUO Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kinatarajia kuanza kutoa Mitihani ya Kimataifa ya Ujuzi wa lugha ya Kiswahili (MKUKi) kuanzia mapema mwakani.Hayo yalibainishwa jana jijini hapa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dk Leonard Akwilapo, alipokuwa akizungumzia mpango huo ambao pia umelenga kukuza na kuinua lugha ya Kiswahili. Alisema hatua hiyo ni jitihada za kuikuza na kuieneza lugha ya Kiswahili ulimwenguni kwa kuwa ni miongoni mwa lugha 10 zenye wazungumzaji wengi duniani.“Mtakumbuka kwamba Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere alishafanya jitihada kubwa kuiendeleza na kuieneza Lugha ya Kiswahili, pamoja na kusimamia ubora wake ndani na nje ya nchi. Pia, marais waliofuata katika awamu zote za uongozi wa nchi yetu walitilia mkazo suala hili,” alisema.Alisema mitihani itafanyika mara sita kwa mwaka ikiendana na kipindi cha masomo ya Kiswahili kwa kila ngazi na itafanyika kwa njia za kielektroniki katika vyuo na vituo mbalimbali vya Kiswahili duniani, ambavyo tayari yamekwishafikiwa makubaliano maalumu kuhusu mitihani hiyo.“Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinakuwa ni chuo kikuu cha kwanza duniani kutunga mitihani hii, kusimamia utahini na usahihishaji na kisha kutoa cheti cha kimataifa kinachoonesha kiwango cha ujuzi wa mtahiniwa,”alisema.Alisema UDSM ina uzoefu wa kutosha na umahiri katika ufundishaji wa lugha ya Kiswahili na vyuo vikuu vingi hapa duniani vimekuwa vikipata uzoefu huo kutoka kwenye chuo hicho. Alisema tayari kuna makubaliano baina ya walimu wa Kiswahili wa UDSM na walimu wanaofundisha Kiswahili katika vyuo vya nje, kuhusiana na mitihani hiyo itakayoanza mwakani.“Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kimejiandaa kuhakikisha kuwa mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano iko madhubuti kuwezesha mitihani hiyo kufanyika kwa ufanisi na kwa viwango vya kimataifa, kwa sababu kuna wahitaji ambao watafanyia mitihani hii wakiwa katika nchi zao, si lazima wasafiri na kuja kufanyia mitihani yao Tanzania,” alisema.Alisema walengwa wa mitihani hiyo ni wote wanaojifunza Kiswahili kama lugha ya pili au lugha ngeni katika ngazi mbalimbali, wakilenga kujipima usanifu katika kusoma, kuandika, kuongea na kusikiliza.Naye Profesa Aidin Mutembi kutoka Taasisi ya Taaluma za Kiswahili (TATAKI) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, alisema hatua hiyo itatoa fursa kwa watu mbalimbali wakiwemo wanadiplomasia, wafanyabiashara na wana taaluma tofauti wanaotaka kufanya kazi nchini kwenye nchi zinazozungumza lugha ya Kiswahili kufanya mtihani huo na kutambuliwa kimataifa.
kitaifa
MAREGESI PAUL Na RAMADHAN HASSAN -DODOMA MBUNGE wa Ukonga, Mwita Waitara (Chadema), amesema wananchi wamewageuza wabunge wa Tanzania na kuwa kama mashine za kutolea fedha (ATM) na Vyama vya Kuweka na Kukopa (SACCOS). Kutokana na hali hiyo, amesema kuna haja Serikali kuboresha mafao yao ili yaendane na majukumu wanayokabiliana nayo. Waitara aliyasema hayo jana mjini hapa wakati wa semina ya wabunge walioko katika mabunge ya nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola (CPA). “Mshahara wa mbunge kila mwezi unakatwa shilingi milioni 1.2, lakini baada ya kumaliza miaka mitano ya ubunge, mafao yake yanakatwa tena. “Hivi huo utaratibu mliutoa wapi wakati haupo nchi yoyote duniani? Sisi wabunge tumegeuzwa kama ATM au saccos kwa sababu tutatoa pesa kila mahali. “Kule Kenya ofisi ya mbunge ni kama taasisi kwa sababu ina mbunge na ina mtafiti anayemsaidia mbunge kila anapotaka kufanya mambo yake. "Hata kukiwa na harambee, mbunge unaitwa na kutakiwa uchangie fedha nyingi, sasa utachanga kwa fedha zipi wakati mnatulipa kidogo, yaani huu ni mzigo kwetu wabunge. “Kwa hiyo, tuongezeeni mafao kwa sababu tunalipwa kidogo sana ikilinganishwa na nchi zingine,”alisema Waitara. Kwa upande wake, Mbunge wa Songwe, Philipo Mulugo (CCM), pamoja na kulalamikia mafao madogo, alitaka kujua takwimu halisi za malipo wanayolipwa wabunge wa Kenya na nchi zingine ili wayalinganishe na wanayolipwa wabunge wa Tanzania. Naye Mbunge wa Viti Maalum, Shally Raymond (CCM), alisema kuna haja kwa wabunge hao kuboreshewa mafao yao ili waweze kufanya kazi kwa mafanikio zaidi. Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), pamoja na kulalamikia mafao, alilalamikia utaratibu wa vyama vya siasa kukutanisha wabunge wao ili wakubaliane kupitisha mambo yenye masilahi ya chama badala ya kuangalia utaifa. Wakati hao wakisema hayo, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola (CCM), alitaka wabunge wawekewe bima ya afya ya maisha kama sheria inavyotaka. “Kwanza kabisa nimeshangaa kusikia makao makuu ya CPA Barani Afrika yapo Tanzania na pia ofisi yao iko hapa bungeni. “Kuhusu hilo suala la bima ya afya ya maisha ya wabunge, nashangaa kwanini Serikali haitaki kuliruhusu kwa wabunge kwani hata Tume ya Utumishi ya Bunge, imekuwa ikisisitiza juu ya jambo hilo. “Yaani Tume ya Utumishi imelifuatilia kwa muda mrefu, lakini Serikali haitaki kukubali, jambo ambalo hakitendi haki kwa sababu baadhi ya wabunge wameshafariki na wengine wamepata ulemavu,” alisema Lugola. Hata hivyo, wakati akijibu hoja hizo, Katibu wa Spika wa Bunge, Said Yakub, alisema chanzo cha wabunge kugeuzwa ATM ni wao wenyewe kwa sababu ndivyo walivyowazoesha wapiga kura wao.
kitaifa
BAADHI ya wachambuzi na makocha wa soka nchini wametaja timu tano zinazoweza kufika mbali kwenye fainali za Mataifa ya Afrika zinazoendelea nchini Misri, huku wenyeji wakipewa asilimia 100.Wakizungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti jana, wachambuzi hao Ally Mayai, Dominick Salamba na Jamhuri Kihwelu ‘Julio’ kila mmoja ameitaja Misri kuwa inaweza kufika mbali zaidi na hata kuchukua Kombe la Afrika. Kwa upande wa Mayai alisema sababu ya kuwapa nafasi wenyeji ni kutokana na historia iliyopita, ikionesha kuwa Misri iliwahi kuandaa michuano hiyo mara nne na mara tatu kombe likabakia kwao.Pia, alizitaja timu nyingine zenye nafasi kuwa ni Cameroon kwa kuwa wameanza vizuri na huenda wakataka kupambana ili kutetea taji walilolitwaa Gabon, huku akisema Algeria ina kikosi bora chenye uwezo, Ghana wana wachezaji wenye uzoefu na Morocco kwa sababu ina kocha aliyewahi kutwaa mataji mara tatu. “Kila timu ina ubora wake na yeyote anaweza kufanya makubwa kutokana na uzoefu wa wachezaji wao kwenye mashindano hayo,” alisema.Kocha wa zamani wa Simba, Mwadui na Dodoma FC, Julio alisema bado pana ugumu kwa sababu ndio kwanza mapema ila anaziona Misri, Algeria na Senegal katika jicho la mbali.Alisema timu nyingi ni bora na nyingine hubadilika kutoka mechi moja kwenda nyingine hivyo, ni kazi kutabiri mapema. Mchambuzi Salamba alisema michuano hiyo inaonekana migumu kutokana na mbinu za kiufundi kutofautiana ila anaipa nafasi Senegal kutokana na kuwepo kwa muunganiko bora wa kikosi chao.Pia, Nigeria kutokana na uwezo wa kumiliki mpira ingawa katika kasi ya kushambulia kwao sio kubwa, Cameroon kuwa wana vijana wenye kasi, Misri ikibebwa na uzoefu na ni wenyeji lakini pia, Algeria kutokana na kucheza mpira wa nguvu na wenye kasi. Nigeria juzi ndio ilikuwa timu ya kwanza kukata tiketi ya kucheza hatuia ya 16 bora kabla ya wenyeji Misri hawajaifuata baadae.
