text
stringlengths
3
16.2k
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA KANISA Katoliki limekana madai kuwa Papa Francis ameidhinisha ndoa baina ya wapenzi ambao ni mashoga na wasagaji, wakisema kuwa ameruhusu makasisi wa kanisa hilo kuwabariki tu watu walio kwa uhusiano wa aina hiyo ambao aliurejelea kama usio wa kawaida akitumia neno ‘irregular’. Baraza la Maaskofu wa Kanisa Katoliki nchini Kenya (KCCB) aidha limesema kuwa agizo lililotolewa na Papa huyo lilikuwa ni la kualika mashoga kanisani “kwa matumaini kuwa watapata wokovu” na wabadili mienendo yao. “Stakabadhi hii inalenga kualika watu wote kwa uwepo wa Mungu na neema. Kanisa Katoliki linalenga kufikia watu wote ili wapate wokovu,” mwenyekiti wa KCCB Askofu Martin Kivuva Musonde akaeleza. Askofu Musonde alikubali kwamba watu wanashangaa ikiwa Kanisa Katoliki linaunga mkono ndoa ya wapenzi wa jinsia moja “au linabadilisha maana ya ndoa kama asasi Sakramenti ya Kanisa kati ya mwanamume na mwanamke”. “Kila wakati Papa Francis amekuwa akiwataka Makasisi kuwa na moyo wazi kama Kanisa na kulifungua kwa wote bila kujali viwango vya maadili yao. Kanisa liwe taasisi inayowakaribisha wote, mahala ambapo wote wanahisi kukaribishwa,” akasisitiza. “Stakabadhi ya Baba Mtakatifu inatambua kuwa wote wamealikwa kupokea baraka kutoka kwa Kanisa au Kiongozi wa Kanisa,” Askofu Musonde akaongeza. Alieleza kuwa baraka hizo zinaweza kupewa hata wale ambao si waumini wa Kanisa Katoliki au si Wakristu na wanataka kupokea baraka za Mungu. Askofu Musonde anasema kuwa stakabadhi hiyo haibadilishi maana ya ndoa kama kuja pamoja kwa mume na mke ili waunde familia ya kudumu. Soma Pia: Waislamu mjini Eldoret walaani hatua ya Papa Francis kukubali wapenzi wa jinsia moja kubarikiwa You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MWANGI MUIRURI POLISI katika Kaunti ya Murang’a wanamsaka mwalimu mmoja wa kiume wa Shule ya Upili ya Kamacharia mwenye umri wa miaka 33 baada ya kushukiwa kuwaua watoto wake wawili kwa kuwachinja shingoni kwa kisu. Mwalimu huyo kwa jina James Gitau Karanja, yuko mafichoni huku makachero wakimsaka baada ya miili ya Roy Irungu aliyekumbana na mauti akiwa na umri wa miaka mitano na Joseph Karanja wa umri wa miaka miwili na nusu kupatikana nyumbani kwake katika kijiji cha Kieni kilichoko eneobunge la Kiharu wakiwa wamelala kwa damu yao kitandani. Seneta wa Murang’a Bw Joe Nyutu ameyataja mauaji hayo kuwa ni unyama na kitendo cha kishetani ambacho hakifai kamwe. Kamanda wa Polisi wa Murang’a Bw Mathiu Kainga alisema kwamba tayari miili ya watoto hao imepelekwa katika mochari ya Murang’a. “Ripoti ya upelelezi inaonyesha kwamba mke wa mshukiwa, Bi Muthoni Gitau, alikuwa amemuacha miezi miwili iliyopita baada ya mzozo wa kinyumbani na akamwachia watoto hao,” akasema Bw Kainga. Hatimaye, majirani baada ya kuingiwa na shaka za kukosa kuona watoto hao walifanya uchunguzi wao na ndipo juhudi zilizoshirikishwa na chifu wa eneo hilo Bw Jason Hiuhu kuishia kuwapata watoto hao wakiwa wanechinjwa shingoni na kuaga dunia ndani ya nyumba yao. “Baada ya kuachiwa watoto hao, mshukiwa aliamua kumpeleka wa kwanza kwa shangazi yake na mwingine