content
stringlengths
1k
24.2k
category
stringclasses
6 values
Na WAANDISHI WETU, DAR ES SALAAM HALMASHAURI Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC), inatarajia kukutana Desemba 13, mwaka huu jijini Dar es Salaam, imefahamika. Taarifa iliyotolewa Dar es Salaam jana na Kaimu Msemaji wa chama hicho, Seleman Mwenda, ilisema mkutano huo utatanguliwa na kikao cha Kamati Kuu (CC), kitakachofanyika Desemba 11 hadi 12, jijini Dar es Salaam. Ingawa hadi sasa ajenda za vikao hivyo hazijajulikana, lakini wachambuzi wa masuala ya  siasa wanasema, kufanyika kwa vikao hivyo kunatajwa kuwa ni mkakati wa Mwenyekiti wa chama hicho, Rais Dk. John Magufuli  kutaka kuisuka upya CCM. Baadhi ya wachambuzi hao wanasema uteuzi wa wajumbe watatu wa sekretarieti ya chama hicho kuwa mabalozi ni mwendelezo wa mkakati huo kuelekea uchaguzi mkuu wa ndani wa chama hicho mwakani. Mbali na hao mjumbe mwingine wa sekretarieti, Dk Asha -Rose Migiro aliteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza na nafasi yake ndani ya chama kuchukuliwa na Pindi Chana ambaye naye ameteuliwa kuwa balozi. Katika Serikali ya awamu ya nne, Pindi Chana alikuwa Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na baadae mwaka huu aliteuliwa kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa. Mjumbe wa Kamati Kuu (CC), Dk. Emmanuel Nchimbi, kuteuliwa kuwa balozi kunathibitisha kuhusu uwapo wa mkakati wa Rais Magufuli kusuka upya chama hicho kwa kuweka sura mpya. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye pia ni Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa chama hatarajiwi kuwapo katika safu hiyo mpya, kwani tayari yupo serikalini. Mwingini ni Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho (Bara), Rajabu Luhwavi ambaye ameteuliwa kuwa balozi anazidi kutoa taswira kuhusu mkakati wa Rais Magufuli kusuka upya chama hicho. Wachambuzi mbalimbali wa siasa waliiambia MTANZANIA jana kuwa Februari 5 mwakani, CCM kitatimiza miaka 40 tangu kuzaliwa kwake huku kikiwa hakijafanya marekebisho makubwa ya muundo wake ili kuendana na hali ya sasa. Baadhi ya wasomi waliozungumzia muundo huo mkongwe wa CCM ni pamoja na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO),Profesa Gaudence Mpangala ambaye alimshauri mwenyekiti wa chama hicho Rais Dk. Magufuli kuifumua safu nzima ya uongozi kwa sababu kilikua chama cha wala rushwa. “Chama hicho kilisababisha kujitokeza kwa matabaka baina ya walionacho na wasio nacho na kusababisha chama hicho kupoteza mvuto, baadhi ya viongozi wake walijigeuza Mungu watu huku wakishindwa kuwatumikia wananchiipasavyo. Profesa Mpangala alisema mpaka sasa wananchi hawakipendi chama hicho kutokana na viongozi hao ambao wanafanya kazi kwa ajili ya kulindana na kuangalia maslahi yao binafsi kuliko wanaowatumikia. “CCM ilipoteza mwelekeo kutokana na baadhi ya watendaji kushindwa kutumia majukumu yao ipasavyo,wengi wao ni wala rushwa, mafisadi na miungu watu ambao wanashindwa kushughulikia matatizo ya wananchi kutokana na ubinafsi. “Kutokana na hali hiyo, Rais Dk Magufuli anapaswa kuifumua CCM kwa sababu ni chanzo cha matatizo na malalamiko yaliyosababisha wananchi kutokuwa na imani nayo. Rais Magufuli anapaswa kuondoa kokoro zote na kupanga safu mpya ambayo itafanya kazi ya kuwatumikia wananchi. “Viongozi wa CCM lazima wajitafakari wamefanya nini katiba kipindi cha miaka 40 kinachotarajiwa kutimizwa Februari mwakani, kwa sababu malalamiko ni mengi kuliko sifa,”alisema mhadhiri huyo wa RUCO. Mwingine aliyezungumzia uhitaji wa mabadiliko ndani ya CCM ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana. Yeye alisema vikao vinavyotarajiwa kufanyika licha ya kuwepo kwenye kalenda ya vikao vya chama lakini pia kunaweza kuwepo mabadiliko ya uongozi yatakayofanywa na Mwenyekiti wake. Alisema, hali hiyo imedhihirika  baada ya baadhi ya wajumbe wa Kamati Kuu na sekretarieti ya chama hicho kuteuliwa kuwa mabalozi wa nchi mbalimbali, jambo linaloonyesha wazi kuwa, nafasi zao zitajazwa na watu wengine. “Kitendo cha kuwaondoa baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na kuwapa ubalozi kinaonyesha wazi kuwa, kuna mabadiliko ya uongozi yanakuja, lakini mabadiliko hayo yaendane na kuwatumikia wananchi,”alisema Dk. Bana. Hata hivyo,Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Profesa Mwesiga Baregu alisema kuwa, mabadiliko hayo ni ya kawaida kama yaliyofanywa serikalini na kwamba sasa hivi yamehamia kwenye chama. Alisema anachotaka kufanya mwenyekiti wa chama hicho ni kupanga safu yake ya uongozi ndani ya chama ili aweze kufanya nayo kazi katika kipindi cha miaka mitano ijayo”alisema Profesa Baregu. Hata hivyo Profesa Baregu haoni jambo jipya kwenye mabadiliko hayo kwa sababu wanachama wa CCM ni wale wale. CCM aitakayo Dk. Magufuli Katika hotuba ya Rais Dk. Magufuli baada ya kukabidhiwa uenyekiti wa chama hicho alisema miongoni mwa mambo atakayoyatekeleza ni kuimarisha utendaji kazi wa chama, huku akimnukuu hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kusema kuwa chama legelege huzaa serikali legelege. “Nitashirikiana nanyi kujenga chama madhubuti chenye uwezo wa kuisimamia vizuri Serikali ili itekeleze ipasavyo majukumu yake, ikiwezekana tutapitia upya katiba na kanuni zetu ili kukidhi mazingira ya sasa na kuweza kuwatumikia wananchi ipasavyo. “Tutahakikisha pia tunakuwa na safu bora ya uongozi katika ngazi zote kuanzia shina hadi taifa. Tutaangalia muundo (structure) wa chama chetu katika ngazi mbalimbali na kuondoa vyeo visivyokuwa na tija katika chama na hasa wakati huu wa mfumo wa vyama vingi” alisema Dk. Magufuli. Dk. Magufuli alihoji kuhusu uhalali wa kuendelea kuwapo vijana wa chipukizi ndani ya chama hicho pamoja na baadhi ya safu za uongozi ndani ya chama hicho. “WanaCCM ni lazima tujiulize je ni kweli katika zama hizi bado tunahitaji mtoto wa miaka 8 hadi 15 kuwa chipukizi kwa ajili ya kumtumia kwenye siasa badala ya kumwacha asome?  Kama akiwepo chipukizi wa CCM, chipukizi wa NCCR au Chadema ama TLP tutakuwa tunajenga nchi ya namna gani? “Je bado kuna umuhimu wa kuwa na makamanda wa vijana ambao mara nyingi wenye kupewa vyeo hivyo ni wale wenye uwezo wa kifedha pekee?  Je walezi kwenye Umoja wa Wanawake (UWT) bado wanahitajika? Je washauri ndani ya Jumuiya ya Wazazi wanahitajika? Alihoji Dk. Magufuli.
kitaifa
Nay wa Mitego alikuwa akitafutwa na Polisi Dar es Salaam na tayari alishafunguliwa kesi akituhumiwa kwa makosa kadhaa.Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro, Ulrich Matei alithibitisha jana kukamatwa kwa mwanamuziki huyo saa nane usiku wa kuamkia Machi 26, 2017 akiwa Mtibwa, Turiani wilayani Mvomero kwenye onesho la muziki.Kamanda Matei alisema walikuwa na taarifa ya juu ya kutafutwa kwake kutokana na makosa aliyokuwa amefanya na kufunguliwa kesi Dar es Salaam.Hivyo alisema,walikuwa wakifuatilia kwa karibu nyendo zake, ambapo awali inasemekana alikuwa maeneo tofauti ya Dodoma, Mpwapwa, Kongwa na siku hiyo alifika Mtibwa, Tarafa ya Turiani wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro.Alisema baada ya kupata taarifa zake kuwa msanii huyo alikuwa Mtibwa walienda kumkamata usiku wa manane akiwa kwenye shoo na utaratibu ulifanyika ili asafirishwe kwenda Dar es Salaam jana, ambako amefunguliwa mashtaka kwa makosa yanayomkabili.“Ni kweli tumemkamata mwanamuziki anayefahamika kwa jina la Nay wa Mitego usiku wa manane kuamkia Machi 26, mwaka huu akiwa kwenye shoo eneo la Mtibwa, Turiani wilayani Mvomero na amesafirishwa kurudishwa Dar es Salaam anakotuhumiwa kitenda makosa yake, ” alisema Matei.Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Morogoro alisema wao hawakuwa na jukumu jingine baada ya kumkamata isipokuwa ni kumsafirisha kwenda Dar es Salaam, ambapo atahojiwa zaidi na kujieleza kuhusiana na tuhuma zinazokambili.Watu kadhaa wa mjini Morogoro kwa nyakati tofauti wakizungumzia kukamatwa kwake wamedai huwenda ni kutokana na wimbo wake mpya alioutoa siku za hivi karibuni unaofahamika kwa jina la ‘Wapo’ ambao unaendelea kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa matumizi ya maneno yake yamekuwa na ukakasi kimaadili mbele ya jamii.
michezo
MAUAJI ya kinyama dhidi ya mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi yalipangwa na kikosi cha mauaji cha Saudi Arabia, Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan ameliambia Bunge la nchi yake jana. Wakati Erdogan akitaka kufahamu aliyeamuru mauaji hayo, akikwepa kumtaja Mwana Mrithi wa Ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman, ushahidi mpya unadaiwa kuzidi kumnyooshea kidole kiongozi huyo mwenye nguvu Saudi Arabia. Vilevile, wakati Erdogan katika hotuba yake hiyo akitaka pia kuonyeshwa yaliko mabaki ya mwili wa mwandishi huyo, taarifa nyingine  ambayo bado haijathibitisha, inadai yamepatikana katika makazi ya balozi mdogo wa Saudi Arabia mjini Istanbul ukiwamo uso uliochunwa. Alichozungumza Erdogan Katika hotuba iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu lakini akaishia kutoa taarifa ambazo tayari zilishavujishwa na vyanzo mbalimbali vya habari vilivyoomba kuhifadhiwa, Erdogan alisema kuna ushahidi wa wazi kuwa kikundi cha wauaji kutoka  Saudi Arabia kilipanga kumuua mwandishi huyo mkosoaji wa ufalme huo kabla ya Oktoba 2 mwaka huu. Erdogan (64) ameeleza mauaji hayo kuwa ya siasa lakini alisita kumlaumu moja kwa moja Mohammed bin Salman maarufu kama MBS, badala yake ametaka kumfahamu aliyeagiza kufanyika kwa operesheni hiyo. Alisema alikuwa na matumaini ya kupata ushirikiano kamilifu kutoka kwa Mfalme Salman, baba wa MBS. “Saudi Arabia imechukua hatua muhimu ya kukiri mauaji. Kwa sasa tunatarajia wale walioshiriki kuanzia ngazi ya juu hadi chini watafikishwa mahakamani,” alisema. Maofisa wakiwamo wa inteljensia, usalama na alama za vidole, walionekana wakiingia katika jingo ambalo Khashoggi alitoweka huku wengine wakiwa wameonekana wakikagua  msitu wa karibu najengo hilo kabla ya mauaji kutokea, alisema Rais Erdogan. Ufichuajii huo wa Rais utachochea minong’ono kuwa kikundi hicho kilikuwa kikitafuta eneo ambalo kilipanga kuuzika mwili wa Khashoggi. Erdogan ametaka watu 18 waliokamatwa na Saudi Arabia kuhusiana na mauaji hayo washitakiwe   Istanbul na kwamba kuwatupia lawama baadhi ya maofisa wa inteljensia kwa mauaji hayo hakutairidhisha Uturuki wala jamii ya mataifa. Akizungumza na wanachama wa Chama chake cha AK Bungeni, Erdogan, ambaye binafsi amekuwa akishutumiwa kwa ukiukaji wa haki za binadamu, alihoji kwa nini mwili wa Khashoggi haujapatikana. Aliitaka Saudi Arabia kumfichua mtu aliyepewa jukumu la kuupoteza mwili huo, ambaye inaaminika ni Mturuki. Sehemu ya mabaki yagundulika Wakati Erdogan akitaka kufahamu ulipo mwili huo, kuna taarifa kuwa uligundulika katika bustani ya balozi mdogo wa taifa hilo, kwa mujibu wa ripoti za Sky News jana, lakini haikufahamika ukubwa wa sehemu iliyogundulika. Ripoti tofauti zinasema sehemu ya mwili huo ilikutwa katika kisima. Iwapo itathibitishwa ni kweli, maswali yataibuka kuhusu sababu ya kupita muda mrefu kugundua yalipo mabaki ya mwili wa Khashoggi. Balozi Mdogo wa Saudi Aarabia, Mohammed al-Otaibi alikimbia Istanbul wiki iliyopita kabla ya nyumba yake hiyo kukaguliwa na polisi wa Uturuki. Nchini mwake, amewekwa chini ya uchunguzi na kuondolewa cheo chake, ufalme ulisema katika taarifa . Mapema jana, Erdogan alisema alimwambia Mfalme Salman kuwa balozi huyo hafai kwa kazi hiyo. Erdogan alizungumza kwa simu mara mbili na Mfalme Salman, kitu kinachotafsiriwa na wengi kama mkakati wa kumweka pembeni Prince Mohammed ambaye baba yake amezeeka. Ingawa   masuala aliyozungumza  tayari yalishavuja, lakini kwa Erdogan kutoa hotuba Bungeni kunayapa nguvu madai hayo. Mmoja wa wanadiplomasa wa Magharibi nchini Uturuki ameuambia mtandao wa Bloomberg kwamba mgogoro huo ni ‘zawadi kutoka kwa Mungu’ kwa Erdogan wakati akijaribu kujijenga kuleta mabadiliko ya uwiano wa nguvu nchini Saudi Arabia na kuongeza ushawishi wake Mashariki ya Kati. “Kwa nini watu hawa 15 wakutane  Istanbul   siku ya mauaji? Tunatafuta majibu  ya swali hili. Watu hawa walikuwa wakipokea amri kutoka kwa nani?” Erdogan alisema. “NInachotaka ni kwamba watu hawa 18 washitakiwe Istanbul,” Erdogan alisema katika hotuba yake, akizungumzia   watu hao wakiwamo maofisa wa usalama ambao tayari wamekamatwa mjini Riyadh. Alisema wote walioshiriki katika mauaji hayo wanapaswa kukabiliwa na adhabu kali. Erdogan alisema  mauaji yanaonekana yalipangwa kulingana na ramani iliyoandaliwa na kikundi cha  Saudi Arabia, ambayo ilitumwa Istanbul kwa madhumuni hayo. Mfumo wa usalama katika ubalozi mdogo wa Saudi Arabia ulizimwa kwa makusudi kwa   madhumuni hayo, alisema. “Haya ni mauaji ya siasa,” Erdogan alisema. Simu saba zapigwa Ofisi ya Mwana Mrithi wa Ufalme Pamoja na kutomtaja Mohamed, ushahidi unaelekezwa huko kwa vile idadi  kubwa ya watu hao 15 walioingia Istanbul wanamfanyia kazi. Mmoja wao, Meja Jenerali  Maher Abdulaziz Mutrib, mwanadiplomasia wa zamani, anadaiwa alipiga simu 14 kwenda Saudi Arabia zikiwamo saba kwenda kwa Ofisi ya Muhammad baada ya Khashoggi kuuawa. Simu hizo zilinaswa na vyombo vya usalama vya Uturuki, maudhui ambayo yanahatarisha hatima ya baadaye ya siasa ya MBS  iwapo yatavujishwa, kwa mujibu wa chanzo cha habari. Mutrib, ambaye amekuwa akisafiri katika ziara karibu zote za Salman, ameelezwa kuwa uti wa mgongo wa kikosi cha mauaji cha Saudi Arabia. Tuhuma hizo ni mwendelezo mwingine unaoelekeza kidole kwa mtawala huyo wa Saudi Arabia mwenye nguvu. MBS adaiwa aliapa kuwakata vidole wakosoaji Wakati Saudia Arabia ikitupia lawama kwa maofisa wengine kwa kumuua Khashoggi (59) kwa utashi wao, chanzo cha habari cha kuaminika kilisema kikosi hicho cha siri kilituma vidole vya Khashoggi mjini Riyadh  kuthibitisha kuwa operesheni hiyo ilifanikiwa na viliwasilishwa kwa MBS. “MBS daima hupanda kusema atakata vidole vya kila mwandishi anayemkosoa,” chanzo hicho kilidai. Kwa mujibu wa gazeti la Yeni Safak, Mutrib alizungumza na Badr al-Asaker, mkuu wa ofisi binafsi ya Mwana Mrithi wa Ufalme, mara nne baada ya Khashoggi kuuawa. Vyanzo vya habari vya Saudia na Uturuki vilisema utawala wa kifalme umemfukuza msaidizi mmoja kwa kuamuru mauaji kupitia mtandao wa video wa Skype. Saud Al-Qahtani, ambaye anasimamia mtandao wa jamii maalumu kwa Mwana Mrithi Ufalme, anadaiwa kumtukana mwandishi huyo baada ya kukamatwa katika ubalozi huo akikiambia kikosi hicho, ‘nileteeni kichwa cha mbwa huyo.’ Alifukuzwa wadhifa wake na kuteuliwa kuwa mwenyekiti wa Shirikisho la Usalama wa Mitandao, Programu na Drone, wadhifa alioukuwa nao awali. Kashfa hiyo imeathiri mkutano wa Jukwaa la Uwekezaji Saudi lililofunguliwa jana baada ya makampuni makubwa ya kimataifa kujitoa. Mradi huo ni ubunifu wa Mwana Mrithi wa Ufalme Mohammed bin Salman, ukilenga kuvutia uwekezaji zaidi wa kigeni kaika ufalme huo na kusaidia kutengeneza ajira kwa   vijana wengi.
kimataifa
TANZANIA inazo rasilimali mbalimbali yakiwamo maziwa, mito na bahari ambayo ni moja ya vyanzo vya uchumi kupitia uvuvi wa samaki. Maziwa makubwa Tanzania ni pamoja na Ziwa Victoria ambalo ni la pili kwa ukubwa duniani, Ziwa Tanganyika ambalo ni la pili kwa kuwa na kina kirefu duniani.Lipo pia Ziwa Nyasa ambalo ni miongoni mwa maziwa makubwa barani Afrika; na Ziwa Rukwa huku nchi ikijivunia bahati ya kuwa na bahari ya Hindi upande wa mashariki. Mhadhiri Mwandamizi kutoka Ndaki ya Sayansi ya Kilimo na Teknolojia ya Uvuvi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Paul Onyango anasema hali ya joto iliyopo katika bahari ya Hindi inapunguza uzalishaji wa chakula kwa viumbe hai kama samaki wa baharini.Katika utafiti huo, Tume ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imetoa fedha kwa ajili ya kufanya utafiti wa samaki aina ya sangara na jinsi ya kuongeza pato la wavuvi. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kilishirikiana na Chuo Kikuu cha Western Cape, Afrika Kusini. Mwaka 2013 Costech ilitoa Sh milioni 36.2 na mwaka jana walitoa Sh milioni 60. Anasema hali hiyo inasababisha Bahari ya Hindi kutokuwa na samaki wengi ukilinganisha na hali ilivyo katika bahari nyingine kama Pacific na Atlantic.Hata hivyo, anasema licha ya hali hiyo, bahari ya Hindi inao samaki wa aina mbalimbali wakiwemo jodari, papa, dagaa na aina nyingine nzuri kwa chakula. Kutokana na rasilimali ya samaki iliyopo, Dk Onyango aliamua kufanya utafiti unaohusu utumiaji wa simu katika kuinua hali ya maisha ya wavuvi uliojikita katika Ziwa Victoria kwa aina ya samaki ajulikanaye kama sangara.Kwa mujibu wa msomi huyo, kutokana na maelezo ya wenyeji wa mikoa ya Mwanza, Mara na Kagera, asili ya samaki huyo siyo Tanzania, bali tu samaki huyo alipelekwa huko miaka ya 50 na 60. Anasema historia ya samaki huyo katika Ziwa Victoria haijakaa vizuri kutokana na maelezo tofauti tofauti yanayotolewa na wenyeji. “Wenyeji wa maeneo hayo wanaeleza kuwa, katika miaka ya 80 samaki aina ya sangara walizaliana sana kupita kiasi hivyo wenye viwanda vya kuchakata samaki wakaajiri watu kwa ajili ya kazi hiyo waliosafirishwa kwenda nchi za Ulaya,” anasema.Anabainisha kuwa, aliamua kujikita katika utafiti huo kwa kuwa samaki wanaosafirishwa zaidi kwenda nchi za Ulaya ni aina hiyo ya sangara, lakini maisha ya wavuvi katika Ziwa Victoria hayaridhishi. “Samaki anayesafirishwa ni sangara. Viwanda vinanunua samaki kutoka kwa wavuvi na bei yake huko Ulaya ni nzuri, lakini wavuvi hali zao haziridhishi,” anasema.Hivyo katika utafiti huo katika Ziwa Victoria amegundua kuwa wavuvi hawapati malipo stahiki ya kile wanachokiuza. Anasema katika utafiti huo amegundua kuwa, wavuvi badala ya kupewa bei nzuri ya soko inayoweza kuwainua kiuchumi, wamekuwa wakipangiwa bei na wanunuzi hali inayowafanya kulipwa chini ya kiwango kisichoendana na bei au faida halisi ya samaki hao. Ndiyo maana anasema kwa kulitambua hilo, utafiti wake ulilenga kuwasaidia wavuvi hao ili nao wawe sehemu katika kupanga bei ya bidhaa wanazoziuza.Kadhalika, Dk Onyango anasema walijikita kubaini namna wavuvi wanavyoweza kutumia teknolojia ya simu kupata taarifa mbalimbali za masoko ya samaki. “Tuliangalia jinsi tutawawezesha kuwa na taarifa mbalimbali za masoko. Sasa tukaangalia watapataje hiyo taarifa? Tukaona wakitumia teknolojia ya simu, wanaweza kupata taarifa.” “Hii ni kwa kuwa bei za masoko mbalimbali zitaonekana na hivyo, kutakuwa na mashindano ya bei ya uuzaji na ununuzi wa samaki,” anasema. Kwa msingi huo, anasema walibaini teknolojia ijulikanayo kama ‘Fishmob’ ndiyo njia pekee itakayowawezesha wavuvi kupata taarifa sahihi za bei na kwa wakati sahihi.“Tulianzisha kwa wavuvi peke yao, lakini tukaona teknolojia hii ni nzuri hata kwa walaji… Teknolojia hii siyo tu kwa ajili ya wavuvi, bali inawasaidia pia hata walaji kujua masoko na bei, pia wauzaji wa samaki kwenye masoko,” anasema. Si hivyo tu bali teknolojia hiyo itasaidia serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kupata takwimu wanazozihitaji katika idara hiyo kwa gharama nafuu.Kwa sasa Wizara ya Uvuvi inatumia fedha nyingi ili kupata takwimu za uvuvi ili kujua samaki wangapi wamevuliwa kwa siku, wiki, mwezi na mwaka. Kadhalika, kujua bei, mialo zinazotumika kwa ajili ya uvuvi na miundombinu iliyopo. Inayohitajika na huduma za miundombinu zinazohitajika. Anasema: “Idara ya uvuvi lazima ipate takwimu kwa ajili ya kupanga na kusimamia rasilimali za uvuvi, inatumia mabilioni kupata takwimu.”“Hivyo kupitia teknolojia hii, takwimu zitapatikana chini ya robo ya pesa zote zinazotumika kuzipata.” “Tumeanza Ziwa Victoria, lakini itaenea kote tukimaliza kuitengeneza tutaitumia nchi nzima,” anasema. Kwa maelezo yake ni kwamba chuo kimetengeneza mfumo huo wa teknolojia kisha kitautoa kwa watakaohitaji kwani siyo kwa ajili ya wavuvi peke yao, bali itatumika na maeneo mengine.Anasisitiza: “Teknolojia hiyo ipo wazi pia kwa sekta nyingine na itakuwa tayari kwa matumizi baada ya Juni mwaka huu.” Anasema kwa mujibu wa utafiti, wavuvi walioanza kutumia teknolojia hiyo wamefurahia kwa kuwa wanajua watakapokuwa wanapata taarifa kuhusu masoko, itawasaidia pia kwenye upangaji wa bei kwa wauzaji wa samaki wanaosubiri.Hata hivyo, Dk Onyango anakiri kuwa kila kitu kina faida na changamoto zake, lakini yeye na timu yake ya utafiti, wanaomba serikali na sekta binafsi zishiriki katika utumiaji wa teknolojia hii. “Teknolojia hii inatumia mfumo wa ujumbe mfupi wa maandishi ya kawaida. Katika kutumia mfumo huu, mtumiaji atahitaji pesa ya kuanzia na baadaye utajiendesha,” anasema.Changamoto nyingine ni za kimtandao zinazoweza kusababisha wahusika kuchelewa kupata taarifa kwa wakati. Onyango anasema: “Wakati mwingine, nishati inaweza kusumbua kwa kuwa kompyuta inatakiwa kuwa kwenye umeme saa 24 kwa siku saba za wiki.” Anafafanua: “Ukatikaji wa umeme unaweza kuathiri upatikanaji wa taarifa kwa wakati.”
kitaifa
BARCELONA, HISPANIA TIMU ya Barcelona itakosa huduma ya mshambuliaji wao wa pembeni Ousmane Dembele kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja baada ya kusumbuliwa na nyama za paja. Mchezaji huyo alicheza dakika 90 katika mchezo wa ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuu nchini Hispania mwishoni mwa wiki iliopita ambapo Barcelona ilikubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Athletic Bilbao likifungwa na Aritz Aduriz dakika za lala salama. Uongozi wa timu hiyo umethibitisha kuwa utaikosa huduma ya mchezaji huyo kwa wiki tano baada ya kuumia mguu wake wa kushoto. Dembele amekuwa na furaha ndani ya mabingwa hao wa Ligi Kuu Hispania tangu alipojiunga mwaka 2017 akitokea Borussia Dortmund, lakini mara nyingi anasumbuliwa na majeruhi ya misuli. Msimu uliopita alipata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara tofauti na Philippe Coutinho, lakini alionekana anakosa umakini uwanjani, wakati huo Coutinho akiachwa benchi kutokana na kuwa chini ya kiwango jambo lililompelekea mchezaji huyo kutolewa kwa mkopo Bayern Munich. Kuumia kwa Dembele kunaweza kuwafanya Barcelona wapambane kuhakikisha wanaipata saini ya mchezaji wao wa zamani Neymar Jr ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya PSG na pia anawindwa na Real Madrid. Dili hilo linaweza kukamilika kabla ya kufungwa kwa usajili Septemba 2. Katika mchezo wa ufunguzi wa Ligi Kuu Hispania, Barcelona ilimkosa mchezaji wao bora duniani Lionel Messi kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia wakati wa maandalizi ya msimu mpya wa ligi. Hata hivyo kuna taarifa kwamba anaweza kuwa ndani ya kikosi wakati wa mchezo wa pili dhidi ya Real Betis ambao utapigwa kwenye uwanja wa Camp Nou mwishoni mwa wiki hii.
michezo
MKUU wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi amewaahidi kwamba Jiji litawatafutia eneo lingine wafanyabiashara waliokuwa wakifanya biashara pembeni ya jengo la makao makuu ya CCM jijini hapa.Kauli hiyo ya mkuu wa wilaya aliitoa baada ya wafanyabiashara kwenda kulalamika kwake baada ya uongozi wa jiji la Dodoma kuamua kuvunja vibanda vyote vilivyo mbele ya jengo hilo.Vibanda hivyo vilivunjwa siku moja kabla ya Kamati Kuu ya CCM na Halmashauri Kuu kufanya kikao chake katika majengo hayo jijini hapo.“Eneo hili sio salama kutokana kufanya biashara na kuwa karibu na barabara kuu, jambo ambalo linaweza kusababisha ajali,” alisema Mkuu wa Wilaya, Katambi.Awali, wafanyabiashara ndogo maarufu kama machinga wanaofanya biashara zao nje ya uzio wa ofisi za makao makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) waliulalamikia uongozi wa Jiji la Dodoma kutokana na kuwavunjia vibanda vyao vya biashara bila kuwapa taarifa.Mwenyekiti wa wamachinga hao, Innocent Mushi alisema wamekuwa wakifanya biashara katika eneo hilo kwa muda mrefu lakini jiji hilo halijawahi kuwapatia taarifa ya kuondoa vibanda vyao.“Sisi hatupingi kuondoka hapa ila tunacholalamika ni kuharibiwa mali zetu, wangetupa taarifa sisi tungetoa mali zetu kuliko hasara tuliyopata,” alisema.Mushi alisema wafanyabiashara hao 65 walifuata utaratibu wa kuomba nafasi hiyo kwa uongozi wa CCM ukawaruhusu kufanya biashara nje ya eneo lao kwa masharti waliojiwekea. Aliyataja baadhi ya masharti hayo kuwa walitakiwa kuacha nafasi ya barabara kuu pamoja na kutoziba mageti ya kuingilia ndani ya Ofisi za makao makuu ya Chama hicho.
kitaifa
VIONGOZI wa dini nchini wamezindua mkakati wa Mfumo wa Uchumi wa Soko Jamii unaolenga kuchochea kasi ya Tanzania kuelekea katika uchumi wa kati unaoendeshwa na viwanda vinavyojengwa.Uzinduzi huo ulifanyika jana jijini Dar es Salaam ukiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Mahusiano ya Dini Mbalimbali, Askofu Steven Munga kwa niaba ya Wakristo, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) na Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) kwa kushirikiana na Kaimu Mufti wa Tanzania, Shehe Ali Muhidin Mkoyogore kwa niaba ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata).Viongozi hao wa dini walisema katika uzinduzi huo mfumo wa uchumi wa soko jamii kwa Tanzania unalenga kuongeza ukuaji wa uchumi shirikishi na endelevu na kuhakikisha ustawi wa baadaye wa nchi.Muhtasari wa Mfumo wa Uchumi wa Jamii wa Soko Jamii kwa Tanzania: Kuelekea Maendeleo Shirikishi na Endelevu ya Kiuchumi unataja tunu za mfumo huo ni ufahamu, hekima, uwajibikaji, taifa kwanza, jumuiya, utu wa binadamu, uadilifu, vijana, tathmini ya sera za maendeleo, uwazi na umoja.Munga ambaye ni Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, alisema umefika wakati Watanzania kumuunga Mkono Rais John Magufuli kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kuongeza tija na kukuza uchumi.“Sasa tuhame kutoka kwenye maneno kwenda kwenye vitendo…dosari zilizopo katika mkakati huu kutegemea mazingira tofauti ya utekelezaji, zinaweza kurekebishwa ili kufikia malengo ya mradi, kila mmoja atimize wajibu wake,” alisema Askofu Munga. Shehe Mkoyogore alisema, “mfumo huu tuusome kwa makini na kuufanyia kazi sawa sawa.”Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustine cha Tanzania (Saut), Ntui Ponsian alisema mfumo huu unahitaji jamii kuwa na taarifa sahihi za kutosha kufanya uamuzi kwa maslahi ya taifa huku watu wakiwa waaminifu. “Mfumo huu pia utazalisha walipa kodi wengi kupitia ajira mbalimbali na biashara na watu watakwenda katika kilimo shambani kwa vile wanajua wana uhakika wa soko na kupata fedha,” alisema. Alisema ili matamanio ya Rais Magufuli kuacha Tanzania ikiwa na mabilionea 100 yatimie,viongozi wa dini wanatamani hayo ndiyo yafanyike huku kukiwa hakuna Mtanzania anayeachwa nyuma kiuchumi.Shehe wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke, alisema uzinduzi wa kitabu hicho utawasaidia viongozi wa dini kuelewa wajibu wao kwani baadhi wanadhani kimakosa suala la uchumi linaihusu serikali pekee. Katibu Mkuu wa TEC, Padri Dk Charles Kitima alisema, “Uchumi wa Soko Jamii ni mfumo unaolenga utu wa mtu bila kunyanyasa wengine; kumfaa binadamu na siyo kumwangamiza; ni mfumo unaolenga kutunza mazingira na siyo kuyaharibu na yote yanakuwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.”Alisema licha ya jukumu lao kubwa kuwaweka binadamu karibu na Mungu, wanatambua wajibu wao kuwafanya binadamu kushiriki uchumi shirikishi wa uzalishaji mali wawe na maisha bora na maendeleo. Padri Kitima alisema Watanzania wanapaswa kushirikishwa na kuelewa zaidi umuhimu wa uzalishaji na uendeshaji biashara adilifu katikati ya uchumi ili Mtanzania ampende Mungu na pia maendeleo ya kweli. Awali katika mazungumzo na wanahabari, Dk Kitima alisema wanataka kuwajenga watu wawe na ushindani na uzalishaji shirikishi katika uchumi hata kupitia Watanzania kumiliki kampuni mbalimbali na kubwa hata kupitia hisa ndiyo maana wanahimiza watu wafundishwe kuzalisha kiadilifu na kulipa kodi.
kitaifa
KHARTOUM, SUDAN SUDAN inahitaji msaada wa dola za Marekani bilioni 8 katika kipindi cha miaka miwili ijayo ili iweze kujinasua na gharama za kuagiza bidhaa za nje pamoja na kuisaidia kuujenga upya uchumi wake uliovurugika baada ya miezi kadhaa ya vurugu za kisiasa. Hayo ni kwa mujibu wa Waziri Mkuu mpya wa taifa hilo, Abdallah Hamdok, ambaye amekula kiapo chake siku chache zilizopita. Kiongozi huyo ambaye ataongoza Serikali ya mpito katika kipindi cha miaka mitatu ijayo, alisema kiasi kingine cha akiba ya fedha za kigeni cha dola bilioni 2 kitahitajika ili kudhibiti kuporomoka kwa thamani ya sarafu ya nchi hiyo. Mchumi Hamdok mwenye umri wa miaka 61, ambaye amewahi kufanya kazi katika kamisheni ya uchumi ya Umoja wa Mataifa kwa Afrika, alisema ameanza kufanya mazungumzo na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na Benki ya Dunia, yenye lengo la kufanya marekebisho ya deni la Sudan na kuyashawishi mataifa rafiki na vyombo vingine vya fedha kuhusu msaada huo. Katika mahojiano yake na Reuters, Hamdok alisema katika kipindi cha miaka miwili ijayo, Sudan italazimika kulipa madeni na kufanya juhudi kubwa za kufufua uchumi wake kwani imedhoofishwa sana na mgogoro wa miezi kadhaa sasa wa kisiasa. Alisema Sudan hivi sasa inahitaji msaada wa kigeni wa zaidi ya dola bilioni nane kuweza kukabiliana na changamoto zake nyingi, hasa za kiuchumi. Aliongeza kuwa mazungumzo baina yake na Mfuko wa Kimataifa wa Fedha na Benki ya Dunia yameshaanza kama juhudi za kuyashawishi mashirika hayo muhimu ya kifedha ya kimataifa kuipatia tena mikopo Sudan. Jumatano iliyopita, Hamdok alikula kiapo cha kuwa Waziri Mkuu wa Serikali ya mpito ya Sudan. Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan limekuwa likitawala nchini humo tangu Aprili 11, mwaka huu baada ya kupinduliwa Jenerali Omar al Bashir. Mara kwa mara baraza hilo lilikuwa likituhumiwa kukwamisha mambo ili kuzuia utawala wa kiraia nchini humo, lakini kusimama imara wananchi katika maandamano kumelilazimisha baraza hilo la kijeshi linaloungwa mkono na Saudi Arabia, Imarati na Misri lisalimu amri na kuruhusu kushirikishwa kikamilifu wananchi katika utawala.