michezo
Kikwete alitoa agizo hilo katika hafla ya kumuaga iliyoandaliwa na wasanii kutokana na mchango wake mkubwa katika tasnia ya sanaa.Katika hafla hiyo iliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City Dar es Salaam, Kikwete alisema kuwa Cosota inatakiwa kuhakikisha inadhibiti wizi wa kazi za wasanii nchini kutokana na watu wengi kunufaika na kazi hizo huku wasanii wakiambulia malipo kidogo ambayo hayaendani na kazi wanazofanya.Alisema katika kutekeleza mpango wa awali wa kupambana na wizi wa kazi za wasanii serikali imejipanga kutekeleza utaratibu wa wasambazaji wote wa kazi za wasanii kubandika stika ya usalama kwenye kila nakala ya kazi itakayosambazwa ili kuhakikisha kazi za wasanii haziibwi.Alisema katika utaratibu huo kila msambazaji ataingia mkataba na msanii kusambaza idadi fulani ya nakala na kupewa stika ambazo zitabandikwa katika kila nakala ili kudhibiti wizi na hatimaye wasanii kunufaika na kazi zao tofauti na ilivyo sasa ambapo anaenufaika ni msambazaji.“Nimeshazungumza na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) kuhakikisha kwamba kazi zote za wasanii zinawekwa stika ili kuondoa usumbufu kwa wasanii kutonufaika na kazi zao ambazo wanatumia muda wao mwingi katika kuzitengeneza,” alisema Kikwete.Akizungumzia malipo ya wasanii katika miito ya simu, Rais Kikwete alisema kua tayari umeshaandaliwa utaratibu mzuri ambao utamwezesha msanii kulipwa kiasi cha fedha kulingana na nyimbo zake ambazo zinatumika katika kampuni za simu kama milio.Akitoa ushahidi wa kuanza kunufaika na mpango huo wa malipo, msanii wa Bongo Fleva Nikki wa Pili alisema kuwa awali kampuni ya Tigo ilikuwa ikimlipa shilingi laki moja kama ada ya nyimbo zake kutumika katika miito ya simu ambapo sasa kila mwezi kampuni hiyo inamlipa shilingi milioni mbili.Hafla hiyo ya kumuaga Rais pia ilihudhuriwa na wageni mbalimbali akiwemo Waziri wa Ujenzi ambae pia ni mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM, John Magufuli, Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, January Makamba.
michezo
Kulwa Mzee, Dar es Salaam Msanii wa Filamu nchini, Wema Sepetu aliyekuwa mahabusu katika Gereza la Segerea ameachiwa kwa onyo na dhamana yake inaendelea. Uamuzi huo umetolewa leo Jumatatu Juni 24, saa nne asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde. Akitoa uamuzi wa aidha Wema afutiwe dhamana au la, Hakimu Kasonde amesema kazingatia kiapo kilichowasilishwa na Wakili Albert Msando na maelekezo ya mshtakiwa lakini mahakama inaona ni kweli alivunja masharti ya dhamana. Amesema sababu kubwa ni kuumwa ghafla ambapo alitakiwa siku ile ile angefika mahakamani kutoa taarifa si kuamua kuondoka. “Mahakama inakuonya, uhakikishe pale ambapo haupo mahakamani, Mahakama ijulishwe kupitia mdhamini wako na si vinginevyo,” amesema Hakimu Kasonde. Hakimu Kasonde amesema kosa hilo likijirudia Mahakama haitasita kumfutia dhamana. Wema alienda gerezani Juni 17 mwaka huu, ambapo anakabiliwa na mashtaka ya kusambaza video ya ngono katika mitandao ya kijamii kupitia simu yake ya kiganjani. Juni 11 mwaka huu  Mahakama ilitoa hati ya kumkamata Wema kwa kosa la kuruka dhamana.
kitaifa
Ramadhan Hassan -Dodoma SERIKALI imesema bado kuna tatizo la matumizi makubwa ya bangi nchini ambapo mwaka 2015 hadi  Juni, 2020, kilo 188,489.93 za bangi zimekamatwa. Hayo yalielezwa jana jijini hapa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira, Vijana, Sera na Watu wenye ulemavu, Jenista Mhagama, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika siku ya  maadhimisho ya kupinga vita dawa za kulevya duniani. Jenista alisema bado tatizo la matumizi ya bangi ni kubwa nchini ambapo Serikali inajitahidi kulitatua na kwamba wamefanikiwa kukamata kilo 124,080.33 za mirungi kilo 58.46 za Cocaine na kilo 635.57 za heroin. Alisema katika ukamataji huo, watuhumiwa 73,920 walikamatwaa ambapo pia Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), imefanikiwa kufanya ukaguzi katika makampuni 167 yanayojihusisha na uingizaji  wa kemikali bashirifu. Alisema katika ukaguzi huo, mamlaka imefanikiwa kukamata kiasi lita za ujazo 480,000 na kilo 22,145 za kemikali bashirifu zilizoingia nchini bila ya kufuata utaratibu. Alisema tatizo la dawa za kulevya katika jamii ni mtambuka linalohitaji ushiriki wa sekta mbalimbali katika kupambana nalo. Alisema DCEA inatekeleza majukumu yake  ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya kwa kushirikiana na wizara mbalimbali, vyombo vya ulinzi na usalama, na taasisi zingine za Serikali na zisizo za Serikali pamoja na mashirika ya kitaifa na kimataifa. Alisema  mwaka 2015-2020, mamlaka imetekeleza kazi mbalimbali katika kukabiliana na dawa za kulevya ikiwa ni pamoja na kufanya maboresho ya Sheria ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya ya mwaka 2017. Pia imetoa elimu kuhusu madhara ya dawa za kulevya ambapo mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu imeweza kuanzisha vilabu vya kupinga dawa za kulevya mashuleni. “Vile vile, elimu bora kuhusu tatizo la dawa za kulevya imekuwa ikitolewa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kama vile televisheni, magazeti, warsha za kitaifa na makongamano pamoja na mitandao ya kijamii kuhusu madhara ya dawa hizo pamoja na udhibiti wa uchepushwaji wa kemikali bashirifu. “Hii imesaidia kwa kiasi kikubwa kuzuia wimbi la vijana kuingia kwenye matumizi na biashara ya dawa hizo,” alisema. Alisema pia imefanikiwa kwa kiasi kikubwa kudhoofisha na kuvunja mitandao mikubwa ya wafanyabiashara wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya ndani na nje ya nchi. Waziri Jenista alisema kwa mujibu wa taarifa ya mwaka 2019 ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Masuala ya Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC), Tanzania  ilifanikiwa kupunguza uingizaji wa dawa za kulevya kwa 90%. Pia, mamlaka imeshinda kesi kubwa za wafanya biashara wakubwa wa dawa za kulevya. “Upanuzi wa huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya, mamlaka kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto na taasisi zingine zisizo za kiserikali imefanikiwa kupanua huduma za tiba kwa waathirika wa dawa za kulevya nchini, ambapo hadi mwaka 2016 kulikuwa na vituo vitatu tu nchini ambavyo vilihudumia waathirika 3,500.