kwa nyanya yake, lakini wiki mbili zilizopita aliwachukua na kuwarejesha bomani huku ikiaminika aliwachinja asubuhi ya Desemba 20, 2023,” akasema Bw Hiuhu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE AKINA mama Waislamu na viongozi wa dini hiyo kutoka North Rift wameghadhabishwa na hatua ya kiongozi Kiongozi wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis kukubali wapenzi wa jinsia moja kubarikiwa na viongozi wa kidini. Wakihutubu wakati wa kufuzu kwa watoto katika Madras ya Maili Nne mjini Eldoret viongozi hao walisema matamshi ya Papa Francis yanadunisha sio dini tu bali maadili ya Kiafrika. Bi Halima Mohammed ambaye alikuwa miongoni mwa wazazi ambao watoto wao walifuzu katika shule hiyo ya Madrassa, alisema hatua ya uongozi wa Kanisa Katoliki ni ya aibu kwa watoto. Bi Mohammed alisema hiyo ni kero inayoweza hata kusababisha migogoro ya kidini. “Sisi kama Waafrika kwa kila hali tunapinga hatua ya Papa kutaka mashoga wabarikiwe kanisani, matamshi hayo ni aibu hasa kwa watoto wetu. Ndoa ya jinsia moja iliharamishwa hata katika Biblia wakati wa Sodoma na Gomora,” alisema Bi Mohammed. Bi Mohammed aliwataka wazazi kuwa macho kwa kufundisha watoto wao maadili mema katika jamii ili kukabiliana na uovu ambao unazidi kuongezeka duniani. Alitishia kuwa huenda wanawake wakalazimika kufika mahakamani kutaka dini ya katoliki nchini kufafanua kuhusu pendekezo la Papa Francis. Msimamo sawa ulitolewa na mwenyekiti wa baraza la wahubiri na Maimam (CIPK) Sheikh Abubakar Bini ambaye alikosoa matamshi hayo kwa kusema kuwa angalau Papa Francis angewataka viongozi wa dini kuombea mashoga na LGBTQ kuokoka na kubadilisha maisha yao. “Matamshi ya Papa Francis yanaenda kinyume na Biblia na Qur’an. Matamshi hayo ni sawa na kuhalalisha usagaji na tabia za wanachama wa LGBTQ kwa jamla.Maaskofu wa Kiafrika wasikubaliane na wito huo kamwe.Lau Papa Francis angewataka maaskofu wa katoliki kuombea mashoga wabadilishe maisha badala ya kusema wabarikiwe Mungu habariki ndoa ya watu wa jinsia moja,” alisema Sheikh Bini. Sheikh Bini alisema matamshi hayo yanahatarisha dini ya Kikristo ambapo huenda waumini wakalazimika kuachana na kanisa na kuanza kudumisha mila za tangu jadi badala ya kwenda kanisani. “Iwapo kanisa litaendele kukosa msimamo huenda waumini wakalazimika kufunga makanisa na kurudia mila n aidikadi za Mwafrika ambazo haziruhusu ndoa ya jinsi moja,” aliongeza Sheikh Bini Naye mwalimu wa mswala ya dini ya Kiislam Mubashr Idris alisema dini ya Kiislam haitayumbishwa na matamshi kama hayo huku akitoa mwaliko kwa wakristo kujiunga na dini hiyo kwa mafunzo bora yenye maadili badala ya kupewa ushauri wa kubariki mashoga. Bw Idris alitaka wazazi kuendelea kufundisha watoto wao maadili mema kupitia mwongozo wa Qur’an na Biblia badala ya kuiga mila na desturi za kigeni. “Tushirikiane na walimu wa kidini kufundisha watoto wetu maadili mema badala ya kukubali mafundisho ambayo yanaunga mkono ushoga,” alisema Idris. Kwa pamoja, viongozi hao wanataka maaskofu wa humu nchini kutoa msimamo wao kuhusiana na matamshi ya Papa Francis. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MAUREEN ONGALA MKUREGENZI mkuu wa Shirika la kupeana mikopo la Chembe Merchants Limited amefikishwa mahakamani Kilifi kwa kosa la kuwatapeli wateja maelfu ya pesa kwa kudai kuwa angewapa mikopo. Maafisa wa upelelezi wa makosa ya jinai (DCI) walimtia mbaroni Bw Ahmed Ali Bahatisha mnamo Jumamosi, Desemba 16, 2023, ambapo walifunga ofisi yake mjini Kilifi. Alikabiliwa na makosa sita mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kilifi Bw Daniel Sitati na kuachiliwa kwa dhamana ya Sh500,000 na mdhamini mmoja wa kiasi sawa na hicho au Sh300,000 pesa taslimu. Miongoni mwa makosa hayo kulikuwa na njama ya kuwaibia wateja wake na kupokea pesa kwa njia ya udanganyifu. Kampuni hiyo ya Chembe Merchants imekuwa ikiendeleza shughuli zake za kupeana mikopo katika ofisi zao zinazopatikana katika soko la Oloitiptip mjini Kilifi. Mbali na kupeana mikopo ya pesa, kampuni hiyo pia hudai kuwasaidia wateja wake kununua na kumiliki magari na mali nyingine. Mmoja wa waathiriwa ni Bw Stephen Chiriba ambaye alitapeliwa Sh170,000 kati ya Agosti 26 na Oktoba 2, 2023, kwa mujibu wa nakala ya mashtaka. Waathiriwa wengine ni Bw Ellon Baya na Joyshine Wairimu ambao walitapeliwa Sh47,000. Kulingana na mashtaka kortini, Bw Bahatisha alitekeleza uhalifu huo pamoja na wenzake ambao hawakufikishwa mahakamani. Kiongozi wa mshtaka alieleza mahakama  kuwa kando na walalamishi katika kesi iliyowasilishwa kotini zaidi ya watu 50 walikuwa wamejitokeza kulalamikia kutapeliwa na mshtakiwa. Kiongozi wa mashtaka alieleza mahakama kuwa mafisa wa polisi bado walikuwa wanendeleza uchunguzi  na ingekuwa bora iwapo angesalia gerezani. Maafisa wa upelelezi wanataka kubainisha iwapo mshtakiwa alikuwa anaendeleza biashara yake kihalali na alikuwa amejisajili na kisheria kukopesha na kupokea pesa kutoka kwa umma. Hata hivyo, hakimu Sitati alipinga ombi la kiongozi wa mashtaka kumnyima dhamana mshtakiwa na kusema ya kwamba hakutoa sababu za kutosha kuunga mkono ombi lake. “Ni lazima kiongozi wa mashtaka athibitishe ya kuwa mshukiwa atatoroka na pia ataharibu uchunguzi unaondelea na kulingana na kiapo cha afisa anayechunguza kesi hii swala hili hali halijapewa sababu za kutosha,” akasema Bw Sitati. Inadaiwa mkurugenzi huyo aliwalaghai wateja wake takriban zaidi ya Sh650 milioni. Kesi hiyo itasikilizwa mnano Machi 25, 2024, baada ya kuwa imetajwa Januari 8, 2024. Mkurugunzi huyo alijitetea na kueleza mahakama kuwa yeye ni kati ya wale ambao wana idhini ya kusimamia maswala ya fedha katika kampuni hiyo ambayo iko katika miji mbalimbali nchini na hatua ya kumnyima dhamana ingeleta changamoto kubwa sana. Alisema maafisa wa polisi walifunga ofisi yake na kuondoka na vifaa vya kazi na stakabadhi muhimu na wafanyakazi wake hawajui la kufanya kwa sasa. Baada ya habari ya kukamatwa kwa mkurugenzi huo kuenea, watu wengi walijitokeza katika afisi za DCI Kilifi kulalamikia kutapeliwa. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LABAAN SHABAAN WAZIRI wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Uchumi Dijitali Eliud Owalo amemteua Mkuu wa Huduma za Mawasiliano Kirais, Bw David Mugonyi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (CA). Akimwandikia barua Mwenyekiti wa Bodi ya CA Bi Mary Wambui, Bw Owalo amemwelekeza kufanya rasmi agizo hilo ili Bw Mugonyi kuanza kazi. “Nimerejelea barua kutoka kwa Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix Koskei ya Desemba 19, 2023 iliyoelekeza kuidhinishwa kwa Bw David Mugonyi kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Kenya,” akasema waziri Owalo. “Unaweza kuendelea kufanya rasmi uteuzi huu,” akaongeza Bw Owalo katika barua aliyoandika na kutuma Desemba 20, 2023. Kabla ya tangazo hili, Mkuu wa Utumishi wa Umma alimwandikia Bw Owalo barua ya kufanya rasmi nafasi mpya ya Bw Mugonyi. Bw Koskei alisema Halmashauri ya Wakurugenzi wa CA iliandaa mahojiano ya kazi ambapo Bw Mugonyi aliibuka kidedea. Bw Mugonyi atahudumu wadhifa huu baada ya Bw Chiloba kujiuzulu Oktoba 19, 2023, bada ya kuandamwa na tuhuma za ufisadi na usimamizi mbaya wa ofisi. Soma Pia: Ezra Chiloba ajiuzulu kutoka wadhifa wake wa Mkurugenzi Mkuu wa CA baada ya kukabiliwa na tuhuma za ufisadi Kulingana na ripoti ya ukaguzi, Chiloba alijipendelea kwa kutuma maombi na kuidhinisha mkopo wake wa nyumba kwa kiwango cha juu kwa thuluthi mbili. Aidha, alidaiwa kujihusisha na mgongano wa kimasilahi kwa kujitwika wajibu wa kuwa mnunuzi na muuzaji katika biashara ambapo CA ililipa Sh25 milioni. Bw Mugonyi, anayerithi mikoba ya Bw Chiloba, amekuwa akifanya kazi na Rais William Ruto tangu 2013 alipokuwa msemaji na katibu wa mawasiliano wakati Rais alihudumu wadhifa wa Naibu Rais. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA LABAAN SHABAAN KIONGOZI wa upinzani Raila Odinga amelaumu Rais William Ruto akidai uhusiano wa Kenya na mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), umedorora sababu ya utepetevu wa kidiplomasia. Akirejelea matukio wakati wa sherehe za Jamhuri Dei mnamo Desemba 12, 2023, Bw Odinga alisema kukosa kwa wawakilishi wa EAC katika maadhimisho hayo kuliashiria uhusiano bora wa muda mrefu umeharibika zaidi. “Wakenya waligundua kuwa kuna shida sana ya uhusiano wetu na majirani wetu wa Afrika Mashariki tulipoadhimisha miaka 60 tangu tupate uhuru,” Bw Odinga alisema kupitia barua kwa vyombo vya habari iliyotumwa Desemba 19, 2023.  “Hakuna nchi ya Afrika Mashariki iliyowakilishwa katika viwango vya Rais, Makamu Rais ama Waziri Mkuu kama ilivyotarajiwa kuwa desturi katika sherehe hizi muhimu hadi ikachukuliwa vivi hivi tu,” aliongeza. Hata hivyo, Rais Ruto alipinga madai kuwa tukio la Rais wa Uganda Yoweri Museveni na mwenzake wa Tanzania Samia Suluhu kutohudhuria sherehe hizo ni ishara ya kutibuka kwa uhusiano wa mataifa haya. “Kwani mimi huhudhuria sherehe za kitaifa za mataifa mengine? Hapana, ina maana kuna shida? Hapana,” alifoka Rais akijibu maswali ya wanahabari katika Ikulu ya Nairobi mnamo Jumapili, Desemba 17, 2023. Akiendeleza msururu wa shutuma kwa serikali ya Kenya Kwanza, Bw Odinga alisema serikali iliyoko madarakani imeanguka mtihani wa masuala ya kidiplomasia akidokeza serikali imelazimisha Uganda kulipia ‘ada ya ubroka’ kwa kutumia barabara ya Kenya kusafirisha mafuta kutoka Bandari ya Mombasa. “Uganda imelazimika kuenda mahakamani kutafuta afueni ili kujilinda kutokana