kimataifa
BARAZA la Utendaji la Chama cha Mahakimu na Majaji Afrika Mashariki (EAMJA), litafanya kikao chake kuanzia leo hadi kesho kutwa, mwaka huu jijini Arusha.Katika kikao hicho, Mahakimu na Majaji watajadili Sera ya Jinsia ya Afrika Mashariki kwa lengo la kuzalisha sheria ambazo zinawawezesha wanawake kupata haki mahakamani bila kukwazwa na mapingamizi yanayotokana na ufundi haba wa kisheria unaowakabili.Kikao cha Baraza hilo kitakuwa chini ya uenyekiti wa, Rutazana Angeline, ambaye pia ndiye Rais wa EAMJA.Wajumbe kutoka Tanzania katika Kikao hicho ni Wilberforce Luhwago, Jaji Robert Makaramba, Jaji Sophia Wambura na Angelo Rumisha.Vyama vinavyounda EAMJA ni Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Chama cha Majaji na Mahakimu Kenya (KMJA), Chama cha Majaji na Mahakimu Uganda (UJOA), Chama cha Majaji na Mahakimu Zanzibar, na Mahakama ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki.Dhima ya EAMJA ni kukuza, kuimarisha na kulinda utawala wa sheria, na upatikanaji wa haki kwa watu wote, kwa njia ya kuwianisha mifumo ya sheria na kujenga uwezo wa maofisa wa Mahakama katika Afrika Mashariki.Rais wa Chama cha Mahakimu na Majaji nchini, Wilberforce Luhwago alisema jana kuwa kwa mujibu wa Katiba ya hicho, Baraza Tendaji hukutana mara 4 kwa mwaka, na mikutatano ya baraza hilo na mikutano mikuu hufanyika kwa mzunguko ambapo kila nchi mwanachama wa huwa mwenyeji wa vikao vya Baraza Tendaji na Mkutano Mkuu. Rais wa chama hicho juzi alisema:“Baraza Tendaji litapokea na kufanya tathmini ya maendeleo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwaka huu huko Zanzibar.”Aliongeza: “Baraza pia litafanya shughuli zake za kawaida za baraza kwa mujibu wa Katiba, kama vile kupokea taarifa za maendeleo ya vyama vinavyounda chama, maendeleo au shughuli zilizofanywa na vyama hivyo tangu baraza hilo lilipokutana mara ya mwisho Machi, mwaka huu, Kigali, Rwanda.
kitaifa
Na Kulwa Mzee -Dodoma MBUNGE wa Bukene, Suleiman Zedi (CCM), amesema ujasiri na hatua zinazochukuliwa na Rais Dk. John Magufuli kupambana na rushwa, ufisadi, ubadhirifu na kuzilinda rasilimali za nchi umevuka mipaka ya Tanzania. Kauli hiyo aliitoa bungeni juzi wakati akichangia mjadala wa Bajeti Kuu ya Serikali ya mwaka wa fedha wa 2017/2018. Zedi anayeiwakilisha Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), alisema kila anaposhiriki vikao vya Bunge hilo, wajumbe wenzake wanamuulizia Magufuli. “Nilipokwenda kwenye vikao vya Bunge la SADC ambalo lina wanachama kutoka nchi 14 za Afrika, kila ninapojitambulisha basi wajumbe wanauliza Magufuli. “Wajumbe wengi wa Bunge hilo wanahoji hivi Magufuli alikuwa nani kabla ya kuwa rais wa nchi,” alisema. Kuhusu gesi asilia, aliishauri Wizara ya Nishati na Madini kutafuta ripoti ya Kamati ndogo ya Bunge lililopita ya Nishati na Madini, ichukue mapendekezo na ushauri wake na wayafanyie kazi. “Nilikuwa miongoni mwa wajumbe wa Kamati ndogo ya Bunge ya Nishati na Madini, hivyo naishauru wizara husika kuitafuta ile ripoti ili ichukue yale mapendekezo yetu kwa sababu ni mazuri na yanaweza kusaidia kwenye sekta ya gesi asilia,” alisema. Kwa upande wake, Mbunge wa Viti Maalumu, Rose Tweve (CCM), alisema Magufuli ameuthibitishia umma kwamba rasilimali za nchi hazipotei. Pia aliitaka Serikali kutoa elimu kuhusu umuhimu wa wananchi kumiliki hisa katika kampuni za simu kwa sababu mwitikio wao bado ni mdogo. Mbunge wa Msimbo, Richard Mbogo (CCM), aliishauri Serikali kuwa na soko la madini ili iweze kukusanya mapato mengi katika sekta hiyo. Alisema wafanyabiashara wengi wa madini hawasemi ukweli kuhusu mapato wanayopata ili waweze kulipa kodi stahiki, hivyo ni vema kukaanzishwa soko la madini.
kitaifa
MAREGESI PAUL Na RAMADHAN HASSAN-DODOMA HALMASHAURI Kuu (NEC) ya Chama cha Mapinduzi (CCM), imemrudisha tena Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Philip Mangula, kuwania nafasi hiyo. NEC pia imewateua na kuwapitisha wagombea wawili wa kugombea nafasi za juu katika chama hicho. Mangula aliteuliwa Novemba 2012, kushika wadhifa huo, akichukua nafasi ya Spika mstaafu wa Bunge, Pius Msekwa. Kurudishwa kwa jina la Mangula, kunaondoa minong’ono ya mwanasiasa huyo kupumzika siasa baada ya kuitumikia CCM katika nafasi mbalimbali, ikiwamo ya Katibu Mkuu. Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa jana, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole, alisema katika kikao kilichofanyika jana, NEC iliwateua Rais Dk. John Magufuli kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho, Rais wa Zanzibar, Dk. Ally Mohammed Shein, kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti Zanzibar na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Mangula, kutetea nafasi yake hiyo. “Majina yaliyopitishwa ni ya Dk. John Magufuli kugombea nafasi ya Mwenyekiti, Dk. Ally Mohamed Shein, kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Zanzibar) na Philip Mangula, kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti CCM kwa upande wa Tanzania Bara. “NEC imefanya uteuzi wa kuwapitisha wana CCM hao ambao wataomba ridhaa ya Mkutano Mkuu wa Taifa utakaofanyika kuanzia kesho (leo) na keshokutwa (kesho),” alisema Polepole. Kwa upande wa nafasi za wajumbe wa Halmashauri Kuu Taifa, Polepole alisema waliochukua fomu ni wanachama 51 kwa upande wa Tanzania Bara. “Hapa tuna nafasi 30 ambapo kwa Tanzania Bara, wanatakiwa wawe 15 na Zanzibar wanatakiwa wawe 15 ingawa hadi sasa tumepata majina 51 ya wagombea kwa upande wa Tanzania Bara,” alisema. Kuhusu Mkutano Mkuu huo, Polepole alisema NEC pamoja na mambo mengine, imepitisha ajenda ili uweze kufanyika kwa mafanikio.   KUPANDA, KUSHUKA KWA MANGULA Mangula aliondoka katika uongozi mwaka 2006, baada ya kuchaguliwa Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, kuwa mwenyekiti wa chama hicho akipokea kijiti kutoka kwa Rais mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa. Baada ya kuchaguliwa Kikwete, alipanga upya safu ya viongozi ndani ya chama hicho huku Mangula akiachwa nje na kugeukia kilimo cha viazi nyumbani kwake wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe. Mangula, ambaye alishika nafasi ya Katibu Mkuu wa CCM kwa kipindi cha miaka 10 ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hadi anateuliwa tena kushika nafasi ya umakamu mwenyekiti mwaka 2012, alikuwa mshauri wa mambo ya siasa wa chama tawala cha Afrika ya Kusini – ANC. Nafasi hiyo alianza kuitumikia tangu mwaka 2008 na amekuwa akisifika kuwa ni mtu mwenye mbinu nyingi za kisiasa, hasa kwenye masuala ya uchaguzi na mikakati ya kueneza siasa. Hata hivyo katika uchaguzi wa ndani ya CCM alitupa kete yake kuwania uenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa kabla ya kugawanywa na kuwa mikoa miwili ya Iringa na Njombe mwaka 2012, lakini alijikuta akishindwa kufua dafu dhidi ya Deo Sanga. Katika hatua nyingine, Polepole alisema awali katika kikao cha Kamati Kuu kilichokaa jana, Waziri Mkuu Mstaafu, Dk. Salim Ahmed Salim, alitoa neno la shukrani kwa utumishi wake wa miaka mitano kuanzia mwaka 2012 hadi 2017. Pamoja na hayo, Dk. Salim alionyesha kuridhishwa na uongozi wa Rais Magufuli kutokana na jinsi anavyotanguliza masilahi ya Watanzania, hasa wanyonge. “Rais Magufuli amekuwa kielelezo tosha na kwa vitendo anaishi maisha yanayomuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kamabarage Nyerere. “Nitazidi kuhakikisha CCM inaimarika kwa manufaa ya amani na umoja wetu ndani ya chama chetu na taifa letu la Tanzania,” alisema Dk. Salim……. Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya MTANZANIA
kitaifa
Na MWANDISHI WETU -DAR ES SALAAM SIKU moja baada ya vyombo vya habari vya kimataifa kuripoti tetesi kwamba Rais Mteule Burundi, Evariste Ndayishimiye mgonjwa, Rais Dk. John Magufuli amezungumza naye kwa njia ya simu. Zaidi Rais Magufuli amempongeza kwa uamuzi wa Mahakama ya Katiba nchini Burundi iliyoagiza Rais huyo mteule aapishwe haraka. Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson  Msigwa, katika mazungumzo hayo, Rais Magufuli amemtakia heri Ndayishimiye kuelekea kuapishwa kwake  hivi karibuni kuwa Rais wa Jamhuri ya Burundi Rais Magufuli amemhakikishia Ndayishimiye kuwa Tanzania itaendeleza na kukuza zaidi uhusiano na ushirikiano wake wa karibu na Burundi kwa kuwa nchi hizo ni majirani, marafiki na ndugu wa kihistoria. Rais Magufuli amerudia kumpa pole kwa msiba wa kuondokewa na Rais wa nchi hiyo, Pierre Nkurunziza aliyefariki dunia Juni 09, 2020. Amemueleza kuwa yeye na Watanzania wote wanaungana na Warundi katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo. Amemuomba kufikisha salamu zake za rambirambi kwa Warundi wote na kuwasihi waendelee kuwa watulivu na wastahimilivu. Kabla ya uamuzi huo wa Mahakama ya Burundi kuagiza Rais huyo mteule aapishwe haraka juzi  Baraza la Mawaziri nchini humo lilisema litaongoza nchi hiyo hadi rais mpya atakapoapishwa. Uamuzi huo ulifikiwa kufuatia mkutano uliyofanywa siku ya Alhamisi chini ya uongozi wa Makamu wa Rais wa kwanza Gaston Sindimwo. Wakati Baraza hilo la Mawaziri likifikia uamuzi huo kabla ya ule wa mahakama, Katiba ya nchini Burundi inaonyesha wazi kuwa Spika wa Bunge la kitaifa, Pascal Nyabenda alitakiwa kuapishwa kushikilia wadhifa wa Rais kwa kipindi cha mpito hadi Rais Mteule atakapoapishwa rasmi kuchukua hatamu ya uongozi. Awali kabla ya kifo cha Rais Nkurunziza, rais huyo mteule ilikuwa aapishwe mwezi Agosti baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu wa mwezi Mei. Juzi pia Shirika la Utangazaji la Uingereza la BBC liliripoti taarifa ambazo ilisema hazijathitibitishwa zilizoeleza kuwa Rais huyo Mteule, Jenerali Évariste Ndayishimiye, pia ni mgonjwa. Taarifa hizo zilieleza kuwa mke tu ndiye aliyeonekana na  alipigwa picha akitia saini kitabu cha maombolezo ya kifo cha Rais Ndayishimiye lakini rais huyo mteule hajaonekana hadharani
kimataifa
RAIS wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amesema lengo la Serikali ni kuona sauti za wajasiriamali zinasikika na zinafanyiwa kazi ili kufikia malengo waliyokusudia ya kuwa wafanyabiashara wakubwa.Dk Shein amesema hayo Ikulu wakati alipokutana na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda ilipowasilisha mpango kazi wa Julai 2018 haadi Juni 2019 jana.Amesema matajiri wengi duniani walianza na hatua ya kuwa wajasiriamali wadogo kwa hivyo ni vyema waliopo wakapewa kipaumbele katika shughuli wanazozifanya ili wapate mafanikio makubwa .Alisema nchini wapo baadhi ya matajiri walioanza wakiwa wajasiriamali wadogo, hivyo si jambo la busara kuwabeza.''Mikakati yetu ni kuona wajasiriamali wanaendelezwa katika hatua mbalimbali ili waweze kufikia malengo waliyokusudia ya kuwa wafanyabiashara wakubwa,'' amesema.Aidha, Dk Shein amesema azma ya ujenzi wa kiwanda cha uzarifu wa bidhaa ya Mwani ipo pale pale huko Chamanangwe Pemba kwa ajili ya kuwawezesha wakulima kupiga hatua kubwa ya uzalishaji wa bidhaa hiyo.Amesema wakulima wengi wa kilimo cha Mwani wamehamasika na kujiajiri na ukulima wa zao hilo zaidi katika maeneo ya mwambao wa pwani huku wanawake wakiongoza.''Mipango yetu ni kujenga kiwanda cha Mwani ambacho kitasaidia kusarifu bidhaa hiyo na kuleta tija kwa wakulima wetu Unguja na Pemba''amesema.Awali, Waziri wa Biashara na Viwanda, Balozi Amina Salum Ali, aliwataka wakulima kujikita zaidi katika kilimo cha mazao ya viungo ambayo hivi sasa soko lake ni kubwa na la uhakika nje ya nchi.Alisema mazao ya viungo aina ya Pilipili manga, Pipilipi hoho, Uzile na Hiliki yana soko la uhakika katika nchi za Bara la Asia na Urabuni.''Tumepewa nafasi ya kuzalisha mazao ya viungo katika nchi mbalimbali za Asia na Uarabuni hadi China ikiwemo mafuta ya Makonyo na Mlangilangi,'' amesema.
kitaifa
“Samsung Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge zitakuwa zikitolewa kupitia maduka yetu yote huku zikiambatanishwa na Power-Bank ya bure; pia wateja 50 wa kwanza watajipatia Bluetooth Earphones za Galaxy za bure pia,” alisema Samson Mwongela, Mkuu wa Kitengo cha Huduma na Bidhaa cha Vodacom Tanzania.Mwongela alibainisha kuwa simu hizo zimekuja zikiwa na maboresho yanayolenga kukidhi mahitaji ya vijana wa kisasa hususan katika msimu huu wa sikukuu ya Pasaka, ambapo watumiaji watafurahia na intaneti ya kasi na haraka zaidi nchini kutoka Vodacom.Akielezea sifa za simu hizo, Meneja Mwendeshaji wa Samsung nchini, Suleiman Mohammed alisema zina uwezo wa kutoingiza maji, hata pale zinapokuwa katika kina cha mita moja na nusu kwa dakika zisizozidi 30.“Hakika kwa sasa hakuna tena kikomo kwa vijana hapa nchini kuweza kuwasiliana na ndugu, jamaa na rafiki zao popote walipo ulimwenguni, hasa ukizingatia tunaelekea kufikia tamati ya matumizi ya simu zisizokuwa halisi na zenye ubora hapa nchini kabla ya kuisha Juni mwaka huu,” alisema Mohammed.
uchumi
Na ELIUD NGONDO, CHUNYA ZAIDI ya Sh milioni 85 zinahitajika katika Hospitali ya Wilaya ya Chunya, mkoani Mbeya kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa chumba cha kuhifadhia maiti hospitalini hapo. Akizungumza jana kwenye harambee ya uchangiaji wa vifaa vya ujenzi wa chumba hicho na fedha, Mganga Mkuu wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Stanford Mwakataghe, alisema wananchi na wadau wanatakiwa kuchangia ujenzi huo. “Wilaya yetu kwa sasa ina miaka 74 tangu ianzishwe na mwakani kuna mkakati wa kusherehekea miaka 75. “Pamoja na mikakati hiyo, hakuna chumba cha kuifadhia maiti katika hospitali ya wilaya, hali ambayo imekuwa ni shida kwa wananchi. “Kutokana na tatizo hilo, kumekuwa na ulazima wa kuzika watu haraka kwa sababu hakuna sehemu ya kuhifadhi miili kwani hata chumba kilichopo kwa ajili ya maiti, kina uwezo wa kuhifadhi mwili mmoja. “Kutokana na tatizo hilo, wananchi wamekuwa wakipata shida kwani hata sisi watumishi inatuwia vigumu kutunza miili ya wapendwa wetu kwa sababu hakuna sehemu ya kuhifadhia,” alisema Mwakataghe. Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sostenes Mayoka, alisema ujenzi wa chumba hicho unategemea sana wadau mbalimbali wa wilaya hiyo pamoja na mchango wa halmashauri. Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Sophia Kumbuli, alisema fedha zilizopatikana wakati wa harambee hiyo, zitaelekezwa katika ujenzi wa chumba hicho cha maiti.
kitaifa
NA DAMIAN MASYENENE  – SHINYANGA SERIKALI imesema imefikia makubaliano na wanunuzi wa pamba kuwa ifikapo Desemba 8, walipe Sh bilioni 47 ambazo ni madeni ya wakulima wa pamba. Makubaliano hayo yalifikiwa juzi katika kikao kilichokaa kwa saa sita kati ya Serikali na wadau wa zao la pamba kilichofanyika mkoani Shinyanga kikihudhuriwa na wakuu wa mikoa inayolima zao hilo.  Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe, alisema changamoto zilizojitokeza msimu uliopita hazitakuwapo msimu ujao. Alisema kila mkulima atalipwa fedha zake moja kwa moja katika akaunti yake ya benki na kupata pembejeo kwa mkopo, huku akitoa onyo kwa viongozi wa Amcos kutowalazimisha wakulima kulipia mbegu. “Wilaya zote ambazo wakulima wake hawajalipwa pesa, wahakikishe Amcos zote zina akaunti benki, na hili ni agizo tumelitoa na zoezi hili lifanywe Jumamosi (jana). “Fedha hizo za wanunuzi zipelekwe kule alafu wakuu wa wilaya wasimamie kulipwa kwa wakulima, kampuni zote zinazodaiwa baada ya kulipa basi wapeleke taarifa hizo kwa wakuu wa wilaya. “Gari zote za mbegu zikifika wilayani ziripoti kwa wakuu wa wilaya ili hawa viongozi wasimamie na kusiwe na kuwalazimisha wakulima kulipia hizo mbegu,” alisema Bashe. Kwa upande wao baadhi ya wanunuzi wa zao la pamba walisema watahakikisha wanalipa haraka iwezekanavyo deni la wakulima ili waweze kuingia msimu mwingine wa kilimo na kusambaza mbegu kwa wakulima. Mmoja wa wanunuzi hao, Fred Shoo alisema wakilipa mapema watapata fursa ya kujiandaa kwa msimu unaofuata, huku akiishukuru Serikali kwa kuwa na usikivu katika kuratibu mazingira ya biashara ili yalete faida kwa pande zote mbili. Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, alisema kikao kimeazimia madeni yote ya mwaka jana yalipwe kabla ya Desemba 8, ili iwe chachu ya kuongeza uzalishaji wa zao hilo kwa msimu ujao. mwisho
kitaifa
HALMASHAURI ya Wilaya ya Chamwino imepewa mwezi mmoja kuhakikisha imepima viwanja na kuuza, ili kuongeza mapato ya ndani huku akitaka wafanyakazi kuwekewa utaratibu wa kuuziwa viwanja kwa bei nafuu.Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa halmashauri hiyo. Jafo ameendelea kusisitiza kuwa Mkurugenzi ambaye halmashauri yake itashindwa kutenga na kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa watu wenye ulemavu, vijana na wanawake kwa mwaka wa fedha unaoishia Juni 30, mwaka huu, atatumbuliwa.Alisema Chamwino ambayo ndio wilaya ilipo Ikulu, haitakiwi kuwa nyuma kimapato kwani wakitumia chanzo cha upimaji na uuzaji wa viwanja, halmashauri hiyo itaongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani.“Ninyi Ikulu iko kwenu, kwanini msipime maeneo yenu na kuuza, tena mnaweza kuuza kwa bei ambayo wananchi wanaweza kununua, kwa kufanya hivi mtakuwa mmeupanga mji wenu vizuri lakini pia mapato ya ndani ya taongezeka.”Jafo aliagiza wapime na kuuza ndani ya mwezi mmoja hadi mwisho wa Julai na kwamba, wakichelewa wanaweza kujikuta mapato yakienda Halmashauri ya Jiji la Dodoma. Jafo pia alisema baada ya kukamilisha upimaji na uuzaji wa viwanja ni vyema wakatoa pia kipaumbele kwa wafanyakazi wa halmashauri hiyo ambao wanaweza kuuziwa kwa bei nafuu na kuwekewa utaratibu wa kulipa kidogo kidogo.“Mkiwaweka wafanyakazi wenu kwenye mpango wa kupewa viwanja na kuwawekea utaratibu mzuri wa kulipa, mtawajengea kuwa na ari ya kufanya kazi, hivyo msiwaache wafanyakazi kwenye mpango wa viwanja,” alisema.Aidha, alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chamwino na uongozi wake kwa ujumla kwa kuhakikisha inatoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya wanawake, vijana na walemavu. Mwaka wa fedha 2018/2019 ni mwaka wa kwanza wa utekelezaji wa sheria iliyotungwa na Bunge ambayo inazilazimisha halmashauri zote nchini kutenga asilimia 10 ya mapato ya ndani na kutoa kwa vikundi vya vijana (asilimia 4), wanawake (asilimia 4) na watu wenye ulemavu (asilimia 2).
kitaifa
Hatua hiyo inatokana na kukamilika vizuri kwa ofa ya awali kwa umma, ijulikanayo kwa kifupi kama IPO baada ya kukamilika ofa ambayo ilianza Juni 9, 2014 hadi Julai 4, 2014.Kampuni hiyo ya Swala ilitarajia kuuza hisa milioni 9.6 za kawaida. Lakini, waliuza hisa zaidi ya lengo na kufikia milioni 13.3 na kwa sasa ina wanahisa wapya 1,868.“Utaratibu wa ofa za awali kwa umma, umekamiliki vizuri na ofa za awali za Swala zilizidi idadi iliyokusudiwa kujiunga na kwa wale ambao hawakuweza kununua hisa za Swala katika mgawo wa awali, wataweza kuzinunua katika soko la hisa katika siku hizo zilizotajwa,” alisema Meneja Mratibu wa DSE, Magabe Maasa.Alisema Kampuni ya Swala itakuwa ya 20 kuorodheshwa DSE. Pia, itakuwa kampuni ya kwanza ya mafuta na gesi kuorodheshwa katika soko la hisa ndani ya Afrika Mashariki. Meneja Mkuu wa Swala, David Mestres aliongeza,“Tunafurahi sana kuongezeka kwa waliojiunga, hali hii inaonesha ari iliyopo Tanzania ya kuwekeza katika maliasili”.Alisema mwamko huo unaonesha maendeleo ambayo DSE imekuwa ikijitahidi kuwashawishi wawekezaji wa ndani na nje ya nchi katika biashara za Tanzania.Swala ni kampuni ya kwanza ya mafuta na gesi katika orodha ya soko la hisa la Afrika Mashariki. Ipo chini ya kivuli cha Swala Energy Limited, kampuni ambayo iko kwenye orodha ya soko la hisa la Australia (ASX), ikijulikana kwa kifupi kama SWE.
uchumi
MKUU wa Mkoa wa Singida, Dk Rehema Nchimbi amewataka wafanyabiashara na wenye viwanda wanaotengeneza na kuuza taulo za kike, kutengeneza zenye ubora. Alisema mkoa wake umeanzisha msako wa kiintelijensia na kimkakati kuzisaka taulo zisizo na ubora na atakayebainika atachukuliwa hatua.Alisema hayo wilayani Ikungi katika uzinduzi wa uchangishaji wa taulo za kike Singida jana, uliopewa jina la “Mjali mtoto wa kike kwa maendeleo yake na Taifa lake”.Alitoa rai kwa wadau wote kuwabaini na kutoa taarifa za wafanyabiashara watakaojaribu kuuza taulo zisizo na ubora kuwalinda watoto wa kike. Alisema kutokana na mageuzi makubwa ya kiuchumi yanayofanywa na Rais John Magufuli, Tanzania imepanda kiuchumi duniani hivyo mikakati ya kudhibiti ubora inahitajika katika kipindi hiki kuliko kipindi kingine chochote. Dk Nchimbi alisema vyombo vya dola, viongozi wa dini na wazazi wana mchango mkubwa kumlinda mtoto wa kike kwa ustawi wa taifa.“Ndiyo maana tunataka kujua mipango ya udhibiti ubora kwa watengenezaji kwani majuto ni mjukuu, tusisubiri kufika huko,” alisema.Alisema ubora wa taulo za kike ni ubora wa maisha yao, hivyo ni muhimu kuchukua hatua za kuangalia na kudhibiti mnyororo mzima wa uzalishaji na usambazaji taulo zisizo na ubora. Alitoa mwito wa wajasiriamali kuja na andiko zuri la utengenezaji wa taulo bora za kisasa zitakazotengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nchini na mshindi atakayepatikana atazawadiwa kiasi cha Sh milioni moja.Aliwataka wadau kutambua thamani ya mtoto wa kike ambapo katika uzinduzi huo lengo lilikuwa ni kuchangia paketi 8,000 za taulo za kike lakini zilipatikana paketi zaidi ya 9,089. Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Ikungi, Justice Kijazi alimshukuru kwa wazo la kutaka Halmashauri zote Singida kutoa elimu ya jinsia shuleni na kuwachangia watoto wa kike taulo.Alizitaja baadhi ya changamoto zinazowakabili watoto wa kike kuwa ni pamoja na mimba za utotoni, kubakwa, kuozeshwa katika umri mdogo na kufanyishwa kazi nyingi nyumbani. Mratibu wa programu hiyo ya uchangiaji wa taulo za mtoto wa kike, Ofisa Maendeleo ya Jamii wilaya ya Ikungi, Haika Massawe alipendekeza wazazi wahusishwe kikamilifu.
kitaifa
INSPEKTA Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amewateua makamishna sita kuwa makamanda wa polisi na wengine watatu waliokuwa makamanda wa polisi mikoa mbalimbali wamepangiwa kazi nyingine.Sirro alisema jana jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na waandishi kuelezea mabadiliko hayo na uteuzi wa makamishna uliofanywa na Rais John Magufuli. Aliwataja walioteuliwa kuwa MaRPC kuwa ni Jonathan Shana kwenda Mkoa wa Arusha na Amon Kakwale kwenda mkoa wa Kipolisi Temeke jijini Dar es Salam.Pia Simon Maigwa kwenda mkoa wa Ruvuma, Salum Hamduni kwenda mkoa wa Njombe, Richard Abwao kwenda Shinyanga na Zuber Chembera kwenda mkoa wa Kipolisi Ilala jijini Dar es Salaam.Aliwataja makamishna waliokuwa maRPC ambao sasa wamepangiwa majukumu mengine kuwa ni Gemin Mushi aliyekuwa Ruvuma sasa anakuwa Mkufunzi Mkuu Chuo cha Polisi Moshi, Renata Mzinga aliyekuwa Njombe na Simon Haule aliyekuwa Shinyanga wanakwenda Makao Makuu Polisi jijini Dar es Salaam. Wakati huo huo aliwataja makamishna wawili ambao wamehamishiwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa ni Albert Nyamhanga kutoka Kamishna wa Polisi Utawala na Menejimenti ya Utumishi pamoja na Nsato Marijani kutoka Kamishna wa Polisi Operesheni ya Mafunzo.Awali alisema Rais John Magufuli amefanya uteuzi na kuwapandisha vyeo baadhi ya maofisa wa polisi kuwa makamishna wa polisi ambao ni aliyekuwa Naibu Kamishna wa Polisi Charles Mkumbo ameteuliwa na kupandishwa cheo kuongoza Kamisheni ya Polisi Intelijensia ya Jinai.Pia Naibu Kamishna wa Polisi Liberatus Sabas ameteuliwa na kupandishwa cheo kuongoza Kamisheni ya Polisi Operesheni na Mafunzo na Naibu Kamishna wa Polisi Shaban Mlai ameteuliwa kuongoza Kamisheni ya Polisi Maabara ya Uchunguzi wa Kisayansi. Vile vile Naibu Kamishna wa Polisi Leonard Lwabuzala ameteuliwa kuongoza Kamisheni ya Polisi Fedha na Lojistiki.
kitaifa
Majaliwa ampa mkurugenzi siku 16 kutoa mil.114/- WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa ametoa siku 16 kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, Magreth John awe amepeleka asilimia 20, sawa na Sh. milioni 114, ya kijiji cha Holili kabla ya Machi 10, mwaka huu.Kiasi hicho kinatokana na mauzo ya madini ya pozolana.Ametoa maagizo hayo leo (Jumamosi, Februari 23, 2019) wakati akizungumza na watumishi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha cha Holili pamoja na wananchi wa kijiji cha Holili, akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Kilimanjaro. Kituo hicho cha Holili kipo katika mpaka wa Tanzania na Kenya.Waziri Mkuu alitoa maagizo hayo baada ya wananchi wa kijiji cha Holili kuwasilisha malalamiko yao kupitia mabango wakimuomba kiongozi huyo awasaidie ili Halmashauri ya Rombo iweze kulipa fedha zao zinazotokana na mapato ya mauzo ya madini hayo yanayochimbwa kijijini kwao. “Mkuu wa wilaya (Agness Hokororo) hakikisha kiasi hicho cha fedha kinakwenda kwa wananchi na Mkuu wa Mkoa (Dk Anna Mghwira) nataka nipate taarifa kuwa fedha hizo zimeshalipwa kwa uongozi wa kijiji husika,” Waziri Mkuu aliagiza. Wakati huo huo, Waziri Mkuu amesema hali ulinzi na usalama katika mpaka huo si nzuri hivyo, serikali imeamua kuimarisha ulinzi kwenye mpaka huo, hivyo ni muhimu kwa wananchi washirikiane katika kuulinda. Ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuwakamata na kuwachukulia hatua watu wote watakaokamatwa wakipita au kuingiza mizigo kupitia njia zisizo rasmi kwa sababu baadhi yao wasio waaminifu hupitisha hata silaha. Waziri Mkuu amesema wananchi wa Tanzania na Kenya hawajazuiwa kufanya biashara upande wowote bali wanatakiwa wafuate sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika nchi husika ikiwa ni pamoja na kutumia njia rasmi. Amewataka viongozi na watendaji waliopo maeneo ya mipaka huo wa Holili kuwa makini kwa sababu mpaka huo hauko salama na kuna mambo mengi yanayoendelea ambayo yapo kinyume cha sheria. 
kitaifa
SERIKALI imetaifi sha jumla ya leseni 33,000 za madini, zilizokuwa zinamilikiwa na baadhi ya wafanyabiashara wa madini ambazo walikuwa hawaziendelezi, na imezikabidhi kwa wachimbaji wadogo wanaotambulika kisheria.Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini, Dotto Biteko (pichani) alipozungumza kwenye hafla maalumu ya uzinduzi wa soko la madini, jana. Hafla hiyo ilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Profesa Simon Msanjila, Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, wakuu wa wilaya, wenyeviti wa halmashauri, wakurugenzi wa halmashauri, wawakilishi wa vyama vya uchimbaji madini, taasisi za fedha na wachimbaji madini.Biteko alisema serikali ilichukua leseni hizo na kuwakabidhi wachimbaji wadogo hao ili kuwawezesha kumiliki uchumi wa nchi kupitia sekta ya madini na wakati huo huo kuboresha mapato ya serikali kupitia kodi. Alisema dhamira ya serikali ni kuona Watanzania wote wananufaika na rasilimali za madini zilizopo nchini hususani wafanyabiashara wakubwa na wadogo wa madini.Alisisitiza kuwa itawatengenezea mazingira mazuri ya kufanya biashara kupitia masoko hayo ya madini. “Tutawekea mazingira mazuri ya kusafirisha madini yenu kwenda kwenye masoko, badala ya kufanya biashara ya utoroshaji wa madini, lakini hatutawavumilia wale wanaofanya biashara za uchochoroni,” alisema Biteko. Alisema baadhi ya watu ambao wamekuwa biashara za madini kwa njia za panya, wengi wao wamekamatwa kimya kimya na serikali na tayari wamefikishwa kwenye vyombo vya sheria.“Watu hao wamekamatwa kwa sababu tu ya kukwepa kulipa kodi ya serikali, lazima tubadilishe nchi yetu, watu wazungumze namna bora ya kufanya biashara hii ya madini, badala ya kukesha mitandaoni na kujadili mambo binafsi ya watu tukuze uchumi wa nchi yetu,” alisema.Alisema haingiii akili kuona mtu anakwepa kulipa kodi halali ya serikali ya Sh milioni tano ya madini na badala yake anatoa mlungula wa Sh milioni 100 kwa kupitia njia za panya. “Tusichezee mitaji yetu, mtu yeyote anayetaka kutorosha madini yetu, cha kwanza atafilisiwa na cha pili ataishia jela, furaha yetu kama serikali ni kuona mnanufaika na rasilimali madini na nchi inanufaika kwa kupata kodi yake kwa ajili ya maendeleo,” alisema.Alisema katika kipindi cha muda mfupi tangu kufunguliwa kwa masoko ya madini ya Geita na Chunya, kwa soko la Chunya serikali ilikuwa inakusanya gramu nne tu, lakini kiasi cha kilo 22 kimenunuliwa kwa siku nne tu. Alisema kwa sasa soko la madini la Geita, limenunua jumla ya kilo 198 za dhahabu katika kipindi cha mwezi mmoja zenye thamani ya mabilioni ya fedha.“Mtaona ni kiasi gani cha dhahabu ambacho tulikuwa hatupati na mapato ya serikali,” alisema na kuongeza kuwa mtu yeyote anaruhusiwa kuuza dhahabu yake kwenye masoko ya dhahabu yaliyoanzishwa nchini isipokuwa anatakiwa kulipa kodi zote stahiki za serikali. “Pelekeni madini yenu ya dhahabu kwenye masoko ya Geita, Chunya na hapa Mwanza, serikali haiwazuii kuuza madini yenu,” alisema.Aliongeza kuwa katika kuwajali wachimbaji wadogo wa madini, Rais John Magufuli amefuta takribani kodi nane za madini zilizokuwa kero kwa wachimbaji hao ili kuongeza mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa. Aliushukuru uongozi wa Mkoa wa Mwanza kwa uzinduzi wa soko kubwa na zuri kuliko masoko yote 13, ambayo tayari yameishazinduliwa nchini, na matarajio ya serikali ni kuona taratibu za ununuzi wa dhahabu zinafuatwa.Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Profesa Msanjila alisema soko hilo la madini ni sehemu ya masoko mengine ya madini matatu yaliyofunguliwa jana ambayo ni Kagera, Iringa na mkoani Songwe.Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella alisema soko hilo la madini, litakuwa ni kituo cha biashara ya madini kwa nchi za Afrika Mashariki. Mwakilishi wa wafanyabiashara wa madini, Makoni Kaniki aliishukuru serikali kwa kuanzisha soko hilo la madini jijini Mwanza, ambalo litawasaidia katika kuinua uchumi wao. “Soko hili ni la kiwango na hatuwezi kulilinganisha na masoko mengine yaliyoanzishwa hapa nchini,” alisema Kaniki.Akizungumza kwa niaba ya taasisi za fedha, Meneja wa Kanda ya Ziwa wa Benki ya NMB, Abraham Augustino aliishukuru serikali kwa kuona umuhimu wa kuanzisha masoko hayo kwa wafanyabiashara wa madini, na NMB iko tayari kufanya kazi na wafanyabiashara hao kwa lengo la kuinua vipato vyao na uchumi wa nchi.