afya
 WASHINGTON, MAREKANI  RAIS wa Marekani, Donald Trump amesema ni ‘’ ni heshima ‘’Marekani ina idadi kubwa ya maambukizi ya virusi vya corona duniani.  ‘’Ninalitazama suala hili kama heshima fulani, kama jambo zuri kwasababu inamaanisha kuwa vipimo vyetu viko vizuri,’’ alieleza akiwa Ikulu ya Marekani.  Marekani ina watu milioni 1.5 walioathiriwa na virusi vya corona na karibu vifo 92,000, kwa mujibu wa takwimu zinazokusanywa na Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.  Nchi inayoshika nafasi ya pili, ni Urusi ikiwa na maambukizi ya watu 300,000.  Jumatatu Rais ,Trump alikuwa akizungumza mkutano wake wa kwanza wa baraza la mawaziri tangu kuanza mlipuko wa virusi nchini humo.  Aliwaambia waandishi wa habari, ‘’Unajua unaposema tunaongoza kuwa na watu wengi walioambukizwa, ni kwa sababu tuna vipimo vingi kuliko mtu mwingine yeyote.  ‘Virusi vya corona vimefichua uongozi wa Trump kuwa haujui unachofanya’  Trump anakunywa ‘dawa ya corona’ isiyothibitishwa  ‘’Sijali. Ninachotaka nikupata chanjo tu inayofanya kazi”  ‘’Hivyo tuna watu wengi walioambukizwa,’’ aliendelea, ‘’Sitazami kama jambo baya, ninalitizama kwa heshima fulani, kama jambo jema kwa sababu ina maanisha kuwa tuna vipimo vizuri.’’  Aliongeza: ‘’Hivyo ninaliona kama nembo ya heshima. Kweli ni heshima.  ‘’Ni heshima kwa vipimo na kazi ambayo wataalamu wameifanya.’’  Kwa mujibu wa kituo cha kupambana na kudhibiti magonjwa , Marekani imepima watu milioni 12.6 mpaka siku ya Jumanne.  Rais Trump, alikuwa akijibu swali kuhusu kama alikuwa akifikiria kuweka marufuku ya kusafiri kwenda Amerika ya Kusini hasa Brazil. Nchi hiyo ni ya tatu kwa kuwa na idadi kubwa ya waathirika.  Kamati ya uongozi ya kitaifa ya Chama cha Democratic, imekosoa kauli ya Rais Trump, ikisema kwenye ukurasa wake wa Twitter kuwa na waathirika wa Covid-19 milioni 1.5 nchini Marekani kunaonesha ‘’kushindwa kabisa kwa uongozi’’.  Wakati Marekani, ikiwa imefanya vipimo zaidi kuliko nchi nyingine yoyote, si ya kwanza duniani kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo nchini humo kwa mujibu wa takwimu za chapisho la kisayansi la Our World in Data la Chuo Kikuu cha Oxford.  Katika chati, Marekani ya 16 kwa vipimo kwa watu 1,000 ikiwa mbele ya Korea Kusini, lakini nyuma ya Iceland, New Zealand, Urusi na Canada.  Katika kipindi cha juma lililopita, Marekani imekuwa ikifanya vipimo kwa watu 300,000 na 400,000 kwa siku, kwa mujibu wa mradi uitwao Covid Tracking, zikiwa ni jitihada za watu waliojitolea.  Mkurugenzi wa Taasisi ya Afya ya Global Health, Ashish Jha wiki iliyopita aliuambia mkutano wa Congress kuwa: ‘’Marekani inahitaji vipimo zaidi ya 900,000 kila siku. Kwa sasa tuna theluthi tu ya vipimo.’’  Marekani pia imeripoti vifo vingi vinavyotokana na virusi vya corona kuliko nchi nyingine yoyote, ingawa kwa ulinganifu wa idadi ya watu na vifo Marekani ni ya sita nyuma ya Ubelgiji, Uingereza na Ufaransa kwa mujibu wa takwimu za Chuo cha Johns Hopkins 
kimataifa
LONDON, ENGLAND UONGOZI wa timu ya Tottenham umethibitisha utaikosa huduma ya mlinda mlango wake Hugo Lloris hadi 2020 baada ya kupata tatizo la kugeuka kiwiko kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Brighton mwishoni mwa wiki iliopita. Katika mchezo huo, Tottenham ambao walikuwa ugenini walikubali kichapo cha mabao 3-0, lakini mlinda mlango huyo hakuweza kuumaliza mchezo huo kutokana na kuumia na kisha kutolewa nje. Kupitia website ya Tottenham, uongozi wa timu hiyo umedai mchezaji huyo amepata tatizo ambalo litaweza kumuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. “Hugo Lloris ataendelea kufanyiwa uchunguzi zaidi kutokana na tatizo alilolipata la kugeuka kiwiko kwenye mchezo wetu dhidi ya Brighton mwishoni mwa wiki iliopita. “Kutokana na uchunguzi wa awali mchezaji huyo anaweza hasifanyiwe upasuaji wowote kutokana na hali hiyo, lakini nahodha huyo hawezi kurudi kufanya mazoezi na timu hiyo kabla ya kumalizika kwa mwaka 2019. “Mchezaji huyo atakuwa nje huku akiendelea kuwa chini ya uangalizi wa madaktari kwa kipindi chote hadi pale atakapokuwa fiti kurudi viwanjani,” waliandika Tottenham. Tottenham kwa sasa wanashika nafasi ya tisa kwenye msimamo wa Ligi wakiwa na pointi 11 baada ya kucheza michezo nane. Hata hivyo, kocha wa timu ya taifa ya Ufaransa, Didier Deschamps, amedai kumkosa mlinda mlango huyo ambaye alibeba taji la Kombe la Dunia mwaka jana nchini Urusi ni pigo kubwa kwake hasa kwenye michezo ya kuwania kufuzu Euro 2020 dhidi ya Iceland na Uturuki, lakini ni nafasi kwa makipa wengine kuonesha uwezo wao. “Hatokuwepo kwenye kikosi chetu, hivyo tutakuwa kwenye wakati mgumu wa kufuzu, yeye ni mchezaji muhimu sana kwetu, lakini ninaamini wachezaji waliopo wanaweza kuziba nafasi hiyo,” alisema kocha huyo.
michezo
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM SERIKALI inapoteza dola za Marekani milioni 100 kila mwaka kutokana na kuagiza dawa kutoka nje ya nchi. Viwanda vya dawa vilivyopo nchini ni 13 tu ambapo uwezo wake wa kuzalisha ni asilimia 20 ya dawa zote zinazohitajika nchini. Hayo yalisemwa juzi na Mfamasia wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Siana Mapunjo, wakati wa mkutano wa wadau wa mradi wa kiwanda cha dawa za binadamu cha Zinga ambacho kinatarajiwa kujengwa wilayani Bagamoyo mkoani Pwani. Mapunjo alikuwa akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. “Hii ni fursa kwa Kiwanda cha Zinga kusaidia nchi kupata dawa muhimu kwa wakati na kuokoa fedha za kigeni, kuongeza ajira na kuiwezesha Tanzania ya Viwanda kufikiwa,” alisema Mapunjo. Alisema gharama hizo zinaongezeka kila mwaka na inakadiriwa ifikapo mwaka 2021 zitafikia Dola za Marekani milioni 350 kwa mwaka. Awali Mkurugenzi wa kiwanda hicho, Dk. Mary Mayige, alisema ujenzi huo utagharimu zaidi ya Sh bilioni 70 na wanatarajia kutumia teknolojia za kisasa kutoka Ujerumani. "Dawa zitakazotengenezwa zitakuwa na kiwango cha juu cha ubora kuweza kushindanishwa na dawa zinazotoka kwenye soko la kimataifa," alisema Dk. Mayige. Alisema kiwanda hicho kitatengeneza dawa za kufubaza Virusi vya Ukimwi (ARVs), antibiotiki, malaria, kisukari, presha, magonjwa ya kuambukiza na zile za magonjwa yasiyoambukiza. Alisema uzalishaji wa dawa za binadamu nchini bado ni mdogo na upatikanaji wa dawa zinazozalishwa na viwanda vya ndani umeshuka kiwango ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
kitaifa
Na MAREGESI PAUL – DODOMA BOMOABOMOA inayoendelea nchini kwa wananchi waliojenga katika maeneo ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), imewakera baadhi ya wabunge. Wabunge hao walionyesha hali hiyo bungeni jana wakati walipokuwa wakichangia Muswada wa Sheria ya Reli ya Mwaka 2017, uliowasilishwa bungeni na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa. Katika mchango wake, Mbunge wa Kaliua, Magdallena Sakaya (CUF), alionyesha kutoridhishwa na bomoabomoa hiyo kwa kuwa baadhi ya wanaovunjiwa majengo, walianza kuyamiliki miaka mingi iliyopita. Kwa upande wake, Mbunge wa Moshi Mjini, Jafary Michael (Chadema), pamoja na kulalamikia bomoabomoa hiyo, alitaka viongozi waliosababisha wananchi wakajenga katika maeneo ya reli, kuchukuliwa hatua. “Hii bomoabomoa inaumiza wananchi na kwa kuwa inaonekana baadhi ya waliojenga katika maeneo hayo walikuwa na vibali vya Serikali, basi waliotoa vibali hivyo wachukuliwe hatua kwani wamesababisha wananchi wapate hasara bila sababu,” alisema Michael. Mbunge wa Tabora Mjini, Emmanuel Mwakasaka (CCM), alisema kuna haja kwa Serikali kuangalia namna ya kuwafidia waliovunjiwa nyumba zao kwa kuwa baadhi waliuziwa viwanja na Serikali. Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM), alilalamikia bomoabomoa hiyo na kusema mkoani Tabora kaya zaidi ya 500 zitavunjiwa nyumba, akiwamo kikongwe mwenye miaka zaidi ya 70 ambaye alianza kumiliki eneo lake miaka mingi iliyopita. Mbunge wa Tunduma, Frank Mwakajoka (Chadema), alisema nyumba zaidi ya 3,244 zitabomolewa na kwamba kuna haja watakaobomolewa, kulipwa fidia ili wakajenge makazi mapya. Mbunge wa Viti Maalumu, Anna Lupembe (CCM), alitaka Serikali iimarishe ulinzi wa reli ili kudhibiti majangiri wanaong’oa mataluma kwa lengo la kupora mali za abiria.
kitaifa
Na RAMADHAN LIBENANGA-MOROGORO WAFUGAJI wilayani Mvomero Mkoa wa Morogoro, wamesema wamekuwa wakitumia fedha nyingi kununua mihtasari ya vikao vya vijiji ili kuzionyesha mamlaka mbalimbali jinsi walivyoruhusiwa kumiliki ardhi waliyonayo. Hayo yalielezwa jana na mchungaji Joseph Sepuke, alipokuwa akizungumza kwenye mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kibaoni wilayani Mvomero. “Wamasai wanapata mihtasari ya kijiji kwa gharama kubwa na viongozi hawa hawa wa vijiji ndio wanaowauzia hii mihtasari ili waweze kumilikishwa maeneo. “Kwa hiyo, tunaomba gharama za mihtasari hiyo zipunguzwe ili tuweze kuzipata kwa urahisi zaidi,” alisema Sepuke. Awali, akizungumza katika mkutano huo, mjumbe wa Serikali ya Kijiji cha Kibaoni, Fabian Beatus, alisema kijiji chao kimegundua kuna baadhi ya wananchi walioghushi mihtasari ya vijiji na kufanikiwa kupata ardhi. “Kuna watu wameghushi mihtasari kwa sababu sharti kuu linalomwezesha mwananchi kumiliki ardhi ni kuwa na muhtasari unaoonyesha vikao halali vya kijiji vilikaa kumjadilli na kuridhia kumpa eneo,” alisema. Akizungumza katika mkutano huo, mfugaji mwingine wa jamii ya kimasai, Songambili Mfaume, aliwatupia lawama baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kwa kusema wamekuwa wakimfuata awape milioni mbili ili wampe muhtasari aweze kumilikishwa eneo lake. Hata hivyo, tuhuma hizo zilikanushwa na Kaimu Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji hicho, Stephano Udoba ambaye alisema wamekuwa wakifuata taratibu wakati wa kuwamilikisha wananchi ardhi. Akizungumza katika mkutano huo ulioandaliwa na Mradi wa Kuendeleza Kilimo katika Safu za Milima ya Uluguru (UMADEP) unaotekelezwa chini ya usimamizi wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Ofisa Miradi wa UMADEP, Pesa Kusaga, alisema SUA inashirikiana na Serikali kuhakikisha migogoro ya ardhi inamalizika mkoani Morogoro.