na uroho wa utawala wa Rais Ruto,” Bw Raila alisema akiongeza imebidi nchi hiyo itafute njia mbadala kupitia Tanzania kusafirisha bidhaa za petroli. Kadhalika, Kiongozi wa Azimio alikashifu Waziri wa Barabara na Usafiri Kipchumba Murkomen kwa kusema Rwanda ni nchi inayoongozwa kidikteta. Bw Odinga alisema kauli ya waziri Murkomen ilikosa lugha ya kidiplomasia huku akiomba msamaha kwa raia wa Rwanda sababu ya tukio hilo. Katika mahojiano ya runinga mnamo Jumatatu, Desemba 18, 2023, Bw Murkomen alisema, “Rwanda si kama Kenya. Rwanda ni taifa linaloongozwa kidikteta ambapo agizo la Rais huwa sheria.” You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA CHARLES WASONGA WAZIRI wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen amelaumiwa kwa kudai kuwa taifa la Rwanda linaongozwa kidikteta ambapo kile Rais husema huchukuliwa kama sheria. Akijibu maswali kuhusu masuala ya usalama wa barabara kwenye runinga ya Citizen, Bw Murkomen alieleza kuwa utekelezaji wa maamuzi ya serikali huchukua muda “kwa sababu Kenya ni demokrasia ambako utawala wa sheria huzigatiwa.” Alikuwa akijibu malalamishi kutoka kwa wananchi kuhusu kucheleweshwa kwa utekelezwa wa kanuni na maamuzi ya usalama barabarani zilizotolewa na wizara yake, kama mafunzo mapya kwa madereva. Wakenya hao, akiwemo Seneta wa Kisii Richard Onyonka, alitoa mfano wa Rwanda ambako sheria na kanuni za usalama barabara hutekelezwa kwa haraka. “Rwanda sio kama Kenya. Rwanda ni taifa linaloongozwa kidikteta ambapo agizo la Rais huwa ni sheria,” akasema Jumatatu usiku. “Kwa kila uamuzi inayofanywa nchini sharti iwe ni pendekezo linalopasa kupelekwa bungeni kisha maoni ya umma yashirikishwe,” Bw Murkomen akaongeza. Kauli ya waziri huyo ilizua kero mingoni mwa Wakenya kwenye mitandao ya kijamii, akiwemo Wakili Mkuu Ahmednasir Abdullahi, alisema kauli hiyo inaweza kuchochea uhasama kati ya Kenya na Rwanda. “Waziri Murkomen hafai kushambulia taifa rafiki ambayo haijachokoza Kenya na yamemkosea heshima Rais wa Rwanda Paul Kagame, bila sababu maalum. Hii ni aibu  na inaweza kusababisha mzozo wa diplomasia kati ya nchi hizo mbili,” akasema Bw Abdullah. “Sharti mawaziri wafundishwe kuhusu wajibu wa afisi zao, haswa kuhusu diplomasia na sheria za kimataifa,” akaongeza jana kupitia mtandao wa kijamii wa X, zamani twitter. Naye msomi katika taalum ya Mahusiano ya Kimataifa Macharia Munene alisema ni makosa kwa waziri kuipaka tope nchi jirani. “Wizara ya Masuala ya Kigeni ya Kenya inafaa kutoa taarifa ya kuomba msamaha kwa taifa la Rwanda kuhusiana na madai ya Waziri Murkomen. Hilo lisipofanyika Rwanda itachukuliwa kauli ya Waziri huyo kama iliyoidhinishwa rasmi na serikali ya Kenya, hali ambayo inaweza kuchochea mzozo wa kidiplomasia kati ya nchini hizi mbili,” Profesa Munene akaeleza. Kwa upande wake, Bw Murkomen amewapuuzilia wanaomsuta kwa kusema kuwa Rwanda inatawaliwa kidikteta. Waziri alisema anaunga mkono mtindo wa uongozi nchini Rwanda ambao alieleza imeisaidia nchi hiyo “kupiga hatua kubwa kimaendeleo.” “Rafiki yangu, Ahmednasir, napendezwa na mtindo wa uongozi unaoendelezwa Rwanda ambao umewasaidia kujenga miundo msingi mizuri ukiwemo