kitaifa
Na MWANDISHI WETU-DAR ES SALAAM KOCHA mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm, amesema sasa yupo makini kupambana katika mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya kushtukia ujanja unaofanywa na timu zinazoshiriki ligi hiyo msimu huu. Yanga ambao ni wabingwa watetezi wa ligi hiyo, tayari wamecheza michezo minne na kufanikiwa kushinda mitatu huku ikilazimishwa sare mara moja. Kocha huyo raia wa Uholanzi, aliliambia MTANZANIA jana kuwa amegundua kuwa timu zote zinakamia zaidi mechi dhidi ya Yanga, changamoto inayowalazimu kucheza mechi zote kama fainali. Alisema ugumu wa mechi zao unatokana na sababu kwamba kila timu inapambana ili kuifunga Yanga kwa kuwa ni mabingwa, ndio maana analazimika kuongeza umakini na kuwapa wachezaji wake mbinu za ziada. “Wapinzani wanajipanga zaidi wanapokaribia kucheza dhidi ya Yanga, maandalizi ambayo ni tofauti kabisa na yale waliyofanya katika mechi zao zilizopita, hii kwetu ni changamoto ambayo nimeanza kuifanyia kazi. Akizungumzia mchezo wa kesho dhidi ya Stand United utakaochezwa katika Uwanja wa Kambarage, Shinyanga, Pluijm alisema anawaheshimu wapinzani wao kutokana na ubora wa kikosi walichonacho, hivyo wanajiandaa kwa mechi yenye ushindani mkubwa. Mholanzi huyo alisema siku zote matokeo ya ushindi yanatokana na maandalizi mazuri, hivyo hawezi kubweteka kwa ushindi walioupata Jumamosi iliyopita dhidi ya Mwadui FC. Aidha, Pluijm alisema sasa ameweka pembeni malalamiko ya ubovu wa viwanja vinavyotumika kwa mechi za ligi kuu, kwa kuwa hakuna mabadiliko yoyote yanayoweza kufanyika kubadilisha hali hiyo.
michezo
KAMPUNI ya Clouds Media Group (CMG) imepata pigo jingine katika muda mfupi baada ya aliyekuwa mtangazaji wake mahiri, Ephraim Kibonde (47) kufariki dunia jana alfariji Mwanza na anatarajiwa kuzikwa jijini Dar es Salaam.Kifo cha Kibonde kimekuja siku chache baada ya kampuni hiyo, kupatwa na msiba wa aliyekuwa mmoja wa waasisi wake na Mkurugenzi wa Utafiti na Vipindi, Ruge Mutahaba aliyefariki nchini Afrika Kusini, Februari 26, mwaka huu.Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk Thomas Rutachunzibwa alithibitisha kuhusu kifo cha Kibonde, akisema jana saa 11:30 asubuhi katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, walipokea mwili wa marehemu Kibonde. Dk Rutachunzibwa alisema Kibonde aliugua ghafla akiwa kwenye maziko ya Ruge wilayani Bukoba.Kwa mujibu wake, Kibonde alipata matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera mjini Bukoba kisha alihamishiwa katika Hospitali ya Uhuru jijini Mwanza, na wakati alipokuwa akipelekwa Hospitali ya Bugando kwa matibabu zaidi baada ya hali yake kubadilika usiku wa kuamkia jana, ndipo umauti ukamkuta njiani.Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa CMG, Joseph Kusaga, mwili wa Kibonde ulitarajiwa kuwasili jijini Dar es Salaam jana usiku ukitokea Mwanza. Ulitarajiwa kupumzishwa kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi, Lugalo.Kusaga alisema Kibonde aliyekuwa akihudumu Clouds FM Radio, atazikwa kesho katika makaburi ya Kinondoni. Kibonde ambaye mbali na kuwa mtangazaji, pia alikuwa mshereheshaji (MC) mahiri, alikuwa MC kwenye msiba wa Ruge akiifanya kazi hiyo siku ya kuagwa kwenye Viwanja vya Karimjee Dar es Salaam, baadaye Viwanja vya Gymkhana, Bukoba na kijijini Kiziru ambako Ruge alizikwa, akishirikiana na mtangazaji mwenzake, Baby Kabaye.Kifo cha Kibonde kimekuja ikiwa ni takribani miezi minane baada ya kifo cha mkewe, Sarah aliyefariki kwa ugonjwa wa saratani na kuzikwa makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Kibonde alikuwa mmoja wa watangazaji wa mwanzo wa Clouds FM, ambako alianza kwa kutangaza vipindi vya michezo kabla ya kuanzisha na kusimamia kipindi cha Jahazi.Akizungumzia kifo hicho, Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete aliandika katika twitter yake, “Majonzi yangali nasi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika akitoa maelekezo kwa mhandisi Lucas Lipambila (kushoto) wakati wa ziara ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Ofisi ya Utumishi katika Mji wa Serikali Ihumwa, Dodoma jana.Katikati ni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Mary Mwanjelwa. (Na Mpigapicha Wetu). nimepokea taarifa ya kifo cha Mtangazaji Ephraim Kibonde wa @cloudsfm.Ni pigo kubwa kwetu sisi wapenzi wa kipindi cha Jahazi. Jahazi litaeleaje bila ya Nahodha Kibonde? Mwenyezi Mungu na aipe faraja familia yake, @ cloudsfm na wasikilizaji wote wa Jahazi.” Alikuwa mtangazaji mahiri mwenye uwezo wa hali ya juu wa kujenga hoja huku akiwa na uelewa mpana katika nyanja za siasa, uchumi, michezo, sanaa na hata masuala ya kijamii, alikuwa mcheshi na mwenye utani mwingi. Ameacha watoto watatu ambao ni Junior, Hilda na Illaria.
kitaifa
['Manchester United wanaweza kumsajili kocha wa timu ya taifa ya England Gareth Southgate endapo watamtimua Ole Gunnar Solskjaer mwishoni mwa msimu. (Sun)', 'Kocha msaidizi wa United Mike Phelan amesema klabu hiyo bado inataka kusajili wachezaji nyota. (Evening Standard)', 'Chelsea wapo tayari kuvunja rekodi yao ya uhamisho ili kumsajili mshambuliaji wa England na klabu ya Borussia Dortmund Jadon Sancho, 19. (Goal)', 'Chelsea itapata majibu hii leo endapo marufuku waliopigwa ya kufanya usajili (kwa madirisha mawili) inayotarajiwa kuisha mwezi Februari kama itaondoshwa na kuruhusiwa kuingia sokoni mwezi Januari. (Daily Telegraph)', 'Kocha wa Real Madrid Zinedine Zidane bado anataka kumsajili kiungo wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba, 26. (Marca)', 'Manchester City wanaamini kuwa mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 24, atasaini mkataba mpya na klabu hiyo utakaomfanya kuwa mchezaji anayelipwa mshahara mkubwa zaidi klabuni hapo. (Metro)', "Liverpool na Arsenal wameungana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Ujerumani Karim Adeyemi, 17 kutoka klabu ya RB Salzburg. (Sport via Mirror)", 'Everton wanajiandaa kumpa mkataba wa muda mrefu kwa beki wa kushoto wa Ufaransa Lucas Digne, 26. (Mail)', 'Kocha wa Atletico Madrid ya Uhispania Diego Simeone, ambaye hapo kabla alikuwa akiwaniwa na klabu ya Everton ya England yu mbioni kuachana na miamba hiyo ya Uhispania. (Marca via Sport Witness)', 'Atletico wamekubali kumsajili kiungo machachari kutoka klabu ya Athletico Paranaense ya Brazili Bruno Guimaraes, 21, kwa dau la pauni 25.4m. (UOL, in Portuguese)', 'Tottenham wanapanga kumsajili beki wa kati wa klabu ya Norwich Ben Godfrey, 21, mwenye thamani ya pauni milioni 25. (Football Insider) ', 'Tetesi bora za Jumatano ', 'Kocha aliyetimuliwa na Tottenham Mauricio Pochettino anataka kumrithi Ole Gunnar Solskjaer kama kocha wa Manchester United. (Manchester Evening News)', 'Tottenham wapo tayari kupokea ofa za usajili za chini ya pauni milioni 40 kwa kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 27. (Evening Standard)', 'Spurs haina mpango wa kumsajili kiungo Mserbia anayechezea Manchester United Nemanja Matic, 31. (Manchester Evening News)', 'Rais wa Shirikisho la Soka Ulaya (Uefa) Aleksander Ceferin amesema teknolojia ya usaidizi ya mwamuzi ama VAR ni "uozo" japo "haiwezekani kurudi nyuma". (Mirror)', 'Arsenal wamefanya mawasiliano na kocha wa zamani wa Valencia Marcelino wakati klabu hiyo ikiendelea kusaka kocha mpya wa kudumu. (Goal - in Spanish)', 'Kocha wa Tottenham Jose Mourinho ameacha kumfuatilia kiungo wa Sporting Lisbon Bruno Fernandes, 25, kutokana na kuwa na dau la pauni milioni 85 katika mkataba wake. (Mail)']
michezo
UPANDE wa utetezi katika kesi ya utakatishaji fedha inayomkabili aliyekuwa Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na wenzake umepinga mahakama kupokea nyaraka zilizotumika kuingiza nyasi bandia na nyaraka za kuomba msamaha wa kodi zilizopelekwa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na klabu hiyo.Wakili wa Utetezi, Nehemiah Nkoko alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba. Awali, Mchunguzi Mkuu kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Frank Mkilanya alidai nyasi hizo zilinunuliwa kwa wakala anayeitwa Hamisi na zilitoka katika Kampuni ya Nina iliyopo China.Alidai wakati wa uchunguzi, alimhoji Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu hiyo, Zacharia Hans Poppe ambaye alidai Hamisi alifariki na akampa cheti cha kusafirishia mwili ambacho aliomba kukitoa kama kielelezo. Wakili wa Serikali, Leonard Swai aliomba kutoa kielelezo hicho mahakamani ili kitumike kama ushahidi. Hata hivyo, Wakili Nkoko alipinga kupokewa kwa kielelezo hicho kwa madai kwamba si nakala halisi na kinachothibitisha kifo ni cheti cha kifo.Alidai kwa mujibu wa sheria ni lazima shahidi aseme kwamba nyaraka halisi iko wapi. Akitoa uamuzi Hakimu Simba alikubaliana na hoja za upande wa utetezi na kukataa kupokea kielelezo hicho.Akiendelea na ushahidi, shahidi huyo alidai katika uchunguzi, alibaini viongozi wa Klabu ya Simba walipeleka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) nyaraka ikionesha nyasi walizinunua kwa zaidi ya Dola za Marekani 40,000 lakini alipohoji aliambiwa walinunua kwa Dola za Marekani 109,000.Alidai viongozi hao walipotakiwa kupeleka nyaraka TBS ili wapate msamaha wa tozo ya ukaguzi wa mzigo walipeleka nyaraka ya Dola za Marekani 40,000. Shahidi alidai mzigo huo haukufanyiwa ukaguzi China hivyo walitakiwa kulipa gharama lakini kutokana na barua waliyoandika TBS walisamehewa.Alidai aliitaarifu TRA kuhusiana na nyaraka hizo. Baada ya kudai hayo, aliomba kutoa nyaraka hizo kama kielelezo mahakamani lakini mawakili wa utetezi walipinga wakidai hana mamlaka ya kutoa kielelezo hicho. Hakimu Simba aliahirisha kesi hiyo hadi Agosti 28 mwaka huu kwa ajili ya kutoa uamuzi mdogo kuhusu mapingamizi hayo.
michezo
Matokeo hayo hayaiweki Stars kwenye nafasi nzuri sana ya kusonga mbele kwenye michuano ambayo mshindi wa kila kundi ndiye atakayefuzu moja kwa moja fainali. Tanzania na Lesotho zipo kundi A pamoja na timu za Uganda na Cape Verde zinazotarajiwa kucheza leo.Nahodha Mbwana Samatta ndiye aliyeanza kuwainua watanzania vitini kwa kuandika bao la kuongoza kwa mpira faulo uliokwenda moja kwa moja nyavuni katika dakika ya 27. Mwamuzi aliamuru faulo hiyo ipigwe baada ya beki wa Stars Gadiel Michael kuchezewa vibaya na beki wa Lesotho.Dakika saba baadae wageni Lesotho walisawazisha bao hilo kupitia kwa Thapelo Tale aliyeunganisha pasi nzuri ya Jane Thaba- Ntso na kuujaza mpira wavuni. Katika kipindi cha kwanza timu hizo zilishambuliana kwa zamu ingawa dakika za mwanzoni Stars ilikosa mabao kadhaa Samatta, Thomas Ulimwengu na Shizza Kichuya.Stars iliendelea na mashambulizi yake mpaka katika kipindi cha pili lakini kutokuwa makini kwa safu yake ya ushambuliaji kuliwakosesha mabao mengi. Katika mechi nyingine zilizochezwa jana, kundi B Malawi iliifunga Comoro bao 1-0 na wenyeji wa michuano hiyo ya 2019 Cameroon wakiwapata matokeo kama hayo dhidi ya Morocco.Kundi C Burundi ilishinda mabao 3-0 dhidi ya Sudan Kusini huku Nigeria ilifungwa mabao 2-0 na Afrika Kusini nyumbani katika kundi E na kundi F Sierre Leone ikiifunga Kenya mabao 2-1.Kundi I Botswana ikiwa nyumbani imefungwa bao 1-0 na Mauritania huku kundi K Zambia ikiwa nyumbani nayo ilikubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Msumbiji na Guinea Bissau ikiifunga Namibia bao 1-0. Mechi hiyo ni ya tatu kwa Stars kucheza chini ya kocha Salum Mayanga baada ya kushinda mabao 2-1 dhidi ya Burundi na 2-0 dhidi ya Botswana katika mechi za kirafiki za kimataifa Machi mwaka huu.
michezo
WAKAZI 680,000 mkoani Pwani wanatarajiwa kuandikishwa kwenye daftari la wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa mitaa vitongoji na vijiji utakaofanyika Novemba 24 mwaka huu. Hayo yalisemwa mjini Kibaha na Mkuu wa Mkoa huo, Evarist Ndikilo mara baada ya kujiandikisha kwenye ofisi za serikali ya mtaa wa Mwanalugali A anakoishi akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiwa ni sehemu ya uhamasishaji wananchi kujiandikisha. Aidha alisema hadi Oktoba 10, mwaka huu idadi ya watu waliojiandikisha ni 160,000 sawa na asilimia 23 na kuwataka wananchi kujitokeza kujiandikisha kwa muda huu uliobakia.Ndikilo alisema kuwa ni vema wananchi wakajitokeza kwa wingi kujiandikisha ili wapate fursa ya kupiga kura wakati wa uchaguzi huo kwani wasipojiandikisha hawatapata fursa ya kupiga kura siku ya uchaguzi. “Mimi nimetumia haki yangu ya kikatiba ya kujiandikisha na ni namba 123 na kwa mtaa huu wanatarajiwa kujiandikisha ni watu 1,332 wenye umri zaidi ya miaka18,” alisema Ndikilo. Alisema kuwa kuna baadhi ya watu wanapo- tosha kwamba ukiwa na kadi ya mpiga kura au kitambulisho cha utaifa utaruhusiwa kupiga kura hivyo wasijiandikishe jambo hilo si la kweli kwani huo ni upotoshaji kwani usipojian- dikisha hutapiga kura. “Hivyo vitambulisho havitatumika bali watakaoruhusiwa kupiga kura ni wale waliojiandikisha kwenye daftari la mpiga kura kwa eneo unaloishi,” alisema Ndikilo.Aidha alitoa mfano wa Halmashauri ya Chalinze kuwa imeandikisha watu 30,785 kati ya wananchi 121,938 na kazi hiyo ilianza Oktoba 8, mwaka huu inatarajiwa kwisha Oktoba 1, mwaka huu hivyo wananchi watumie muda huo uliobaki kujiandikisha ili wasikose fursa ya kuwachagua viongozi wanaowafaa. Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete alisema kuwa changamoto kubwa ni baadhi wananchi kushinda mashambani baada ya mvua kunyesha. Ridhiwani alisema wataendelea kuwahamasisha wananchi wajitokeze kujiandikisha kabla ya muda kwisha na kusema kuwa kazi hiyo ni la muda mfupi lisije kuwagharimu kwa kipindi cha miaka mitano endapo watachaguliwa viongozi wasio na uwezo.
kitaifa
ASKOFU Mkuu Mstaafu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amewataka waumini wa kanisa hilo kutambua kuwa hakuna dhiki wala mateso yanayoweza kuwatenga na upendo wa Mungu aliyouonesha kupitia msalaba. Amesema katika utamaduni wa Wayahudi, kifo cha kutundikwa msalabani kilikuwa cha aibu na udhalilishaji mkubwa hivyo Wakristo wa leo wanapotakiwa kujiimarisha kiimani ili jambo lolote kati ya hayo (mateso, udhalilishaji na dhiki) visiwatenge na Mungu.Kardinali Pengo aliyasema hayo jana wakati akihubiri katika Misa Takatifu ya Kutukuka Msalaba kijimbo iliyofanyika eneo la hija la Pugu, Jimbo Kuu la Dar es Salaam. Misa hiyo ilikuwa na nia kuu mbili; kubariki jengo jipya la ibada na kumuombea Askofu Mkuu mpya wa jimbo hilo, Yuda Thadeus Ruwai’chi katika utume wake. Hata hivyo Askofu Mkuu Ruwai’chi aliyetakiwa kuwepo kwenye ibada hiyo, hakuwepo. Askofu Msaidizi wa jimbo hilo kuu, Eusebius Nzigilwa alisema Ruwai’chi ameshindwa kutokana na kupata tatizo la kiafya alipokwenda kumzika mjomba wake mkoani Kilimanjaro, Jumatano iliyopita na madaktari wanaomhudumia wameomba kuangalia afya yake kwa karibu zaidi kabla ya kumruhusu. Katika mahubiri yake, Pengo alisema, “Hakuna dhiki itakayotuweka mbali na injili ya Yesu Kristo....tupo wengi zaidi ya wamisionari waliotuletea injili, tufanye kama wao kusambaza upendo wa Mungu kwa watu”.Pengo alisema kuuawa kwa kutundikwa msalabani kwa Wayahudi kulihesabiwa kuwa ni adhabu ya mtu aliyelaaniwa hivyo Mungu kukubali jambo hilo kwa mwanaye (Yesu Kristo) ni ili kumrejesha mwanadamu kwa upendo kwake na asiangamie kwa sababu ya aibu yoyote itakayomkuta katika maisha yake. “Historia ya mahali hapa (Pugu), tulipenda kuunganisha hili fumbo la msalaba na mwanzo wa sisi kupokea injili ya Kristo kupitia kwa wamisionari wa Benedictine.Wamisionari waliokuja kwetu hawakuwa na hitaji walilotaka kuridhia, hawakuwa wanatafuta dhahabu na fedha, hawakuja kutengeneza watumwa wala kuua tembo wachukue meno, walikuja kwa lengo moja tu, kumuiga Yesu Kristo kutuletea wokovu.“Zaidi walichotafuta (wamisionari), mahangaiko waliyoyapata, na hata kukabili kifo mbali kabisa na nyumbani kwao, jambo ambalo lingeweza kwa mwanadamu kumkatisha tamaa, wanauawa na bado sisi tunaona ni jambo la kuonea fahari juu ya wafuasi wa Kristo waliokuja kwetu........ tunapaswa kuwa wanadamu wenye upendo wa Mungu ndani yetu,”Alisema adhimisho la shereke za Kutukuka kwa Msalaba ni la upendo wa Mungu kwa wanadamu hivyo kwamba tunapaswa kuuona huo upendo wa Mungu na kuueneza kwa binadamu wengine. Ibada hiyo kijimbo hufanyika Septemba 15 kila mwaka lakini mwaka huu imefanyika jana kutokana na maaskofu hao kuwa na tukio la kitaifa Septemba 15 jimboni Tanga. Hata hivyo, Askofu Msaidizi Nzigilwa alisema jana kuwa parokia zitaadhimisha kama ilivyo kalenda ya kanisa kwa tarehe husika.
kitaifa
KILIMANJARO Queens imekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali ya michuano ya Wanawake ya CECAFA inayoendelea kwenye uwanja wa Chamazi Complex Dar es Salaam.Hiyo inatokana na vipigo inavyoendelea kuvitoa katika kundi A, ambapo hadi sasa wameweza kushinda mechi zote mbili na kufunga mabao 13. Kilimanjaro Queens ambao ndiyo mabingwa mara mbili wa michuano hiyo, huu ni msimu wa tatu na kocha wake, Bakari Shime amepania kuhakikisha wanatwaa kwa mara ya tatu taji hilo ili kuweka rekodi ya kipekee kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati.Katika mchezo wa jana Kilimanjaro Queens iliingia kwa kuwashangaza wapinzani wao baada ya kocha Shime kubadilisha asilimia kubwa ya kikosi chake kilichocheza mechi ya kwanza dhidi ya Sudani Kusini na kuibuka na ushindi wa mabao 9-0, mmoja wao akiwemo nahodha Asha Rashid na Fatma Abdallah.Mabao ya Kilimanjaro Queens katika mchezo wa jana dhidi ya Burundi yalifungwa na Donisia Daniel aliyefunga mabao mawili dakika ya 34 na 65, Asha Mwalala dakika ya 72 na Mwanahamisi Omary dakika ya 86.Mbali na Kilimanjaro Queens timu nyingine inayofanya vizuri kwenye mashindano hayo ni timu ya taifa ya Uganda ambayo Jumapili iliibuka na ushindi wa mabao 13-0 dhidi ya Djibout na pengine inaweza kuwa timu inayoweza kutoa changamoto kwa timu yoyote kati ya zinazoshiriki mashindano hayo.Uganda ambayo ipo kundi B, pamoja na mataifa ya Kenya, Ethiopia na Djibout ni miongoni mwa nchi ambazo imewahi kutolewa na Tanzania katika hatua ya nusu fainali mwaka 2016 jijini Kampala.Wakati hali ikiwa hivyo kwa Kilimanjaro Queens, mambo sio mazuri kwa ndugu zao, Zanzibar Queens ambao walikubali kipigo cha mabao 5-0 kutoka kwa Sudan Kusini ikiwa ni muendelezo wa matokeo mabaya kwa timu hiyo kwenye mashindano hayo kwani kwenye mchezo wao uliopita, walipokea kipigo kama hicho kutoka kwa timu ya taifa ya Burundi.
michezo
['Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 26, amekuwa akifanya mazoezi mjini New York licha ya wachezaji wenzake kurejea kambini kwa mazoezi ya kabla ya msimu mpya kuanza. (Sun)', 'Barcelona wako tayari kulipa euro milioni 100 ya kumwezesha mshambuliaji wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 21 kuondoka klabu hiyo kabla mkataba wake kukamilika. (Corriere dello Sport - in Italian)', 'Ofa ya Manchester United ya £31m ya kumnunua kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes, 24, imekataliwa na Sporting Lisbon. (Gazzetta dello Sport, via Express)', 'Ni rasmi sasa Meneja wa Derby County Frank Lampard amerejea Chelsea baada ya mchezaji huyo wa zamani wa blues kutia saini mkataba pauni milioni 4 kwa mwaka. (Mail)', 'Kocha wa zamani wa Newcastle Rafael Benitez amekubali kujiunga klabu ya Uchina ya Dalian Yifang kwa mkataba wa thamani ya euro milioni 12 kwa mwaka baada ya kuondoka St James Park. (Sky Sports)', 'Rams wanajiandaa kufanya mazungumzo na kiungo wa kati wa zamani wa Uholanzi Phillip Cocu wiki hii kabla ya Lampard kuondoka. ', 'Cocu alitupwa nje na kocha wa Fenerbahce mwezi Oktoba. (Telegraph)', 'Kocha wa United, Ole Gunnar Solskjaer amewaambia wakuu wa klabu hiyo kumsajili kiungo wa kati wa Newcastle Muingereza Sean Longstaff, 21, kwa dau la pauni milioni 25 wiki hii. (Star)', 'Arsenal wanashauriana na mshambuliaji wa Algeria, Yacine Brahimi 29 ambaye yuko huru na kujiunga na klabu nyinhine baada ya kuhama Porto. (Sky Sports)', 'Gunners pia wamepewa nafasi ya kusaini mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Nabil Fekir - kwa uero milioni 30. (Mirror)', 'Winga wa Manchester City Mjerumani Leroy Sane ameangaziwa katika uzinduzi wa jezi za msimu wa mwaka 2019-20, licha ya tetesi kuwa Bayern Munich wamekuwa wakimnyatia nyota huyo wa miaka 23. (Express)', 'Crystal Palace wanamtaka mlinzi wa Arsenal Muingereza Carl Jenkinson, 27, kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na mlinzi Aaron Wan-Bissaka, ambaye amejiunga na Manchester United. (Sun)', 'Gunners wanajiandaa kuweka dau la pauni milioni 12 kumnunua mshambuliaji wa Hull City wa miaka 22-year- Muingereza Jarrod Bowen. (Sun)', 'Mshambuliaji wa Uholanzi Hossein Zamani, 16, amevifahamisha villabu vya Manchester United, Manchester City na AC Milan kuwa aAjax. (Mail)', 'Manchester United wameshaafikiana kuhusu matakwa binafsi na mshambuliaji wa Sevilla Wissam Ben Yedder, 28. Mshambuliaji huyo raia wa Ufaransa anatarajiwa kujiunga na mashetani hao Wekundu endapo mshambuliaji wa Ubelgiji Romelo Lukaku atauzwa ama la. (Express) ', 'Liverpool wanaweza kumrudisha kiungo mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 27, baada ya mchezaji huyo kushindwwa kuwa na wakati mzuri kwenye klabu ya . (Le10 Sport, via Mirror)', 'Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amesema hana uhakika kama Neymar, 27, atakuwa na makali yaleyale aliyokuwa nayo kabla atakaporejea klabu ya Barcelona akitokea klabu ya Paris St-Germain. (Ara, via Mirror)', "Manchester United wanaweza kuwapoka Tottenham tonge mdomoni katika usajili wa kiungo wa klabu ya Lyon ya Ufaransa, Tanguy Ndombele. Spurs tayari wameshakubali kumnunua mchezaji huyo lakini hawajamalizana naye kuhusu matakwa yake binafsi mchezaji huyo mwenye miaka 22. (L'Equipe, via Metro)"]
michezo
HASSAN DAUDI NA MITANDAO HAIJALISHI una shida zinazoweza kujaza mfuko mkubwa kiasi gani, linapokuja suala la uhai, acha kabisa. Kama hujui, hiyo si kwa binadamu tu, hakuna kiumbe kisichoujua utamu wa kuendelea kuvuta pumzi. Kuliweka sawa hilo, ni tukio la hivi karibuni mjini Istanbul, Uturuki, ambapo mbwa amejikuta akiingia katika duka la dawa baada ya kuumia akiwa kwenye mihangaiko yake. Wengi wameonekana kuvutiwa na kipande cha video kinachomuonesha mbwa akipata matibabu, lakini iliwashangaza zaidi baada ya kusikia kuwa alikwenda mwenyewe, tofauti na wengine ambao hupelekwa na wamiliki wao. Aliyefichua kuwa aliingia bila usaidizi wa binadamu ni video iliyonaswa na kamera za duka hilo, ambayo inamuonesha mbwa huyo akiwa amesimama mlangoni, kana kwamba alikuwa akiomba msaada. Akisimulia ilivyokuwa siku hiyo, mhudumu wa duka hilo, Banu Cengiz, anasema: “Alikuwa ananitazama. Nilimuuliza, ‘mtoto, kuna tatizo lolote?” Cengiz anasema kwa kuwa yeye ni mpenzi wa wanyama, alimpa bakuli ya maji, akidhani alikuwa akisumbuliwa na kiu, lakini mbwa huyo alimpa mguu wake wa mbele. Hapo ndipo Cengiz alipohisi mbwa huyo ameumia na alipomchunguza alibaini kuwa alikuwa na jeraha lililokuwa likivuja damu. “Nilipompa kitanda, badala ya kwenda kulala, aliendelea kusisimama usawa niliokuwa, hadi pale nilipomaliza kumtibu,” anasema Cengiz. Katika huduma yake, Banu, ambaye duka lake lina chumba maalumu kwa mapumziko ya mbwa wa mitaani, anasema alianza kwa kulisafisha jeraha kwa dawa, kabla ya kumpaka nyingine kwa ajili ya kuzuia wadudu. “Nilipomaliza, alilala chini, ishara fulani hivi kama kushukuru, utadhani alikuwa akiniambia ‘nakuamini’,” anaeleza mwanamama Cengiz. Baada ya matibabu, mbwa jike huyo alipumzika dukani hapo kwa muda, kabla ya kuondoka zake. Akizungumzia umuhimu wa kuwasaidia wanyama, Cengiz anasema: “Huwa nafanya hivyo kwa sababu nao wana hisia. Tunapaswa kuwasaidia wale wenye uhitaji. Watu wanatakiwa kuwafundisha watoto wao juu ya kuwapenda na kuwaheshimu wanyama. Kwa kufanya hivyo, tunaweza kuishi pamoja katika ulimwengu mzuri kabisa.” Aidha, video hiyo imewavutia walio wengi, huku baadhi wakielekeza shukurani na pongezi zao kwa Cengiz, wakisema alikuwa na utu kumsaidia mbwa huyo. Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, mmoja kati ya walioitazama video hiyo, Shivam Kumar, anaandika: “Utu upo kwa sababu ya wewe mama. Shukurani kwa wema wako kwa ulimwengu huu.” Wakati huo huo, huko mitandaoni wapo walioonekana kuwasifia wanyama aina ya mbwa, wakisema wana akili hata kuliko baadhi ya binadamu. Hao ni wale walioandika ‘Mbwa kiboko yao’, ‘Huwa napenda mbwa, wakati mwingine ndiyo navutiwa na binadamu’.
kimataifa
WAKATI takribani asilimia 20 ya pamba ambayo imelimwa msimu uliopita bado haijanunuliwa hadi sasa, serikali imeonya kuingizwa siasa katika zao hilo. Pia serikali imetaka mikoa inayolima zao hilo kujipanga vyema kwa msimu huu kwa kuwa kilimo hicho ni cha biashara. Kauli hiyo ilitolewa juzi na Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe wakati akizungumza na wakuu wa mikoa inayolima zao la pamba nchini. Wakuu hao wamekutana mjini hapa kupokea na kujadili taarifa ya kamati ndogo kuhusu changamoto zinazokabili kilimo cha pamba na kutoa mapendekezo ya utatuzi wake. Kamati hiyo ndogo ya wadau iliundwa Oktoba mwaka jana jijini Mwanza kwa lengo la kuja na mapendekezo ya utatuzi wa changamoto za zao hilo hapa nchini. Akifungua kikao hicho mjiniDodoma, alisema kikao hicho ni muhimu ili kutengeneza mustakabali mzuri wa tasnia ya pamba kwenye mikoa 17 inayolima zao hilo. Bashe alisema msimu ujao wa kilimo cha pamba unapaswa uwe mzuri na usiwe na matatizo. “Pamba na kilimo ni biashara tusipeleke siasa. Msimu huu ulikuwa mgumu. Tumekubaliana serikalini kuwa biashara hii ifanywe kwa uwazi zaidi ili mkulima apate manufaa ya jasho lake,” alisema. Naibu Waziri Bashe alisema Wizara ya Kilimo imetengeneza mkakati wa miaka mitano kuhusu sekta ndogo ya pamba ili kukidhi mahitaji ya soko na upatikanaji wa pembejeo kwa wakulima nchini. Bashe aliongeza kusema tayari wizara imefanya majadiliano na wizara za Viwanda na Biashara na ya Fedha na Mipango juu ya mustakabali wa zao hili msimu ujao. “Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025-2020 imeelekeza ushirika kusimamia sekta ya pamba kwa manufaa ya wakulima nchini, hivyo lazima tutafute suluhu ya changamoto za masoko “ alisisitiza. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mwenyekiti wa kamati ndogo ya wadau wa pamba, Adam Malima alisema ni wakati sasa Wizara ya Kilimo ikaweka mikakati mahususi ya upatikanaji wa bei nzuri ya pamba ya wakulima kupitia mfumo wa ushirika. “Ushirika nchini lazima uwe na takwimu sahihi za wakulima, kiasi cha pembejeo kinachotakiwa na eneo linalolimwa ili kuepusha hasara kwa wakulima kubebeshwa madeni yasiyowahusu,” alisema. Malima amebainisha kuwa suala la utafiti na ugani kwenye zao la pamba ni muhimu lipewe kipaumbele, lakini Wizara ya Kilimo haioneshi jitihada. Alisema Wizara ya Kilimo inatakiwa pia kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo za pamba kwa wakati na zenye ubora kuhakikisha zinawafikia kwa wakati na bei nafuu. Kikao hiki maalumu cha wadau kinahudhuriwa na Wakuu wa Mikoa ya Mara, Simiyu, Morogoro, Kagera, Kigoma,Singida, Mwanza, Geita, Shinyanga, Kilimanjaro na Katavi
kitaifa
NA VERONICA ROMWALD-DAR ES SALAAM WATU 18 wamejeruhiwa katika ajali iliyotokea saa 10:30 alfajiri katika eneo la Madafu barabara ya Pugu. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamdani alisema ajali hiyo ilihusisha  gari  namba T 337  BKN Nissan Civilian iliyokuwa inatoka Gongo la Mboto – Mombasa kwenda Kariakoo kupitia Banana. “Gari hilo liliigonga gari  la mchanga namba T 656 DHL Scania 94   lililokuwa likitokea Banana kwenda Gongo la Mboto,. “Watu 18 walijeruhiwa katika ajali hiyo na kupelekwa katika Hospitali ya Amana wakati wengine walipelekwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).  Hali za  majeruhi watatu   zilikuwa mbaya,” alisema. Ofisa Uhusiano wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha hospitali hiyo   ilipokea majeruhi tisa na mwili mmoja wa marehemu. Mwangomo aliwataja majeruhi waliopokelewa hospitalini hapo kuwa ni  Masiku Werema (45), Mohamed Juma (37), Adam Rashid (25) na Joshua Stephen (32). Wengine ni Said Juma (17), Eliza Chacha (14), Maua Malick (48), Stella Mpahe (35) na Juma Mtally. “Kati ya majeruhi hao, Adam Rashid alipatiwa matibabu na kuruhusiwa kurejea nyumbani baada ya hali yake kutengamaa,” alisema. Mwangomo alisema majeruhi wengine bado wamelazwa  wakiendelea kupatiwa matibabu.
afya
Rais John Magufuli amesema, Tanzania na Afrika Kusini zinaongoza kwa kufanya biashara ndani ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).Amesema jijini Dar es Salaam kuwa, mwaka jana biashara baina ya nchi hizo ilikuwa na thamani ya Dola za Marekani bilioni 1.18 kutoka Dola za Marekani bilioni 1.11 mwaka 2017.Ameyasema hayo baada ya kuzungumza faragha na pia kufanya mazungumzo rasmi na Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa Ikulu, Dar es Salaam.Magufuli amesema, mwaka jana 70% ya mauzo ya bidhaa za Tanzania kwenye nchi za SADC yalifanywa Afrika Kusini na kiasi hicho ni sawa na asilimia 16.7 ya mauzo yote ya bidhaa za Tanzania nje ya nchi.Amesema, Afrika Kusini imepiga hatua kubwa kwa maendeleo ya viwanda, inashika nafasi ya pili kwa ukubwa wa uchumi Afrika na ni nchi pekee kwenye bara hilo iliyo kwenye kundi la nchi tajiri 20 duniani (G20).Amesema, tangu mwaka 1990 Kituo Cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimesajili mitaji 228 kutoka Afrika Kusini yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 803.15.Kwa mujibu wa Rais Magufuli, miradi hiyo imetoa ajira kwa 21,000.“Hii imefanya nchi ya Afrika Kusini kushika nafasi ya 13 kwa kuwekeza nchini na kuwa nafasi ya nne katika nchi zote zilizowekeza nchini ambazo zipo ndani ya Bara la Afrika."amesema.
uchumi
KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amewatoa hofu mashabiki wa timu hiyo juu ya muelekeo wao katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya TP Mazembe ya Congo.Mchezo wa kwanza wa hatua ya robo fainali uliochezwa Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita timu hizo zilitoka suluhu na kuifanya mechi ya marudiano Lubumbashi mwishoni mwa wiki hii kuwa wazi kwa kila mmoja. Kocha Aussems alisema matokeo hayo ni wazi kuwa yaliwachanganya Mazembe wanaosifika kwa ubora Afrika na kwamba anaamini wakiwa makini wataifunga timu hiyo.“Ninaamini tunaweza kuwafunga kwao na kufuzu hatua inayofuata, natarajia utakuwa ni mchezo mzuri,” alisema. Simba inahitaji ushindi wowote au sare kuanzia bao 1-1 ili kujihakikishia nafasi ya kusonga mbele katika hatua inayofuata. Mwekezaji wa timu hiyo Mohamed ‘Mo’ Dewji alisema juzi kuwa kikosi hicho kinatarajiwa kuondoka kesho kwa ndege ya kukodi. Dewji aliwahimiza mashabiki wanaotaka kusafiri na timu hiyo kwa ajili ya mchezo huo wa marudiano kujitokeza kuungana nao.Mchezo huo wa marudiano utamkosa beki wao Pascal Wawa atakayekuwa nje kwa wiki moja kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo uliopita. Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye viwanja vya Gymkhana Wawa alikwenda kwenye mazoezi hayo ila alikuwa pembeni akitizama wenzake. Katika hatua nyingine, kutokana na umuhimu wa mchezo huo wa kimataifa, Bodi ya ligi imeahirisha mchezo wa ligi kati ya Simba dhidi ya Biashara uliokuwa uchezwe jana ili kuipa nafasi kujiandaa dhidi ya Mazembe.
michezo
NA MSHAMU NGOJWIKE, DAR ES SALAAM KOCHA Mkuu wa Azam FC, Stewart Hall raia wa Uingereza, amegundua dosari ndani ya kikosi chake huku akieleza kuwa hajaridhishwa na ubora wa nyota wake kutokana na uwezo walioonyesha katika mechi ya ufunguzi wa michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons. Azam ambao wameanza mkakati wa kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara baada ya kushindwa kuutetea msimu uliopita, juzi waliwakaribisha Prisons kwenye Uwanja wa Azam, Complex na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1. Mabao ya Azam katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kusisimua yalifungwa na mshambuliaji, Kipre Tchetche raia wa Ivory Coast pamoja na kinda, Farid Mussa, huku la kufutia machozi kwa Prisons likiwekwa wavuni na Jeremia Juma. Akizungumza na MTANZANIA mara baada ya mchezo huo, Stewart alisema wachezaji wake walipoteza nafasi nyingi za kufunga na hata safu ya ulinzi haikufanya vizuri jambo lililomfanya asifurahie kabisa mechi hiyo ya ufunguzi wa ligi. “Siwezi kusema kikosi changu kipo vizuri kwani kuna makosa mengi yamejitokeza leo (juzi) ambayo kama tungekuwa tunacheza na timu imara yangetugharimu sana,” alisema. “Kwa jinsi Prisons walivyotusumbua inabidi kuyafanyia kazi haraka makosa yaliyojitokeza kabla ya kucheza na Stand United mechi inayofuata ambayo tutakuwa ugenini kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga,” alisema. Stewart ambaye amerejea Azam baada ya Mcameroon, Joseph Omog, kutimuliwa alisema changamoto waliyoipata kwa Prisons inaonyesha ni jinsi gani ligi itakavyokuwa ngumu msimu huu kwani kila timu imejiandaa kupambana kupata ushindi. Mabingwa hao wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (Kombe la Kagame), watashuka tena dimbani keshokutwa kuvaana na Stand United ambao walianza ligi hiyo kwa kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar nyumbani. Azam wanatarajiwa kuondoka leo kuelekea mkoani Shinyanga kujiandaa na pambano lao dhidi ya wenyeji, Stand United.  
michezo
Ushauri huo ulitolewa na Mwenyekiti wa Baraza la Biashara la Mkoa huo ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo, Daudi Ntibenda katika kikao cha kawaida cha baraza hilo hivi karibuni.“Tunahitaji yale yote tuliyoyajadili hapa yatekelezwe kwa vitendo ili kuvutia zaidi biashara na uwekezaji katika mkoa wetu,” alisema.Mabaraza ya Biashara ya Mikoa yanafanya kazi chini ya Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) na kuundwa na wajumbe kutoka sekta ya umma na binafsi.Ntibenda alisema mkoa wao una fursa nyingi za biashara na kuwa sasa baraza na wajumbe wake ni lazima wajipange kuzitangaza kuvutia wawekezaji.Pia aliwataka maofisa wa Biashara wa wilaya mkoani humo kuwasaidia wenyeviti wa Mabaraza ya Biashara ya wilaya kuhakikisha shughuli za biashara zinashamiri katika wilaya zao.Alifafanua kwamba ili mabaraza ya wilaya yaweze kufanya vyema, halmashauri zinatakiwa kutenga bajeti za uendeshaji mabaraza hayo sababu yapo kisheria.Mkurugenzi wa Mazingira ya Biashara wa TNBC, Arthur Mtafya alisema Baraza la Mkoa linatakiwa kufanya vikao kwa mujibu wa uendeshaji wa baraza kwa nia ya kuchochea shughuli za biashara na uwekezaji.“Vikao hivi vya baraza ni muhimu kwa sababu wajumbe wote hupata fursa ya kujadili kwa pamoja maswala ya biashara na uwekezaji,” alisema.Alisema pia mikutano ya majadiliano na wawekezaji iandaliwe kwa mujibu wa taratibu za mabaraza hayo kukuza biashara mkoani humo.
uchumi
WASHINGTON-MAREAKANI  MAHOJIANO yaliyofanywa Jumapili kati ya Rais Donald Trump wa Marekani na kituo cha ABC News yalikatishwa kwa muda, baada ya msaidizi wake kukohoa kwa bahati mbaya jambo ambalo lilimkera rais huyo. Wakati Rais Trump akizungumzia juu ya taarifa za fedha, Katibu Mkuu wake, Mick Mulvaney, kwa bahati mbaya alikohoa. Rais Trump alionekana kuchukizwa na kitendo hicho na kusimamisha mahojiano hayo. Trump  alisema; “Hebu tufanye basi, anakohoa katikati ya taarifa yangu. Sipendi, unajua, sipendi kabisa.” Tangu alipoanza kampeni mwaka 2016 Trump amejikuta katikati ya moto kwa kutotoa taarifa zake za fedha.  Wakati akizungumzia juu ya utawala wake hata katika siku za hivi karibuni aligoma kuweka hadharani rekodi zake, akisema; “ kuna muda natumaini wanazipata kwa sababu ni taarifa nzuri mno za fedha.” Wakati mafundi mitambo wakiweka sawa ili mahojiano hayo yarejee tena, Trump alimuonya Mulvaney akisema; “Kama utakohoa, tafadhali ondoka. Kama huwezi, huwezi kukohoa sawa.” Trump alilazimika kurudia tena taarifa yake juu ya kutotoa rekodi zake za kodi wakati mahojiano yalipoanza tena. Kitendo  hicho cha kusimamisha mahojiano kiliibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii hasa Twitter. Brit.@Bretana_ aliandika katika mtandao huo akihoji hivi ni kweli huyu jamaa kakasirika kwa sababu ya mtu fulani kukohoa!? Jude @truejbru naye aliandika; kila ninapomuona anaongea nakasirika kwa sababu watu kweli walimpigia kura huyu.
kimataifa
MANCHESTER, England KATIKA miaka ya hivi karibuni, upinzani kati ya makocha Jose Mourinho na Pep Guardiola umeibuka kuwa kivutio kwenye ulimwengu wa soka. Kinachovuta hisia za mashabiki wengi wa kandanda ni pale makocha hao wanapokutana na jinsi ambavyo wamekuwa wakitupiana  maneno makali hata kabla ya timu zao kuingia uwanjani. Kwa mara ya kwanza leo wawili hao watakutana wakiwa Ligi Kuu ya England. Mourinho akiwa na Manchester United, Guardiola atakuwa na mahasimu wao, Manchester City, katika mchezo mkali wa ‘Manchester derby,’ utakaochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford. Kabla ya mchezo wa leo utakaochezwa saa 8:30 mchana, Guardiola na Mourinho wamekutana mara 16. Katika mitanange hiyo, Guardiola ndiye anayeonekana mbabe mbele ya hasimu wake huyo, ambapo ameibuka na ushindi mara nane. Moja kati ya mechi hizo, Guardiola aliibuka na ushindi wa penalti. Mourinho ameshinda mechi tatu, huku zilizobaki tukizishuhudia zikitoka sare. Ukiachana na upinzani mkali wa makocha hao, timu wanazozinoa sasa, yaani Man United na Man City nazo ni hasimu. Rekodi inaonesha kuwa kwa mara ya mwisho timu hizo za jijini Manchester zilikutana Machi 20, mwaka jana. Katika mtanange huo wa kuwania Taji la Ligi Kuu England, vijana wa Old Trafford waliibuka kidedea baada ya kuwabanjua wapinzani wao bao 1-0. Hiyo ilikuwa ni Manchester derby ya 171 katika historia ya Soka la England. Historia inaonesha kuwa katika michezo hiyo, Man United imeibuka na ushindi mara 71, huku wenzao wa Etihad wakishinda mara 49.
michezo
  Na VERONICA ROMWALD – DAR ES SALAAM  WAZIRI Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye, amesema Katiba mpya imewekwa pembeni kwakuwa watawala hawataki madaraka yao yadhibitiwe kupitia sauti huru za wananchi ambazo ni Katiba. Alisema mchakato wa Katiba mpya umeigharimu nchi na kupoteza fedha nyingi za walipa kodi, sawa na mchanga wa dhahabu uliokuwa unasafirishwa nje ya nchi (makinikia). Sumaye ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Kanda ya Pwani, aliyasema hayo Dar es Salaam  juzi kwenye mahafali ya vijana wafuasi wa chama hicho wa vyuo vikuu (Chaso) Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Alisema Katiba inayopendekezwa pamoja na mambo mengine, inayo maoni ya wananchi na ilipitishwa na Bunge lakini inaonekana si jambo la kipaumbele na wala haitashughulikiwa tena kwa sababu itawadhibiti watawala. “Mchakato wa Katiba mpya umeigharimu nchi fedha nyingi za walipa kodi sawa na makinikia lakini imetupwa, leo tunazungumzia makinikia, najua Rais Dk. John Magufuli  amekwishasema yeye haambiwi la kufanya, lakini sisi tutaendelea kumkumbusha yale ambayo tunadhani ni muhimu kwa mustakabali wa taifa letu,” alisema Sumaye na kuongeza: “Si jambo la kupuuzwa, kama ni la kupuuzwa basi awakamate wote waliohusika na uamuzi huo maana ni ubadhilifu unaofanana na ule wa makinikia,” alisema. Aidha, sumaye alisema Chadema  pamoja na washirika wake wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wataendelea kudai Katiba mpya hadi itakapopatikana. Aidha, kiongozi huyo wa Chadema  alieleza kwamba Tanzania ina mfumo bandia wa vyama vingi, huku kukiwa na chama kimoja kilichovaa ngozi ya vyama vingine. “Tuna mfumo wa chama kimoja kilichovaa ngozi ya vyama vingi, mfumo wa vyama vingi vya siasa ni lazima ufuate utawala wa sheria na unaolinda, unaoheshimu na kuitetea Katiba ya nchi ambayo watawala wameapa kuilinda wanapokabidhiwa madaraka.
kitaifa
MKOPO uliotolewa na Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) kuendeleza sekta ya kilimo kupitia zao la kahawa mkoani Kagera, umesaidia kufufua viwanda na kuongeza ajira za wanawake wilayani Karagwe. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Karagwe, Godfrey Mheruka, wilaya yake ina viwanda vitano vya kukoboa kahawa ambavyo kwa sasa vinafanya kazi na kila kiwanda kina wanawake wasiopungua 400. “Tangu mkopo utolewe na Benki ya Kilimo, kasi ya ukusanyaji wa kahawa katika msimu wa mwaka 2018/19 umeweza kuleta manufaa makubwa kwa wananchi wilaya hapa. Zaidi ya wanawake 2,000 wamepata ajira za kufanya kazi za upembuaji kahawa ili kuongeza thamani katika soko la kimataifa,” alisema.Mheruka alisema tangu Benki ya Kilimo itoe mkopo kunusuru zao la kahawa mkoani Kagera, kasi ya ukusanyaji zao hilo imeongezeka na pia mzunguko wa fedha kwa wakulima umekuwa mzuri. Mheruka alisema mfumo mpya wa serikali na TADB, umeleta mafanikio makubwa kwa uzalishaji wa kahawa wilayani humo na kuinua maisha ya wakulima. “Baada ya kahawa kukobolewa kiwandani, wanawake ndiyo wanaochambua punje bora na zile ambazo si nzuri, kila kiwanda kina wanawake wasiopungua 400, hii ndiyo dhana ya Rais John Magufuli anayotaka Tanzania ya viwanda itakayozalisha ajira kwa Watanzania,” alisisitiza.Alisema kurejewa kwa mfumo wa zamani wa kununua kahawa kupitia vyama vya ushirika umechagiza kuwepo kwa ongezeko la kahawa ya kutosha na kupelekwa viwandani na hivyo kudhibiti mianya yote ya utoroshaji zao hilo nje ya nchi. “Kupatikana kwa mkopo wa Benki ya TADB sisi kama serikali ya wilaya kumetuhamasisha na kuweza kudhibiti mianya yote iliyokuwepo kupitia Butura ambao ulikuwa ni mfumo wa kiunyonyaji kwa mkulima,” alisema Mheruka.Kwa upande wao baadhi ya wamiliki wa viwanda vya kukoboa kahawa wilayani humo wamekiri kuongezeka kwa makusanyo ya kahawa ambapo Meneja wa Kiwanda cha Ukoboaji Kahawa cha Kaderes, Ernest Makelele alisema mkopo kutoka benki ya TADB umesaidia kuongeza uzalishaji. Mwenyekiti wa Chama cha Ushirika Wilaya ya Karagwe (KDCU), Anselm Alphonce akizungumzia upande wa makusanyo ya kahawa kutoka kwa wakulima alisema hadi mwishoni mwa Agosti mwaka huu, KDCU ilipokea zaidi ya tani milioni 29 ikilinganishwa na tani laki 9 za msimu wa mwaka 2017/2018.
kitaifa
MWENYEKITI wa Chama cha Tanzania (TLP) , Augustine Mrema amemlilia Rais Dk John Magufuli amnusuru ili asiweze kupotea kwenye ramani ya siasa. Mrema alisema hayo jana akilalamika kwamba Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemhujumu ili atoke kwenye ulingo wa siasa.“Niliposhindwa ubunge, ulinichagua kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Taifa na ninashukuru kwa hilo, maana mimi ni mtu pekee ulinipa cheo nikiwa upinzani bila kulazimishwa kujiunga na CCM,”alisema.Alisema aliamua kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji mwaka jana 2019 kikamilifu, hata baada ya majina ya wagombea wa TLP kukatwa nchi nzima na kubakiwa kijiji kimoja cha nyumbani kwake Kiraracha.Alisema wagombea wake walikatwa katika vijiji vingine vitano na halmashauri 19 nchini. Mrema ambaye alishiriki katika uchaguzi kwenye kijiji cha Kiraracha pekee ambako ndiko anakoishi, alidai aliamua kushiriki uchaguzi huo ili kumsaidia Rais Magufuli.Lakini, alisema hajatendewa haki, kwani katika Kituo cha Karisa, Uomboni alichezewa mchezo mchafu hali iliyosababisha uchaguzi huo kutokuwa wa huru na haki.“Namuomba Rais aingilie kati, kwa kuwachukulia hatua wote waliohusika na vitendo hivi vya hujuma dhidi yangu, ili kukomesha hali hiyo isijirudie tena mahali popote,”alisema.
kitaifa
MJUMBE wa zamani wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), John Nchimbi amesema wanaoitabiria CCM kufa, wanakosea kwa kuwa ina misingi imara na haiwezi kutetereka.Mzee Nchimbi ambaye amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kwa vipindi viwili kupitia kundi la majeshi na baadaye katibu wa CCM wa mkoa, alikoma kushiriki masuala ya kisiasa mfumo wa vyama vingi ulipoanzishwa.Amesema kwenye mahojiano maalumu, kuwa, wanaotabiria CCM kufa watasubiri sana, kwani chama hicho kipo imara kutokana na mfumo uliowekwa tangu enzi za Mwalimu Julius Nyerere.Nchimbi, ambaye ni baba mzazi wa Balozi wa Tanzania nchini Brazil, Emmanuel Nchimbi amesema, wimbo wa CCM kufa au kupoteza mwelekeo umekuwa ukiimbwa miaka mingi na hakuna jipya.Mzee Nchimbi, ni askari mstaafu wa Jeshi la Polisi na hadi wakati anastaafu alikuwa Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara.“Chama chochote chenye wanachama hata Tadea ambacho kina wanachama 15 hakiwezi kufa kwa sababu tayari kina wanachama wake ambao hawatapenda kuona kinakufa,” amesema.Hata hivyo, Mzee Nchimbi aliwakumbusha viongozi wa chama hicho kutumia vikao halali kuwasilisha hoja zao badala ya kuongea nje ya vikao halali vya chama kwani kitendo hicho kinaleta tafsiri mbaya kuwa ndani ya chama kuna mgogoro.“Kumekuwa na baadhi ya viongozi ukiwasikiliza wana hoja nzuri sana, lakini sasa badala ya kuzungumzia barabarani waziwasilishe kwenye vikao halali vya chama ili utekelezaji ufanyike.“Na kama mtu anaona kuna kasoro sehemu basi akosoe kwenye vikao halali hii itaondoa minong’ono kuwa ndani ya chama kuna mgogoro,”alisema.
kitaifa
MAHAKAMA ya Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi imemhukumu aliyekuwa Meneja wa Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (Tarura) Manispaa ya Songea mkoani Ruvuma, Godfrey Majuto ambaye ni marehemu sasa, kulipa faini ya Sh milioni 3.6 au kutumikia kifungo cha miaka mitano jela.Hiyo ni baada ya kupatikana na hatia ya makosa matatu ya kupanga ya uhujumu uchumi, baada ya Majuto na wengine wanne kushtakiwa kwa kosa la kuisababishia Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda hasara ya Sh 61,157,342. Aidha, mahakama hiyo imeamuru yeyote atakayeteuliwa kuwa msimamizi wa mirath ya marehemu Majuto atalipa faini ya Sh milioni 3.6 ili fedha hiyo iingine serikalini.Washtakiwa wengine Peter Mwanoni ambaye ni mtumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Chiyando Matoke aliyekuwa mkandarasi wa ujenzi wa barabara, kila mmoja kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh 600,000. Hata hivyo, washtakiwa hao wawili wamenusurika kutumikia kifungo cha mwaka mmoja jela kila mmoja baada ya kila mmoja kulipa faini ya Sh 600,000.Aidha, washtakiwa wawili akiwemo aliyekuwa kwa wakati huo Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Naomi Nko na Beatus Bisesa ambaye ni mwajiriwa wa halmashauri hiyo, hawakutiwa hatiani kwa kosa lolote hatimaye, hivyo waliachiwa huru. Hukumu hiyo iliyosomwa jana na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gasper Luoga, inaelezwa kuwa ya aina yake ambayo iliwasisimua wakazi wengi mkoani Katavi na kuwaacha baadhi vivywa wazi kwa mshangao wakidai hawajawahi kusikia wala kushuhudia mshtakiwa ambaye ni mfu akihukumiwa kifungo jela au kulipa faini.Hakimu Luoga alieleza kuwa mahakama ilipokea hati ya kifo cha Majuto ambaye ni mshtakiwa wa kwanza, ikionesha kuwa alifariki dunia Desemba 4, mwaka huu, akiwa tayari ametoa utetezi wake mahakamani hapo.Ilidaiwa mahakamani hapo Majuto alikuwa akifanya kazi zake kama Meneja wa Tarura katika Manispaa ya Songea alikokuwa amehamishiwa akitokea iliyokuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda. Hakimu Luoga alisisitiza kuwa kabla ya kufikwa na umauti, Majuto alishatoa utetezi wake mahakamani hapo, “hivyo hakuna tena sababu ya kuifanya mahakama hii ishindwe kumwadhibu mshtakiwa ambaye ni marehemu.” Awali, Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Bahati Haule alidai mahakamani hapo kuwa washtakiwa hao walitenda makosa matatu ya kuhujumu uchumi katika nyakati tofauti mwaka 2012.
kitaifa
NA MWANDISHI WETU KAMPUNI ya Statoil Tanzania imetangaza majina ya vijana watano walioingia fainali za shindano la biashara la mashujaa wa kesho lenye lengo la kuhamasisha ujasiriamali kwa mikoa ya Kusini mwa Tanzania yaani Mtwara na Lindi. Meneja wa shindano hilo, Erick Mchome, amewataja washindi hao kuwa ni Razaki Kaondo, Edward Timamu na Sifael Nkiliye (walioshiriki timu moja), Saleh Kisunga, Azizi Doa na Yunus Mtopa. Shindano la Mashujaa wa Kesho lilihusisha vijana wenye umri kati ya miaka 18 na 25 kutoka mikoa ya Mtwara na Lindi kuwasilisha mawazo yao ya biashara ambayo baadaye yalibadilishwa na kuwekwa kwenye andiko la biashara. Mwaka huu shindano hili lilivutia vijana zaidi ya 400 waliowasilisha mawazo ya biashara zao zinazolenga sekta mbalimbali za uchumi kama kilimo, ufugaji, mawasiliano na biashara nyingine ndogondogo. Vijana waliruhusiwa kushiriki mmoja mmoja au hata kuunda vikundi vya watu wawili mpaka watatu. Mshindi wa shindano hili atatangazwa Ijumaa 15 Aprili jijini Dar es Salaam katika hafla maalumu iliyoandaliwa na Statoil ili kumpongeza mshindi huyo na wenzake wanne waliofanikiwa kuingia fainali. Mshindi huyo atajinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 5,000 wakati washindi wanne waliobakia watapata dola 1,500 kila mmoja. Washindi wengine watano waliofanikiwa kuingia kumi bora watapata dola 1,000.
burudani
RAMADHAN HASSAN MBUNGE wa Viti Maalumu, Zainab Katimba (CCM) amependekeza mbakaji apewe adhabu ya kuhasiwa ili asije akarudia tena kosa kama hilo ambalo linaleta ukatili mkubwa kwa wanawake na watoto kutokana na kuwaathiri. Lakini Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Profesa Adelardus Kilangi, amesema kuruhusu adhabu ya kuhasiwa kwa watuhumiwa wa makosa ya ubakaji na ulawiti ni kuvunja katiba ya nchi na kwamba adhabu zilizopo zinajitosheleza. Alisema ibara ya 13 ibara ndogo ya 6 ya katiba inasema ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu zinazomdhalilisha hivyo pendekezo hilo likichukuliwa ni kuvunjwa kwa katiba. Kauli hiyo aliitoa bungeni jana wakati akijibu swali la nyongeza la Katimba (CCM), ambaye alisema kuna changamoto kubwa sana ya ukatili wa wanawake na watoto kwenye masuala ya ubakaji wakati Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inataka kuwahakikishia usalama Watanzania wote. Katimba alisema kwenye makosa ya ubakaji kama ilivyoainishwa kwenye kifungu cha tano cha Sheria ya Sexual offences ya mwaka 1998 ambayo imeenda kufanya marekebisho ya kifungu cha 130 cha sheria ya adhabu ya ubakaji. ”Kigezo au masharti ya kuthibitisha kosa la ubakaji ni mpaka yule aliyebakwa athibitishe kwamba kulikuwa na kuingiliwa, na mazingira hayo ni magumu sana katika utaratibu wa kawaida kuthibitisha kwamba mtu amekuingilia, hasa kwa watoto. “Je, Serikali haioni katika mazingira haya kwamba kufanyike marekebisho ya sheria ili vigezo vya kuthibitsiha au kuthibitisha kosa la ubakaji ipunguzwe kiwango chake ili kusiwe na haja ya kufanya hivyo sababu watoto sio rahisi kwao kuweza kuthibitisha jambo kama hilo na mazingira yaangaliwe ili kuweza kutoa haki? “Serikali haioni kwamba kuna haja ya kuongeza adhabu kwa wale watakaothibitika kwamba wamefanya kosa la ubakaji ili adhabu yao iwe kali ili kuhakikisha kwamba makosa haya ya ubakaji yanakwisha ili watu waogope?” aliuliza Katimba. Alitolea mfano kuwa Serikali haioni kwenye kosa la ubakaji, mbakaji apewe adhabu ya kuhasiwa ili asije akarudia tena kosa kama hilo ambalo linaleta ukatili mkubwa kwa wanawake na watoto kutokana na kuwaathiri. Akijibu maswali hayo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk. Augustine Mahiga alisema kuwa wameondoa baadhi ya vigezo vilivyokuwepo hasa watoto kutoa ushahidi wenyewe na kuachia mahakama uamuzi wa busara na wa kitaalamu kuweza kutoa ushuhuda huo kama kitendo hicho kimetokea. Alisema kuwa kwa sasa kuna mfumo wa kutazama na kuboresha mfumo mzima wa kesi za jinai likiwamo suala la ubakaji na kama itatoa mapendekezo yatafuatana na adhabu. ”Lakini niwaambie kweli kwamba kwenye makosa haya adhabu ambazo zipo mpaka sasa ni kali na inafika mpaka miaka 30 na limejadiliwa bungeni, hivyo kama itabidi kuongeza adhabu hizo baada ya marekebisho na mapitio ya sheria hizi ninashauri kwamba Bunge hili likae na tushauriane kwakuwa linahitaji uamuzi wa kisheria,” alisema Dk. Mahiga. Akitoa majibu ya nyongeza, Profesa Kilangi alisema sheria inayohusu mambo ya jinai ilipopitishwa mojawapo ya masuala iliyoyaondoa kwenye sheria ya ushahidi ilikuwa ni kifungu kinachoeleza ni lazima kuonyesha ishara fulani zilizosalia baada ya tendo la ubakaji jambo ambalo lilikuwa linadhalilisha. Alisema mwisho ni lazima hayo yote yafuate misingi ya sheria za jinai, kwamba lazima kuomba kuthibitisha pasipo kuacha shaka na kwamba anayetuhumiwa asituhumiwe au kupewa adhabu isivyo sahihi. ”Na kwenye hili suala la kuongeza adhabu tayari sheria ile imeiongeza adhabu imekuwa kali sana ambayo ni miaka 30, sasa hili pendekezo la kuhasiwa lina tatizo moja, litatupelekea kuvunja katiba. “Kwa sababu ibara ya 13 ibara ndogo ya 6 inaeleza kwamba ni marufuku kwa mtu kuteswa kuadhibiwa kwa kinyama au kupewa adhabu zinazomdhalilisha, kwahiyo tukichukua pendekezo la kuhasiwa linatupeleka tena kwenye upande mwingine ambapo tutavunja katiba kwakuwa adhabu zilizopo zinajitosheleza,” alisema Profesa Kilangi. Naye, Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu alisema hata ziwepo sheria kali kiasi gani, matatizo ya ubakaji nchini hayataisha kutokana na kuwa ni suala la malezi. Aliwataka wazazi, walezi na jamii kutimiza wajibu wa malezi na ulinzi wa watoto huku akitolea mfano kuwa kuna watoto wanabakwa miezi mitatu bila mzazi kujua, hivyo kuwataka wawakague, wawaulize na kuwafuatilia ili waeleze matatizo wanayopata. Awali katika swali la msingi, Katimba alihoji kuwa Serikali haioni ni wakati mwafaka wa kuleta bungeni marekebisho ya sheria ili kupunguza kiwango cha ushahidi kwenye kesi za ubakaji na hasa wa watoto. Akijibu swali hilo, Dk. Mahiga alisema suala la ushahidi katika kesi za jinai husimamiwa na Sheria ya Ushahidi, Sura ya 6. “Makosa ya ubakaji hususan kwa watoto wenye umri chini ya miaka 18 yaadhibiwa kwa mujibu wa kifungu cha 130(1) na 131(2)(e) cha kanuni ya adhabu, sura ya 20,” alisema Dk. Mahiga. Alisema kuwa makosa haya kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi yanahitaji kuthibitishwa pasipo kuacha shaka yoyote ili mtuhumiwa atiwe hatiani. Dk. Mahiga alisema kwa kuwa kiwango cha kuthibitisha mashauri ya jinai ni pasipo kuacha shaka yoyote, kiwango cha ushahidi kitategemea mazingira ya kosa husika, namna lilivyotendeka na mashahidi walioshuhudia kutokea kwa tukio hilo. Sheria haijatoa masharti ya idadi ya mashahidi wanaotakiwa kutoa ushahidi. “Hivyo, kila kesi uangaliwa kwa kuzingatia mazingira yake na kwamba pamoja na hayo, na kwa lengo la kumlinda mtoto aliyeathirika na tukio la ubakaji, mwaka 2016 Bunge lako tukufu lilifanya marekebisho katika kifungu cha 127 cha Sheria ya Ushahidi, kwa kuondoa masharti ya kumhoji mtoto ili kupima ufahamu wake na badala yake kuweka masharti ya mahakama kujiridhisha kuwa mtoto ana uwezo wa kusema ukweli pekee. ”Hivi sasa Serikali inaendelea na itaendelea kufanya maboresho ya mfumo wa haki jinai ili kuondoa vikwazo vyote vinavyokwamisha usikilizwaji, si tu wa mashauri ya namna hii, bali mashauri yote yanayohusu makundi ya watu katika jamii yetu ili kulinda utu wao, ikiwemo watoto, wanawake, wazee na watu wenye ulemavu wanaoathirika na vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na ubakaji,” alisema Dk. Mahiga.
kitaifa
*Asema kulakamika watambue haki huja baada ya kazi Na DERICK MILTON-SIMIYU RAIS Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, amewataka Watanzania, wakiwamo wanasiasa, kuacha kulalamika kwa kukosekana kwa haki, huku akiwataka kujiuliza iwapo wametimiza wajibu wao. Amesema amekuwa akichukizwa na baadhi ya wanasiasa hapa nchini, ambao kila siku wamekuwa wakilalamika kutaka haki, hali ya kuwa wao hawatimizi wajibu. Rais huyo mstaafu ametoa kauli hiyo huku kukiwa na malalamiko kutoka kwa baadhi ya viongozi wa upinzani kudai haki ya demokrasia na kupinga kuzuiwa kufanya shughuli zao za kisiasa kupitia mikutano. Hatua hiyo imekuwa ikizua malalamiko ikiwemo kuwaomba marais wastafu kujitokeza na kumshauri Rais Dk. John Magufuli kutokana na maamuzi yake mbalimbali aliyoyachukua kwa nchi. Kutokana na hali hiyo, Mkapa amewataka wasomi na wafanyakazi kuendesha midahalo na makongamano ya kuhakikisha nchi inajitegemea badala ya kulalamika kila siku. Kauli hiyo aliitoa jana wilayani Itilima, mkoani Simiyu, alipokuwa akikabidhi Jengo la Upasuaji (Theater) katika Kituo cha Afya Nkoma, lililojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation kwa gharama ya Sh milioni 270. Rais huyo mstaafu alisema wanasiasa hao, licha ya kulalamika, lakini hawatimiza wajibu wa kuhakikisha wanafanya kazi ili kuletea nchi maendeleo. Katika kile kinachoonekana kuchukizwa na hali hiyo, Mkapa alisema kila Mtanzania ana wajibu wa kuhakikisha taifa linajitegemea na kuwaletea wananchi wake maendeleo. “Kila siku utasikia watu wanadai haki, makongamano, midahalo ya kudai haki, swali la kuwauliza wao je, wametimiza wajibu kama Watanzania… maana hakuna haki bila wajibu, ni lazima kubadilika na kuendesha makongamano ya kuonyesha nchi itajitegemea vipi,” alisema Mkapa. Rais huyo Mstaafu alisema ili kuweza kujitegemea, ni lazima kila Mtanzania atimize wajibu wa kufanya kazi kama Rais Dk. John Magufuli anavyosema, huku akitoa mfano katika nchi ya Japan ambapo wananchi wake jambo la kwanza ni kufanya kazi. “Kama tunatarajia mataifa kuja kutuinua wakati sisi tumekaa ni dhana potofu, viongozi tubuni miradi ili tujiendeleze na kujiletea maendeleo sisi wenyewe, kama nchi ya Japan wanavyofanya,” alisema Mkapa. Aliongeza kuwa, toka utawala wa Baba wa Taifa na sera ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), tangu enzi ilikuwa ni ujamaa na kujitegemea, jambo ambalo ameeleza lazima litekelezwe kwa kila mmoja katika kutimiza wajibu kwa nafasi yake. Akizungumzia jengo hilo, Mkapa aliishukuru Japan, ambao walitoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo kupitia Taasisi ya Mkapa Foundation, lengo likiwa ni kupunguza vifo vya akina mama wajawazito na watoto wachanga. “Nchi yetu bado tunakabiliwa na changamoto ya vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto wachanga, nchi ya Japan wametoa msaada huo kwa ajili ya kukabiliana na changamoto hii. “… taasisi ya Mkapa itaendeleza ushirikiano na Serikali katika kutatua changamoto mbalimbali za afya,” alisema. Baada ya kukabidhi jengo hilo la upasuaji, Rais Mkapa na msafara wake walielekea wilayani Chato, mkoani Simiyu, ambapo leo anatarajiwa kukabidhi nyumba 50 za watumishi wa sekta ya afya zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa wilayani humo. Taarifa kwa umma iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Wilaya ya Chato, Richard Bagolele, ilieleza makabidhiano hayo yatafanyika leo wilayani Chato, mkoani Geita, kwa niaba ya mikoa ya Kagera na Simiyu. Alisema hafla ya makabidhiano hayo itahudhuriwa na Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ambaye yupo wilayani Chato kwa mapumziko mafupi. “Makabidhiano hayo yatafanyika katika uwanja wa mpira wa miguu wa Chato mjini, ambapo katika wilaya yetu Taasisi ya Mkapa imefadhili ujenzi wa nyumba tano za familia kumi katika zahanati na vituo vya afya. “Tukio la makabidhiano haya litarushwa mubashara kupitia vituo mbalimbaaali vya runinga na redio vya hapa nchini, wananchi wote mnakaribishwa kushuhudia tukio hili,” alisema Bagolele. Alisema tukio hilo linatarajiwa pia kuhudhuriwa na Balozi wa Japan hapa nchini, Masaharu Yoshinda, ambaye ataungana na Rais Mkapa kukabidhi mtambo wa kukamua mafuta ya alizeti (Double Refine), uliojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Japan. Rais huyo Mstaafu jana aliwasili Chato akiwa na mkewe, mama Anna Mkapa na kulakiwa na mwenyeji wake, Rais Dk. John Magufuli na mkewe, mama Janeth Magufuli.
kitaifa
Hayo yalisemwa mjini hapa jana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Stella Manyanya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kongamano la uwekezaji la Ukanda wa Ziwa Tanganyika, litakalofanyika mjini Sumbawanga kuanzia Oktoba 26 hadi Novemba Mosi mwaka huu.Alisema baada ya makongamano ya uwekezaji kwenye Ukanda wa Ziwa Tanganyika yaliyofanyika miaka iliyopita wawekezaji kadhaa wameonesha nia ya kuwekeza katika ukanda huo wa mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma.Alisema baadhi yao wametembelea mkoa na halmashauri kwa lengo la kupata taarifa zaidi na kuona maeneo husika.Alisema orodha ya wawekezaji waliopo Mkoa wa Rukwa pekee na kila halmashauri zake ni 56 na kati ya hao walioanza kuwekeza ni 39 na wapatao 17 wanaendelea na taratibu za uwekezaji katika hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za umilikaji wa ardhi.Alisema kutokana na mazingira ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika kuna fursa kubwa za kufanya biashara za kimataifa kati ya Tanzania na nchi za Kongo, Burundi na Zambia.Alisema mikoa ya Ukanda wa Ziwa Tanganyika ina fursa nyingi za uwekezaji ambazo bado hazijawekezwa ipasavyo ikiwemo sekta za viwanda, madini, kilimo, mifugo, uvuvi, maliasili, afya, elimu, utamaduni, michezo, usafiri na usafirishaji kwa njia ya barabara, anga na majini, katika Ziwa Tanganyika.Pia vivutio vya kihistoria vinavyohitajika kuhifadhiwa na kuendelezwa, vivutio vya kitaliii ikiwemo Maporomoko ya Kalambo, samaki wa mapambo, mbuga za Lwafi, Katavi, Gombe na Mahale pamoja na mabwawa ya asili ya Kwela, Sundu na Chimchemi ya Majimoto.
