content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
KOCHA wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali amemuondoa kipa aliyeasi wa timu hiyo Beno Kakolanya na kumbeba kipa chipukizi wa timu hiyo, Ramadhani Kabwili.Ramadhani Kabwili alicheza kwa dakika 90 kwenye mchezo wa juzi dhidi ya mahasimu wakubwa wa timu hiyo, Simba na kuonesha kiwango bora, hali iliyomuibua kocha wa makipa wa Yanga, Juma Pondamali aliyesema kuwa kipa huyo wa timu ya taifa ya vijana alionesha kiwango kizuri kwenye mechi hiyo.“Baada ya mechi ya jana hakuna atakayemkumbuka Beno Kakolanya kwa namna ya kipa wetu chipukizi Ramadhani Kabwili alivyocheza, alionesha utulivu mkubwa langoni na alijiamini muda wote wa mchezo.“Kuna wakati alitumia akili wakati Yanga wakishambuliwa mfululizo alijifanya ameumia na kutuliza presha ya timu. Pale alionesha ukomavu mkubwa, maana pengine kama asingefanya vile Simba wangeweza kupata bao wakati ule,” alisema Pondamali aliyedai kuitumikia nafasi ya ugolikipa kwa zaidi ya miaka 15.Pondamali alisema Kakolanya hawezi kuwa mkubwa zaidi ya timu kwa kuwa alidaka vizuri mechi moja ya Simba na Yanga na kusema kuwa hiyo ilikuwa mechi yake ya kwanza kudaka baada ya kuondoka Ally Mustapha’Barthez’ na Deogratius Munishi’Dida’.“Kakolanya amekuwa kipa chaguo la kwanza msimu huu, msimu uliopita Youthe Rostand alikuwa chaguo la kwanza, lakini wakati wapo Dida na Barthez yeye alikuwa kipa chaguo la tatu, sasa kwa kuwa alidaka mechi moja ya Simba na Yanga anataka kuikalia kichwani Yanga, hilo haliwezekani,” amesema Pondamali aliyekuwemo kwenye kikosi cha Tanzania kilichoshiriki fainali za Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza, Lagos, Nigeria.
michezo
Beatrice Mosses, Manyara Kijana mmoja aitwae Pascal Mananga (22), amehukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa kidato cha tatu wa Shule ya sekondari Chief Dodo aliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Babati. Akitoa hukumu hiyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Manyara, Simon Kobero aMEsema ameridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo. Hakimu Kobero ameieleza mahakama kuwa Machi 25 mwaka jana mwanafunzi aliyebakwa alimuaga mama yake anaenda kanisani na badala yake alikutana na kijana Pascal ambaye alimwambia aambatane nae hadi anapoishi kijana huyo ili ampe pesa kiasi cha Sh 10,000 akampe baba yake aliyekuwa akimdai na alipofika alimwambia kuwa hana pesa hiyo ndipo mwanafunzi akaendelea na safari yake kuelekea Kanisani. Aliongeza kuwa wakati  mwanafunzi huyo anaelekea Kanisani kijana Pascal alikuwa akimfuatilia kwa nyuma na hadi kufika eneo hilo la korongoni kijana huyo akaanza kumshika akamdondosha chini na kumvua nguo na kuzitupa mbali na baadaye kumbaka. Baada ya maelezo hayo hakimu aliuliza upande wa mashtaka kama wana chochote cha kueleza mahakama, ndipo Wakili wa serikali, Petro Ngassa akaiomba mahakama itoe adhabu kali kwa mshtakiwa ili kutoa onyo kwa watu wote wanaojihusisha na vitendo  hivyo na hasa ikizingatiwa makosa kama hayo yamekuwa yakijirudia sana katika mkoa huo. Baada ya ukimya huo Hakimu Kobero akamwambia mshtakiwa hana namna ya kumpunguzia adhabu hivyo utakwenda jela maisha na atachapwa viboko vinne pamoja na kutoa fidia kwa muathirika kiasi cha Sh milioni nne.
kitaifa
Kibadeni anayesaidiwa na kocha msaidizi Juma Mgunda, alisema wachezaji aliowaita wapo katika hali nzuri na wamekuwa wakifanya mazoezi na kikosi cha Taifa Stars, ambapo wao kama benchi la ufundi wamepata nafasi ya kuwa nao kwa muda mrefu na kutambua maendeleo yao.Wachezaji walioitwa ni magolikipa, Ally Mustafa (Yanga) na Aishi Manula (Azam), Said Mohamed (Mtibwa Sugar), walinzi Shomari Kapombe (Azam), Hassan Kessy (Simba), Mohamed Hussein (Simba), Hassan Isihaka (Simba), Salim Mbonde (Mtibwa), Juma Abdul (Yanga) na Kelvin Yondani (Yanga).Viungo: Himid Mao (Azam), Jonas Mkude (Simba), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Salum Abubakar (Azam), Deus Kaseke (Yanga), washambuliaji John Bocco (Azam), Elias Maguri (Stand United), Ibrahim Hajibu (Simba), Malimi Busungu (Yanga) na Saimon Msuva (Yanga).Michuano ya Kombe la Chalenji inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Novemba 21 na kumalizika Desemba 6, ambapo Kilimanjaro Stars imepangwa kundi A, lenye wenyeji Ethiopia, Rwanda na Somalia.Wachezaji Said Mohamed, Juma Abdul, Hassan Kessy, Hassan Isihaka, Salum Abubakar na Ibrahim wanaendelea na mazoezi jijini Dar es Salaam chini ya kocha msaidizi Juma Mgunda wakati wanawasubiri wachezaji wengine walioko nchini Algeria na kikosi cha Taifa Stars.
michezo
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
uchumi
MSHAMBULIAJI wa timu ya Simba, John Bocco ‘Adebayo’ ataukosa mpambano wa leo dhidi ya Walima Alzeti, timu ya Singida United wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini hapa.Meneja wa klabu ya Simba, Patrick Rweymamu alisema jana kuwa Bocco ataukosa mchezo huo kutokana na kuwa majeruhi, lakini anaendelea kuwa fiti akifanya mazoezi mepesi.Alisema msafara wa timu hiyo umetua Arusha ukiwa na wachezaji 22, lakini majeruhi wengine waliobaki jijini Dar es Salaam ni Mohamed Hussein ‘Shabalala’, Jonas Mkude, Ally Salehe na Shomari Kapombe, ambaye yeye ana mata- tizo ya kiafya kidogo. Rweymamu alisema wamewasili salama Arusha na msafara wa watu 32, 22 waki- wa na wachezaji na wako vizuri tayari kwa kipute hicho cha leo, kwani wanataka kuendeleza ushindi ili kuzidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo yenye timu 20. Pia alisema timu yao inaelekeza nguvu zake katika Kombe la FA ili kuhakikisha wanafanya vizuri katika michuano hiyo ambayo hutoa mwakilishi wan chi katika Kombe la Shirikisho Afrika. Alisema Nia yao ni kuweza kupata matokeo ili kurudi katika mashindano ya kimataifa msimu unaokuja. Alisema kwa mapokezi waliyoyapata wanawashukuru wana Arusha na mikoa ya jirani kwa mapenzi makubwa waliyoyaonesha na kupitia hilo wapo tayari kutoa burudani ya ushindi, ambapo aliwaomba kujitokeza kwa wingi kuishambulia timu yao. Mabingwa hao wa soka Tanzania Bara waliwasili jijini Arusha jana saa tano asubuhi na kupokelewa kifalme na mamia ya mashabiki kuanzia Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).Naye Kocha Mkuu wa Singida United, Ramadhan Nsanzurimo alisema wamejiandaa vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo. Alisema Simba ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri, lakini wao wamejiandaa vyema kukabiliana nao licha ya kwamba wako katika nafasi ya mwisho na hiyo itakuwa chachu kwao kufanya vizuri ili kujinasua mkiani.
michezo
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ameibua madudu ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa jana, ikiwa ni siku yake ya tano ya ziara yake mkoani Iringa, yakimhusisha Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Hamid Njovu na ofi sa ardhi wake. Madudu hayo yameibuliwa ikiwa ni siku moja tu baada ya kushusha rungu lingine kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo Asia Abdallah anayetuhumiwa kuwanyanyasa na kuharibu mahusiano ya kazi na wasaidizi wake na baadhi ya watumishi wa halmashauri ya wilaya hiyo. Akizungumza na watumishi wa halmashauri mbili za wilaya ya Iringa jana, Majaliwa aliyetumia muda mwingi kuzungumzia miiko ya uongozi, maadili ya kazi na mahusiano mahali pa kazi, alisema mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa ya Iringa amepuuza waraka wa serikali, unaozuia kugawa maeneo ya shule kwa matumizi mengine nje ya shule hizo. Waziri Mkuu alisema katika Shule ya Msingi Gangilonga, Mkurugenzi huyo Hamid Njovu amegawa eneo la michezo la shule hiyo kwa mwekezaji (hakumtaja jina) aliyejenga ukumbi wa burudani na milango ya biashara kinyume na taratibu. “Mkurugenzi wa Manispaa unauza viwanja vya shule. Umeuza eneo katika shule hiyo ya Gangilonga halafu unajifanya mmekodisha. Mnaruhusu vipi ujenzi wa ukumbi wa burudani katika eneo la shule?” alisema na kumtaka mkurugenzi huyo kupitia waraka, unaozuia kuwekeza miradi tofauti na ya elimu katika viwanja vya shule. Akiendelea kushangazwa na uamuzi huo, Waziri Mkuu alisema katika makubaliano yao na mwekezaji huyo, halmashauri hiyo “eti itakuwa ikijipatia shilingi 400,000 kila mwezi. Nyie...nyie...inawezekanaje?” Katika shule za msingi Wilolesi na Lugalo zilizopo katika eneo moja, Waziri Mkuu alisema mkurugenzi huyo amemega eneo kwa mwekezaji aliyeanzisha bustani ya maua na anayetaka kujenga ukumbi kwa ajili ya shughuli za burudani. Alisema wakati mkurugenzi aliyepita wa halmashauri hiyo, alikataa shinikizo la ugawaji wa maeneo ya shule hizo kwa wawekezaji, Njovu alitoa maeneo hayo kwa kisingizio cha kuongeza vyanzo vipya vya mapato. “Nakuagiza mara tu baada ya kumaliza kikao na watumishi hawa, nataka ukawaandikie barua wawekezaji ya kusitisha ujenzi wanaoendelea nao katika viwanja vya shule hizo na kubomoa chochote walichojenga,” alisema na kutoa saa nne za kukamilisha kazi hiyo. Mbali na barua hizo kupelekwa kwa waliopewa maeneo ya shule hizo ndani ya saa hizo nne, aliagiza nakala zake zipelekwe Ofisi ya Rais Tamisemi na ofisini kwake.“Nataka ofisi ya Waziri Mkuu ipate barua leo (jana) na nitakapokuja tena Iringa Novemba mwaka huu nikute maeneo hayo ya shule yako safi na yawe yamezungushiwa ukuta,” alisema huku akishangazwa na uamuzi huo uliofanywa bila kushirikisha kamati za shule hizo. Pamoja na kutozishirikisha kamati hizo, alisema kumekuwepo na shinikizo kutoka kwa uongozi wa halmashauri hiyo wa kuwahamisha wakuu wa shule hizo, kwa sababu ya kutokubaliana na maamuzi hayo.“Naagiza wakuu hao wa shule waendelee na majukumu yao na sitaki kusikia mkiendelea na mipango yoyote ya kuwahamisha,” alisema huku akishangiliwa na watumishi waliokuwa wakimsikiliza.Waziri Mkuu alimgeukia mwanasheria wa manispaa hiyo, Nicholaus Mwakasungura na kumshangaa kwa kutoa ushauri mbovu kwa mkurugenzi na kamati ya madiwani iliyoridhia uamuzi huo. “Huenda hawa madiwani sio wataalamu kama ninyi. Kazi yenu ni kutoa ushauri wa kitaalamu na kisheria pale mambo mazito yanapopelekwa kwao. Sasa wewe mwanasheria umeshauri maeneo hayo wapewe wafanyabiashara hao halafu kwenye mkataba umemuacha mkurugenzi wako asaini ili likitokea la kutokea ujue namna ya kumruka,” alisema. Alisema wakati mkurugenzi huyo akiingia mikataba hiyo ya hovyo, shule hizo zinaelemewa na idadi kubwa ya wanafunzi, ambao wangeweza kupunguzwa kwa kujenga vyumba vingine vya madarasa katika maeneo waliyopewa wafanyabiashara hao. Akizungumzia tuhuma za Ofisa Ardhi wa Manispaa hiyo, Wenslaus Mtui, Waziri Mkuu alisema ni mtumishi anayelalamikiwa sana kujinufaisha kupitia idara yake hiyo kwa kujimilikisha viwanja vingi. Huku akiamuru asimame katika kikao hicho ili ajibu tuhuma zake, Majaliwa alisema mbali na kujimilikisha viwanja, ofisa ardhi huyo alibadilisha umiliki wa viwanja namba 1MD na 2MD kutoka kwa wamiliki wa awali na kumpa mtu aliyetajwa kwa jina la Musa Ngezi.Akikiri kuufahamu mgogoro huo, Mtui alikataa kummilikisha Ngezi viwanja hivyo na ndipo Waziri Mkuu alipomuagiza Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kuushughulikia hadi majibu yake yatakapopatikana. “Mkuu wa Mkoa nakukabidhi taarifa hii na naomba ulifuatilie jambo hili. Serikali hii inahitaji watumishi waadilifu na wachapa kazi,” alisema.Awali Mkuu wa Mkoa wa Iringa Ally Hapi aliwakumbusha watumishi wa wilaya hiyo kujiepusha na rushwa, huku akiwataka kuchapa kazi kwa bidii ili kuongeza kasi ya maendeleo ya taifa na wananchi wake. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa, Dk Abel Nyamahanga alisema katika halmashauri hizo, wapo baadhi ya watumishi wamejigeuza na kuwa kama miungu watu na kuwanyanyasa watumishi wa chini yao. Aliwakumbusha watumishi hao wazingatie kauli ya Rais John Magufuli, inayotaka Serikali ya Awamu ya Tano iongoze watu wenye furaha
kitaifa
Na  BENJAMIN MASESE-MWANZA NDEGE  ya  Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) aina ya Bombardier Q Dash 400 namba   5H TCB, juzi ilizua taharuki kwa abiria baada ya kushindwa kuruka katika  uwanja  ndege wa Mwanza, imefamika. Kitendo hicho kilisababisha abiria kupiga kelele wakitaka  kushushwa. Tukio hilo lilitokea juzi saa 1.00 jioni wakati ndege hiyo ikijiandaa kuruka   kwenda Dar es Salaam ikiwa na abiria zaidi ya 30.  Mmoja wa abiria wa ndege hiyo, Juma Robi mkazi wa Musoma alisema ndege ilishindwa kuondoka  huku   ikitoa mlio tofauti ilivyo kawaida yake. Hilo ni tukio la pili kutokea kwa ndege  za shirika hilo baada ya mwezi uliopita kuruka na baada ya dakika mbili  ikarejea na kutua  tena katika uwanja huo. Ilidaiwa  kuwa ilitokana na kutofungwa   vizuri mlango wa mizigo huku taarifa nyingine zikidai ilikuwa ni hitilafu ya  kawaida. Abiria waelezea  Mwandishi aliyefika  katika uwanja huo alikuta abiria  wakiwa wameshushwa huku kila mmoja akiwa anampigia ndugu yake simu kujumlisha hali ilivyokuwa. Nao uongozi wa uwanja huo  ulilazimika kuwachukua abiria  wote  na kuwapeleka katika hoteli kwa ajili ya chakula. Robi akizungumza na MTANZANIA  akiwa katika Hoteli ya Kigdom,  alisema alifika  uwanjani  saa 11 jioni kwa mujibu wa tiketi yake na akapanda kwenye ndege hiyo saa 1.00. Alisema wakati wanajiandaa kuondoka    ndege   ilitoa sauti   ambayo si ya kawaida hali iliyosababisha abiria waangaliane kwa mshangao na hofu. “Ilipojaribu kuisogea  mbele ilishindikana maana sauti ilikuwa kubwa ya muungurumo,  yaani kila mmoja alikuwa na hofu na wengine wakaanza kupiga kelele kutaka kushushwa, hali ilivyozidi tukawa hatuelewani ndipo walipoamua kutushusha na mizingo yetu. “Walitupandisha  kwenye gari lao na kutuleta mitaani kula, tumeanzia katika  Hoteli ya  Starmax ya Kirumba lakini hatukupata chakula. “Tumehamishiwa hapa  Kigdom  na  kupata chakula, wametueleza saa 6.00 tutaondoka kwenda Dar es Salaam lakini hii ni hasara maana wengine tulikuwa tumekodi nyumba, gari za kutupokea sasa sijui itakuaje. Kauli ya ATCL Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Bodi ya ATCL,  Emmanuel Koroso, alikiri ndege hiyo kupata hitilafu wakati ikijiandaa kuruka   kwenda Dar es Salaam. “Ni kweli  kuna tukio la  moja ya ndege zetu kupata hitilafu wakati ikijiandaa kuruka hapa ikiwa na abiria,    kilichotokea katika ndege yetu ni hitilafu ya mawasiliano baada ya kutoa  indicator (viashiria) ya mfumo wa mafuta ambayo  kwa namna moja au nyingine si sahihi. “Baada ya hapo kama unavyojua ATCL ina ndege nyingine…ilikuja nyingine na kuwachukua usiku huo huo na kuwapeleka Dar  es Salaam, walifika salama muda wa saa 7.00  usiku. “Tunavyozungumza hivi tayari mafundi wamefanya utafiti wa tatizo hilo lililojitokeza na wamerusha ndege hiyo kwa majaribio hapa uwanjani wakiwa na rubani. “Wamejiridhisha ni salama, tulichoamua ni kwmaba ndege hii irudi Dar es Salaam bila abiria   iweze kupangiwa ratiba nyingine ya safari,” alisema. Uongozi wa TAA   Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Uwanja wa Ndege Tanzania (TAA), Mkoa wa Mwanza, David Matovolwa, alisema ndege hiyo ilikuwa katika ratiba yake ya kila siku na iliwachukua abiria hao kama kawaida lakini kabla ya kuruka ikatokea kuwapo na hitilafu.  Mazoezi ya ndege hiyo Baada ya ndege hiyo kushindwa kuruka juzi usiku, iliwekwa pembeni ya uwanja ambapo jana asubuhi ilikuwa ikifanyiwa marekebisho  huku ikiwasha mara kwa mara na baadaye kuijaribisha kuruka na kutua. Ilipofika saa 3.50 ilijaribiwa kurushwa angani ambako ilizunguka na kurejea tena saa 4:01 asubuhi. Hata hivyo ilipofika saa 4.40  iliruka kwenda Dar es Salaam ikiwa na rubani na wahandisi waliokuwa wakiifanyia uchunguzi wa tatizo lake.
kitaifa
['Ghana, Senegal na Ivory Coast zote zilishindwa kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani (CHAN) 2020 siku ya Jumapili', 'Ghana ilishindwa kulipiza bao moja iliyofungwa katika mkondo wa kwanza dhidi ya Burkina Faso, na kutoka sare tasa mjini Ouagadougou.', 'Hii inamanisha kuwa Black Stars hawatashiriki fainali za mashindao hayo ya Cameroon 2020 ambayo yanachezwa na wachezaji wa Afrika katika mataifa waliozaliwa.', 'Senegal, pia ni timu kubwa iliyoondolewa katika fainali hizo baada ya kushindwa na Guinea kupitia mikwaju ya penati.', 'Senegal ilienda Conakry ikiwa kifua mbele kwa bao 1-0 lakini Guinea ilijitutumua katika mechi yao ya nyumbani na kujipatia ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Mamadouba Bangoura.', 'Baada ya kutoka sare ya 1-1 katika mechi zote, wenyeji walifuzu kupitia mikwaju ya penalti 3-1.', 'Ivory Coast ilishindwa kufuzu katika fainali hizo licha ya kushinda mechi yao ya nyumbani dhidi ya Niger 1-0. ', 'Timu hiyo ilishindwa mabao 2-0 na Niger katika mkondo wa kwanza kumaanisha waliondolewa kupitia wingi wa mabao 2-1 .', 'Siku ya Jumapili pia, Zimbabwe ilijikatia tiketi ya kushiriki mashindano hayo ya Cameroon mwaka 2020 baada ya kutoka sare tasa dhidi ya Lesotho lakini ikafuzu kwa wingi wa mabao 3-1.', 'DR Congo iliichapa Jamhuri ya Afrika ya Kati mabao 4-1 mjini Kinshasa ushindi ambao uliwapatia jumla ya mabao 6-1 huku nao Congo Brazzaville wakifuzu kwa bao 1-0 la nyumbani dhidi ya Equatorial Guinea na kunyakua jumla ya mabao 3-2.', 'Katika eneo la kaskazini,Tunisia ilijikatia tiketi ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa jumla wa mabao 3-1 dhidi ya Libya.', 'Mali pia itashiriki mashindano hayo baada ya Cameroon, baada ya kuinyuka Mauritania jumla ya mabao2-0. ', 'Nigeria iliathiriwa zaidi katika mashindano hayo baada ya kushindwa na Togo siku ya Jumamosi huku bingwa watetezi Morocco wakipata ushindi dhidi ya Algeria. ', 'Timu zilizofuzu kwa mashindano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za ndani, (CHAN) yatakayoandaliwa na Cameroon:']
michezo
Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia Na Mwandishi Wetu-DAR ES SALAAM KAMPUNI ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania PLC, imetangaza kuongeza muda wa uuzaji wa hisa zake hadi Mei 11. Akizungumza Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Rosalynn Mworia, alisema hatua hiyo inatokana na kupokea maombi mengi ya kutaka kununua hisa za kampuni hiyo. “Vodacom Tanzania PLC inatarajia kupokea maombi mengi ya kununua hisa katika kipindi cha wiki hii. “Pia kutokana na ushauri kutoka serikalini na makundi mbalimbali muhimu ya kijamii yanayohitaji kuwekeza, wakiwamo wabunge, makundi ya watumishi wa kada mbalimbali wa serikali na maofisa wa vyama vya ushirika kutoka sehemu mbalimbali za nchi, tumewasilisha maombi na kupata idhini kutoka Mamlaka ya Soko la Mitaji na Dhamana (CMSA) kuongeza muda wa zoezi la kuuza hisa kwa kipindi cha wiki tatu hadi kufikia Alhamisi ya Mei 11, mwaka huu,” alisema Mworia. Mkurugenzi huyo alisema kuongezeka kwa muda wa mwisho wa kununua hisa kutawezesha wanaohitaji kununua hisa kwa makundi binafsi na taasisi zilizoomba muda uongezwe kushiriki kikamilifu katika mchakato huo. Alisema wanatoa shukrani kwa Watanzania ambao wamejitokeza kuwekeza kupitia kununua hisa na kuwakaribisha ambao bado hawajanunua kuchangamkia fursa hiyo katika muda huo wa nyongeza. “Mgawanyo na mchanganuo wa umiliki wa hisa inapendekezwa utafanyika kuanzia Mei 19, mwaka huu na kuendelea kabla ya kumaliza mchakato wa mwisho wa kujisajili katika Soko la Hisa la Dar es Salaam katika tarehe iliyopangwa ya Juni 6, mwaka huu,” alisema.
kitaifa
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kwa wananchi juu ya mazoezi mawili tofauti yanayoendelea nchini ya kuandikisha wapiga kura. Aidha imesema Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume haitatumika kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwenzi ujao.Akizungumza Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume, Dk Wilson Charles amesema kwamba uandikishaji unaoendelea ambao ulianza Oktoba 8 mwaka huu unahusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019 ambao hausimamiwi na Tume.“Tume ya Taifa ya Uchaguzi inapenda kuwataarifu wananchi kuwa uandikishaji unaofanyika kuanzia tarehe 08, Oktoba 2019 hadi Oktoba 14, 2019 na kusimamiwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR- TAMISEMI) kupitia Halmashauri mbalimbali kote nchini unahusika na uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika Novemba 24, 2019. Mwananchi asipojiandikisha hataweza kupiga kura katika uchaguzi huo,” alisema Dk Mahera.Aliongeza kwamba mwananchi ambaye hatajiandikisha kwenye uandikishaji unaofanywa na OR-TAMISEMI hatapata fursa ya kushiriki kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa Novemba 24 mwaka huu, hata kama atakuwa na Kadi ya Mpiga Kura inayotolewa na Tume na kwamba uchaguzi huo hausimamiwi na Tume bali unasimamiwa na Ofisi ya Rais-TAMISEMI Amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hilo la kujiandikisha ili wapate fursa ya kuwachagua viongozi wa mitaa yao siku hiyo ya tarehe 24 Novemba 2019.Aidha, Dk Mahera amesema kwamba Tume kwa mujibu wa Ibara ya 74 (6) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ina jukumu la kuandikisha Wapiga Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani kwa Tanzania Bara.“Uandikishaji huo (wa OR-TAMISEMI) ni tofauti na uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura unaofanywa na Tume kwenye mikoa mbalimbali Nchini. Uboreshaji huu unahusu Uchaguzi wa Rais, Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Madiwani wa Tanzania Bara utakaofanyika mwakani 2020,” amesema.Dk Mahera ameeleza kwamba zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura linaendelea kwa sasa katika mikoa ya Tabora, Katavi na Halmashauri ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma ambako uboreshaji utafanyika kuanzia Oktoba 14 hadi Oktoba 20 mwaka huu.Ameongeza kwamba zoezi hilo litaendelea kwenye mikoa ya Songwe, Dodoma na Singida kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba 1, 2019. “Wanaostahili kujiandikisha ni wale ambao wana miaka 18 na wale ambao watafikisha miaka 18 mwakani (2020) kabla ya uchaguzi, lakini pia zoezi linawahusu wale ambao kadi zao zimeharibika au zimepotea ili wapate fursa tena ya kuwepo kwenye Daftari la Kudumu la Wapiga Kura,” alismema Dk Mahera.
kitaifa
Klabu ya Yanga imefiki uamuzi wa kumsafirisha kwa ndege kiungo wake Mohammed Banka kwenda mkoani Kagera ili kuziba kuongozea nguvu kwenye kikosi hicho kinachojianda na mchezo dhidi ya kagera Sugar Uamuzi wa yanga unakuaja ikiwa nis iku moja tangu kutokakwa ripoti ya daktari wa timu juu ya hali umajeraha ya kiungo wao Haruna Niyonzima Haruna. Akizungumza na kituo kimoja cha redio mkoani Kagera muwakilishai wa wadhamini wa klabu hiyo GSM, mkurugenzi wa uwekezaji wa GSM Hersi Said  amesema tayari kiungo huyo yupo njiani kwenda Kagera tayari kwa mchezo wa kesho na anweza kuwa sehemu ya mchezo kulingana na mahitaji ya mwalimu. Ikumbukwe Haruna Niyonzima aliumia kwenye dakika ya sita ya mchezo wa ligi kuu bara dhidi ya Biashara United siku kadhaa zilizopita na kwa mujibu wa vipimo vya madaktari Niyonzima anatakiwa kukaa nje kwa wiki kadhaa.   -Mkurungezi wa Uwekezaji wa GSM, Eng Hersi Said amesema kuwa Baada ya Kiungo Haruna Niyonzima kuumia leo asubuhi kiungo Mohamed Issa Banka anakwea pipa kwenda Bukoba kuongeza nguvu kwenye kikosi cha Yanga kinachotarajia kucheza mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara dhidi ya Kagera Sugar hapo kesho. ⏩Mechi za Simba na Yanga zinasaidia kutatua matizo ya wachezaji A post shared by Soka Extra (@sokaextra_) on Jul 7, 2020 at 7:01am PDT
michezo
JESHI la Polisi mkoani Katavi linawasaka askari wa Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) kwa tuhuma za kuwapiga risasi na kuwajeruhi vibaya watu watano, wanne kati yao wakiwa ndugu wa familia moja ambao ni wakazi wa kijiji cha Ikongwe kilichopo katika wilaya ya Mpanda .Watu hao wamelazwa Hospitali Teule ya mkoa wa Katavi iliyopo katika Mji wa Mpanda. Wakazi hao wanadaiwa kuvamia Hifadhi ya Misitu Msaginya ulioko katika Halmashauri ya Nsimbo wilaya ya Mpanda, ambao unahifadhiwa na kumilikiwa na TFS na kufanya shughuli za kibinadamu ikiwemo kilimo. Majeruhi hao wametambuliwa kuwa ni Filbert Patrick (40) ambaye amejeruhiwa mguuni na wadogo zake watatu Joseph Patrick (27) ambaye amejeruhiwa kifuani, Geofrey Patrick (39) ambaye amejeruhiwa mkono wa kushoto na Januari Patrick (22) aliyejeruhiwa begani. Mwingine ni Nkuba Sai aliyejeruhiwa mkono wake wa kushoto.Kamanda wa Polisi mkoa wa Katavi, Damas Nyanda alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba alifika eneo hilo la tukio na kuokota ganda tupu la risasi ya SMG . “Tayari nimeshaagiza kukamatwa mara moja kwa askari wote wa TFS waliohusika katika tukio hilo ili wahojiwe na sheria iweze kuchukua mkondo wake kwa wale watakaobainika kutenda uhalifu huo.”Kwa upande wake, Mbunge wa Nsimbo, Richard Mbogo alisema amesikitishwa na na kitendo kilichofanywa na askari wa TFS huku akisisitiza kuwa hawakuwa na sababu yoyote ya kutumia nguvu kubwa kiasi hicho. Akisimulia mkasa huo kwa kirefu, Diwani wa Sitalike, Adamu Chelehani alieleza kuwa siku hiyo ya tukio baada ya kupata taarifa kuwa mahindi yanafyekwa na askari wa TFS ambao walikuwa na silaha nzito ...wakazi wa kijiji hicho wapatao 10 walifika eneo hilo na kuwasihi askari hao waache kuyafyeka mahindi kwamba wanayategemea kulisha familia zao.“Hata hivyo, askari hao wa TFS walikaidi na kuendelea kufyeka mahindi ambayo yalikuwa yamekomaa yakitarajiwa kuvunwa mwezi ujao, jambo hilo lilisababisha waanze kuwazomea askari hao ..... Baada ya kuwa wamemaliza kufyeka mahindi kwenye mashamba ya wanakijiji hao, askari hao wa TFS wakiwa na silaha nzito walipanda kwenye gari lao aina ya Land Cruiser huku wanakijiji hao wakiendelea kuwazomea kwa nguvu zao zote,” alieleza. Alidai wakati gari hilo linaondoka askari hao walianza kuwashambulia wananchi hao kwa kuwapiga risasi za moto.
kitaifa
WASHINGTON, Marekani RAIS wa Marekani, Donald Trump alijaribu kuomba msaada wa Rais wa China, Xi Jinping ili kushinda awamu ya pili ya urais, mshauri wake wa zamani  kuhusu usalama wa taifa, John Bolton ameeleza katika kitabu chake kipya. Bolton alisema Rais Trump, aliitaka China kununua bidhaa za chakula kutoka kwa wakulima wa Marekani, kwa mujibu wa maelezo ya awali ya kitabu ambacho kimeanza kuchambuliwa na vyombo vya habari nchini Marekani. Mwandishi wa kitabu pia anasema Rais Trump “alisalia kuwa mbumbumbu wa namna ya kuendesha Ikulu ya White House”. Serikali ya Trump inajaribu kuzuia kitabu hicho kuingia sokoni. Kitabu cha Bolton chenye kurasa 577 kiitwacho The Room Where It Happened (Chumba ambacho yalitokea), kinatarajiwa kuanza kuuzwa Juni 23, mwaka huu. Hata hivyo, Jumatano usiku, Wizara ya Sheria ya Marekani, ilipeleka maombi ya dharura kwa jaji wa mahakama kuzuia uzinduzi wa kitabu hicho. Mchapishaji wa kitabu hicho Kampuni ya Simon & Schuster, imeeleza: “Maombi ya leo ya Serikali hayana uzito na yamechochewa kisiasa.” Imesema maelfu ya nakala za kitabu hicho tayari zimeshasambazwa sehemu mbalimbali ulimwenguni na pingamizi la Serikali halitafua dafu. Kwa upande mwingine, Rais Trump alipiga simu katika runinga ya Fox News na kueleza kuwa: “Bolton amevunja sheria. Hizi ni taarifa za siri na hakupata kibali cha kuzitoa.” “Alikuwa ni mtu ambaye amekwisha kabisa,” aliongeza Rais Trump. “Nilimpatia nafasi .” Bolton ambaye anatajwa kuwa mfuasi wa sera za kimataifa za mabavu, alikuwa kiungo na Ikulu ya White House Aprili 2018 na kuondoka Septemba, mwaka jana.  Bolton alitangaza aliamua kujiuzulu nafasi yake, lakini Rais Trump alisema alimfukuza kwa kuwa alikuwa anapingana naye vikali. Madai ya Bolton ni kuwa mazungumzo hayo yalifanyika baina ya Rais Trump na Rais Xi wakati wa mkutano wa G20 jijini Osaka, Japan Juni, mwaka jana. Rais wa China alilalamika kuwa wakosoaji nchini Marekani, walikuwa wanachochea vita baridi baina ya mataifa hayo mawili, bw Bolton anaeleza kwenye kitabu kama ilivyochapishwa kwenye gazeti la New York Times. “Alisisitiza umuhimu wa wakulima na kuongezeka kwa manunuzi ya China ya magaharage ya soya na ngano kutakuwa na mchango wa matokeo ya uchaguzi.” Baada ya rais Xi kukubali kufanya majadiliano ya manunuzi ya bidhaa za wakulima kuwa kipaumbele katika majadiliano ya kibiashara ya nchi hizo mbili, Trump akamsifu kuwa “kiongozi bora zaidi katika historia ya China.” Mpinzani wa Rais Trump kutoka Chama cha Democrats Joe Biden, ameeleza kuhusu kitabu hicho kuwa: “Kama maelezo haya ni ya kweli, si tu kwamba ni jambo ambalo halikubaliki kimaadili, bali pia ni ukiukaji wa Donald Trump wa majukumu yake kwa Wamarekani.”
kimataifa
Msemaji wa Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara Simba, Haji Manara kalbu hiyo haiendeshwi na maamzi ya mtu mmoja kuna unataratibu naye anatoa taarifa kwa kufuata utaratibu huo. Manara amesema hayo leo Mei 7, 2020 wakati akihojiwa na kituo cha habari cha Wasafi walipomuuliza kuhusu baadhi ya wachezaji kutaka kununuliwa na timu nyingine. “Hakuna ofa yeyote iliyokuja kwa mchezaji wetu,kwa sasa Vilabu vinahangaika kupambana na janga la ugonjwa wa corona bado hizo ofa hatujazipokea” “Simba inafanya mambo yake kwa utaratibu ndio maana Kuna bodi ya wakurugenzi. Simba haiendeshwi na maamuzi ya mtu mmoja, ina utaratibu wake na mimi natoa taarifa za klabu kwa utaratibu,” amesema Manara. Kuhusu tetesi za usajili kwa wachezaji wa Simba SC " Hakuna ofa yeyote iliyokuja kwa mchezaji wetu,kwa sasa Vilabu vinahangaika kupambana na janga la ugonjwa wa corona bado hizo ofa hatujazipokea. Simba inafanya mambo yake kwa utaratibu ndio maana Kuna bodi ya wakurugenzi. Simba haiendeshwi na maamuzi ya mtu mmoja, ina utaratibu wake na mimi natoa taarifa za klabu kwa utaratibu". Haji Manara ,Afisa habari Simba SC #WasafiSports #SportArena #SportsCourt #HiiNiYetuSote A post shared by Wasafi FM (@wasafifm) on May 7, 2020 at 5:17am PDT
michezo
BAADA ya kusimama kwa siku kadhaa kupisha mechi za kimataifa, Ligi Kuu Tanzania Bara inarejea tena mwishoni mwa wiki hii huku kila timu ikiwa na moto wa kutaka kushinda. Ligi ilisimama kuipisha timu ya taifa, Taifa Stars iliyocheza na Uganda mechi ya kuwania kufuzu fainali za kombe la Mataifa Afrika, Afcon 2019, mechi iliyochezwa mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kampala na kumalizika kwa suluhu.Timu zote 20 zipo kwenye maandalizi kabambe kuhakikisha zinafanya vizuri kwenye mechi hizo ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa ligi. Washindi wa pili msimu uliopita, Azam wataendelea na kampeni zao Ijumaa wakiwa ugenini kucheza na Mwadui FC ya Shinyanga saa nane mchana huku kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, African Lyon ikiwaalika Wagosi wa Kaya, Coastal Union kutoka Tanga.Azam inaingia uwanjani na nguvu mpya baada ya kurejea kwa mshambuliaji wake mpya Donald Ngoma iliyomsajili msimu huu kutokea Yanga. Ngoma hajaonekana uwanjani muda mrefu kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, lakini sasa anaendelea vizuri na ameshaanza mazoezi takriban wiki mbili zilizopita. Jumamosi, mabingwa watetezi Simba watakuwa ugenini uwanja wa Nagwanda Sijaona Mtwara kumenyana na Ndanda iliyoahidi kupindua meza na kufuta uteja wa kufungwa na Simba mara nyingi. Siku hiyohiyo, Prisons itaialika Ruvu Shooting kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.Mechi nyingine siku hiyo ni kati ya Mbao watakaokuwa nyumbani kwenye uwanja wa CCM Kirumba kuikaribisha JKT Tanzania huku KMC ikiwaalika Singida United kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Lipuli FC itakuwa nyumbani uwanja wa Samora Iringa kuwakabili Mtibwa Sugar na mechi ya mwisho siku hiyo itakuwa Mara ambako wenyeji Biashara watakwaana na Kagera Sugar.Jumapili ya Septemba 16 kutakuwa na mechi mbili, mabingwa wa zamani Yanga wakiwa nyumbani Uwanja wa Taifa kuwaalika Stand United ya Shinyanga na kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya wenyeji Mbeya City watacheza mechi yao ya kwanza nyumbani msimu huu dhidi ya Alliance ya Mwanza. Mpaka sasa Mbao FC, ndiyo vinara wa ligi hiyo wakiwa wamejikusanyia pointi saba baada ya kushinda mechi mbili na sare moja huku Azam FC wakiwa nafasi ya pili na pointi zao sita sawa na mabingwa watetezi Simba waliopo nafasi ya tatu.Yanga wapo nafasi ya 10, baada ya kucheza mechi moja na kuchukua pointi zote tatu dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa ufunguzi. Na timu za Mwadui FC na Mbeya City zinaburuza mkia zikiwa hazina pointi, City wakipoteza michezo yote mitatu wakati Mwadui michezo miwili. Kiujumla timu tatu zinazoshika nafasi za juu zimeonekana kufanya vizuri kwenye mechi za awali hasa Azam FC ambao mpaka sasa katika mechi mbili wamefunga mabao matano huku wakiwa hawajaruhusu nyavu zao kutikishwa.Wanafuatiwa na Simba ambao wamefunga mabao matatu yote yakifungwa na mshambuliaji wake nyota Meddie Kagere na wao hawajaruhusu nyavu zao kutikiswa wakati vinara Mbao FC wao wameruhusu bao moja na kufunga mabao matatu kwenye mechi zao tatu walizocheza. Simba, Yanga na Lyon zilitumia mapumziko kujiweka sawa kwa kucheza mechi za kirafiki ambapo Simba ilicheza dhidi ya AFC Leopard ya Kenya na kushinda mabao 4-2 huku Yanga ikijipima na Lyon na kushinda bao 1-0.