kitaifa
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
uchumi
Na Said Ameir, MAELEZO KUWAPATIA wananchi dawa zenye viwango bora, salama na ufanisi ni moja kati ya malengo makuu ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika kuimarisha afya za watu. Pamoja na lengo hilo, utekelezaji wake mbali ya kukabiliwa na chagamoto za kibajeti, changamoto nyingine kubwa ni upungufu wa wataalamu wa ukaguzi na kudhibiti ubora na usalama wa dawa. Kwa mujibu wa takwimu za miaka ya hivi karibuni, soko la dawa katika nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki linategemea bidhaa hiyo kutoka nje kwa kati ya asilimia 70 na 75 hivyo uzalishaji wa ndani ni kati ya asilimia 30 na 25. Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Ulisubisya Mpoki anasema Tanzania huagiza nje ya nchi asilimia 80 ya mahitaji yake ya dawa. Nchi nyingine zinazoagiza dawa nje ya nchi ni Rwanda asilimia 90, Uganda asilimia 90, Burundi asilimia 100, Zanzibar asilimia 100 na Sudan Kusini asilimia 100. Katika nchi wanachama wa Jumuiya hii, ni Kenya pekee ambayo imepiga hatua katika utengenezaji dawa ambapo takwimu zinaonesha kuwa inatengeneza karibu asilimia 25 ya mahitaji ya soko la nchi wanachama. Mbali ya Jumuiya kuwa na mpango maalumu wa muda mrefu kuwezesha nchi wanachama kutengeneza zaidi dawa kuliko kutegemea watengenezaji wa nchi za nje, lakini pia imeweka mkazo katika kuwapatia uwezo na ujuzi  wa udhibiti na ukaguzi wa viwango vya ubora na usalama wa dawa wataalamu wa nchi wanachama. Mkakati wa Jumuiya katika kujenga uwezo wa wataalamu wa nchi wanachama umejikita katika kuhakikisha dawa zinazotengenezwa katika nchi wanachama na zile zinazoingizwa toka nchi za nje zinakidhi viwango vya ubora unaotakiwa. Nchi hizo zimekubaliana kuwianisha viwango vya dawa ili dawa zinazotengenezwa na kuingizwa katika Jumuiya ziwe na viwango vinavyofanana ubora, usalama na ufanisi. Hivi karibuni, Jumuiya hiyo kupitia Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) na Shule ya Famasi ya Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi za Afya Muhimbili (MUHAS) waliendesha mafunzo maalumu kwa wataalamu wa udhibiti na ukaguzi wa dawa kutoka nchi wanachama. Mafunzo hayo yaliyofanyika katika Kituo Mahsusi cha Kanda cha Ukaguzi na Udhibiti wa Dawa kwa Afrika Mashariki, kilichopo Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi ya Afya, Muhimbili yaliendeshwa kwa pamoja na wataalamu wa TFDA, MUHAS, Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) na mtaalamu mbobefu kutoka Bodi ya Dawa ya Uholanzi. Kituo hicho kilianzishwa mwaka 2014 na kuanza shughuli zake mwaka 2015 na kinaendeshwa kwa pamoja kati Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA na Shule ya Phamasi ya Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili. Mafunzo hayo ni ya pili tangu kuanzishwa kwa kituo hicho ambapo mafunzo ya kwanza yalifanyika mara tu kilipoanza kufanya kazi mwaka 2015. Ni vyema kubainisha kuwa katika programu ya uwianishaji wa dawa katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, TFDA ndio taasisi kiongozi ya uratibu na usajili dawa. Hii inadhihirisha uwezo mkubwa wa kitaalamu na kitaasisi ilionao TFDA katika masuala hayo katika nchi wanachama wa jumuiya. Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo anaeleza kuwa moja ya majukumu ya mamlaka za udhibiti wa dawa katika nchi wanachama ni kufanya tathmini ya dawa kabla hazijaingia katika soko kuhakikisha kuwa zinakidhi viwango vya ubora, usalama na ufanisi vilivyokubalika kisheria. “Mafunzo haya ni sehemu ya uwezeshaji wa utekelezaji wa majukumu ya Mamlaka za Udhibiti na Usimamizi wa Dawa katika nchi zetu, pia ni sehemu ya mpango wa uwianishaji  wa dawa wa jumuiya ili kujenga uwezo kwenye ngazi ya nchi za ukanda huu  kwa kufanya tathmini ya maombi ya usajili wa bidhaa za dawa,” anafafanua Sillo. Akizungumzia tathmini ya mafunzo hayo, Mratibu wa Mafunzo Mhadhiri Mwandamizi na Meneja wa Maabara ya Utafiti na Maendeleo, Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, Profesa Eliangiringa Kaale anasema yana umuhimu mkubwa katika kulinda afya ya wananchi wa Jumuia ya Afrika Mashariki. Kama takwimu za uingizaji dawa katika nchi wanachama zinavyoonesha, ni vyema kueleza kuwa kiwango hicho kikubwa cha dawa kinachoagizwa kutoka nje kinalazimu nchi wanachama kushirikiana kwa karibu kwa sheria, kanuni na viwango vinavyofanana ili ukanda wote uwe salama katika suala la dawa. Kama inavyoeleweka biashara ya dawa na vifaa tiba ni moja kati ya biashara inayonyemelewa na kushamiri kwa udanganyifu, hivyo ushirikiano wa karibu ni kitu muhimu katika udhibiti. Ukaguzi wa mipakani na ukaguzi wa mara kwa mara kwenye soko ndio utakaowalinda wananchi. Zaidi, uwezo mkubwa wa kitaalamu, rasilimali na kimiundombinu ndio silaha madhubuti kukabiliana na udanganyifu huo ambao Jumiya imekuwa ikichukua hatua kuimarisha uwezo wa wananchama wake wa usimamizi, ukaguzi na kudhibiti.
afya
MWILI wa binadamu na viumbe wengine kama vile wanyama, una mfumo unaosaidia kujilinda dhidi ya magonjwa mbalimbali. Mfumo huu wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa kwa kitaalamu huitwa ‘Immune system.’ Pamoja na mwili kuwa na mfumo wa kujilinda dhidi ya magonjwa, kuna nyakati ambazo kinga hii ya mwili inakuwa haijakomaa mfano kwa watoto. Pia kutokana na tafiti mbalimbali za kitabibu juu ya afya na uwezo wa mwili kujilinda, imesababisha kuwapo umuhimu wa kuimarisha kinga ya mwili kupitia matumizi ya chembe chembe ambazo hujulikana kwa jina la chanjo au kwa kitaalamu ‘Vaccine.’ Chanjo au ‘Vaccine’ ni chembechembe ambazo huandaliwa kupitia viumbe au bakteria wasababishao magonjwa (microbes), au chembechebe zinazoandaliwa kwa kutengenezwa (synthetic) ili kutumika katika kuuandaa mwili au kuamsha kinga ya mwili iweze kupambana na ugonjwa au magonjwa mbalimbali. Kutokana na aina ya matumizi, chanjo zimegawanyika katika makundi makuu mawili. Makundi hayo ni chanjo itokanayo na bakteria au virus ambao wameondolewa uwezo wao wa kusababisha ugonjwa (An attenuated vaccine) na kundi lingine ni chanjo ambayo hutokana na bakteria au virus ambao tayari wameuliwa/hawana uhai (Inactivated vaccines). Miongoni wa chanjo ambazo zimekuwa zikitolewa kwa binadamu ni pamoja na chanzo dhidi ya magonjwa kama vile surua, tetenasi, polio, homa ya ini (Hepatitis A and B) pamoja na chanjo ambayo imezinduliwa hivi karibuni nchini, Tanzania, chanjo ya kumkinga mwanamke dhidi ya saratani ya shingo ya kizazi (Human papilloma virus (HPV) vaccine). Chanjo imekuwa na umuhimu mkubwa katika mnyororo wa tiba za magonjwa mbalimbali. Baada ya kinga ya mwili kuamshwa na kuimarishwa, athari za magonjwa mbalimbali kwa binadamu zimekuwa zikipungua, mfano ulemavu (kupooza kwa viungo), magonjwa ya ini na vifo vimepungua. Sababu kubwa ya matumizi ya chanjo au utoaji wa chanjo ni kufanya mwili uweze kuzalisha kinga dhidi ya ugonjwa husika (Specific antibodies to each individual disease).   Je, chanjo hutolewa kwa kundi lipi la watu? Kama ambavyo nimetangulia kwa kufafanua maana ya chanjo, kuwa ni chembechembe ambazo zinatokana na aina ya viumbe au bakteria wanaosababisha magonjwa, kuna tahadhari katika makundi ya watu ambao watakuwa na sifa ya kupatiwa chanjo husika. Kwa mtu ambaye tayari analo tatizo husika, mfano mtu mwenye tatizo la homa ya ini (Hepatitis A au B), hatopatiwa chanjo ya ugonjwa huo, kadhalika na magonjwa mengine. Si salama kumpatia mtu chanjo wakati tayari analo tatizo au ugonjwa husika. Kumpatia mtu chanjo huku akiwa na tatizo au ugonjwa husika, kunaweza kusababisha tatizo likawa kubwa zaidi hatimaye kuhatarisha afya na uhai wa mgonjwa. Pia, chanjo zimekuwa zikitolewa kulingana na umri wa mlengwa/mteja. Baada ya chanjo kutolewa, kwa baadhi ya nyakati pia zimekuwa zikisababisha maudhi madogo madogo kwa mtumiaji. Mfano kwa watoto wadogo zimekuwa zikisababisha joto kupanda, usumbufu katika kusikia, maumivu sehemu iliyo chanjwa mfano sehemu ya mkono au paja. Maudhi haya madogo madogo siku zote yamekuwa si lengo kuu la chanjo, bali hujitokeza kwa baadhi ya watu. Matibabu ya maudhi haya yanategemeana na aina ya usumbufu ambao umejitokeza kwa mtu, si matibabu ya jumla kwa watu wote. Miongoni mwa matibabu au msaada wa kitabibu ambao umekuwa ukitolewa kwa watu ambao wamepatwa na matatizo baada ya kupatiwa chanjo ni pamoja na matumizi ya dawa za kushusha joto au homa, dawa za kuondoa degedege (convulsions) pamoja na matibabu mengine kutegemeana na namna ambavyo yamejitokeza. Ili kuepukana na magonjwa mbalimbali pamoja na athari zake kiafya na kijamii, ni vyema walengwa wote wakapatiwa chanjo kulingana na miongozo inayotolewa na wataalamu wa afya.