uchumi
 MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM  KLABU ya Simba kwa kushirikiana na Taasisi ya Mo Dewji, wamekabidhi msaada wa vizimba vya kuosha mikono, sabuni pamoja na vitakasa mikono (sanitizer) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) ili kusaidia kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.  Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mbatha, wanatambua mchango mkubwa unaofanywa na watumishi wa sekta nzima ya afya na hivyo wameona wachangie sabuni pamoja na vitakasa mikono ili kuweza kukabiliana na virusi vya corona. Kwa upande wao, Mkurugenzi wa MNH Dk. Hedwiga Swai, Mkurugenzi wa MOI, Dk. Samuel Swai na Mkuu wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya ya Moyo wa JKCI, Dk. Tulizo Shemu, wameshukuru kwa msaada huo kwa kuwa utasaidia kupunguza kazi ya usimamizi wa kuosha mikono ambayo mwanzo ilibidi ifanyike na walinzi katika milango mikuu na milango ya kuingia majengo yote ya hospitali. Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Mo Dewji, Barbara Gonzalez, alisema kuwa ujenzi wa vizimba hivyo ambavyo ni zaidi ya 50 ni mwanzo wa zoezi ambalo litaendelea katika hospitali nyingine kama Mloganzila, Mwananyamala, Temeke na Amana. Alisema wanatumia nafasi hiyo kwa kuwashukuru uongozi wa hospitali zote tatu na kila mmoja katika kufanya kazi, kufanikisha zoezi hilo licha ya kuwa na changamoto ya ugonjwa wa Covid-19. Aliongeza kuwa wataendelea kutoa misaada mbalimbali ikiwamo barakoa na vitakasa mikono katika hospitali nyingine za jijini Dar es Salaam.
michezo
Mwandishi Wetu -Dodoma MRADI wa kuendeleza zao la mtama nchini wa kampuni ya Bia ya TBL Plc, unaendelea kunufaisha wakulima wa zao hilo mkoani Dodoma, ambapo wanapatiwa mbegu za kisasa, mbinu za kuendesha kilimo cha kisasa kinachofanikisha kuongezeka kwa mavuno pia wanakuwa na uhakika wa kuuza mavuno yao kwa kampuni hiyo. Akizungumza n kwa niaba ya wakulima wenzake katika mahojiano yaliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni, Issa Dinya,  alisema kutokana na mradi huo wameanza kulima zao la mtama kibiashara kwa kuwa wana uhakika wa soko tofauti na ilivyokuwa hapo awali ambapo walilima zao jilo kwa ajili ya matumizi ya chakula. Kupitia mradi huo wa majaribio unaoendeshwa kwa ushirikiano wa TBL Plc, WFP na FtMAumenufaisha zaidi ya wakulima wadogo 2,000 ambao mavuno yao yaameongezeka kwa asilimia 77 na maisha yao kuwa bora, mkakati wa kampuni ni kuinua wakulima wadogo kupitia kununua mazao yao kwa bei nzuri kwa ajili ya malighafi za kuzalisha biadhaa zake. Mradi huo wa ushirikiano ulianza mwezi Januari Mwaka 2020 ambapo TBL Plc, Ilikubaliana na wakulima kununua zao lao la mtama mkoani Dodoma na Manyara, ambapo taasisi za WFP na FtMA zimewezesha wakulima kupata mbegu za mtama, bima, ushauri wa kilimo cha kitaalamu na uhakika wa masoko. Akizungumzia mafanikio ya mradi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Plc, Philip Redman, alisema anafurahia kuona mafanikio ya mradi huo wa mtama kwa kuwa umeenda sambamba na mkakati wa kampuni hiyo wa kuboresha kilimo cha mtama nchini Tanzania na kuwezesha wakulima wa zao hilo kuendelea kuwa na kipato cha uhakika kuanzia sasa na katika siku za mbele.  “Mkakati wetu wa kununua malighafi ni mkakati wetu mojawapo wa kuchangia jitihada za Serikali za kukuza uchumi wa nchi,” alisema Redman. Akiongea katika moja ya mikutano ya uhamasishaji wa kilimo cha mtama mkoani Dodoma karibuni, Mkurugenzi wa Wilaya ya Kondoa, Mustapha Yusuf, aliipongeza TBL kwa mkakati wake wa kununua malighafi kutoka kwa wakulima nchini. “Mkakati huu kwa kiasi kikubwa umeleta hamasa kwa wakulima kuzalisha zao la mtama kibiashara nchini na utawanufaisha kwa kuboresha maisha yao sambamba na kupata mbegu bora ambazo zinafanikisha kuzalisha mtama wenye kiwango kizuri na mavuno yao kuongezeka,” alisema
uchumi
RAIS Dk John Magufuli amesema katika kipindi cha miaka minne, Serikali imejitahidi kwa kiasi kikubwa, kushughulikia kero zinazoukabili mhimili wa Mahakama, ili kuboresha mfumo wa utoaji haki.Amekerwa na tabia ya wapelelezi kuchelewesha kesi na kusababisha mateso kwa watuhumiwa na familia zao, hivyo kusababisha mlundikano wa mahabusu magerezani na kuikwaza Mahakama.Lakini, pia amekasirishwa na mabaraza ya ardhi, kwa kusababisha migogoro ya ardhi nchini.Amebainisha hayo jana jijini Dar es Salaam kwenye kilele cha maadhimisho ya Siku ya Sheria Tanzania, ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi.Dk Magufuli aliyataja baadhi ya mafanikio ambayo serikali yake imeyafanya kwenye sekta ya sheria na mahakama kuwa ni kuimarisha mfumo wa utoaji haki kwa kupiga vita rushwa, ucheleshaji wa kesi, ucheleshaji wa upelelezi na mlundikano wa mahabusu magerezani.Kuhusu ucheleweshwaji wa kesi, alisema katika kipindi cha mwaka 2019, mahakama iliweza kusikiliza mashauri yote kwa asilimia 100, wakati mwaka 2016 mlundikano wa mashauri mahakamani ulipungua kutoka asilimia 12 hadi kufikia asilimia 5. Katika Mahakama za Mwanzo mlundikano wa mashauri, ulipungua hadi kufikia asilimia 0.Awali, Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, alimweleza Rais kuwa katika kipindi cha kuanzia Januari Mosi hadi Desemba 31,2019, mashauri 272,326 yalifunguliwa katika mahakama zote nchini na kati ya hayo, mashauri 271,214 yalisikilizwa. Jaji Mkuu alisema kuwa asilimia 70 ya mashauri hayo, yalisikilizwa katika Mahakama za Mwanzo.Alisema mashauri yote yaliyofunguliwa kwenye mahakama hizo za mwanzo, yalisikilizwa.“Katika kupunguza tatizo la ucheleweshwaji wa kesi, Serikali ya Awamu ya Tano iliajiri majaji wapya 11 wa Mahakama ya Rufaa, majaji 39 wa Mahakama Kuu na Mahakimu 396. Mahakimu wengine 195 walipewa mamlaka na serikali ya kusikiliza mashauri katika Mahakama Kuu mwaka 2019 ambapo mahakimu 98 waliweza kumaliza jumla ya mashauri 1,132. Nakuomba Waziri wa Katiba na Sheria uniletee majina ya mahakimu hawa,”alieleza Rais Magufuli.Kwa mujibu wa Rais, mafanikio mengine ambayo mahakama imeyapata katika kipindi cha miaka minne ya serikali yake ni kuanzishwa kwa Mahakama ya Rushwa na Uhujumu Uchumi mwaka 2016.Alisema mahakama hiyo iliweza kusajili mashauri 119 na mashauri 89 sawa na asilimia 64, yalimalizika na kuingiza Sh bilioni 13.6 kutokana na faini na Sh bilioni 30.6 kutokana na fidia.Aliyataja mafanikio mengine katika sekta ya sheria na mahakama kuwa ni kuanzishwa kwa mahakama zinazotembea na kuanzishwa kwa mfumo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), ambao umerahisisha usajili wa mashauri na kusikiliza mashauri kwa njia ya video.Kuanzishwa kwa mfumo wa Tehama, pia kumeongeza maduhuri ya serikali kutoka Sh bilioni 1.6 mwaka 2017 hadi Sh bilioni 2.5 mwaka 2019. Jambo jingine ambalo serikali yake imefanikiwa kulifanya ni kusaini hati mbili mwaka 2018, ambazo zilisaidia kuitenganisha Ofisi ya Mwendesha Mashitaka Mkuu wa Serikali (DPP) kujitegemea kutoka kwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), hali iliyopunguza tatizo la watu kubambikiwa kesi.Rais Magufuli alisema kabla ya Ofisi ya DPP kujitegemea, baadhi ya vyombo kama vile Polisi na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru), vilikuwa na mamlaka ya kukamata, kupeleleza na kumfikisha mtuhumiwa mahakamani, ambapo watumishi wasiokuwa waaminifu, walitumia fursa hiyo kuwabambikia watu kesi.Kwamba baada ya DPP kuanza kufanya kazi zake kwa uhuru, aliweza kuwaachia huru watuhumiwa 1,422 katika kipindi cha kuanzia Julai mwaka jana, ambao miongoni mwao wapo waliobambikiwa kesi. Kwamba katika kipindi cha miaka minne, serikali yake imesamehe wafungwa 38,801 huku wafungwa 5,533 aliwasamehe wakati wa sherehe za miaka 58 ya Uhuru, zilizofanyika jijini Mwanza.Magufuli alisema washitakiwa 335 waliokiri makosa yao kwa DPP, walisamehewa. Alisema majadiliano kuhusu kuwarudisha nchini kwao raia wa kigeni 1,415 wa Ethiopia, walioko kwenye magereza nchini, yanaendelea.“Pia tumeshughulikia maslahi ya watumishi na ukarabati wa miundombinu mbalimbali ya mahakama. Katika kipindi cha miaka minne tumejenga Mahakama Kuu mbili moja mkoani Mara na nyingine Kigoma, tumekarabati Mahakama Kuu nne ikiwemo ya Dar es Salaam, Mbeya na Shinyanga, tumejenga mahakama za wilaya 15 na mahakama za mwanzo 11, pia nitatoa shilingi bilioni 10 ili muanze ujenzi wa Mahakama Kuu Dodoma,”alisema Rais Magufuli.Changamoto Mbali na mafanikio hayo, Rais Magufuli alikerwa na tabia ya wapelelezi kuwa chanzo cha ucheleweshaji wa kesi na kuwataka wabadilike kwani jambo hilo linawanyima haki watu na kuwapa shida mahakimu kwa kuwa wanalaumiwa wao kuwa wanachelewesha kesi wakati kosa ni la wapelelezi.Alisema kutokana na hilo kumekuwa na msongamano magerezani ambako kuna jumla ya wafungwa na mahabusu 32,208 takwimu ambayo inathibitisha kuwa kuna tatizo kwa upande wa wapelelezi kwa kuweka mazingira yanayotaka watu watoe hongo ili kesi zao zisikilizwe mahakamani.Sambamba na hilo Magufuli alikerwa na tabia ya mabaraza ya ardhi ambayo yako chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa kusababisha migogoro ya ardhi na dhuluma kwa wananchi hususani wanawake na wajane.Kutokana na hilo, alimweleza Jaji Mkuu kwamba iko haja ya mabaraza hayo kuwa chini ya mhimili wa mahakama, kwa kuwa matendo yao yanaichafua mahakama.“Nilikuwa Wizara ya Ardhi na kuna majina niliyaweka kwenye orodha ya watu waliotakiwa kufukuzwa kazi, lakini nashangaa mpaka leo bado wapo,” alisema Rais Magufuli.Jaji MkuuPamoja na mambo mengine, Jaji Mkuu Profesa Juma alimweleza Rais kuwa kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu inayosema “Uwekezaji na Biashara: Wajibu wa Mahakama na Wadau Kuweka Mazingira Wezeshi ya Uwekezaji,” inawakumbusha wadau wa mahakama, kutokuwa kikwazo na kizuizi katika kufanikisha shughuli za biashara na uwekezaji nchini ili taifa liweze kufikia uchumi wa kati, shindani na wa viwanda ifikapo mwaka 2025.“Nadharia ya sheria na falsafa ya sheria inazungumzia mambo mawili, kwanza ni Falsafa Kuu ambayo inataka sheria ziambatane na maadili kama ilivyo sheria zetu zinavyopinga ushoga, hivyo sheria inatakiwa kusimamia maadili katika biashara na uwekezaji, jambo la pili ni Falsafa Tanzu ambayo inataka sera zinazotungwa zilete furaha na mafanikio kwa watu, mambo haya mawili ndiyo yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano,”alisema Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi.Katika hatua nyingine, Rais Magufuli alifurahishwa na hotuba ya Rais wa Chama cha Mawikili wa Tanyanyika (TLS), Dk Rugemeleza Nshalla na kuahidi kuifanyia kazi hotuba hiyo.
kitaifa
Leah Mushi, Dar es Salaam Kwa baadhi ya Mashirika ya Kimataifa kama Umoja wa Mataifa (UN) na Internews kufanyia kazi nyumbani ni moja ya sera ambayo mfanyakazi anaweza kuitumia wakati wowote. Kufanyia kazi nyumbani haimaanishi usiende kutembea na kufanya shughuli zako, la hasha bali hautakuwa katika jengo la ofisi tu lakini shughuli nyingine ikiwamo kujibu emails na kuhudhuria mikutano kwa njia ya mtandao na shughuli zako zote zinapaswa kuendelea kama kawaida. Kwa wengi hapa nchini kufanyia kazi nyumbani ni jambo jipya na kwa mara ya kwanza kutokana na janga la homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya corona. Wafanyakazi wengi nchi mbalimbali duniani ambao kazi zao zinaruhusu kutokuwepo mahala pa kazi wanajikuta wanapaswa kufanyia kazi nyumbani ikiwa ni namna moja wako ya kujikinga na kusambaza ugonjwa huu ambao hadi sasa hauna tiba wala chanjo. Kwa hapa nchini bado ugonjwa huo haujaenea sana kiasi cha kuhitajika kufanyia kazi nyumbani lakini ni vema kujiandaa kisaikolojia endapo itatokea umuhimu wa kufanya hivyo kama tahadhari. JE, UMEJIANDAAJE? Kupitia makala hii fupi iliyoandikwa na Katie Morell kupitia jarida la American Express unaweza kupata dondoo muhimu za kukuwezesha kufanyia kazi nyumbani kwa ufanisi. Kwa kifupi dondoo hizo ni pamoja na kujiandaa kisaikolojia kuwa utakuwa mpweke kulinganisha na vile ambavyo umekuwa ukishirikiana na kuwasiliana na wenzako kazini. Umuhimu wa kuweka muda maalumu wa kufanya kazi na vile vile kufanya shughuli za nyumbani. Nidhamu ya kupokea simu binafsi na kutazama mitandao ya kijamii. Nguo uvaazo wakati unafanya kazi zinaweza kukupa hisia ya kuwa upo kazini au la. Lakini pamoja na yote hayo ni muhimu kupanga mambo yako vema na uwe na muda wa kupumzika na kuacha kufanya kazi pale muda wa kazi ukiisha funga computer yako mpaka kesho yake na upumzike. Mwandishi wa makala haya Leah Mushi ni Mkufunzi Mwandamizi katika masuala ya Kidijitali.
kitaifa
Kwa mujibu wa upangaji wa ratiba hiyo uliofanyika mjini Cairo, Misri, Makao Makuu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf), Yanga itacheza mchezo wake wa kwanza ikianzia nyumbani kati ya Aprili 7 hadi 9, mwaka huu huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 14 hadi 16, mwaka huu.Yanga ilitinga hatua hiyo baada ya kutolewa na Zanaco ya Zambia katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Zanaco kupata faida ya bao la ugenini kwa kuwa mchezo wa kwanza ulimalizika kwa sare ya bao 1-1 jijini Dar es Salaam kabla ya kutoka suluhu waliporudiana nchini Zambia.Wakati Waarabu hao wapo hatua hiyo baada ya kuiondoa Renaissance du Congo ya DRC katika hatua iliyopita ya Kombe la Shirikisho la Afrika. Endapo Yanga itafanikiwa kuitoa Alger itaingia kwenye hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho la Afrika kama ilivyofanya msimu uliopita.Yanga msimu uliopita ilitolewa na Al Ahly ya Misri na kuangukia katika Kombe la Shirikisho, ambako walipangwa na timu ya Angola na kuishinda, ambako walipata nafasi ya kucheza makundi ya Shirikisho.Ratiba hiyo imechukua timu 16 zilizofuzu raundi ya kwanza ya Kombe la Shirikisho dhidi ya timu 16 zilizoondolewa kutoka Ligi ya Mabingwa Afrika.Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi nyingine zitakazokutana ni TP Mazembe vs JS Kabylie, AC Leopards vs Mbabane Swallows, FUS vs MAS, Rangers vs Zesco United, CF Mounana vs ASEC Mimosas, Rail Club K vs CS Sfaxien na Bidvest Wits vs Smouha, CNAPS vs CRD Libolo.Nyingine ni Kampala CCA vs El Masry, Gambia Ports vs Al Hilal Obeid, ASPL 2000 vs Club Africain, Rivers United vs Rayon Sports, BYC vs SuperSport United, AS Tanda vs Platinum Stars na Horoya AC vs IR Tanger.MC Alger ni nani?Ni timu kongwe iliyoundwa mwaka 1921. Inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Algeria ikiwa na pointi 35 nyuma ya USM Bel Abbes yenye pointi 38 na kinara wao ni Es Setif inayoongoza kwa pointi 47. Pia, ni mabingwa watetezi wa Kombe la Algeria ‘Algerian Cup’.MkwasaAkizungumzia ratiba hiyo Katibu Mkuu wa Yanga ambaye pia ni Kocha wa zamani wa klabu hiyo, Charles Mkwasa alisema itakuwa mechi ngumu, lakini ni muhimu kwao kujipanga kuhakikisha wanapata matokeo mazuri kwenye mchezo wa nyumbani.Mkwasa aliliambia gazeti hili jana kuwa timu hiyo ni nzuri kama ilivyo kwa wao, wana wachezaji wazuri pia na wanawaheshimu.Alisema ni timu ambayo imechukua makombe kadhaa kama ilivyo kwa Yanga, na kwamba kichatakiwa kwao ni kuhakikisha wanajipanga kwa mchezo huo kwa sababu lengo lao ni kuingia hatua ya makundi.“Tumeona ratiba ni ngumu, tunaijua ile timu nzuri ina wachezaji wazuri kama Yanga, kikubwa kwetu tutajitahidi kujipanga na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri tufikie lengo letu la kuingia hatua ya makundi,” alisema.Mkwasa aliweka wazi kuwa kabla ya kufikiria mchezo huo, wanaangalia namna gani watapata matokeo mazuri katika mchezo wao ujao dhidi ya Azam FC utakaochezwa Aprili mosi mwaka huu.
michezo
Mchezo huo wa kirafiki ni sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC iliyopo kambini Unguja.Katika mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine ambapo wenyeji Mbeya City ndio walianza kupata bao la kwanza mnamo dakika ya nane kupitia mchezaji wake Bakari Mwinjuma baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Yanga.Dakika nane baadaye Yanga SC ilisawazisha bao hilo kupitia kwa mchezaji wake, Mbrazil Andrey Coutinho ambaye alimalizia krosi safi kutoka kwa Mzimbabwe, Don ald Ngoma.Yanga iliendelea na harakati zake za kutafuta mabao ambapo mshambuliaji wa kimataifa wa Burundi, Amissi Tambwe dakika ya 45 ikiwa ni muda wa mapumziko aliiongezea timu yake hiyo bao la kutoka krosi safi ya Ngoma.Dakika mbili tu baada ya kuanza kipindi cha pili, Yanga walifanikiwa kupata bao la tatu lililofungwa na Ngoma, aliyemalizia krosi ya Simon Msuva. Mchezaji Meshack Ilemi wa Mbeya City aliiongezea timu yake hiyo bao jingine dakika ya 83 na hivyo kufanya kuwa sare ya 2-2 hapo ikiwa ni bado dakika saba kumalizika kwa mchezo.Mchezaji huyo alifumua shuti kali lililowapita mabeki wa Yanga pamoja na na kisha kumwacha mlinga mlango wa timu hiyo Ally Mustafa ‘Barthez’. Yanga imeendeleza ushindi katika mechi za kujipima nguvu mkoani Mbeya baada ya kuzifunga Kimondo na Prisons katika mechi zilizotangulia.Yanga SC itaendelea na kambi yake ya Tukuyu mjini humo hadi hapo itakaporejea kwa mchezo wao wa Ngao ya Jamii Agosti 22.Wachezaji wa Yanga walikuwa ni kipa Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul, Mwinyi Hajji, Kevin Yondan, Vincent Bossou, /Mbuyu Twite dk46, Thabani Kamusoko, Simon Msuva/Deus Kaseke dk64, Haruna Niyonzima, Amissi Tambwe/Malimi Busungu dk67, Donald Ngoma/Sadi Juma dk70 na Andrew Coutinho/ Godfrey Mwashiuya dk46.Mbeya City; Hanington Kalyesubula, Kabanda John/Haroun Shamte dk.68, Hassan Mwasapili, Rajab Seif/Christian Sembuli dk.49, Juma Nyosso, Steven Mazanda, Hassan Selemani/Richard Peter dk68, Daud Raphael, Themi Felix/Geoffrey Mlawa dk.62, Bakari Slang na Joseph Mahundi/Meshack Ilemi dk.56.
michezo
['Huku akiwa alifunga magoli 17 msimu uliopita , matatu katika mechi moja msimu huu- Raheem Sterling yuko tayari kwa msimu mwengine bora mwaka huu. ', 'Mshambuliaji huyo wa Man City alikuwa na kampeni ya kipekee 2018-19 , akichaguliwa na waandishi kuwa mchezaji bora, mchezaji mwenye umri mdogo wa mwaka pamoja na kushirikishwa katika timu bora ya mwaka baada ya magoli yake kuisaidia timu yake kushinda taji la ligi ya Premia katika msimu wa pili mfululizo ambao pia waliweza kushinda mataji matatu. ', 'Pia amekuwa mchezaji muhimu katika kikosi cha Garry Southgate akitajwa kuwa mchezaji maalum na mkufunzi wake Pep Guardiola na akiwa na umri wa miaka 24 miaka yake bora iko siku zijazo.', "Katika kipindi cha BBC Radio 5 siku ya Jumatatu usiku - swali liliulizwa iwapo Sterling anaweza kuwa na msimu kama ule wa Messi - mshindi mara tano wa taji la Ballon d'Or na mfungaji mabao 30 na zaidi kila msimu ambaye kila mtu anaweza kujivunia.", 'Sterling alifunga magoli 25 katika mashindano yote msimu uliopita - yakiwa ndio mabao mengi aliyowahi kufunga katika msimu mmoja na aliendeleza msururu huo wa magoli kwa kufunga hat-trick katika mechi ambayo City iliibuka mshindi kwa magoli 5 wakicheza dhidi ya West Ham siku ya Jumamosi. ', 'Akiwa na umri wa miaka 24 na siku 245 - Sterling alicheza na kutoa mchango kama ule wa Messi wakati mshambuliaji huyo wa Argentina alipokuwa na umri kama huo.', 'Tofauti iliopo kuhusu kiwango cha usaidizi wa kila mchezaji alichochangia katika wakati huo sio mkubwa - 90 kwa Messi ikilinganishwa na Sterling aliyekuwa na 68 - lakini ni ufungaji wa magoli mengi wa Messi ambao unamfanya kuwa mchezaji wa kipekee. ', 'Huku Sterling akijishasha kwa kufunga magoli 25 msimu uliopita, magoli machache yaliofungwa na Mesi katika misimu yake 11 ni magoli 38.', 'Kwa Sterling kulinganishwa na Messi atalazimika kuongeza kiwango chake cha magoli maradufu.', '"Raheem anaendelea kuimarika\' , alisema aliyekuwa mshambuliaji wa zamani wa Arsenal Ian Wright akizungumza na BBC Radio 5 Live. ', "''Ni hodari sana jinsi anavyocheza na na kutamba na mpira na ufungaji wake ni mziuri zaidi. Ni rahisi kumuona mtu kama Raheem akimaliza na magoli kati ya 35 - 40 msimu huu kutokana na jinsi anavyocheza , fursa zinazotengezwa na Man City na jinsi anavyofunga magoli''.", ' Wakati Manchester City ilipomsaini Sterling kutoka Liverpool 2015 kwa dau la £49m, alikuwa mchezaji ghali zaidi kutoka Uingereza. ', 'Thamani yake ilitokana na shinikizo nyingi kwa mchezaji mwenye umri wa miaka 20 na pengine haishangazi ni kwa nini Sterling hakuweza kuonyesha mchango wake aliotaka kutoa. ', 'Lakini mtu mmoja ambayo hakuwa na wasiwasi naye ni mkufunzi Pep Guradiola. ', "Msimu wa 2016, wakati Sterling alipokuwa na msimu mbaya wa Ulaya ambapo alitolewa baada ya kipindi cha kwanza akiichezea England dhidi ya Wales kufuatia kipindi kibaya cha kwanza, alipokea ujumbe katika simu yake uliosema: ''Usijali najua wewe ni mchezaji mzuri, Utakaponifanyia kazi, nitakupigania''. ", 'Ujumbe huo ulitoka kwa mkufunzi wake mpya wa klabu ambaye alimtambua Sterling kama mchezaji mwenye kipaji cha kuwa mchezaji bora sawa na Messi. ', 'Katika msimu wake wa pili akishirikiana na Guardiola, Sterling alifunga magoli 23 - ikiwa ni mara mbili ya magoli aliyofunga katika misimu yake sita aliyocheza soka ya kulipwa. ', 'Kama Sterling, ufungaji magoli wa Messi kabla ya kucheza chini ya ukufunzi wa Guardiola ulikuwa mzuri lakini sio bora - alifunga magoli 16 katika kipindi cha msimu wa 2007-08. ', 'Lakini msimu uliofuata aliongezaa idadi hiyo na kufikia 38.', 'Kwa Sterling kuweza kujumuishwa na kulinganishwa na Messi idadi yake ya magoli itahitaji kuimarika zaidi.', 'Uimarikaji huo uliambatana na hatua ya Guardiola kumchezesha Messi kama mshambuliaji wa katikati na pia ameweza kumchezesha Sterling katikati katika mechi ya maandalizi ya msimu huu ambapo Sterling alifunga magoli matano. ', "''Kwa mkufunzi kama Pep hatakua na nafasi ya kupumzika'', Wright aliongezea. ", "''Amejitahidi vilivyo na imani yake imeongezeka kwa kwa kile ambacho amekuwa akifanya katika mazoezi. Sasa atakuwa akivunjika moyo kwa kufunga magoli matatu na kushindwa kufunga goli moja zaidi kwa sababu hilo ndio lengo lake sasa'' . Anataka kuongeza idadi ya magoli yake.", 'Huku ukufunzi wa Guardiola ukiwa umesaidia kuimarika kwa Sterling, kitu muhimu ni kuimraika kwa mafikra yake. ', 'Mshambuliaji huyo amekabiliwa na ukosoaji mkubwa katika mchezo wake wa soka kufikia sasa kutoka kwa mashabiki na vyombo vya habari.', 'Lakini amefanikiwa kuwanyamazisha kwa kuendelea kujiimarisha kama mchezaji na kuwakosoa wakosoaji wake. ', 'Kiungo wa kati wa West Ham Jack Wilshere amefanikiwa kucheza na Sterling England lakini alikua mpinzani wa mchezaji huyo siku ya Jumamosi. ', "''Nadhani ni mchezaji mzuri sana na alikuwa mchezaji mzuri sana mwaka uliopita. Inaonyesha tabia yake baada ya kombe la dunia 2014 na kua mmoja wapo wa wachezaji bora katika ligi mwaka huu''."]
michezo
SERIKALI ina mpango wa kuanza kuwasajili na kutoa leseni kwa wataalamu wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (Tehama), lengo likiwa ni kuwatambua na kuhamasisha wataalamu hao kuja na ubunifu mpya. Hayo yamelezwa na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Isack Kamwelwe wakati wa kufunga Kongamano la nne la masuala ya Mtandao Jamii katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Kondoa wilayani Kondoa. Mkutano huo uliandaliwa na Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), kufuatia mradi wa utafiti ambayo ulichangia kuunganzisha Mitandao ya Jamii wilayani Kondoa. Leseni ambazo zitatolewa kwa vipindi na wataalamu hao watalazimika kufanya ubunifu ili kuweza kuendelea kuwa nazo.“Tutasajili wataalamu wote wa IT na kutoa leseni kwa kufanya hivyo kutahamasisha kuwa wabunifu. Watatakiwa kuhuisha leseni zao baada ya kipindi fulani. Katika kipindi cha leseni yao, wanapaswa kuleta kitu kipya katika suala la uvumbuzi vinginevyo leseni hizo zitachukuliwa,”alisema. Kamwelwe alimpongeza mhadhiri wa UDOM na mtafiti, Jabhera Matogoro kwa kuja na mradi wa kufunga mitambo ya mawasiliano kwa kufikisha huduma ya mtandao wa intaneti kupitia mawimbi ya televisheni katika kuboresha upatikanaji wa mtandao vijijini.Kamwelwe alisema serikali itaendelea kusaidia wataalamu wazawa wa IT wakati watatekeleza miradi, inayolenga kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wananchi. Kuhusu mradi huo, Kamwelwe alisema serikali itafanyia kazi changamoto zinazokabili teknolojia mpya. Alibainisha baadhi ya changamoto kuwa ni ukosefu wa sera ya kitaifa kwenye mitandao vijijini na kiwango cha chini cha uelewa wa jamii kuhusu uboreshaji wa mtandao vijijini.“Niwahakikishie kuwa ofisi yangu iko tayari kupokea mapendekezo na ushauri kutoka maeneo tofauti ili kukabiliana na changamoto hizo,”alisema. Kamwelwe alisema takwimu za hivi karibuni, zinaonesha kuwa hadi Juni mwaka 2019, Tanzania ina watumiaji wa simu za kiganjani milioni 43.75 na watumiaji wa simu za mkono 23.14 tu, ndio wanaopata huduma ya intaneti.“Takwimu zinaonesha kuwa kuna tofauti kati ya watumiaji wa simu za kiganjani na wale wanaopata huduma ya intaneti. Hii inamaanisha kwamba wale ambao hawapati huduma ya intaneti hawatashiriki katika uchumi wa dijiti,”alisema. Kamwelwe alielezea kuwa uchumi wa dijiti ni muhimu katika kuboresha huduma za afya mtandao, maktaba mtandao na elimu mtandao.Naye Mhadhiri na mwazilishi wa mradi wa kupeleka huduma ya mtandao kwa kutumia mawimbi ya televisheni, Matogoro, alisema alikuja na wazo la kutumia mawimbi ya televisheni kuboresha upatikanaji wa mtandao kwa wakazi wa Kondoa.
kitaifa
ADDIS ABABA, Ethiopia FAMILIA  zilizopoteza ndugu katika ajali ya ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia,  zimeanza kukabidhiwa shehena ya majivu ili wafanye maziko kama ishara ya kuwaenzi waliofariki dunia.  Kwa mujibu taarifa zilizopatikana mjini hapa, maofisa walianza kutoa vifurushi vya majivu hayo jana yaliyokusanywa kutoka eneo la ajali kwa familia za abiria 157 pamoja na wafanyakazi wa ndege, kufuatia shughuli ya utambuzi wa mabaki ya miili kuchukua muda mrefu. Taarifa hizo zinaeleza kuwa uchunguzi wa vinasaba umeanzishwa kwa lengo la kutambua mabaki ya miili iliyopatikna, lakini wataalam wanasema unaweza kuchukua muda wa miezi sita. Shirika la Habari la Ufaransa  AFP, liliripoti kwamba  familia za waliokufa katika ajali hiyo kutoka mataifa 35 zinapewa  kiasi cha kilo mbili za majivu. Shirika hilo liliripoti kwamba ibada ya kuwaombea waliopoteza maisha ilifanyika jana mjini hapa. Shirika la  Habari la Marekani, AP nalo liliripoti kwamba familia hizo zilipewa mifuko hiyo yenye uzito huo  wa kilo mbili   kwa ajili ya  kufanya mazishi hayo ya wapendwa zao.  “Tumepewa majivu haya baada ya kazi ya utambuzi wa mabaki ya ndugu zetu kushindikana,”alisema mmoja wa wanafamilia hao. “Hatutapumzika hadi tupewe mwili halisi au sehemu za mwili ya wapendwa wetu,”aliongeza mwanafamilia huyo. Ndege hiyo ya Shirika la Ethiopia Airlines aina ya  Boeing 737 Max 8 ilianguka Jumapili iliyopita dakika chache baada ya kuruka kutoka Uwanja wa ndege mjini hapa ikiwa safarini kuelekea Nairobi  Kenya na kuua watu wote waliokuwemo.
kimataifa
Matumizi ya bangi kwa kujiburudisha yatahalalishwa nchini Canada ifikapo tarehe mosi Julai mwaka 2018. Serikali ya Canada itawasilisha muswada wa kuhalalisha bangi ifikapo Aprili kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la CBC. Taarifa ziliiambia CBC kuwa wanachama wa chama tawala cha Liberal hivi majuzi walijulishwa kuhusu muswada huo. CBC imesema kuwa sheria hizo mpya zitaambatana na mapendekezo yaliyotolewa na jopo lililoteuliwa na serikali. Baadhi ya mapendekezo hayo ni kuwa Canada itaruhusu kuuzwa kwa bangi wa kujiburudisha kwa watu walio na zaidi ya umri wa zaidi ya miaka 18. Jopo hilo pia lilipendekeza kuwa watu wazima wataruhusiwa kupanda hadi mimea minne ya bangi na wamiliki hadi gramu 30 ya bangi iliyokaushwa. Kwa mujibu wa CBS, serikali itasimamia kusambazwa wa bangi na kuwapa leseni wazalishaji. Kwa upande mwingine, mwaka jana Desemba wapiga kura katika majimbo ya California na Massachusetts waliidhinisha matumizi ya bangi (marijuana) kwa kura. Kura ya kuidhinisha matumizi ya mmea huo iliyopigwa sambamba na ile ya uchaguzi wa rais, iliidhinisha kisheria uzalishaji na matumizi ya bangi kwa watu wenye umri wa miaka 21. Wapigaji kura katika majimbo mengine waliopigia kura kuidhinisha kwa matumizi ya bangi kwa ajili ya kujifurahisha ni Arizona, Maine, na Nevada, ambako matokeo bado hayajajulikana. California ilisema ushuru juu ya mauzo na kilimo cha bangi utasaidia kuboresha mipango ya vijana, mazingira na utekelezwaji wa sheria. Vilevile, mwaka jana huo huo mwezi Septemba, kundi moja la wabunge nchini Uingereza lilitoa wito wa kuhalalishwa kwa matumizi ya bangi kwa sababu za kimatibabu nchini humo. Kundi hilo linalojumuisha wabunge kutoka vyama mbalimbali vya kisiasa, na ambalo limekuwa likitetea mageuzi kuhusu matumizi ya dawa, lilisema kuna ushahidi bayana kwamba matumizi ya bangi huwa na manufaa katika kutibu baadhi ya matatizo ya kiafya, yakiwemo maumivu makali na kutatizwa na wasiwasi. Kwa mujibu wa wataalamu, mmea wa bangi huwa na karibu kemikali 60. Lakini Taasisi ya Taifa ya Afya Uingereza imetahadharisha kwamba bangi huwa na madhara makubwa kwa mwili, ikiwemo kutatiza uwezo wa mtu kuendesha gari na kudhuru mapafu na afya ya kiakili, kuathiri uwezo wa mtu kuzaa na kuathiri pia watoto ambao hawajazaliwa.
kimataifa
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi wa mkoa wa Pwani ufanye tathmini kuhusu changamoto na mafanikio ya maonesho ya viwanda na uwasilishe taarifa kwa viongozi wa juu wa Serikali.Katika hotuba ya Mama Samia iliyosomwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhandisi Stella Manyanya, ameagiza kuwa, tathimini hiyo pia iainishe matarajio kwa maonesho yajayo.Manyanya amesoma hatuba hiyo mjini Kibaha wakati wa ufunguzi wa maonesho ya pili ya viwanda mkoa wa Pwani yatakayomalizika Oktoba 23.Maonesho ya kwanza ya viwanda mkoa wa Pwani yalifanyika mwaka jana kwenye uwanja wa CCM Mkuza, Kibaha na kushirikisha wenye viwanda 166.“Wakati nikifanya ziara ndani ya mkoa wa Pwani mwaka jana nilipewa taarifa kuwa, mkoa una takribani viwanda 429 vikubwa, vya kati na vidogo. Naamini idadi hii itakuwa imeongezeka kwa sasa. Wingi huu wa viwanda ndani ya mkoa umewezesha kukuza hamasa ya kuwepo kwa uendelevu wa maonyesho haya”amesema mama Samia.Amesema, kutokana na umakini wa uongozi wa mkoa wa Pwani anaamini kuwa maonesho hayo yatafanyika kila mwaka.Ameupongeza uongozi wa mkoa huo na wilaya zake, taasisi za serikali, taasisi binafsi na wadau kwa kushirikiana kuandaa maonesho ya mwaka huu kwenye viwanja vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Kibaha.
uchumi
TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Queens, leo inashuka dimbani kutetea ubingwa wa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) itakapocheza fainali dhidi ya Kenya kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.Kilimanjaro Quees ilifuzu kwa fainali hiyo baada ya kuifunga kwa mbinde Uganda kwa bao 1-0 katika mchezo wa nusu fainali ulipigwa kwenye uwanja huo wakati Kenya wenyewe waliifunga Burundi kwa mabao 5-0 katika mchezo uliopigwa mapema juzi.Mchezo huo wa fainali unatarajia kuwa mgumu kwa timu zote, kwani zina uwezo wa hali ya juu, huku Kilimanjaro Queens ikitaka kutetea ubingwa wake kwa kutwaa taji kwa mara ya tatu mfululizo wakati Kenya ikitaka kulipa kisasi cha kufungwa katika fainali ya mwaka jana.Kocha wa Tanzania Bara, Bakari Shime alisema kuwa timu yake imejiandaa vizuri kwa mchezo huo na ni matarajio yake kuwa watashinda tena na kulitwaa kabisa kombe hilo.Bao hilo pekee la Kilimanjaro Queens lilifungwa na Asha Rashid ‘Mwalala’ katika dakika za lala salama baada ya kuunganisha wavuni mpira uliopigwa kutokea pembeni mwa uwanja na Mwanahaisi Omary ‘Gaucho’.Wakati mabao ya Kenya dhidi ya Burundi iliyochapwa pia 5-0 na Tanzania Bara katika mechi ya Kundi A yalifungwa na Dorcus Nixon dakika ya 14, Jentrix Shikangwa dakika ya 53 na 71, Mwanalima Jereko dakika ya 67 na Carazone Aquino dakika ya 87.Leo kuanzia saa 8:00 mchana, Burundi itaanza kumenyana na Uganda katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu kabla ya fainali itakayoanza saa 10:00 jioni.
michezo
Arodia Peter, Dodoma Hospitali  ya Benjamini Mkapa iliyopo jijini Dodoma,  imefanikiwa  kupandikiza figo kwa wagonjwa nane kwa kipindi cha miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. Hayo yalisemwa na daktari bingwa wa figo hospitalini hapo Dk. Kessy Shija, jana Mei 4,  alipokuwa akiongea na waandishi wa habari waliokuwa kwenye ziara ya kutembelea miradi  inayofadhiliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) mkoani humo. Dk. Shija alisema kuanzishwa kwa huduma hiyo ya kibingwa hospitalini hapo kumepunguza gharama kwa wagonjwa kwenda kupata matibabu hayo nje ya nchi, hususani India. “Niwashauri Watanzania kujiunga na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, kwa sababu  magonjwa ya kudumu kama figo yanachukua wastani wa Sh, 200,000 hadi 250,000 kwa wiki ambazo ni gharama za kusafishwa, ambapo  kwa matibabu ya kupandikizwa figo huchukua wastani wa hadi Sh, 6, 000, 000 kwa mgonjwa mmoja,” alisema. Aidha Dk. Shija alisema mbali na figo, hospitali hiyo pia inatoa matibabu ya kibingwa kwa wagonjwa wa moyo kama ilivyo kwa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) iliyopo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
afya
Habari za Ukimwi na Virusi vya Ukimwi (VVU), kodi na manunuzi ya umma, habari za uchambuzi na matukio na kundi la Afya ya Uzazi kwa Vijana, zimeondolewa katika makundi yatakayowania Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari(EJAT) kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo rasilimali fedha. Tuzo hizo zimezinduliwa rasmi leo ambapo makundi makundi matano kati ya 19, yamepunguzwa kutokana na sababu hizo. Mwenyekiti wa maandalizi ya tuzo hizo zinazosimamiwa na Baraza la Habari nchini (MCT), Kajubi Mukajanga amesema mwaka huu kutakuwa na ushindani wa umahiri wa habari katika makundi 14 kati ya 19 yaliyokuwa yakishindaniwa mwaka jana. Amevitaja vipengele vilivyobaki katika tuzo hizo ni habari za afya, habari za michezo na utamaduni, habari za uchumi, biashara na fedha, na uandishi wa habari za biashara, kilimo, elimu, utalii na uhifadhi, uchunguzi, data, haki za binadamu na utawala bora, mpiga picha bora wa magazeti na runinga, mchoraji katuni bora, habari za jinsia, wazee na watoto na kundi la wazi. “Kazi zitakazoshindanishwa ni zile zilizochapishwa na kutangazwa kati ya Januari Mosi hadi Desemba 31 mwaka huu, na mwisho wa kuwasilisha kazi zao ni Februari 16, mwakani na tuzo hizi zitatolewa Aprili 27, mwakani,” amesema.  
kitaifa
BAADA ya miezi 12 ya kukaa katika Hospitali ya Kisarawe na Muhimbili na kushindwa kuendelea na matibabu, Rashid Mtepo (30) amewaomba wasamaria kumsaidia fedha za kulipa deni Muhimbili ili arejee kwa matibabu.Mtepo mkazi wa Mpingoni, Nanguruku wilayani Kilwa amesema tatizo la mguu wake lilianzia mwaka 2015 ambapo alipatiwa tiba ya takribani mwezi mmoja katika Hospitali ya Kisarawe kabla ya kuhamishiwa Hospitali ya Muhimbili ambapo alikaa miezi 11 na kufanyiwa upasuaji wa kubadili ngozi ili kuziba eneo la kidonda. Tatizo lake lilianza kama jipu kabla halijasambaa katika mguu wake wa kushoto, kubabuka ngozi na kuzalisha kidonda kikubwa.Upasuaji ulifanyika Hospitali ya Muhimbili mwaka 2016 kama sehemu ya tiba, lakini baada ya kukaa miezi 11 ya matibabu alilazimika kuondoka hospitalini hapo kutokana na deni kubwa alilokuwa amelipata. Mpaka anaondoka deni lake lililikuwa Sh 961,042. Kutokana na hali yake kuwa mbaya alirejea nyumbani kwao Likawage wilayani Kilwa ambapo mpaka leo analazimika kutumia vidonge vya kupunguza maumivu vya diclopar mbili huku kidonda chake akikifunga na kitambaa cha kawaida ambacho hukifua kila mara.“Ni muda mrefu nashindwa kumudu kwenda hata kufunga kidonda kutokana na hali duni niliyonayo na kushindwa kutembea nalazimika kufunga tambala na kulifua kufunga tena” alisema.Hali yake ya sasa na umaskini wa familia yake unafanya ashindwe kupata msaada wa kurudi tena Muhimbili kukamilisha matibabu. Aliitaka jamii imsaidie kupata fedha za kumaliza deni Muhimbili na kuendelea na matibabu.“Mimi nahitaji msaada wa matibabu. Maisha yangu ya mbele hata siyaelewi. Naomba nisaidiwe matibabu. Namuomba kila mtu anayeweza kunisaidia. Naiomba wizara ya Afya, Namuomba Waziri wa Afya nawaomba wananchi wote watakaoguswa na hali yangu wanaotaka kunisaidia kwa chochote wanitumie katika simu ili niweze kupata matibabu” alisema Mtope ambaye namba yake ya simu kwa anayetaka kumsaidia ni 0659376885.Ofisa Ustawi wa Jamii, Bahiya Akida alisema kwamba Mtepo alifika ofisini kwao na hali yake hairidhishi waliweza kumsaidia walichoweza lakini akasema wasamaria wanaweza kusaidia ili kijana huyo aende kumalizia matibabu Muhimbili na kupona.
kitaifa
Na DERICK MILTON – SIMIYU SIKU moja baada ya kuripotiwa habari juu ya kuibiwa kwa mashine ya kupima magonjwa ya ndani mwa mwili wa binadamu (ultrasound) katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bariadi ya Somanda, Mkuu wa Wilaya hiyo, Festo Kiswaga, ameagaza wafanyakazi wa hospitali hiyo kujichangisha na kuinunua. Katika kikao chake na watumishi wa hospitali hiyo, Kiswaga ametoa siku saba kwa watumishi wote kuchanga kulingana na mishahara kwa kila mmoja kuhakikisha wananunua mashine hiyo. Kikao hicho ambacho kilifanyika jana katika ukumbi wa hospitali hiyo, Kiswaga alimtaka Mganga Mkuu wa Halmashuari hiyo, Mkurugenzi wa Halmashuari kuhakikisha ikifika Agosti 21, wapeleke mashine hiyo Ofisini kwake. “Kwa kuwa mashine hii iliibiwa mchana na ikaibiwa na vifaa vyake vyote, inaonyesha kuwa walihusika ni wataalamu na kwa maana hiyo watumishi wote 137 wa hospitali hii mnahusika na wizi huu, hivyo nyie ni watuhimiwa wa kwanza wa wizi huu. “Kila mmoja kuanzia kwa Mganga Mkuu wa Halmashuari mtachangia kulingana na kila mtu na mshahara wake, nataka ndani ya siku saba nikabidhiwe hiyo mashine, ambaye atagoma kuchangia huyo itakuwa halali yangu,” alisema Kiswaga. Pia  alisema kuwa watumishi 17 ambao walikamatwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi, kesi yao itaendelea kufanyiwa kazi, huku akimtaka Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) kukamilisha uchunguzi unakamilika haraka. Aidha Kiswaga alimtaka Ofisa Utumishi wa Halmashuari hiyo kuorodhesha majina yote ya watumishi hao kwenye karatasi kisha kumpatia kwa ajili ya kuangalia nani atakaidi kuchanga ili mashine hiyo inunuliwe. Aidha alisema tabia ya wizi katika hospitali hiyo imekuwa sugu ambapo wahusika wakuu wamekuwa watumishi wake, hali ambayo alieleza hawezi kuivumilia kama kiongozi wa Wilaya. “Siyo mara ya kwanza kutokea wizi kwenye hospitali hii, mlihusika na wizi wa darubini (Microscope) ambapo baadaye ilipatikana ikiwa juu ya mti imeninginizwa, mkaiba tena mashine ya kufulia nguo ambayo mpaka sasa haijapatikana na leo tena Ultrasound hii haiwezekani na wala haikubaliki,” aliongeza Kiswaga. Alisema kitendo hicho ni uhujumu uchumi hivyo watumishi wote lazima wahusike katika kuhakikisha mashine hiyo inarudishwa kwa gharama zao. Kiswaga alisema yuko tayari kufukuzwa kazi kwa hatua yeyote ambayo atachukua kwa watumishi hao ikiwa watashindwa kuhakikisha wanarudisha mashine hiyo kupitia michango yao ndani ya muda ambao ametoa. Awali akizungumza katika kikao hicho Mkurugenzi wa Halmashuari, Merkzedeck Humbe, alisema kitendo hicho ni fedhea kwa halmashuari na Serikali hivyo alisema hatua kali zitachukuliwa kwa wahusika. “Mashine hii haiwezi kuibiwa na mtu yeyote kutoka nje bila ya kuwepo kwa ushirikiano kutoka kwa watu wa ndani, lazima wahusika wapo humu humu, kama ambavyo mlirudisha darubini basi fanyeni hivyo kwa mashine hii,” alisema Humbe. Awali akitoa taarifa ya wizi huo Mganga Mkuu wa Halmashuari, Mike Mabimbi, alisema mashine hiyo iliibiwa Agosti 5, majira ya mchana ikiwa kwenye wodi ya akina mama wajawazito hospitalini hapo. Mabimbi alisema baada ya kupata taarifa za wizi huo walitoa taarifa polisi ambapo, watumishi 17 walikamatwa na wamehojiwa ambapo uchunguzi dhidi yao bado unaendelea. Wakati huo huo Mkuu huyo wa Wilaya ametaifisha pamba inayodaiwa kuwa ya magendo ikiwa ni siku mbili baada ya kukamatwa kwa gari aina ya scania yenye namba za usajili T917 BCN ikiwa na pamba tani zaidi ya 20. Pamba hiyo ilikamatwa katika Kijiji cha Dutwa Wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Agosti 12, saa tano usiku, ikisafirishwa bila kibali maalumu huku ikiwa haijulikani wapi inapelekwa na wapi imenunuliwa.  “Baada ya wahusika kushindwa kujitokeza, sasa kama Mkuu wa Wilaya nachukua uamuzi wa kuitaifisha pamba hii na tunaenda kuiuza kwenye viwanda vya kuchambua pamba leo hii na fedha zote zitapelekwa kununua vifaa vya kukamilisha ujenzi wa bweni katika Shule ya Sekondari Simiyu,” amesema Kiswaga.
afya
KAMANDA wa Polisi Mkoa (RPC) wa Dodoma, Gilles Muroto amewataka viongozi wa madhehebu ya dini mkoani hapa, kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini wao katika suala la ulinzi na usalama kwenye kipindi cha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Alitoa ushauri huo alipozungumza na viongozi wa madhehebu ya dini katika kikao cha pamoja kuhusu hali ya usalama katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya. Alisema kuwa viongozi wa madhehebu ya dini, wanayo nafasi kubwa ya kuwashirikisha na kuwaelimisha waumini juu ya suala la ulinzi na usalama na maeneo yao yakawa salama na amani.“Jeshi la polisi kwa kushirikiana na viongozi wa dini pamoja na waumini wakiwa kitu kimoja, kuna asilimia kubwa ya kuwepo kwa salama kwa kipindi hiki cha tunachoendea sikukuu,” alisema.Kamanda huyo alitoa tahadhari kwa waumini katika kipindi hiki cha sikukuu, kujiwekea ulinzi wa kutosha kwenye maeneo yao wanayoishi Kamanda huyo aliwataka viongozi hao wa dini, kuhakikisha nyumba zao za ibada wanafunga kamera, ambazo zitasaidia kudhibiti ulinzi wa maeneo yao.Mwenyekiti wa Umoja wa Madhehebu ya dini ya Kikristo Mkoa wa Dodoma Askofu Damas Mukassa, alilipongeza jeshi hilo la polisi kwa kuwatambua viongozi wa dini kwenye mchango wao wa kushirikiana suala la ulinzi na usalama.Alisema viongozi wa madhehebu ya dini pamoja na waumini wanaowaogoza, watashirikiana na jeshi hilo muda wote katika suala la ulinzi na usalama, bila kuangalia kama kuna sikukuu. Alisema moja ya majukumu ya viongozi wa dini ni kuhakikisha usalama unakuwepo. Alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama, vipo kwa ajili ya kuhakikisha amani inakuwepo.
kitaifa
MAMLAKA ya Mapato nchini (TRA) imetoa ufafanuzi kuhusu ucheleweshwaji wa kutoa leseni za udereva na kusema jambo hilo limesababishwa na mabadiliko ya mfumo wa utoaji leseni ambao hivi sasa unaboreshwa ili leseni ziwe imara na kwamba kazi hiyo itakamilika kabla ya mwisho wa mwezi huu.Akizungumza na HabariLeo jana, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo alisema ni kweli kumekuwa na ucheleweshaji wa kupewa leseni kwa madereva walioomba leseni kutokana mfumo wa sasa kubadilishwa. Aliongeza kuwa wataalamu hao wakandarasi wameshafika na wanaendelea kukamilisha kazi hiyo na kwamba ndani ya siku chache kuanzia sasa watakuwa wamemaliza na kuanza kutoa leseni kabla ya mwisho wa mwezi huu.“Nia ya serikali na TRA ni kuboresha leseni zetu ili ziwe imara na tumekubaliana na Jeshi la Polisi kwa sasa madereva waendelee kutumia leseni za zamani ili mradi tu anaposimamishwa aoneshe risiti ya malipo aliyolipia leseni mpya,” alisema Kayombo. Alisema lengo la kuanzisha mfumo mpya wa kompyuta wa leseni ya kuendesha ni kuisaidia serikali kukusanya taarifa sahihi kuhusu dereva ambazo zitasaidia katika kufuatilia mienendo yao na kuhakikisha kuwa serikali inapata mapato yake ya kutosha.Alisema matarajio ya serikali ni kwamba mfumo huo mpya wa kutoa leseni utapunguza ajali za barabarani ambazo nyingi zinasababishwa na madereva ambao hawana sifa za kutosha za kuendesha magari. Kayombo aliwataka madereva ambao wamelipia leseni na hawajazipata kuwa watulivu kwani maboresho hayo yanayofanywa ni katika kuzifanya leseni hizo mpya kuwa imara na kwamba ndani ya wiki mbili kuanzia sasa zitaanza kutolewa. Alisema mfumo mpya wa leseni unachukua nafasi ya mfumo wa zamani ambao hakuweza kutofautisha kati ya aina ya leseni kwa ajili ya kuendesha gari na magari ya abiria ya uwezo tofauti.
kitaifa
Safina Sarwatt, Moshi Zaidi ya Dola za Marekani milioni 10, zimetengwa na Shirika lisilo la kiserikali la Candy and Candy Group Limited, kwa ajili ya kuwawezesha kiuchumi vikundi vya wanawake wajane, watoto waishio katika mazingira magumu na vijana walioathirika na matumizi ya dawa za kulevya. Akizungumza katika uzinduzi wa mradi huo jana mjini Moshi, Meneja wa shirika hilo, Fortunate Macha, amesema lengo la shirika hilo ni kuwasaidia makundi hayo kujikwamua kichumi na kuondokana na hali ya umaskini. “Shirika limetenga fedha hizo kwa makundi hayo ili kuwasaidia kujikwamua kichumi na kuanzisha biashara mbalimbali itakayowawezesha kuwaongezea kipato. “Mradi huo kwa mkoa Kilimanjaro unatarajia kuanza katika vijiji vya Kata ya Pasua na Kahe wilayani Moshi na kuendelea,” amesema. Kwa upande wake Ofisa Mradi wa shirika hilo, Elizabeth Sabula, amesema mradi huo pia unatarajia kufikia vijana zaidia 200 wenye vipaji vya uimbaji. Akizungumza kwa niaba ya Ofisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Kilimanjaro, Gerald Sakaya, aliipongeza shirika la hilo kwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwasaidia makundi hayo kuondokana na umaskini.
afya
    Na ELIYA MBONEA-ARUSHA SHIRIKA la Mfuko wa Msamaria la Marekani linaloendeshwa na Frankline Graham, mtoto wa Muhubiri maarufu duniani, Bill Graham, limetoa ndege kubwa kwa ajili ya kubeba wanafunzi majeruhi watatu wa ajali ya basi la Lucky Vincent iliyoua watu 35. Ndege hiyo DC 10, inatarajiwa kuruka usiku wa leo (jana) Alhamisi kutoka  Uwanja wa ndege wa Charllote katika  Jimbo la North Carolina, Marekani na inatarajiwa kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo. Akizungumzia kukamilika kwa baadhi ya hatua za safari hiyo mjini hapa jana, mratibu wa safari hiyo, Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, alithibitisha kukamilika  maandalizi ya safari hiyo. “Kuna mambo nimeamua kuyasimamia, nimewasiliana na Shirika la Mfuko wa Msamaria linasimamiwa na Frankilin Graham mtoto wa Bill Graham nimewaeleza kilichotokea kwa watoto wakakubali kutoa ndege,” alisema Nyalandu na kuongeza: “Tunashukuru Mungu Hati za kusafiria zimekamilika kwa wazazi, madaktari na watoto maandalizi ya VISA yanaendelea kushughulikiwa safari hii tunatarajia itakuwa Jumamosi (kesho) endapo tu VISA itakuwa imekamilika”.   Alisema  ndege hiyo DC 10 baada ya kutoka KIA itakwenda moja kwa moja hadi Uwanja wa ndege wa Charllotte,  North Calorina. Alisema baada ya kuwasili uwanjani hapo Shirika hilo la Msamaria limeandaa ndege nyingine maalumu (Air Ambulance) itakayoondoka uwanjani hapo hadi Hospitali ya Mercy iliyopo Jiji la Sioux katika Jimbo la IOWA.
kitaifa
Na Christina Gauluhanga -Dar-es-salaam MANISPAA ya Ilala imetumia Sh milioni 86 kwa awamu mbili tofauti kudhibiti homa za dengue na magonjwa mengine ya mlipuko ili kutokomeza maradhi hayo. Akizungumza na MTANZANIA ofisini kwake juzi, Mganga Mkuu Manispaa ya Ilala, Dk. Emily Lihawa alisema jitihada zimefanyika kupuliza dawa sehemu mbalimbali, hasa katika madimbwi. Alisema awali walitumia Sh milioni 52 kununua dawa ya kungamiza viluilui wa mbu na awamu ya pili wametumia Sh milioni 34 kununua dawa nyingine za kuua mbu pevu ambayo wamepiga katika shule mbalimbali ili kutokomeza ugonjwa huo.  Emily alisema pia tayari wamehamasisha wananchi kupima ugonjwa huo ambapo Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii wameleta vifaa mbalimbali vya upimaji.  “Ndani ya kata 36 tumejitahidi kuhamasisha upimaji, usafishaji mazingira lengo likiwa ni kutokomeza magonjwa ya mlipuko ambapo takwimu halisi zitatolewa na wizara,” alisema Emily. Alisema hata hivyo ugonjwa huo kwa sasa umeshuka tofauti na miaka ya 2011 /2012 ambapo ulianza na kushambuliwa wananchi kwa kasi ikiwamo watumishi wa afya. Akizungumzia kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, alisema hali ni shwari katika manispaa hiyo kwa kuwa kwa siku tano sasa hakuna mgonjwa aliyeripotiwa.
afya
Na MALIMA LUBASHA – SERENGETI ZAIDI ya tani 4.1 za chakula zinahitajika wilayani ya Serengeti mkoani Mara ili kunusuru maisha ya kaya zaidi ya 32,000 kutokana na mahindi yao  kukauka kutokana na ukame. Akizungumza  na waandishi wa habari ofisini kwake  juzi, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdin Babu alisema hali ya chakula  kwa mwaka huu sio ya kuridhisha kutokana na  mvua vuli  kutonyesha kwa wakati. Alisema wapo  baadhi ya watu, wanakula mlo mmoja na wengine mitatu kwa siku na hakuna mtu wala mifugo iliyokufa kutokana na ukame, kwa sasa bei ya mahindi debe moja linauzwa  Sh 15,000 ambapo upatikanaji wa chakula kwenye masoko wa kiwango kinachohitajika. Alisema wilaya bado inaendelea kufanya tathimini kwa kupita kila kaya ili kubaini hali ya chakula kwa wale wenye upungufu wa chakula, kaya zisizo na uwezo,zenye uwezo na zile zinazohitaji msaada wa chakula  na tayari wameomba kibali ili wafanyabiashara waruhusiwe kuuza mahindi kwa bei nafuu. “Maofisa kilimo wamefanya tathimini kwenye  kaya 32,055 zilizopo katika  kata 22 kati ya 30,wamebaini kaya 8,582 ambazo ni maskini  zinahitaji chakula cha bure tani 811, kaya 10,655 wenye hali ya nafuu wanahitaji tani 1,454.4 na kaya 12,818 zilizo na uwezo wa kununua kwa bei yoyote zinahitaji tani 1,749.7 za mahindi,” alisema Babu. Hata hivyo, Babu  amewataka wananchi kuhifadhi chakula kilichopatikana na kuacha utamaduni wa kutumia nafaka kutengenezea pombe za kienyeji na kila familia iwe na ghala la kuhifadhi chakula. Alisema mbali ukame, mvua kutonyesha kutokana na mabadiliko ya tabianchi pia yapo malalamiko ya wananchi kuhusu tembo kuvamia mashamba yao na kula mazao yote na kueleza kuwa changamoto hiyo serikali inalifahamu na takwimu za uharibifu zilikwisha wasilishwa wizara ya maliasili na utalii ili kuli pa kifuta machozi kwa wote walioathirika.
kitaifa
HIVI karibuni, Tanzania ilishitushwa na tukio la kutekwa nyara kwa mfanyabiashara maarufu barani Afrika, Mohamed Dewji (MO). Tukio hilo liliwasikitisha Watanzania wengi, ingawa baadhi ya wanasiasa walitaka kulitumia kama mtaji wa kisiasa kwa kuwa lilikuwa na sura ya kulipaka matope taifa ili wasio makini kufikiri, wadhanii au waamini kuwa Tanzania sio salama.Wengine wameamua kulitumia kuumba maneno yanayofanana na ukweli mengi yakilenga kuipaka matope serikali. Wengine wakataka hata kujaribu kushinikiza Taifa liombe msaada wa wapelelezi kutoka nje ya nchi, huku wakijua wazi kabisa kuwa vyombo vya dola nchini vipo na vinaweza kufanya kazi zake kuhakikisha ulinzi na usalama wa kutosha.Ndiyo maana Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Simon Siro, alilihakikishia taifa kupitia vyombo vya habari kuwa, Jeshi la Polisi lipo makini, lina uwezo na litahakikisha MO anatafutwa na kupatikana. Bahati nzuri, ukweli huo ukathibitishwa kwa kupatikana kwa mfanyabiashara huyo.Ndiyo maana Watanzania wanalipongeza na kujivunia kuwa na jeshi lao makini na lenye uwezo wa kuwahudumia, licha ya changamoto kadhaa zinazoweza kujitokeza. UTEKAJI HAUJAANZA LEO Vitendo vya utekaji nyara mara nyingi hutumiwa na baadhi ya watu (wahalifu) kwa madhumuni kadhaa, mojawapo ikiwa ni kujipatia fedha kutoka kwa ndugu wa mtu aliyetekwa.Lakini pia hutumiwa kisiasa kwa maana ya kupunguza nguvu za wapinzani na wakati mwingine hutumiwa kuipaka matope serikali ili kudhoofisha nguvu za kiutawala. Hata hivyo, asilimia kubwa ya utekaji nyara huwa unalenga kujiingizia kipato kwa njia kudai kikombozi ili kumwachia mateka.Uhalifu huu ni kati ya matendo ya kale yaliyofanyika hata kabla ya kuzaliwa Yesu Kristo zaidi ya miaka 2000 iliyopita kama yalivyo matendo ya rushwa, ugaidi, ukahaba, sanaa ya urembo, ujangili, uharamia, ujambazi, mihadarati na kadhalika.WATU MAARUFU WALIVYOATHIRIWAMtaalamu wa Kuzuia Utekaji El Nahual wa blogu ya Mexico Para los Mexicanos nchini Mexico akitoa maoni juu ya kutekwa Felix I Batista, mtaalamu wa kuzuia utekaji nyara wa Marekani alisema: “Jambo la kwanza kufanya ni kucheka; la pili linalonijia ni woga…Kama mtaalamu wa kijeshi mstaafu mwenye uzoefu wa miaka 24 katika nyanja ya usalama anaweza kutekwa, je, sisi wengine tuna nafasi gani ya kusema kwamba hatuwezi kutekwa?” Batista alitekwa na watu waliovaa vinyago usoni akiwa nchini humo kuendesha semina kama mtaalamu wa kukodiwa wa kampuni ya usalama yenye makao huko Texas ASI Global LLC.Blogu ya The Mex Files ilikuwa na maswali yafuatayo kuhusiana na tukio hilo: Kama Batista ni mtaalamu, imekuwaje akaruhusu atekwe yeye mwenyewe? Batista alikuwa mfanyakazi wa ‘kampuni ya usalama’ yenye makao yake huko Texas ASI Global.Imeelezwa kwamba alikuwa huko Saltillo kwa shughuli za kibinafsi. Je, alikuwa akimfanyia nani kazi huko? Je, kampuni ya ASI Global siyo moja ya kampuni za Kimarekani zinazopokea fedha kwa ajili ya ‘Mpango wa Merida’…Na hili linatuambia nini juu ya utendaji kazi wa wataalamu wake wa ukufunzi? Takwimu kadhaa zinaonesha kuwa utekaji unatokea kwa takribani mara mbili kwa siku na hasa katika majimbo ya mpakani kaskazini mwa nchi hiyo. Mexico ina wastani wa juu zaidi wa utekaji nyara ikilinganishwa na nchi nyingine duniani.Matukio haya huathiri marafiki na familia za waliotekwa, kama alivyoathirika bloga Tony Scotti, Rafiki wa karibu wa Batista, Tonny alisema hivi: “Ninamfahamu Felix (Batista), ni mtu mwenye uwezo mkubwa wa kuzuia utekaji nyara, Felix ana uzoefu wa zaidi ya miaka 20 katika shughuli za kuokoa mateka.”Akaendelea kusema: “Felix ni mtu anayejulikana, ambaye mara nyingi hunukuliwa kwenye magazeti na hata katika jarida la mwezi huu la Usalama. Kujulikana kwake kunaweza kuwa ndiko kulikomsababishia kutekwa.Baada ya kusoma magazeti ninaweza kuhisi kwamba Felix aliwekewa mtego, na aliwekewa mtego huo na mtu anayemuamini.” Julius Caesar Amiri jeshi aliyefanikiwa zaidi katika hitoria ya dunia, Julius Caesar, alitekwa nyara ili kupata fidia katika karne ya kwanza, ndivyo na Richard wa Kwanza (King Richard I), mfalme wa Uingereza mwenye roho kama simba alivyotekwa.Katika karne ya12 fidia kubwa zaidi iliyowahi kulipwa ilikuwa tani 24 za dhahabu na fedha ambazo Wainka walimpa mvumbuzi maarufu Mhispania Francisco Pizzaro asaidie kuachiwa huru kwa chifu wao Atahuallpa mwaka wa 1533.Hata hivyo, watekaji hao walimuu kwa kumnyonga. Aldo Moro Inaelezwa katika vyanzo mbalimbali kuwa, jambo lililoduwaza ulimwengu ni kutekwa nyara kwa Waziri Mkuu wa Italia, Aldo Moro.Waziri Mkuu huyo alikuwa mwanasiasa maarufu nchini humo aliyependwa sana na raia. Alihudumu kama Waziri Mkuu kati ya 1963-1968. Moro alikuwa ndiye waziri mkuu aliyekuwa amehudumu muda mrefu zaidi tangu wakati wa Vita Kuu vya Dunia.Kundi la Red Brigades lilifanya mashambulio mabaya, ikiwa ni pamoja na utekaji nyara na mauaji ya Waziri Mkuu huyo wa mwaka 1978. Kundi hilo liliweza kuzuia msafara wa Waziri Mkuu huyo na kuwaua walinzi wake kadhaa na kufanikiwa kumteka nyara likidai Serikali kuwaachilia washirika wake.Serikali haikukubali matakwa hayo ndipo kundi hilo lilipomuua kiongozi huyo kikatili. Moro alikuwa mwanachama wa chama cha Kidemokrasia cha Kikristo cha Italia na alishika madaraka ya uwaziri mkuu kwa duru tano.Umaarufu wake na kupendwa na watu pengine vilisababisha kiongozi huyo kuwindwa na kundi hilo la Red Brigades. Machi 1978, wanachama wa kundi la wanamgambo wa Red Brigades, waliwaua walinzi wake watano na kumteka kwenye barabara moja jijini Roma, wakitaka kuachiliwa huru kwa wenzao 16 waliokuwa wanazuiliwa na serikali,.Moro alipigwa risasi mara kumi akiwa kwenye gari na kutelekezwa akiwa marehemu baada ya kuzuiliwa kwa siku 55. UTEKAJI NCHINI MEXICO Polisi wa mji wa Axapusco walifanikiwa kuwaokoa wahamiaji 103 waliokuwa wametekwa nyara wakiwa wanaelekea kuvuka mpaka wa Marekani katika jengo lililokuwa nje ya mji wa Mexico.Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na polisi wa kijiji hicho, waathirika wengi zaidi walitoka mji wa Guatemala na El Salvador walipofungiwa katika jengo hilo kwa muda wa siku 35.Mmoja kati wa wahamiaji hao alifanikiwa kutoroka na kukimbilia kituo cha polisi kilichopo kijijini hapo kutoa taarifa ya kutekwa kwao. Viongozi wa vikosi bora vya kukabiliana na utekajinyara nchini Mexico, Colombia na katika nchi zilizokuwa jamhuri za Sovieti walilaumiwa kwa kujihusisha na utekaji nyara huo. Naye Mtekaji nyara sugu wa Mexico alisema kuwa alizingirwa na ulinzi rasmi uliotokana kwa kuwahonga maofisa na waendesha mashtaka wa manispaa, jimbo na serikali.UTEKAJI NYARA NA MAUAJIUtekaji nyara na mauaji yanayofanywa na vikundi mbalimbali vya watu walioficha sura zao, limekuwa ni jambo la kawaida katika nchi za Amerika ya kusini. Watu wengi wasiokuwa na hatia wamekuwa wakiuawa. Inakadiriwa kwamba katika kipindi cha mwaka mmoja, zaidi ya watu laki tano waliuawa na wahalifu; idadi hiyo ni kubwa kuliko ya watu waliouawa vitani.Mataifa mengine yanafika mbali na kuilaumu serikali ya Rais Hugo Chaves kuwa imelea magenge ya watekaji na mauaji. Kwa mujibu wa ripoti hiyo katika kipindi cha mwaka mmoja, watu zaidi ya 100,000 waliuawa na wahalifu katika bara la Amerika ya Kusini.Nchini Brazili peke yake zaidi ya watu 50,000 waliuawa, nchini Venezuela na Honduras suala la mauaji kama hayo ni jambo la kawaida, kila baada ya dakika 9 hadi 10 utekaji au mauaji hutokea katika nchi hizo.Aidha Sheria ya Kimusa ilitoa adhabu ya kifo kwa watekaji nyara huko nyuma katika karne ya15 (Kumbukumbu la Torati 24:7 Ni kwa msingi huo, unapotokea uhalifu wa namna hiyo na mwingine wowote, wajibu wa raia ni kuvisaidia vyombo vya dola kwa kutoa taarifa sahihi kusaidia uhalifu usitendeke au kuwakamata wahalifu na sio kujaribu kuwakatisha tamaa watendaji wa vyombo hivyo na wengine kuvutumia kujitafutia umaarufu wa kisiasa.
kitaifa
MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara, Simba, leo watakuwa na kibarua kigumu cha kutaka kuendeleza ushindi katika mchezo wake na timu ya JKT Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Jamhuri wa Morogoro.Mchezo wa leo unatabiriwa kuwa mgumu kwa timu zote mbili kutokana na Simba kuhitaji ushindi ili iendelee kujiweka vizuri kwenye kutetea taji lake huku JKT ikihitaji kujiweka sawa ili ibaki kwenye ligi kwani haipo salama sana. Mechi hiyo ni ya pili kufanyika katika Uwanja wa Jamhuri baada ya Simba kuufanya uwanja wake wa nyumbani kupisha matengenezo kwenye Uwanja wa Taifa. Simba inaingia kwenye mechi hiyo ikiwa na pointi 57 na ushindi wa leo unaweza kuisogeza mbali zaidi.Simba kwa sasa inajivunia kuwa na hazina ya mabao ya kufunga tofauti na timu zinazoshiriki Ligi Kuu kwa vile hadi sasa imefikisha mabao 41 wakati wapinzani wake wakuu Azam FC wakiwa na mabao 28 na Yanga ina mabao 26 ya kufunga. JKT ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo ikiwa na pointi 31, kwa maana hiyo ushindi leo ni muhimu kwake. Kwa sasa timu hiyo inaongozwa na kocha Abdallah Balesi aliyekatishiwa mkataba wake na Prisons kutokana na kuwa na mwenendo mbaya kwenye ligi kabla haijakaa sawa baada ya kocha huyo kuondoka.Balesi amechukua mikoba ya Bakari Shime ambaye pia alikatishiwa mkataba na timu hiyo kutokana na kuwa na mwenendo mbaya. Mechi ya kwanza iliyofanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga, JKT Tanzania ilifungwa mabao 2-0 hivyo ni kazi kwao kubadili matokeo leo.Simba inatambia safu yake ya ushambuliaji na hivyo mabeki wa JKT watakuwa na kazi ngumu ya kuwazuia washambuliaji wenye uchu wa mabao kama Meddie Kagere na nahodha John Bocco aliyefunga mabao mawili mechi iliyopita huku Kagere akifunga bao moja. Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems aliliambia gazeti hili kuwa anaichukulia mechi hiyo kwa uzito wa hali ya juu. Aussems alisema, kila mchezo wa Ligi Kuu kwao una umuhimu mkubwa katika kusaka ushindi utakaochangia kutetea taji lao.
michezo
SERIKALI imebaini asilimia 88.6 ya waajiri ambao ni wamiliki wa vyombo vya usafi rishaji, hawatekelezi kikamilifu Sheria ya Kazi ikiwemo kutowapa kabisa madereva mikataba ya ajira na likizo ya mwaka. Pia, imebainika waajiri hao wamekuwa wakiwafanyisha kazi madereva kwa saa nyingi zaidi na kutowasajili kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii. Hayo yamebainishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama wakati wa kikao cha mashauriano kati ya ofisi yake na viongozi wa vyama vya wafanyakazi, madereva na wamiliki wa vyombo vya usafirishaji. Alisema katika kushughulikia malalamiko kutoka kwa wafanyakazi wa sekta ya usafirishaji (madereva) za kunyimwa haki zao za msingi na waajiri wao, serikali ilifanya ukaguzi maalumu uliolenga kubaini hali halisi ya utekelezaji wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini.Mhagama alisema uchunguzi huo, uliofanyika kati ya Julai 15 hadi Agosti 26 mwaka huu, kwa kukagua kampuni au wamiliki wa vyombo vya usfirishaji 787 kutoka mikoa 24, ulibaini kuwa kati ya waliokaguliwa, ni waajiri 90 tu waliotekeleza kikamilifu sheria ya kazi. “Uchunguzi ulilenga kukagua kama madereva wana mikataba ya ajira, kukagua viwango vya mishahara kwa kulinganisha na Agizo la Serikali Namba 196 kuhusu mishahara ya sekta binafsi la mwaka 2013. Pia tulikagua kama madereva wamesajiliwa katika mifuko ya hifadhi ya jamii na kupokea malalamiko ya madereva kuhusu masuala ya saa za kazi na mambo mengine ya ajira,” alisema. Jenista alisema kuwa, “Ukaguzi umebaini kuwa hali ya utekelezaji wa sheria za kazi na kanuni zake katika sekta ya usafirishaji si ya kuridhisha, hii imechangiwa kwa kiasi kikubwa na uelewa mdogo wa sheria za kazi miongoni mwa waajiri na wafanyakazi na hivyo kusababisha kuwepo kwa malalamiko na migogogoro ya mara kwa mara.” Kutokana na ukaguzi huo, serikali na vyama vya wafanyakazi madereva na waajiri walikutana juzi katika kikoa kilichochukua takribani saa sita na kufikia maazimio yaliyosainiwa na pande zote tayari kwa ajili ya utekelezaji. Akisoma maagizo ya kikao hicho, Jenista alisema Mkataba wa Ajira ulioboreshwa uanze kutumika na waajiri wote wawapatie madereva wao mkataba huo. “Mwaka 2017, serikali ilitoa maagizo ya madereva kupewa mikataba wa ajira ulioboreshwa, lakini utekelezaji wake haukuwa mzuri, kwa hiyo sasa ni lazima waajiri kutekeleza hili,” alisema na kuongeza kuwa pia wameazimia Kanuni zinazoandaliwa na Wizara ya Uchukuzi, zitengeneze mazingira yatakayoruhusu Sheria za Kazi kutekelezwa na waajiri. Pia wameazimia kutolewa kwa elimu ya Sheria ya Kazi itolewe kwa vyama vya wamiliki wa vyombo vya usafirishaji na vyama vya madereva. “Tunatakiwa kuanza kutoa upya elimu ya sheria za kazi kwa waajiri na waajiriwa katika sekta hii na itolewe kwa nguvu zote.”“Maazimio mengine ni kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu ambayo mimi nasimamia kuendela kusimamia kikamilifu Tume ya Usuluhishi na Uamuzi ili iweze kutekeleza majukumu yake kwa weledi,” alisema. Alisema pia wameazimia vyama vya wafanyakazi na waajiri, wapewe nakala ya taarifa ya ukaguzi uliofanyika Julai hadi Agosti 2019 ili viweze kujadilianna na wanachama wao na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua changamoto. Alisema kikao hicho kimeazimia kuendelea kuheshimu na kuthamini utu na heshima ya mtu kati ya madereva na waajiri na wameazimia kufanyika kwa kikao kitakachojumuisha wizara zote zinazogusa sekta ya usafirishaji na madereva.
kitaifa
LONDON, ENGLAND NYOTA wa mabingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, Riyad Mahrez, amekata mzizi wa fitina na kuamua kumalizana na klabu hiyo kwa kusaini mkataba wa miaka minne. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25, alikuwa anahusishwa na kujiunga na klabu ya Arsenal, lakini hadi sasa dili hilo linaonekana kufikia mwisho baada ya kumalizana na klabu hiyo ya King Power. Mkataba huo mpya utamfanya mchezaji huyo aendelee kuwa katika uwanja wa King Power hadi Juni 2020, huku akipokea kitita cha pauni 100,000 kwa wiki. Hata hivyo, mchezaji mwenzake wa klabu hiyo, Jamie Vardy, ameonekana kufurahishwa na kitendo cha mpambanaji mwenzake kujitia kitanzi ndani ya klabu hiyo. Kwa upande mwingine kocha wa klabu hiyo, Claudio Ranieri, amezidi kupata nguvu baada ya kumalizana na mchezaji huyo huku akiwa tayari amemkosa mchezaji wake muhimu katika safu ya kiungo, N’Golo Kante, aliyejiunga na klabu ya Chelsea. Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 25, alionesha uwezo wa hali ya juu katika michuano ya Kombe la Euro 2016 nchini Ufaransa, akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya nchi hiyo, hivyo kuwashawishi Chelsea kuweka kitita mezani cha pauni milioni 32 katika kipindi hiki cha usajili. Mwenyekiti wa klabu ya Leicester City, Vichai Srivaddhanaprabha, amefanya mazungumzo ya kina na Mahrez na kumwambia kwamba klabu hiyo inataka kuwapigania wale wote ambao walipambana na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu uliopita, ili waweze kuendelea kukaa kwenye klabu hiyo kwa muda mrefu. Hata hivyo, mshambuliaji mwingine wa timu hiyo, Jeffrey Schlupp, ambaye alikuwa anawindwa na klabu ya West Brom, amekubali kubaki kwa mabingwa hao na yupo tayari kwa dili jipya. Mahrez, raia kutoka nchini Nigeria, alikuwa mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita, aliyefunga mabao 17 na kutoa pasi za mwisho 11. Alijiunga na klabu hiyo mwaka 2014, akitokea Le Havre ya nchini Ufaransa.
michezo
NEW YORK, MAREKANI NYOTA ya msanii wa filamu nchini Marekani ambaye ni mzaliwa wa Kenya, Lupita Nyong’o, inazidi kung’ara baada ya kuweka wazi kwamba yupo kwenye maandalizi ya kufanya filamu ya pamoja na nyota wa muziki wa RnB, Robyn Rihanna. Inasemekana kuwa, wawili hao walikutana mwaka 2014 kwenye mashindano ya urembo yajulikanayo kwa jina la Miu Miu, kisha walipiga picha ya pamoja na baada ya hapo mazungumzo yao yaligusia masuala ya filamu. Licha ya muda mrefu kupita tangu walipokutana, lakini Lupita alijikuta akimkumbusha Rihanna mbali pale alipoweka picha waliyopiga pamoja na Rihanna walipokutana mwaka huo 2014, huku mashabiki wao wakiwapongeza kwa kupendeza. Baada ya picha hiyo na kujali kwa mashabiki wao, Rihanna alimtaka Lupita wafanye kitu cha pekee kitakachowaongezea furaha mashabiki wao. Ndipo wawili hao wakafikia makubaliano ya kufanya filamu ya pamoja inayotarajiwa kufanyika hivi karibuni. “Picha ambayo niliiweka kwenye akaunti ya Twitter imetufanya mimi na Rihanna tufanye filamu, hivyo mashabiki wakae tayari kwa kazi yetu,” aliandika Lupita.
burudani
BUNGE la Tanzania limeombwa kuunga mkono kampeni ya kuondoa mfumo dume unaowanyima haki ya kurithi ardhi wanawake wanapofi wa na waume zao.Ombi hilo limetolewa na asasi 12 zinazojishughulisha na kutetea haki za wajane kurithi ardhi kwenye mafunzo yaliyowakutanisha na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Utalii.Akitoa ombi hilo Ofisa Programu wa Asasi ya Tanzania Land Alliance (TALA), Jamal Kafumbee aliitaka kamati hiyo kuwatetea wanawake hasa wajane kumiliki ardhi baada ya kufiwa na waume zao.Kafumbee alisema sheria nyingi za kimila zimekuwa zikitoa ardhi kwa wanaume au watoto wa kwanza wa kiume, lakini hazitoi ardhi kwa wajane na hata watoto wa kike hata kama wanakuwa wa kwanza kuzaliwa.Alisema wakati wa ukoloni mfumo huo uliruhusu wanaume pekee kulimiki ardhi, lakini wanaliomba Bunge kupitia wabunge majimboni kusaidia kutoa elimu kwa viongozi wa kamati za vijiji kuwapa haki wajane na watoto wa kike katika kumiliki ardhi.Ofisa Programu Mwandamizi kutoka HakiArdhi, Joseph Chombola alisema baadhi ya sheria zinatoa haki upande wa kiume wala si wanawake kuhodhi ardhi ya ukoo zinatakiwa kuendelea kupigiwa kelele ili kuondoka miongoni mwa jamii kwani binadamu wote wana haki ya kumiliki ardhi.Alisema mila na desturi katika baadhi ya makabila zinapendelea wanaume na makabila machache kiasi cha asilimia 15 yanayoongozwa na wanawake ndiyo yanatoa nafasi kwa wanawake kusimamia ardhi.Alisema hali hiyo pia inachangiwa na tamko la kimila la mwaka 1964 ambalo linampa haki mwanaume kumilikishwa ardhi na mwanamke kunyimwa. Akizungumza Mbunge wa Babati Mjini, Paulina Gekul (CCM) alisema hivi sasa watoto wa kike wanatakiwa kupewa haki ya kumiliki ardhi alisema atashangaa kuona familia za wasomi wa karne hii wanashindwa kuwaridhisha ardhi watoto wao wa kike.Mbunge wa Korogwe Mjini, Timotheo Mnzava (CCM) alisema elimu inatakiwa kuendelea kutolewa katika maeneo mbalimbali hasa katika ngazi za vijiji ambako mabaraza ya vijiji yamekuwa yakiwanyima haki wanawake pamoja na kuwapo wanawake wawakilishi.Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii, Shaban Shekilindi (CCM) alisema wao kama wabunge wamesikia ombi la asasi hizo na watalifanyia kazi.
kitaifa
  Na ABDALLAH NG’ANZI  (TUDARCo) KUNA wakati unatafakari namna mambo yanavyokwenda, hasa katika zama hizi za kidigitali. Moja ya jambo kuu linaloumiza vichwa vya wahitimu wengi  ni ukosefu wa ajira. Ajira imekuwa changamoto si kwa Tanzania pekee bali duniani kwa ujumla. Ripoti ya Shirika la Kazi Duniani (ILO) inaonesha kuwa mwaka huu idadi ya watu wasio na ajira itaongezeka kwa asilimia 5.8(awali ilikuwa asilimia 5.7) na kufanya jumla ya watu wasio na ajira kufikia milioni 500.8 duniani . Hili si jambo zuri kulisikia likitamkwa kwani ndoto za wasomi wengi ni kujiajiri au kuajiriwa na kufaidi kile ambacho wamekitafuta kwa jasho kwa zaidi ya miaka 18. Binafsi nimegundua kuwa zipo sababu ambazo zinawakosesha ajira vijana wengi, mojawapo ni ujuzi binafsi wa mtu ukiachana na vyeti alivyo navyo. Kwa mfano, mhitimu akiulizwa mbali na elimu aliyonayo ni kipi cha ziada alicho nacho? Katika dunia ya sasa elimu si stashahada, shahada ya uzamili au uzamivu. Elimu ni namna gani unaweza kukabiliana na mazingira magumu ya ushindani. Kwa sasa kama Taifa tumeanza na soko la pamoja la Afrika Mashariki (EAC) lakini pia sisi tukiwa sehemu ya Taifa tunachanganyika na watu wa mataifa mengine. Kuna fursa nyingi tu zinazoweza kubadilisha maisha yetu. Mathalani, mara nyingi watu wanauliza kozi gani inalipa. Ukweli ni kwamba kila kilichopo duniani ukiweza kukitumia vizuri na kwa maarifa kinalipa. Lakini pia lazima uelewe kuwa milango haipo wazi kana kwamba utaweza kupata kila kitu kama unavyotarajia, inahitaji uvumilivu na kuvuja jasho. Mambo yamebadilika, kuna wasomi wengi wenye sifa wanazurura, sasa mwenzangu uliyehitimu juzi tu kama unadhani umefika basi ukweli ni kwamba bado una safari ndefu. Soko la ajira la sasa haliangalii shahada wala stashahada, bali wewe ukiwa mwajiriwa utaleta mabadiliko gani chanya kulisaidia shirika au taasisi? Una ujuzi gani zaidi ya shahada yako? Ikifika hapo kuna mambo yanajitokeza Je, una kitu gani kinachokutofautisha na washindani wengine? Wasomi msibweteke, endeleeni kutafuta ujuzi ili kujiongezea thamani.
kitaifa
RAIS mpya wa Baraza la vyama vya soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Wallace Karia (pichani) ameahidi kuimarisha na kuboresha michezo ndani ya nchi wanachama.Karia ambaye pia ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) alichaguliwa bila kupingwa kuongoza Cecafa miaka minne katika uchaguzi mkuu uliofanyika Kampala.“Nitaboresha michezo kwa maana ya upatikanaji wa wadhamini kwa mashindano ya klabu, wanawake na yale yanayoshirikisha nchi pia nitaimarisha michuano ya soka la ufukweni na nitasimamia nchi waalikwa kushiriki kikamilifu kwenye michuano inayoadaliwa na Cecafa,” alisema Karia.Pia Karia alisema atahakikisha yanakuwepo mashindano yanayohusisha umri chini ya miaka 15 ili kuwa na timu bora za taifa za baadae.“Kwa sasa tuna mashindano kuanzia U-17 hadi timu za wakubwa nitahakikisha tunakuwa na mashindano ya U-15 kwa wanawake na wanaume ili baadaye tuwe na timu za taifa imara zitakazoweza kushindana,” alisema Karia.Karia ambaye atakuwa madarakani kwa miaka minne atakuwa na Makamu wa Rais wawili, Francis Amin kutoka Sudan Kusini na Esayas Jiro kutoka Ethiopia. Pia aliyekuwa Katibu Mkuu wa CECAFA, Nicholas Musonye amejiuzulu nafasi yake baada ya kuhudumu kwa miaka 20.
kitaifa
WANAWAKE wawili Mwajuma Hussein (23) mkazi wa kijiji cha Ikongolo wilayani Uyui na Mwanza Kushaha (34) mkazi wa kijiji cha Kombe kata ya Igagala wilayani Kaliua wameuawa na waume zao kutokana na wivu wa kimapenzi.Ametoa taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani Tabora, ACP Emmanuel Nley alisema Agosti 21, mwaka huu, majira ya saa 11.00 jioni kata ya Ikongolo wilayani Uyui Mwajuma aliuawa kwa kupigwa risasi na mume wake Saidi Ramadhani.Amesema mwanamke huyo alipigwa risasi idhaniwayo kuwa ya gobori huku taarifa za awali zikisema chanzo kikiwa ni wivu wa kimapenzi.Inadaiwa kuwa, mumewe baada ya kutenda unyama huo alikimbilia msituni na kujitundika juu ya mti na pembeni yake kukiwa na silaha ambayo katika uchunguzi ilibainika ndiyo iliyotumika kumuua mke.Kamanda Nley aliongeza kuwa tarehe hiyo hiyo majira ya saa 5:00 katika msitu wa Isawima kata ya Igagala wilayani Kaliua ulikutwa mwili wa Mwanza Kushaha ukiwa na majeraha kichwani na maeneo mengine ya mwili.Ameeleza kuwa uchunguzi wa Polisi ulibaini kuwa aliuawa na mumewe kwa wivu wa kimapenzi.Mume huyo Chuga Lutumbiga (46), mkazi wa Kaliua amekamatwa.Mtuhumiwa huyo alimuagiza mke wake kwenda kijiji cha Uganza kununua mahitaji na baada ya kuchelewa kurudi nyumbani alimfuatilia na kumkuta njiani akiwa anarudi, ndipo akaanza kumpiga.Aliongeza kuwa baada ya kipigo hicho alimwacha porini akiwa mtupu na kurudi nyumbani na kuanza kupiga kelele za kuomba msaada kwa majirani ya kumtafuta mke wake.Amesema, mtuhumiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya upelelezi zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
kitaifa
Na AZIZA MASOUD -DAR ES SALAAM OFISI ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA) imeiomba Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kutenga bajeti kukarabati mitambo na majengo yake ambayo yamechakaa. Akizungumza katika ghafla ya kutoa zawadi kwa walimu wanne na wanafunzi 18 waliohitimu na kufanyaa vizuri katika masomo ya Kemia na Biolojia kwenye mitihani ya taifa kidato cha nne 2015 na sita 2016, Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele, alisema moja ya changamoto inayoikabili ofisi hiyo ni uchakavu wa majengo ambayo yamejengwa tangu kipindi cha ukoloni. “Majengo yaliyopo mengi ni yale yaliyorithiwa kutoka ukoloni wa Kijerumani, zipo jitihada zinazoendelea za kurekebisha majengo haya, lakini kutokana na ufinyu wa bajeti zinafanyika kwa kasi ndogo,” alisema Profesa Manyele. Alisema wakala pia ina changamoto ya ukosefu wa vifaa na mitambo ya kisasa na upungufu wa rasilimali watu unaotokana na ufinyu wa bajeti. Aliongeza kuwa ufinyu wa bajeti unatokana na wakala kutopata ruzuku kutoka serikalini na kulazimika kutumia mapato yake ya ndani kutekeleza vipaumbele vinavyotolewa na wizara. Akizungumzia lengo la kutoa zawadi hizo, alisema ni kuleta hamasa kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sayansi nchini waweze kufikia malengo waliyojiwekea. Naye Mganga Mkuu wa Serikali, Profesa Mohammed Bakari, alisema mkakati wa wizara wa kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Afya ya Msingi (MMAM) hauna budi kwenda sambamba na kuongeza idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika vyuo vya afya na ustawi wa jamii. “Wizara inaendelea na juhudi za kuhamasisha vijana wetu kupenda masomo ya sayansi na hatimaye waweze kuongeza idadi ya wanaodahiliwa katika michepuo ya masomo ya sayansi,” alisema Dk. Bakari. Wanafunzi wa kidato cha nne waliopata zawadi ni Marynas Duduye na Julieth Zannie kutoka Sekondari ya St. Francis, David Joseph kutoka Ilboru na Asha Mlanzi wa Jangwani. Wanafunzi wa kidato cha sita waliofanya vizuri katika masomo hayo ni Sheikhas Rashid  wa shule ya Feza Wasichana, Prisca Kyando kutoka Kilakala na Gastory Munishi wa Mzumbe. Mbali na wanafunzi, walimu waliokabidhiwa zawadi ni Vaileth Kalangali na Frank Mella wa Ilboru, Habil Selemani wa Feza Wavulana na Joram Yohana wa Uwata.
kitaifa
Na Harrieth Mandari , Geita MWANAMKE mkazi  wa Kijiji cha Buligi, Kata ya Senga, Wilaya ya Geita mkoani hapa, Happyness Shadrack (36),  amedaiwa kufanya tukio la kinyama la kumuua kwa kumchinja mtoto wake wa kuzaa, Martha Yakobo mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi sita na kisha kumkatakata vipande na kumpika. Tukio hilo limetokea Juni 21, mwaka huu saa nane mchana.  Inadaiwa Happyness akiwa nyumbani kwa mama yake mzazi, Ruth Shadrack, alimchukua mtoto huyo aliyekuwa amelala kitandani na kumkatakata vipande vidogo vidogo na kisha kumweka ndani ya sufuria. Kwamba baada ya kumkatakata mtoto huyo, aliwasha jiko na kuweka sufuria kisha kuanza kupika kama kitoweo. Mtoto wa pili wa mwanamke huyo, Doris Yakobo, alisema alimuona mama yake akiwa anaweka sufuria jikoni na kuendelea kuchochea moto  lakini alipomuuliza alimjibu kuwa anachemsha maji na alipotaka kufunua kuangalia alimkataza. “Mimi ndiyo nilikuwa mara nyingi nakaa na kumwangalia mtoto (marehemu), na siku hiyo baada ya mtoto kusinzia nilimpeleka chumbani nikamlaza kitandani, mama naye alikuwa kwenye chumba hicho hicho akiwa amelala,” alisema Doris. Alisema baada ya kumlaza alitoka nje kwenda kulinda karanga  za bibi yake ili zisiibwe na kumwacha mama yake akiwa na mdogo wake wamelala. Doris alisema baada ya muda alimuona mama yake akitoka na kuanza kuwasha moto, huku mkononi akiwa na sufuria iliyofunikwa ambayo aliinjika jikoni na kuanza mapishi. Mwenyekiti wa Kitongoji cha Buligi, Manyoni Manyoni (CCM), alisema kuwa alipata taarifa za mauaji hayo akiwa kwenye kikao ofisini kwake. Manyoni alisema alifika mwendesha bodaboda ofisini hapo na kumtafuta askari ambaye naye alikuwa katika kikao hicho. Alisema mwendesha bodaboda huyo, alitoa taarifa kwa askari huyo kwamba kuna tukio la mama kumchinja mtoto wake. “Baada ya taarifa hiyo, wote tuliokuwa kikaoni tulipatwa na mshtuko na tulilazimika kusimama na kwenda kwenye eneo la tukio ambako tulikuta unyama huo wa mauaji ya mtoto huyo umeshafanyika na mwanamke huyo alikuwa ameshakamatwa na polisi kwa hatua zaidi za mahoajiano na uchunguzi wa tukio hilo,” alisema Manyoni. Ndugu wa mwanamke huyo, Amoni Mtani, alisema Happyness, amewahi kuathiriwa na ugonjwa wa malaria, hivyo anaamini kitendo hicho amekifanya kutokana na kutokuwa na akili ya kawaida. “Ndugu yangu Happyness (mtuhumiwa) alishawahi kuugua malaria kali sana sasa hatujui labda imeathiri akili hadi kufikia kutenda kitendo hiki cha kinyama, unachinja mtoto na kisha kumpika jamani jamani tumuogope Mungu wetu,” alisema Amoni. Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Dismas Kisusi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo pamoja na kushikiliwa kwa mtuhumiwa. “Ni kweli tukio hili limetokea Juni 21 na tayari Jeshi la Polisi tunamshikilia mwanamke huyo kwa uchunguzi zaidi. Na uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa mwanamke huyo ana historia ya kuwa na ugonjwa wa afya ya akili,” alisema Kamanda Kisusi Alisema uchunguzi utakapokamilika jalada la mtuhumiwa huyo litapelekwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ili aweze kulipitia kabla ya kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi za kisheria.
kitaifa
RAIS John Magufuli amekabidhi zaidi ya hati 1,000 kwa wakazi wa jiji la Mwanza na Manispaa ya Ilemela, baada ya kufanyiwa urasimishaji kwenye maeneo yao ambapo hati hizo zitawasaidia kupata mikopo kutoka katika taasisi za fedha na kujikomboa kiuchumi.Hati hizo zimekabidhiwa rasmi mwishoni mwa wiki kwa nyakati tofauti na Naibu Waziri wa Ardhi na Makazi, Dk Angeline Mabula kwa niaba ya Rais Magufuli kwenye hafla iliyofanyika katika Mtaa wa Mecco katika Kata ya Mecco Manispaa ya Ilemela na katika mtaa wa Nyangulugulu katika Kata ya Mahina katika Halmashauri ya jiji la Mwanza.Akikabidhi hati hizo kwa wananchi hao, Dk Mabula alisema rais amesikia vilio vya muda mrefu vya wananchi hao juu ya changamoto za ardhi zilizokuwa zinawakabili ikiwemo kuporwa viwanja vyao.Aliwataka wananchi waliokabidhiwa hati zenye umri wa miaka 99, kutosahau kulipa kodi ya serikali, ambayo ndiyo inaiwezesha serikali kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye maeneo yao ikiwemo miradi mikubwa ya kitaifa.Alizitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinapima maeneo yote ambayo hayapo kwenye mpango wa urasimishaji, kuwapatia wananchi leseni ya makazi itakayotozwa Sh 5,000 katika kipindi cha mpito cha miaka mitano na baadaye makazi yao yataingizwa kwenye mfumo rasmi wa urasimishaji makazi na kuwapatia hati za umiliki wa maeneo yao.Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza, Hosiana Kusiga alisema urasimishaji katika jiji la Mwanza umefanyika na kufanikiwa kwa kiwango kikubwa, ambapo jumla ya viwanja 19,635 vimepimwa ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli la kuondokana na ujenzi kwenye makazi holela katika halmashauri hiyo.Amesema halmashauri yake ilikuwa na lengo la kupima jumla ya viwanja 24,000 kupitia mradi huo wa urasimishaji makazi, ambapo viwanja 25,766 ikiwa ni sawa na asilimia 107.3 vimepimwa katika kata za Buhongwa, Mkolani, Igoma, Mhandu, Luchelele, Mahina, Isamilo, Kishiri na Nyegezi.Kusiga aliongeza kuwa kazi ya upimaji wa viwanja bado inaendelea katika kata za Butimba, Mahina, Kishiri na Luchelele, ambapo jumla ya viwanja 19,635 upimaji wake umekamilika ikiwa ni sawa na asilimia 80.
kitaifa
SHIRIKA la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR) lipo tayari kuingia kwenye mjadala na serikali kuangalia njia mbadala za kuwasaidia wakimbizi wanaohudumiwa hapa nchiniPia limeahidi kufuatilia kila aina ya mavazi yanayoingizwa nchini kuwasaidia wakimbizi ili kuhakikisha hayaingii mavazi yanayofanana na sare za wanajeshi kama ilivyotokea karibuni na kuleta mtafaruku.Akizungumza na waandishi wa habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa UNHCR, Fillippo Grandi alisema Tanzania imekuwa ikisaidia wakimbizi kwa miaka mingi na kuna changamoto ambazo UNHCR imebaini na kuwa zinahitajia mjadala wa pamoja na serikali ili kuwasaidia wakimbizi waliopo nchini.Alizibainisha changamoto hizo kuwa ni pamoja na njia bora za kuwahudumia wakimbizi ambapo alisema kuwa wakimbizi sio lazima wakae kambini tu kama ilivyo ila wanaweza kufanya shughuli za kiuchumi. Alitolea mfano kwenye kambi ya Nyarugusu ambapo awali kulikuwa na soko lililokuwa likitumiwa na wakimbizi hao pamoja na wananchi wa eneo jirani kuuzia na kununua mazao kama njia mojawapo ya wakimbizi kujipatia kipato na kuwa kutokana na kufungwa kwa soko hilo baadhi yao sasa wameathirika.Pia alisema kwenye mfumo wa kuwapokea wakimbizi kuna changamoto za baadhi kukataliwa kuingia nchini wakati wengine ni wagonjwa. Alisema kuna haja ya kuwapokea kwanza wote wanaoomba kuingia. Aliongeza kuwa licha ya Tanzania kufanya kazi kubwa ya kuwapokea wakimbizi hao nchini na kuwasaidia kwa kila hali, imeonekana bado kuna changamoto ambazo UNHCR na wadau wengine wanalo jukumu la kusaidiana na Tanzania kuzitatua hasa kwenye sekta ya elimu, afya na maji. “Tanzania inakabiliwa na changamoto kadhaa katika namna ya kuwapokea na kuwarejesha majumbani kwao wakimbizi.Sina maana ya kuwa haifanyi kazi nzuri ila ninachomaanisha kuwa kuwa kuna haja ya kuwa na mjadalana Serikali tena shirikishi kubainisha sababu za changamoto hizo na kuzitatua,” alisema. Pia alisema suala la wakimbizi kurejea makwao linatakiwa kuwa ni la hiari zaidi na sio lazima au mkimbizi kuwekewa mazingira yoyote ya kuwalazimisha wakimbizi kurejea kwenye nchi waliyotoka.Aliongeza kuwa nchi ambazo wakimbizi wanarejea makwao pia zinapaswa kuandaa mazingira rafiki ya kiuchumi kwa wakimbizi ambayo yatawawezesha kuendeleza shughuli za kiuchumi kwa muda mrefu. Kuhusiana na mavazi yanayofanana na sare za jeshi yaliyokamatwa kambi ya wakimbizi Kigoma, Grandi alibainisha, sio lengo la UNHCR kuziingiza nchini na kuwa zilitokana na misaada ya watu mbalimbali. Alisema kuna nchi ambazo mavazi ya aina hiyo ni kitu cha kawaida na ndio walisaidia kuyaingiza nchini.Hata hivyo, alikiri k hilo ni kosa kwa kuwa haitakiwi mavazi yenye kuendana na sare za kijeshi kupewa wakimbizi kwani haitakiwi kujihusisha na shughuli za kijeshi hivyo hata mavazi yanayofanana sio mazuri. Mkuu huyo wa UNHCR alipongeza juhudi za Rais Mstaafu wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa za kupigania amani nchini Burundi na kutoa mwito kwa nchi za Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) kupigania amani kwenye nchi zao ili wakimbizi waliotoka huko warejee nchini mwao.“Nimekutana na Rais John Magufuli, Waziri wa Mambo ya Nje, Augustine Mahiga na mawaziri wengine wanaohusika moja kwa moja na kuhudumia wakimbizi na nimefanya majadiliano yenye tija kubwa kwa faida ya wakimbizi. Ninaishukuru Tanzania kwa msaada wao mkubwa kwa wakimbizi hawa, “alisema. Grandi aliwasili nchini Jumanne wiki hii na kufanya mazungumzo na Rais Magufuli, Ikulu, Dar es Salaam ambapo alimwomba radhi kwa kupatikana kwa sare za jeshi kwenye kambi ya wakimbizi ya Kigoma.
kitaifa
Taarifa ya Ofisa habari wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kwa vyombo vya habari jana, Alfred Lucas ilisema Mkude analazimika kubaki kutokana na ushauri wa Daktari aliyemtaka kupumzika kutokana na majeraha aliyoyapata katika ajali juzi.Nahodha wa Simba, Mkude alikuwa miongoni mwa abiria sita waliopata ajali wakitokea Dodoma kwenye mechi ya fainali ya kombe la FA kati ya Simba na Mbao juzi ambapo shabiki mmoja wa Simba Shose ‘Wazza’ Fidelis alifariki dunia.Simba ilishinda mabao 2-1. Stars inakwenda Misri kwa ajili ya kambi ya wiki moja kujiandaa na mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (Afcon) dhidi ya Lesotho Juni 10, mwaka huu kwenye uwanja wa Taifa, Dare s Salaam.“Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga ameridhia Mkude kubaki na kusema kuwa ataungana na wenzake Juni 8 mwaka huu timu itakaporejea kutoka Misri. Mayanga hajajaza nafasi ya Mkude,” alisema.Aidha, Mkude aliliambia gazeti hili jana muda mfupi baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa akipatiwa matibabu tangu juzi usiku kwamba ana majeraha kidogo shingoni lakini anaendelea vizuri.“Nashukuru Mungu naendelea vizuri, daktari aliniambia sina tatizo kubwa ni mshtuko wa ajali na kwamba naweza kuendelea na ratiba zangu ndio maana nilikwenda kambini kuungana na wenzangu,” alisema.Lucas alisema wachezaji wanaocheza soka la kulipwa nje ya Tanzania Nahodha Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu na Faridi Mussa wataungana na wenzao moja kwa moja katika kambi ya Misri.Katika mechi hizo za kufuzu, Tanzania imepangwa kundi L pamoja na Lesotho, Uganda na Cape Verde . Kikosi cha Taifa Stars kinaundwa na makipa Aishi Manula (Azam FC), Benno Kakolanya (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar).Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Kapombe (Azam FC) na Hassan Kessy (Yanga SC) wakati upande wa kushoto wapo Mohammed Hussein (Simba) na Haji Mwinyi (Yanga SC).Walinzi wa kati Erasto Nyoni (Azam FC), Salim Mbonde (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Agrey Morris (Azam FC) ilihali viungo wa kuzuia ni Himid Mao (Azam FC) na Jonas Mkude kutoka Simba SC ambaye hatasafiri na timu kwa sasa.Viungo wa kushambulia ni Salum Abubakar (Azam FC), Said Ndemla (Simba SC) na Mzamiru Yassin (Simba) wakati viungo wa pembeni ni Simon Msuva (Yanga SC), Shizza Kichuya (Simba SC) na Farid Mussa (Teneriffe, Hispania).Washambuliaji wapo Mbwana Samatta (KRC Genk- Ubelgiji), Thomas Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Ibrahim Ajib (Simba SC), Mbaraka Yusufu (Kagera Sugar) na Abdurahman Mussa (Ruvu Shooting). Wasaidizi wa Mayanga katika benchi la ufundi ni Novatus Fulgence ambaye ni kocha msaidizi Patrick Mwangata - kocha wa makipa, meneja wa timu, Danny Msangi, mtunza vifaa Ally Ruvu, Daktari wa timu Richard Yomba na Daktari wa viungo Gilbert Kigadya.
michezo
WADAU wa maendeleo na wahisani wanaosaidia miradi ya afya nchini wamepongeza maboresho makubwa yaliyofanywa na serikali nchini katika kuimarisha utoaji huduma, upatikanaji wa vifaa na dawa za kutosha hali inayochangia kupunguza vifo ikiwemo vifo vya wanawake wajawazito na watoto.Kauli hiyo ya wadau wa maendeleo imetolewa mjini Kigoma wakati wa hafla ya kufungwa kwa mradi wa miaka 13 wa afya ua uzazi, mama na mtoto uliokuwa ukilenga kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wakati wa kujifungua ambapo mradi huo umesaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha huduma za afya mkoani humo na kuwezesha kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto.Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Engender Health Tanzania, Prudence Masako alisema kuwa pamoja na uboreshaji wa maeneo ya utoaji huduma uliofanywa kwa pamoja baina ya serikali na wadau, uhakika wa upatikanaji wa madawa na vifaa tiba lakini uboreshaji wa miundo mbinu ya barabara umekuwa na mchango mkubwa katika kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto mkoani Kigoma.Masako alisema kuwa dhana ya ujenzi wa uboreshaji wa vituo vya afya maeneo ya mbali na hospitali za wilaya na mkoa inatokana na miundo mbinu duni ambapo mama wajawazito na watoto walikuwa wakifia njiani hali ambayo kwa sasa ni tofauti ambapo mgonjwa anayehitaji rufaa anaweza kusafirishwa kwa haraka kwenda hospitali ya wilaya na mkoa kwa matibabu ya kitaalam zaidi.Mratibu wa Shirika la Bloomberg Philanthropies, ambao ndiyo wafadhili wa mradi huo, Dk Godson Maro alisema kuwa mradi umekuwa na mafanikio makubwa na hiyo inatokana na ushirikiano mkubwa ambao serikali imetoa katika utekelezaji wake kuanzia ngazi za zahanati hadi kwa waziri wa afya ambaye amesaidia sana mradi kutekelezwa hadi kufikia mafanikio yaliyopo sasa.Dk Maro alisema kuwa katika utekelezaji wa mradi huo kwa miaka 13 mkoani Kigoma jumla ya vituo vya utoaji huduma 100 vimeboreshwa kwa majengo, uwekaji wa vifaa tiba na elimu kwa watoa huduma 400 ambapo takwimu hizo zinaonyesha kuwa jumla ya vituo afya 13 vimepandishwa hadhi na kuweza kutoa huduma za dharula za upasuaji kwa mama wajawazito.Mratibu wa Miradi ya Afya ya Uzazi kutoka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk Hamad Makuwani alisema kuwa utekelezaji wa mradi huo umekuwa na mafanikio makubwa na kuwa serikali imetekeleza ujenzi wa vyumba vya upasuaji wa dharula kwenye vituo vya afya nchi nzima lengo ikiwa kusaidia kuokoa vifo vya wanawake na watoto wakati wa kujifungua.
kitaifa
WAWAKILISHI pekee wa Tanzania katika mashindano ya kimataifa, Yanga wamewataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia timu yao ‘ikipindua meza kibabe’ wakati wakirudiana na Gor Mahia ya Kenya katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la Afrika hatua ya makundi.Yanga ambao wanashika mkia katika Kundi D wakiwa na pointi moja tu, wanaikaribisha Gor Mahia iliyopo katika nafasi ya pili katika msimamo huo, mchezo utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo katika mitaa ya Twiga na Jangwani, msemaji wa Yanga, Dismas Ten alisema kuwa timu yao itashinda baada ya kufungwa 4-0 katika mchezo wa mwanzo.Mbali na kutamba kulipa kisasi, Yanga pia ilitangaza viingilio vya mchezo huo, ambavyo ni Sh 10,000 kwa VIP A wakati VIP B na C ni Sh 7,000 huku mzunguko ni Sh 3,000.Aliwataka wapenzi wa soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia mchezo huo, ambao umepangwa kuanza saa 1:00 usiku kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Tayari Yanga katika mechi tatu ilizocheza hadi sasa za Kombe la Shirikisho imefungwa mabao manane baada ya kufungwa 4-0 na kutoka suluhu na Rayon Sports ya Rwanda.Yanga iliangukia katika Kombe la Shirikisho baada ya kutolewa katika raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa wa Afrika katika.
michezo
NA THERESIA GASPER, DAR ES SALAAM KOCHA wa timu ya Simba, Jackson Mayanja, amewafunda wachezaji wa Tanzania na kuwataka kujituma wanapokuwa uwanjani ili wapate soko la kimataifa na kufikia hatua kama ya Mbwana Samatta, anayechezea klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji. Kocha huyo raia wa Uganda alisema hayo mara baada ya kushuhudia mchezo wao uliopita  dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo wachezaji wa timu pinzani walikuwa wakitumia muda mwingi kulinda lango lao na kushindwa kupambana ili kupata mabao. Akizungumza jana mara baada ya kumalizika kwa mazoezi yaliyokuwa yanafanyika katika Uwanja wa TCC Chang’ombe jijini hapa, Mayanja alisema ni vema mchezaji akaonyesha kiwango chake vizuri pindi anapopata nafasi ya kucheza ili aweze kujitangaza zaidi. “Wachezaji wanatakiwa kubadilika na kuangalia zaidi mbele ili wafanikiwe kama wenzao ambao wanacheza soka la nje, mfano mzuri ni Samatta ambaye kwa sasa anaendelea kuipaisha Tanzania Ulaya, hivyo wanatakiwa kufahamu wanapocheza  watu wengi wanawaangalia huo ndio mwanzo wa kuvitangaza vipaji vyao,” alisema. Akizungumzia mchezo unaowakabili dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Jumamosi hii Uwanja wa Mkwakwani, Tanga kocha huyo alisema wanataka kuvunja mwiko kwa kuamini kuwa timu kubwa lazima zifungwe na timu hiyo wanapokutana katika uwanja wao. Alisema mpira wa sasa hauna desturi ya kufungwa ugenini, isipokuwa kila mtu anakuwa na mipango yake itakayomfanikisha kupata ushindi, kitu ambacho wao wamejiwekea ili kupata pointi tatu muhimu ili waendelee kupeta kileleni mwa Ligi Kuu Tanzania Bara. “Tunatarajia kuondoka Alhamisi au Ijumaa kuelekea Tanga, ila kwa sasa kikosi kipo vizuri tunaendelea na mazoezi kwa ajili ya kupambana katika mchezo huo na majeruhi wanaendelea kuimarika,” alisema.
michezo
KAIMU Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN), Tuma Abdallah amesema hivi sasa mitandao ya kijamii ya kampuni hiyo inatembelewa na takribani Watanzania 1,500,000.Tuma ametoa maelezo hayo kwa washiriki takribani 400 walioishriki kwenye Jukwa la Biashara mkoani Geita mwishoni mwa wiki, hivyo kuwataka kufanya kazi na taasisi hiyo.Ameitaja mitandao hiyo kuwa ni DailyNews digital ambayo huendesha mtandao wa Youtube, Twitter, Facebook, Instagram na pia habari kupitia tovuti yake. TSN pia huchapisha magazeti ya HabariLeo, Daily News na SpotiLeo.Tuma ametoa mwito kwa Watanzania kutumia vyombo vya TSN ambavyo amesema haviripoti mambo ya kuzua isipokuwa kuandika ukweli kwa ajili ya maendeleo ya nchi yetu.Amesema kutokana na mapinduzi ambayo TSN imekuwa ikifanya, kwa sasa mbali na habari pia hutengeneza makala za video (documentaries) na kwamba tayari mashirika kadhaa yamefaidika na kazi hizo ikiwemo Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).Pia amesema TSN inafanya kazi ya kutafsiri, hususani kutoka Kiswahili kwenda Kingereza au kutoka Kingereza kwenda Kiswahili pamoja na uchapishaji wa vitabu na mabango.Kuhusu Jukwaa la Biashara, aliwataka wananchi wa Geita kufanyia kazi yote yaliyojitokeza kwenye jukwaa hilo.Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk Jim Yonazi, aliushukuru Mkoa wa Geita hususani Mkuu wa Mkoa huo, Robert Gabriel, kwa namna ulivyolipokea Jukwaa hilo.Dk Yonazi ambaye alikuwa Mhariri Mtendaji wa TSN kabla ya hivi karibuni kuteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu, ameipongeza pia idadi ya watu waliojitokeza kwenye jukwaa hilo jana hadi watu wengine kukosa viti.“Mwitikio huu unaonesha kuwa wana-Geita tuko tayari kupokea mabadiliko,” amesema.Dk Yonazi ambaye ndio mwanzilishi wa Majukwaa ya Fursa za Biashara, alishukuru taasisi kadhaa zilizojitokeza kudhamini jukwaa hilo.“Wengi wametupokea na kuwa tayari kufanya kazi na sisi katika kufanikisha majukwaa haya toka tumeanza,” amesema Dk Yonazi na kutaja baadhi ya taasisi hizo ambazo zilikuwepo jukwaa hilo la Geita ni GGM, NBC, CRDB, TIRA, TRA, TCRA, TBC, Busowala Mining, TAGB (Benki ya Kilimo), Waja General, Rex Energy, ATCL na SSRA.
kitaifa
Akizungumza na gazeti hili, baada ya mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Taifa, Mkwasa alisema kikosi chake kipo tayari kutetea bendera ya Taifa, kwani wameshafanyia kazi upunguzo waliouona katika mchezo wa kwanza.“Timu ipo vizuri na wachezaji wote wapo isipokuwa Mbwana Samatta ambaye anatarajiwa kuwasili kesho (jana) kuungana na wenzake na kama ulivyoona morali ipo juu, nina uhakika wa kushinda ili kujiweka nafasi nzuri,” alisema Mkwasa.Mshambuliaji Thomas Ulimwengu anayecheza TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ni miongoni mwa wachezaji ambao walikuwepo mazoezini juzi. Katika mazoezi hayo, Mkwasa alionekana kutilia mkazo zaidi safu ya ushambuliaji akiwasimamia Elias Maguli, Ulimwengu na John Bocco.Mchezo huo wa kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani kutoka Kundi G unatarajiwa kuwa na ushindani, kwani Misri wana pointi saba na Taifa Stars ina pointi moja.Misri utakuwa mchezo wao wa mwisho, wakati Taifa Stars baada ya mchezo huo itabakisha mchezo mmoja ugenini dhidi ya Nigeria. Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), mchezo wa Jumamosi utachezeshwa na mwamuzi Meya Bastred akisaidiana na Mihndou Gauthar na Vinga Theophil na mwamuzi wa mezani ni Oboga Eric wote kutoka, Gabon.Katika kundi hilo, Misri ndiyo wanaongoza wakiwa na pointi saba wakifuatiwa na Nigeria wenye pointi mbili Tanzania na Tanzania ya tatu ikiwa na pointi moja. Kundi lina timu tatu tu baada ya Chad kujitoa. Wakati huo huo, msafara wa watu 60 wakiwemo wachezaji, viongozi na mashabiki wa Misri uliwasili Dar es Salaam jana tayari kwa mchezo huo.
michezo
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Katibu Mtendaji wa Basata, Godfrey Mngereza, alisema kabla ya kufanya uchaguzi huo mashirikisho hayo yanatakiwa kulipa ada zao ili kuwa hai kwa ajili ya uchaguzi huo.“Ieleweke kwamba hakuna chama au shirikisho litakaloruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi bila kuwa hai kwa maana ya kulipa ada zote kama zinavyoelekezwa,”alisema.Mngereza alisema uchaguzi ufanyike mara moja kabla ya Februari mwaka huu viongozi wapya wawe wamekwishapatikana.Pia, alizungumzia umuhimu wa wasanii kuhakikisha wamesajiliwa, kuwa na vibali vya kufanya kazi za sanaa na kushiriki kikamilifu kujenga mfumo wa utawala katika sekta ya sanaa utakaokuwa unatumika kama mfumo sahihi na rasmi wa mawasiliano baina ya serikali na wasanii.Alisema kutokana na huko nyuma serikali kupata ugumu wa kuwasiliana na msanii mmoja mmoja, wanahamasisha umuhimu wa kuanzishwa vyama na mashirikisho ya wasanii na kuwalekeza kujiunga katika umoja huo kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa sekta hiyo.Alitaja mashirikisho baadhi yaliyoundwa kuwa ni shirikisho la wasanii wa muziki, ufundi, maonesho na filamu.“Mashirikisho yote haya yanajumuisha tanzu zote za sanaa na yanaundwa na vyama wanachama ambavyo kimsingi vinaundwa na vikundi vya wasanii na mmoja mmoja kulingana na fani husika,” alisema.Alisema licha ya kuwa wasanii huhamasika kuunda mashirikisho hayo, bado idadi kubwa ya wasanii hasa wenye majina makubwa wameendelea kuwa nje ya mfumo huo wa utawala katika sekta ya sanaa hali ambayo sio tu imeyafanya maslahi yao kukosa sauti ya pamoja bali pia kudhoofisha juhudi.
michezo
MBUNGE wa Kwanza wa Jimbo la Kondoa Kusini (1985 -1990) Shaban Muyombo, amesema serikali inakwenda kutekeleza mradi mkubwa wa Bwawa la Farkwa ambayo ilikuwa ni ndoto ya Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.Akizungumza jana wakati wa mahojiano na gazeti hili, Muyombo alisema sasa, ndoto hiyo inatimia baada ya serikali kutoa fedha za kulipa wananchi ili kupisha ujenzi wa bwawa hilo.Alisema wazo hilo lilitolewa kabla ya uhuru na liko kwenye mpango wa mji wa Dodoma kuwa maji yatatoka katika chanzo cha Mzakwe na bwawa la Farkwa.“Tunafurahi kuona kuwa ndoto za Mwalimu zinakwenda kutekelezwa kwenye serikali ya awamu ya tano baada ya serikali kuwa na vyanzo vingi vya mapato pamoja na Rais mwenye nia ya kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo,” alisema.Alisema vijiji vya Bubutole na Mombose vinapitiwa na mto bubu ambao unaanzia milima ya Hanang mkoa wa manyara na sasa utamwaga maji bwawa la Farkwa. Alisema miaka ya 1974 wachina walifanya mradi wa visima katika kijiji cha Jogolo kwa kutoboa maji ambayo yanatumiwa na wananchi na uwepo wa mradi wa ujenzi wa bwawa la Farkwa utasaidia sana upatikanaji maji katika wilaya za mji wa Dodoma, Serikali imetenga kiasi cha Sh bilioni 7.8 kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi wa vijiji vya Mombose na Bubutole wilaya ya Chemba mkoani Dodoma ili wapishe ujenzi wa bwawa hilo.Wananchi zaidi ya 2,868 wataanza kulipwa kuanzia Oktoba 15 hadi 31 mwaka huu. Bwawa hilo linatarajia kumeza vijiji viwili. Hivi karibuni Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Profesa Kitilya Mkumbo alitoa mwito wa serikali kwa wananchi hao baada ya kulipwa fedha hizo wapishe maeneo hayo.“Viongozi lazima mkawaeleze wananchi ukweli wakishalipwa lazima wapishe eneo, tukishakulipa uondoke ili kazi ya ujenzi ianze,” alisema.Alisema bwawa hilo baada ya kukamilika litakuwa likisambaza maji katika Jiji la Dodoma na wilaya za Chamwino, Bahi na Chemba. Profesa Kitilya alisema mradi huo upo kwenye vitabu vya bajeti na upo katika kipaumbele cha juu na serikali inaendelea kufuatilia fedha za ujenzi na kujenga miradi mingine. Alisema bwawa hilo litakuwa ni fursa kwa wananchi na litaleta fursa nyingi za kiuchumi na kijamii.
kitaifa
LISBON, URENO MSHAMBULIAJI wa Juventus, Cristiano Ronaldo, amewatoa wasiwasi mashabiki wa timu hiyo baada ya kuumia mapema wiki hii akiitumikia timu ya taifa Ureno kwenye michuano ya kuwania kufuzu Euro 2020. Katika mchezo huo, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, lakini mchezaji huyo hakumaliza dakika 90 kutokana na kuumia nyama za paja na kuwaweka wasiwasi mashabiki wa Juventus kuelekea michezo yao mbalimbali ya Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa. Hata hivyo, mchezaji huyo amedai kwamba, japokuwa alitolewa kwenye mchezo huo, lakini hana tatizo kubwa la kutisha na kumfanya awe nje ya uwanja kwa kipindi kirefu. “Sina wasiwasi kwa kuwa ninaujua vizuri mwili wangu, haya yanatokea kwenye soka, hivyo ninaamini ninaweza kuwa nje ya uwanja kwa wiki moja au mbili, nitakuwa imara. “Najua mashabiki wana hofu, lakini nataka kuwatoa wasiwasi kwamba nitarudi viwanjani siku za hivi karibuni,” alisema mshambuliaji huyo. Ronaldo amekuwa na mchango mkubwa ndani ya Juventus tangu alipojiunga na timu hiyo akitokea Real Madrid mwishoni mwa msimu uliopita. Mchango wake umeifanya Juventus kuingia hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwaondoa Atletico Madrid. Mchezo wa kwanza Atletico Madrid walifanikiwa kushinda mabao 2-0, huku mchezo wa mwisho wa marudiano Ronaldo aliifungia Juventus mabao matatu katika ushindi wa 3-0 na kuifanya timu hiyo kufuzu, ambapo inatarajia kukutana na Ajax, Aprili 10, mwaka huu. Endapo hali ya mchezaji huyo itakuwa bado haiko sawa ndani ya wiki mbili, basi ataukosa mchezo huo wa kwanza wa robo fainali dhidi ya Ajax. Timu hiyo ya Ajax imefanikiwa kuingia hatua hiyo baada ya kuwaondoa wababe wa michuano hiyo Real Madrid, hivyo timu hiyo inaonekana kuwa tishio kubwa msimu huu.
michezo
KATIKA simulizi nilizowahi kuzisikia kuhusu maeneo ya Mkoa wa Dar es Salaam ni kuhusu eneo la Gongo la Mboto. Simulizi hii nilisimuliwa na jirani yangu zamani kwenye miaka ya 1998 alipokuwa akinielezea asili ya maeneo kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam na mengine ya mikoa kadhaa. Wakati huo, nilikuwa makini zaidi kwa Mkoa wa Dar es Salaam labda kwa sababu naishi hapa na nayafahamu. Miongoni mwa maeneo hayo ni Gongo la Mboto ambapo nilielezwa kuwa asili ya jina hilo ni mkulima mmoja aliyekuwa maarufu akiitwa Mboto. Alikuwa na tabia ya kutembea na gongo. Siku moja wakati alipokwenda shambani kwake kulima, hakurudi nyumbani nyakati za jioni kama kawaida yake.Ilipofika siku ya pili hakurudi nyumbani hadi mchana, taarifa ikatolewa, watu wakakusanyika kumtafuta.Hali ikawa ngumu kidogo kwa sababu wakati ule kwenye maeneo hayo kulikuwa hakujachangamka yaani hakuna makazi kama sasa, mapori na vichaka vilikuwa vingi na kuleta hali ya giza. Msako ule ulifanyika siku kadhaa na baadaye walikuta nyayo za mnyama mkubwa ambaye hakufahamika ni mnyama gani zaidi ya kuhisi labda chui au simba na kwa kuangalia vichaka, wakabaini kulitokea purukushani fulani hivi. Aidha,walikuta gongo la Mzee Mboto ambalo siku zote hutembea nalo. Kutokana na ishara hizo na kupatikana kwa hilo gongo, wakahisi Mzee Mboto ameshafariki dunia na atakuwa ameliwa na mnyama mkali na mkubwa. Tangu siku hiyo eneo hilo likaitwa Gongo la Mboto na mwili wa Mzee Mboto haukuwahi kuonekana hadi leo. Hiyo, ndiyo sababu ya eneo hilo kuitwa Gongolamboto Imeandikwa na MAULID AHMED
kitaifa
Na MOHAMED KASSARA -DAR ES SALAAM KOCHA wa timu ya Taifa Tanzania, ‘Taifa Stars’  Etienne Ndayiragije amesema  hakuna kikwazo kitakachokizuia kikosi chake hicho kuibuka na ushindi kitakaposhuka dimbani leo kuumana na  Burundi ( Intamba m’Urugamba), katika mchezo wa marudiano kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwaka 2022 nchini Qatar. Pambano hilo linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa  litapigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mchezo wa kwanza kati ya timu hizo ulipigwa kati kati ya wiki hii jijini Bujumbura, ambapo Stars ililazimisha sare ya bao 1-1. Ili kusonga mbele hatua ya makundi, Stars italazimisha kusaka sare ya aina yoyote au ushindi, huku wapinzani wao Burundi wakihitaji ushindi pekee ili kupiga hatua nyingine mbele. Faida iliyonayo Stars kuelekea mchezo huo ni akiba ya bao moja la ugenini ililolipata katika mchezo wa kwanza nchini Burundi. Kikosi hicho cha Stars kitashuka kuikabili Burundi kikijiamini kutokana na rekodi nzuri inapokutana na timu hiyo nyumbani. Katika michezo mitano ya mwisho ya timu hizo katika ardhi ya Tanzania, Stars imeshinda mitatu, sare moja na kupoteza mmoja. Hata hivyo, rekodi za jumla pia zinaibeba Stars inapokuana na Burundi. Kwa ujumla timu hizo zimekutana mara 19, Stars imeshinda  11, sare tatu na kupoteza mitano. Mara ya mwisho zilikutana Machi 28, 2017. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Taifa na Stars kushinda mabao 2-1. Ushindi wa  mwisho wa Burundi dhidi ya Stars iliupata Novemba 28, mwaka 2012. Katika mchezo huo  wa michuano ya Chalenji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa), Burundi ilitakata kwa bao 1-0. Kocha Mkuu wa Stars, Etienne Ndayiragije akizungungumzia maandalizi ya kikosi chake alisema wamejiandaa kiasi cha kutosha kwa ajili ya kuhakikisha wanapata ushindi na kusonga mbele. Alisema imani aliyonayo inatokana na sehemu kubwa ya kazi waliifanya ugenini hivyo leo watamalizia ungwe iliyobaki kwa kuibuka na ushindi. “Mchezo wa marudiano utakuwa wa kufa au kupona kwa sababu ndio utakaamua mustakabali wetu, lazima tutumie vema uwanja wetu wa nyumbani  kupata matokeo mazuri na kusonga mbele. “Kasoro tulizoziaona katika mchezo wa kwanza tumezirekebisha, lakini hata yale mazuri tuliyoana pia tumeyaboresha zaidi mazoezini, vijana wameahidi kukata kiu ya Watanzania kwa kupata ushindi, kikubwa mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kutupa sapoti,” alisema Mgunda. Mshambuliaji wa timu hiyo, Simon Msuva ambaye alifunga bao la kusawazisha la Stars kule Burundi alisema kwa upande wao wa wachezaji wamejiandaa kupeperusha vyema bendera ya Tanzania. “Tunashukuru tulikuwa na mchezo mzuri ugenini, tumerudi nyumbani kwa ajili ya kumaliza kazi, sisi kama wachezaji tuko tayari kujitoa kwa hali yeyote, Huu ni mchezo muhimu kwa Watanzania wote hivyo ni muhimu kuwa na mshikamano ili tufanikishe lengo kwa pamoja,” alisema Msuva. Naye mshambuliaji Adi Yussuf alisema baada ya kuanza vizuri ugenini watahakikisha wanamaliza kazi nyumbani.  “ Tulicheza vizuri mchezo wa kwanza ugenini, wachezaji walijituma , tunakila sababu ya kushinda kwani tutakuwa nyumbani huku tukipata sapoti ya Watanzania wenzetu,” alisema mshambuliaji wa  Blackpool ya Ligi Daraja la Kwanza England.
michezo
    ELIZABETH HOMBO NA HARRIETH MANDARI, DAR ES SALAAM RAIS Dk. John Magufuli amemwomba Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma kumsaidia namna ya kuzungumza na Umoja wa Nchi tano zinazochipukia katika uchumi (Brics), ili apate mkopo wa riba nafuu utakaosaidia kujenga reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge). Pia amesema wamekubaliana na Rais Zuma kuwa atapeleka walimu wa Tanzania kwenda Afrika Kusini kufundisha   Kiswahili. Rais Magufuli alitoa kauli hiyo Ikulu   Dar es Salaam jana wakati wa hafla ya kutia saini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini. Rais Zuma ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku mbili, kabla ya kutiliana saini hizo,  aliteta na Rais Magufuli kwa saa takribani mbili.   Hati hizo ni pamoja na muhtasari wa makubaliano ya mkutano wa tume ya pamoja ya marais, makubaliano ya ushirikiano katika masuala ya bioanuwai na uhifadhi na makubaliano ya ushirikiano katika sekta ya uchukuzi. Viongozi hao pia walizindua rasmi Tume ya Pamoja ya Marais (Bi- National Commission- BNC), kwa kufanya kikao cha kwanza cha tume hiyo tangu ianzishwe mwaka 2011, huku wakipokea makubaliano yaliyofikiwa katika kikao cha tume ngazi ya mawaziri. Akizungumza baada ya utiaji saini huo, Rais Magufuli alisema katika mazungumzo yake na Rais Zuma, alimweleza kuhusu ujenzi wa reli ya kati, mradi wa Liganga na Mchuchuma na kuwataka wafanyabiashara wa nchi hiyo   kuwekeza nchini.  “Nimemuarifu Rais Zuma kuhusu miundombinu ikiwa ni pamoja na ujenzi wa reli ya kati kwa kiwango cha kisasa (Standard Gauge), mradi wa Liganga na Mchuchuma na nimewakaribisha wawekezaji kutoka Afrika Kusini. “Nimemwomba kupitia zile nchi zenye utajiri unaoinukia, Brazil, Urusi, India, China na Afrika Kusini kutusaidia kupata mkopo wa riba nafuu utakaotusaidia kujenga Standard Gauge. Najua yeye hatashindwa akitia neno. “Pia tumekubaliana  na Rais Zuma kuwa  Tanzania itapeleka walimu wa   Kiswahili ambacho kinazungumzwa na watu takribani milioni 120 duniani   wakafundishe lugha hiyo katika vyuo vya nchi hiyo,”alisema Rais Magufuli. Alisema kwa kuwa Tanzania imefanya mengi katika ukombozi wa nchi hiyo, hivyo waifikirie namna ya kuisaidia. Alisema hivi sasa biashara kati ya Tanzania na Afrika Kusini kwa mwaka ni Sh trilioni 2.4, uwekezaji wa Afrika Kusini   nchini ni Dola za Marekani milioni 803.15 uliozalisha ajira 20,916 na kwamba kiwango hicho kinaweza kuongezeka. Pia alimshukuru Rais huyo wa Afrika Kusini kwa mchango wa madawati 1000 yaliyotolewa na Serikali ya nchi hiyo wakati wa kampeni za kuchangia madawati. Rais Zuma Naye  Rais Zuma  alitoa pole kwa Watanzania kuhusiana na ajali iliyosababisha vifo vya wanafunzi 32 wa Shule ya Lucky Vicent, walimu wawili na dereva wa basi mkoani Arusha. “Napenda kutoa pole kwa vifo vya watoto iliyotokana na ajali huko Arusha. Tunaungana na Watanzania kuwalilia hawa watoto ambao wamepoteza maisha yao wakiwa wadogo,”alisema Rais Zuma. Rais Zuma ambaye alifuatana  na mawaziri sita   na wafanyabiashara zaidi ya 80 wa nchi hiyo, alimpongeza Rais Magufuli kwa kuanza ujenzi wa reli ya kati huku akiahidi kuunga mkono juhudi hizo. Alisema anatambua kuwa ujenzi wa reli ya kati utaleta manufaa makubwa kwa Tanzania na nchi za Maziwa Makuu hivyo atahamasisha wafanyabiashara na wawekezaji wa nchi yake kushirikiana kufanikisha mradi huo.  “Pia nimefurahi tumekumbuka tulikotoka katika uhusiano wetu, nimekumbuka Mazimbu mkoani Morogoro hatuwezi kusahau pia Dakawa. “Jana nilipofika wakati natambulishwa viongozi, mmoja akasema katokea Kinondoni nikasema kanikumbusha mbali,”alisema Rais Zuma. Rais  Zuma alimwalika Rais Magufuli kufanya ziara nchini humo   kuendelea kuimarisha uhusiano wa nchi hizo mbili. WAFANYABIASHARA A. KUSINI Wafanyabiashara kutoka  Afrika   Kusini wamesema wamewashauri Watanzania kuongeza uzalishaji wa bidhaa na kuuuza nchini mwao   kuinua uchumi  kati ya nchi hizi mbili. Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Mkuu wa Uwekezaji Afrika, Kitengo cha  Biashara na Viwanda Afrika   Kusini, Zanele Mkhize wakati wa mkutano kati ya wafanyabiashara Tanzania na Afrika Kusini,  Dar es Salaam jana. Akieleza umuhimu wa   uhusiano wa uchumi endelelvu kati ya nchi hizo mbili, alisema ingawa kwa sasa   bado idadi ya wawekezaji  Watanzania nchini  Afrika Kusini ni ndogo,   ipo haja ya wengine kuendelea kuwekeza nchini humo.
kitaifa
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema hatarajii kuona 'disco-toto' ikifanyika popote pale jijini katika kuadhimisha sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya.Ameeleza kuwa hadi sasa hakuna aliyepeleka maombi kwa jeshi hilo ili kutoa huduma hiyo kwenye siku za sikukuu, ili ukaguzi wa kina ufanyike kwenye kumbi hizo kwa ajili ya usalama wa watoto.Amesema hayo alipofanya mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake, asubuhi ya leo, Jumamosi.Kamanda Mambosasa pia amewataka wazazi kuwa makini na watoto wao katika kusherehekea sikukuu hizi ili kuepusha matukio ya watoto kupata ajali, kupotea na kuzama kwenye fukwe, kama ilivyokuwa ikitokea miaka ya nyuma."Jeshi la polisi limejipanga kikamilifu kulinda raia na mali zao kwenye siku za sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya ikiwa ni pamoja na mikesha yake," alieleza.Kamanda Mambosasa ametia wito pia kwa wakazi wa Dar es Salaam kuhakikisha wanazingatia sheria na taratibu zote katika maadhimisho ya sikukuu hizo ili kuwepo na amani na usalama.
kitaifa
Na BENJAMIN MASESE MKUU wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha, amewatahadhirisha wananchi kutodhubutu kupewa pipi na mtu yeyote ndani ya gari binafsi au basi la abiria. Amesema  baadhi ya pipi hizo hupakwa dawa za kulevya na kusababisha kupoteza fahamu. Amesema tayari madhara ya ulaji wa pipi yalimkuta mtumishi mmoja wa Serikali ambaye alipewa pipi ndani ya basi na kujikuta akizinduka akiwa katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekeo Toure, akipatiwa matibabu. Tahadhari hiyo aliitoa alipozungumza na wananchi wa Kata za Igoma na Kishili kuhusu  mambo mbalimbali ya ulinzi na usalama ndani ya wilaya ya Nyamagana. Tesha ambaye hakutaka kutaja jina lake la mtumishi huyo aliyekula pipi lakini alidokeza cheo chake kuwa ni mkurugenzi. Alisema  alipewa pipi na abiria mwenzake aliyekuwa jirani na muda mfupi alisinzia na kupoteza fahamu. “Naombeni wananchi tuwe na tahadhari sana juu ya ulaji wa vitu  ndani ya vyombo  vya usafiri, hili nalisema wazi kwani limekuwa likijitokeza. “Hivi karibuni kuna mtumishi mmoja alikuwa anasafiri  ambako alipopewa pipi na abiria mwenzake kumbe ilikuwa imepakwa dawa za kulevya. “Mtumishi huyo ambaye tena ni mkurugenzi alijikuta akizindukia Sekeo Toure, hajui alifikishwa vipi katika hospitali hiyo. “Epukeni ulaji wa pipi pia kwa sababu umekuwapo   utapeli kwa njia ya simu nao umeendelea kutikisha nchi na watu kuibiwa mamilioni ya fedha,”alisema. Tesha alizungumzia  suala la wana wanafunzi  waliofaulu  mtihani  wa darasa la saba akiwaonya wazazi  watakaoshindwa kuwapeleka kuanza kidato cha kwanza watafikishwa mahakamani. Alisema ifikapo Januari 31, 2017 ataanza ziara ya kutembelea shule zote ndani ya Nyamagana  kubaini wanafunzi walioshindwa kuanza masomo ya kidato cha kwanza na kuwachukulia hatua wazazi wao. Wananchi wa Igoma na Kishili walimweleza DC  kwamba   kumekuwapo na kero ya kukatika daraja la Fumagila linalounganisha wilaya za Misungwi na Nyamagana na kusababisha wananchi kushindwa kwenda shule hasa   mvua inaponyesha. Akitoa majibu, alisema tayari Serikali imetenga Sh milioni 300 kwa ajili ya kujenga daraja la Fumagila na kuwataka wazazi kuwasindikiza wanafunzi na kuwavusha upande wa pili  mvua inaponyesha.
kitaifa
ASHA BANI-DAR ES SALAAM WAUAJI wilayani  Rufiji Mkoa wa Pwani ‘wamembipu’ Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon  Sirro, kwa kuua mtu mwingine usiku wa kuamkia jana katika Kitongoji cha Kazamoyo Kijiji cha Ikwiriri Kaskazini wilayani humo. Wauaji hao   walivamia  kijijini hapo   na kumpiga risasi shingoni,  Erick Mwarabu (38) ambaye ni  fundi rangi. Kwa mujibu wa mtoa taarifa,  Mwarabu akiwa nyumbani kwake   saa 8.00 usiku juzi, wauaji hao walifika na kumpiga     risasi   shingoni ambayo ilitokea kichwani upande wa kulia   kati  ya jicho na sikio na akafariki dunia papo hapo.   Mkuu wa  Wilaya ya Rufiji,  Juma Njwayo, aliithibitishia MTANZANIA  kwa  simu kwamba tukio hilo la mauaji lilitokea usiku wa kuamkia jana. Alisema   tayari mwili wa marehemu umekwisha kufanyiwa uchunguzi na kukabidhiwa kwa ndugu zake  kwa mazishi. Kifo cha Mwarabu kinafanya   idadi ya watu waliouawa   hadi sasa katika wilaya za Mkuranga, Kibiti na Rufiji mkoani Pwani kufikia 30. Kutokana na vitendo hivyo vya mauaji, hivi karibuni IGP Sirro, alitangaza mkakati wake ikiwamo jinsi ya kukomesha mauaji katika maeneo hayo.   IGP Sirro aliapa kupambana na wauaji hao huku akiahidi donge nono la   Sh milioni 10 kwa yeyote atakayetoa taarifa za kuwezesha kukamatwa wauaji hao. Alisema polisi  wanaendelea na operesheni mbalimbali  kuhakikisha  vitendo hivyo haviendelei na kwamba lazima watafanikiwa kubaini mzizi wa mauaji hayo. Mei 21  mwaka huu, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba, alitembelea eneo hilo na kuteta na askari wa operesheni maalumu ya kuwasaka wauaji wilayani Kibiti.  Alisema  mauaji hayo sasa yametosha akisisitiza  Serikali haitakuwa tayari kuona vitendo hivyo vikiendelea kama ilivyo  Somalia. Ziara hiyo ya ghafla ya Waziri Nchemba ilitokana na   mauaji ya mara kwa mara ya raia  ambayo yamekuwa yakifanywa na watu wasiojulikana. Akizungumza baada ya kuwatembelea   polisi  katika kambi maalumu ya operesheni ya kusaka wahalifu katika Kata ya Bungu, alisema  Serikali  imejipanga kukomesha hali hiyo kwa sababu kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama. “Tunaendelea kufuatilia kazi   mnayoendelea kufanya,   tuendelee kusonga mbele. Nikiziangalia takwimu na mwenendo, nazidi kupata maswali na naendelea kuona kuwa kuna kamchezo kanachezwa.  “Mauaji haya waliyoyafanya inatosha. Lazima tuwatie nguvuni, hatuwezi kuruhusu jambo hili likaendelea na kamchezo haka kakaendelea. “Anayefanya mauaji haya, anayeshirikiana na anayeshangilia hiki kinachofanyika wote tunawaweka katika kundi moja. Kufuga wauaji na wahalifu kuna gharama,”alisema. Nchemba  aliwataka polisi hao kukaa kimkamkati kuwakamata wauaji hao. Alisema ni muhimu polisi waondokane na dhana kwamba wametokomea kusikojulika bali wawakamate.
kitaifa
TAASISI ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) imekuwa ikipokea wagonjwa wengi wa moyo kutoka nchi za Afrika Mashariki na Kati na 217,016 wameshahudumiwa. Kaimu Mkurugenzi wa Upasuaji wa JKCI, Dk Angela Swai, alisema hayo jijini Dar es Salaam jana.Alisema wagonjwa hao wamepatiwa huduma hiyo katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita. Wapo wagonjwa kutoka Zimbabwe, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Ethiopia na hata katika visiwa vya Comoro ambao wamekuwa wakipatiwa huduma hapa ikiwamo za shida za mishipa ya moyo iliyoziba.”“Gharama sio kubwa sana hata kwa wagonjwa wanaotoka nje ya nchi, hatujazitofautisha sana na wagonjwa wa ndani, gharama hizo ni sawa na zile anazotoa mgonjwa anayetibiwa katika hospitali za binafsi,” alisema.Alisema ni muhimu wananchi wakatambua huduma za moyo zinazotolewa katika taasisi hiyo na kuchukua hatua pindi wanapobaini kuwa na shida za aina hiyo. Dk Angela alisema tangu kuanzishwa kwa JKCI Septemba 2015, imekuwa ikihudumia wagonjwa kutoka mikoa yote nchini ambao wamekuwa wakipewa rufaa kutoka hospitali za mikoa kwa ajili ya kupata huduma ya kiwango cha juu cha tiba ya moyo.“Wagonjwa katika taasisi hii hupata huduma za matibabu za kibingwa za magonjwa yote ya moyo zikiwamo za upasuaji wa kufungua na bila kufungua kifua, urekebishaji wa mfumo wa umeme wa moyo, tiba ya mishipa ya damu na utayarishaji wa wagonjwa wanaokwenda kupandikizwa figo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili,” alisema.Kuhusu viwango vya vifo katika taasisi hiyo kila upasuaji unaofanyika, alisema JKCI hufanya uchunguzi kwa mwezi kwa wagonjwa waliofariki, jambo ambalo huwasaidia kujitathmini zaidi kiutendaji. Lengo la tathmini hii ni kujipima katika ufanisi wa utoaji wa huduma za upasuaji wa moyo na kuweza kujipanga zaidi kwa huduma zilizo bora kwa kipindi kingine.Kwa upande wake, Daktari Bingwa wa Moyo katika taasisi hiyo, Dk Tulizo Sanga, alitoa mfanokuwa, kwa kipindi cha miaka mitatu imeweza kutoa huduma kwa wagonjwa wa nje ya nchi 217,016, huku waliolazwa wakiwa ni 11,587 na waliofanyiwa upasuaji wa kufungua kifua ni 1,098.Alisema hali hiyo inatokana na kuwapo kwa huduma madhubuti zinazotolewa na wataalam wazalendo wanaofanya kazi ya kuwahudumia wananchi wenye matatizo na wasio na matatizo ya moyo kwa kutoa mada mbalimbali zinazowasaidia kujikinga na maradhi hayo.
kitaifa