michezo
UMOJA wa Vijana wa CCM (UVCCM), umesema unaridhishwa na utendaji wa Serikali ya Mapinduzi  Zanzibar chini ya Rais Dk. Ali Mohamed Shein. Hayo yalisemwa Ikulu mjini Unguja juzi na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Kheri James, alipokutana na Dk. Shein. Katika kikao hicho Kheri aliambatana na Makamu Mwenyekiti UVCCM, Tabia Maulid Mwita, Kaimu Katibu Mkuu, Shaka Hamdu Shaka na Kaimu Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Abdulghafar Idrissa Juma. Akizungumza katika kikao hicho, Kheri alisema uongozi wa UVCCM, unafurahishwa namna ambavyo Dk. Shein anavyoendelea kujali, kuthamini na kutekeleza ilani ya uchaguzi kwa kuyapatia ufumbuzi matatizo ya wananchi kwa wakati. “Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya Rais Dk Ali Mohamed Shein, imeendelea kujali, kuthamini na kushughulikia shida, kero na matatizo ya wananchi hatimaye kuyapatia ufumbuzi stahili. UVCCM tumeridhishwa mno na kasi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/20,” alisema. Kheri, alitumia nafasi hiyo kuwaasa vijana kuwa na desturi ya kwenda kuchota busara na hekima toka kwa wazee kama njia ya kukomaa kisiasa. “Vijana mnapokwenda kwa wazee, kiuhalisia mnakwenda kuchota busara na hekima. Vijana bila ya msukumo wa fikra na mawazo ya wazee, hatuwezi kujifunza jambo lolote na kukomaa kisiasa. UVCCM tumeridhika na utendaji wa SMZ katika mkakati wa kuzitazama shida na maisha ya wananchi,” alisema.
kitaifa
Ratiba ya hatua ya mtoano ya michuano hiyo inatarajiwa kupangwa leo ambapo itazikutanisha timu zilizotolewa kwenye hatua ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika na zile zilizotinga hatua ya mtoano Kombe la Shirikisho.Yanga ilitolewa na Township Rollers kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 iliyofungwa nyumbani kabla ya kutoka suluhu Botswana hivyo imejikuta ikiwa ni moja kati ya timu zilizoangukia kwenye michuano hiyo.Akizungumza na waandishi wa habari klabuni Yanga jana, msemaji wa timu hiyo, Dismas Ten, alisema benchi la ufundi limetathmini mchezo uliopita na kujua makosa hivyo wanataka kujipanga vizuri wasiyarudie kwenye michuano hiyo na hatimae wafike mbali.Alisema kuwa lengo lao kwa sasa ni kutaka kuhakikisha inajiandaa mapema kwa kukabiliana na mpinzani wao kwani lengo lao ni kutinga hatua ya makundi na hatimae kusonga mbele zaidi.“Baada ya kumjua mpinzani wetu timu itaanza maandalizi makali kwa ajili ya michuano hii, safari hii hatutaki kurudia makosa, tumeshajirekebisha na tunataka kuona jinsi timu itafanya vizuri kwenye michuano hii.Wakati huohuo, Yanga kwa kushirikiana na kituo cha runinga cha Azam TV kimeandaa kipindi maalumu kwa ajili ya klabu hiyo kitakachojulikana kama Yanga TV Show. Azam imekuwa ikifanya hivyo kwa baadhi ya timu za Ligi Kuu ambapo tayari kuna kipindi cha Azam Tv na Simba Tv.Mkuu wa Kitengo cha Michezo wa Azam Media, Baruani Muhuza, alisema jana kuwa kipindi hicho kitaanza kurushwa mapema mwanzoni mwa mwezi ujao.Alisema kuwa kipindi hicho kitakuwa ni tofauti na vipindi vya timu zilizopita kama Azam na Simba kwani wamejiandaa vizuri. Alisema kuwa utofauti utakaokuwa ni kwamba kitakuwa kikiandaliwa kwa sehemu kubwa na klabu ya Yanga hivyo kutoa fursa ya kuonesha mambo mengi ya klabu hiyo.“Aprili mosi kipindi hicho kitaanza kuruka hewani na kila kitu kinakwenda vizuri, tumeingia mkataba na Yanga na kwa asilimia kubwa kipindi kitakuwa kikiandalia kwenye klabu…“Kutakuwa na wachambuzi ambao ni wataalamu wakiwemo wachezaji wa zamani wa Yanga na hata wa sasa hivyo kitakuwa ni cha utofauti mkubwa zaidi ya vile vya timu zingine,” alisema Muhuza.Mbali na hilo, pia Yanga wameingia mkataba na Kampuni ya Media Solution ambapo itatoa huduma kwa mashabiki na wapezni wa Yanga kupata taarifa kila wakati kupitia simu zao za mkononi.Mmoja wa wawakilishi wa kampuni hiyo, Philemon Kabuje, alisema kuwa shabiki atajiunga na mara moja ataanza kupata taarifa kila mara zinapotokea.“Huduma hii itawawezesha wale wote wanaopenda kupata taarifa za Yanga kuzipata mara moja kila zinapotokea hivyo ni wao kujiunga na huduma hii,” alisema Kabuje. Mahasimu wa Yanga, Simba tayari wameshaingia kwenye mfumo huo tangu mwaka jana ambapo mashabiki wake na wale wa soka hupata taarifa za klabu hiyo kwenye Simba App.
michezo
NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dk Angeline Mabula ameagiza kupelekwa timu maalumu kuichunguza Idara ya Ardhi katika Manispaa ya Shinyanga kutokana na kubainika kupunguza kiasi cha fedha kwa baadhi ya wadaiwa wa kodi ya pango la ardhi katika madeni wanayodaiwa.Dk Mabula alitoa maagizo wakati akifunga mkutano wa siku tatu wa Wataalamu wa Sekta ya Ardhi uliomalizika jijini Dodoma.Amesema, sekta ya ardhi katika Manispaa ya Shinyanga imekuwa na mchezo mchafu wa kuwapunguzia wadaiwa sugu wa wa kodi ya pango la ardhi kiasi cha fedha kwa kucheza na mfumo na hivyo kuikosesha serikali mapato kupitia sekta hiyo.“Manispaa ya Shinyanga kuna madudu ya mchezo wa kupunguza madeni, mtu anadaiwa shilingi milioni 20 halafu anapunguziwa deni lake, hili haliwezi kuvumilika,” alisema Dk Mabula.Mbali na mchezo, Naibu Waziri wa Ardhi alisema, manispaa hiyo imekuwa pia ikiandaa hati nyingi kwa udanganyifu na kusisitiza kuwa timu maalumu ya uchunguzi lazima ipelekwe ili kubaini udanganyifu huo kwa kuwa Manispaa hiyo imetia aibu na kuondoa uaminifu kwa serikali.Sambamba na hilo, Dk Mabula alishangazwa na idara ya ardhi katika Manispaa hiyo kushindwa kufuatilia hati za madai ilizowapelekea wadaiwa sugu wa kodi ya pango la ardhi na kusubiri Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi Wilaya kuwakumbusha jambo alilolieleza kuwa ni kinyume na taratibu za utendaji kazi.Akigeukia suala la makusanyo ya kodi ya pango la ardhi tangu kuanza kwa operesheni maalumu ya kufuatilia wadaiwa sugu wa kodi hiyo, Dk Mabula alisema zoezi hilo limekuwa na mafanikio makubwa kwa kuwa Wizara imefanikiwa kukusanya Sh bilioni 20 ndani ya mwezi mmoja jambo ambalo halijawahi kutokea.Kwa mujibu wa Dk Mabula, Wizara ya Ardhi sasa inaanza utendaji wa kimatokeo badala ya kusubiri hadi mwisho wa mwaka ndiyo ianze ufuatiliaji wa wadaiwa kodi ya pango la ardhi na kubainisha kuwa lengo katika mwaka wa fedha 2019/2020 ni kukusanya Sh bilioni 180.Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo ameziagiza halmashauri za wilaya nchini kuainisha maeneo yote ya wazi kwa lengo la kubaini maeneo yaliyovamia na kutuma taarifa ya matokeo ya zoezi hilo Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi ifikapo Oktoba 1, mwaka huu.Naibu Waziri Mabula alisema, maeneo mengi ya wazi yamevamiwa kwa kuwa baadhi ya watendaji wa sekta ya ardhi wasio waaminifu wameuza ama kutoa vibali vya ujenzi katika maeneo hayo bila kufuata taratibu na hivyo kusababisha kukosekana maeneo ya wazi.“Tuwe na tabia ya kutunza maeneo ya wazi baadhi ya watendaji wameuza maeneo hivyo maeneo yote yapitiwe upya na yale yaliyovamiwa kwa kiasi kidogo taratibu za kuwaondoa zifanyike na Oktoba 1, mwaka huu taarifa kuhusiana na zoezi hilo ziwe zimefika wizarani.”Pia Dk Mabula amepiga marufuku ofisi za ardhi katika halmashauri kukodisha vifaa vya upimaji pale ambapo kuna vifaa vya Wizara na kusisitiza kuwa halmashauri hizo zinaweza kuazima vifaa pale tu ambapo kuna idadi kubwa ya wananchi wanaotaka kupimiwa huku vifaa vilivyopo vikiwa havitoshi.Vile vile, alizitaka halmashauri wakati wa kuchukua makampuni kwa ajili ya kupima maeneo kama vile urasimishaji kuzingatia zile kampuni zenye uwezo na kasi ya kufanya kazi hiyo badala ya kuchukua zile ambazo utendaji unategemea fedha kutoka kwa wapimiwa na kuzionya zile halmashauri ambazo hazijaomba kupima maeneo.Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi aliwataka washiriki wa mkutano huo kuhakikisha wanabadilika kwa kutatua kero za wananchi na kusisitiza kuwa migogoro ya ardhi katika maeneo yao lazima imalizwe haraka badala ya kusubiri viongozi wa kitaifa waende kuitatua.
kitaifa
Shirika la Afya Duniani (WHO), imeitaja Tanzania kuwa  miongoni mwa nchi 10 kinara kwa watu wake kuugua ugonjwa wa kipindupindu. Mataifa  mengine yaliyotajwa ni pamoja na India ambayo ndiyo inayoongoza. Nyingine ni Haiti, Jamhuri  ya  Kidemokrasi  ya  Congo, Tanzania, Bangladesh, Uganda,  Msumbiji na Kenya, ambayo ilikumbwa na mlipuko mkubwa wa maradhi hayo kwa nyakati tofauti mwaka huu. Katika ripoti yao iliyotolewa hivi majuzi, imesema kuwa sababu kuu ya kuandamwa na maradhi hayo ni kukithiri kwa mazingira machafu katika mataifa hayo. Ripoti hiyo inasema kuwa watu bilioni 1.2 sawa na moja ya sita ya watu wote duniani wako hatarini kukumbana na maradhi hayo hatari. Wakati Bara la Afrika likikumbwa na kadhia hiyo kutokana na unywaji wa maji yasiyofaa, hali ni tofauti kwa  Ulaya na Amerika ya Kaskazini ambako mifumo imara ya maji taka imeyafanya mabara hayo yawe huru na kipindipindu kwa miongo mingi sasa. Lakini watu zaidi ya bilioni mbili wamebakia bila maji safi na mifumo ya maji taka, hivyo, kipindupindu kinaendelea bila huruma kuathiri watu masikini zaidi duniani na ndani ya kila nchi athirika.
afya
Wao Yanga watawakaribisha Stand United kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, huku Azam itakuwa ugenini mjini Songea kucheza na Majimaji, Simba itakuwa jijini Mwanza kucheza na Toto Africans na Mtibwa Sugar itakuwa mgeni kwa Prisons kwenye uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.Aidha, Kagera Sugar itakuwa mwenyeji wa African Sports na Mwadui dhidi ya Ndanda FC. Ngoma itakuwa nzito kwa timu hizo ambazo zimekuwa zikipishana nafasi kutoka wiki moja kwenda nyingine.Wiki hii Yanga imekaa kileleni kwenye msimamo wa Ligi baada ya kushinda katika mchezo uliopita dhidi ya African Sports ya Tanga kwa bao 1-0 na kuwashusha Azam hadi nafasi ya pili, baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Simba wiki iliyopita.Michezo ya leo ni muhimu kwa kila timu kuhakikisha inashinda kujisogeza katika nafasi nzuri ya kuleta ushindani. Bado ligi ni ngumu kwa kuwa timu nyingi zimetofautiana kwa pointi ndogo kiasi kwamba iwapo moja itashindwa kuna nyingine itapanda.Vinara ambao ni Yanga tayari imecheza michezo 11 na ina pointi 27, iwapo itashinda itaendelea kuwa kileleni na ikiwa itatoka sare na Azam ikashinda, basi Yanga itashuka na kuipa nafasi Azam ambayo imecheza michezo 10 kuongoza.Yanga inakutana na Stand United ambayo pia ni nzuri na inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 19. Stand itakuwa na hasira ya kutaka kushinda kwa kuwa mchezo uliopita ilipoteza nyumbani dhidi ya Mwadui baada ya kula kichapo cha mabao 2-0.Msimu uliopita Yanga iliifunga Stand mabao 2-1 katika mchezo wa raundi ya kwanza na iliporudiana Uwanja wa Taifa ikafunga bao 1-0. Mechi hiyo haitakuwa rahisi kwa kuwa Stand United kwa sasa ina kikosi kizuri ambacho kimekuwa kikipambana kupata matokeo mazuri.Pia, kwa Azam inayokutana na Majimaji inahitaji ushindi ili kujihakikishia nafasi yake ya kulikaribia taji la ubingwa wa ligi. Majimaji imetoka kufungwa mabao 5-1 kwenye uwanja wao. Hiyo ni kutokana na mgawanyiko wa wachezaji uliopo hivi sasa, wakigoma kucheza kwa kudai fedha zao za usajili.Iwapo kutaendelea kuwa na mgawanyiko uliowagharimu wiki iliyopita, itakuwa na faida kwa Azam ambayo kwa hali na mali kushinda kujiongezea pointi. Azam imekuwa ikijitahidi kufanya vizuri katika michezo ya ugenini na nyumbani na kufanikiwa.Kwa upande wa Simba inashika nafasi ya nne ikiwa na pointi 22 nyuma ya Mtibwa inayoshika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 23, zikitofautiana kwa pointi moja. Mechi ya Simba na Toto haitakuwa rahisi, kwani timu hiyo ya Mwanza imekuwa ikipambana kwa hali na mali kushinda katika uwanja wao wa nyumbani.Iwapo kuna ambayo itashinda na nyingine kushindwa, zitapishana kwa moja kupanda na nyingine kushuka. Simba inategemea kuwachezesha wachezaji wake iliyowasajili wakati wa dirisha dogo la usajili, Brian Majwega na Paul Kiongera baada ya kuruhusiwa kucheza na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).Kagera Sugar inayoshika nafasi ya 15 ikiwa na pointi sita, Ndanda inayoshika nafasi ya 12 kwa pointi tisa zinahitaji ushindi kujinasua katika hatari ya kushuka daraja.
michezo
GENK, UBELGIJI NAHODHA wa timu ya K.R.C Genk ya nchini Ubelgiji, Mbwana Samatta ambaye pia ni nahodha wa timu ya Taifa Tanzanian ‘Taifa Stars’ amedai hana bahati na mfumo wa VAR. K.R.C Genk wiki moja iliopita ilishuka dimbani kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya wapinzani wao Liverpool kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huku K.R.C Genk ikikubali kichapo cha mabao 4-1. Samatta alifanikiwa kupachikanbao, lakini lilikataliwa na mfumo wa VAR huku ikidaiwa Junya Ito ambaye alipiga pasi ya mwisho alikuwa kwenye eneo la kuotea. Samatta amedai anajiona mtu ambaye hana bahati na mfumo wa VAR ikiwa hadi sasa jumla ya mabao yake matatu yamekataliwa kwenye michezo mbalimbali. “Hilo lilikuwa bao langu la tatu ambalo limekataliwa na mfumo wa VAR msimu huu, ukweli ni kwamba nilikuwa na furaha kubwa kufunga bao dhidi ya moja kati ya timu kubwa duniani, lakini mwisho wa siku halikukubaliwa. “Wakati mchezo umesimama kupisha VAR ifanye maamuzi nilikuwa nafanya maombi ili likubaliwe kwa kuwa niliamini ni jambo la kihistoria katika maisha yangu yote ya soka. “Lakini ukweli ni kwamba nitaendelea kulikumbuka bao hilo, hata kama halikukubaliwa nitaendelea kuliweka kwenye kichwa changu kwa kuwa nilifunga dhidi ya Liverpool na likakataliwa.” Alisema Samatta. Samatta aliongeza kwa kusema, mchezo wa marudiano dhidi ya Liverpool kwenye uwanja wa Anfi eld utakuwa mgumu, huku klabu yake hadi sasa ikiwa haijafanikiwa kupata ushindi katika hatua hiyo ya makundi. “Niwe mkweli, mchezo kwenye uwanja wa Anfi eld utakuwa mgumu sana kwa kuwa wao hawatokuwa tayari kuupoteza mchezo huo kwenye uwanja wa nyumbani dhidi ya idadi kubwa ya mashabiki huku sisi tukipambana kutafuta ushindi wetu wa kwanza,” aliongeza mchezaji huyo.
michezo
KAMPUNI ya uchimbaji madini ya Acacia imesaini makubaliano ya kusambaza vifaa vya ujenzi kwenye shule za msingi na sekondari nchini vyenye thamani ya Dola za Marekani 300,000 sawa na Sh milioni 700, ikiwa ni sehemu ya mchango wao katika jamii inayowazunguka.Kwa mujibu wa taarifa yao ya fedha ya kipindi cha robo mwaka wa 2019 iliyotolewa hivi karibuni, kampuni hiyo itasambaza vifaa hivyo vya ujenzi kwenye maeneo yaliyopo kwenye migodi yao mkoani Shinyanga ambayo ni Bulyanhulu na Buzwagi.Pamoja na kusambaza vifaa hivyo vya ujenzi, kampuni hiyo pia katika kipindi cha robo mwaka wa fedha wa 2019, imejizatiti kusaidia miradi ya kijamii ya maji kwa wakulima, lengo likiwa kuinua uchumi wa wananchi wanaozunguka migodi hiyo. Katika kutekeleza hilo, kwenye mgodi wa Buzwagi, wananchi wa eneo hilo watafaidika na mradi wa pamoja wa kilimo cha shairi, mpunga kwa kuwafundisha wananchi kupitia mashamba darasa ya mfano ambapo zaidi ya Dola za Marekani Milioni 1.1 zimetengwa kusaidia kuimarisha mradi huo.Pia, katika kurudisha fadhila kwa jamii mradi wa ujenzi wa bomba la maji la urefu wa kilometa 55 karibu na mgodi wa Bulyanhulu, unatoa maji Ziwa Victoria unaendelea na ukikamilika utawanufaisha wakazi zaidi ya 100,000. Ripoti hiyo imezungumzia pia uzalishaji wa dhahabu kwenye migodi yake nchini kwa kipindi cha robo mwaka na kusema kiasi wa wakia za dhahabu 104,899 kimezalishwa.Ofisa Mtendaji Mkuu wa Acacia, Peter Geleta alisema uzalishaji huo ni wa chini kwa asilimia 13 ya uzalishaji wa mwaka 2018 na kwamba umechangiwa na sababu mbalimbali. Alisema uzalishaji wa dhahabu kwenye mgodi wa North Mara umeendelea kuzalisha kiwango kidogo kuliko kilichotarajiwa. Haya hivyo, alisema pamoja na uzalishaji huo kuwa mdogo kwenye baadhi ya migodi yake bado wanatarajia kuzalisha wakia kati ya 500,000 hadi 550,000 kwa mwaka.
kitaifa
MAMLAKA ya Usimamizi wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA) imefafanua kuhusu vikokotoo vya pensheni ikisema vimeanza kutumika tangu 2014, kuwa kuunganishwa kwa mifuko ya hifadhi ya jamii hakujapunguza vikokotoo hivyo.Imesema kilichobadilika ni kiwango cha mkupuo kwa kundi dogo la wanachama takribani asilimia 20 ya wanachama wote wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50, kwamba sasa ili wawe sawa na wanachama wenzao wa mifuko mingine wanaopokea asilimia 25.Aidha, imesema si wakati mwafaka kuilaumu serikali hasa inaposimamia misingi ya hifadhi ya jamii.Ufafanuzi huo umetolewa na Mkurugenzi Mkuu wa SSRA, Irene Isaka jana, baada ya kuwapo kwa taarifa mbali mbali kuhusu kupungua kwa vikokotoo vya pensheni baada ya kuunganishwa mifuko.Agosti mosi, mwaka huu, Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF), ulianza rasmi ukiwa ni utekelezaji wa Sheria Namba 2 ya 2018, ambayo pamoja na mambo mengine, iliunganisha mifuko ya pensheni minne ya PSPF, LAPF, PPF na GEPF na kuunda mfuko mmoja kwa ajili ya watumishi wa umma yaani PSSSF.Sambamba na kuanzishwa kwa PSSSF, sheria hii ilifanya marekebisho kwenye Sheria ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Sura ya 50 ili kuufanya mfuko wa NSSF kuwa utakaohudumia wafanyakazi wa sekta binafsi na sekta isiyo rasmi.Isaka alieleza jana kuwa hivi karibuni kumetokea upotoshaji kwa wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba kwa kuunganisha mifuko, serikali imepunguza vikokotoo vya pensheni.Alisema jambo hilo si kweli, kwani vikokotoo vinavyotumika vilianza kutumika tangu Julai Mosi, 2014; na tayari wastaafu wa mifuko ya pensheni ya NSSF na PPF ambao ni wengi walishakuwa wakipokea pensheni kwa kikokotoo hiki.“Mwaka 2014 ilikubalika kwamba wanachama wa PSPF na LAPF ambao walikuwa kwenye mifuko hiyo kabla ya Julai Mosi, 2014 waendelee na kikokotoo cha 1/540: 15.5 na mkupuo wa asilimia 50. “Hivyo ukisoma kwa makini Sheria Namba 2 ya Mwaka 2018 iliyounda mfuko wa PSSSF Kanuni za Mafao: Public Service Social Security (Benefits Regulations) zilizotolewa imezingatia kwa kina jambo hilo.Nafikiri si wakati muafaka kuilaumu serikali,” alieleza bosi huyo wa SSRA. Aliwaondoa hofu wanachama wa mifuko ya hifadhi ya jamii kwamba kikokotoo hicho sio kipya kwani kimetumika kwa muda wa miaka minne tangu 2014.Aliwashauri kutembelea tovuti ya SSRA walinganishe Amri ya 2014 na Kanuni za 2018. “Kilichobadilika ni kiwango cha mkupuo kwa kundi hili dogo la wanachama takriban asilimia 20 ya wanachama wote wa sekta ya hifadhi ya jamii nchini waliokuwa wakipokea mkupuo wa asilimia 50 kwamba sasa ili wawe sawa na wanachama wenzao wa mifuko mingine wanaopokea asilimia 25,” alisema Isaka.Alieleza kuwa haikuwa sahihi kundi dogo la wanachama kulipwa mkupuo mkubwa. “Taarifa halisi za malipo zinaonesha kwamba mwanachama wa PSPF/ LAPF anapokea mkupuo ambao ni zaidi ya mara tatu ya michango aliyochanga kwa kipindi chote cha ajira yake tofauti na wanachama wenzake waliopo mifuko mingine kama vile NSSF na PPF.“Tungependa kusisitiza kwamba hii asilimia 25 iliyopunguzwa kwenye mkupuo imewekwa kwenye pensheni ya mwezi ambapo pensheni ya mwezi imeongezeka kwa asilimia 50. Kwa hiyo si sahihi kusema wanachama wamepunjwa mafao yao,” alifafanua zaidi Isaka.Alisema lengo la kuinganisha mifuko ni pamoja na kuweka usawa kwa wanachama kwa kuwa wote wanachangia asilimia 20.“Tena kwa watumishi wa umma, serikali ambaye ni mwajiri anawachangia asilimia 15, mtumishi anachangia asiliami tano. “Je, ni sawa mwanachama wa NSSF anayechangia asilimia 10 apate mkupuo asilimia 25 wakati mwenzake wa PSPF anayechangia asilimia tano apate asilimia 50, kwa nchi inayofuata misingi ya Hifadhi ya Jamii (Solidarity Principle),” alihoji. Aidha, Isaka alisema malalamiko ambayo SSRA imepokea na kuanza kuyafanyia kazi ni kwamba wanachama wa PSPF walikopa mikopo ya nyumba kwa kutegemea watalipwa mkupuo wa asilimia 50.“Hivyo kwa kuwa sasa wanapokea asilimia 25 wanaona kwamba mkupuo hautoshi kulipa deni la nyumba. Hili si jambo gumu kwani kunaweza kufanyika makubaliano na mfuko kuona namna ya kuondokana na changamoto hiyo,” alieleza.Alisisitiza kwa kuwahakikishia wanachama kwamba pensheni hailipwi kwa miaka 12.5 tu, bali kwa muda wote wa uhai wa wastaafu. Pia kwa wastaafu wa PSPF na LAPF bado wanapokea kikokotoo cha 15.5 na si kikokotoo cha 12.5 kama inavyopotoshwa.Ili kuhakikisha wastaafu hawapunjwi na mfuko mpya wa PSSSF, alisema SSRA imetuma wakaguzi maalumu kujiridhisha kwamba ukokotoaji umefanyika kwa mujibu wa kanuni na taratibu. Hivi karibuni, baada ya kutolewa kwa taarifa kuhusu kuanza kwa mfuko wa PSSSF, baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa walikuja juu na kudai kuna mabadiliko ya vikokotoo yenye nia ya kuwapunja mafao wastaafu wa mifuko ya hifadhi ya jamii.Mbunge wa Bunda Mjini, Ester Bulaya akizungumza na waandishi wa habari wiki iliyopita jijini Dar es Salaam, alidai sheria hiyo mpya inamuumiza mtumishi mwenye kipato cha chini katika mafao yake pindi anapostaafu.Wadau wataka elimu zaidi itolewe Katika hatua nyingine, wadau mbalimbali wamesema elimu kwa umma inahitajika zaidi kwani inaonekana wadau hawajaelewa namna ambavyo ukokotoaji unafanyika na nini manufaa kwa wastaafu. Ofisa Mwandamizi wa Serikali mstaafu, Isaac Mruma alisema elimu ya kutosha haijatolewa kwa wadau wa sheria hiyo pamoja na kanuni zake, jambo ambalo linawafanya watu kupotosha.“Nadhani elimu haijatolewa ya kutosha kwa wadau ndio maana tunaona watu wanatoa maoni mbalimbali yasiyo na ukweli lakini mimi mpaka sasa sijaona athari yoyote kwa mstaafu, hiyo miaka 12.5 haijatajwa kokote kwenye sheria, bali imetajwa kwenye kanuni ya kukokotoa,” alisema Mruma. Naye Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhokya alisema tatizo linalojitokeza sasa ni elimu ndogo kwa umma juu ya ukokotoaji wa mafao ambapo ameshauri kuendesha kampeni kubwa ya kutoa elimu.Alisema hata hivyo TUCTA inaendelea kufanya majadiliano na serikali kuona namna bora ya kuboresha mafao ya mstaafu lakini pia kuhakikisha mifuko ya hifadhi za jamii haifi. Makamu Mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT), Profesa Tolly Mbwete aliishauri serikali kuongeza fao la kuanzia, yaani isiwe mstaafu anapata asilimia 25 mwanzo na asilimia 75 aipate kwa miaka 12.5 badala yake fedha ya mwanzo apewe angalau asilimia 40.Alisema pia kuwa malalamiko juu ya ukokotoaji huo umekuja kwa sababu watumishi wengi walikuwa wakikopa asilimia 25 ya mafao yao lakini kwa ukokotoaji wa sasa watakapokwenda kuchukua mafao watajikuta hawana kitu kwani walishazichukua kama mkopo.“Mtu mwenye mipango hata kidogo fedha hiyo ya mwanzo yaani asilimia 25 haitamfaa atashindwa kujipanga na kuanzisha miradi ya kumsaidia kuishi, kabla mradi haujakaa vizuri fedha imeshaisha kwa hiyo kwa ushauri wangu ingeongezwa angalau ya mwanzo iwe asilimia 40,” alisema Profesa Mbwete. Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk Benson Bana alisema sheria na kanuni zake zimetungwa na serikali na serikali ya awamu ya tano ni sikivu itapokea maoni ya watu na kufanya mabadiliko yanayofaa.Imeandikwa na Mgaya Kingoba na Regina Mpogolo.
kitaifa
HUDUMA ya App (EPaper) inayowezesha magazeti ya serikali kupatikana na kusomwa kupitia mtandao wa simu za mkononi, imezinduliwa rasmi na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.Waziri Majaliwa alizindua huduma hiyo juzi wakati akifungua Jukwaa la Biashara Tabora lililoandaliwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayochapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo kwa kushirikiana na Mkoa wa Tabora.Alisema TSN imekuwa ikifanya kazi kubwa ya kuhabarisha na kuelimisha jamii kupitia vyombo vyake, lakini sasa inakuja na mbinu mpya inayoendana na teknolojia ya huduma ya magazeti hayo kupitia mtandao.Alibainisha kuwa serikali imekuwa ikifarijika na utendaji wa kampuni hiyo hususani ubunifu wake wa kuanzisha majukwaa katika kila mkoa na kutoa taarifa za mikoa hiyo kwenye majukwaa na vyombo vyake, hivyo kutangaza fursa zilizopo nchini. “TSN inatekeleza wajibu wake kwa ufasaha na umahiri mkubwa kuhabarisha wananchi kupitia magazeti na majukwaa haya.Sasa leo wamekuja na mbinu mpya ya kuhabarisha wananchi kwa kutumia mbinu mpya E Paper, yote ni kuhakikisha serikali inafikisha ujumbe kwa Watanzania,” alieleza. Kwa upande wake, Kaimu Mhariri Mtendaji wa TSN, Tuma Abdallah akielezea huduma hiyo alisema inapatikana kupitia tovuti zote za TSN pamoja na App ya TSN inayopatikana kwenye simu za mkononi (Mobile TSN App).Alisema ili mtu aweze kuipata huduma hiyo, ni lazima aingize App hiyo kwenye simu yake na kisha kufuata maelekezo, ikiwa ni pamoja na kulipia huduma hiyo kwa muda anaotaka kupata huduma kuanzia siku, mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita hadi mwaka.Katika huduma hiyo, utapata magazeti yote yanayochapishwa na kampuni hiyo ya TSN ambayo ni Daily News, SpotiLeo na HabariLeo. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe, alimuelezea Waziri Mkuu Majaliwa kuhusu huduma hiyo mpya ya TSN na namna itakavyosaidia kufikisha magazeti hayo si ndani tu ya nchi bali hata nje ya nchi.
kitaifa
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM BUNDI ni kama ameanza kuing’ang’ania klabu ya soka ya Simba, baada ya uongozi kutangaza kumsimamisha kwa muda usiojulikana nahodha msaidizi wa timu hiyo, Hassan Isihaka, kwa madai ya kuonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu. Mbali na sakata la kufungiwa kwa beki huyo wa kati, uongozi unapigana chini kwa chini kuhakikisa unanasa saini ya mlinzi wake wa kulia, Hassan Ramadhani ‘Kessy’, ambaye mkataba wake umemalizika na amekuwa akiwazungusha kwa kutaka kulipwa dau kubwa. Kamati ya Utendaji ya klabu ya Simba jana ilitangaza uamuzi wa kumsimamisha Isihaka kutokana na kumtolea maneno yasiyo na staha kocha wa timu hiyo Mganda, Jackson Mayanja, kabla ya mchezo wa Kombe la FA dhidi ya Singida United, uliochezwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana, imeeleza kuwa kitendo hicho si cha kiungwana na kilifanywa mbele ya wachezaji wengine na kukiuka waraka wa maadili, ambapo licha ya kusimamishwa, kamati imeagiza beki huyo alipwe nusu mshahara kwa kipindi atakachokuwa anatumikia adhabu yake. Aidha, kamati hiyo imewataka wachezaji wengine kuzingatia nidhamu na weledi katika kipindi chote watakapoitumikia Simba. Inadaiwa kuwa Isihaka alitofautiana na Mayanja kutokana na kuwekwa benchi muda mrefu, lakini baadaye kocha alimweleza kuwa anataka apumzike kutokana na kucheza mechi nyingi. Jambo la kushangaza ni kwamba beki huyo alipangwa kucheza dhidi ya Singida United juzi, kitendo ambacho hakutarajia na kumfanya aropoke kwa kutaka kujua kama muda aliotakiwa kupumzika umekwisha. Kwa upande wa Kessy, inadaiwa kwamba amekuwa akizungushana uongozi wa Simba juu ya maslahi anayotaka, huku akisusa kujiunga na wenzake mazoezini, ikiwa ni pamoja na kambi ya Morogoro ambayo timu iliondoka jana. Chanzo cha habari za uhakika ambazo zimelifikia MTANZANIA, kinaeleza kuwa awali Kessy alitaka alipwe dau la Sh milioni 30 kwa pamoja, lakini baada ya muda mfupi alibadili mawazo na kutaka kulipwa kiasi cha Sh milioni 60, jambo ambalo limewachanganya viongozi. Hata hivyo, kikosi cha Simba kiliondoka jana kuelekea mkoani Morogoro ambako kitaweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mbeya City, utakaofanyika Jumapili hii katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Simba iliondoka kwenda Morogoro ikiwa ni siku moja baada ya kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la FA, baada ya kuichapa Singida United mabao 5-1 katika mchezo uliopigwa juzi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kabla ya kuondoka, Mayanja aliliambia MTANZANIA kuwa kambi hiyo ni maalumu kwa ajili ya kujiimarisha zaidi kabla kukutana na Mbeya City, ambapo amepanga kuifanyia kazi kubwa safu ya ushambuliaji. “Nitatumia muda mfupi uliobaki kuzisoma vizuri mbinu za wapinzani wetu ili tuweze kupanga mikakati kabambe ya kukabiliana nao, kwani hii itakuwa ni mara yangu ya kwanza kucheza nao tangu nianze kibarua cha kuinoa Simba,” alisema. Habari za uhakika mbazo zimelifikia gazeti hili, zinadai kuwa Simba wameamua kuweka kambi Morogoro ili kuwakwepa mashabiki ambao bado wana hasira na baadhi ya wachezaji kutokana na kipigo walichopata cha mabao 2-0 dhidi ya watani wao wa jadi, Yanga. Chanzo hicho kimeeleza kuwa Simba wanaogopa kelele za mashabiki zinaweza kuwaathiri kisaikolojia wachezaji wakati wakijiandaa na mchezo wao dhidi ya Mbeya City. Chanzo hicho kilieleza kuwa, Simba hawajawahi kuweka kambi mkoani humo kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu isipokuwa ile ya Yanga.