afya
Na WAANDISHI WETU – ZANZIBAR/DAR ES SALAAM RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema iwapo Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) litaikatia umeme Zanzibar kutokana na deni wanalodaiwa, wataweza kurudi katika matumizi ya asili ambayo ni kutumia vibatari kupata mwanga. Dk. Shein aliyasema hayo mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amaan Abeid Karume, akitokea nchini Indonesia katika mkutano maalumu aliomuwakilisha Rais Dk. John Magufuli. Kauli hiyo imekuja wakati Tanesco jana ikiwa imetoa siku 14 kwa wadaiwa wote sugu, ikiwa ni pamoja na Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), linalodaiwa Sh bilioni 127, kulipa deni hilo ndani ya muda huo kabla ya kukatiwa umeme. Wiki iliyopita, Rais Magufuli aliiagiza Tanesco kukata umeme kwa wadaiwa wote sugu, akisema hata kama Ikulu ya Magogoni inadaiwa, nayo pia ikatiwe nishati hiyo. Jana mara baada ya Dk. Shein kuwasili, alizungumzia mafanikio ya safari yake ikiwa ni pamoja na mipango ya viwanda, kauli iliyofanya waandishi kuuliza viwanda hivyo vitaendeshwa vipi ilihali Tanesco imetangaza kuikatia umeme Zanzibar. Kutokana na swali hilo alisema: “Naamini Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Serikali ya kiungwana, inayojali watu wake, hivyo haiwezi kufanya hivyo kwenye suala hili la kuzima umeme visiwani Zanzibar na iwapo ikitokea umezimwa, Zanzibar watakuwa tayari kurudi kwenye matumizi ya vibatari.” Alisema akiwa safarini alisoma magazeti mawili yaliyoandika juu ya Zanzibar kukatiwa umeme, lakini haamini kama taarifa hizo zina ukweli, huenda waandishi walinukuu vibaya vyanzo vya taarifa hiyo. “Siamini kama umeme wanaweza kuzima, lakini natungojee wazime tuone,” alisema Dk. Shein. Alisema atashangazwa iwapo umeme utakatwa, ikizingatiwa mahusiano mazuri yaliyopo baina ya pande mbili hizi zinazounda Tanzania. Alieleza kwa kipindi cha miaka mingi, ikiwa ni pamoja na wakati yeye akiwa Makamu wa Rais wa Tanzania, Zanzibar imekuwa ikidaiwa na Tanesco na wamekuwa wakilipa kwa utaratibu maalumu. Alisema suala la kudaiwa si geni na lipo kwa muda mrefu na wao kama Serikali hawajawahi kukataa kulipa, hivyo ni utaratibu maalumu ambao unapaswa kutumika ili kuondoa hali hiyo.   SIKU 14 Wadaiwa sugu wa Tanesco, wakiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco), wizara na taasisi za Serikali, wamepewa siku 14 kulipa madeni yao kabla kukatiwa huduma. Hayo yalisemwa na Kaimu Mtendaji wa Tanesco, Dk. Tito Mwinuka, katika mkutano wa waandishi wa habari uliofanyika Dar es Salaam jana. Katika mkutano huo uliohusisha vyombo vichache vya habari – televisheni moja binafsi, moja ya Serikali, magazeti ya Serikali na ya kampuni moja binafsi, Dk. Mwinuka alisema hadi sasa shirika hilo linadai zaidi ya Sh bilioni 275 kwa Zeco, Wizara, Taasisi za Serikali na makampuni ya watu binafsi. Dk. Mwinuka alisema jambo hilo limechangia kurudisha nyuma utendaji wa shirika hilo katika kusambaza huduma ya umeme nchini. Alisema kutokana na hali hiyo, baada ya muda waliotoa kwisha bila deni hilo kulipwa, Tanesco itachukua uamuzi mgumu wa kuwakatia umeme wadaiwa hao. Katika deni hilo, Zeco inadaiwa Sh bilioni 127, mashirika ya serikali, wizara na taasisi  Sh bilioni  52, huku kampuni binafsi na wateja wadogo wakidaiwa Sh bilioni 94. “Tumetoa siku 14 kwa wadaiwa sugu wote wa Tanesco, wakiwamo Shirika la Umeme Zanzibar (Zeco) ambao tunawadai Sh bilioni 127 hadi Januari mwaka huu, wizara na taasisi za Serikali ambazo na zenyewe tunazidai, wanapaswa kulipa deni lao ili kuepusha usumbufu wa kukatiwa umeme,” alisema Dk. Mwinuka. Alisema hadi sasa wameshatoa notisi ya siku 14 kwa wadaiwa hao ili waweze kulipa madeni yao na watakaoshindwa kufanya hivyo, watakuwa wamekaidi notisi hiyo. Dk. Mwinuka alisema malimbikizo ya madeni hayo yamekuwa yakikwamisha jitihada za utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya msingi ndani ya shirika hilo. Alisema shirika hilo linahitaji fedha kwa uendeshaji wa shughuli mbalimbali, ikiwamo matengenezo ya miundombinu na utekelezaji wa miradi mbalimbali. Dk. Mwinuka alisema mkakati wao ni kuhakikisha wanakusanya madeni hayo na fedha zitakazopatikana zisaidie kufanya shughuli za usambazaji umeme ili huduma hiyo iwafikie watu wengi zaidi. Alisema upatikanaji wa umeme utasaidia kuchochea maendeleo na kusaidia ukuaji wa sekta mbalimbali zinazotegemea nishati ya umeme.   Taarifa hii imeandaliwa na MUHAMMED KHAMIS (UOI – ZANZIBAR) na PATRICIA KIMELEMETA (DAR ES SALAAM)
kitaifa
Alitoa pongezi hizo alipozindua rasmi hatua ya benki hiyo, Mwalimu Commercial Bank (MCB) kujiorodhesha DSE mwishoni mwa wiki Dar es Salaam tayari kwa kuanza kuuza hisa zake. “Soko la hisa ni njia mpya ya kuwakwamua walimu kiuchumi na kuzidi kujiendeleza kimaisha,” alisema Majaliwa.Alisema Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuendeleza elimu ikiwamo kuboresha maslahi ya watendaji wake na kwamba hatua iliyofikiwa na CWT ni chachu ya kufikia malengo hayo ya maendeleo.“Chama kimepiga hatua kubwa ya kuanzisha benki kwa kushirikiana na wataalamu mbalimbali, wanachama kuhamasika kuchangia fedha kwa kununua hisa za benki na hatimaye leo kujiunga na soko hili,” alisema Waziri Mkuu.Pia aliipongeza Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko na Mitaji kwa kutoa mwongozo hadi benki ya chama hicho kufikia hatua ya kuuza hisa kwa walimu Machi mwaka huu.“Mimi ni mwalimu na kwa kweli walimu tupo wengi nchini, majengo ya chama cha walimu yaliyopo mikoani pia yatumike katika kufungua matawi ya benki ili kuwafikia walimu wote na wadau mbalimbali,” alisema Majaliwa.Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Walimu, Herman Kessy alisema mafanikio ya benki yaliyopatikana yanatokana na wanahisa wakiwemo walimu wote wa Tanzania, Mfuko wa pensheni wa PSPF, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) na wanahisa wengine wote wa benki.“Tumekusanya mtaji wa shilingi bilioni 31 na matarajio yalikuwa kupata bilioni 25,” alisema Kessy na kufafanua kuwa walikusanya zaidi ya matarajio yaliyokuwepo kupitia wanahisa 235,494.Katibu Mkuu wa CWT, Yahaya Msulwa alisema maandalizi ya awali ya kuanzisha benki hiyo yamefikia hatua nzuri kwani wamepata leseni kutoka Benki Kuu ya Tanzania na wanatarajia itafunguliwa rasmi Mei mwakani.