uwanja mpya wa ndege na kuleta nidhamu barabarani. Sio Rwanda tu, nchi kama vile Umoja wa Milki ya Kiarabu (UAE), Morocco, Saudi Arabia, miongoni mwa nyingi imekumbatia mitindo ya uongozi ambayo ileta ufanikisi kwa sababu viongozi wao wanayo mamlaka ya kufanya maamuzi makali,” Murkome akaeleza. Mnamo Mei 15, mwaka huu Katibu wa Wizara ya Masuala ya Kigeni Korir Sing’oei alimkaripia Waziri wa Utumishi wa Umma Moses Kuria kwa kutoa kauli tata kuhusu mzozo unaoendelea nchini Sudan. Bw Kuria alidai kuwa suluhu la kipekee la kukomesha mzozo huo ni kwa wanajeshi wa Umoja wa Afrika (AU) kushambulia Khartoum kwa mabomu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA SAMWEL OWINO MKUU wa Mawaziri Musalia Mudavadi anamtaka Rais William Ruto kushauriana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ili kuwaombea msamaha Wakenya zaidi ya 41 waliofungwa jela katika taifa hilo jirani. Bw Mudavadi ambaye vilevile ni Waziri wa Masuala ya Kigeni, amesema mbinu zote zinapaswa kutumika kuwezesha kuachiliwa huru kwa Wakenya hao. Kauli ya waziri huyo inajiri wakati ambapo muungano wa Azimio ukiongozwa na Raila Odinga kudai serikali ya Kenya Kwanza haijui namna ya kupalilia uhusiano mzuri na mataifa jirani.
Tags
You can share this post!
Previous article
Pendekezo la kufungwa mangweni za pombe ya mnazi lazua...
Next article
Murkomen motoni kwa kudai Rwanda ni taifa la kidikteta
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA SAMWEL OWINO MKUU wa Mawaziri Musalia Mudavadi anamtaka Rais William Ruto kushauriana na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni ili kuwaombea msamaha Wakenya zaidi ya 41 waliofungwa jela katika taifa hilo jirani. Bw Mudavadi ambaye vilevile ni Waziri wa Masuala ya Kigeni, amesema mbinu zote zinapaswa kutumika kuwezesha kuachiliwa huru kwa Wakenya hao. Kauli ya waziri huyo inajiri wakati ambapo muungano wa Azimio ukiongozwa na Raila Odinga kudai serikali ya Kenya Kwanza haijui namna ya kupalilia uhusiano mzuri na mataifa jirani.
Tags
You can share this post!
Previous article
Pendekezo la kufungwa mangweni za pombe ya mnazi lazua...
Next article
Murkomen motoni kwa kudai Rwanda ni taifa la kidikteta
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA ALEX KALAMA VIONGOZI wa kidini na wale wa kibiashara katika Kaunti ya Kilifi wamehitilafiana vikali kuhusu pendekezo la kufungwa vituo vya kuuzia pombe ya mnazi mjini Malindi. Hatua hiyo imejiri baada ya mwenyekiti wa vuguvugu la usalama wa wafanyabiashara mjini Malindi, Bw Athman Said, kupendekeza kufungwa kwa maeneo ya kubugia mnazi almaarufu kama mangweni kwa misingi kuwa yanaharibu watoto katika eneo hilo. “Mangweni ambazo ni za kuuza mnazi zimekuwa nyingi sana katika mji wetu wa Malindi na kuna nyingi ambazo zinatumika kama sehemu ya kuficha majambazi na kama sehemu ya kuuzia dawa za kulevya na kuharibu vijana wetu. Nakuomba naibu kamishina wa eneo hili la Malindi ukishirikiana na serikali ya kaunti uweze kushughulikia hilo jambo ipasavyo,” akasema Bw Said. Ni kauli ambayo ilipingwa vikali na aliyekuwa Mwakilishi wa Wadi ya Ganda Bw Abdulrahaman Omar aliyeshikilia kwamba sehemu hizo hazifai kufungwa kwa