michezo
Wenye mnauliza anaficha mimba Kuna mimba zenu zimepotea 🤷🏾‍♀️ Hiyo ni moja ya comment iliyoniacha sina mbavu aisee imeandikwa na davine.ke akimanisha wale wanaomwambia Tanasha Juu ya kuficha mimba kwani kuna mimba imepotea !! Comment hiyo imekuja baada ya wau wengi kucoment kwenye picha ya Tanasha ambaye ni mpenzi wa Diamond Platnumz  wakitaka asifiche ujauzito. Katika siku za hivi karibuni kumekuwepo na gumzo kubwa mitandaoni kuwa mlimbwende huyo ana ujauzito, hii ilitokana na picha ambayo alipost kwenye insta story  akidai kuongeza uzito na imekuja kukolezwa hivi majuzi waliporekodi a video na mpenzi wake Diamond Platnumz wakicheza wimbo mpya wa ‘Inama ‘na katika video hiyo wanazengo wakapata conclusion kuwa ni mjamzito. https://www.instagram.com/p/Byff8GBARld/ Siku ya jana mrembo huyo ambaye ni mtangazaji kwenye kituo cha Nrg kenya alipost a pic akiwa amevalia a black clothes flani hivi iliyomtoa vyema huku akiwa amekaa sehemu inayonyesha kama ilikua saluni huku akiweka mtandio-like akiiupitisha karibu na tumbo lake kama kuficha kitu hivi. Baadhi ya wafuasi wake katika mtandao huo wa instagram wakashindwa kujizuia huku wakiamini Tanasha analificha tumbo lake asionekane mjamzito. Ndo wakaanza kutupia vitu Can you just let us know…una Mumbai or not, tutakufa udaku😂😂😂 thomas_nyarutu Sasa mm huwa nawashangaa mnavyojifichaficha wakati mwisho wa siku utazaa tu..badala ya kufurahia unajificha wakati kuna wengine hiyo bahat wanaitafuta miaka na miaka… Tumbo linatokeza tu @tanashadonna There’s no need to cover tumbo lako every time cause y’all know already what’s going on…😅😃😀😀 https://www.instagram.com/p/ByneaxjgAdc/        
burudani
JESHI la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limesema, hadi mchana huu, mfanyabiashara Mohammed Dewji Mo bado hajapatikana na juhudi za kumtafuta zinaendelea.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema, tukio hilo ni la aina yake, limefanywa na raia wa kigeni na kwamba, polisi wanaendelea na oparesheni kali ya kimya kimya katika mikoa mitatu.Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa polisi, Mo Dewji atapatikana mapema iwezekanavyo na ana kila sababu ya kuamini hivyo."Zipo taarifa mtaani kwamba ameshapatikana, wengine wanadai kwamba amepatikana kule Coco Beach, lakini taarifa kutoka meza yangu hii, na taarifa ambazo sasa ni taarifa rasmi bado hajapatikana na wahusika bado hawajakamatwa" amesema Kamanda Mambosasa.Amewaeleza waandishi wa habari kuwa, Polisi wanafanya jitihada ili tukio hilo lisichafue taswira nzuri ya Tanzania inayotambulika kuwa ni kisiwa cha amani."Tunaendelea na opereshein kali kufuatia taarifa hiyo lakini bado Mo hajapatikana" amesema Mambosasa ofisini kwake.Watu wenye silaha wamemteka Mo Dewji leo saa 11 alfajiri wakati akiingia kufanya mazoezi katika gym ya Colosseum, Oysterbay jijini Dar es Salaam.Kwa mujibu wa Kamanda Mambosasa waliomteka mfanyabiashara Mohamed Dewji (Mo) ni wazungu wawili.Leo asubuhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda alikwenda eneo la tukio na akasema, anaamini Dewji atapatikana akiwa salama.
kitaifa
 DERICK MILTON – TARIME WAJANE sita katika Kijiji cha Sombanyasoko, Kata ya Komaswa, Wilaya ya Tarime mkoani Mara, wamemwomba Rais Dk. John Magufuli awasaidie ili waweze kurudishiwa mashamba yao zaidi ya ekari 80 ambazo wamedai wamenyang’anywa na mmoja wa wanakijiji. Walidai kuwa wamenyang’anywa maeneo yao ambayo waliachiwa na waume zao kabla ya kufariki, na wamehangaika kutafuta haki hadi mahakamani, lakini wameshindwa kwa kile walichodai uwepo wa vitendo vya rushwa katika kesi yao. Mbali na wajane hao, katika mgogoro huo wa ardhi ambao umedumu kwa muda wa miaka saba, zipo familia nyingine nne kwenye ekari hizo 80 ambazo nazo zimemwomba Rais Magufuli kuwasaidia wapate haki yao. Mmoja wa wajane hao, Mang’era Nyaswi alisema kuwa wamenyang’anywa mashamba yao baada ya kuingizwa katika mgogoro wa ardhi ekari sita za watu watatu ambao walikuwa wanashtakiana katika baraza la ardhi la kata. Mang’era aliwataka wananchi hao kuwa ni Daniel Chacha na Meng’anya Magoti waliokuwa wanashtakiwa na Mseti Gachuma kwa madai ya kumiliki ardhi ekari sita ambayo siyo mali yao. Alisema kuwa katika kesi hiyo Gachuma alishindwa baada ya hukumu ya baraza hilo kutoa haki kwa washtakiwa, na baaada ya hukumu hiyo alikata rufaa Baraza la Ardhi Wilaya Tarime. “Baada ya Mseti kukata rufaa kesi iliendelea na mwaka 2015 hakimu wa mahakama hiyo aliyejulikana kwa jina la Mayeye. S. M alitoa ushindi kwa Mseti na wale walioshinda Baraza la Kata wakashindwa,” alisema Mang’era. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji, Chacha Fanusi alikiri kuwepo kwa mgogoro huo, huku akishangaa kuona maeneo ya wajane hao yakichukuliwa wakati hawakuwamo katika kesi. Ofisa Ardhi wa Halmashuari ya Wilaya hiyo, Privatus Mafuru alikiri kuwepo kwa mgogoro huo na tayari ofisi yake imetoa maelekezo kwa walalamikaji wafike ofisini wakiwa na vielelezo vyote ili wasaidiwe.
kitaifa
OUAGADOUGOU, BURKINA FASO KANSELA wa  Ujerumani, Angela  Merkel  ameonya  kuhusu  hatari ya kuongezeka ugaidi katika  eneo  la Afrika  Magharibi na kuyataka  mataifa  ya  Ulaya  kuchukua  hatua dhidi  ya hali hiyo. Kansela  Merkel  ameyasema  hayo  katika  siku  yake  ya  kwanza ya  ziara  ya  siku  tatu  katika  eneo hilo la Sahel, ambapo juzi aliwasili hapa akitarajia kuzitembelea Mali na Niger. Mapambano dhidi ya ugaidi  ni suala  la  kimataifa, alisema baada ya kukutana na viongozi wa mataifa  ya Burkina Faso, Mali, Mauritania, Niger na Chad marufu kama G5. Alisema tatizo lingine ni kuwa Marekani  inajaribu  kuzuia  kupatikana mamlaka ya vikosi  vya  mataifa  ya  Sahel  katika  Baraza  la Usalama  la  Umoja  wa  Mataifa. Aliahidi kuwa Ujerumani itazipatia  nchi  hizo kiasi  ya  euro  milioni  60  kwa  ajili  ya  jeshi  la pamoja kukabiliana na ugaidi Aidha Rais  wa Burkina  Faso,  Roch Marc Kabore, ametaka  kuchukuliwe  hatua  za kutatua  suala  la  mzozo  wa  Libya. Alisema vita  vya wenyewe  kwa  wenyewe  katika  nchi  hiyo  vinaathiri  eneo  lote  la Afrika  Magharibi. Tatizo  hilo  ni  lazima  lipatiwe suluhisho, amesema  na  kuongeza  kwamba  bila  hivyo haitawezekana  kupiga hatua.
kimataifa
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Hassan Simba Yahya, ambaye amemtaka akaimarishe uhusiano baina ya nchi zote mbili. Amekutana na Balozi Yahya jana katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu pamoja na mambo mengine amemtaka balozi huyo kuhakikisha anaboresha shughuli za kidiplomasia kati ya Tanzania na Zambia.Pia, Waziri Mkuu amemtaka akakutane na wafanyabiashara wa Zambia na awahamasishe waje wawekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya viwanda. Alisema balozi huyo anaweza kuandaa kongamano la biashara na uwekezaji kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Zambia ili kuboresha uchumi. Kwa upande wake, Balozi Yahya alisema atahakikisha anayafanyia kazi maelekezo yote aliyopewa ikiwa ni pamoja na kuimarisha biashara pamoja na kuboresha ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amewakaribisha wawekezaji kutoka nchini Italia waje wawekeze nchini na serikali itawapa ushirikiano wa kutosha.Aliyasema hayo jana alipokutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Italia nchini, Roberto Mengoni. Akizungumza na balozi huyo ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni, Dar es Salaam, Waziri Mkuu alisema Tanzania ipo tayari kuwapokea wawekezaji kutoka kwenye nchi hiyo. Naye Balozi Mengoni aliishukuru serikali kwa ushirikiano mzuri uliopo baina ya Tanzania na Italia, hivyo alimhakikishia Waziri Mkuu kwamba watauendeleza, na wapo tayari kushirikiana na Tanzania kuhakikisha mkakati wa serikali wa kukuza uchumi kupitia sekta ya viwanda unafanikiwa.
kitaifa
Appiah aliyasema hayo jana baada ya timu yake kumaliza mazoezi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam na kusema hatua ambayo wamemaliza ilikuwa ngumu.“Nashukuru ushindi niliopata kwani kuifunga APR si kwamba tulibahatisha bali ni mipango ambayo tulikuwa tumeiandaa tangu tunakuja kwenye mashindano haya kuwa ni kuchukua ubingwa na hapa tulipofikia fainali tutahakikisha tunatwaa ubingwa,” alisema Appiah Khartoum National Club imetinga hatua ya nusu fainali baada ya kuifunga APR ya Rwanda mabao 4-0 hivyo itacheza na Gor Mahia ambayo iliifunga Malakia ya Sudan Kusini mabao 2-1.Appiah ambaye amewahi kufundisha timu ya Taifa ya Ghana kwenye michuano ya Kombe la Dunia iliyofanyika nchini Brazil mwaka 2014, lakini timu hiyo ilitupwa nje ya michuano hiyo kwenye hatua ya makundi akisifia utulivu wa wachezaji wake.Appiah alizidi kusema mashindano haya yanajenga uzoefu kwa wachezaji kwenye mechi za kimataifa kwani yanakutanisha timu kutoka nchi mbalimbali za Afrika Mashariki na Kati, uzoefu utakaosaidia kwenye mashindano mengine makubwa kama klabu bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho.Naye kocha wa Gor Mahia kutoka nchini Kenya, Frank Nuttal amesema anaheshimu kila mpinzani anayekutana naye kwenye mashindano kwa sababu kila timu iliyoshiriki ina sifa za kuwepo japo kufungwa na kushinda ni matokeo ya soka.Nuttal alisema timu yake imekuja kushindana ili irudi na kombe hivyo akijiamini kuwa ana uwezo wa kushinda kila mchezo itawafanya wachezaji wajisahau, kitu ambacho hataki kitokee.“Nawashukuru wachezaji na viongozi kwa ushirikiano wao kwani ndio umetufikisha hadi tunacheza nusu fainali, Khartoum ni timu nzuri hivyo tumejipanga kuhakikisha tunashinda”, alisema Nuttal.
michezo
  NA KULWA MZEE DAR ES SALAAM MBUNGE wa Singida Mashariki, Tundu Lissu amekatazwa kuuliza swali kuhusu uhalali wa Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, Jecha Salum Jecha kama alikuwa halali kufuta Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar. Uamuzi wa kumkataza Lissu umetolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akitoa uamuzi kuhusu mabishano yaliyojitokeza yakimtaka shahidi kueleza uhalali wa mwenyekiti huyo kufuta uchaguzi. Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alitakiwa kujibu swali hilo katika kesi ya uchochezi, inayomkabili Lissu na wahariri wa Gazeti la Mawio. Lissu alipotakiwa kuzungumza kama ana cha kuzungumza, alisema amekubaliana na uamuzi wa mahakama kwa maana haruhusiwi kuuliza kama Jecha Salum Jecha alikuwa na mamlaka ya kufuta matokeo ya uchaguzi Zanzibar. Kesi hiyo ya uchochezi inamkabili Lissu, mhariri wa gazeti la MAWIO, Simon Mkina, mwandishi wa habari Jabir Idrisa na Mchapishaji wa Kampuni ya Jamana, Ismail Mehboob.Hakimu Simba ameahirisha kesi hiyo hadi Machi 8 na 9, mwaka huu,  kwa usikilizwaji.
kitaifa
POLISI katika Kanda Maalumu ya Tarime/Rorya imekamata gari likiwa na katoni 15 zenye simu 897 aina ya iTel ambazo zinadaiwa zimeingizwa nchini kupitia njia za panya kutoka nchini Kenya.Gari hilo aina ya Probox lenye namba za usajili T 228 DGD, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Ngwena, likiwa ni mali ya John Makumba anayeishi Sirari.Dereva wake aliposimamishwa na gari la askari wa doria alikaidi kusimama na kuendesha kwa kasi kwenda Kijiji cha Nkende wakifukuzana na gari la Polisi na kuharibu mazao ya watu na kutoroka. Anasakwa na Polisi.Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe alisema gari hilo liligunduliwa juzi jioni katika Kijiji cha Nkende, wakati askari wa doria walipopata taarifa ya kuwepo gari lenye bidhaa za magendo kutoka nchini Kenya na walipojaribu kulisimamisha dereva wake alikaidi kusimama.“Askari wetu walijaribu kulifuata nyuma gari hilo liliongeza mwendo kwa kasi na kutaka kugonga magari mengine kwa kukimbia na kisha kuingia barabara ya Shule ya Msingi Nkende na kuvamia mashamba ya watu na kuharibu mazao yakiwemo mahindi. Liligonga na kupasuka tairi ya mbele na kukwama kisha dereva wake kutoroka na kuingia porini na kuacha gari hilo na kukamatwa likiwa na simu hizo,” alsema Kamanda Mwaibambe.Alisema wamejipanga kupambana na vitendo vya uhalifu vikiwemo kudhibiti biashara za magendo kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika kufanya doria katika vijiji vya mipakani vikiwemo Kogaja, Ikoma, Shirati, Kubiterere, Sirari, Gosebe Kipimo, Borega na Kegonga.“Dereva wa gari hili kwa jina Ngwena tunamsaka kwani ni mtuhumiwa wa mara kwa mara kuhusika na biashara ya magendo ikiwemo ya dawa za kulevya na kisha kuwatoroka Polisi na mmiliki wa gari hili, John Waswa Makumba ambaye inadaiwa ni ‘clearing agent’ (wakala wa huduma za forodha) huko Sirari anatakiwa kujisalimisha mara moja kituo cha Polisi mwenyewe kabla hajakamatwa,” alieleza Kamanda.Alisema simu hizo zitakabidhiwa kwa TRA Kituo cha Sirari ili watoe thamani ya simu hizo na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), nao wazikague kama zina ubora wa matumizi.Katika hatua nyingine, Kamanda Mwaibambe alisema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu, wakiwa doria usiku na mchana wamekamata pikipiki 28 zikiwa na magunia ya bangi na mirungi, huku baadhi ya watuhumiwa wakitoroka na wengine wamefikishwa mahakamani.
kitaifa
NA WAANDISHI WETU-BEIRA NA KIGALI TIMU za Simba na KMC zimechanga vema karata zao, baada ya jana kulazimisha suluhu ugenini, katika michezo yao ya Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho iliyochezwa jana. Simba ilivuna suluhu hiyo dhidi ya wenyeji UD Songo, katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali wa Ligi ya Mabingwa uliochezwa Uwanja wa Estadio da HCB jijini Beira, Msumbuji. Kwa upande wa KMC iliibana timu ya AS Kigali,katika mchezo wa kwanza wa hatua ya awali wa Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa Uwanja wa Amahoro jijini Kigali, Rwanda. Matokeo hayo ni faida kwa wawakilishi hao wa Tanzania, kuelekea michezo yao ya  marudiano itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, kati ya Agosti 23 na 25, mwaka huu. Simba, UD Songo zilivyocheza Simba itahitaji ushindi ili kutinga raundi ya kwanza ya michuano hiyo, ambapo kama itafanikiwa itacheza na mshindi wa jumla kati ya Nyasa Big Bullets ya Malawi na FC Palatinum ya Zimbabwe. Simba ilianza taratibu kwa kusoma nyendo za wapinzani, lakini hata UD Songo nao ilicheza kwa kwanza kuepuka kuruhusu bao la mapema. Dakika ya 13, John Banda alijaribu kumiliki mpira na kuachia mkwaju mkali uliopanguliwa na kipa wa Simba, Beno Kakolanya na kuzaa kona ambayo hata hivyo haikuzaa matunda. Meddie Kagere alipoteza nafasi ya wazi kuindia Simba bao la kuongoza  dakika ya 18 baada ya kupigiwa pasi safi na John Bocco, lakini aliukosa mpira. Pachoio Lau Há King alishindwa kutumia vema nafasi aliyopata dakika ya 22, kuindikia UD Songo bao la kuongoza baada ya kupiga shuti lililopita ju ya lango la Simba wakati akiunganisha mpira wa kona. Kiungo wa Simba, Sharaf Eldin Shiboub alilimwa kadi ya njano dakika ya 26, baada ya kumchezea rafu John Banda. Nahodha wa Simba, Bocco alishindwa kutumia nafasi aliyoipata dakika 40, kuindikia Simba bao baada ya kuingia na mpira hadi ndani ya eneo la hatari la UD Songo kabla ya kuachia mkwaju uliotoka nje. Kipindi cha kwanza kilimalizika kwa timu hizo kwenda mapumziko zikiwa zimetoshana nguvu, hata hivyo UD Songo itabidi ijilaumu kwani ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga, lakini washambuliaji wake walikosa utulivu wa kutumia. Simba ilishindwa kuwika kipindi cha kwanza kutokana na kushindwa kucheza kandanda lao la pasi nyingi fupi fupi, baada ya kubanwa hasa sehemu ya katikati ya uwanja. Hata hivyo, ilitengeneza nafasi mbili ambazo washambualiji wake Kagere na Bocco walikosa maarifa ya kuutia mpira kimiani. Kipindi cha pili kilianza kwa kocha wa Simba, Patrick Aussems kufanya mabadiliko kwenye safu yake ya kiungo kwa kumtoa Clatous Chama na kumwingiza Mzamiru Yasssin. Dakika ya 60, UD Songo ilifanya mabadiliko, alitoka Frank Banda na nafasi yake kujazwa na Sebastiano Mario. Safu ya ulinzi ya Simba ilionekana kufanya makosa ya mara kwa mara,lakini hata hivyo washambulaji wa UD Songo walishindwa kutumia nafasi hizo kujipatia mabao. Simba ilifanya mabadiliko mengine dakika ya 70, alitoka Francis Kahata na kuingiza Deogratius  Kanda. Mabadiliko hayo yaliiongozea Simba nguvu kwenye eneo la kiungo na kufanikiwa kutengeneza nafasi nzuri ya bao dakika ya 77, lakini mpira wa kichwa uliopigwa na Shiboub ulipanguliwa na kipa wa UD Songo,Charles Swini. Dakika ya 78, Aussems alifanya mabadiliko mengine kwenye kikosi chake, alimtoa Jonas Mkude na kumwingiza Hassan Dilunga. Dakika ya 82, UD Songo ilifanya mabadiliko, alitoka Ernesto Sterio na kuingia Jose Junior. Dakika ya 90, Jose Junior  wa UD Songo, alilimwa kadi ya njano, baada ya kumchezea rafu Hassan Dilunga. Katika mchezo huo, UD Songo watajilaumu wenye kwa kukosa utulivu na kushindwa kutumia nafasi nyingi walizotengeneza kwenye mchezo huo. Hadi dakika tisini zinakamilika matokeo yalikuwa suluhu. Wakati huo huo, Wawakilishi wa Zanzibar katika Ligi ya Mabingwa Afrika, KMKM iliianza vibaya michuano hiyo, baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Primeiro de Agosto ya Angola. Wawakilishi wengine wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho, timu ya Azam FC itashuka dimbani leo ugenini nchini Ethiopia kuumana na Kenema. Kocha Msaidizi wa Azam, Iddi Cheche alisema jana kuwa, wachezaji wake wana morali ya juu ya kutaka kupata ushindi ugenini kabla ya kurejea nyumbani kumaliza kazi.
michezo
NA MWALI IBRAHIM, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Yanga, Mbrazil Marcio Maximo, amemkingia kifua mchezaji wake, Mbrazil Genilson Santos ‘Jaja’ kwa kuwataka mashabiki wasitegemee vitu vingi kutoka kwa wachezaji warefu kwani wana vitu vichache vyenye mafanikio. Maximo aliyasema hayo juzi baada ya mechi yao ya kirafiki dhidi ya Thika United ya nchini Kenya iliyochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lilofungwa na Jaja, huku baadhi ya mashabiki wakihoji uwezo wake kutokana na kutoonyesha makeke zaidi uwanjani. Alisema siku zote wachezaji warefu hawana vitu vingi lakini wana nafasi kubwa hasa wanapokuwa katika eneo la umaliziaji, kwani pale ndio wanaonekana umuhimu wao. “Wachezaji kama Bonifance Ambani na John Bocco, ni wachezaji warefu lakini wana vitu vichache sana vizuri na ndio maana wanazidi kuonekana bora, hivyo wachezaji warefu hawana mambo mengi lakini kwa sasa sitaki kumzungumzia mchezaji mmoja mmoja nataka kuizungumzia timu nzima kwa uwezo waliouonyesha uwanjani,” alisema. Alisema, wachezaji wake wameanza kumuelewa na wameonyesha kiwango kizuri katika mchezo huo kwani wameweza kubadilisha mchezo, mfumo na wameanza kuelewa licha ya makosa machache yaliyojitokeza ambayo atatumia wiki moja kuyarekebisha kabla ya kukutana na Azam FC katika mechi yao ya Ngao ya Hisani, Septemba 14, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Alisema, Thika ni timu nzuri na ni timu ngumu na yenye kasi lakini wachezaji wake wameweza kuikabili vema na hatimaye kuibuka mabingwa, hayo ni mafanikio makubwa kwake na anaimani kadiri siku zinavyokwenda timu yake itazidi kuwa timu bora zaidi. Alisema, uwezo huo wa wachezaji wake unamuhakikishia kuwa wataibuka na ubingwa mbele ya Azam ambayo nayo ni timu nzuri yenye uwezo mkubwa, lakini watahakikisha wananyakuwa ubingwa mbele yao na kuanza vema Ligi Kuu msimu huu.
michezo
Na Safina Sarwatt-MOSHI WANANCHI  wa vijiji vya Mikocheni na Chemchem, Kata ya Arusha Chini wilayani Moshi mkoani Kilimanjaro,  wamekimbia makazi yao baada ya kuzingirwa na maji kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha na kusababisha mafuriko.  Pia wameeleza hofu yao ya kukumbwa na magonjwa ya mlipuko yakiwamo ya matumbo na corona kutokana na kuwekwa kwenye eneo la shule ambapo kuna msongamano.  Wakizungumza na waandishi wa habari kijijini hapo, wananchi hao wameomba msaada wa vifaa vya kujikinga na ugonjwa wa corona kutokana na kuishi kwenye msongamano wa watu.  Inaelezwa kuwa hadi sasa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Ally Rajabu, amepoteza maisha huku kaya zaidi ya 500 zikikikosa makazi kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji yanayotiririka kutoka Mto Kikuletwa, Ronga, Bwawa la Maji ya Kiwanda cha Sukari TPC Moshi kuvunja kingo zake na kuelekeza maji kwenye Kijiji cha Mikocheni. Mmoja wa waathirika wa mafuriko hayo, Vicent Kalonga alisema kuwa kwa sasa wana hali mbaya kutokana kwamba hawana makazi, nyumba zao zimebomoka, mifugo imechukuliwa na maji pamoja na chakula. “Hali ni mbaya, tunahofia usalama wa afya zetu kwani hatuna vifaa vya kujikinga na corona, hatuna chakula, tunaomba Serikali itusaidie mahali pa kuishi pamoja na vifaa vya kujikinga na chakula,” alisema Kalonga.  Diwani wa Kata ya Arusha Chini, Roger Mmary, alisema kuwa hayo ni maafa makubwa na kwamba hayaijawahi kutokea tangu miaka ya 1970. Mmary alisema kuwa kwa sasa wananchi hao wamehifadhiwa katika majengo ya msingi Mikocheni, msikiti  na kanisani.  Alisema kuwa kaya zaidi 2,700 katika vijiji viwili vya Mikocheni na Chemchem zimeathiriwa na mafuriko na kwamba kwa sasa hakufikiki hivyo  huku akiiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuwasaidia wananchi hao ambao kwa sasa wamehifadhiwa kwenye mashule na makanisani.  Naye Mwenyekiti wa Kijiji cha Mikocheni, Evarist Komba alisema jumla vitongoji vinne vimeathirika na kwamba hali kwa sasa ni mbaya kutokana na nyumba zilizokuwa zimesalia kuendelea kuanguka na maji yanazidi kuongezeka. 
kitaifa
Wananchi hao wamesema bei hiyo ya sukari ni kinyume cha bei elekezi ya Serikali ambayo iliagiza kilo moja ya sukari iuzwe kwa Sh 1,800.Anitha John ni mfanyabiashara katika soko kuu la Bukoba anayeuza bidhaa mbalimbali ikiwemo sukari ambaye amesema sukari imepanda bei na ameamua kuacha kuuza kwa sababu kwa wakala kilo 50 zinauzwa Sh 100,000 na kwenye stakabadhi wanaandikiwa 90,000 na wakati wa nyuma kilo hizo 50 walinunua kwa Sh 76,000.“Jambo la kushangaza si kwamba sukari haipo maana sukari inashushwa na kupelekwa kwenye maghala ukienda kwenye ghala kununua unaambiwa hakuna sukari, jambo ambalo ni tatizo kwa wafanyabiashara wadogo kama mimi, vinginevyo Serikali itoe vibali kwa kila mtu akajinunulie kiwandani ili biashara isikwame,” alieleza John.Sebastiani Tweyambe ambaye ni mfanyabiashara mwingine wa bidhaa hiyo, alisema wiki mbili zilizopita sukari iliuzwa kwa Sh 2,000 wakati Rais John Magufuli alipotoa bei elekezi ya Sh 1,800, sasa baada ya bei kushuka inazidi kupanda mpaka sasa imefikia Sh 2,400 hadi 2,500 kutokana na wanavyonunua mzigo.“Ukitizama bei hiyo ya kununulia kilo 50 kwa Sh 100,000, mimi mfanyabiashara inanishinda je, kwa wale wasio na uwezo kabisa wa kupata hata Sh 2,000 iliyokuwepo mwanzo wataiweza bei ya Sh 2,500?”Alihoji Tweyambe.Naye Ofisa Biashara wa Mkoa wa Kagera, Aloyce Tendega alisema, uhaba wa sukari pamoja na bei ya juu ya bidhaa hiyo vinasababishwa na kupungua kwa sukari katika mikoa mingine pamoja na kusimama kwa uzalishaji katika kiwanda cha sukari cha Kagera kutokana na mvua.
uchumi
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania Simon Sirro ameagiza askari wawashughulikie wanaume wanaopiga au kuwanyanyasa wake zao.IGP Sirro ameyasema hayo wakati akizindua Ofisi ya Dawati la Jinsia na Watoto Serengeti mkoani Mara.Amesema kuna namna nyingi za ukiukwaji wa haki za wanawake na watoto ukiwemo ubakaji, ulawiti, ndoa za utotoni, na mfumo dume kwenye jamii.“Mfumo dume ndugu zangu wana Mara ndio unaotusumbua, hatubadiliki, hatubadilishi fikra, hatuendani na wakati, dunia inakwenda mbele sisi tunabaki palepale” amesema Sirro.Amebainisha kuwa, suala la wanawake kupigwa au kunyanyaswa ni kubwa kwa jeshi hilo, na kwamba, mwaka jana kulikuwa na matukio 43, 487 ya kijinsia na watoto na mwaka huu yamepungua hadi 41,416.“Na nimewaambia askari ukipata mtu amempiga mke wake, kamnyanyasa mke wake na wewe mshughulikie, narudia, mshughulikie kwa nguvu ya kadri, la msingi tutakushughulikia kwa nguvu ya kadri” amesema Sirro.Amesema, wanaume wakishughulikiwa itasaidia jamii kubadilika kwa kuwa sasa imekuwa vigumu hata kupata wachumba.“Sio mtu wako, sio mtoto wako, mnakorofishana ugomvi wa kawaida, unampiga, unampiga nini, unamfundisha nini, wewe ni nani kwake. Yule mmekubaliana tu, kama unaona ndoa imekuwa na matatizo achana nae tafuta mwingine. Unamkata sikio, unampiga wewe ni nani, upo juu ya sheria? Hizo nguvu umezipata wapi, mamlaka amekupa nani kufanya hivyo” amesema Sirro.
kitaifa
Timu hiyo imetoka kushinda mchezo wake uliopita dhidi ya Mtibwa Sugar bao 1-0 na kuishusha Yanga nafasi ya tatu, ikipanda nafasi ya pili kwa pointi 49 katika michezo 26 iliyocheza.Akizungumza na waandishi wa habari jana, Ofisa Habari na Mawasiliano wa Azam FC Jaffar Iddi alisema timu yake imejipanga kuhakikisha inashinda michezo yote minne iliyobaki.“Timu yetu imejipanga vizuri kushinda michezo yote ingawa tunajua kuna michezo mingine itakuwa migumu kutokana na kwamba baadhi ya timu tunazotarajiwa kukutana nazo zinapambana kushuka daraja,”alisema.Alisema kikosi hicho kitaondoka chini ya Kocha Msaidizi Idd Cheche kwani Kocha Aristica Cioaba amefungiwa mechi tangu walipocheza dhidi ya Njombe Mji na Shirikisho la soka Tanzania (TFF) hivyo, aliondoka tangu juzi kuelekea Hispania kwa mafunzo ya muda mfupi.Katika hatua nyingine, beki majeruhi wa Azam Yakubu Mohamed anatarajiwa kuondoka leo kuelekea Afrika Kusini kwa uchunguzi wa jeraha lake baada ya kudai kuwa bado anapata maumivu.Iddi alisema mchezaji huyo atapelekwa katika hospitali ya St. Vicent Parot kutazamwa kama inawezekana kufanyiwa upasuaji tena.Wakati huo huo, Azam imewatakia kila la heri wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika Yanga wanaoondoka leo kuelekea Algeria kwa mchezo wa hatua ya makundi dhidi ya USM Alger.“Mchezo sio uadui wale ni wenzetu tuweke tofauti zetu pembeni, ni wawakilishi wan chi, tunawaombea wakafanye vizuri,”alisema.
michezo
Mwandishi wetu, Tanga MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itawasaidia wafanyabiashara wanaokwepa kodi kuacha vitendo hivyo vya kuikosesha Serikali mapato. Shigela ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na maafisa wa TRAwanaofanya kampeni hiyo mkoani humo ambayo imelenga kuwaelimishawafanyabiashara kuhusu masuala ya kodi ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.  Amesema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikwepa kulipa kodi pengine kwa kujua au kutokua, jambo ambalo linahitaji elimu ya uelewa ili kila mwananchi afahamu wajibu wake kwenye ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Akiizungumzia kampeni hiyo, Shigela ameipongeza TRA kwa kuendesha zoezi hilo katika mikoa mbalimbali na kusema litaongeza ukusanyaji wa mapato baada ya wafanyabiashara kuelimishwa na kufahamu kuwa maendeleo ya nchi yanasababishwa na ulipaji wa kodi kwa ajili ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, barabara, umeme na maji. Shigela amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari bila kusubiri kubugudhiwa na serikali, huku akieleza kuwa serikali itaendelea kupambana na wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa za magendo nchini kwa kupitia bandari bubu zilizopo kandokando ya Bahari ya Hindi. “Nchi yoyote haiwezi kupiga hatua ya maendeleo bila wananchi wake kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa sababu kodi ndio kila kitu huwezi kujenga barabara kama wafanyabiashara hawataki kulipa kodi, huwezi kuimarisha huduma za afya kama hakuna kodi na pia huwezi kuimarisha mifumo ya elimu bila kodi,” alisema Shigela. Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Tanga, Specioza Owure amesema kuwa, maafisa hao wa TRA wanaofanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi, watafika maeneo mbalimbali yenye wafanyabiashara katika mkoa wa Tanga na watawaelimisha kuhusu umuhimu wa kodi na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati. “Maafisa hawa wanatumia jitihada zote kuwaelimisha wafanyabiashara, tunafanya hivi ili kila mmoja afahamu wajibu wake wa kulipa kodi sambamba na kusogeza huduma za TRA karibu na wateja,” alisema Owure.Kampeni ya elimu kwa mlipakodi mkoani Tanga inatarajia kumalizika Juni 30, 2020 ambapo lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, kusikiliza maoni na changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati.
uchumi
SHIRIKISHO la Soka la Misri (EFA) limechapisha tiketi 30,000 kwa ajili ya mchezo wa kirafi ki kati ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars na Misri kwa ajili ya mchezo wa kujiandaa na mashindano ya Mataifa ya Afrika, Afcon 2019 utakaofanyika keshokutwa.Mafarao hao na Taifa Stars, kila timu inatarajia kucheza mechi mbili za majaribio ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya fainali za Afcon 2019 zitakazofanyika hapa kuanzia Juni 21 hadi Julai 19. Misri baada ya kucheza na Taifa Stars itacheza mchezo mwingine wa kujipima nguvu dhidi ya Guinea wakati Tanzania itacheza mchezo wa pili dhidi ya Zimbabwe.Kwa mchezo huo wa kirafiki dhidi ya Tanzania, EFA imetangaza kuwa mashabiki 30,000 wanatarajia kuingia uwanjani kushuhudia mchezo huo, ambao utachezwa kwenye Uwanja wa Borg El-Arab, Alexandria. Gharama ya tiketi za kawaida itakuwa 30 EGP (ambayo ni sawa na sh 4,114.40), wakati zile za VIP tiketi moja itauzwa kwa 100 EGP (ambayo ni sawa na Sh 13,716.94), ambapo tiketi hizo zimeanza kuuzwa kwenye Klabu ya Olimpiki, El-Teram SC, na Kiwanja cha Ndege cha Borg El- Arab.Mwamuzi wa kimataifa wa Misri, Mohamed Adel atachezesha mchezo huo, huku akisaidiwa na Wamisri wenzake Samir Gamal na Youssef El-Bossaty. Mafarao wamepangwa katika Kundi A pamoja na timu ya taifa ya Uganda, The Cranes, na Zimbabwe, huku mchezo wao wa ufunguzi utafanyika Juni 21.Kwa upande mwingine, Tanzania, ambayo inatarajia kucheza mchezo wa pili baada ya huo na Misri, wako katika kundi gumu la C pamoja na vigogo wa Afrika, Senegal na Algeria, pamoja na Kenya. Wakati huohuo, Taifa Stars inaendelea na mazoezi yake jijini Cairo baada ya kuwa timu ya kwanza kutua nchini humo tayari kwa maandalizi ya mwisho kwa ajili ya fainali hizo, ambazo kwa mara ya mwisho ilishiriki miaka 39 iliyopita.
michezo
Elizabeth Kilindi – Njombe                MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Njombe leo inatarajiwa kuanza kusikiliza ushahidi wa Jamhuri katika kesi ya inayomkabili Ezroni Ndone(44) Mkazi wa Joshoni mjini Njombe, anayedaiwa kumbaka na kumlawiti mtoto wake. Shauri hilo namba 14 la mwaka 2020 linasikilizwa na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Njombe, Hassan Makube. Awali mawakili wa Serikali Nuru Minja na Andrew Nandwa, waliiomba mahakama kufanya mabadiliko chini ya kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya mwenendo ya makosa ya jinai sura ya 20 marejeo 2002 kubadilisha hati ya mashitaka umri wa muathirika wa tukio usomeke miaka 10 badala ya 11 kama inavyosemeka kwenye kosa la kwanza na pili. Shauri liliendelea kwa kusomwa hoja za awali ambapo wakati upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na wakili wa serikali Minja na Mandwa upande wa mshtakiwa unawakilishwa na wakili Emmanuel Chengula. Mara baada ya kusikiliza hoja za awali, Hakimu Makube alihairisha kesi hiyo hadi Februari saba kwa ajili ya hatua kusikiliza ushahidi wa Jamhuri. Hata hivyo mstakiwa huyo ameshindwa kutimiza masharti ya dhamana kwa sababu alitakiwa awe na bondi ya Sh milioni 10 na wadhamini watatu wawili kati yao wawe wanatoka taasisi zinazotambulika na wathibitishe. Kesi hiyo imeonekana kubeba hisia kwa wananchi wa Njombe hali iliyopelekea kujaa kwenye chumba cha mahakama na wengine kuzuiwa kuingia.