uchumi
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM  TEKLA (si jina lake halisi), ni mwalimu katika shule moja ya msingi jijini Dar es Salaam. Katika harakati za kutafuta maisha amekumbana na changamoto nyingi ambazo kama si mama yake kupambana huenda leo angekuwa na maisha mabaya zaidi. Tekla anasema alikuwa akiishi na mama na baba yake wa kambo na kwamba mara nyingi mama yake alikuwa akiingia kazini usiku na kurudi asubuhi. “Wakati nikiwa kidato cha tatu, siku moja wakati nimelala baba alinifuata na kunitongoza. Nilikataa na kukimbia kwenda kukaa nje hadi asubuhi alipoondoka kwenda kazini ndio nikarudi ndani kujiandaa na kwenda shule. “Tulikuwa tumepanga vyumba viwili hivyo mimi nilikuwa nalala sebuleni halafu wazazi wangu chumbani, siku nyingine baba akaja tena akiwa ameshika panga. Niliogopa sana nilijua ataniua hivyo nikajikuta nimefanya naye mapenzi,” anasema Tekla. Anasema baba yake huyo aliendelea kumfanyia vitendo hivyo huku akimpa vitisho na kwamba hakuwahi kumwambia mama yake. “Wakati naendelea na masomo nikashtukia nimepata ujauzito, sikumwambia mtu niliendelea kwenda shule hadi mimba ilipofikisha miezi saba. Niliongeza kipimo cha sketi nikawa navaa na sweta kila siku ili kuficha tumbo,” anasema. Anasema wakati mimba ilipofikisha umri wa miezi saba ilikuwa ni Desemba na baada ya kufunga shule alimuomba mama yake amruhusu asafiri kwa ajili ya likizo. Anasema alikwenda kwa bibi yake mkoani Dodoma na alipofika aliamua kumweleza ukweli bibi yake huyo. “Mama alitaarifiwa na kuja Dodoma, sikuwahi kusema kama baba ndiye aliyenipa ujauzito ule nilikuwa naogopa sana. Nilikaa Dodoma hadi Februari nilipojifungua…nilijifungua mtoto wa kiume lakini alifariki dunia baada ya siku mbili,” anasema. Mwalimu huyo anasema alipumzika kwa bibi yake na baada ya likizo ya Aprili aliamua kurudi shule lakini akamuomba mama yake asomee huko huko mkoani Dodoma ambapo aliamua kurudia kidato cha tatu. “Niliumia sana kwa sababu mama yangu ndiye alikuwa anahangaika kwa kila kitu na kunitafutia ada halafu baba akaja kunibaka…sitaki kukumbuka, namshukuru sana mama yangu hakunifukuza wala kunichukulia hatua yoyote ile na hata nilipotaka kurudi tena shule alikubali. “Nilisoma kwa bidii na nilipomaliza kidato cha nne nilifaulu vizuri kwa kupata daraja la nne na alama 27, nilienda kusomea ualimu na baada ya kumaliza nikaajiriwa kuja kufundisha hapa Dar es Salaam.  Kisa cha Tekla ni mfano wa matukio mengi yanayowakumba wasichana nchini, wako wanaobakwa bila kutaka na kulazimika kuacha shule kutokana na sheria kutoruhusu kuendelea na masomo. Kitendo cha ukatili kama alichofanyiwa Tekla kinamnyima fursa ya kupata haki zake kama vile ya elimu. Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto uliozinduliwa Jumanne wiki hiii, jijini Dar es Salaam unasisitiza juu ya kupunguza vitendo vya ukatili wa kimwili kwa wanawake na watoto kwani vinaleta kikwazo katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2015. Tafiti zinaonyesha sababu nyingi zilizochangia wasichana kupata mimba na kukatisha masomo yao zinahusishwa pia na vitendo vya ukatili. SABABU ZA KUPATA MIMBA  Faustin Mroso ni Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kwamatuku iliyoko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, anasema wazazi wengi pia wamekosa mwamko wa elimu na hata shule ikipeleka taarifa za kutooneka kwa mwanafunzi wazazi huwa hawatoi ushirikiano. Pia wazazi wanalaumiwa kwa kushindwa kuwatimizia watoto wa kike mahitaji yao ya msingi ya kimasomo. Mmoja wa wanafunzi katika shule moja ya sekondari mkoani Dar es Salaam, anasema amejikuta akianza uhusiano wa kimapenzi ili kupata fedha za kujikimu. “Mama yangu ni mfanyabiashara ndogondogo na baba yangu ni mtumishi wa umma, kila mwezi baba hunipa Sh 50,000 kwa ajili ya nauli na mahitaji mengine ya shule. Lakini baba akishanipa mama hunifuata na kuniomba zile fedha ili aongezee katika mtaji wake. “Huwa naingiwa na huruma na kumpa kwa jinsi ninavyoona anavyohangaika kwa sababu aliwahi kuniambia baba huwa hatoi fedha za matumizi ya nyumbani, anachojua ni kulipa ada na mahitaji mengine ya shuleni,” anasema mwanafunzi huyo ambaye ni mtoto wa pili kuzaliwa kati ya watoto sita wa familia hiyo. Anasema alilazimika kuanza uhusiano wa kimapenzi na kwamba mwanamume aliyekuwa naye alikuwa akimpa Sh 3,000 kila alipokuwa akikutana naye kimwili. Naye Mwalimu…ansema kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi kumechangia wanafunzi wengi kushindwa kupokea mabadiliko ya makuzi kwa umakini. HALI ILIVYO Kila mwaka zaidi ya wasichana 8,000 huacha shule kutokana na mimba. Takwimu za Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi za mwaka 2010 zinaonesha katika shule za sekondari wanafunzi waliokatisha masomo walikuwa 66,069. Katika shule za msingi waliokatisha masomo kwa sababu ya utoro (baadhi ni watoro kwa sababu ya mimba) walikuwa wanafunzi 76,246 na waliofukuzwa kwa sababu ya mimba ni 1,056. Shule ya Sekondari Nanyamba iliyoko mkoani Mtwara ni miongoni mwa shule zilizokumbwa na tatizo hilo ambapo kwa mwaka huu wanafunzi wanane wa kidato cha pili na nne wamepata mimba. Pia katika Shule ya Sekondari ya Kwamatuku iliyoko Wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kati ya Januari hadi Juni mwaka huu, wanafunzi sita wamepata mimba. Mkoani Kilimanjaro wanafunzi 238 wa shule za msingi na sekondari wamepata ujauzito katika kipindi cha kuanzia Januari hadi Agosti mwaka huu. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiki, anasema Wilaya ya Rombo ndiyo inaongoza ambapo wanafunzi waliopata ujauzito ni zaidi ya 60. Kulingana na Sheria ya Elimu ya Mwaka 1978 kifungu 35 na kanuni zake za mwaka 1978 na marekebisho ya 1995 na 2002, mtoto wa kike akipata mimba ni ushahidi tosha kuwa amefanya vitendo vya ngono vilivyo kinyume na sheria za shule hivyo anafukuzwa shule.  MJADALA WARUDI SHULE, WASIRUDI  Kumekuwapo na malumbano ya muda mrefu kuhusu wanafunzi wanaoapata mimba kama waendelee na masomo baada ya kujifungua au la. Kumekuwa na hoja zinazopingana na kukinzana juu ya suala hilo huku nyingi zikitawaliwa na hisia, mitazamo na imani bila kuwapo na ushahidi wa kisayansi. Watoto wanaendelea kuteseka, wanapata mimba na kukatisha masomo, wanaathirika kisaikolojia, wanajikuta wakianza majukumu ya ulezi wangali bado wadogo na kubaki wajinga. Shirika lisilokuwa la kiserikali linalojihusisha na masuala ya elimu (Hakielimu), mwaka 2011 lilifanya utafiti juu ya suala hilo na kupendekeza njia za kufuatwa ili kufikia mwafaka wa jambo hilo. Chapisho la Hakielimu la mwaka 2011 linaonyesha hakuna ushahidi wa wazi ndani ya jamii unaoonesha kuwapo kwa faida za kuwafukuza shule wasichana waliopata mimba. Kulingana na chapisho hilo, maamuzi ya kuwafukuza shule wasichana yanawasukumia kwenye umasikini wa kudumu watoto wanaozaliwa na wasichana hao na hivyo kuendeleza duara la umaskini kwenye familia zao na taifa kwa ujumla. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Bunge, Hadija Telela, anasema kuruhusiwa kwa jambo hilo kutasababisha mmomonyoko wa maadili na hivyo kushusha ubora wa elimu nchini. “Mimi naona wasirudi shule kwa sababu wakiruhusiwa vitendo vya ngono vitaongezeka na kutakuwa na upotovu mkubwa wa nidhamu,” anasema Mwalimu Telela. Naye Sheikh Khalifa Khamis anapinga hoja hiyo kwa sababu mafundisho ya dini hayaruhusu ngono kabla ya ndoa. “Dini zote haziruhusu ngono kabla ya ndoa hivyo, ukiruhusu watoto waendelee na masomo maana yake unahalalisha ngono kabla ya ndoa,” anasema Sheikh Khamis. Naye mkazi wa Temeke, Dar es Salaam, Zawadi Fundiyaya, anashauri watoto wanaopata mimba wakiwa shuleni wasamehewe na kuruhusiwa kuendelea na masomo kwa sababu wengi wanakuwa bado hawajapevuka kiakili. WAZIRI WA AFYA, ELIMU  Waziri Ummy Mwalimu wakati anazindua Mpango kazi wa taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto, alipaza sauti na kutaka wanafunzi wanaopata mimba wafikiriwe kurudi kuendelea na masomo. “Tufikirie watoto wa maskini wanaopata mimba shuleni waendelee na masomo kwa sababu wa kwangu mimi na wewe tutampeleka private (shule binafsi) wataendelea na masomo. “Elimu kwa watoto wa kike ndiyo mwarobaini wa kutokomeza vitendo vya ukatili kwa wanawake na watoto,” anasema Mwalimu. Anasema wataanzisha sehemu rafiki katika shule za msingi na sekondari ili mtoto atakapofanyiwa jambo baya la ukatili aweze kupata msaada wa haraka. “Kutakuwa na kamati za ulinzi na usalama wa mtoto wa kike katika kila mtaa na kijiji na pia utaanzishwa mtandao wa wanaume katika kila kata ili kulinda vitendo vya ukatili,” anasema. Naye Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Mhandisi Stella Manyanya, anasema “Suala la mwanafunzi kupata ujauzito akiwa shuleni ni jambo zito tunaliangalia kwa umakini na kipekee. Tutalifanyia kazi liweze kupata ufumbuzi, liangaliwe kwa mapana utekelezaji wake usiwe na athari kwa maeneo mengine. Pia baadhi ya wadau mbalimbali wa maendeleo wanapendekeza ziwepo shule maalumu za ufundi stadi ambazo watapelekwa wasichana waliojifungua kuendelea na masomo na kupata ujuzi wa kimaisha. Mwalimu mlezi wa wanafunzi wa kike katika Shule ya Sekondari ya Kwamatuku, Christina Kavishe, anashauri kuwekeza kwenye elimu ya afya ya uzazi na uzazi wa mpango kwani pia kutasaidia kunapunguza maambukizi ya virusi vya Ukimwi. “Changamoto zingine zinazoathiri makuzi ya kimaadili kwa vijana ni kutopewa maarifa na taarifa sahihi jinsi ya kutumia miili yao bila kuathiri ndoto zao,” anasema Mwalimu Kavishe. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Said Meck Sadiq, anasema “Kuna mila ya kupeana jani linaloitwa Mashale na kusuluhishana, mila hii ni potofu na inawakandamiza watoto wa kike wanaopewa mimba na wale wa kiume ambao hulawitiwa. Jambo hili linasababisha Jeshi la Polisi kufanya kazi katika mazingira magumu sana. Elimu inabaki kuwa kitovu cha maendeleo ya binadamu popote alipo hivyo cha msingi ni kufanya utafiti kubaini ukweli na uhalisia wa jambo hilo ili tuwe na mtazamo wa kujenga na wala si kubomoa.
kitaifa
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Dk Rehema Nchimbi wakati alipokutana na Watumishi wa Halmashuri ya Mji wa Makambako, alisema mradi wa Liganga na Mchuchuma utatoa ajira zaidi ya 30,000, zikiwepo za wazawa na wageni.Aliwataka watumishi wa Halmashauri ya Mji Makambako hasa sekta ya ardhi kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ya matumizi ya ardhi.Mipango hiyo ni pamoja na kupima viwanja kuwavutia wawekezaji mbalimbali katika ujenzi wa hoteli za kisasa na halmashuri kuhakikisha wanaboresha miundombinu ya maji na barabara.Dk Nchimbi alisema mpaka sasa Shirika la Maendeleo ya Taifa (NDC), limeanza mchakato wa uthamini wa mali za wananchi ili waweze kulipwa fidia kupisha mradi huo.Aliwataka wananchi wa Makambako na Njombe kujiandaa na ujio wa wageni mbalimbali kwa kufuga kuku, ng’ombe na mifugo mingine kuuzia wageni hao ili kuongeza kipato cha familia.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Makambako, Hanana Chesco Mfikwa alisema kuwa wanajiandaa kupokea wageni hao kwa kuhakikisha wanaweka mipango mizuri ambayo itasaidia wageni kuwekeza zaidi katika eneo la Makambako.
uchumi
MABINGWA wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara, Simba, wameialika Asante Kotoko ya Ghana kucheza nayo mechi ya kirafiki katika kilele cha maadhimisho ya Simba Day Agosti 8, mwaka huu.Simba hufanya tamasha hilo Agosti ya kila mwaka ambapo kabla ya kufikia kilele tarehe nane, hufanya shughuli mbalimbali za kijamii ikiwa ni pamoja na kutembelea wagonjwa na kutoa misaada kwa wasiojiweza na kumalizia na kucheza mechi ambapo pia hutambulisha kikosi chake pamoja na jezi watakazotumia kwa msimu mpya.Akizungumzia mechi hiyo Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara amesema wamechagua Asante Kotoko kutokana na historia yake ya kufanya vizuri ukanda wa Afrika Magharibi na michuano ya Klabu bingwa Afrika.“Hii ni timu kubwa Afrika na inatajwa kuwa klabu namba moja kwa Ghana, na namba mbili kwa Afrika katika karne ya 20 nyuma ya Al Ahly ya Misri,” alisema.Alisema timu hiyo iliwahi kucheza na Yanga mwaka 1969 kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika na kutoka sare mechi zote mbili nyumbani na ugenini.Pia, iliwahi kuchukua mataji mawili ya Afrika mwaka 1970 na 1983 na Ligi Kuu ya Ghana mara 24, mara ya mwisho ilikuwa msimu wa mwaka 2013/2014.Kwa sasa wekundu hao wa Msimbazi wanaendelea na mazoezi ya kujiandaa na msimu mpya nchini Uturuki na wanatarajiwa kurejea mwishoni mwa wiki hii tayari kwa tamasha hilo.Kuhusu tamasha la wiki ya Simba, Mratibu wake ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya EAG, Imani Kajula alisema watatumia wiki hii kutambulisha jezi za nyumbani na ugenini keshokutwa.Amesema pia, maveterani wa klabu hiyo watawatembelea wenzao wa Yanga na kuchangia damu kwenye matawi, kutembelea vituo vya watoto yatima na kutoa misaada na shughuli nyingine mbalimbali.Kajula amesema, baada ya mchezo siku hiyo ya tamasha kutakuwa na hafla ya chakula cha jioni itakayohudhuriwa na mashabiki, wachezaji na wadau kwa ajili ya kuwashukuru wachezaji.
michezo
WIKI iliyopita, nilianza makala haya yanayolenga kuwahimiza Watanzania wenzangu kumsaidia Rais wetu, John Magufuli, kutekeleza ahadi yake kubwa kwa Watanzania ya kuipeleka nchi katika uchumi wa kati ifi kapo mwaka 2025.Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, hatuna rais mwingine zaidi ya Magufuli aliyechaguliwa kidemokrasia na Watanzania na hivyo hata ambao hawakumchagua wanapaswa kumuunga mkono kwa sababu hakuna namna nyingine na siku rais atakapochaguliwa kila Mtanzania atapaswa kumuunga mkono pia.Ili kufikisha ujumbe wangu sawia, katika makala haya nimewagawa Watanzania katika makundi manne ambayo kila kundi lina nafasi muhimu sana katika kuchagiza maendeleo ya nchi yetu.Tumeshaangalia kundi la kwanza la viongozi au wasaidizi wa karibu wa Rais kuhusu mambo ambayo wanapaswa kuzingatia katika usaidizi wao huo utakaoharakisha nchi yetu kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda. Kwa muhtasari nilisema kwamba watanzania wenzetu hawa wenye mamlaka ya kuongoza na kutoa uamuzi wanapaswa kumwelewa Rais anataka nini na hataki kitu gani, kuzifahamu kwa uhakika wake sheria, sera, kanuni na miongozo mbalimbali wanayopewa, kuwa wabunifu, kuwa wacha Mungu na kadhalika na kadhalika.Leo tutaendelea na makundi mengine ambayo ni ya wanasiasa wa kambi ya upinzani, wafanyakazi walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi na watanzania wenzangu ambao hawana kazi ya kuajiriwa au kujiajiri.Nikianza na wanasiasa wa kambi ya upinzani ni muhimu kwao pia kuunga mkono mambo mazuri yanayofanywa na serikali iliyoko madarakani na kuonesha penye upungufu kama upo wakilenga kuboresha zaidi mambo kwa faida ya wananchi na siyo vinginevyo. Kinacholeta mushkeli ni hulka yao ya kupinga kila kitu, kukatishana tamaa na kuvizia makosa ya kibinadamu yanayofanywa na viongozi wetu na kuyavalia njuga badala ya kufanya ukosoaji wenye kujenga.Yaani wapinzani wetu ni kama vile wanaombea kila mara viongozi wetu wakosee kama si kuiombea nchi mabaya! Ni kweli kwamba nchi haiongozwi na malaika na kama ndivyo, huwezi kutotegemea waliopo madarakani wasifanye makosa kama binadamu, lakini kinachotakiwa ni kukosoa kwa njia yenye staha na stara.Lakini tunachoshuhudia kwa wapinzani wetu ni kutounga mkono hata mambo mengi mazuri yanayofanywa kama vile ujenzi wa reli ya kisasa, ujenzi wa bwawa la kufua umeme (Stiegler’s Gorge) utakaoihakikishia nchi yetu umeme wa uhakika, ununuaji wa ndege ili kuboresha utalii wetu na kadhalika na kadhalika. Sijawahi kusikia hata siku moja mpinzani akipongeza yale yanayofanywa na serikali ya JPM hata yale ambayo huko nyuma walikuwa wakiyapigia kelele kama vile kupambana na ufisadi, kudhibiti rushwa, kuhimiza uwajibikaji katika sekta ya umma, kudhibiti mapato ya serikali na kudhibiti ubadhirifu.Matarajio ya wengi ni kwamba upinzani ungekuwa unaunga mkono yanayofanyika na kisha kutoa mapendekezo kwa ukijipigia debe kwamba pamoja na mazuri hayo, wenyewe ungekuwa madarakani ungefanya vizuri zaidi na kueleza njia mbadala ambazo wangetumia. Katika siku za karibuni tumemsikia kiongozi mmoja wa upinzani akiwa nje ya nchi akishambulia serikali na kuipaka matope kadri anavyoweza ili ionekane haina hata moja la maana walilofanya kwa ajili ya mustakabali wa nchi yetu.Katika hali kama hii huwezi kusema kuna mchango wa maana unaofanywa na upinzani hata kama ni jicho mbadala (watch dog) katika kuiletea nchi maendeleo. Kundi la tatu ambalo ningependa kulielezea, kwa jinsi gani lina nafasi adhimu katika kuchangia maendeleo ya nchi yetu kuelekea Tanzania ya uchumi wa kati ni la wafanyakazi wa nchi hii; walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi.Hawa ndio wazalishaji wakubwa na watoa huduma muhimu kwa Watanzania. Ni kundi ambalo linahusisha pia wakulima wa nchi hii. Jambo muhimu kabisa kufanywa na kundi hilo ni kuchapa kazi kwa bidii kwa maana ya kuwajibika ipasavyo kuanzia asubuhi hadi jioni. Walioko maofisini, hususani katika sekta ya umma, hawapaswi kufanya kazi kwa mazoea na wanapaswa kumwelewa Rais anataka nini kwao kupitia falsafa ya hapa kazi tu.Kwa wale wanaojishughulisha na kazi katika sekta zisizo rasmi ili kujipatia riziki zao, mbali na kuchapa kazi kwa bidii wanao wajibu mwingine muhimu wa kulipa kodi stahiki, kwa mujibu wa kanuni, taratibu na sheria za nchi. Ni kwa kulipa kodi wataiwezesha serikali kuboresha huduma muhimu kwa wananchi na ambazo ni muhimu katika kuchagiza maendeleo ya nchi yetu.Kundi hili linapaswa kujiepusha na aina yoyote ya uhujumu uchumi au kuhujumu mipango mingine ifanywayo na serikali au kuleta upinzani dhidi ya mikakati mbalimbali inayosimamiwa na Serikali iliyopo madarakani. Kundi hili linapaswa pia kuendeleza kielimu na kiujuzi ili kuzalisha zaidi na kujiandaa kwa ajili ya Tanzania ya viwanda. Watanzania hawa walio katika sekta rasmi na isiyo rasmi wanapaswa kuwa tayari kutoa taarifa zozote zinazohatarisha amani ya nchi kwa uongozi husika.Lakini pia wanapaswa kujiepusha na upinzani wowote usio wa msingi dhidi ya mikakati ya maendeleo, inayobuniwa na kusimamiwa na serikali iliyopo madarakani. Hata kama wao ni wafuasi na mashabiki wa vyama vya siasa vya upinzani, wasipige siasa katika masuala ya msingi ya maendeleo ya nchi yetu au kuikwaza serikali isifanikiwe katika malengo yake bali wapige siasa zenye maendeleo.Washiriki kwa kila lenye manufaa kwa nchi yao na hususani nyakati maalumu za uchaguzi ili kuchagua viongozi bora wanaowataka na siyo bora viongozi. Kundi la mwisho kwa mtazamo wangu ambalo nilipenda kulizungumzia katika makala haya ni la Watanzania wenzangu ambao hawana kazi ya kuajiriwa au ya kujiajiri. Hawa ni Watanzania tegemezi.Kundi hili kwa kiasi kikubwa linahusisha wanafunzi walio katika ngazi mbalimbali kuanzia shule za msing hadi vyuo vikuu. Ni kundi pia linalohusisha walemavu wa aina mbalimbali, wazee, watoto, akina mama wasiojishughulisha zaidi ya kuwategemea waume zao na wale ambao bado wanahangaika kutafuta kazi na kadhalika. Nianze na wanafunzi wa shule za msingi na sekondari pamoja na wanavyuo (hususani waliokwenda vyuoni wakitokea mashuleni).Kundi hili linalo nafasi ya kumsaidia Rais kutimiza ndoto zake kwa kutimiza majukumu yao ya kujifunza kwa bidii, kwa umakini ili kuelewa kwa uhakika wanachofundishwa. Inaelezwa na wataalamu kwamba hakuna uwezekaji muhimu kwa nchi kama wa kuwekeza katika rasilimali watu ambao ni msingi mkubwa wa maendeleo ya taifa lolote. Ni katika muktadha huo serikali hii imeamua kurejesha utaratibu uliokuwepo wakati wa serikali ya awamu ya kwanza wa kutoa elimu bure kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.Watanzania hawa walioko mashuleni na vyuoni sasa, ndio wanaotarajiwa kuungana na wenzao walioko makazini muda huu katika kujenga uchumi huo wa kati unaojikita katika maendeleo ya viwanda. Hivyo wanafunzi na wanavyuo, mbali na kutumia muda wao vizuri katika masomo, wanatakiwa kumsaidia Rais kwa kutii na kusikiliza maelekezo yote halali yatolewayo na viongozi wao, na kuyatekeleza kwa muda mwafaka.Kwa wale walioko kwenye taasisi za umma wanapaswa kutumia mali za shule na vyuo kwa uangalifu na kwa usahihi. Kwa kutekeleza haya na mengine mengi watakuwa wametimiza wajibu na majukumu yao vema, hivyo kwa namna moja au nyingine kumsaidia Rais kutimiza azma yake ya kulifikisha Taifa katika uchumi wa kati. Kwa wale wasio na ajira ya aina yoyote nao wanayo nafasi adhimu ya kutekeleza majukumu na wajibu wao mbalimbali katika sehemu zao wanamoishi. Kwanza kwa wale wenye uwezo wa kufanya kazi watafute kazi badala ya kujibweteka.Katika jamii yetu, mbali na kilimo zipo shughuli nyingi za kufanya na mtu kujiingizia kipato. Lakini kama ilivyo kwa makundi mengine, hawa wanapaswa pia kuwa waaminifu na kutii maagizo na miongozo ya viongozi wa ngazi mbalimbali katika maeneo yao, kutoshiriki katika uhalifu au matukio ya uvunjifu wa amani na sheria, kusikiliza maelekezo mbali mbali kutoka kwa viongozi wao na kuyatekeleza kwa uaminifu.Inawezekana yapo makundi niliyoyasahau lakini kama nilivyosema mwanzo, baada ya John Magufuli kuchaguliwa kuwa rais na Watanzania walio wengi, ndiye sasa rais wetu watanzania wote kwa sababu hiyo ndio demokrasia na hivyo hatuna budi kumuunga mkono hadi atakapochaguliwa rais mwingine.Ni kwa mantiki hiyo, kila mtanzania anao wajibu na jukumu la kumsaidia kuweza kufikia malengo aliyojiwekea katika serikali yake, kwa kutekeleza majukumu, wajibu na kutii sheria za nchi. Waswahili wanasema usione vyaelea vimeundwa na hivyo tunavyoona mataifa makubwa yameendelea, tusidhani maendeleo yale yalishuka kutoka mbinguni bali wananchi waliwaunga mkono viongozi wao kwa hali na mali. Shime kila mtanzania amuunge mkono Rais kwa nafasi yake. Mwandishi wa makala haya ni msomaji na mchangiaji wa gazeti hili.
kitaifa