misingi kuwa zimekuwa za misaada kwa uchumi wa wakazi wa Malindi na Kilifi kwa ujumla. “Usalama kupatikana haimaanishi mangweni lazima kufungwa tafuteni njia ya kutatua shida ya ukosefu wa usalama, manake kuwa mangweni ndizo zinazochangia usalama kudorora hapa Malindi mimi hilo sikubaliani nalo. Kwa sababu mangweni zile ndizo tegemeo kubwa la jamii za sehemu hii katika kujipatia riziki ya kujikimu kimaisha na kulea familia zao, na mnazi sio haramu. Kwa hivyo tafuteni njia mbadala ya kutatua shida ya ukosefu wa usalama,” akasema Bw Omar. Hata hivyo badala yake Bw Omar amesisitiza haja ya kunaswa kwa walanguzi wa mihadarati badala ya wauzaji wa mnazi. “Dawa za kulevya ziko kila mahali… kila mwaka ni dawa za kulevya lakini mbona haziishi. Shikeni wale wenye kuuza ndio wale wanaovuta watakoma lakini acheni kusumbua wauzaji mnazi. Na hizi mangwe kuna vijana wamesoma ndani ya hii nchi kupitia mnazi au kuuza pombe. Kama kuna changamoto waangalie njia ya kusuluhisha lakini swala la kufunga mangwe hilo hatukubali manake hapa ndipo jamii inapata mkate wa siku,” alisisitiza Bw Omar. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA FRIDAH OKACHI MADEREVA, utingo na vijana kutoka Kikuyu na Kawangware walishiriki mchezo wa kandanda kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya na unywaji wa pombe kiholela msimu huu wa Krismasi. Makundi hayo yalikusanyika katika uwanja wa michezo wa Kawangware na kushiriki kwenye mchezo ili kupunguza utumiaji wa pombe na kujihusisha na kazi za kuwanufaisha huku wakiepuka wizi. Msimamizi wa kituo cha kupigania haki Dagoretti, Bw Wainaina Kamau, alisema hatua hiyo itasaidia idadi kubwa ya vijana kuepuka utumiaji wa mihadarati na unywaji pombe kupitia mchezo huo ambao umeandaliwa kufanyika kila wiki siku ya Jumatatu. “Wakati huu wa sherehe, madereva na utingo ambao ni vijana hujipata kwa majaribu ya kubugia mvinyo kupita kiasi. Pia, kuna wale wana mkono mrefu wakati wa kuelekeza abiria. Katika muda wanaotumia kuja kucheza na kurejea kazini, utawafanya kuwa watu bora wakati huu. Dakika wanazotumia hapa ni wakati, wameegesha magari yao wakisubiri abiria,” alisema Bw Wainaina. Kwenye mchezo huo, umejumuisha kundi la utingo saba ambalo linafahamika Chini ya Mnazi na kundi la Team Change ambalo lina vijana ambao zamani walikuwa wakishiriki wizi wa kimabavu lakini wakabadilika kuwa watu wema. Bw George Ochieng aliambia Taifa Leo kuwa ni miongoni mwa vijana ambao walikuwa wakitekeleza wizi wa kimabavu na kisha kutumia mihadarati kwa wingi. Alisema hatua hiyo itasaidia vijana kujumuika na kutangamana na viongozi wanaohakikisha usalama unadumishwa. “Hapa tuna makundi matatu. Unapata dawa za kulevya na wizi zinaandamana. Iwapo hatutaweza kushirikisha kila mmoja, jamii itaumia kwa kuporwa au hata kufa iwapo madereva watakunya pombe kupita kiasi. Team change lina vijana zaidi ya 50 ambao wamebadilika,” alisema Bw Ochieng. Dereva wa matatu za ruti ya Kikuyu-Kawangware alisema unywaji wa pombe huongezeka wakati huu, kutokana na mapato ya juu na wengi wakishindwa jinsi ya kutumia. Dereva huyo alishukuru kupata mafunzo ya kutumia pesa zake. “Nashukuru kwa sababu sasa