kitaifa
SHIRIKA la Umeme Tanzania limesema kwa sasa kituo cha kuzalisha umeme cha Ubungo II kiko katika matengenezo makubwa ya kinga ambayo itasaidia kutokuwa na upungufu wa umeme unaotokana na sababu za matengenezo makubwa.Aidha, Tanesco imesema matengenezo hayo ni pamoja na kufanya mitambo mitatu iliyopo katika kituo hicho isizimike kila baada ya umeme gridi ya taifa kukatika kama ilivyo sasa hadi muda wa matengenezo makubwa ya mitambo hiyo itakapofikiwa tena ambayo ni baada ya kufanya kazi saa 40,000 nyingine.Akitoa taarifa kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Dk Hamisi Mwinyimvua, Mkuu wa Kituo hicho, Nicholas Busunge alisema matengenezo hayo ni baada ya mtambo kutembea kwa saa 40,000 tangu kituo kuanza kuzalisha umeme na pia kusaidia mitambo kuanzisha gridi kurudisha umeme mapema.“Marekebisho hayo yataiwezesha mitambo kuanzisha gridi kama ilivyo katika kituo cha Kidatu kwa kurudisha umeme mapema katika maeneo ya Dar es Salaam wakati umeme wa gridi ya taifa unapokatika,” alisema Busunge.Busunge alisema matengenezo hayo yanafanyika kwa hatua ambapo utazimwa mtambo mmoja baada ya mwingine wakati ikifanyiwa matengenezo hadi itakapokamilika mitambo yote.“Kwa sasa tuna matengenezo ya hatua C, awali yalishafanyika ya hatua B ambayo ni baada ya mtambo kutumika kwa saa 20,000 na matengenezo haya ni kutokana na maelekezo ya mtaalamu mtengenezaji wa mitambo hii,” alisema.Alisema kuwa matengenezo hayo yalianza Januari 9, mwaka huu katika mtambo namba mbili, mtambo namba tatu matengenezo yake yataanza Machi 12,mwaka huu, hadi Aprili 15, mwaka huu baada ya mtambo namba mbili kukamilika na mtambo namba moja utafanyika kuanzia Aprili 30 hadi Juni 5, mwaka huu.Aidha, Busunge alisema kuwa matengenezo hayo yanafanywa na wataalamu wa shirika hilo wakishirikiana na mkandarasi Siemens Industial Turbomachinery AB ambaye ni mtengenezaji mitambo hiyo.Busunge alisema kuwa baadhi ya vipuri viliharibika sana hivyo kusababisha kuagizwa vingine kuagizwa nchini Sweden jambo ambalo lililosababisha muda wa matengenezo katika mtambo namba mbili ulioanza kutengenezwa kuchelewa utakamilika Machi mosi mwaka huu.Alisema kuwa kuzimwa kwa mtambo mmoja sasa kwa ajili ya matengenezo hayo kunasababisha upungufu wa umeme kwenye mfumo wa gridi ya taifa unaofikiamegawati 43 upungufu ambao utaendelea kutokea hadi matengenezo ya mitambo yote utakapokamilika Juni mwaka huu.Busunge alisema hakutakuwa na tatizo la kuzimika mitambo jambo ambalo upotevu wa megawati 86 kwa masaa 40 kama ilivyo sasa ambapo itawezesha kuanzisha gridi ya taifa.Mwinyimvua alipongeza kituo hicho kwa kazi zake za kufanya upatikanaji umeme uwepo ambao aliwataka pia kukamilisha utengenezaji wa mitambo hiyo kwa wakati.“Mimi niwapongeze tu kwa kazi mnayoifanya, umeme ni nishati iliyohitajika sana katika uchumi wetu wa sasa kwahiyo tujitahidi sana kukamilisha kazi hii kwa wakati umeme upatikane,” alisema Dk Mwinyimvua.
kitaifa
WADAU wa kilimo cha alizeti mkoani Dodoma, wameiomba serikali kuandaa mafunzo maalumu kwa maofisa ugani kuwaongezea uwezo katika kutoa elimu stahiki kwa wakulima.Ombi hilo lilitolewa na wadau hao wakati wa kikao cha wajumbe wa Bodi ya Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo Tanzania (AMDT), ambao walifanya ziara hivi karibuni mkoani Dodoma kujifunza na kuona changamoto zinazowakabili wakulima.Wadau katika Wilaya za Bahi na Kongwa wamesema, changamoto kubwa ambayo wakulima hao wanakabiliana nazo ni kukosekana kwa wataalamu wa kilimo waliobobea katika kilimo cha zao hilo.Wamesema pamoja na changamoto hiyo, pia kuna idadi ndogo ya maofisa ugani ukilinganisha na mahitaji halisi ya idadi ya wakulima waliopo katika maeneo mengi mkoani humo.Mmoja wa wadau hao, Yohana Mwanjara ambaye anajihusisha na usambazaji wa mbegu na pembejeo kwa ajili ya alizeti amesema, licha ya jitihada kubwa ambayo serikali imekuwa ikifanya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali, bado tatizo la ukosefu wa wataalamu wenye weledi wa zao hilo ni kikwazo kikubwa.Amesema wengi wa wataalamu waliopo hawaendani na mabadiliko na teknolojia za kilimo zilizopo na hivyo kuwa kikwazo katika kumsaidia mkulima."Unamkuta mkulima anahangaika kupata maarifa ya nini cha kufanya lakini hawezi pata msaada matokeo yake unakuta mkulima huyu anaishia kulima tu kwa mazoea," amesema Mwanjala.Ofisa Kilimo wa Wilaya ya Kongwa, Jackson Shija amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kuongeza kuwa mbali na changamoto ya elimu duni ya zao la alizeti kwa maofisa ugani, aliitaja changamoto nyingine kuwa ni uwepo wa idadi ndogo ya maofisa ugani kama kikwazo kingine katika kumfikia mkulima mmoja mmoja."Idadi yetu ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wakulima waliopo, hali hii imetulazimu wakati mwingine kuwatumia maofisa mifugo kusaidia kwenye maeneo ambapo hatuwezi kufika na hii kiukweli ni changamoto kubwa maana hata ambapo tunaweza fika wakati mwingine unakuta baadhi yetu uelewa wa zao hili kuwa ni mdogo na hata kuzidiwa maarifa na wakulima," amesema Shija.Hadi sasa takribani maofisa kilimo 38 pekee ndio wanaotajwa kupata mafunzo maalumu kuhusu zao hilo ndani ya mkoa huo, idadi inayotajwa kuwa ni ndogo ukilinganisha na idadi ya wakulima takribani 33,400 waliopatiwa mafunzo rasmi ya zao hilo.Katika kuhakikisha mkoa wa Dodoma unaondokana na changamoto hiyo, na kulifanya zao hilo kama mojawapo ya mazao ya kibiashara yanayotegemewa na mkoa huo, uongozi wa Serikali mkoani humo umeanza mkakati wa kuwapatia mafunzo maalumu maofisa ugani ili kuwaongezea umahili katika kutoa elimu na huduma kwa wakulima.Hatua hiyo inatajwa kuwa itachochea katika kuongeza hamasa kwa wakulima wengi kujihusisha na kilimo cha zao hilo na hivyo kuvutia wawekezaji wengi kuwekeza viwanda vitakavyokuwa vikichakata mazao yatokanayo na zao hilo.Katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma, Maduka Kessy amesema wao kama mkoa wanatambua uwepo wa tatizo hilo na tayari hatua mbalimbali zimekwisha anza kuchukuliwa kwa lengo la kuhakikisha mkoa wa Dodoma unaondokana kabisa na ukosefu wa wataalamu wasiokuwa na maarifa ya kujitosheleza.Ameongeza kuwa kwa kuanzia uongozi wa mkoa huo umekirasimisha kituo cha utafiti wa kilimo cha Hombolo, mkoani Dodoma, kuwa kituo kitakachotoa mafunzo ya ubobevu kwa wataalamu wa kilimo katika mazao ya alizeti na ufuta. Maduka aliongeza kuwa hatua hiyo itasaidia katika kuwaongezea maarifa wataalamu wa kilimo na hivyo kuondokana na tatizo hilo."Pamekuwepo na dhana kwamba Afisa Kilimo yoyote anayomaarifa ya kila zao, dhana hii kiukweli imekuwa ikiturudisha nyuma maana haiwezekani maafisa hawa wakajua kila kitu kwenye kilimo, na ndio maana sisi kama mkoa tumeliona na tumeanza mchakato wa kukipandisha hadhi kituo cha Hombolo ili kiweze kutoa mafunzo ya Ubobevu wa zao la Alizeti" amesema Bwana Maduka.Katika kuunga mkono jitihada za mkoa wa Dodoma, Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko ya Kilimo nchini (AMDT), Kupitia Mradi wake wa alizeti ni mmoja wa wadau walioitikia wito huo kwa kushirikiana na wadau wengine katika kumwezesha Mkulima pamoja na maofisa ugani kwa kuwapata elimu stahiki pamoja na mbegu bora zenye kuleta tija katika kilimo cha Alizeti.Meneja wa Mradi wa Alizeti, Martin Mgalah kutoka Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko (AMDT), amesema taasisi yao imelenga kumsaidia mkulima kupata elimu sahihi na masoko ambayo yatamwezesha mkulima katika kufungua fursa mbalimbali za kiuchumi."Taasisi ya AMDT imelenga sana Kumwezesha mkulima mdogo kuweza kupata elimu na maarifa ya namna nzuri ya kufanya kilimo cha Alizeti, Maana sisi kama taasisi tunaina fursa iliyopo na tungependa mkulima huyu mdogo anufaike nayo," alisema Mgalah.Kwa Upande wao baadhi ya wakulima wa zao hilo, Jackson Mazoya na Angelina Sudayo kutoka wilaya ya Bahi na Kongwa wameipongeza Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Masoko na Uongozi wa Mkoa wa Dodoma kwa jitihada wanazozifanya, wameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau wake kuhakikisha mpango huo unatekelezwa kwa wakati ili wakulima waweze kunufaika kupitia zao hilo.Taasisi ya Kuendeleza Mifumo ya Kimasoko Katika Kilimo Tanzania, AMDT imekuwa ikitekeleza miradi mbalimbali katika mikoa 15 nchi ambapo mpaka sasa Zaidi ya wakulima 150,000 wamekwisha fikiwa kupitia mradi huu ambao lengo lake kubwa ni kumwezesha mkulima mdogo kupata tija katika kilimo hicho kwa kulima na kuzingatia kanuni bora za kilimo.
uchumi
WAKATI Yanga ikishuka dimbani leo kuchuana na Alliance katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) Kocha Mkuu Mwinyi Zahera ametoa ruksa kwa wachezaji wanaotaka kuondoka.Akizungumza jana, Zahera alisema ameshazungumza na viongozi wa klabu hiyo na kuwataka kutoogopa dhidi ya wale walioonyesha nia ya kuondoka na badala yake wawaruhusu. “Nimewaeleza viongozi kama kuna mchezaji yeyote anatakiwa na timu fulani wasitetereke, wawape ruhusa ya kuondoka wao wenyewe wataona mabadiliko makubwa katika ligi ijayo,”alisema.Kauli hiyo ya Zahera imekuja siku chache baada ya kuwepo kwa taarifa za baadhi ya wachezaji wake kuondoka mwishoni mwa msimu akiwemo Ibrahim Ajibu anayedaiwa kurejea Simba. Zahera alisema baada ya kumalizika kwa ligi anatarajia kusajili wachezaji wakubwa watakaoisaidia timu hiyo kufanya vizuri msimu ujao huku akiongeza kuwa anataka kuhakikisha hadi kufika Mei 15 mwaka huu awe amemaliza usajili wake.Alisema sababu ya kutaka kumaliza usajili mapema ni ili apate muda wa kwenda kwenye majukumu ya timu ya taifa ya Congo DR inayotarajia kwenda kuweka kambi Ulaya kwa maandalizi ya fainali za Afrika (AFCON) zinazotarajiwa kufanyika Misri baadaye mwaka huu.Kuhusu mchezo wa leo, Zahera alisema wachezaji wake wako vizuri na tayari kwa mchezo huo huku akihamasisha mashabiki wajitokeze kwa wingi kwani watafurahia ushindi. “Maandalizi yako vizuri na tayari kwa mchezo, naamini mashabiki watakuja kwa wingi kuipa nguvu timu iweze kupata ushindi,”alisema.Katika mchezo wa kwanza wa ligi waliocheza hivi karibuni kwenye uwanja huo wa Mwanza Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0 hivyo unatabiriwa huenda ukawa mchezo mgumu. Vinara hao wa ligi watawakosa nyota wao kadhaa akiwemo Gadiel Michael aliyekwenda Afrika Kusini kufanya majaribio katika klabu ya Superspot, Abdallah Ninja anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, Mwinyi Haji, Ibrahim Ajibu, Juma Mahadhi na Juma Abdul ambao ni majeruhi.
michezo
Mwandishi wetu, Tanga MKUU wa mkoa wa Tanga, Martine Shigela amesema kampeni ya elimu kwa mlipakodi inayoendeshwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) itawasaidia wafanyabiashara wanaokwepa kodi kuacha vitendo hivyo vya kuikosesha Serikali mapato. Shigela ameyasema hayo ofisini kwake alipotembelewa na maafisa wa TRAwanaofanya kampeni hiyo mkoani humo ambayo imelenga kuwaelimishawafanyabiashara kuhusu masuala ya kodi ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha kulipa kodi kwa wakati.  Amesema kuwa, kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakikwepa kulipa kodi pengine kwa kujua au kutokua, jambo ambalo linahitaji elimu ya uelewa ili kila mwananchi afahamu wajibu wake kwenye ulipaji wa kodi kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla. Akiizungumzia kampeni hiyo, Shigela ameipongeza TRA kwa kuendesha zoezi hilo katika mikoa mbalimbali na kusema litaongeza ukusanyaji wa mapato baada ya wafanyabiashara kuelimishwa na kufahamu kuwa maendeleo ya nchi yanasababishwa na ulipaji wa kodi kwa ajili ya kuboresha sekta mbalimbali ikiwemo afya, elimu, barabara, umeme na maji. Shigela amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanalipa kodi kwa hiari bila kusubiri kubugudhiwa na serikali, huku akieleza kuwa serikali itaendelea kupambana na wakwepa kodi wanaoingiza bidhaa za magendo nchini kwa kupitia bandari bubu zilizopo kandokando ya Bahari ya Hindi. “Nchi yoyote haiwezi kupiga hatua ya maendeleo bila wananchi wake kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa sababu kodi ndio kila kitu huwezi kujenga barabara kama wafanyabiashara hawataki kulipa kodi, huwezi kuimarisha huduma za afya kama hakuna kodi na pia huwezi kuimarisha mifumo ya elimu bila kodi,” alisema Shigela. Kwa upande wake Meneja wa Mamlaka ya Mapato Tanzania Mkoa wa Tanga, Specioza Owure amesema kuwa, maafisa hao wa TRA wanaofanya kampeni ya elimu kwa mlipakodi, watafika maeneo mbalimbali yenye wafanyabiashara katika mkoa wa Tanga na watawaelimisha kuhusu umuhimu wa kodi na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati. “Maafisa hawa wanatumia jitihada zote kuwaelimisha wafanyabiashara, tunafanya hivi ili kila mmoja afahamu wajibu wake wa kulipa kodi sambamba na kusogeza huduma za TRA karibu na wateja,” alisema Owure.Kampeni ya elimu kwa mlipakodi mkoani Tanga inatarajia kumalizika Juni 30, 2020 ambapo lengo la kampeni hiyo ni kutoa elimu ya kodi kwa wafanyabiashara, kusikiliza maoni na changamoto zao ikiwa ni pamoja na kuwahamasisha kulipa kodi kwa wakati.
uchumi
USAFIRI wa treni kutokea Dar es Salaam kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro utafanyika wakati wa usiku, huku treni hiyo ikianza majaribio ya siku mbili ya kuangalia ufanisi wa treni hiyo jana.Akizungumzia safari ya treni hiyo itakayoanza Desemba 6, mwaka huu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alifafanua kuwa treni hiyo itakuwa ikifanya safari zake usiku kwa kuondoka Dar es Salaam kwenda Moshi na kurejea Dar es Salaam kuanzia jioni na kushika safarini usiku kucha kabla ya kufika kituo husika asubuhi.Kadogosa amesema jana watendaji wa TRC wakishirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini (LATRA), walisafiri kutokea Dar es Salaam kwenda Moshi ikiwa ni matakwa ya kisheria yanayoitaka TRC kufanya majaribio ya safari zake kwanza kabla ya kuanza kwa safari rasmi.Alisema leo usiku treni hiyo itaondoka Moshi kurejea Dar es Salaam ikiwa ni jaribio la kuangalia uwezo wake wa kusafiri usiku.“Hapa ninaongea na wewe tumefikia Korogwe na tunaendelea na majaribio ya usafiri huu, ni safari ya treni nzima kwa maana ya mabehewa yote yapo kwenye majaribio,” alisema Kadogosa jana saa alasiri.Aliongeza: “Tupo na wadau wote wa usafiri wa ardhini ambao kila mmoja atatoa tathimini yake kuhusiana na usafiri huu kwa namna walivyouona na TRC itatoa tathmini kamili kabla ya kuanza kwa usafiri huu.”Usafiri huo wa treni kwenda mikoa hiyo ya Kanda ya Kaskazini ulisitishwa miaka mingi iliyopita na ulipaswa kuanza Septemba 5, mwaka huu lakini ukasogezwa mbele hadi hiyo Desemba 6, kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo ya kutokamilika kwa miundombinu yake kutokana na mvua.Kuanza kwa usafiri huo itakuwa ni neema kwa wasafiri wanaokwenda mikoa inayopita treni hiyo hasa wanaoenda mkoani Kilimanjaro ikizingatiwa kuwa inaanza wakati wa kipindi cha mwisho wa mwaka ambacho kunakuwa na abiria wengie wanaokwenda mkoani Kilimanjaro kwa mapumziko ya Sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Usafiri wa treni ni nafuu kwao kutokana kiwango kidogo cha nauli kitakachokuwa kikitozwa ikilinganishwa na kiwango cha nauli ya mabasi ya kawaida ambayo huanzia Sh 20,000 huku bado kukiwa na uhuni wa kuongeza bei iya nauli bila utaratibu maalumu.Bei za usafiri wa treni kutokea Dar es Salaam hadi Korogwe daraja la tatu itakuwa Sh 10,700, daraja la pili kukaa itakuwa Sh 15,300 na daraja la pili kulala Sh 25,400.Usafiri wa Dar es Salaam kwenda Moshi daraja la tatu itakuwa Sh 16,500, daraja la pili itakuwa Sh 23,500 na daraja la pili kulala Sh 39,100.Tangu kuingia madarakani miaka minne iliyopita, Rais John Magufuli amekuwa akisisitiza nia ya serikali yake ya kuimarisha miundombinu ya usafiri, ambao tayari amerejesha usafiri wa treni ya mizigo ya Tanga – Moshi na sasa usafiri huo wa abiria wa Dar es Salaam – Tanga – Moshi ambao ulikuwa maarufu miaka ya nyuma.Licha ya kuhakikisha usafiri huo wa treni ya kaskazini unarejea, ameanza mchakato wa treni ya umeme kutokea Dar es Salaam hadi Makao Makuu ya Nchi Dodoma, huku katika sekta ya anga akiwa amenunua ndege nane na akiendelea na ujenzi wa barabara na madaraja sehemu mbalimbali za nchi.
kitaifa
Na Christian Bwaya, FIKIRIA unavyojisikia pale mtu wa karibu unayemwamini anapokudanganya. Huwezi kufurahia. Uongo, kwa kawaida, unakatisha tama na unaumiza. Wakati mwingine unatafsiriwa kama usaliti. Mtu asiyesema ukweli anasaliti imani waliyonayo watu kwake. Uongo haupendezi. Ingawa wengi wetu hatupendi kudanganywa, kuna mazingira fulani fulani nasi hujikuta tumedanganya. Kwa mfano, rafiki yako anakuuliza uliko au unakokwenda, unaamua kumtajia kwingine. Unaweza kufikiri ni jambo dogo lakini tabia hii inatia doa uhusiano wako na watu. Kwanini watu hudanganya? Kisaikolojia zipo sababu kuu mbili zinazofanya watu wadanganye. Kwanza, watu hutumia uongo kama njia ya kurekebisha mambo pale wanapokabiliwa na hatari ya kupoteza heshima yao. Kwa mfano, unaposhindwa kufanya jambo unalojua linatarajiwa au unapofanya jambo unalojua halikutarajiwa, unajisikia vibaya. Ndani yako unasikia hatia ya kuwa mkosaji. Unakuwa na wasiwasi kuwa kosa ulilofanya linaweza kuharibu uhusiano wako na yule uliyemkosea. Uongo, kwenye mazingira kama haya, unakuwa ni chaguo baya lakini lenye unafuu kwa lengo la kulinda uhusiano na mtu aliyekosewa. Sababu ya pili ni kudanganya kwa lengo la kusababisha maumivu kwa mtu aliyekuumiza. Hapa mwongo hadanganyi kulinda uhusiano wake na yule anayemdanganya bali kulipiza kisasi kwa maumivu anayoamini amesababishiwa na huyo anayemdanganya. Kwa mfano, unapomfanya mtu ajisikie umemvunjia heshima, labda kwa kumdanganya, ni rahisi na yeye kutafuta namna ya kukuvunjia heshima kwa kukudanganya. Ikiwa unapenda watu wanaokuzunguka wakuambie ukweli, siri ni kufanya mambo matatu makubwa. Usiweke mazingira ya kudanganywa  Si kila taarifa unayoihitaji kwa mtu ni ya lazima. Pia, si kila taarifa unayoihitaji kwa mtu inapatikana. Kuna maswali unaweza kumwuliza mtu yakamshawishi kukudanganya. Kwa mfano, maswali ambayo majibu yake yanaweza kuibua utata, yakamfanya mtu asijikie vibaya, yakamkumbusha uchungu aliowahi kukutana nao, ni kichocheo cha kudanganywa. Kabla hujauliza kupata taarifa fulani kwa mtu, jiulize kama kufanya hivyo ni lazima. Ikiwa ni lazima kuulizia suala hilo, angalia namna ya kuuliza ili majibu ya swali yasimfanye mtu akajisikia kudhalilika. Kwa mfano, kama una mpenzi wako, unapohoji masuala ya wapenzi wake wa zamani unaowafahamu, ni wazi unachokoza mzinga wa nyuki bila sababu. Je, ni lazima ujue historia isiyokusaidia? Ikiwa ni lazima kuijua, basi epuka kuonekana unatafuta habari zinazomdhalilisha mwenzako. Hilo la kwanza.  Angalia unavyoupokea ukweli Labda ni namna unavyouchukulia ukweli usioupenda. Unadanganywa kwa sababu pengine anayekudanganya anajua ukweli haulindi uhusiano wenu. Unapoambiwa ukweli unajenga mazingira ya kumfanya aliyesema ukweli huo ajilaumu kwa nini alisema alichokisema. Ukweli unageuka kuwa ugomvi usiotarajiwa, unakasirika, unahukumu na kulalamika kwa sababu tu umepewa taarifa usizozitarajia. Unafanyaje unapoambiwa ukweli usioutaka? Unakasirika au unalaumu? Haipaswi kuwa hivyo. Jenga tabia ya kuupokea ukweli bila ugomvi hata kama anayekwambia anakiri kosa. Shughulikia kosa kwa namna chanya ukijua hata wewe unaweza kukosea. Unapofanya hivyo, unamfanya mwenzako siku nyingine asisite kukuambia jambo lolote kwa sababu anajua ukweli hautamgharimu.  Onesha mfano Wakati mwingine unadanganywa kwa sababu hicho ndicho unachokifanya wewe. Huwezi kutegemea watu wanaoathirika na uongo wako wakuambie ukweli. Unavuna kile ulichokipanda. Unahitaji kufanya kinyume. Onesha mfano kwa watu kwa kuwaambia ukweli. Sema kweli, na wewe utaambiwa ukweli. Lakini pia, kama tulivyodokeza awali, wakati mwingine watu huweza kukudanganya kwa sababu wanalipiza kisasi kwa mambo uliyowafanyia. Kwa mfano kama huna tabia ya kuwaheshimu watu na wao watatumia uongo kama namna ya kukuadhibu. Jenga tabia ya kuwaheshimu watu unaofanya nao kazi au unaoishi nao. Heshima itawasukuma kukuheshimu. Ukweli ni namna moja wapo ya kukuheshimu. Mwandishi ni Mhadhiri wa Saikolojia, Chuo Kikuu cha Kikatoliki Mwenge, Moshi. Blogu: http://bwaya.blogspot.com, 0754870815.
afya
MWANDISHI WETU-MOROGORO WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amechukizwa na mgongano uliopo kati ya Mkuu wa Wilaya (DC) ya Malinyi, Majura Kasika na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya hiyo (DED),  Mussa Mnyeti, hivyo kumwelekeza Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza weledi wa utendaji kazi wao. Agizo hilo alilitoa jana wakati akizungumza na watumishi wa Wilaya ya Malinyi pamoja na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Toboa, akiwa katika siku ya tatu ya ziara yake ya kikazi mkoani Morogoro. “Ni aibu, Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli amewateua vijana wawe viongozi, lakini leo hadi wananchi wa kawaida wanajua mgongano wenu maofisini. Ni aibu Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi mnagombana, tena wakati mwingine mnagombania miradi, mmesahau kutekeleza majukumu yenu,” alisema Majaliwa. Alisema  Serikali imewapa nafasi hiyo ili wakasimamie maendeleo ya wananchi na inapeleka fedha kuboresha maendeleo ya jamii kama kuimarisha huduma za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara, lakini wao wanagombania miradi na mingine wanaichakachua. Majaliwa alisema mbali na CAG na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora kwenda kuchunguza utendaji wa viongozi hao, pia ameuelekeza uongozi wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) wakakague miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwenye wilaya hiyo kama ubora wake unalingana na thamani halisi. “Baada ya kupata majibu ya uchunguzi na kubaini kiini cha tatizo ndani ya wilaya hii hatua zitachukuliwa,” alisema. Awali, Mbunge wa Malinyi, Dk. Haji Mponda (CCM),  alimweleza Waziri Mkuu kwamba kwenye wilaya hiyo kuna matatizo ya uhusiano kati ya Serikali na halmashauri jambo linalosababisha kukwama kwa shughuli za maendeleo. Mbunge huyo alisema kutoelewana kwa viongozi wa wilaya hiyo – DC na DED, kumesababisha mgawanyo mkubwa kuanzia katika Baraza la Madiwani hadi kwa wananchi mitaani, hivyo alimwomba Waziri Mkuu awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo. Katika hatua nyingine, Majaliwa alisema kuwepo kwa mabango mengi kwenye mikutano ya hadhara  ya viongozi wakuu, kunadhihirisha wazi kwamba watendaji wa halmashauri hawawatembelei  wananchi katika maeneo yao na kutatua kero mbalimbali zinazowakabili. “Watendaji hamuendi kuwatembelea wananchi na kusikiliza matatizo yao, haiwezekani wawe wanawasubiri viongozi wa juu na kuwasilisha kero zao kwa njia ya mabango, sasa jipangeni, haya mabango yote mtakuja kuyajibu kwa sababu katika mabango yao hakuna hoja hata moja inayomuhusu Waziri Mkuu, zote ni za ngazi ya halmashauri,” alisema. Alisema Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Magufuli imeelekeza nguvu kubwa katika kuwatumikia wananchi na kutatua kero zao, hivyo itasimamia kuhakikisha kila mtumishi anawajibika kwa kiwango kinachostahili.
kitaifa
NAIBU Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe kwa kushirikiana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na wadau wengine, wamemaliza utata wa faini ya Sh trilioni 11 ambayo Tume ya Ushindani (FCC) iliamuru kampuni nne za ununuzi wa tumbaku kulipa, jambo lililosababisha baadhi yao kufunga virago na kuondoka nchini.Wakati kesi inayohusu faini hiyo ikiwa inarindima huku FCC akiwa ndiye mshitaki na kampuni hizo ni washitakiwa, baadhi wanunuzi wa zao hilo waliacha kununua zao hilo hivyo kupeleka kilio kwa wakulima.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Bashe amesema kulikuwa na changamoto kadhaa zilizokuwa zikikwamisha wanunuzi kuwekeza fedha zao kwenye zao hilo hivyo kuwaathiri wakulima, na sasa tumezimaliza.“Makampuni yote yatakutana na FCC katika kipindi cha siku saba zijazo na kufikia uamuzi wa kufuta faini zinazofikia shilingi trilioni 11. Tumekubaliana na Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa na amekubali faini hizo zitafutwa,” alisema Bashe.Alisema hadi sasa tani 12,000 za tumbaku hazijauzwa na ziko mikononi kwa wakulima.Kutokana na tatizo hilo, hali ya baadaye ya sekta hiyo haikuwa na uhakika baada ya mnunuzi mkuu wa tumbaku nchini, Kampuni ya Tanzania Leaf (TLTC) kuijulisha serikali kwamba ilipanga kufunga biashara nchini, kwa sababu ya faini ya zaidi ya Sh bilioni 452.Kampuni ya tumbaku zilizopigwa faini ya jumla ya Sh trilioni 11 ni Kampuni tumbaku ya Alliance One (AOTTL), Kampuni ya tumbaku ya Premium Active (PAT), Kampuni ya tumbaku ya Japan Leaf (JTILS) na Kampuni ya tumbaku ya Tanzania Leaf (TLTC).“Kiukweli hakuna kampuni ambayo ingeweza kuilipa faini hiyo, na kwa hatua hii sasa tuna uhakika wakulima wa tumbaku wana uhakika wa soko baada ya kufikiwa makubaliano kati ya wanunuzi wa za hilo na serikali,” alisema.Bashe alisema baadhi ya masuala yanayoathiri sekta ya tumbaku ni pamoja na madai ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kampuni hizo zinaidai serikali kwa mabilioni ya fedha.Mkutano ulikubaliana fedha hizo lazima zirejeshwe kwa kampuni hizo nne za ununuzi wa tumbaku katika kipindi cha siku 90 kuanzia Septemba 4, mwaka huu.Mkurugenzi wa Sheria wa Kampuni ya TLTC, Richard Sinamtwa amesema uamuzi huo ni hatua muhimu kuinua sekta hiyo kwani faini hiyo ilikuwa haiendani na uhalisia na kwamba madai yao ya VAT ni ya muda mrefu.Mwenyekiti wa Bodi ya Tumbaku nchini, Hassan Wakasuvi alisema hatua iliyofikiwa ni faraja kubwa mno kwa wakulima kwani sasa wana uhakika kuwa tumbaku iliyoko kwenye maghala yao itanunuliwa.
uchumi
    Na NORA DAMIAN -DAR ES SALAAM KAMATI Maalumu iliyoundwa na Rais Dk. John Magufuli kuchunguza kiwango cha madini yaliyopo katika mchanga wa dhahabu (makinikia) unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, imeanika namna nchi inavyotafunwa bila huruma kwenye sekta ya madini. Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyokabidhiwa jana kwa Rais Magufuli, kamati hiyo imebaini kontena 277 za mchanga huo zilizokuwa Bandari ya Dar es Salaam na maeneo mengine ya nchi, zina dhahabu na madini mengine yenye thamani ya takribani Sh trilioni 1.441. Wakati kamati hiyo ikibaini hayo, taarifa za Wakala wa Serikali wa Ukaguzi Madini (TMAA) na nyingine za kusafirisha mchanga huo zilizokaguliwa na kamati, zinaonyesha mchanga huo una madini yenye thamani ya Sh bilioni 112.1. Mwenyekiti wa kamati hiyo, Profesa Abdulkarim Mruma, akizungumza kabla ya kumkabidhi rais ripoti hiyo, alisema walifanya uchunguzi wa kimaabara kubainisha aina, kiasi na viwango vya madini yatakayoonekana katika makinikia kisha kubainisha thamani ya madini hayo kwa kuzingatia bei katika soko la dunia. “Tulifuata taratibu za kisayansi katika kufanya uchunguzi wetu, katika baadhi ya makontena tuliyapakua yote na kukagua na mengine tulichimba mashimo sehemu ya chini, katikati na juu. “Tulichunguza utendaji wa TMAA na utaratibu mzima wa ufungaji sealed (lakiri) kabla ya kutoa vibali vya kusafirisha makontena,” alisema Profesa Mruma. MATOKEO YA UCHUNGUZI Kwa upande wa dhahabu, kamati hiyo ilibaini kuwapo kwa viwango vya juu ndani ya mchanga (makinikia) yaliyofanyiwa uchunguzi.  Katika makontena yote 277, madini ya dhahabu yalikuwa na uzito wa kati ya tani 7.8 na 13.16 zenye thamani ya kati ya Sh bilioni 676 na trilioni 1.147. “Taarifa tulizopata kutoka kwa wazalishaji pamoja na TMAA, zinaonyesha kuwa makinikia yana wastani wa tani 1.2 za dhahabu zenye thamani ya Sh bilioni 97.5. “Kutokana na tofauti hii kubwa kati ya viwango vya dhahabu vilivyopo kwenye taarifa za usafirishaji na vile ambavyo kamati imevibaini, ni dhahiri kuwa taifa linaibiwa sana kupitia usafirishaji wa makinikia nje ya nchi,” alisema Profesa Mruma. Alisema madini ya fedha yaliyopatikana katika makinikia hayo ni kati ya tani 1.7 na 1.9 ambazo zina thamani kati ya Sh bilioni 2.1 na bilioni 2.4.  Wazalishaji na TMAA walisema madini yaliyopo ni kilogramu 831 yenye thamani ya Sh bilioni 1.0.   Katika uchunguzi huo, madini ya shaba yalikuwa kati ya tani 1,440.4 na 1,871.4 ambayo yana thamani kati ya Sh bilioni 17.9 na bilioni 23.3. Nyaraka za usafirishaji zilizopatikana bandarini zilionyesha kuna tani 1,108 tu za shaba zenye thamani ya Sh bilioni 13.6.  Kamati pia ilichunguza shehena ya mbale za shaba ndani ya makontena matano yaliyozuiliwa bandarini na kubaini kulikuwa na viwango vya dhahabu hadi kufikia gramu 38.3 kwa tani viwango ambavyo havikuonyeshwa kwenye ripoti ya upimaji wa kimaabara wa TMAA. Profesa Mruma alisema kamati haikuonyeshwa mahala popote yanakopelekwa makinikia hayo na kubaini kuwa wanauziwa watu wengine na makampuni. MADINI MENGINE Katika uchunguzi huo, kamati hiyo ilibaini kuwapo kwa madini mengine ambayo thamani yake inakaribiana na dhahabu, lakini hayakuorodheshwa wala kujumuishwa kwenye ukokotoaji wa mrabaha. “Uchunguzi pia umeonesha kuwepo kwa madini mkakati (strategic metals) ambayo kwa sasa hivi yanahitajika sana duniani na yana thamani kubwa sambamba na thamani ya dhahabu.  “Pamoja na kuwa na thamani kubwa, lakini hayatumiki katika kukokotoa mrabaha, wanasema hawayahitaji. Lakini tulipoingia kwenye mtandao tuliona yanahitajika na huu ni upotevu wa mapato,” alisema Profesa Mruma. Aliyataja madini hayo kuwa ni iridium, rhodium, ytterbium, beryllium, tantalum na lithium. Profesa Mruma alisema thamani ya aina zote za Metali Mkakati katika makontena 277 yaliyoko bandarini, ni kati ya Sh bilioni 129.5 na bilioni 261.5. Alisema madini ya iridium ni wastani wa kilogramu 1,773 na 3,808.8 zenye thamani kati ya Sh bilioni 108 na 231. Rhodium ni kati ya kilogramu 9.4 na 21.6 zenye thamani kati ya Sh bilioni 0.7 na bilioni 1.5. Ytterbium ni kati ya kilogramu 1024.9 na 1,357.3 zenye thamani ya Sh bilioni 12.4 na bilioni 16.4. Beryllium ni kati ya tani 5.4 na 7.5 zenye thamani kati ya Sh bilioni 6.0 na bilioni 8.3. Tantalum ni kati ya kilogramu 3240.9 na 4,792 zenye thamani kati ya Sh bilioni 1.9 na bilioni 2.8. Lithium ni kati ya kilogramu 5,955.5 na 8,254.6 zenye thamani kati ya Sh bilioni 1.0 na bilioni 1.4.  “Kwa kuwa viwango hivi vya thamani havitumiki kukadiria mapato ya Serikali, ni wazi kuwa kuna upotevu mkubwa sana wa mapato kwa nchi yetu,” alisema Profesa Mruma. Pia alisema katika makinikia hayo kulikuwa na madini ya sulfur yenye uzito wa kati ya tani 2,161 na 2,825.4 ambayo yana thamani kati ya Sh bilioni 1.4 na bilioni 4.9. Madini ya chuma ni wastani wa tani 1,496 na 1,695 ambayo yana thamani kati ya Sh bilioni 2.3 na bilioni 2.6. “Kulikuwa na madini mengine kama Zinc, lakini thamani yake hazikuwa kubwa sana… hata haya madogo nashauri tusiyatupe,” alisema. UZITO WA MAKONTENA Profesa Mruma alisema walibaini makontena yalikuwa na uzito mkubwa wa tani 23.1 tofauti na ulioelezwa awali wa tani 20 kwa kila kontena. Alisema walipima makontena manne yaliyokuwa bandarini na kubaini kuwa yalikuwa na uzito wa ziada kati ya tani 3.1, 2.95, 2.7 na 2.2. “Hivyo basi, ongezeko hili la uzito linaongeza thamani ya makinikia na hivyo kuongeza upotevu zaidi wa mapato ya Serikali,” alisema Profesa Mruma. TMAA Ripoti hiyo ilibainisha kuwa TMAA haifungi utepe wa udhibiti mara baada ya kuchukua sampuli kwenye makontena na badala yake udhibiti hufanyika baada ya siku kadhaa katika hatua za mwisho za usafirishaji wa makontena.  “Hali hii inatoa mianya ya kufanyika udanganyifu, viwango na thamani ya makinikia baada ya uchukuzi wa sampuli. Mtu anaweza kutempa kwa kuongeza viwango vya makemikia au hata uzito,” alisema Profesa Mruma. MAPENDEKEZO Kamati hiyo ilipendekeza Serikali ichukue hatua kwa watendaji wa TMAA na wizara kutokana na kutosimamia vyema tathmini ya viwango halisi vya madini/metali mbalimbali vilivyopo katika makinikia na kuisababishia Serikali upotevu wa mapato. Pia ilipendekeza Serikali iendelee kusitisha usafirishwaji wa mchanga nje hadi mrabaha stahiki utakapolipwa serikalini kwa kuzingatia thamani halisi ya makinikia kama ilivyoainishwa kwenye uchunguzi huo.  “Ujenzi wa mashine ya kuchenjulia makinikia nchini ufanyike haraka iwezekanavyo. TMAA ifunge tepe kudhibiti udanganyifu unaoweza kutokea baada ya uchukuaji wa sampuli na ipime madini yote ambayo yamo ndani ya makinikia na kujua thamani yake bila kujali kilichoandikwa na msafirishaji,” alisema Profesa Mruma. Pia kamati ilipendekeza Serikali iweke mfumo wa kushtukiza kwa lengo la udhibiti na usafirishaji madini nje ya nchi. Kuhusu uwezo wa scanner inayotumika bandarini kukagua vilivyomo ndani ya makontena, Profesa Mruma alisema haina uwezo kwani inaonyesha umbo tu la shehena ya makinikia. “Tulichukua vipande vya chuma na kuweka kwenye kontena, lakini scanner haikuona kitu. Hivyo, mtu akiamua kuficha kitu kwenye makinikia scanner haziwezi kuona, Serikali itumie wataalamu wa mionzi kufunga scanner zitakazofanya kazi kwa usahihi,” alisema scanner.  
kitaifa
WAKALA wa Mabasi Yaendayo Haraka jijini Dar es Salaam (DART) imeanza kutekeleza maagizo matano kati ya sita ya Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo, aliyoyatoa hivi karibuni kuondoa kero wanazopata abiria wanaotumia usafi ri huo.Maagizo hayo ni Kampuni ya Mabasi yaendayo Haraka (UDART) kufanyia matengenezo mabasi yote mabovu na kuzuia magari na pikipiki binafsi kupita katika barabara inayotumiwa na mabasi hayo.Mengine ni kuchukua mabasi 10 yanayofanya safari Mbezi kwenda Kimara yabebe abiria wanaoanzia Kimara kwenda Kivukoni na Kariakoo, kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) kuongeza daladala za kawaida zinazotoka Mbezi kwenda Kawe na Makumbusho na kupeleka majina ya watendaji wa DART wanaohujumu mradi kwa Katibu Mkuu wa Tamisemi. Agizo la sita lilimhusu Mkurugenzi wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano wa Tamisemi kuhakikisha kuwa anashirikiana kwa karibu na Wakala wa Serikali Mtandao (eGA) na Wizara ya Fedha na Mipango, kurejesha matumizi ya kadi kwa abiria na kuondoa tiketi ambazo Waziri Jafo alisema zinapoteza mapato.Akizungumza na gazeti hili jana kwa simu, Mtendaji Mkuu wa DART, Ronald Lwakatare alisema tayari wametekeleza baadhi ya maagizo na kwa sehemu kubwa na wanatarajia kuyakamilisha ndani ya wakati. “Ingawa tulikuwa tumeanza kuruhusu baadhi ya mabasi ya Mbezi kwenda moja kwa moja Kariakoo kabla ya agizo la waziri, jana (juzi) tumeanza rasmi kupeleka mabasi 10, matano Kivukoni na matano Kariakoo, lakini tunaangalia uhitaji kwa kuwa si kila siku kunakuwa na watu wengi,” alisema Lwakatare.Alisema baadhi ya mabasi yametengenezwa na UDART na juzi Jumatatu kulikuwa na mabasi 115 barabarani kati ya 126 yanayopaswa kusafirisha abiria kwa siku kwa mujibu wa mkataba. Awali mabasi kati ya 90 mpaka 100 ndiyo pekee yalifanya kazi kwa siku kutokana na ubovu wa mabasi mengi. Alisema kuna baadhi ya vifaa vya mabasi hayo ambavyo havipo nchini vimeagizwa tayari nje ya nchi ili kukamilisha matengenezo ya magari yaliyobakia. Kwa mujibu wa Lwakatare, mabasi 30 hufanya safari za Kivukoni kila siku na kati ya hayo, 12 ni yasiyosimama katika vituo vya kati (express) na 18 ni ya kawaida.Kuhusu kumpelekea Katibu Mkuu Tamisemi majina ya watendaji wa DART walio chini yake wanaodaiwa kukwamisha utendaji kazi, alisema analifanyia kazi ili ndani ya siku saba awe amekamilisha. Usafiri wa mabasi yaendayo haraka umekuwa na usumbufu mkubwa kwa wananchi wanaoutumia kutokana na kushindwa kukidhi mahitaji ya wingi wa abiria hasa nyakati za asubuhi na jioni.Machi 13, mwaka huu, katika kituo cha mabasi hayo cha Kimara, vurugu ziliibuka baada ya abiria kukaa kituoni hapo kwa saa mbili wakisubiri abiria kutokana na DART kuondoa mabasi ya express barabarani. Hata hivyo, walikiri kosa na kuyarejesha, lakini bado kumekuwa na msongamano mkubwa wa abiria katika vituo vya mabasi hayo asubuhi na jioni na imeelezwa ni kutokana na mabasi mengi kuwa mabovu.
kitaifa
Mwandishi Wetu,Dar es Salaam ZAIDI ya wafanyabiashara 2000 katika mkoa wa kodi wa Ilala wamepatiwa elimu ya kodi inayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini.Mamlaka hiyo imekuwa na ikifanya kampeni ya elimu ya kodi mara kwa mara kwa kuwafata wafanyabiashara kwenye biashara zao (mlango kwa mlango). Akizungumzai zoezi hilo Afisa Msimamizi wa Kodi wa mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Zakeo Kowelo alisema kuwa katika siku sita za zoezi hilo, jumla ya wafanyabiashara 2,165 wamepatiwa elimu mbalimbali ya kodi. Alisema maeneo ambayo wamewafikia wafanyabiashara na kuwapatia elimu ni Tabata, Relini, Bima, Liwiti, Barakuda, Kimanga, Segerea, Kinyerezi, Kisiwani na Bonyokwa Mkoa wa Kodi wa Ilala. Alisema zoezi limeenda vizuri na kwamba wafanyabiashara wametoa ushirikiano wa kutosha kwa kutoa taarifa muhimu na kuonyesha nyaraka ambazo zilihitajika jambo ambalo limewawezesha kuwapa ushauri na elimu inayostahili. “Kwa hili tunawashukuru sana kwani tumeweza kuwaelimisha kama tulivyopanga”, alisema KoweloAlisema zoezi lilihusisha kupita duka kwa duka na kuangalia taarifa za wafanyabiashara za kodi ambapo baada ya kuangalia taarifa walifanya majadiliano na kumshauri mfanyabiashara jinsi ya kutunza kumbukumbu. Aliongeza kuwa kwa wale ambao hawajasajili biashara zao wameelekezwa taratibu za kusajili ili watambulike kuwa walipakodi na kwamba pamoja na kusajili biashara pia wafanyabiashara wameshauriwa jinsi ya kujisajili na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) na wale wanaostahili kutumia mashine za kodi za kielektroniki wamepewa utaratibu wa kupata na kuzitumia mashine hizo. “TRA ni sehemu ya biashara za wananchi hivyo lengo letu ni kuwaelimisha wananchi ili wafanye biashara kwa usalama zaidi na kutimiza wajibu wao wa kulipa kodi sahihi na kwa wakati’, alisema Kowelo. Naye Stewart Kimbaga mfanyabiashara wa duka la urembo maeneo ya Bonyokwa alisema kuwa kampeni hiyo ya elimu ya kodi ni nzuri na kwamba itasaidia kutokana na kuwa baadhi ya wafanyabiashara hawana uelewa wa jinsi ya kufanya biashara ikiwa ni pamoja na utaratibu mzima wa kulipa kodi. Alisema hiyo ni fursa muhimu na kwamba ukaguzi peke yake hautoshi bali unatakiwa uambatane na elimu ili kuwaongezea wananchi uelewa na kujenga uhusiano mzuri baina ya TRA na walipakodi. Zoezi la kutembelea walipakodi katika maeneo yao ya biashara ni mkakati ambao TRA inautekeleza ili kuwaelimisha walipakodi, kuwapa ushauri wa kitaalamu kuhusu taratibu za kulipa kodi, kusajili biashara ambazo hazijasajiliwa, kuwakumbusha kulipa kodi, kutatua changamoto zinazo wakabili na kupata maoni yao kuhusu huduma inayotolewa na TRA kwa ajili ya kuboresha utendaji wake.
uchumi
Beatrice Mosses, Manyara Wazee wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Kati Jimbo la Babati, Usharika wa Babati wamezuia ruzuku ya sadaka zinazopelekwa kwenye dayosisi na majimbo kwa madai kuwa Askofu wa Dayosisi hiyo, Dk Solomon Masangwa kukataa kumhamisha Mkuu wa Jimbo la Babati, Niiteel Panga. Sakata hilo lilianza Jumapili iliyopita na jana baada ya Francis Lazaro ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Matengenezo ya Kanisa, kuingilia katikati ya ibada bila ruhusa ya Mchungaji Godlsten Mkenda wa Usharika wa Babati, na kudai wamechoshwa na mienendo ya mkuu huyo wa jimbo. “Tulikubaliana mama ahamishwe lakini Novemba 2, mama akarudi Jimboni tukasema sawa tumuache akae kae ofisini, Novemba 6 tulikaa tukafanya kikao chetu cha tathmini kuwa mama amesharudi sasa tunafanyaje, tukakubaliana kwamba kwa kuwa amerudi na sisi hatuna haja ya kupigana nae cha msingi hapa ni kuanza kuzuia sadaka. “Mmemsikia mzee wa Kanisa alivyosema kwenye matangazo kuwa taarifa nyingine mtasikia baadae ni kwamba hakuna uwiano ulioenda usharikani, jimboni wala Dayosisi, sadaka zote za Jumapili iliyopita zipo kwenye akaunti ya mtaa kwa hiyo niwaombe sana leo tutoe sadaka kwa wingi maana zinaingia kwenye akaunti ya mtaa iliyopo Benki ya Posta na fedha zenu ziko salama kabisa,” amesema. Pamoja na mambo mengine amesema Novemba 13 walikaa kikao wakakubaliana lazima kuwe na maazimio na azimio la kwanza ni lazima mkuu wa jimbo ahamishwe, azimio jingine ni kuendelea kuchukua sadaka zote na kupeleka kwenye akaunti ya mtaa. “Azimio kama Dayosisi haitamuhamisha mkuu wa jimbo tutapeleka kesi mahakamani na tutamfungulia kesi ya udhalilishaji na tunazo ‘clip’ nne zilizosimama,” amesema Lazaro.
kitaifa
    LONDON, UINGEREZA Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Uingereza, Boris Johnson, ameendeleza mashambulizi yake jana dhidi ya Serikali ya Waziri Mkuu Theresa May, akitabiri ushindi kwa Umoja wa Ulaya (EU) katika mazungumzo kuhusu kujitoa kwa Uingereza katika umoja huo maarufu kama Brexit. Tangu alipojiuzulu wadhifa wake wa uwaziri wa mambo ya nje Julai mwaka huu, Johnson amekuwa akiandika makala katika gazeti la Daily Telegraph akiikosoa Serikali ya May namna inavyoshughulika na mchakato wa kujiondoa Brexit. Johnson ambaye alikuwa mstari wa mbele wakati wa kampeni ya kura ya maoni kuhusu Brexit na baadaye kushika wadhifa wa uwaziri wa mambo ya nje wakati Uingereza ilipoanza mazungumzo kuhusu mchakato huo, alisema anahofia matokeo yasiyoepukika kuhusu mchakato huo yatakuwa ni ushindi kwa EU. Mpango wa May pamoja na mambo mengine ni kuiondoa Uingereza kutoka soko la pamoja baada ya hatua ya Brexit, lakini akitaka ibakie katika biashara huru kwa baadhi ya bidhaa kupitia makubaliano yanayohusu ushuru wa forodha na taratibu nyingine kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya. Hata hivyo, Jonson na kundi lake wanaupinga mpango huo wa May wakisema unaifanya Uingereza kuendelea kuwa karibu zaidi na EU hata baada ya kujiondoa kwenye umoja huo Machi mwakani.      
kimataifa
Na Mwandishi wetu, Mbeya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imewataka wafanyabiashara ambao hawajakadiriwa Kodi ya mapato kwa kipindi kinachoishia Marchi 31, mwaka huu kufika katika ofisi za mamlaka hiyo kukadiriwa na kulipa Kodi zao kabla ya Juni 30,2020. Hayo yamezungumzwa leo jijini Mbeya na Kaimu Meneja wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Stephen Kauzeni ambaye amewahimiza hayo wakati wa kampeni ya uhamasishaji wa ulipaji kodi inayoendelea mkoani humo. Aidha amewakumbusha wafanyabiashara wote ambao mwaka wao wa mahesabu unaishia Desemba 31,2019  kuwasilisha ritani zao TRA kabla ya mwisho wa mwezi huu. Amesema kwa upande wa wafanyabiashara wanaolipa kwa awamu lakini bado hawajakadiriwa kodi zao ni vyema wakafika TRA ili wakadiriwe na walipe mapema kabla ya tarehe ya mwisho ili kuepuka adhabu na riba. “Tunawatembelea wafanyabiashara kwenye maeneo yao ya biashara ili kuwakumbusha na  kuwahimiza wale ambao bado hawajafanyiwa makadirio, wakakadiriwe na wawahi kulipa kodi zao kwa wakati bila bughudha kuliko kusubiri siku ya mwisho kabisa”, amesema. Kauzeni ameongeza kuwa, kutokana na janga la ugonjwa wa korona, TRA isingependa kuona msongamano wa watu katika ofisi zake na kwamba imewalazimu maofisa wake kuwafuata walipakodi  kwenye maeneo ya biashara zao ili kuwapa elimu ya kodi na kuwasisitiza wakailipe kwa. “Ni wajibu wa mlipakodi kulipa kodi zake kwa wakati lakini pia TRA ina wajibu wa kutoa elimu pamoja na  kumkumbusha mlipakodi kulipa kodi na ndiyo maana tumewafuata huku madukani kwao kuwapatia elimu na kuwahimiza kulipa kodi kwa wakati,’’ amesema Kauzeni. Amesema kwa wafanyabiashara ambao mwaka wao wa hesabu unaishia Desemba 31, 2019 wanatakiwa kuhakikisha wanawasilisha ritani zao kabla au Juni 30, 2020 ili ritani zao ziweze kuhakikiwa na kufanyiwa kazi kwa wakati kwa mujibu wa sheria za kodi zinavyoelekeza.  “Niwasihi walipakodi wafuate sheria ya Usimamizi wa kodi na kuwasilisha ritani zao ziweze kufanyiwa kazi mapema”, amesisitiza Kauzeni. Kauzeni amesema kampeni hii ya uhamasishaji ulipaji kodi kabla ya Juni 30, 2020 inalenga kuwakumbusha walipakodi kulipa kodi zao kwa wakati pamoja na kuongeza hamasa ya ulipaji kodi kwa hiyari miongoni mwa wafanyabiashara na watoa huduma zinazolipiwa kodi kama vile mawakili, wahasibu na fani zingine zilizosajliwa. Amesema kampeni hii ya utoaji elimu na uhamasishaji ulipaji kodi kwa wakati na hiyari inaendelea katika mkoa wa Mbeya na wilaya zake.
uchumi
Na TIMOTHY ITEMBE WANACHAMA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya Tarime   wameonywa kuacha tabia ya kuwachafua  wagombea wenzao katika mitandao ya  jamii katika kipindi hiki cha uchaguzi wa ndani wa chama. Onyo hilo lilitolewa  na Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamis Mukaruka ambaye alisema watakaobainika kujihusisha na tabia hiyo hatua za  nidhamu zitachukuliwa dhidi yao. “Chama hakitawavumilia wanachama na wagombea au wanachama wowote ambao wanatumia njia ya kuwachafua wenzao wanaogombea kwenye mitandao ya  jamii. “Niseme kwa sasa tuko makini na watakaobainika watachukuliwa hatua za  nidhamu,” alisema. Aliwataka wanachama waliokisaliti chama wakati wa uchaguzi mkuu   wa mwaka 2015 kutopoteza muda wao kwa kugombea nafasi za uongozi kwa kuwa wataenguliwa. Katibu wa Jumuiya ya Wazazi ya CCM Wilaya ya Tarime, Mathias Lugola aliwasihi wanachama kuendelea kujitokeza kuwania nafasi za uongozi wa jumuiya hiyo. Nafasi hizo ni mwenyekiti, katibu wa siasa na uenezi, wajumbe wa halmasghauri kuu ya wilaya nafasi 10, wajumbe wa mkutano mkuu wa taifa nafasi tatu na wajumbe wa mkutano mkuu mkoa nafasi tano.
kitaifa
KLABU ya Usalama Barabarani ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge jijini Dar es Salaaam, imetoa elimu ya usalama wa barabarani kwa madereva wa magari na bodaboda kuzingatia sheria za usalama barabarani haswa vivuko vya watembea kwa miguu ili kuepusha ajali na vifo.Wanafunzi hao zaidi ya 20 walikuwa wakitoa elimu kwa madereva hao jana jijini Dar es Salaam waliokuwa wakiweka mafuta katika Kituo cha Mafuta cha Puma kilichopo Upanga jijini humo. Akizungumza wakati wa utoaji elimu kwa madereva, Rosenice Senyandumi ambaye ni mwanafunzi wa shule hiyo, alisema ajali za barabarani zimekuwa zikikatisha uhai wa binadamu wasio na hatia wakiwemo wanafunzi na mara nyingi huchangiwa na madereva wazembe.“Ajali za barabarani zinapunguza nguvu kazi ya Taifa na kuathiri watoto kwa kuwa wengi hupoteza wategemezi wao na wakati mwingine watoto wenyewe kupoteza maisha au kupata ulemavu wa kudumu kutokana na ajali,” alisema Senyandumi. Alisema kutokana na athari na madhara mbalimbali yanayotokana na ajali, walipatiwa mafunzo na wadau mbalimbali kuhusu usalama barabarani kwa ufadhili wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania. “Tunawaomba madereva wote mzingatie sheria za usalama barabarani, tunajua nyie ni wazazi wetu, kaka zetu na dada zetu... naamini sote tukichukua hatua tatizo la ajali zinazogharimu maisha ya watanzania wasio na hatia litakuwa ni historia nchini kwetu,” alisema mwanafunzi huyo.Kwa upande wake, Kassim Juma ambaye ni dereva aliyepatiwa elimu ya usalama wa barabarani, alisema wanafunzi hao wameonesha uzalendo na wanapaswa kuungwa mkono ili kuwafikia madereva wengi zaidi na kuwapatia elimu ya usalama wa barabarani. “Nawapongeza hata walioanzisha wazo la kuwawezesha wanafunzi hawa kutoa elimu kwa kuwa tunafahamu kwamba misingi bora ya elimu huanzia chini, hivyo watoto hawa watakuwa ni mabalozi bora wa vizazi vijavyo,” alisema Juma.Mapema, Meneja Mkuu wa Kampuni ya Mafuta ya Puma Tanzania, Dominic Dhanah alisema kampuni hiyo imedhamiria kuhakikisha inashiriki kikamilifu katika masuala ya usalama barabarani ili kudhibiti ajali.
kitaifa
NA MWANDISHI WETU, SONGEA MSANII Ruby na kundi la Weusi, wameacha mjadala wa nguvu mjini Songea baada ya juzi kushusha burudani ya nguvu katika tamasha la Tigo Fiesta Vibe Kama Lote, lililofanyika Uwanja wa Majimaji mkoani humo. Kabla ya kuingia mkoani humo, tamasha hilo lililoanzia Mkoa wa Morogoro kabla ya kwenda mikoa ya Rukwa, Iringa, Songea, wakati leo litatimua vumbi katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara. Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Christina Mndeme, ambaye aliongozana na Mkuu wa Wilaya ya Songea Mjini, Pololite Mgema, ndiye aliyefungua tamasha hilo. Mkuu huyo wa mkoa aliishukuru Kampuni ya Tigo na Clouds Media kwa kulipeleka tamasha hilo kubwa. “Hii si kwa burudani pekee, bali ni fursa kwa wakazi wa mkoa huu kwa kuwa umewawezesha kuongezea kipato kipindi hiki chote cha wiki nzima. “Niwapongeze tena Tigo na Clouds Media, nakuwaomba mwakani msiache kuja tena mkoa wetu,” alisema Christina. Kwa upande wa burudani, ilianza kwa kumsaka mshindi wa shindano la kusaka vipaji la Tigo Supa Nyota, ambapo msanii Single Baba aliibuka kidedea hivyo ataiwakilisha Ruvuma kwenye fainali zitakazofanyika jijini Dar es Salaam mwezi ujao. Shoo rasmi ilianza kwa msanii, Mesen Selekta, kufuatiwa na Rubby. Rubby miaka kadhaa nyuma aliibuliwa kupitia shindano la Supa Nyota, aliteka hisia za mashabiki kupitia nyimbo tofauti tofauti zikiwemo Niwaze, Ntade, Na Yule, Forever na nyingine. Wasanii 12 walipanda jukwaani katika tamasha la Songea na kuwarusha vilivyo mashabiki wa muziki akiwemo Rostam, Weusi, Ruby, Mr. Blue, Barnaba, Zayd, Fid Q, Masen Selekta, Lulu Diva, Chege, Fobya.   Wasanii hao pia ndio watakaotoa burudani leo katika Uwanja wa  Nangw’anda Sijaona, Mtwara. Mdhamini mkuu wa msimu huu, Kampuni ya Tigo imewakumbusha mashabiki wote wa muziki mjini Songea kufurahia promosheni zake katika msimu huu wa vibes. Data Kama Lote inawapa wateja hadi mara mbili ya vifurushi vya intaneti watakavyonunua kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*0#. Hii itawawezesha wateja wa Tigo kufurahia msimu huu wa vibes kupitia mtandao wa kasi ya juu zaidi wa Tigo 4G+.   Tigo pia inatoa punguzo kubwa la bei kwa tiketi za tamasha la Tigo Fiesta 2018 zitakazonunuliwa kupitia Tigo Pesa Masterpass QR. Tiketi zitakazonunuliwa kwa mfumo wa TigoPesa Masterpass QR zitagharimu Sh 5,000, badala ya Sh 7,000 kwa watakaonunua kwa pesa taslimu. Wateja wanapaswa kupiga *150*01#  na kuchagua 5 (lipia huduma) kisha kuchagua namba 2 (lipa Master pass QR) na kutuma kiasi husika kwenda namba ya Tigo Fiesta 78888888.   Wateja wa Tigo pia watapata faida zaidi kupitia shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo Trivia linalotoa zawadi za kila siku za Sh 100,000, zawadi za kila wiki za Sh milioni moja, simu janja za mkononi zenye thamani ya Sh 500,000 kila moja pamoja na donge nono la Sh milioni 10 kwa mshindi wa jumla. Kushiriki wateja wanapaswa kutuma neno MUZIKI kwenda 15571 au kutembelea tovuti ya  http://tigofiesta.co.tz nakuchagua Trivia. Huu ni mwaka wa 17 wa tamasha la muziki na kitamaduni la Tigo Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote ambapo mwaka huu kwa asimilia 100 wasanii wa nyumbani watakaozuru mikoa 15 ikiwemo; Morogoro, Sumbawanga, Iringa, Singida, Songea, Mtwara, Moshi, Tanga, Muleba, Kahama, Mwanza, Musoma, Arusha na Dodoma, huku kilele kikifanyika Dar es Salaam.
burudani
Na Bakari Kimwanga-DODOMA WABUNGE wamegomea hatua ya Serikali kutaka kusimamia posho na marupurupu yao, huku wakitaka suala hilo waendelee kujipangia wenyewe. Msimamo huo uliotolewa na Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, umetolewa  baada ya Serikali kuwasilishwa Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali namba tatu ya mwaka 2016. Awali Serikali ilitaka suala la stahiki hizo kwa watumishi wa umma liamuliwe na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora. Akisoma maoni ya Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, Mohammed Mchengerwa, alisema wametoa pendekezo hilo katika  Sheria ya Utumishi wa Umma sura 298    kulinda dhana  ya mgawanyo wa madaraka. “Tume ya Utumishi wa Bunge na Tume ya Utumishi wa Mahakama zipewe uhuru  kusimamia upangaji wa mishahara, posho na marupurupu mengine,” alisema. Akizungumzia mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu, alisema kifungu cha 18 cha Muswada huo kuhusu muda wa mnufaika   kurejesha mkopo, Mchengerwa alisema kamati inashauri mkopo uwe mwaka mmoja baada ya kumaliza masomo. Alisema hali hiyo itasaidia kutoa fursa kwa mnufaika kuanza kulipa mkopo wake,   utaratibu ambao hutumika katika nchi nyingine kama Kenya na Zambia. “Kuhusu wanufaika waliojiajiri kamati inapendekeza kiwango cha kurejesha mkopo kisipungue Sh 100,000 badala ya Sh 120,000 kama Serikali ilivyopendekeza,” alisema Mchengerwa. Awali, akiwasilisha hotuba ya mabadiliko ya sheria hiyo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), George Masaju, alisema   kifungu cha 8 cha Sheria hiyo kinaanisha mamlaka ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais (Utumishi) kuwa ni pamoja na kufanya uchunguzi kwa ajili ya kuendeleza ufanisi wa utumishi wa umma. Alisema Ibara 24 ya Muswada huo inapendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A cha Sheria kinachoweka masharti kuwa Taasisi, Wakala au Tume za Serikali hazitakuwa na mamlaka ya kuidhinisha mishahara na marupurupu kwa watumishi wa taasisi hizo na badala yake kibali kwa ajili hiyo kitatolewa na Katibu Mkuu,Ofisi ya Rais (Utumishi). “Marekebisho hayo yanalenga kuwa na mamlaka moja inayoratibu mishahara, posho na marupurupu na watumishi katika taasisi za Serikali na pia kuwianisha mishahara posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa taasisi hizo. “Masharti yaliyopendekezwa hayatatumika. Ibara hiyo imefutwa na kuandikwa upya masharti yanayopendekezwa hayatatumika kwa mishahara, marupurupu na masilahi mengine kwa Bunge,Mahakama, Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ),Polisi,Magereza,JKT, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji na Idara ya Usalama wa Taifa ili utaratibu huo kuendelea kama ilivyo sasa katika sheria zinazosimamia taasisi hizo. “Kifungu cha 20 (1) (c) cha Sheria ya Utumishi wa umma kinaipa Tume ya Utumishi wa Umma mamlaka ya kutunga kanuni kuhusu usaili wa watumishi wa umma unaofanywa na tume hiyo,” alisema Masaju Awali kifungu cha 8 kilikuwa kinapendekeza kufanyiwa  marekebisho  kumpa mamlaka Katibu Mkuu (Utumishi) kurekebisha na kuwianisha  mishahara, posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma wakiwamo   wabunge na idara ya mahakama. Huku ikipendekeza kuongeza kifungu kipya cha 9A kinachozizuia taasisi za umma, wakala, bodi na tume zisirekebishe au kuwianisha mishahara, posho na marupurupu mengine  kwa watumishi. Sehemu ya tano inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura ya 298 kwa lengo la kutoa tafsiri ya neno “recruitment secretariat”, maneno hayo yametumika katika Sheria lakini hayakuwa yamepewa tafsiri. Kiama kwa waajiri Alisema Ibara ya 19 ya Muswada huo, inapendekeza kufuta kifungu cha 20 na 21,ambacho kilikuwa kinaeleza kwa kuwa si rahisi mwajiri kufahamu kama mtumishi anayeajiriwa ni mnufaika wa mkopo. Kutokana na hali hiyo,alisema Muswada unaainisha kuwa mwajiri atatakiwa kuifahamisha Bodi ya Mikopo ndani ya siku 28,baada ya mwajiriwa huyo mwenye Shahada au Astashahada ili bodi  iangalie kama mwajiriwa huyo ni mnufaika wa mikopo. “Mwajiri ambaye atashindwa kutekeleza masharti ya kifungu hicho atakuwa anatenda kosa la jinai ambalo adhabu yake ni Sh milioni moja au kifungo cha miezi sita gerezani. Pia inapendekezwa baada ya mnufaika wa mkopo mwajiri atatakiwa kukata asilimia 15 ya mshahara wa mwajiriwa. “Bodi au mawakala wake wawe na mamlaka ya kukagua kumbukumbuku za waajiriwa kwa lengo la kufuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo pamoja na kumbukumbu za  waajiriwa kwa lengo la kutafuta taarifa zinazohusiana na wanufaika wa mkopo kwa hatua zao muhimu kuhusu makusanyo wa mikopo,” alisema AG Masaju alisema kifungu cha 57 cha sheria hiyo, kinaweka masharti kuhusu zuio kwa shughuli za binadamu zinzoathiri ulinzi wa bahari, mito, mabwawa zisifanyike ndani ya mita 60 kutoka kingo za bahari, mito au mabwawa. Alisema hatua hiyo imekusudiwa kuimarisha ulinzi na usalama wa mazingira ya maeneo husika ya bahari, maziwa na mito na mabwawa. “Ibara ya 11 ya Muswada inapendekeza kifungu hicho kirekebishwe katika kifungu kidogo cha pili   kuweka mwongozo wa namna ya kupima mita 60 ambako shughuli za  binadamu zimezuiliwa kufanyika. “Kifungu cha 184 kinaeleza athari na uthamini wa mazingira. Ibara ya 12 inapendekeza kuwa kitendo cha mtu yeyote kushindwa au kukataa kufanya tathimini ya athari za Mazingira kwa mradi unaohitaji tathmini hiyo kufanyika ni kosa la jinai ambalo adhabu yake ni faini isiyopungua Sh milioni tano na isiyozidi Sh bilioni moja au kifungo kisichopungua miaka miwili,” alisema.
kitaifa
KWA mujibu wa katiba yetu, Tanzania ni nchi ya vyama vingi. Lakini swali ni je, tunao upinzani makini na wa kweli kwa ajili ya maendeleo ya taifa? Kama walivyowahi kusema wenye kusema kwamba bila kuwepo kwa Yanga imara, hakutakuwa na Simba imara, vivyo hivyo naamini bila ya kuwepo kwa upinzani makini, hakutakuwa na CCM imara na makini.Tunapoiangalia CCM ambayo inaweza kuendelea kutawala nchi yetu hatuishii kwa hii inayoongozwa na Rais John Magufuli bali pia itakayokuwepo baada ya muda wake wa uongozi kumalizika.Imethibitishwa pasipo shaka kwamba katika nchi zenye upinzani legelege, husababisha vyama tawala kubweteka kwa kukosa changamoto, hivyo upinzani makini, imara na wa ukweli ni muhimu kwa maendeleo ya taifa.Kazi ya upinzani makini na wa kweli ni kukosoa kwa hoja mbadala na zenye mashiko na sio kupinga tu alimradi unapinga. Upinzani makini unapinga kwa kutumia nguvu ya hoja ili kutoa changamoto kwa chama tawala na sio hoja za nguvu. Upinzani wetu hapa Tanzania, ukiondoa vyama vichache ambavyo angalau vinaweza kutoa hoja zenye mashiko zikiambatana na takwimu au ushahidi, unabwabwaja bila ya kuwa na hoja mbadala za kushindanisha na hoja za serikali. Ni kwa mantiki hiyo unaonekana kama upinzani wa kupiga kelele zaidi na matokeo yake ni kuwa na upinzani uchwara usiotimiza majukumu ya upinzani makini. Kutokana na kasi ya Rais Magufuli, uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu wa 2020, kuna hatari kubwa ya upinzani kufutika na hivyo CCM kubakia peke yake, hali inayoweza kukifanya chama hicho kubweteka kwa kukosa changamoto. Ni vyema pia kujiuliza kwa nini upinzani unashindwa sana katika chaguzi mbalimbali za awamu hii ya Rais Magufuli? Je, inawezekana kushindwa kwa upinzani ni kutokana na kisingizio cha kuzuiliwa kwa mikutano ya kisiasa na maandamano, au ni ulegelege wao katika kutoa hoja mbadala ndio umewafikisha hapo. Kumbuka tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu 2015 hadi sasa kumefanyika chaguzi ndogo kwa zaidi ya majimbo 10, na CCM imeshinda majimbo yote.Ikumbukwe hata kama wamezuiliwa kuendesha siasa za mitaani za kila siku lakini wanashiriki kwenye chaguzi mbalimbali zinazowapa jukwaa la kusema, wanafanya mikutano ya ndani, wako bungeni na wanatoa taarifa kwenye vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kama kawaida.Wabunge pia hawazuiliwi kufanya mikutano halali kwenye majimbo yao. Ulegelege ninaousema hapa ni upinzani kuendesha siasa rahisi za matukio, badala ya siasa za hoja na hivyo kufuatia utendaji uliotukuka wa Rais Magufuli na awamu yake ya tano katika baadhi ya maeneo, wapinzani wamejikuta wakimkubali Rais kutokana na utendaji wake na hivyo kuamua kujiunga na CCM ambako wanaamini watamauunga mkono vyema zaidi katika juhudi zake.Wapinzani waliozoea kusubiri viongozi wa chama tawala wakosee, yakiwemo makosa ya kibinadamu, ili wapate cha kusema wamekosa cha maana cha kusema na hivyo kujikuta wakipinga hata yale ambayo huko nyuma waliyapigia kelele na kutaka serikali iyafanye. Yaani hata kiwe ni kitu kizuri vipi kimefanywa wao watapinga tu na wakikosa kabisa kitu cha kupinga, watalazimisha kukitafutia kasoro kitu kizuri! Je, upinzani makini na wa kweli ni upi na unatakiwa kufanya nini? Upinzani legelege na uchwara ni upi na unafanya nini? Je, kwa nini kasi ya Rais Magufuli itaua upinzani huu uchwara na kuimarisha upinzani makini? Kadri ya maoni yangu ni vyema tujue kwamba takwimu zilizopo zinaonesha kuwa Tanzania tuna vyama 21 vya siasa vyenye usajili wa kudumu.Lengo kuu la chama chochote cha siasa, ni kushika dola na kuongoza serikali, yaani kutawala. Kila chama kinaandaa ilani yake ya uchaguzi kwa kueleza iwapo wananchi watakipa ridhaa ya kutawala, kupitia uchaguzi huru, na wa haki, kitafanya hivi na vile katika maeneo haya na yale. Vyama vinashindanisha sera kwa kuzinadi ilani zao kwa wananchi kupitia kampeni za uchaguzi, kura zinapigwa, chama kilichoshinda ndicho kinaunda serikali na kuongoza kwa kuitekeleza ilani yake iliyopewa ridhaa na wananchi, hivyo chama kilichoshinda kinakuwa ni chama tawala na vyama vilivyoshindwa kwenye urais vinakuwa ni vyama vya upinzani (wengine wanaita vyama vya ukinzani).Vyama hivi vimeshindwa kwa sababu ilani zake zimekataliwa kitaifa, lakini kuna maeneo katika ubunge, udiwani na serikali za mtaa vimekuwa vikishinda, hivyo baadhi ya vyama hivi kuongoza halmashauri, kata au mtaa kwa kutumia ilani zao. Hata hivyo, katika muktadha wa kushindwa kuunda serikali vinatakiwa kushirikiana na serikali ya chama tawala kuongoza kata au mitaa walioshinda. Baada ya uchaguzi, kazi ya upinzani makini duniani kote ni kupinga sera za chama tawala kwa hoja mbadala na sio kupinga tu alimradi kupinga kama ilivyo hapa kwetu. Kati ya vyama vyote zaidi ya 20 vilivyosajiliwa, ukitazama vyama vinavyofanya siasa za kila siku na vile vyenye wabunge, madiwani na viongozi katika serikali za mitaa na havizidi vitano, ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, NCCR Mageuzi, na ACT Wazalendo. Vyama kama TLP na UDP vimebaki kuwa vyama watu, na vingine vilivyobaki ni vyama majina tukutokana na kuwa usajili lakini havionekani kwenye siaza za kila siku isipokuwa wakati wa uchaguzi tu.Kulegalega kwa upinzani na kukosa mbinu na sera mbadala kuimeifanya CCM hii ya Magufuli inayojitahidi kuleta mabadiliko nchini kuwa chama imara zaidi na sasa itamchukua mtu makini kuviamini ili kuvikabidhi nchi. Tuchukulie hoja moja kuu ya vita dhidi ya adui ujinga, umasikini na maradhi. CCM alitangaza kutoa elimu bure tangu darasa la kwanza hadi kidato cha nne na kwamba kwa upande wa alimu ya juu, itatoa mikopo. Ukawa wakaja na elimu bure kuanzia chekechea hadi chuo kikuu kwa maana ya kwamba wangefuta hata bodi ya mikopo! Lakini ni CCM iliposhinda, inatoa elimu bure hadi kidato cha nne na pia inatoa mikopo ya elimu ya juu. Kwa kifupi inatekeleza ahadi yake sawia. Baada ya uchaguzi ilitegemewa upinzani ujenge hoja mbadala hata kupitia bungeni ukieleza kwa hoja za kisayansi na kitakwimu namna ambavyo ingewezekana kutoka elimu bure hadi chuo kikuu. Ikifika 2020, CCM itapanda majukwaani kueleza mafanikio ya elimu bure na idadi ya wafaidika wa mikopo lakini sioni upinzani utakaokuja na maelezo ya kisayansi namna ambavyo wao wangeweza kutoa elimu bure katika ngazi hizo bila mkopo. Kabla sijaendelea nimeona niwatake radhi wapinzani waliokwazika kwa kutumia hili neno ‘upinzani uchwara’. Neno hili siyo langu bali lilianza kutumiwa na mmoja wa viongozi wenyewe wa upinzani! Ilikuwa ni kwenye mjadala fulani uliokuwa ukirushwa na kituo cha Star Tv kuhusu kasi ya Rais Magufuli kwenye kupambana na rushwa, uzembe na ufisadi ambapo wageni waalikwa walikuwa ni Renatus Mkinga na Profesa Kitila Mkumbo, enzi hizo akiwa mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kiongozi wa upinzani kupitia chama cha ACT-Wazalendo. Profesa Kitila aliuita upinzani wa Tanzania kuwa ni uchwara na kwamba umekuwa ukiendeshwa na siasa za matukio kwa kupigia kelele rushwa, na ufisadi tu. Profesa huyo akatabiri kwamba katika awamu hii ya Magufuli kadri anavyoiona, tabia ya upinzani kusubiri kufanyia kazi makosa ya CCM na kupinga kila kitu utapwaya sana kwani watafilisiwa (preemptied) na kukosa cha kusema na hasa kama Magufuli atafanikiwa kukomesha rushwa na ufisadi ambayo ndiyo ilikuwa ajenda kubwa ya upinzani! Naomba nihitimishe mada hii kwa kwa maswali yangu ya mwanzo.Je, upinzani uliopo Tanzania ni upinzani makini, na wa kweli au ni upinzani legelege yaani uchwara usio na hoja mbadala? Upinzani wa aina hii, utatufikisha wapi? Je, utendaji uliotukuka wa Rais Magufuli utaua upinzani huu uchwara uliopo na kuibua upinzani makini wa kweli au utaleta ombwe la upinzani kwa kuirudishwa Tanzania kuwa mithili ya nchi ya chama kimoja? Mimi ninaamini, bili kuwepo kwa upinzani makini, hakutakuwa na CCM imara. Kama ndivyo, nini kifanyike ili tupate upinzani imara utakaoleta changamoto kwa CCM ili isibweteke kwani hilo ni jambo jema? Mwandishi wa makala haya ni mchangiaji wa gazeti hili. Anapatikana kwa namba 0754 270403, au pascomayalla@gmail.com
kitaifa
Na MWANDISHI WETU, MANYARA WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amewataka wananchi kuacha tabia ya kuhifadhi fedha nyingi majumbani na badala yake wajenge utamaduni wa kuzipeleka benki. Waziri Mkuu Majaliwa ametoa ushauri huo jana wakati akifungua tawi la Benki ya Biashara ya Uchumi lililopo wilayani Karatu, mkoani Arusha akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani hapa. “Tabia ya baadhi ya wananchi kuhifadhi kiasi kikubwa cha fedha majumbani si nzuri kwa sababu wanahatarisha usalama wao. Hivyo basi, ni vema wakatumia benki mbalimbali zilizoko kwenye maeneo yao kwa ajili ya kutunza fedha zao,” alisema Waziri Mkuu. Akizungumzia kufunguliwa kwa tawi la benki hiyo wilayani Karatu, Waziri Mkuu alisema unaashiria ukuaji wa uchumi wa wilaya hiyo kwa kuwa benki ni kichocheo cha maendeleo. Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu aliushauri uongozi wa benki hiyo kuangalia uwezekano wa kupunguza kiasi cha riba wanachokitoza katika mikopo wanayoitoa ili kuwawezesha wananchi kukopa na kupata faida. Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo,Wilson Ndesanjo, alisema benki hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mtaji mdogo, jambo linalowasababisha washindwe kufungua matawi katika mikoa mingine. “Changamoto nyingine ni baadhi ya wateja kushindwa kurejesha mikopo kwa wakati, ambapo hatua za kisheria zikichukuliwa wanakimbilia mahakamani.
kitaifa
Juhudi za karibuni kuimarisha uhusiano huo, zimeshuhudiwa wiki hii ambapo wawakilishi wa wafanyabiashara kutoka nchi hiyo kubwa kiuchumi Afrika walitembelea nchini kwa mazungumzo zaidi.Ujumbe huo ulihudhuria semina kuhusu biashara kati ya nchi hizo iliyofanyika juzi jijini Dar es Salaam, ambayo ilitayarishwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kwa kushirikiana na Ofisi ya Ubalozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini.Akizungumza na waandishi wa habari baada ya semina hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Juliet Kairuki, alisema mazungumzo yao yalilenga kuangalia namna nchi hizo zitakavyofaidika kwa kuboresha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji.Wawekezaji hao kutoka Afrika Kusini, wameonesha nia ya kuwekeza kwenye sekta ya kilimo na kuchagua mikoa ya Mwanza na Morogoro kama maeneo ambayo wangependa kuwekeza.Semina ya biashara ya wiki hii ni matunda ya Kongamano la Uwekezaji Kanda ya Ziwa lililofanyika mkoani Mwanza Februari mwaka huu.Baada ya kongamano hilo, Balozi wa Afrika Kusini hapa nchini, Thanduyise Chilliza ambaye alichukua hatua na kuwa mjumbe wa kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana Tanzania kwa wawekezaji katika nchi yake.Kairuki alisema kwa kushirikiana na Afrika Kusini, Tanzania itafaidika na teknolojia mpya, masoko, uongozi na usimamizi wa miradi mikubwa ya kilimo miongoni mwa faida nyingine.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Joel Bendera alisema amejifunza mengi katika semina hiyo.“Tumejifunza mengi kutoka kwa hawa wenzetu wa Afrika Kusini hasa katika masuala ya kilimo cha mboga na viungo,” alisema Mkuu wa Mkoa.Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini, Radhia Msuya, alisifu semina hiyo na kusema TIC imefanya kazi nzuri. “Semina hii imetufungua macho katika mambo mbalimbali,” alisema.Meneja Mtendaji, Export Development and Promotion, Trade and Investment KwaZulu Natal, Lester Bouah alisema ni kwa kushirikiana pamoja ndipo fursa zitapatikana na maendeleo ya kweli kufikiwa.
uchumi
HABARI ZOTE Na WINFRIDA NGONYANI-DAR ES SALAAM KATIBU Mkuu wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Filbert Bayi, amesema kanuni zinamruhusu kugombea tena uongozi katika kamati hiyo. Bayi ametoa kauli hiyo kutokana na baadhi ya wadau wa michezo nchini kudai kuwa anang’ang’ania madaraka, kwani ameiongoza kamati hiyo kwa muda mrefu. Katibu huyo bado hajaweka wazi kama atagombea kutetea nafasi yake katika uchaguzi mkuu ujao ambao umepangwa kufanyika Desemba 10, mwaka huu mjini Dodoma. Alisema akiamua atagombea kwani kanuni za Kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC),  zinaeleza kuwa mwisho wa ukomo wa mgombea ni miaka 70 ambayo bado hajaifikisha. “Umri wangu unaniruhusu kugombea tena kama nitataka kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za IOC, lakini ninaamini kabla sijafika huko nitawapa nafasi wengine,” alisema. Akizungumzia uchaguzi ujao wa TOC,   mwanariadha huyo wa zamani aliwataka wadau wa michezo kujitokeza kwa wingi kugombea nafasi mbalimbali ili waweze kutoa michango yao kwenye kamati hiyo. Fomu za kuwania uongozi zitaanza kutolewa kesho katika ofisi za TOC upande wa Tanzania Bara na visiwani, ambapo gharama kwa nafasi ya Rais, Makamu wake, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina Mkuu na msaidizi wake ni Sh 200,000 na wajumbe ni Sh 150,000. Sifa za mgombea ni kuwa raia wa Tanzania anayekubalika kwenye jamii na mwenye uzoefu katika uongozi wa michezo kitaifa na kimataifa.
michezo
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam mbele ya Jaji Dyansobela katika shauri No. 28/2017 leo tarehe 31/03/2017 imetoa amri dhidi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi kumzuia Prof Lipumba kutoa fedha za Ruzuku ya  Chama cha Wananchi- CUF mpaka shauri namba 21/2017 dhidi ya Msajili na Mwanasheria  Mkuu wa Serikali kuhusu kutoa fedha za ruzuku shilingi milioni 369 kwa njia za wizi na udanganyifu litakaposikilizwa na kutolewa maamuzi.  Amri hiyo ya Mahakama Kuu imekuja baada ya Jopo la Mawakili wa Chama wanaoiwakilisha Bodi ya Wadhamini ya CUF ambao ni Mhe. Juma Nassor, Mhe Daimu Halfani na Hashim Mziray kuwasilisha maombi hayo mbele ya Mahakama Kuu kuiomba kutoa amri hiyo kwa kuwa fedha zilizotolewa awali milioni 369 hazijulikani zimetumika vipi, na hazikuwa katika mikono salama wala hakuna udhibiti wowote wa Chama –CUF juu ya fedha hizo ikizingatiwa kuwa Lipumba alishavuliwa Uanachama.  Hata hivyo Wakili Juma Nassor aliyewasilisha maombi hayo aliweka mkazo na kusisitiza kuwa kwa mazingira yaliyopo ni vyema na Busara kwa fedha za umma zilizopaswa kutolewa kama Ruzuku kwa Chama Cha CUF kwa sasa ziendelee kubaki serikalini. Jaji Dyansobela amekubaliana na hoja zote.
kitaifa
HADIJA OMARY, LINDI Kampuni ya mafuta na gesi (Equinor Tanzania), imetoa kiasi cha Sh milioni 20 kwa Hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kuwafanyia upasuaji wanawake 80 wanaougua fistula katika Mkoa wa Lindi. Akitoa salamu za kampuni, Mkurugenzi mkazi wa kampuni hiyo Dk Mette Ottoy amesema  mpango huo  ya matibabu kwa wagongwa wa fistula kwa Mkoa huo utaendeshwa kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza inafanyika mwaka huu na awamu ya pili itaendeshwa mwakani. Naye Mkurugenzi wa CCBRT Dk Blenda Msangi  amesema miongoni mwa changamoto zinazowakabili akinamama wengi wanaougua fistula katika maeneo yaliyomengi ni kushindwa gharama za matibabu pamoja na gharama za usafiri kutoka maeneo wanayoishi mpaka katika vituo vya kutolea huduma, hivyo wanawake wengi hukosa kupatiwa matibabu ya haraka kwa kushindwa kumudu gharama hizo. “Takwimu zinaonyesha zaidi wanawake 3,000  wa kitanzania wanapata tatizo la Fistula kila mwaka  hali ambayo huwaacha akina mama hawa katia mazingira magumu  huku mkojo na kinyesi vikiwa vinawatoka bila udhibiti  lakini ni wanawake wachache ambao wanaenda kupatiwa matibabu,” amesema. “Changamoto nyingine ni imani potofu  ambapo wanawake wengi hudhani ugonjwa wa kutokwa na mkojo ama kinyesi bila udhibiti ni kunatokana na mama wakati wa ujauzito wake kushiriki kimapenzi na wanaume wengi ama kulogwa jambo hilo huwafanya akinamama wengi kuchelewa kuwahi katika vituo vya kutolea huduma kwa kuona aibu,” amesema. Kwa upande wake kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa huo Dk Stellha Kihombo amesema sababu zinazopelekea  mwanamke kupatwa na tatizo la fistula ni kukosa huduma bora ya afya wakati wa kujifungua, ikiwa sambambana na kuchelewa kufika kwa wakati kituo cha Afya.
afya
NDANI ya ulimwengu wa mapenzi kuna kitu ambacho ni vyema kila mtu akakijua. Kila mmoja katika mapenzi  anapaswa kuwa na njaa na mwenzake. Yaani ampende, amjali na awe na hofu kumpoteza.   Ikiwa mmoja anaonekana ana hofu zaidi ya kumpoteza mwenzake, huku mwingine akiona hilo si jambo baya, ni vyema ukajiuliza. Kwanini hali iko hivyo? Mapenzi ni suala linalotakiwa kuhusisha pande zote mbili. Baina ya mwanamke na mwanaume.  Kama mwanaume ndiye anaonekana anashida sana na mwanamke, hapo kuna walakini. Na hata mwanamke anapoonekana kuwa ni yeye mwenye shida sana na mwenzake, hapo pia kuna walakini.  Japo kitaalamu hapo kunaweza kuwa na sababu nyingi, ila hapa tuone thamani na maana ya kila mmoja kuwa na uhitaji na mwenzake. Uhitaji huu hasa huwa katika maana ya mapenzi, japo pia wengine wanaweza kuwa na uhitaji kwa fulani kwa sababu tofauti ikiwemo suala la kipato. Tuangalie thamani ya kuihitaji katika namna ya kimapenzi. Kama mtu hakupendi hawezi kuwa na uhitaji na wewe.  Kama mbali na kila matendo mazuri unayomfanyia haoni hatari kuwa na mbali na wewe, kuna jambo. Mapenzi ni suala linalohitaji uwepo wa unayempenda. Bila kujali gharama au umbali kila mmoja uhitaji kuwa karibu na mtu ampendaye. Ni vipi fulani aseme anakupenda ikiwa haathiriki na kuachana kwenu? Si vyema kujidanganya, ukweli ni kwamba hakuna anayetaka kuwa mbali na mtu anayempenda kwa dhati. Kama kila unalotakiwa kumfanyia, unamtendea. Kama kauli zako kwake ziko vizuri. Ikiwa tabia yako haina mashaka na unamfanya kuwa bora na wa kipekee katika maisha yako. Ni kwa namna gani kama anakupenda apende uachane nawe?  Najua kuna watu wako radhi kuachana na watu wanaowapenda kutokana na tabia fulani za wahusika. Ila hii hutokea kama anayependwa haonekani kujali wala kuthamini upendo wa mwenzake. Hata siku moja anayekupenda hawezi kutamani kuachana na wewe ikiwa uko katika tabia njema na za kupendeza. Huyo anayetaka muachanye naye, mtazame vizuri. Kweli anakupenda? Na kama kweli anakupenda ni furaha ipi ataipata kama akiachana na yule ampendaye? Anayekupenda hata siku moja hawezi kutaka kuachana na wewe.  Atahitaji uwe karibu yake, apate pendo lako na furaha ya maneno yako. Bila kuwaza sana ila huyo anayependa muachane jua kuna suala na uhaba wa mapenzi katika nafsi yake juu yako. Ni nani hapendi furaha? Na iko wapi furaha katika mapenzi kama furaha ya kuwa na mtu unayempenda?     Kwa ajili ya mapenzi yao kwa akina fulani baadhi wako radhi kufanya kila kitu na kwenda kila mahali kwa ajili ya kunusuru penzi lao. Vipi fulani awe anakupenda na bado apende kuwa mbali na wewe?  Ni uongo na wala haiwezi kuwa kweli. Daima anayekupenda atahitaji kuwa karibu na wewe. Akujali. Akuthamini na aone thamani ya maisha yako kama anavyoiona fahari ya maisha yake. Mapenzi si suala haba. Ni suala maalum na linalogusa mahala maalum.  Hakuna anayetaka kuwa mbali na suala hili, hasa baada ya kuwa na mtu anayempenda. Ukiona mbali na mazuri yako anahitaji kuchana na wewe, ujue hujamgusa mahala, mahala maalum katika nafsi yake na katika maisha yake na ndiyo maana anahitaji kuachana na wewe.   Acha kutumia nguvu nyingi kumvuta. Mapenzi yana nguvu ikiwa utakuwa mwema sana kwake. Kama baada ya kila kitu kizuri hakuhitaji, jua mti uliotua siyo mufaka kwa ndege wa aina yako. Anza safari!
burudani
Na Mwandishi Wetu, Njombe WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa, amesema Serikali itahakikisha inawasaka watu wote waliohusika na upotevu wa mali za Kiwanda cha chai cha Lupembe na kuwachukulia hatua. Amesema pia Serikali haitoipa nafasi migogoro yote ya uwekezaji inayosababisha wananchi kutopata ajira, bali itatatuliwa bila ya kusimamisha uzalishali. Pia amewataka wawekezaji waliomilikishwa viwanda, wahakikishe wanafuata kanuni na sheria ili kufikia malengo yaliyokusudiwa na wananchi waweze kupata tija. Waziri Mkuu, alitoa kauli hiyo juzi, wakati alipotembelea Kiwanda cha Lupembe akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Njombe. Mali za kiwanda hicho, vikiwamo vipuri na vyombo vya usafiri; malori na magari madogo 17 vilipotea, baada ya Ushirika wa Wakulima wa Chai Muvyulu kuvamia kiwanda. Kiwanda hicho kinakabiliwa na mgogoro kati ya mwekezaji, Lupembe Tea Estate na Ushirika wa Wakulima wa Chai Muvyulu ambao Waziri Mkuu ameahidi kuutafutia ufumbuzi.                                “Migogoro yote inayosababisha watu kutopata ajira, haitapewa nafasi. Tutaisikiliza na kuipatia ufumbuzi bila ya kusimamisha uzalishaji. “Ushirika uliyumba na umekuwa ukiharibiwa na waliopewa dhamana, ndiyo sababu tuliamua kuufumua uongozi kuanzia juu na tutashuka hadi chini,” alisema. Alisema Serikali itahakikisha mwenye haki anapata haki yake na haitakubali kuona kiwanda hicho kikisimamisha uzalishaji. Pia inafuatilia kujua mwekezaji huyo alipataje kiwanda. “Lupembe ni miongoni mwa viwanda ambavyo vilikufa, sasa kimeanza uzalishaji, hatutakubali kife kutokana na migogoro ya wanaushirika na mwekezaji. Kiwanda hakitasimama ng’o. “Hatuwezi kukubali migogoro iendelee kwani haina tija, inaumiza wananchi. Najua ushirika ni wa wakulima, tunataka uwe imara, hatutaki ushirika wenye mizengwe mizengwe,” alisema. Katika hatua nyingine, Majaliwa amemtaka Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwenda kufanya uchunguzi katika kiwanda hicho.
kitaifa
  NA KULWA MZEE DAR ES SALAAM MJANE aliyelalamika kudhulumiwa mirathi mbele ya Rais John Magufuli, katika sherehe za siku ya Sheria, amefunguliwa kesi na mtoto wa marehemu akidai fidia ya Sh milioni 400 kwa kumtaja kuwa anajihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya. Kesi hiyo ya madai imefunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na mmoja wa watoto wa Marehemu Shosi, Saburia Shosi dhidi ya mjane wa marehemu, Swabaha Shosi.  Katika kesi hiyo namba 38 ya mwaka 2017, Saburia ambaye anawakilishwa na Wakili Abdon Rwegasira, anaiomba mahakama itamke kuwa tuhuma hizo zilizotolewa na mama huyo dhidi yake ni kashfa, pia imwamuru mama huyo amlipe kiasi hicho cha fedha kama fidia ya madhara aliyoyapa kutokana na kwa kashfa hizo, riba pamoja na gharama za kesi. Kwa mujibu wa hati ya madai ya kesi hiyo, Saburia anadai kuwa yeye ndiye aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu baba yao, Shosi na kwamba mdaiwa alitoa taarifa hizo kwa nia mbaya kwa lengo la kumdhuru kwa kumharibia jina lake, tabia na mahusiano ya kijamii ndani na nje ya nchi pamoja na hali yake kiuchumi. “Mdaiwa alitoa taarifa hizi kwa hasira na kwa nia mbaya ya kutaka kupata huruma ya rais kwa jambo ambalo liko katika Mahakama za Kisheria na kwamba matokeo ya taarifa hizo zimesababisha watu waniepuke, maumivu makubwa kimwili, kiakili na kisaikolojia na biashara zangu kuvurugika,” inasema hati yake ya madai.   
kitaifa
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA MBUNGE wa Viti Maalumu, Kunti Majala (Chadema), amenusurika kipigo kutoka kwa wanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kupita na gari lake mbele ya jengo la Makao Makuu ya chama hicho mjini hapa. Majala alipita eneo hilo, gari lake likiwa limefungwa bendera mbili za Chadema, huku akiwa amefungulia kwa sauti kubwa muziki wa kunadi sera za chama chake. Tukio hilo lilitokea wakati Mwenyekiti wa CCM, Rais Dk. John Magufuli akiwa ndani ya jengo hilo akiongoza Mkutano wa Halmashauri Kuu ya chama hicho tawala. Sekeseke hilo lilianza saa 7 mchana kwa Majala na wenzake wawili kupita mara tatu na gari hilo mbele ya jengo hilo wakati mkutano ukiendelea hali ambayo ilionekana kuwakera wana-CCM, hivyo kuamua kulisimamisha. Gari hilo lenye namba T 152 CDA lilisimamishwa wakati likitokea barabara ya One Way karibu na Benki ya NMB. Baada ya kusimamishwa, dereva wa gari hilo, Stephen Masawe na kijana mmoja aliyekuwamo ndani ya gari, waliamrishwa washuke kisha wakaanza kuhojiwa sababu za kupita mara kwa mara katika eneo hilo wakiwa wamefungulia muziki kwa sauti kubwa na kupeperusha bendera za Chadema. Wakati dereva huyo na mwenzake wanatoa ufafanuzi, Majala alikuwa kimya ndani ya gari. Majadiliano ya vijana hao na wana-CCM hayakuchukua muda mrefu kwani ghafla makada wengine wa CCM walivamia eneo hilo na kuanza kuwashushia kipigo. Wakati vijana hao wawili wakipata kipigo, bado Majala alikuwa kimya akishuhudia wenzake wanavyoshughulikiwa na kuchaniwa nguo zao. Hali hiyo iliwalazimu askari walikuwapo katika lango la kuingia uzio wa jengo la CCM Makao Makuu kuingilia kati na kuwazuia makada wa CCM kuwashambulia vijana hao. Baada ya kutuliza mashambulizi, askari waliwachukua vijana hao pamoja na Majala na kuwapeleka kituo cha polisi kwa mahojiano. Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alphonce Mbasa, alikiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa wamepigwa na kuchaniwa mashati yao. “Ni kweli tukio hilo lipo, waliopigwa zaidi ni dereva Stephen Masawe na mtumishi wa chama kanda, Justin William ambao kwa sasa taratibu zinafanyika ili wapelekwe hospitali, lakini mbunge aliokolewa na polisi,” alisema Mbasa. Mwenyekiti huyo alieleza sababu za gari hilo kupita katika eneo la mkutano wa CCM kuwa walikuwa wanatoka benki ambako mbunge alikwenda kuchukua pesa ili kuwasaidia watumishi hao kupeleka gari gereji kwa matengenezo. Mbasa alisema gari hilo lilikuwa limefungwa bendera kubwa mbili ambazo wakati wote hutumika katika magari hayo maarufu kama M4C na ndiyo sababu likatambulika kwa haraka kuwa ni la Chadema. Kwa upande wake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa alikiri kutokea kwa tukio hilo.
kitaifa
WATU wanne wameuawa wakiwamo askari wawili mmoja wao akiwa ni Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Nguruka, Inspekta Ramadhani Mbini, wilayani Uvinza mkoani Kigoma, katika vurugu zilizoibuka baina ya wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa na Polisi.Katika vurugu hizo, askari hao wawili waliuawa na taarifa zaidi ambazo hazijathibitishwa zinasema pia wananchi wawili walipoteza maisha kwenye tukio hilo. Mauaji hayo yalitokea Oktoba 18, mwaka huu, katika kijiji cha Mpeta wilaya ya Uvinza mkoani Kigoma wakati polisi hao walipokuwa kwenye operesheni ya kuwaondoa wafugaji waliovamia maeneo ya hifadhi na yasiyoruhusiwa kwa ajili ya ufugaji.Diwani wa Mganza, Evidius Kapukutu alithibitisha kutokea kwa mauaji ya askari hao wawili waliotambulika kuwa ni Mkuu wa kituo cha polisi Nguruka, Inspekta Mbini na askari wa upelelezi Mohamed Zengo.Sambamba na vifo vya askari hao pia imeelezwa kuwepo kwa vifo vya wananchi wawili ambapo diwani huyo alisema kwa sasa hali ya amani na usalama imedhibitiwa kwenye eneo hilo.Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Uvinza, Jackson Mateso akizungumza na gazeti hili alikiri kuwepo kwa vurugu na mauaji hayo ingawa ametaka taarifa rasmi zitolewe na jeshi la polisi kwa sababu hana taarifa za kina kuhusu jambo hilo.Mateso alisema kuwa vurugu hizo zimekuja wakati polisi chini ya kamati ya ulinzi na usalama wakitekeleza agizo la kuwaondoa wafugaji hao waliovamia maeneo ya misitu na kufanya uharibifu wa mazingira sambamba na kuendesha kilimo isivyo halali.Mwenyekiti huyo alisema kuwa eneo ambalo operesheni hiyo ilikuwa inafanyika ni kati ya kijiji cha Chakuru na Mpeta wilaya ya Uvinza ambako kuna sehemu ya eneo la Halmashauri ya Uvinza na sehemu ya serikali kuu ambayo ni msitu wa hifadhi.“Baada ya kutokea vurugu na mauaji hayo, operesheni hiyo ilisimamishwa kusubiri maelekezo ya nini kifanyike au hatua gani zichukuliwe ingawa operesheni hiyo ilishafanyika awali na kusimamishwa na sasa ndiyo ilikuwa inaanza tena na ndiyo mauaji yakatokea,” alisema Mwenyekiti huyo.Hata hivyo, hakuna msemaji yeyote wa polisi mkoa wa Kigoma aliyekuwa tayari kutoa taarifa za tukio hilo ambapo kwa siku tatu mfululizo Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa Kigoma, Simon Ngowi amekuwa akipiga chenga waandishi kuelezea tukio licha ya kila anapopigiwa simu kuahidi kutoa taarifa.Mkuu wa Wilaya Uvinza, Mwanamvua Mrindoko na Mkuu wa Mkoa Kigoma, Emanuel Maganga hawakupatikana kuelezea tukio hilo kutokana na kuwa kwenye kikao cha Kamati ya Ulinzi na Usalama cha mkoa ambacho kinafanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Kigoma, Maganga.
kitaifa
Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM KIKOSI cha Simba jana kimewasili salama nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kikisubiri kuivaa AS Vita katika mchezo wa hatua ya makundi  ya Ligi ya Mabingwa Afrika, utakaopigwa kesho jijini Kinshasa. Kikosi cha Simba kiliondoka jana kwenda DRC kikiwa na wacheza 20, pamoja na viongozi kadhaa wa utawala na benchi la ufundi ambalo linaongozwa na kocha mkuu, Patrick Aussem. Wekundu hao wa Msimbazi wataivaa AS Vita wakiwa na kumbukumbu ya kuinyuka JS Saoura ya Algeria mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza wa hatua ya makundi uliochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Licha ya mchezo wake wa kesho kutarajiwa kuwa mgumu, mashabiki wa timu hiyo wana imani na kikosi chao kwamba kina uwezo wa kushinda  ugenini. Matumaini hayo yanatokana na kasi ya washambuliaji wa timu hiyo katika kupachika mabao. Safu ya ushambuliaji ya Simba imekuwa ikiongozwa na Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na John Bocco, ambaye hataambatana na timu kutokana na kuwa majeruhi. Aussems, ameweka wazi kuwa hana sababu ya kucheza soka la kujilinda, wakati ana kikosi chenye washambuliaji wakali ingawa pia sehemu ya kiungo cha timu hiyo imeonekana imara kwani Jonas Mkude, James Kotei na Clatous Chama, wamekuwa wakitakata. “Nafahamu mchezo utakuwa mgumu kutokana na uwezo wa wapinzani wetu ambao tunaenda kukutana nao, hata hivyo nimekiandaa kikosi changu kwa ajili ya kushambulia ili kupata mabao na hatimaye ushindi,” alisema. Alisema mara nyingi mechi za ugenini zinakuwa na ushindani, lakini ushindi walioupata kwenye mechi zilizopita umewapa morali ya kuendelea kufanya vizuri. Simba ipo Kundi D pamoja na timu za Al Ahly ya Misri, AS Vita ya DRC na JS Saoura ya Algeria. Miamba  hiyo ya soka yenye makao yake Msimbazi jijini Dar es Salaam, inaongoza kundi hilo ikiwa na pointi tatu, sawa na Al Ahly iliyoko nafasi ya pili kutokana na wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa, AS Vita katika nafasi ya tatu na JS Saoura ikikamata mkia, zote zikiwa haina pointi yoyote. Simba ilitinga hatua ya makundi baada ya kuitoa mashindanoni Nkana FC ya Zambia kwa ushindi wa jumla ya mabao 4-3, ikianza kuchapwa mabao 2-1 mjini Kitwe, kabla ya kushinda mabao 3-1 nyumbani, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
michezo
Wapinzani wa Simba, Yanga ndiyo mabingwa kwa mara ya pili mfululizo baada ya kufikisha pointi 71, ambazo haziwezi kufikiwa na timu za Azam inayoshika nafasi ya pili na pointi 60 wala Simba iliyopo nafasi ya tatu kabla ya mchezo wa jana jioni dhidi ya Majimaji wakiwa na pointi 58.Akizungumza na gazeti hili Poppe, alisema wametenga kiasi kikubwa cha pesa kwa ajili ya usajili na baada ya kutofurahishwa na mwenendo wao wa msimu huu, tayari wameanza mikakati ya kukijenga upya kikosi kitakachorudisha heshima ya Simba.“Najua tunapata lawama kubwa kutoka kwa mashabiki na wanachama, lakini kwa kuwa sisi ndio viongozi hatuna namna ya kuzikwepa ingawa nasi tunaumizwa na matokeo…ili kurekebisha hali, tumeamua kuja kivingine msimu ujao kwa kusajili wachezaji wenye viwango vya kuichezea Simba ili tuweze kufanya vizuri,” alisema Hans poppe.Amekiri kuwa, walikuwa na nafasi nzuri ya kufanya vyema katika ligi, lakini vipigo kutoka kwa watani wa Yanga pia vimechangia kuwavuruga, achilia mbali baadhi ya wachezaji kushindwa kuwajibika ipasavyo.
michezo
NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Faustine Ndugulile ameagiza kuboreshwa kwa mfumo wa ukusanyaji wa takwimu za afya nchini, utakaosaidia upatikanaji wa takwimu sahihi na zinazofanana katika taasisi zote za afya.Amesema hayo Dar es Salaam juzi katika mkutano wadau wa afya kuhusu mnyororo mzima wa upatikanaji na usambazaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi.Dk Ndugulile amesema serikali inataka kuona mifumo yote inayohusu ukusanyaji wa takwimu za afya inaboreshwa mara moja huku akisisitiza kuwa mifumo hiyo ni lazima ihuishwe na kuwasiliana, jambo litakalosaidia kupata takwimu sahihi na zinazofanana kwa mifumo yote."Tunataka kuona mnaboresha mfumo wa ukusanyaji takwimu, kwani bado suala hilo ni changamoto kubwa katika utoaji wa huduma za afya na katika mfumo mzima wa usambazaji, ni lazima kuhakikisha kuwa mifumo hii inawasiliana na inakuwa endelevu," amesema.Dk Ndugulile amewaonya watumishi wa serikali hususani kutoka Wizara ya Afya wanaokwamisha mawazo endelevu yenye kuwezesha kupigwa hatua hiyo na kuahidi kuwachukulia hatua endapo yeyote atabainika kufanya hivyo.Kadhalika, aliwaagiza waganga wafawidhi wote nchini kuhakikisha wanaandaa orodha ya dawa zilizopo kila mwanzo wa wiki ili kusaidia kufahamu kiwango cha dawa kilichopo na zinazohitajika kwa kipindi hicho."Serikali inanunua dawa muhimu na anayeandika nje ya dawa hizo, zipo taarifa kwa baadhi ya wadau kupita katika hospitali zetu, hususani hospitali kubwa na kuwarubuni madaktari wetu kuandika kwa MSD orodha ya dawa ambazo hazipo katika mwongozo wetu wa serikali,” amesema.Amewataka wadau wa ugavi wa mnyororo wa dawa kuzingatia mapendekeo ya mfumo wa mahitaji ya dawa nchini, kutumia teknolojia ili kuzalisha takwimu ambazo zimehuishwa, kutoa taarifa za wahusika wote na kuweka vigezo vya utaratibu wa dawa kwa viwango vya vifaa vya afya kwa kuwa vingine hutofautiana.Naibu Katibu Mkuu kutoka Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, anayeshughulikia afya, Dk Zainab Chaula aliwasisitiza madaktari nchini kuzingatia kile walichokisoma vyuoni ikiwa ni pamoja na kutowaandikiwa wagonjwa dawa kwa jina la kampuni ama biashara, badala yake kuandika kwa jina la asili.
kitaifa
KAMPUNI ya Multichoice- Tanzania imeingia mkataba wa mwaka mmoja wenye wenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 150 kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa ya mwanariadha chipukizi, Francis Damiano.Mkataba huo mbali na maandalizi, pia utamuwezesha mchezaji huyo kupata posho ya kujikimu kila mwezi ili kumsaidia kuondokana na matatizo ya kutafuta fedha kwa ajili ya chakula, malazi na matibabu, na badala yake ataelekeza nguvu na muda wake katika mazoezi tu.Mkuu wa Mawasiliano wa Multichoice-Tanzania aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa, dhamira yao kubwa ni kuhakikisha mchezo wa riadha unakuwa na mchango mkubwa katika kuliletea taifa sifa, kutoa ajira kwa vijana wengi na kuchangia kikamilifu kukuza uchumi wa nchi.“Tunataka taifa hili lijulikane ulimwengu mzima kama chimbuko la mabingwa, na tumeanza na riadha. Tumedhamiria kukuza mchezo na kuufanya kama chanzo kikubwa cha ajira kwa vijana wetu, lakini pia riadha ni mchezo ni burudani na ni sekta nyeti…,” alisema Mshana.Alisema kuwa mwanariadha huyo kwa kuanzia ataanza na mashindano ya Kanda ya Tano ya Afrika yanayoanza leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na kuendelea na mashindano mengine kama ya mashindano ya vijana ya Dunia yatakayofanyika mwezi ujao Finland, Michezo ya Olimpiki ya vijana Kanda ya Afrika na mengine mengi.Wakati huohuo, Multchoice imetangaza kuacha rasmi na aliyekuwa balozi wao, Alphonce Simbu baada ya kukamilisha kumjenga kimsingi na sasa wanaelekeza nguvu zao kwa Damiano na wanariadha wengine chipukizi.Awali, walipoanza kumsaidia Simbu, mwanariadha huyo kila mwezi alikuwa akilipwa kiasi cha Sh milioni 1 kama mshahara wake ukiondoa gharama zingine za vifaa, na ushiriki wa mashindano mbalimbali. Simbu
michezo
LIGI Kuu ya soka ya wanawake inatarajiwa kuendelea leo baada ya kusimama kwa mwezi mmoja kupisha michuano ya kombe la Chalenji iliyofanyika nchini mwezi uliopita. Ligi hiyo ambayo inaingia katika mzunguko wa tatu leo itachezwa michezo sita katika viwanja vya miji tofauti.Bingwa mtetezi JKT Queens itacheza na Simba Queens kwenye Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Mbweni Dar es Salaam. Mchezo huo unatarajiwa kuwa na upinzani kwani Simba Queens itahitaji kufuta uteja kwa JKT Queens kwa sababu katika michezo minne waliyokutana tangu msimu wa mwaka 2017 hadi 2018 Simba Queens imefungwa mechi zote.JKT Queens inaongoza msimamo ikiwa na pointi sita walizopata katika mechi za ugenini wakati Simba Queens ina pointi nne ilizozipata katika uwanja wake wa nyumbani, Karume. Endapo Simba Queens itashinda mechi hiyo itakuwa timu ya pili kuifunga JKT kwani Mlandizi Queens iliwahi kufanya hivyo msimu wa mwaka 2016/2017 walipotwaa ubingwa ligi ilipoanza lakini kama JKT Queens haitafungwa itaendeleza rekodi ya kutofungwa kwa msimu wa tatu.Mchezo mwingine utazikutanisha Yanga Princess ambayo itaialika Mlandizi Queens katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam. Yanga Princess msimu huu imeanza vyema kwa kushinda mechi zote mbili ilizocheza na kujikusanyia pointi sita huku Mlandizi Queens ikiwa na pointi tatu baada ya kucheza michezo miwili ikiifunga Panama Queens na kufungwa na Ruvuma Queens katika uwanja wa nyumbani Mabatini, Pwani.Mji wa Songea utakuwa unaandika historia kwa mara ya kwanza tangu Ligi Kuu ya wanawake Tanzania Bara ianzishwe msimu wa mwaka 2016/2017 kwani hawakuwa na timu ya wanawake lakini safari hii Ruvuma Queens itamenyana na TSC Queens katika Uwanja wa Majimaji Ruvuma Queens yenye pointi nne, mechi za mwanzo mbili ilicheza ugenini hivyo haijawahi kutumia uwanja huo kwa mechi za Ligi Kuu zaidi ya zile za kirafiki.Mchezo huo unatarajiwa kuwa mgumu kwasababu timu zote zimepanda daraja msimu huu lakini Ruvuma Queens inaonekana kuwa vizuri zaidi kutokana na kuwa na wachezaji wazoefu zaidi kwenye ligi ukilinganisha na TSC Queens yenye pointi tatu.Panama Queens ya Iringa ambayo haina pointi itaialika Alliance Girls ya Mwanza yenye pointi sita katika Uwanja wa Samora Iringa, Sisterz ya Kigoma yenye pointi tatu itacheza na vibonde Tanzanite Queens ambayo inashika mkia katika msimamo kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma.Marsh Queens ya Mwanza itacheza na Baobab Queens ya Dodoma katika Uwanja wa Nyamagana, Mwanza, mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani kwani hakuna timu iliyoshinda mchezo wake katika ligi ya msimu huu.Katika kuwania kiatu cha ufungaji bora Fatuma Mustafa wa JKT Queens ana mabao sita akifuatiwa mchezaji mwenzake wa JKT Asha Rashid mwenye mabao matano na Mwapewa Mtumwa wa Yanga Princess ana mabao manne.Mwanahamisi Omar wa Simba Queens ana mabao mawili sawa na Philomena Daniel na Jamila Hassan wa Mlandizi Queens na Janeth Matulanga wa Alliance Girls.
michezo
NA VERONICA ROMWALD WATOTO 24 waliozaliwa na matatizo ya usikivu (viziwi) watafanyiwa upasuaji wa kupandikizwa vifaa vya usikivu kila mwaka katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa Muhimbili, Aminiel Aligaesha alisema hayo mwishoni mwa wiki alipozungumza na MTANZANIA. “Hii ni huduma mpya ambayo Muhimbili tumeianzisha na ilizinduliwa hivi karibuni na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. “Tumepanga kila mwaka kufanya upasuaji katika awamu nne, kila robo tatu ya kwanza ya mwaka tutawafanyia watoto sita,” alisema. Alisema tayari katika robo tatu ya kwanza ya mwaka, Aprili hadi Juni, wamefanyiwa upasuaji watoto sita kwa mafanikio makubwa. “Watoto hao wanaendelea vizuri baada ya upasuaji, sasa hivi madaktari wanaendelea kutoa huduma za kliniki kama kawaida na kufuatilia hali zao. “Hivyo watapanga tena orodha nyingine ya watoto ambao watafanyiwa upasuaji katika awamu inayofuata,” alisema. Inakadiriwa kila mwaka watoto 200 huzaliwa na tatizo la usikivu na hivyo kuhitaji upasuaji awali walikuwa wakipewa rufaa kwenda  India kupata huduma hiyo ya upasuaji. Tangu mwaka 2003 hadi sasa wagonjwa 50 pekee ndiyo walionufaika na mpango wa ufadhili wa serikali.
afya
  Na Mwandishi wetu, MWENYEKITI wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dotto Biteko, amempongeza Rais Dk. John Magufuli kutokana na uamuzi wake wa kuunda kamati maalum kwa ajili ya kuchunguza mchanga wa madini. Akizungumza na MTANZANIA Dar es Salaam jana baada ya Rais Magufuli kukabidhiwa ripoti ya pili, Biteko alisema ripoti zote mbili zimethibitisha kilio cha Watanzania kuhusu kuibiwa rasilimali za madini uliofanywa kwa miaka mingi. “Rais amejibu kilio hiki cha Watanzania, wananchi walikuwa wanaamini na hasa wale wanaozunguka migodi kwamba tulikuwa tunaibiwa. “Ripoti zote mbili zimethibitisha ukweli juu ya kilio hiki na katika hili nampongeza Rais kwa uamuzi wake wa kuunda kamati maalumu ambazo zimetuletea matokeo chanya,” alisema. Hata hivyo Biteko ambaye pia ni Mbunge wa Bukombe, alisema kamati yake inasubiri maelekezo ya Spika wa Bunge, Job Ndugai, atakapounda kamati ya kufuatilia uchimbaji wa madini ya almasi. “Spika ameahidi kuunda kamati ya kufuatilia suala la uchimbaji wa madini ya almasi kabla ya Bunge hili la Bajeti halijaisha. “Siku zote sisi wabunge na wajumbe wa kamati za Bunge tumekuwa tukifanya kazi chini ya maelekezo ya Spika, hivyo katika hili tunasibiri mwongozo na maelekezo yake,” alisema.
kitaifa
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imeandika historia iliposaini Makubaliano ya Mgawanyo wa Uzalishaji wa Mafuta na Gesi Asilia (PSA) na Kampuni ya RAKGAS ya Ras al Khaimah ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE).Mkataba huo wa kwanza wa aina yake katika historia ya mafuta na gesi asilia Zanzibar, unaelezea majukumu, haki, matumizi, mapato na mgawanyo wake baina ya pande hizo mbili.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Ali Mohamed Shein alisema mjini hapa mkataba huo unahusisha kitalu cha Pemba – Zanzibar tu ambacho kinajumuisha maeneo yaliyopo nchi kavu na ya baharini.Ulisainiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa RAKGAS, Kamal Mohamed Ataya, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta ya Zanzibar (ZPDC), Mwanamkaa Abdulrahman Mohamed na Waziri wa Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Salama Aboud Talib.Ulitiwa saini juzi usiku Ikulu ya Zanzibar mjini Unguja, ukishuhudiwa na Rais , Dk Shein na mgeni wake, Mtawala wa Ras Al Khaimah, Shekhe Saud Bin Saqr Al Qasimi ambaye aliwasili Zanzibar juzi jioni kwa shughuli hiyo, pamoja na ziara ya siku mbili visiwani hapa.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Ali Khalil Mirza, mikataba mingine kama hiyo ijayo itahusisha maeneo mengine ya Zanzibar ambayo yamo hatua za matayarisho na taasisi husika.“Kwa mnasaba huo, siku ya leo inaungana na nyingine chache kwenye orodha ya siku muhimu katika kumbukumbu ya nchi yetu. Ni safari ndefu ya kuweka misingi ya kuhakikisha kwamba rasilimali ya Zanzibar ni kwa ajili ya Wazanzibari na kwamba vizazi vilivyopo na vijavyo vitanufaika ipasavyo na manufaa ya rasilimali hiyo itakapopatikana,” alisema Mirza.Akielezea historia fupi ya kazi ya utafutaji mafuta na gesi asilia Tanzania alisema ilianza miaka ya 1950 ambayo kwa Zanzibar, Kampuni ya British Petroleum (BP) na Shell kwa pamoja zilifanya utafiti huo kwa kuchimba visima vya utafiti maeneo ya visiwa vya Unguja na Pemba.Alisema utafiti huo haukukamilika na miaka ya 1962/1963, ulitoa matokeo ya matumaini ya utafiti zaidi kuendelezwa baada ya kugundulika kuwepo kwa miamba ya mafuta na gesi asilia.“Harakati mpya za kuendeleza utafiti wa mafuta na gesi asilia zilianzishwa tena mwaka 2011 Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Ras Al Khaimah walipoanzisha mazungumzo ya ushirikiano ukiwemo ushirikiano katika sekta ndogo ya mafuta na gesi asilia,” alisema katibu.Alisema Novemba 12, 2011, SMZ na Serikali ya Ras Al Khaimah walisaini Hati ya Ushirikiano (MoU) kufanya kazi kwa pamoja na kuleta ufanisi katika maendeleo ya Zanzibar. “Hati hiyo ya Ushirikiano ilikuwa na mambo tisa, moja ya hayo ni “Kuanzisha na kuingia katika makubaliano ya Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia (Hydrocarbon) ndani ya eneo la mipaka ya Zanzibar,” alisema Mirza.Alisema katika utekelezaji wa ushirikiano huo, serikali hizo mbili ziliunda Kamati Maalumu ya Utekelezaji wa Hati ya Makubaliano (JISC) yenye lengo la kusimamia utekelezaji wake.Alisema jumla ya vikao saba vilifanyika kati ya Januari 31, 2012 na Agosti 22, 2016. Alisema mwaka 2015, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliridhia Sheria ya Mafuta Namba 21 ya 2015 ambayo imeipa SMZ mamlaka ya kushughulikia rasilimali za mafuta na gesi asilia wenyewe.Alisema baada ya kukamilika kwa Sera na Sheria, SMZ iliunda Kamati Maalumu ya Majadiliano kwa ajili ya kufanya majadiliano na Kampuni ya RAKGAS kuhusu PSA na baada ya mijadala na mikutano mingi, ndiyo iliyozaa matunda ya mkataba uliosainiwa juzi usiku.Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetumia Mkataba wa PSA kwani unaweza kutoa mfumo mzuri wa kimkataba unaoweza kudhibiti na kutoa uhakika wa kisheria kwa muda wote wa shughuli za mafuta na gesi asilia.Akihutubia baada ya kushuhudia utiaji saini huo, Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein alisema tukio la juzi ni kusonga mbele. Alieleza juhudi za serikali zote mbili, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuzitafutia ufumbuzi changamoto zilizokuwapo, ikiwamo kulazimika kutunga sheria muhimu mpya zilizo bora zaidi, madhubuti na zenye kuzingatia maslahi ya pande zote mbili za Muungano.Alimshukuru Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete kwa kuhakikisha kabla ya kustaafu, suala la mafuta na gesi linapatiwa ufumbuzi na kuondoa kero ya muda mrefu. Alisema matokeo ya juhudi hizo yatakuwa na manufaa na mchango mkubwa kuendeleza uchumi. Alisema faida yake ni kama mfano wa afya na kiwiliwili, yaani afya inapoimarika na kiwiliwili cha binadamu huimarika na kunawiri.
kitaifa
NA NORA DAMIAN, KIGOMA WATALII wengi katika Hifadhi ya Taifa ya Gombe iliyoko mkoani Kigoma, wamevutiwa na vipande vya video ya wimbo wa ‘Leka Dutigite’ ulioimbwa na wasanii wanaotokea Mkoa wa Kigoma ‘Kigoma All Stars’, kutokana na kutumia mazingira ya hifadhi hiyo. Kipande kinachouliziwa zaidi na watalii wanaofika katika hifadhi hiyo ni kile kinachomwonyesha mkali wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’ akiwa anabembea katika mti ulioko katika hifadhi hiyo. Mhamasishaji Utalii Msaidizi katika hifadhi hiyo, Isaya Mkude, alisema watu wengi hasa wazawa wamekuwa wakifika na kutaka waonyeshwe sehemu alipobembea msanii huyo. “Tumeamua kuiita bembea ya Diamond kwa sababu baada ya yeye kubembea imekuwa kivutio kwa watu wengi kuja na kutaka kwenda kupaona na wengine kubembea,” alisema Mkude. Alisema miaka ya nyuma wageni ndio walikuwa wengi wanaotembelea hifadhi hiyo lakini hivi sasa kuna mwamko mkubwa kwa wazawa. Takwimu za mwaka 2014/15 zinaonyesha wazawa waliotembelea hifadhi hiyo ni 527 wakati wageni ni 927. Kwa mwaka 2015/Mei 2016 wazawa ni 374 na wageni ni 645. Gharama ya kuingia katika hifadhi hiyo ambayo ni maarufu kwa wanyama aina ya sokwe ni Sh 10,000 kwa Mtanzania mmoja na Dola 100 kwa mgeni kwa siku.
burudani
NA KULWA MZEE -DAR ES SALAAM WAKAZI wanne wa Jiji la Dar es Salaam, wamehukumiwa kwenda jela miaka 30 na kuchapwa viboko 12 kila mmoja kwa wizi wa simu nne za kiganjani. Watu hao ambao ni wakazi wa eneo la Boko Magengeni katika Wilaya ya Kinondoni, katika kutekeleza adhabu hiyo watachapwa viboko sita wakiingia gerezani na sita siku wakitoka. Washtakiwa hao walihukumiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage baada ya Jamhuri kuthibitisha makosa yao bila kuacha shaka. Waliohukumiwa ni Donald Nzwenka,  Michael Paschal, Ally Akili na Kurwa Mwakagenda. Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Mwijage, alisema washtakiwa kwa pamoja Julai 7, 2013 maeneo ya Boko Magengeni, Dar es Salaam waliiba simu nne aina ya Nokia, Sumsung, Teckno zikiwa na thamani ya Sh 1,300,000. Pia washatakiwa hao waliiba, fedha taslimu Sh 150,000, cheni za dhababu mbili zenye thamani ya Sh 750,000, ambapo mali yote jumla ina thamani ya Sh 2,050,000. Hakimu Mwijage alisema kabla ya wizi huo, washtakiwa walimtishia na jambia Hobokela Mwakijambile, ambaye ndiye mwenye mali hizo. Katika kesi hiyo Jamhuri iliita mashahidi 11 na washtakiwa walijitetea wenyewe. “Baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili, mahakama ilijiuliza kwamba kosa la kutumia silaha ili lithibitike Jamhuri wana wajibu wa kuthibitisha bila kuacha shaka kwamba washtakiwa kabla ya kutenda awe na kifaa hatari. ” Pia washtakiwa kabla ya kutenda  wawe zaidi ya mmoja na kwamba baada ya tukio hilo walitumia nguvu kwa mtu aliyeporwa,” alisema. Alisema katika shauri hilo, mlalamikaji na mashahidi wengine walieleza usiku wa Julai 7 mwaka huo majambazi walivunja mlango mkuu wa nyumba yao kwa kutumia bomu ambalo lilitambuliwa na polisi kuwa baruti. Ushahidi ulieleza kwamba, washtakiwa waliendelea kuvunja milango mingine na baadae waliingia katika chumba walichokuwa wamekaa mashahidi. Wakiwa katika chumba hicho chenye mwanga, mshtakiwa wa nne alishika panga na alianza kuwapiga nalo kwa kutumia ubapa. “Kwa kuzingatia ushahidi huo, hakuna shaka kwamba mashahidi waliweza kuwatambua hao majambazi kwamba ni washtakiwa katika kesi hiyo. “Kwa kuangalia maelezo yao, waliyotoa Polisi yanaonyesha jinsi walivyoshiriki katika tukio na kwamba washtakiwa ndio walioiba vifaa hivyo kwa kutumia silaha kali,”alisema. Hakimu alisema utetezi wa washtakiwa kwamba walikamatwa maeneo tofauti na kupelekwa Oysterbay Polisi na kupigwa na kunyanyaswa hauaminiki. Mahakama ilisema ushahidi huo hauaminiki na hauwezi kupewa uzito wowote. Alisema utetezi wa kukanusha tu kuhusika katika kosa siku hiyo, haukutikisa kwa namna yoyote ushahidi wa Jamhuri. “Kutokana na hayo, hakuna shaka kwamba washtakiwa walitenda kosa na walitambuliwa ipasavyo. “Nimeridhika Jamhuri imethibitisha kosa bila kuacha shaka dhidi ya washtakiwa, hivyo nawatia hatiani kwa kosa la kutumia silaha kama walivyoshtakiwa,”alisema. Jamhuri katika kesi hiyo iliwakilishwa na Wakili wa Serikali Gloria Mwenda, ambaye alisema washtakiwa ni wakosaji wa mara ya kwanza na akaomba wapewe adhabu kali.
kitaifa
NA MWAMVITA MTANDA, Kigali LICHA ya aliyewahi kuwa kocha msaidizi wa Simba, Mrundi, Masoud Djuma, kuondoka ndani ya kikosi cha AS Kigali, lakini mashabiki wa soka nchini Rwanda wanataka arejee kuinoa Rayon Sport.  Kabla ya kupata kibarua ndani ya klabu ya Wekundu wa Msimbazi, Simba, Djuma alikuwa akiifundisha Rayon Sports,  ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa. Na baada ya kutemana na Simba, kocha huyo alijiunga na AS Kigali ya hapa ambayo hakudumu nayo, baada ya kutokuwa na maelewano mazuri na watendaji wengine wa benchi la ufundi la timu hiyo. Akizungumza na MTANZANIA, jana, shabiki maarufu wa Rayon Sports, Akizimana Godfrey alisema anaamini Djuma ni kocha mwenye uwezo mkubwa na bado wanamkumbuka kwa kuisaidia Rayon Sport kutwaa ubingwa. Aliutaka uongozi wa klabu hiyo kuangalia uwezekano wa kumrudisha kufanya kazi naye kwa mara nyingine. “Kitu ambacho timu zetu zinashindwa kubaki na Djuma ni kwamba hawaelewi nini anataka, Djuma anataka kupewa nafasi ili afanye kazi yake vizuri.  “Kwa uwezo alionao,  hata akikabidhiwa timu bila msaidizi anaweza kufanya vizuri, ni kocha mzuri na mwenye mbinu za kimataifa,”alisema Akizimana na kuongeza. “Hata kama Rayon inafanya vizuri,lakini bado haijafikia kiwango ilichokuwa nacho Djuma.”
michezo
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani, Mkoa wa Arusha, Nuru Suleiman ameieleza mahakama kuwa basi lililosafarisha wanafunzi wa Shule ya Lucky Vincent, lilikuwa linamilikiwa na mtu mwingine na si Mkurugenzi wa shule hiyo. Amedai basi hilo limewahi kumilikiwa na watu watatu tofauti na mmiliki wa mwisho alikuwa Swalehe Kiluvia kabla ya Kampuni ya Lucky Vincent. Suleiman ambaye ni shahidi wa pili katika kesi ya makosa ya usalama barabarani ikiwamo kusafirisha watoto bila vibali muhimu inayomkabili Mkurugenzi wa Shule ya Lucky Vincent, Innocent Moshi, Mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Arumeru, Desderi Kamugisha, amedai mahakamani hapo leo kuwa gari hilo pia halikuwa na leseni ya kubeba wanafunzi na badala yake lilikuwa na leseni ya kusafirisha abiria kutoka Arusha hadi Mererani. “Baada ya kupokea barua kutoka kwa mpelelezi wa shauri linalohusu ajali hiyo ikinitaka kupata baadhi ya uthibitisho kutoka mamlaka tofauti kwa ajili ya upelelezi ambapo tuliandika barua Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Idara ya Kazi, Mamlaka ya Mapato (TRA) na Kampuni ya Bima, Zanzibar Insurance,” amedai. Shahidi huyo amedai barua hizo aliandika Mei 8, mwaka huu kwa taasisi hizo ili kufahamu kuhusu uhalali wa bima ya gari hilo, uchunguzi wa leseni ya usafirishaji, mkataba kati ya dereva na mmiliki wa gari pamoja na kutaka kujua iwapo gari hilo limewahi kumilikiwa na mtu mwingine. “Mei 9, mwaka huu tulipata majibu kutoka taasisi hizo ambapo Sumatra ikieleza basi hilo halikuwa na leseni ya kubeba wanafunzi na badala yake lilikuwa na leseni ya kusafirisha abiria kutoka Arusha kupitia Mbuguni kuelekea Mererani, huku likionyesha mmiliki alikuwa ni mwingine anayetambulika kwa jina la Swalehe Kiluvia. “Zanzibar Insurance walisema bima ya mwisho kukatiwa basi hilo ilikatwa na Kiluvia na Lucky Vincent hawakukata, hivyo kuendelea kutumia bima ya mmiliki mwingine, bima hiyo inakuwa siyo halali, huku Idara ya kazi ikitoa majibu kuwa ofisi hiyo haikuwa na mkataba wanaoutambua kati ya dereva wa basi hilo Dismas na shule hiyo,” amedai.  
kitaifa
RAYMOND MINJA IRINGA Katibu wa itikadi na uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humfrey Polepole, amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu badala yake wawe suluhisho kwa kufuata malengo ya chama ambayo ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo. Ameyasema hayo leo Juni 12 katika semina ya kuwafunda makatibu wa uenzi wa ngazi zote mkoani humo ambapo amesema kuwa chama hicho kimejengwa kwenye misingi bora ya kutumikia wananchi na kuwasikiliza ili kujua shida zao. “Hii ni CCM mpya chini ya mwenyekiti rais John Magufuli na hana utani anataka kazi tu na wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani kuna siku itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia serikali ”amesema. Amesema kuwa kwasasa mlango uko wazi na kwamba endapo kuna mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya chama hicho chini ya rais Magufuli ni vyema akapisha na kuacha wanaojua kufanya kazi. Pia amewataka viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoani humo, Ramadhani Baraza kuendelea kuwatumikia wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.
kitaifa
WAKATI mpiga picha raia wa Marekani John Moore akiibuka mshindi wa picha duniani, wapiga picha wa vyombo vya habari nchini wametakiwa kujielimisha zaidi kuhusu lugha ya picha na kuwa wabunifu.Rai hiyo ilitolewa jana na Balozi wa Uholanzi nchini, Jeroen Verheul aliyesema kuwa wapiga picha wa Tanzania wanakosa ubunifu na hawajui ipasavyo kutambua lugha za picha, kitu kilichofanya wakashindwa kwenye mashindano hayo ya picha duniani maarufu kwa jina World Press Photo, yanayofanyika kila mwaka.“Haihitaji kuwa na vifaa ya kisasa ili kupiga picha bora, hata simu unaweza kutumia kupiga picha na ikawa bora na kushinda tuzo, kinachotakiwa ni maarifa na ufahamu wa lugha za picha ambazo wengi wanakosa,” alisema Verheul.Alisema kutokana na hilo, wameandaa mafunzo ya siku mbili kwa wapiga picha wa vyombo mbalimbali vya habari na kuwajengea uwezo wa kuwa wabunifu na kuwapa maarifa zaidi juu ya upigaji picha. Mafunzo hayo ya siku mbili yamemalizika jana, Oktoba 25.“ Tumetoa mafunzo kwa wapiga picha ili wajitafakari kuhusu taaluma zao na fursa zilizopo nchini za uandishi wa habari shirikishi, lengo kuu ni kuamsha ubunifu na kukuza taaluma yao,” alisema Balozi huyo wa Uholanzi Picha iliyoshinda mwaka huu ilipigwa Juni 25 mwaka jana ikimuonesha mtoto wa Kihandurai aliyekua akilia wakati yeye na mama yake wakipelekwa kizuizini na maofisa wa mipaka ya Marekani.Mshindi wa pili katika picha duniani ni Pieter Hoopen kutoka Uholanzi ambaye picha yake ilihusu msafara wa wahamiaji wa Marekani ya Kati wakielekea katika mpaka wa Marekani katika kipindi cha mwezi Oktoba na Novemba 2018.Meneja wa maonesho ya picha kutoka kituo cha Alliance Francaise, Sanne Vanderleef alisema jumla ya picha 78, 813 ziliwasilishwa kwenye mashindano hayo nakufanya jumla ya wapiga picha 4,000 kutoka nchi 128 duniani. Alisema baada ya kupitia picha hizo, 140 zilifanikiwa kuingia kwenye maonesho ya mwaka huu.“Picha 140 zilizofanikiwa kushinda zitakuwa kwenye maonesho kuanzia leo (Jana) Oktoba 25 hadi Novemba 14,” alisema na kuongeza kuwa kwa Tanzania maonesho hayo yanafanyika kituo cha utamaduni cha Ufaransa, kilichopo Upanga.Vanderleef alisema maonesho hayo yanafanyika sambamba na warsha za waandishi wa habari kuanzia Novemba 11 na 12, mwaka huu.
kitaifa
LONDON, UINGEREZA WATU nchini Uingereza wameombwa kuwa katika tahadhari baada ya ugonjwa usio wa kawaida unaosambaa kwa kuumwa na kupe kubainika kwa mara ya kwanza nchini humo. Wizara ya Afya imesema hatari iliyopo kwa umma ni ya chini lakini ni muhimu wawe waangalifu kuhusu kupe hasa wanapokuwa kwenye maeneo ya bustani msimu wa joto. Imeelezwa kuwa ugonjwa huo unasababishwa na vimelea ambavyo vinaathiri chembe nyekundu za damu. Tayari mgonjwa wa pili aliyeambukizwa ugonjwa huo ambao ni nadra sana kutokea amegunduliwa. Ugonjwa huo unaosambazwa na kupe unaosababisha ubongo kufura mara nyingi hutokana na maambukizi ya virusi. Dk. Katherine Russell kutoka Wizara ya Afya nchini humo amesema ugonjwa huo ni nadra sana na hivyo basi uwezekano wa maambukizi ni wa chini mno. “Kupe hupatikana sana kati ya msimu wa kuchipua na pukutizi, kwahiyo ni muhimu ikiwa raia watachukua tahadhari ya juu ili kuhakikishi hawaumwi na kupe wanapokuwa nje wakijivinjari. Na pia tafuta ushauri wa daktari unapoanza kusikia vibaya baada ya kuumwa na kupe,” alisema Dk. Katherine. Wizara ya afya imesema imepima mamia ya kupe katika eneo la Devon karibu na anapoishi mgonjwa wa kwanza aliyebainika na ugonjwa huo, lakini wote hawakupatikana nao. Na pia vipimo vya damu kutoka Hampshire katika maeneo karibu na anapoishi mgonjwa mwingine vimeonekana kuwa salama. Wagonjwa wote wanapata matibabu hospitalini na kulingana na Kituo cha Kuzuia Magonjwa Ulaya kimesema ugonjwa huo unasambazwa tu na kupe ambao hupata maambukizi kwa kuumwa na ng’ombe walio na maambukizi na panya buku. Kuna watu 39 waliothibitishwa kupata maambukizi barani Ulaya, nje ya Ulaya, ugonjwa huo mara nyingi hutokea Marekani. DALILI Watu wengi wenye ugonjwa huo ama hawatakuwa wanaonesha dalili au dalili za maambukizi ni za wastani.  Hata hivyo, watu wenye mfumo wa kinga ya mwili dhaifu wanaweza kuumwa sana, wakilalamikia dalili za kama mafua, homa, kuhisi baridi, kuumwa na misuli, uchovu na homa ya nyongo ya njano. Karibia theluthi mbili ya watu wenye maambukizi ya ugonjwa huo hawataonesha dalili, kwa walio na mafua na homa, kuumwa kichwa na uchovu wanaweza kupata ugonjwa wa utando wa ubongo au kufura kwa ubongo na kupooza mwili. Shingo inapokakamaa na kuumwa kichwa, kupata maumivu kwa kuangalia mwanga wa taa, kuzimia, kuwa na mabadiliko ya tabia- kama kuchanganyikiwa ghafla na kuhisi baadhi ya sehemu za mwili zinashidwa kusongea.
kimataifa
JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Tarime- Rorya, limefanikiwa kuwaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi akiwemo aliyewahi kudaiwa kunyang’anywa bunduki aina ya SMG na mwanamke mkazi wa Buriba katika Kata ya Sirari wilayani Tarime.Kamanda wa Polisi wa Tarime-Rorya, Henry Mwaibambe alisema jana katika tukio hilo, zimepatikana bunduki 2; moja AK 47 na goboro, na risasi 5 zikiwa ndani ya magazine.Alisema majambazi hao walikufa Novemba 7, mwaka huu saa nne usiku baada ya majibizano ya risasi walipovamia nyumbani kwa mfanyabiashara wa samaki, David Ogutu maarufu Baba Ouma Kijiji cha Obwere Shirati wilayani Rorya kupora fedha.“Kundi la majambazi hao likiwa limejihami kwa silaha za moto, lilivamia nyumbani kwa mfanyabaishara huyu wa samaki kwa nia ya kufanya uhalifu wa kupora fedha; walifyatua risasi hewani kuwatishia wananchi wasijitokeze kutoa msaada lakini mfanyabiashara huyo alipiga simu kwa askari polisi Kituo cha Shirati waliofika,” alisema Mwaibambe.Aliongeza kuwa, “majambazi hao walipowaona polisi, waliwarushia risasi na kuanza majibizano ya risasi hatimaye polisi kufanikiwa kuwajeruhi majambazi hao watatu… wananchi na polisi walifuatia nyayo na damu iliyoonekana katika eneo la tukio.”Kutokana na mwito wa polisi wa kutaka taarifa zitolewe mapema kuhusu watu watakaoonekana wamejeruhiwa, siku iliyofuata (Novemba 8, mwaka huu), wananchi Mjini Tarime walimwona mtu aliyejitambulisha kwa jina la Kesanta Chacha akiwa na majeraha amejifunika jaketi akipanda gari dogo la abiria kutaka kwenda Sirari.Kamanda Mwaibambe alisema walimtilia shaka na kutoa taarifa kwa polisi kabla gari hilo halijaondoka na kumkamata mkazi huyo wa Kebeyo aliyewahi kupatikana na bunduki AK 47, lakini akaachiwa na mahakama akiwa na umri wa takriban miaka 16.
kitaifa
Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA SERIKALI imetangaza kuwapandisha vyeo watumishi wa umma 193,166 kuanzia Mei Mosi. Hayo yalielezwa jana bungeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika wakati akitoa kauli kuhusu upandishwaji vyeo kwa watumishi wa umma. Mkuchika alipewa nafasi hiyo na Spika wa Bunge, Job Ndugai mara baada ya kumalizika kwa kipindi cha maswali na majibu. Alisema watumishi hao watakaopandishwa vyeo ni wenye utendaji kazi mzuri ambao wanakaribia kustaafu, watumishi waliokaa katika vyeo walivyonavyo kwa muda usiopungua miaka minne na kukasimiwa kwenye ikama ya bajeti ya mwaka wa fedha 2017/18. Mkuchika aliwataka waajiri wote kuhakikisha wanawapandisha vyeo watumishi stahiki kwa wakati na kwa kuzingatia TANGE (Seniority List) ya taasisi husika, sifa za kimuundo na kuwepo kwa nafasi iliyoidhinishwa kwa mujibu wa matokeo ya tathimini ya utendajikazi. “Waajiri na maofisa watakaotekeleza zoezi hili kinyume na maelekezo yaliyotolewa na Serikali kuhusu upandishaji vyeo watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma,” alisema. Alisema upandishwaji vyeo ulihairishwa Mei mwaka 2016 kupisha uhakiki wa watumishi hewa na mishahara batili pamoja na vyeti vya utumishi wa umma. “Baada ya kukamilika kwa mazoezi tajwa, Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli aliridhia upandishaji vyeo watumishi kwa awamu,” alisema. Mkuchika alisema awamu ya kwanza iliyoanza Novemba Mosi mwaka juzi, ilihusisha upandishaji na uidhinishaji wa taarifa za watumishi 59,967 ambao taarifa zao za kupandishwa vyeo zilikuwemo katika Mfumo wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCMIS), lakini zilikuwa hazijaidhinishwa wakati wa usitishaji tajwa Mei mwaka 2016. Alisema kuwa awamu ya pili iliyoanza Aprili Mosi mwaka jana, ilihusisha watumishi zaidi ya 53,553 ambao walipandishwa vyeo, lakini taarifa zao zilikuwa hazijaingizwa kwenye mfumo wa HCMIS. Mkuchika alisema uidhinishaji wa taarifa za watumishi 113,520 katika makundi hayo mawili kupitia mfumo wa HCMIS umekamilika. “Baada ya kukamilika upandishaji vyeo watumishi wa umma wapatao 113,520, Serikali imewaelekeza waajiri kuendelea na upandishaji vyeo kwa watumishi 193,116 waliokasimiwa ikama na bajeti ya mishahara kwa mwaka wa fedha 2017/18 kuanzia Mei mwaka huu,” alisema Mkuchika
kitaifa
Na ESTHER MNYIKA-DAR ES SALAAM SERIKALI imeitaka Kampuni ya M/s China Civil Engineering Construction Corparation (CCECC) kukamilisha mradi  wa ujenzi wa barabara za juu  ‘interchange’ katika makutano ya Ubungo ndani ya miaka ya mitatu.  Mkataba uliofikiwa unamtaka Mkandarasi ambayo ni Kampuni ya CCECC kutoka China kuanza ujenzi huo mara moja na ujenzi huo ambao unatarajiwa kutumia takriban miezi 30  kukamilika   Mtendaji Mkuu  wa Wakala wa Barabara Tanzania  (TANROADS), Patrick Mfugale aliyesema hayo Dar es Salaam jana baada ya kusaini mkataba na kampuni hiyo ya  ujenzi wa barabara za juu   katika makutano ya Barabara ya Sam Najoma, Morogoro na Mandela. “Zaidi ya Sh bilioni 177.4 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi huo ambao utakawekewa jiwe la msingi Machi mwaka huu. “Hakikisheni mnaanza ujenzi mara moja kwa sababu Serikali imeshakamilisha taratibu zote na tayari Sh bilioni 2.1 zimelipwa kwa ajili ya fidia kwa wananchi walioguswa na mradi huo,”  alisema Mfugale. Alisema ujenzi wa Ubungo interchange unatekelezwa  kwa fedha ya mkopo kutoka Benki ya Dunia  kwa ajili ya   uboreshaji miundombinu ya usafiri Dar es Salaam.
kitaifa
UTUMIKISHWAJI wa watoto wa kike ili kusaidia familia, umaskini, mazingira magumu kwenye shule, mimba za utotoni ni miongoni mwa sababu zinazowafanya wasichana kuacha shule katika wilaya ya Bahi mkoani Dodoma.Akizungumza wakati wa mahojiano jana, Mratibu wa Programu wa Shirika lisilokuwa la kiserikali la Marafiki wa Elimu Dodoma (MED), Luhaga Makunja alisema kuna idadi kubwa ya wasichana wanaoacha shule kutokana na sababu mbalimbali. Alisema shirika hilo lilikuwa likitekeleza mradi wa kutatua changamoto za unyanyasaji wa kijinsia katika elimu ya msichana ambapo eneo la mradi lilikuwa kata nne za Chibelela, Mapanga, Mtitaa, Mwitikila na Chipanga. Alisema mradi huo ulilenga watoto wetu umri kuanzia tisa hadi 19 ambao wako shuleni.“Ukatili mkubwa tuliouona ulikuwa ni kuachishwa masomo kutokana na mimba za utotoni,” alisema. Alisema kulingana na takwimu walizopata kutoka Idara ya Elimu wasichana 3,179 walioanza shule 2013 miongoni mwao 1,238 hawakumaliza kidato cha nne mwaka 2017 ambapo ni asilimia 39 sababu kubwa ikiwa ni mimba za utotoni. Makunja alisema tulikuwa na wasichana kutumikishwa kazi za majumbani ambapo wasichana wamekuwa wakiachishwa shule na kwenda mijini kufanya kazi za ndani kusaidia familia.“Bado kuna mila na desturi ambazo hazioni thamani ya mwanamke kwenye elimu hata inapofikia umri wa mtoto kuandikishwa shule suala la kusoma linaokana sio muhimu,” alisema. Makunja alisema umasikini, utumikishwaji wa watoto kusaidia familia, mazingira magumu shuleni kutokana na umbali kutoka makazi Hadi shuleni inaonekana ni kikwazo cha elimu kwa mtoto wa kike.“Kuna wanafunzi wanalazimika kwenda kupanga vijijini ili wawe karibu na shule, wanakosa ulinzi wa wazazi na kujikuta wakiingia kwenye ngono na hivyo wengi hujikuta wakikatisha masomo kutokana na ujauzito,” alisema. Pia alisema mazingira magumu ya nyumbani hupelekea watoto kufika shule wakiwa hawajala huku akitembea umbali mrefu kufika shuleni.“Anatoka nyumbani hajala anakaa muda mrefu na njaa, hata masomo haelewi vizuri anajua atafeli tu alishakata tamaa anaona amalize tu shule,” alisema. Makunja alisema ukosefu wa mabweni na chakula unasababisha watoto kutoshawishika kwenda shuleni.Alisema kumekuwa na mtazamo hasi wa wazazi na walimu juu ya elimu kwa wasichana. “Jitihada kubwa zinahitajika kuhakikisha elimu inatolewa ili kupunguza unyanyasaji wa kijinsia unaosababisha wasichana kukosa elimu,” alisema. Pia alisema wasichana wengi walikuwa hawashiriki katika maamuzi hata kwenye mipango ya shule na vijiji.
kitaifa
WAZIRI wa Kilimo Japhet Hasunga ametembelea na kujionea maandalizi ya Maadhimisho ya 27 ya Sikukuu ya Wakulima maarufu kama Nanenane.Maadhimisho hayo yana lengo la kuwatambua na kuwaenzi wadau wakuu wa sekta ya kilimo ambao ni wakulima, wafugaji, wavuvi, wanaushirika, wasindikaji wa mazao ya kilimo, mifugo, uvuvi na maliasili kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika kuendeleza uchumi wa nchi.Hasunga pamoja na mambo mengine akiwa katika Banda la Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), aliutaka uongozi wa taasisi hiyo kuongeza juhudi za utoaji elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa matumizi ya mifuko maalumu ya kuhifadhia nafaka ya PIC’S.Alisema NFRA inapaswa kutoa elimu hiyo ili iwafikie wakulima wengi kwani kufanya hivyo itarahisisha huduma za uhifadhi wa mahindi ya wakulima, ambao kwa muda mrefu wamekumbwa na kadhia ya kushindwa kuhifadhi mahindi kwa ufasaha.Pamoja na NFRA kutoa elimu kwa wakulima kupitia vipindi mbalimbali vinavyorushwa na televisheni, pia alisisitiza kuwa NFRA inapaswa kuongeza uwezekano wa kuwafikia wakulima wengi zaidi. Mwaka huu sherehe za Nanenane zinafanyika kitaifa mjini Bariadi katika Viwanja vya maonesho ya kilimo Nyakabindi katika Mkoa wa Simiyu. Waziri huyo aliupongeza uongozi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara kwa juhudi zao za kufanikisha kuingiza uwanjani huduma za msingi ambazo ni maji na umeme. Alisema jukumu hilo kwa serikali na wadau wa sekta binafsi ni kuendeleza viwanja hivyo vya Nyakabindi kwa kujenga mabanda ya maonesho ya kudumu, kuboresha huduma muhimu za kijamii ili kuwe na maonesho endelevu yenye sura ya kitaifa na Kimataifa.
kitaifa
BENJAMIN MASESE-MWANZA SERIKALI imepokea injini mbili kutoka Korea Kusini ambazo zitafungwa kwenye meli mpya ya MV Mwanza, huku ikizindua pia safari za ndege kusafirikisha minofu ya samaki kwenda nchini Uholanzi ambapo Shirika la ndege la Rwanda litakuwa likiisafirisha. Mbali na kuzindua usafirishaji huo wa samaki, pia imetangaza kwamba sasa uwanja wa ndege wa Mwanza unakuwa wa kimataifa. Meli Akizungumza jijini Mwanza jana baada ya kuzindua safari za ndege na kupokea injini hizo, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Isaack Kamwelwe, meli inayotengenezea jijini Mwanza itakuwa ikifanya za Mwanza-Bukoba na nchi jirani za Kenya na Uganda Alisema meli hiyo inayogharimu Sh bilioni 159 inatarajia kukamilika na Januari 2021 na kuwataka wakandarasi  ambao ni  Gas Entec Co. Ltd, Kangnam Corporation zote kutoka Korea ya Kusini zikishirikiana na Suma JKT ya Tanzania kuhakikisha zinakamilisha shughuli hiyo  kama mkataba unavyoelekeza.  “Meli hii itakuwa kubwa kuliko meli zote katika ukanda huu wa maziwa makuu, itakuwa na mita 92.6, kimo chake kitakuwa mita 11.2, upana mita 17 na uzito wa tani 3,500 kwa takwimu hizo ndio itakuwa meli kubwa kuliko zote na itakuwa inatumia masaa saba kutoka Mwanza hadi Bukoba,”alisema. Akitoa ufafanuzi wa injini hizo, Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania (MSCL), Erick Hamisi, alisema injini hizo zimenunuliwa kwa Dola za Marekani 39,000,000 sawa na Sh bilioni 89.764  na kila moja ina tani 35 na uwezo wa kuzaliza KW 2,380. Alisema uwezo huo wa injini utaiwezesha meli hiyo kusafiri kwa saa sita kutoka Mwanza hadi Bukoba na kwamba hadi sasa wakandarasi hao wamelipwa Sh bilioni 55.618 sawa na asilimia 64 ya gharama zote. “Kila injini itakuwa na uwezo wa kutumia mafuta lita 9,300 kutoka Mwanza hadi Bukoba, hivyo kwa injini mbili zitatumia lita 18,600  kwa kusafirisha abiria 1200, tani 400 za mizigo na magari madogo 20 lakini meli hii  itakuwa na madaraja sita, daraja la uchumi abiria 834, daraja la biashara abiria 200, darala la pili la kulala abiria 100, darala la kwanza abiria 60 na daraja la hadhi ya juu abiria wanne, mwisho ni VIP abiria wawili. Safari za ndege Katika hatua nyingine Kamwelwe alizindua safari za Mwanza hadi hadi Uholanzi katika kwa kutumia shirika la Ndege ya Rwanda ambapo  jana ilisafirishwa tani  nane za minofu ya samaki huku akifafanua kwamba kila wiki kutakuwa na safari moja. Kutokana na safari hizo, amewaagiza wakuu wa mikoa ya Mwanza, Mara, Simiyu na Kagera kuunda mtandao wa pamoja wa kuhakikisha samaki wote wanaletwa kwenye viwanda ili kurahisisha upatikanaji wa minofu hiyo na kufikishwa uwanja wa kimataifa wa Mwanza.
kitaifa
Na NORA DAMIAN-DAR ES SALAAM CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimelituhumu Bunge kwa madai ya kuvunja sheria kwa kuomba fedha za ziada nje ya bajeti yake iliyoidhinishwa bila kupitisha maombi hayo bungeni kama katiba inavyotaka. Chadema imesema Bunge limevunja katiba, ibara ya 137 (3), (a) na (b) huku wakidai pia Waziri wa Fedha amevunja ibara ya 136 na 137 (3) kwa kutoa fedha za ziada nje ya bajeti iliyopitishwa. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chadema, Dk. Vincent Mashinji, alisema kati ya Juni 21 na Agosti 15, mwaka huu, Katibu wa Bunge aliandika barua tatu tofauti akiomba zaidi ya Sh bilioni 9 kwa Waziri wa Fedha na kwa Katibu Mkuu Hazina kugharimia bajeti ya ziada. “Tangu wakati huo hadi Agosti 15, Serikali ilishatoa shilingi bilioni 7 kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina bila kufuata masharti ya katiba na inategemewa itaendelea kutoa shilingi bilioni 2.5 kulipia gharama za posho ya jimbo ya Juni ambayo haijalipwa kwa ukamilifu,” alisema Dk. Mashinji. Alisema fedha zilizotolewa kama bajeti ya ziada zilitumika kulipa posho za jimbo, kujikimu, vikao, saa za ziada kwa watumishi na posho ya kamati maalumu kwa kipindi cha Mei hadi Juni. “Katiba inamtaka waziri kuwasilisha bungeni maombi ya bajeti ya ziada na baada ya Bunge kuyakubali, atawasilisha bungeni Muswada wa Sheria ya Matumizi ya Fedha za Serikali kuidhinisha matumizi ya fedha kutoka Mfuko Mkuu wa Hazina ya Serikali. “Hatutaki kuamini kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amehusika kuidhinisha malipo haya, maana hata kwenye mawasiliano yaliyopo hajawahi kupewa nakala,” alisema. Alisema Bunge likiwa kama mhimili unaojitegemea, linapaswa kujiendesha bila kuwa tegemezi kwani ndilo linalopitisha bajeti yake na ya Serikali. Alisema katika mwaka wa fedha wa 2016/17 Bunge liliidhinisha Sh bilioni 92.7 kwa matumizi ya kawaida, Sh bilioni 23.80 mishahara, Sh bilioni 68.27 matumizi mengineyo na Sh bilioni 7 miradi ya maendeleo. “Bunge ni taasisi ambayo kalenda yake na idadi ya wajumbe vinafahamika, hivyo wanapopitisha bajeti wanakuwa wakijua ni kiasi gani kitahitajika katika mwaka husika wa fedha. “Tukianza kupuuza katiba, maana yake tunarudi kwenye hali ya kuangalia nani ana nguvu na ataamua nini kukicha,” alisema. Dk. Mashinji alisema pia uendeshaji wa shughuli za Bunge umekuwa ukiichanganya jamii na alitahadharisha kuwapo hatari ya kutengeneza nchi isiyofuata na kuzingatia taratibu. “Kuna udhaifu mkubwa katika uongozi wa Bunge ukiongozwa na Spika. Kiongozi jasiri ahitaji kuongea kwa sauti kali, kutumia nguvu kubwa ama ubabe bali ni yule anayefuata taratibu tulizojiwekea. “Ajipe muda kutafakari je, uongozi wake unaleta hali ya utengamano ama utavuruga jamii… kipimo cha uimara wa kiongozi ni kusimamia katiba,” alisema Dk. Mashinji. Chadema imeitaka Serikali na Bunge kutoa majibu ya kina kuhusu ukiukwaji na uvunjwaji wa katiba na wale wote waliohusika wachukuliwe hatua kwa mujibu wa sheria. “Tunaamini kuwa haya yanaweza kumalizika kama tutakuwa na katiba mpya iliyotokana na maoni ya wananchi, tutatumia njia za kidemokrasia na kidiplomasia kuhakikisha tunapata mwafaka wa katiba mpya. Endapo hazitazaa matunda tutaomba wananchi wafanye maamuzi,” alisema. Kutokana na madai hayo ya Chadema MTANZANIA lilimtafuta Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila ili kupata ufafanuzi, lakini simu yake ya mkononi iliita bila kupokewa.
kitaifa
VYAMA vya siasa nchini vimetakiwa kutekeleza matakwa ya sheria ya msajili wa vyama vya siasa ambayo inavitaka vyama hivyo kuzingatia uwepo wa Muungano katika katiba za vyama vyao ikiwa ni moja ya tunu ya taifa.Akizungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu ya miaka 55 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Naibu Msajili wa Vyama vya Siasa, Mohamed Ali Ahmed alisema muungano ndiyo utambulisho wa taifa la Tanzania. Alisema sheria ya vyama vya siasa imetambua umuhimu wa kuwepo kwa muungano katika katiba za vyama hivyo kwa ajili ya kupata viongozi ambao watafahamu umuhimu wa muungano.Alisema marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019 kifungu cha 6 (5) unavitaka vyama vya siasa vyenye usajili nchini katika maandalizi ya katiba zao na sera kuzingatia suala la muungano kama kipaumbele cha kwanza. Aidha katika marekebisho ya sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 2019 pia umevitaka vyama vilivyopata usajili kuyatambua Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 kuwa ndiyo yaliyowakomboa wananchi wa Zanzibar na wazalendo kushika hatamu ya kuongoza dola. ‘’Katika marekebisho ya sheria ya msajili wa vyama vya siasa suala la kuyaenzi Mapinduzi ya Zanzibar limetambuliwa rasmi kwa lengo la wanachama na wananchi kwa ujumla kuyatambua kwa mujibu wa sheria,’’alisema.Mambo mengine ya msingi ambayo yametakiwa kutambuliwa na kuingizwa katika katiba na sera za vyama vya siasa ni mwenge wa uhuru, demokrasia na utawala bora. Akifafanua zaidi kuhusu Mwenge wa Uhuru, alisema upo kwa ajili ya kujenga umoja na mshikamano wa wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ndiyo maana hutembezwa nchini kote. Alisema Mwenge wa Uhuru hata muundo wake umewekwa alama ya Adamu na Hawa ambayo ni nembo rasmi ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ukionesha ushirikiano wa pamoja.
kitaifa
WIKI hii, Julai 1, Benki ya Dunia iliingiza Tanzania katika kundi la nchi zenye kipato cha kati. Hizi ni habari njema hata pamoja na kwamba wapo wanaoona kuna mapungufu fulani fulani katika utendaji. Hatua ya kutoka katika umaskini na kupanda kwenda katika hatua nyingine ya juu huusisha suala zima la uchumi au maendeleo ya kiuchumi. Lakini pamoja na hayo maendeleo ya kiuchumi huguswa na vitu au mambo mengi mfano kutenda haki, amani, usalama, utulivu nakadhalika. Mtu yeyote anapokuwa katika mazingira yenye kutenda haki, amani, utulivu humwezesha kufanya kazi kwa bidii na hatimaye kuwa mzalendo kwa nchi yake ikiwa ni pamoja na kulipa kodi. Sasa mazingira yanapokuwa tofauti na hayo, ndiyo ambayo yanachangia kwa kiasi kikubwa kurudisha nyuma maendeleo ya nchi . Kwa sababu hiyo sisi tunaweza kusema tumekuwa mabalozi wazuri wa kusisitiza suala la haki kila wakati, kwa sababu tumekuwa tukiamini haki ni msingi wa mambo yote mazuri. Na ndio maana tumekuwa tukikosa na wakati mwingine kukumbusha kutenda haki hasa katika vyombo vile vya kimaamuzi na kiutendaji. Tumekuwa tukisisitiza kwamba vyombo hivyo vinapaswa kutambua wajibu wao kuwa ni kutafuta namna ya kutatua matatizo na si kuyaongeza. Yapo baadhi ya matukio si yote ambayo yamefanywa na vyombo hivyo na hivyo kutoa taswira ya kukomoa au kuumiza baadhi ya watu kwa makusudi. Tumekuwa tukisisitiza  hayo kutokana na kuwapo kwa ripoti ambazo zinaonyesha kuwa barani Afrika kwa muda mrefu sasa watu wameumizwa na vitendo vya kudhulumiwa haki zao msingi. Kwa mujibu wa ripoti hizo hata kutopea katika umaskini wa kimawazo, na hivyo wengi kuhadaika na kauli za wanasiasa, viongozi na watu wenye nafasi katika jamii, msingi wake ni dhuluma ya haki zao za msingi.  Kwa misingi kama hiyo sisi kama  chombo cha habari  tunao wajibu wa kukumbusha kwamba vyombo hivyo kila inachofanya kabla ya kutoa uamuzi wowote basi vitambue vinao wajibu wa kuchunguza, kusikiliza, kubadilisha na kuboresha. Zipo nyakati tumeshuhudia vyombo hivi vikichukua uamuzi wa ghafla hata katika masuala nyeti sana katika mifumo ya sheria, utumishi nk.  Vyombo hivi vinapaswa kutambua kwamba chochote kitakachofanyika bila kufuata misingi hiyo tuliyoitaja hapo juu kitakwenda kuathiri mustakabali mwema wa Taifa letu. Wakati fulani aliyepata kuwa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Baba Mtakatifu Benedikto wa XVI, alitoa changamoto kubwa kwa watawala wa dunia.  Kwa maneno yake mwenyewe alisema; “jamii yenye haki hujengwa na wanajamii wenye haki”.  Maana yake tukitaka kujenga jamii yenye haki hatuna budi sisi wenyewe kuwa wenye haki. Kiongozi huyo alikwenda mbali na kusema; wao kama kanisa hawana mbinu za kiufundi wala nafasi ya kuingilia mambo ya siasa moja kwa moja lakini alibainisha wazi utume ambao alisema kama kanisa haliwezi kuuacha hata kidogo ni ule wa kuutangaza ukweli. Ukweli si jambo ambalo linapaswa kubebwa na taasisi zetu za kidini tu bali hata katika serikali zetu na taasisi zake, mahakama zetu, vyombo vya ulinzi na uslama kama Jeshi la Polisi,  Bunge nk. Kuna msemo mmoja kwamba; ukweli ndio utakaowaweka watu wote huru: iwe katika siasa au katika nyanja yoyote ya kijamii.  Kwa sababu hiyo tunaamini ujenzi wa jamii yenye misingi ya haki ni wajibu wetu sote lakini serikali, mahakama na Bunge linawajibika kujenga dhamira hiyo.  Mahakama itambue kama ni taasisi ya kupigania haki, serikali ni wakala wa haki vivyo hivyo hata Bunge.  viongozi  wakiwamo wale wa kisiasa, na wananchi watambue kuwa wao ni wawajibikaji katika shughuli za kijamii na iwapo wote hawa watauzingatia ukweli ndani ya dhamiri zao zilizojengwa juu ya ukweli na ukweli tupu, basi jamii ina uhakika wa kujenga haki na amani na matokeo ya hayo ni kupaa kimaendeleo.
uchumi
  Na UPENDO MOSHA-ROMBO KIFO cha Mwanafunzi wa Chuo cha Usafirishaji (NIT), jijini Dar es Salaam, aliyeuawa kwa kupigwa risasi juzi, Akwilina Akwilini, kimezua simanzi nyumbani kwao, Kijiji cha Marangu Kitowo, Kata ya Olele, Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, huku wazazi wake wakitoa ujumbe mzito kwa Serikali. Kutokana na hali hiyo wameitaka Serikali itoe maelezo ya kina kuhusu mauji ya ovyo ya raia wasiokuwa na hatia sambamba na kutaka uchunguzi huru na waliohusika na mauji ya mtoto wao wachukuliwe hatua za kisheria. MTANZANIA ilifika nyumbani kwao marehemu jana na kutembelea maeneo mbalimbali ya kijiji hicho, alishuhudia watu walivyokuwa na simanzi na jinsi walivyokuwa wakizungumzia kifo hicho. Akizungumza na MTANZANIA nyumbani kwake, mama mzazi wa marehemu, Constansia Akwilini, alisema familia yake imepokea tukio hilo kwa mshtuko wa aina yake. “Huu ni msiba uliogusa moyo wangu sana na familia yetu kwa ujumla nashindwa nikuelezeeje. “Kitendo hiki hakipaswi kufumbiwa macho, haya ni mauaji ya ovyo ya raia wasiokuwa na hatia na yanapaswa kupingwa kwa nguvu zote ili kulinda amani na usalama wa nchi yetu. “Kifo hiki kimeacha pengo kubwa katika familia yetu kwa sababu huyo ndiye mtoto pekee tuliyekuwa tukimtegemea katika familia yetu kwa siku zijazo kwa sababu ndiye aliyekuwa na mwelekeo wa kusoma,” alisema Constansia huku akitokwa na machozi. Kwa mujibu wa mama huyo, Akwilini alifikia hatua hiyo kielimu kutokana na ufadhili wa shangazi yake na kwamba alikuwa ni mtoto wa sita kuzaliwa kati ya watoto wanane wa familia hiyo. BABA MZAZI ATOA NENO Akizungumzia historia ya marehemu baba mzazi wa marehemu, Akwilini Shirima, alisema Akwilina alizaliwa Aprili Mosi, mwaka 1996, katika Kijiji cha Marangu Kitowo, Kata ya Olele, wilayani Rombo. Alipata elimu yake ya msingi katika Shule ya Msingi Kitongoria na kuhitimu mwaka 2009. Baada ya hapo, Akwilina alijiunga na shule moja ya sekondari iliyoko mkoani Iringa ambako alihitimu mwaka 2014. Baadaye, alichaguliwa kujiunga na masomo ya kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Embauwai, iliyoko Wilaya ya Ngorongoro, mkoani Arusha. Kwa mujibu wa mzazi huyo, Akwilina hakumaliza kidato cha sita shuleni hapo kwani baada ya afya yake kudhoofika mara kwa mara kutokana na hali ya hewa ya Ngorongoro, alihamia mkoani Iringa ambako alihitimu kidato cha sita, mwaka 2016 Kuanzia Oktoba mwaka jana hadi alipofikwa na mauti, Februari 16, mwaka huu, alikuwa mwanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), akisomea shahada ya kwanza ya ugavi na ununuzi. TABIA YA MAREHEMU  Akizungumzia tabia ya binti yake huyo, Akwilini alisema mtoto wake alikuwa ni mtu mwenye misimamo ya kimaisha na alipenda kuzungumza na kucheka na kila mtu. “Watu wanasema mtu akishakufa ndiyo tunamzungumzia vizuri, lakini mwanangu alikuwa ni mcheshi, asiyependa kugombana na watu. “Alipenda kazi na kusoma na pia alikuwa na misimamo ya kimaisha na niliamini kama angefanikiwa kuishi zaidi, angetusaidia kuondokana na umasikini kwa sababu ndiye mtoto pekee aliyesoma kati ya watoto wangu wanane,” alisema. DADA WA MAREHEMU Naye dada wa marehemu, Teddy Akwilini, alisema alizungumza na mdogo wake, Februari  12 na 15, mwaka huu ambapo walizungumzia masuala ya maisha na kuwaahidi kwenda Rombo kuwatembelea, Julai mwaka, huu baada ya kufunga chuo. “Aliniambia anatamani sana kuja nyumbani na kasema Julai angekuja kutuona maana alikuwa amewakumbuka baba na mama. “Nakumbuka aliniambia alikuwa akitafuta sehemu ya kufanyia masomo yake kwa vitendo, lakini inaniuma sana, kwamba amefariki bila kutuona na atakuja akiwa kwenye jeneza. “Mimi ndiye mtoto wa kwanza katika familia yetu na kwa bahati mbaya mimi na wengine hakutubahatika kusoma zaidi ya darasa la saba kutokana na ufukara wa familia yetu. “Kwa hiyo, kifo cha mdogo wangu ni pigo kubwa sana tena sana katika familia yetu kwa sababu kila mmoja alikuwa akimtegemea na tulikuwa tukimwombea kila siku kwani alikuwa na ndoto nyingi za kutubadilisha kamaisha,” alisema dada huyo huku akibubujikwa na machozi. MAJIRANI WAZUNGUMZA Mmoja wa majirani wa Akwilina, Dismas Shirima, alisema marehemu alikuwa ni mtu wa watu na alikuwa ni mtu wa kupenda kuwasaidia ndugu zake. Kwa upande wake, jirani mwingine, Fausta Focus, alisema marehemu alikuwa ni mfano wa kuigwa kijijini hapo kutokana na tabia yake ya kupenda kujitolea katika shughuli mbalimbali za kijamii. SERIKALI KUGHARIMIA MAZISHI Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako amesema wizara yake itagharimia mazishi ya mwanafunzi huyo aliyeuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Ndalichako alisema yeye pamoja na katibu mkuu wa wizara yake, watasimamia shughuli zote za msiba huo. “Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa kifo cha mwanafunzi huyu na alikuwa miongoni mwa wanafunzi wa kike waliojipambanua  kwa kujua umuhimu wa elimu, alihakikisha anasoma kwa bidii kwa manufaa yake na familia yake, lakini pia alikuwa miongoni mwa wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu. “Kifo chake kimeleta simanzi kwa wananchi wote na Serikali kwa ujumla alikuwa katika majukumu yake ya kawaida akipeleka barua yake ya mafunzo kwa vitendo Bagamoyo ndipo umauti ukamkuta,” alisema Profesa Ndalichako. Kutokana na tukio hilo, Profesa Ndalichako alivitaka vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua hatua stahiki kwa wahusika. Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamad Yusuph Masauni, alisema Serikali haiwezi kuyaacha matukio hayo yapite kama yalivyo, hivyo imeyachukulia kwa uzito unaostahili. Masauni alisema uchunguzi wa tukio hilo utafanyika haraka iwekezanavyo, kwa weledi na utaalamu ili haki itendeke. “Tutafanya uchunguzi na kuwachukulia hatua kali za kisheria wote watakaobainika kuhusika na tukio hilo, Serikali tunasikitishwa na kifo cha mwanafunzi huyu, pia na kujeruhiwa raia,” alisema Masauni. Alisema uchunguzi huo utakuwa mpana na utakuwa fundisho kwa kuwachukulia hatua kali za kisheria. ASKARI SITA WASHIKILIWA Baada ya tukio hilo la kuuawa kwa mwanafunzi huyo Jeshi la Polisi limtangaza kuwashikilia askari wake sita ambao wanadaiwa kuhusika na tukio hilo la mauaji ya mwanafunzi huyo. Mwanafunzi huyo, aliuawa juzi jioni kwa risasi wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), waliokuwa wakielekea kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi, Jimbo la Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa Polisi, Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro  Mambosasa, alisema mbali na kuwashikilia askari hao, pia wamewakamata wafuasi 40 wa Chadema. Pia, alisema wanaendelea kuwatafuta viongozi wa chama hicho, walioshiriki kushawishi maandamano hayo. “Februari 16, mwaka huu, Chadema walikuwa na mkutano wa kufunga kampeni katika Viwanja vya Buibui, Mwananyamala ambapo Mwenyekiti wao Mbowe, alisikika akikatisha mkutano na kuhamasisha wafuasi wao kuingia Kinondoni ili kumshinikiza mkurugenzi awape barua za viapo vya mawakala wa chama hicho. “Pia Mbowe alisikika akiwatukana viongozi wakuu wa nchi akiwa jukwaani, suala hili linaendelea na uchunguzi wake. “Kadiri wanachama hao walipokuwa wakisogea mbele, idadi ya waandamanaji iliongezeka na walipofika Barabara ya Kawawa, maeneo ya Mkwajuni, walifunga barabara ya mabasi ya mwendo kasi na ya kawaida na kusababisha msongamano mkubwa wa magari. “Polisi walifika katika eneo la tukio na kuzuia maandamano hayo, lakini ghafla wafuasi wa Chadema walianza kuwashambulia askari kwa mawe na chupa, fimbo na silaha zingine za jadi na kuwajeruhi askari wawili. “Katika harakati za kujihami na mashambulizi  yaliyozidi, polisi walitumia silaha za kutuliza ghasia, lakini nazo zilionekana kushindwa kuwatawanya waandamaji hao, ndipo walipiga risasi za moto hewani na kufanikwa kuwakamata watuhumiwa 40 na kutawanya maandamano hayo. “Siku hiyo hiyo, saa 1:30 usiku, polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ilipata taarifa za kiintelijensia, kwamba katika purukushani hizo, kuna mwanamke mmoja alipoteza maisha na mwili wake umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala. “Pamoja na kuendelea na uchunguzi wa kifo cha mwanafunzi huyo, tumepata taarifa zingine, kwamba watu wawili walijeruhiwa maeneo ya miguuni na kitu chenye ncha kali ambao ni Erick John (24) na Innocent Mushi (23),” alisema Kamanda Mambosasa. JPM AAGIZA UCHUNGUZI Rais Dk. John Magufuli, amesikitishwa na kifo cha mwanafunzi huyo na kutoa pole kwa familia, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huo. “Nimesikitishwa sana na kifo cha mwananafunzi Akwilina Akwilini wa chuo cha NIT, natoa pole kwa familia, ndugu, wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huo. “Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili,” aliandika Rais Magufuli katika ukurasa wake wa twitter. MTANDAO WA WANAFUNZI Wakati huo huo, Mtandao wa Wanafunzi Tanzania (TSNP), umesema utafungua kesi ya madai dhidi ya Jeshi la Polisi nchini kutokana na kifo cha mwanafunzi Akwilina. Akizungumza jana waandishi wa habari, Mwenyekiti wa TSNP, Abdul Nondo, alisema watafungua kesi hiyo kwa kushirikiana na wanasheria wa taasisi mbalimbali ili iwe fundisho kwa askari wengine. Alisema kwamba, sheria ya Jeshi la Polisi na Huduma Saidizi, sura ya 332, kifungu cha 29, kinaeleza mazingira ambayo polisi wanatakiwa kutumia nguvu kutuliza ghasia. “Kama mwanafunzi huyu asiye na hatia ameuawa kwa mazingira ya namna hii, TSNP tunaona kuwa hili ni shambulizi dhidi ya wanafunzi nchini bila sababu yoyote. “Tunataka hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya askari polisi waliotenda unyama huu na kukatisha haki ya kusoma na ya kuishi kwa mwanafunzi mwenzetu. “Polisi, wamekiuka maadili ya kazi yao katika kulinda amani, Jeshi la Polisi, lijitathmini upya na kujipima namna linavyoenenda na kama lipo kwa ajili ya kulinda usalama wa raia,” alisema Nondo. Mtandao huo pia umemtaka Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk. Mwigulu Nchemba kujiuzulu ili kuonyesha uwajibikaji. “Tumeshuhudia watu wakipigwa risasi, kutekwa, miili kuokotwa kandokando ya bahari na haya yote yanatokea pasipokuwapo kwa uchunguzi wa kina. “Tanzania tumekuwa na chunguzi nyingi zinazoendelea na hadi sasa hazina majibu. Hivyo basi, sisi hatuamini kama uchunguzi pekee ndiyo utakuwa chachu ya kukomesha matendo yanayoendelea nchini. “Ni muda muafaka sasa, waziri husika (Dk. Nchemba), kujiuzulu kama njia ya kuonyesha uwajibikaji kama alivyowahi kujiuzulu, Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi, wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani. “Lakini niwaambie kwamba, kama matukio ya aina hii yataendelea, basi tutaitisha maandamano ya wanafunzi ya vyuo vyote nchini kulalamikia uvunjwaji wa haki za binadamu,” alisema Nondo. Naye Mwalikishi wa Klabu za Haki za Binadamu nchini, Alfahad Thabo, alisema hivi sasa wana mashaka na usalama wao kwa sababu vitendo hivyo vimekuwa vikijirudia mara kwa mara. ACT  WAMVAA MWIGULU Nayo ngome ya Vijana wa Chama cha ACT Wazalendo, imemtaka Dk. Mwigulu ajiuzulu kutokana na kuongezeka kwa matukio ya mauaji nchini. Pia, ngome hiyo imewataka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro na Kamanda Mambosasa, nao wajiuzulu. Aidha ngome hiyo imewataka viongozi wote wa vyama vya upinzani kushirikiana na kuitisha maandamano nchi nzima ili kupinga mauaji, utekaji watu na ubakwaji wa demokrasia. Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Ngome hiyo, Likapo Likapo, alisema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuongezeka kwa matukio ya mauaji, utekaji na kupotea kwa watu huku jeshi hilo likishindwa kutoa taarifa za kina. CHADEMA WATUPA MZIGO Mkurugenzi wa Operesheni na Mafunzo wa Chadema, Kigaila Benson aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa mtu wa kwanza aliyesababisha kifo cha Akwilina ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Kinondoni, Aron Kagurumjuli kwa kukataa kutoa viapo kwa mawakala wao. Kigaila alisema polisi siku hiyo walilenga kuwapiga risasi viongozi wakuu wa chama hicho kwa sababu majeruhi wote wanne ambao wako hospitali ni walinzi wa viongozi hao. “Tulikuwa na msafara siku ile kwa sababu tulikuwa tunakwenda kwa mkurugenzi kudai viapo vya mawakala wetu hivyo mtu wa kwanza alisababisha kifo cha huyu mwanafunzi ni msimamizi wa uchaguzi. “Risasi iliyopigwa ikamwua yule mwanafunzi Mambosasa (Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa) anasema ni moja halafu wamekamata askari sita, sasa askari wote hao walipiga risasi moja na aliyeamuru risasi zipigwe juu ni nani? “Risasi zile zililenga viongozi wa chadema ndio maana waliopatwa ni walinzi wao. Watu wanne wote waliopigwa risasi ukiachana na huyo mwanafunzi wako hospitali wamepigwa sehemu za nyonga na miguu,”alisema Kigaila. Kwa upande wake Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema alisema chama hicho kinatoa pole kwa familia ya marehemu na kwamba tayari Mbunge wa Kibamba, John Mnyika na Meya wa Ubungo wametangulia nyumbani kwa ndugu wa mwanafunzi huyo eneo la Kibamba. “Kwa sasa kina Mnyika wametangulia nyumbani kwa ndugu ambao walikuwa wakimlea marehemu baada ya hapo tutawaeleza ushiriki wetu kwenye msiba huu mzito. “Jeshi la polisi lichukue hatua waache visingizio, tumechoka na mauaji haya…tumechoka viongozi wetu kuwindwa kama digidigi ,”alisema Mrema. Alieleza kushangazwa kwa hatua ya Kamanda Mambosasa kumtafuta Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe wakati hajajificha na kwamba hajapewa wito wowote wa kwenda kuripoti polisi. “Wanazo taratibu za kumwita mtu polisi, wanafahamu nyumbani kwake, ofisini kwake makao makuu ya chama au ofisi za Bunge,”alisema. HABARI HII IMEANDALIWA NA UPENDO MOSHA (KILIMANJARO), Asha Bani, Nora Damian, Elizabeth Hombo na Tunu Nassor (DAR)
kitaifa
Inatarajiwa kuwa fedha hizo za kigeni zitokanazo na kahawa, ni kutoka Dola za Marekani milioni 230 kwa sasa na kufikia Dola milioni 325 kwa mwaka 2020.Taarifa ya Bodi ya Kahawa (TCB) mjini Moshi juzi imeeleza kuwa uzalishaji kwa sasa umeongezeka kutoka tani 55,000 mwaka 1983/84 hadi kufikia zaidi ya tani 75,000 za Kahawa.Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa zaidi ya kaya 400,000 zinajihusisha na kilimo cha mibuni aina ya Robusta na Arabika nchini.Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakulima hao huchangia asilimia 90 ya uzalishaji wote huku asilimia 10 ya kahawa ikitokana na wakulima wanaomiliki mashamba makubwa (Estate).TCB imesisitiza kuwa hivi sasa kilimo cha mibuni nchini hutoa ajira kwa Watanzania milioni 2.4, ambapo kahawa aina ya robusta huchangia asilimia 40 ya uzalishaji wa kahawa hapa huku arabika ikichangia asilimia 60 Taarifa hiyo imeeleza kuwa zaidi ya hekta 265, 000 nchini ndizo zinazotumika kwa kilimo cha zao hilo katika maeneo mbalimbali ya nchi.Aidha, imeelezwa kuwa kilimo cha mibuni kinakabiliwa na changamoto nyingi zikiwemo za kukidhi mahitaji makubwa ya miche.Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na TCB kuongeza upatikanaji wa miche ya uhakika ya aina bora ya mibuni ya arabika na robusta, ambapo mkazo unapaswa ulenge kuzalisha miche milioni 75, ili kupanda eneo la hekta 56,000 ndani ya miaka mitano ijayo.
uchumi
Kwa mujibu wa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga Jerry Muro, kikosi kitakachoondoka sio 21 na sasa hata wale waliopangwa kuachwa yaani Antony Mateo, Geofrey Mwashiuya na Benedikti Tinoco watakwenda na kufanya idadi ya wachezaji jumla kufikia 24.Awali, walitangaza kuondoka juzi kwa ndege ya Shirika la Ndege ya Afrika Kusini lakini ilishindikana baada ya shirika hilo kushindwa kuwapatia ndege ya kuunganisha mapema mjini Johannesburg kwenda Curepipe na hivyo wakaamua kukodi ndege ambayo itawasubiri baada ya mechi kesho na kuwarudisha.“Safari imeiva, jumla ya wachezaji 24 wataondoka kuelekea Mauritius wakiongozana na viongozi saba wa benchi la ufundi, kikosi kimekamilika tunaomba mashabiki waiombee timu ifanye vizuri,” alisema Muro.Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Jumamosi kuanzia Saa 9:30 alasiri kwa saa za Mauritius Uwanja wa Curepipe kabla ya timu hizo kurudiana wiki mbili baadaye Dar es Salaam. Kikosi hicho jana kilifanya mazoezi ya mwisho kwenye uwanja wa Chuo cha Polisi Kurasini.Lengo la kwanza lililowekwa na timu hiyo ni kufika katika hatua ya makundi. Kocha wa Yanga Pluijm alisema kikosi kimejipanga na kiko tayari kwa mapambano.Alisema mbinu atakazotumia hazina tofauti na zile ambazo amekuwa akitumia kwenye Ligi Kuu Tanzania bara.Mkuu wa Msafara wa Yanga katika safari hiyo ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Ayoub Nyenzi wakati upande wa viongozi wa timu hiyo wanaokwenda ni Kaimu Katibu Mkuu, Baraka Deusdedit na Muro.Kikosi kitakachoondoka leo ni Makipa; Ally Mustafa ‘Barthez’, Deo Munishi ‘Dida’ na Benedicto Tinocco.Washambuliaji ni; Malimi Busungu, Paul Nonga, Amissi Tambwe (Burundi) na Donald Ngoma (Zimbabwe).Mabeki; Juma Abdul, Mbuyu Twite (DRC), Oscar Joshua, Mwinyi Mngwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Vincent Bossou (Togo) na Pato Ngonyani huku Viungo ni; Said Juma ‘Makapu’, Salum Telela, Thabani Kamusoko (Zimbabwe), Haruna Niyonzima (Rwanda), Simon Msuva, Issoufou Boubacar (Niger), Godfrey Mwashiuya na Deus Kaseke.Kikosi hicho kitakaporejea kitakwenda moja kwa moja kuweka kambi Pemba kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya watani wao Simba utakaochezwa Februari 20, mwaka huu.
michezo
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amewaagiza wakuu wa mikoa, wilaya na viongozi wengine kuhakikisha wanasimamia uanzishwaji wa Kamati za Ulinzi wa Wanawake na Watoto katika ngazi za mikoa, halmashauri, kata na vijiji. Alisema maelekezo hayo yapo katika mwongozo wa uratibu wa Mpango wa Taifa wa Kutotokemeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.Waziri Mkuu Majaliwa vile vile aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini kuanzisha programu za kijamii za kutokomeza ukatili wa kijinsia katika halmashauri husika zitakazozingatia hali halisi na kuzitengea bajeti kama ilivyoelekezwa kwenye mpango huo wa kitaifa .Alisema serikali imefanya mambo mengi katika kutukomeza ukatili huo, lakini pia inatumia gharama nyingi katika kushughulikia waathirika wa ukatili wa kijinsia ambapo fedha hizo zingeweza kutumika katika kutoa huduma nyingine katika jamii.“Kimsingi, Serikali ya Awamu ya Tano haiwezi kuvumilia vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwa vinaathiri maendeleo yetu na kusababuisha uvunjivu wa amani,” alisema. Alisema serikali tayari imeanzisha madawati 415 kwa ajili ya kuhudumia waathirika wa ukatili, lakini akalitaka Jeshi la Polisi nchini kuongeza huduma hiyo kwa kushughulikia ukatili wa kijinsia dhidi ya watu wenye ulemavu.Waziri Mkuu akizungumzia vitendo vya ukatili wa kijinsia unatumika mitandano, alizitaka kampuni za simu kudhibiti na kuwachukulia hatua kali wote wanaotumia mitandano kudhalilisha na kutukana wengine. Pia aliitaka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kusimamia kikamilifu wale wote wanaojidanganya kwamba kuna mitandao haionekani na kuhakikisha wanaendesha vitendo vya udhalilishaji wakamatwe na kushughulikiwa. Pia alizitaka taasisi kama Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) kuendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao wanatumia mitandao kwa nia ya kudhalilisha watu wengine.
kitaifa
Wakati mabingwa watetezi wa Ligi kuuya soka Tanzania bara Simba wakishusha kipigo cha goli 3 kwa bila dhidi ya Mtibwa wakiwa ugenini watani zao Yanga wameshindwa kutamba nyumbani. Katika mchezo uliopigwa uwanja wa uhuru Yanga ambayo maskani yake ni Jangwani jiji Dar es Salaam imeshindwa kutamba na kujikuta ikiambukia droo ya goli 1 kwa 1 dhidi ya Mbeya City. Mbeya City walianza kuongoza katika mchezo huo baada ya beki wa Yanga Lamine kujifunga goli dakika ya 42 ya mcgezo huo ulioanza saa 1 jioni katika uwanja wa uhuru. 'Bao la kujitundika', Lamine Moro alipowazawadia Mbeya City. 60' | Yanga SC 0-1 Mbeya City. LIVE #AzamSports2 #LigiKuuTanzaniaBara #VodacomPremierLeague #VPLUpdates #VPL #YangaSC #MbeyaCity #YangaMbeya @yangasc @baraka_mpenja @officialmbeyacityfc @antonionugaz A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Feb 11, 2020 at 9:16am PST Hata hivyo kipenzi cha wanajangwani Bernard Marrison alifanikiwa kuisawazishia Yanga kwa bao la kichwa Dakika ya 72 ya mchezo huo ambao ulijawa na shamrashamra kwakuwa Yanga ilikuwa inaadhimisha miaka 85 tangu kuanzishwa kwake. Bao la Wananchi, Bernard Morrison alipoisawazishia Yanga kwa assist ya Juma Abdul tena. FT: Yanga SC 1-1 Mbeya City. #AzamSports2 #LigiKuuTanzaniaBara #VodacomPremierLeague #VPLUpdates #VPL #YangaSC #MbeyaCity #YangaMbeya @yangasc @baraka_mpenja @officialmbeyacityfc @antonionugaz A post shared by Azam Sports (@azamsports2) on Feb 11, 2020 at 10:18am PST Yanga ilitawala mchezo huo kwa asilimia 66 na ilipiga mashuti ya kulenga goli matano kwa sifuri huku ikipata kona 9 kwa moja. Aidha katika maandalizi ya mchezo huo Yanga ilijinasibu kuwa ingeifunga timu hiyo ambayo haijawa na msimu mzuri kwa mwaka huu lakini imekuwa tofauti wameishia kulingana nguvu.
michezo