nitajua jinsi ambavyo nitatumia pesa zangu. Anasa ya pombe hukolea wakati tunasimama sehemu mbalimbali. Kwa siku kadhaa nimeweza kuelimika kwamba nahitaji kufanya nini na nina uhakika Januari sitasumbuana na familia yangu kwa kukosa karo ya mtoto wangu katika wakati unaofaa,” alisema dereva huyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA STEPHEN ODUOR WAKAZI wa kijiji cha Ziwani, Kaunti Ndogo ya Tana Kaskazini, wameililia serikali kwa kuwakejeli baada ya kukosa kupokea misaada waliyotumiwa wiki mbili zilizopita, baada ya kuathiriwa na mafuriko. Wakazi hao, walitoa lalama zao huhuku maelfu wakiendelea kukabiliwa na athari hizo za mafuriko. Wiki mbili zilizopita, malori 14 yaliyobeba misaada, ilitumwa na serikali ya kitaifa katika hafla ambayo iliongozwa na Naibu Rais Rigathi Gachagua. Hata hivyo, kufikia sasa wakazi hao wanasema bado hawajapokea usaidizi huo na wamebaki kushangaa bidhaa hizo zilipelekwa wapi muda mfupi baada ya hafla hiyo. Manusura wa mafuriko ambao wanaishi kwenye kambi za muda, wanahisi kuwa walikusanywa kwa ajili ya picha ili kujenga taswira kuwa walikuwa wamepokea msaada huo. “Kwa muda tulicheza densi na tukadhani afueni imefika. Tuliambiwa kuwa chakula kitagawanywa baadaye lakini tangu wakati huo, tumezungushwa tu,” alisema Bi Fatuma Ali. Juhudi zao za kutafuta vyakula hivyo hazijazaa matunda. Bi Mariam Saladh, nyanya anayelea wajukuu wake sita, alisema kila ofisi ambayo wamekuwa wakiulizia kuhusu msaada huo imewatuma kwingine. Mkuu wa Kambi ya Ziwani, Bw Abdalla Dulo, alisema kwamba ameacha kuulizia, kwani kila mmoja anaonekana kumkwepa. “Nimeenda kila ofisi, wanaendelea kunituma huku na kule. Ilibidi nije kuwaambia watu wangu kwamba ni mbio zisizo na tija, tunakubali hatima yetu, lakini bado tunataka majibu,” alisema. Kulingana na Bw Dulo, kambi mbalimbali ziliwakilishwa kwenye hafla ya kuzindua usambazaji wa chakula. Alisema kuwa waliahidiwa kupokea msaada huo baadaye, lakini unachukua muda mrefu na wanakijiji wana mahitaji . Kamishna wa Kaunti ya Tana River, Bw Mohammed Noor, hata hivyo alisema kuwa zoezi la usambazaji linaendelea.Kulingana na Bw Noor, kambi hiyo itahudumiwa ndani ya mpango wa usambazaji. “Zoezi hilo bado linaendelea, tumefika kambi chache na bado tunaendelea. Hakuna atakayeachwa. Kambi ya Ziwani pia iko katika mpango huo na vitu vyao vitaletwa hivi karibuni,” alisema Bw Noor. Zaidi ya familia 35,000 zimeathiriwa na mafuriko hayo. Wakati huo huo, Gavana wa Tana River, Bw Dhadho Godhana, tangu wakati huo amebatilisha likizo ya msimu huu wa sherehe kwa wafanyakazi wa kaunti, akisema kuwa juhudi zote zitahitajika ili kudhibiti athari za mafuriko. “Hatuwezi kwenda kufanya sherehe wakati ndugu na dada zetu wanateseka kambini,” alisema. Zaidi ya hayo, amelitaka bunge la kaunti kurejea kutoka mapumzikoni na kuidhinisha bajeti ya ziada ili kurahisisha mipango ya kuingilia kati. Gavana huyo pia ametoa wito kwa wasamaria wema kuchangia misaada, akibainisha kuwa utawala tangu wakati huo umetumia zaidi ya nusu ya fedha za Hazina ya Kudhibiti Hatari za Maafa, lakini pengo hilo bado halijapungua. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA