text
stringlengths
3
16.2k
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAKAZI wa mtaa wa Mazembe viungani mwa mji wa Nakuru wamekiri kuhangaishwa na wezi ambao huwaibia na kuwasindikiza hadi nyumbani. Huwawekea ulinzi huo makusudi ili kuhakikisha kwamba wateja wao wanafika nyumbani salama salimini. Kwa kawaida, wahuni wamebuni mbinu mpya ya kutembea na mbwa wakubwa nyakati za usiku, ili kujiwekea ulinzi wa kibinafsi. Owen Shibala mwendeshaji bodaboda kati ya Nakuru mjini na Mazembe, anasema hajui walikotoa ujasiri walio nao kushika doria usiku utadhani ni polisi. Mazembe ni mojawapo ya mitaa ambayo hushuhudia visa vya kihalifu na utumiaji wa mihadarati mara kwa mara. “Ukikutana nao usiku ni lazima usalimishe kila kitu lau sivyo utaona cha mtema kuni. Watakucharaza viboko na kuiba kila kitu cha nguvu,”akasema. Hata hivyo, wanapoiba hujitwika jukuma la kuwasindikiza wakazi, wasije wakakutana na vibaka wengine barabarani. Aidha, wanalia sare za polisi jambo linalowafanya baadhi ya raia kuamini huenda wanashirikiana na maafisa wa polisi. Baadhi yao wanajifanya ni maafisa wa polisi ambao huwa wameshika doria, wakilenga kuhangaisha wapita njia wanaotoka kazini usiku. Agnes Wahome mfanyibiashara mtaani Rhonda anasema huwa wamejihami kwa visu, rungu na wako tayari kupigana. Kulingana na Bi Wahome, hii ni hali ya kawaida siku hizi katika mitaa ya Manyani, Bondeni na Freearea ambapo vijana wengi wamejiingiza kwenye uhalifu. Bi Wahome anasema wahalifu wengi wanajulikana, kwani ni vijana wadogo kutoka mitaa jirani ya Flamingo na Lakeview. Mkazi huyo angependa polisi kushika doria katika maeneo husika ili kuzuia kuzuka kwa magenge hatari yanayohangaisha wenyeji. Hili linajiri siku chache baada ya Taifa Leo Dijitali kufichua visa vya wizi ambapo baadhi ya wezi kutoka kwenye mtaa wa Gioto, Nakuru wamekuwa wakipika chakula katika kila nyumba wanamoingia kuiba. Mtaa wa Bondeni, Kaunti ya Nakuru ambapo wezi huwaibia wakazi na kuwasindikiza mpaka nyumbani. PICHA|RICHARD MAOSI
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
Tags
You can share this post!
Previous article
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya...
Next article
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika...
T L
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti,  baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
NA CECIL ODONGO NDOA kati ya utawala wa Kenya Kwanza na mwanaharakati Miguna Miguna imeanza kuingia doa, wakili huyo maarufu akikosoa Rais William Ruto kutokana na madhila mbalimbali yanayozonga nchi. Bw Miguna ambaye alikuwa mfuasi sugu wa Kenya Kwanza na hata kuunga mkono azma ya Rais Ruto katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2022, ameonekana kuishiwa na subira kutokana na Wakenya kulimbikizwa ushuru, ufisadi miongoni mwa changamoto nyinginezo Mnamo Jumatano, wakili huyo mkosoaji mkubwa wa Kinara wa Azimio Raila Odinga, alimkaba koo Rais mtandaoni, akisema katika uchaguzi mkuu wa 2027, Wakenya watakumbuka tu changamoto walizopitia kwenye utawala wa  Kenya Kwanza. “Nawahakikishia kuwa mnamo 2027, Wakenya hawatamkumbuka ufasaha wa @WilliamsRuto, safari zake za ng’ambo wala suti za kaunda anazovaa. Watakumbuka tu njaa yao, umaskini, ukosefu wa ajira na ufisadi ambao unaendelea kupanda. Msiseme si kuwaonya,” akaandika Bw Miguna katika mtandao wake wa X (zamani twitter). Rais Ruto amekuwa akikashifiwa kwa safari zake za ng’ambo ambazo sasa zimefikia 45 ya mwisho ikiwa ni ya Djibouti mnamo Disemba 9. Hata hivyo, Rais amekuwa akijitetea kuwa ziara hizo ni za kusaka kazi kwa Wakenya hasa katika milki ya kiarabu. Bw Miguna anaonekana kuungana na Bw Odinga ambaye ameitaka serikali ibuni nafasi za ajira akisema kuwatafutia Wakenya kazi nje kunaonyesha serikali imeshindwa katika wajibu wake. Juzi Bw Miguna, alishambulia Tume ya Maadili ya Kupambana na Ufisadi Nchini (EACC) kwa kushindwa kupigana na ufisadi. Bw Miguna alisema maafisa wa tume hiyo wanamakinikia kuwahangaisha polisi barabarani wanaochukua hongo za Sh20 ilhali kuna samaki wakubwa wanaopora pesa za umma. “Rais @WilliamsRuto. Ufanisi wa uongozi wako utaamuliwa na iwapo ufisadi ukuwa chembechembe za DNA ya nchi wakati wa utawala wako,” akaandika kwenye mtandao wa X. Alikuwa akirejelea ufichuzi wa ripoti ya Mdhibiti wa Bajeti ulioonyesha kuwa baadhi ya magavana hawajatumia hata senti kwenye miradi ya maendeleo. Mnamo Novemba 10, Bw Miguna alikosoa hatua ya  utawala wa Kenya Kwanza kuwaongezea Wakenya mzigo wa ushuru na kuitaka serikali pia iache kukopa kutoka kwa Shirika la Fedha Duniani (IMF) na Benki ya Dunia. “Serikali ya Kenya Kwanza haitabadilisha Kenya na kuimarisha hali ya maisha ya raia iwapo haitajiondoa kwenye minyororo ya IMF na Benki ya Dunia. “Bila kujiondoa, matrilioni yanayokusanywa  kama ushuru na mikopo nchi inapewa, itaishia mikononi mwa viongozi wanaoshikilia afisi za umma wawe wamechagulia au kuteuliwa,” akaandika  Bw Miguna. Kabla ya kuhamia mrengo wa Rais Ruto,  Bw Miguna alikuwa mshirika wa karibu wa kisiasa wa Bw Odinga na ni kati ya wale ambao walimwaapisha baada ya uchaguzi tata wa 2017. Hata hivyo, alitofautiana na Raila baada ya waziri huyo mkuu wa zamani kuanzisha ushirikiano na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta ambaye wakati huo alikuwa uongozini. Uhasama wa Bw Miguna dhidi ya utawala wa Jubilee mnamo 2017 ulichangia kufurushwa kwake nchini mnamo Februari 7 2018 kisha Uhuru na Raila wakakubaliana kisiasa mnamo Machi 9, 2018. Alirejea nchini mnamo Oktoba 20 baada ya kuwa Canada kwa siku 1687 na hata amewahi kufika ikulu kumsalimia Rais Ruto ambaye alimpigia debe sana kabla ya uchaguzi kufanyika. Kwa mujibu wa mchanganuzi wa kisiasa Martin Andati, Bw Miguna anazidisha mashambulizid dhidi ya serikali kwa sababu hajapewa kazi jinsi alivyotarajia baada ya kupigia UDA debe 2022. “Alikuwa amemwambia Rais ampe kazi lakini ni kama Rais amekataa. Miguna ni kichwa ngumu  na hawezi kuchukua maagizo kama kile anachoambiwa haiko katika Katiba. Alituma maombi ya kupata kazi ya DPP lakini akakosa kuorodheshwa na hilo linaonyesha alitemwa,” akasema Bw Andati. “Sasa ameishiwa subira na pia serikali haiwezi kumfurusha tena kwa sababu ndiyo ilimresha. Pia hawezi kurudi mrengo wa Raila kwa sababu alishakosana nao vibaya. Ataendelea kupiga kelele ila sioni akipewa kazi ndani ya Kenya Kwanza,” akaongeza Bw Andati. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WANDERI KAMAU RAIS Mstaafu Uhuru Kenyatta mnamo Jumatano alizuru bwawa lenye utata la Karimenu, katika eneo la Gatundu Kaskazini, Kaunti ya Kiambu, akiwa pamoja na mkewe, Bi Margaret Kenyatta. Kwenye picha zilizotolewa na Afisi ya Bw Kenyatta, wawili hao walionekama wakiwa wamesimama kwenye kuta za bwawa hilo. Familia ya Bw Kenyatta imekuwa ikiepuka kuonekana hadharani wala kuzumgumzia masuala tofauti yanayoendelea nchini. Bwawa hilo, ambalo lina kina cha mita 59, liko kwenye shamba la ekari 600. Ni mmojawapo wa miradi mikuu iliyokamilishwa na serikali ya Rais William Ruto, japo ujenzi wake ulianzishwa wakati wa uongozi wa Bw Kenyatta. Tangu ujenzi wa bwawa hilo kuanza mnamo Aprili 2019, shughuli za ujenzi wake zilitatizika mara kadhaa kutokana na maandamano ya wakazi, wakidai kutopata malipo ya kutosha. Baadhi ya wakazi walikuwa wamekataa kuondoka kwenye mashamba yao, wakidai “kuhadaiwa” na serikali kuhusu bei halisi ya mashamba yao. Majuzi, maji kutoka bwawa hilo yalianza kuvunja kuta zake, hali iliyozua malalamishi makali kutoka kwa wenyeji. Serikali ilisema kwamba imetenga Sh150 milioni za muda kusaidia kwenye shughuli za kuwahamisha wakazi walioathiriwa. Waziri wa Maji, Bw Zachariah Njeru, alisema kuwa watu 122 ambao malo yao iliharibiwa na maji hayo watalipwa fidia na serikali na kutafutiwa makao mbadala. Mnamo Septemba 20, 2023, viongozi kutoka eneo la mfumo mzima wa Athi Water Basin wakiongozwa na Mbunge wa Gatundu Kusini Bw Kagombe Gabriel Gathuka waliwahutubia wanahabari katika makao makuu ya Wizara ya Maji ambapo walishinikiza wenyeji walioathirika kutokana na ujenzi wa mradi huo wa Sh24 bilioni, walipwe fidia. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WANDERI KAMAU SERIKALI mnamo Alhamisi ilisema kuwa mapato yake kutokana na huduma zinazotolewa kupitia kwa e-Citizen yaliongezeka na kufikia Sh900 milioni kwa siku moja, ikilinganishwa na nyakati zilizopita. Katibu katika Idara ya Uhamiaji na Huduma za Raia, Dkt Julius Bitok, alitaja mikakati mipya ya serikali kulainisha ulipaji wa huduma zake kama sababu kuu ya kuongezeka kwa mapato hayo. Dkt Bitok alisema fedha hizo zilikusanywa mnamo Jumatano, Desemba 20, 2023. Alisema kuwa fedha hizo zilitokana na malipo yaliyofanywa kupitia pesa za humu nchini na dola za Amerika. Kiwango hicho ni ongezeko kubwa la mapato ya serikali tangu Rais William Ruto kutoa agizo kwamba lazima malipo yote ya huduma za serikali yawe yakifanywa kupitia nambari ya Paybill 222222. “Huu ni mwelekeo mzuri tunaotarajia kuendelea kushuhudia katika siku zijazo,” akasema Dkt Bitok. Hilo linajiri mwezi mmoja tu baada ya aliyekuwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Sekretariati ya Vituo vya Huduma Kenya nchini, Bw Benjamin Kai Chilumo, kuondolewa kwa muda kutoka nafasi hiyo. Bw Chilumo aliondolewa kutoka nafasi hiyo pamoja na maafisa wakuu wengine watendaji 17 wanaosimamia idara tofauti za serikali. Wanadaiwa kuhusika katika makosa tofauti, yakiwemo ufisadi na matumizi mabaya ya mamlaka. Baadhi ya wakuu wengine waliosimamishwa ni mkuu wa Halmashauri ya Kustawisha Kazi za Maji ya Tananathi, Mhandisi Frederick Mwamati, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Kitaifa ya Mafunzo ya Kibiashara (NITA) Syanvas Ong’alo kati ya wengine. Wanatarajiwa kuchunguzwa na Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC). You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA BRIAN OCHARO WATU 66 waliookolewa katika msitu wa Shakahola watasota jela Krismasi na Mwaka Mpya baada ya mahakama kuipa serikali siku nyingine 130 kuamua ikiwa inakusudia kuwafungulia mashtaka au kuwachukulia kama mashahidi. Hakimu Mwandamizi Mkuu wa Shanzu Joe Omido alisema alishawishiwa kuwa serikali ilihitaji muda zaidi kukamilisha uchunguzi wake. “Ni maoni yangu kuwa muda mfupi kuliko makadirio ya siku 160 utatosha. Nitawaruhusu washtakiwa kuendelea kukaa rumande kwa siku 130 ambazo naamini zitatimiza malengo yaliyokusudiwa,” alisema hakimu huyo. Muda wa siku 130 utaanza Septemba 11, 2023, na utaisha Januari 18, 2024. Mahakama iliambiwa kuwa uchunguzi umebaini kuwa manusura hao wanaweza kuwa wamefanya makosa ya jinai dhidi ya watoto wao, ambao hawajulikani waliko. “Katika baadhi ya matukio, familia nzima ya msingi kabisa inaweza kuwa imeangamizwa,” Inspekta wa Polisi Raphael Wanjohi alisema. Uchunguzi huo utajumuisha chembechembe za  DNA kutoka kwa miili 429 iliyofukuliwa hadi sasa. Afisa huyo pia alisema anahitaji muda wa kutosha kusafiri nchi nzima kuwatafuta na kuwafikia jamaa za marehemu kwa madhumuni ya kufanya uchunguzi na kukusanya sampuli za DNA kwa ajili ya uchunguzi na kulinganisha na wale waliofukuliwa. “Kwa kuwa kuna miili  ilizikwa bila vibali vya kuzika, ipo haja ya kuwatambua marehemu, jambo ambalo linaleta changamoto kwa kuwa wapelelezi hawana vitambulisho wala nyaraka nyingine za watu waliofariki,” alisema Mpelelezi alisema mchakato wa utambuzi wa wahasiriwa na shahidi uko katika gia na unahitaji muda wa kutosha kutokana na ugumu wa upelelezi. Bw Wanjohi aliendelea kusema kwamba polisi wako katika harakati za kuchimba data ya mawasiliano kutoka kwa vifaa vilivyopatikana na miamala ya kifedha kwa nia ya kupata utambulisho wa mamia ya watu waliofariki. Lakini manusura hao kupitia kwa wakili wao Bw Mureti walipinga ombi hili, wakisema kwamba halijafichua sababu za msingi zinazoweza kulazimiza mahakama kutoa amri ya kuwazuilia zaidi. “Serikali ina uwezo wa kufanya na kuhitimisha upelelezi wa suala hili bila ulazima wa kuwashikilia washtakiwa,” alisema. Bw Mureti alisema ikiwa wengi wa waliohojiwa walikataa kurekodi taarifa, walikuwa wakitumia haki zao za kikatiba kunyamaza na hivyo hawawezi kulaumiwa kwa kufanya hivyo. Alisema zaidi kwamba ripoti ya uchunguzi wa kijamii iliyotayarishwa na kuwasilishwa na ofisi ya afisa wa urekebishaji wa tabia inaonyesha kuwa wengi wa washtakiwa hawawezi kutoroka na kuwa familia zao ziko tayari kuwakubali.   Mkurugenzi Msaidizi wa Mashtaka ya Umma Jami Yamina alifahamisha mahakama kuwa serikali inawachukulia manusura hao kama washukiwa, akisema kuwa tabia zao zimebadilika na sasa wanachukuliwa kuwa washukiwa katika uchunguzi unaoendelea. “Tabia zao zimebadilika. Kwa sasa ni washukiwa. Watu wanaoshukiwa kutekeleza uhalifu, ambao wanachunguzwa, hawawezi kuitwa waathiriwa,” akasema Bw Yamina. Bw Yamina amesema tayari serikali imekusanya ushahidi mwingi dhidi ya manusura hao  hivyo kuna  haja ya kuwaweka gerezani hadi mashtaka yatakapofunguliwa dhidi yao. “Jinsi uhalifu uliotendwa huko Shakahola kama ilivyoonyeshwa kwenye maombi ya awali ni kwamba masalio ya mwisho ya uhuru wa marehemu yalichukuliwa baada ya vyeti vyao vya kuzaliwa na hata kitambulisha kuharibiwa,” alisema. Serikali pia imeeleza kuwa ndugu wa marehemu watatakiwa kutoa ushahidi mahakamani mara mshukiwa mkuu Paul Mackenzie na wenzake watakapofunguliwa mashtaka rasmi. Kesi hiyo itatajwa Januari 18, 2024. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA TITUS OMINDE WAKATI watoto wengine wakisherehekea Krismasi pamoja na jamaa zao na familia zao, zaidi ya watoto 700 wenye umri wa kati ya siku moja hadi miaka mitano wataadhimisha sikukuu hiyo jelani wakiwa na akina mama zao ambao wanatumikia vifungo au wako rumande wakisubiri mchakato wa kesi zao. Duniani kote, Wakristo hutumia siku ya Krismasi kuwa ni ya kuleta familia pamoja ambapo wanasherehekea na kuangazia mwaka ulivyokuwa na kujipangia malengo ya Mwaka Mpya. Lakini sasa kuna watoto wasio na hatia ambao wako gerezani, si kwa sababu wao ni wafungwa, bali kwa sababu ya uhalifu uliofanywa na akina mama zao au walezi wao. Hakuna jambo la kuhuzunisha zaidi kuliko kuona mpendwa amewekwa rumande wakati dunia nzima inasherehekea Krismasi na Mwaka Mpya. Miongoni mwa watoto zaidi ya 700 walio katika magereza, 12 kati yao wako katika gereza la wanawake la Eldoret huku wengine wakisambaa katika magereza 18 ya wanawake nchini. Katibu wa Idara ya Urekebishaji wa Tabia katika Magereza Bi Salome Wairimu Beacco, alisema idara ya magereza inashirikiana na wadau wengine ili kuweka mazingira mazuri kwa watoto kama hao. Bi Beacco alisema kuna mipango ya kuanzisha vituo vya kulelea watoto katika magereza mbalimbali nchini ambavyo vitakuwa vya ubora wa hali ya juu. Lengo ni kuhakikisha watoto hao wanakua wakiwa katika mazingira shwari. “Hapa katika gereza la wanawake la Eldoret, tuna watoto 12 ambao waliandamana na akina mama zao. Tunashirikiana na washikadau na washirika wa maendeleo ili tuwe na huduma ya hali ya juu ya kutwa kwa watoto hawa,” alisema Bi Beacco. Katibu huyo alieleza haja ya kuchunguza njia zote za kisheria ambazo zitasaidia katika kuwaokoa watoto gerezani pamoja na kupunguza msongamano katika magereza yote nchini. “Tunawashukuru sana washirika wetu wa maendeleo na tunawahimiza wadau wengine kujitokeza na kutusaidia si tu kupunguza msongamano ndani ya magereza lakini pia kuhakikisha wateja wetu wanaishi maisha ya staha kwa kuzingatia ibara ya 28 inayoendana na ibara ya 43 ya Katiba,” aliongeza. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA KALUME KAZUNGU NI afueni kwa mamia ya wasafiri baina ya Lamu na Garsen baada ya mawe kupangwa kufunika eneo la Gamba lililosombwa na mafuriko yaliyobeba mchanga uliokuwa ni sehemu muhimu ya barabara majuma mawili yaliyopita. Eneo hilo la barabara lenye urefu wa karibu nusu ya kilomita lilikuwa limegeuka mto wenye maji mengi badala ya barabara,hali ambayo ilikuwa imelemaza kabisa usafiri kwenye barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen. Kwa kipindi cha majuma mawili sasa, wasafiri waliokuwa wakitoka Lamu kuelekea Mombasa na wale wa Mombasa kuingia Lamu hawangeweza kuvuka eneo la Gamba. Aliyekuwa na azma ya kusafiri kwenye barabara hiyo alilazimika kusafiri kwa magari na kisha kushuka na kutumia madau madogo ambayo yalikuwa yakitumika kuwavukisha.
Wasafiri hao kisha walitakiwa kuunganisha upya na kuendeleza safari zao Kwa magari mengine ambayo yalikuwa yakisubiri upande mwingine. Hali hiyo ilikuwa imeathiri pakubwa uchukuzi na hata kupelekea miji mikuu kama vile Witu, Mpeketoni,Hindi,Mokowe na kisiwa cha Lamu kuanza kushuhudia uhaba wa bidhaa muhimu,ikiwemo chakula,mafuta ya petroli na dizeli kutokana na usafiri wa barabarani kukatizwa. Ni kutokana na hali hiyo ambayo iliisukuma serikali kuanzisha harakati za kurejelewa kwa usafiri wa barabarani Lamu kupitia ukarabati wa sehemu hiyo ya Gamba iliyoharibiwa na mafuriko. Kwa karibu kipindi cha juma moja sasa serikali kupitia kwa Mamlaka ya Ujenzi na Usimamizi wa Barabara kuu nchini (KeNHA), imekuwa ikiendeleza ukarabati,ikiwemo malori yaliyojazwa mchanga, mawe na kokoto yakifika Gamba kumwaga vifaa hivyo vya ujenzj kwa minajili ya kufunika shimo la barabara. Ni shughuli ambayo ilitekelezwa kwa mwendo wa konokono kwani matingatinga yaliyokuwa yakitumiwa kutandaza mawe hayo yalipata taabu kutokana na hali mbaya iliyokuwepo Gamba. Kufikia Jumatano aidha, mwanakandarasi wa mradi huo wa ukarabati tayari alikuwa amefaulu kuunganisha sehemu hiyo ya barabara iliyokatwa,hivyo kupisha wasafiri,japo wachache wa miguu wakianza kutumia sehemu hiyo kuvuka pande nyingine. Bw Emmanuel Wanyoike, mmoja wa watumiaji wa barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen, alishukuru serikali kwa juhudi zake katika kuhakikisha usafiri wa barabara unarejelewa. “Tumefurahia sana kuona bidii za serikali yetu tukufu ikikarabati eneo hili la Gamba lililokatwa na mafuriko. Japo ukarabati umechukua muda kabla uanze lakini twaona mwanga wa matumaini mbele. Najua kuna zile familia zinazomiliki magari ya kibinafsi ambazo tayari zilikuwa zimekata tamaa ya kufika Lamu au kutoka eneo hili kwenda kujumuika na ndugu,jamaa na marafiki kusherehekea sikukuu ya Krismasi na Mwaka Mpya. Nataka kuwaambia nipo hapa na tayari wenye miguu wameanza kuvuka kwani eneo limeunganishwa. Magari pia yataanza kupita hapa si kitambo,” akasema Bw Wanyoike. Naye Bw Abdulrahman Yusuf, mkazi wa Lamu, alishukuru kuona kwamba usafiri wa barabarani unarejelewa. Bw Yusuf alikumbuka mateso ambayo wakazi wa Lamu wamepitia hasa tangu usafiri wa barabarani kusitishwa kutokana na athari za mafuriko. “Kipindi cha majuma mawili yaliyopita kimekuwa cha dhiki si haba. Ila twashukuru kwamba angalau serikali imeonyesha kutujali kwa kukarabati eneo hili la Gamba lilillsombwa na mafuriko. Mimi ni mmoja wa wale waliovuka Gamba kwa miguu mnamo Jumatano baada ya barabara kuunganisha,” akasema Bw Yusuf. Wamiliki wa magari ya usafiri wa umma ni miongoni mwa wanaofurahia kukarabatiwa na kuunganishwa kwa barabara ya Lamu-Witu-Garsen. Bw Said Swaleh,mmoja wa makondakta wa mabasi ya usafiri wa umma yanayohudumia barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen, alitaja kurejelewa kwa usafiri barabarani kuwa mwanzo mpya kwao. “Hata sisi watoaji huduma za mabasi ya usafiri wa umma tumeumia. Biashara ilikosekana kipindi chote cha majuma mawili ya mafuriko. Kukarabatiwa kwa Gamba ni kumaanisha biashara ya usafiri imerejea sasa. Twashukuru angalau familia zetu zitapata riziki,” akasema Bw Swaleh. Barabara kuu ya Lamu-Witu-Garsen ndicho kiunganishi cha pekee cha Lamu na maeneo mengine ya Kenya, hasa kwa wale wanaotumia usafiri wa nchi kavu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA WINNIE ATIENO MALALAMISHI yameibuka miongoni mwa wamiliki wa shule za kibinafsi baada ya wanafunzi wa shule za umma kusajiliwa kujiunga na shule za upili za kitaifa, wengine wao wakiwa na alama chini ya 400. Wamiliki hao wametaja hatua ya serikali kuwa ya ubaguzi wakiitaka Wizara ya Elimu kuwatendea haki watoto ambao walifanya mtihani wa kitaifa wa darasa la nane (KCPE) katika shule za kibinafsi. Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi ya Memon Academy iliyoko Mombasa, Joseph Ndoro, alisema hawakuridhishwa na uteuzi wa wanafunzi kujiunga na shule za upili mwaka huu. “Wanafunzi wangu bora ambao walipata alama 400 katika KCPE wameitwa shule za upili za hapa hapa tu karibu. Nilishangaa kuona wanafunzi wangu bora ambao walipata alama 406 na 405 wakiitwa Shule ya Upili ya Wasichana ya Mama Ngina na mwenzake akipata Kenyatta High,” alisema Bw Ndoro. Alisema kwa mara ya kwanza wanafunzi wake wamesajiliwa katika shule za Pwani badala ya zile za kitaifa zilizo Nairobi na sehemu nyinginezo za bara kama ambavyo imekuwa kawaida. “Sijaridhishwa na usajili na namna shughuli hiyo ilivyotekelezwa. Tulidhania wanafunzi wetu bora wangeitwa shule maarufu za kitaifa kama vile Alliance High, Pangani, ama Mang’u High lakini tulishangaa sana wameitwa Kenyatta High, Mama Ngina na Ribe Girls,” aliongeza. Walimu wenzake wakuu katika shule za kibinafsi nao walieleza kutoridhishwa na uteuzi huo wakiwataka viongozi wa kisiasa na wale wa kidini kuingilia kati suala la elimu wakisisitiza kuna dosari. Wamiliki wengine wa shule ya kibinafsi walitoa mfano wa shule ya umma huko Mombasa ambayo wanafunzi wake 23 walipata shule za kitaifa. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Muungano wa Kitaifa wa Wazazi, Silas Obuhatsa, na Mwenyekiti wa Kitaifa wa Muungano wa Walimu Wakuu, Johnson Nzioka, walisema hakukuwa na ubaguzi kwenye uteuzi huo. “Tunampongeza Waziri wa Elimu, Ezekiel Machogu, kwenye uteuzi huu ambao ulikuwa na usawa. Nimeona wanafunzi wote ambao walipata alama 400 wakipewa nafasi katika shule za kitaifa. Sijaona ubaguzi wowote,” alisema Bw Obuhatsa. Bw Nzioka alisema uteuzi huo ulifanywa kwa njia ya kielektroniki. “Tuwache kuweka dosari kwa kila jambo. Kwa mfano kama mwanafunzi alichagua Shule ya Upili ya Nyeri High ama Alliance High, halafu Alliance isajili wanafunzi kulingana na idadi yake ilhali wengi zaidi walitaka kujiunga na shule hiyo, tutalalamikia nini?” aliuliza Bw Nzioka. Alitoa mfano wa Shule ya Upili ya Kitaifa ya Wasichana ya Pangani jijini Nairobi ambayo wanafunzi 144,542 walikuwa wanataka kujiunga nayo licha ya kuwa na nafasi ya wanafunzi 384 pekee wa Kidato cha Kwanza. “Je tutaweza kusajili watoto wote 144,542 hapo Pangani Girls High?” aliuliza. Hata hivyo, Mwenyekiti wa Muungano wa Wamiliki wa Shule za Kibinafsi, Charles Ochome, alisema bado wanaendelea kuchambua uteuzi huo. “Ni mapema sana kutoa kauli yangu kuhusu uteuzi huu sababu bado tunaendelea kuchambua utaratibu uliotumika katika uteuzi huo. Tukimaliza tutazungumza,” alisema Bw Ochome. Hata hivyo, waziri Machogu, alieleza kuwa baadhi ya wanafunzi wapatao 28,052 ambao walipita mtihani huo wa kitaifa hawakupokea mialiko ya kujiunga na shule zozote za kitaifa kwa sababu hawakuzichagua. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA EVANS JAOLA SERIKALI ya Kenya inapoteza mamilioni ya pesa katika ulaghai wa bima ghushi za magari unaohusisha maajenti wa kampuni zinazotoa huduma, upelelezi wa Kitengo cha Uchunguzi wa Udanganyifu wa Bima (IFIU) na Chama cha kampuni za Bima Kenya (AKI) umefichua. Bw Linus Ogwango, Mkuu wa IFIU, alisema kuwa baadhi ya madereva kote nchini wanatumia vyeti ghushi vya bima bila kujua, ulaghai ambao unainyima serikali mapato. Akizungumza mjini Kitale, Kaunti ya Trans Nzoia wakati wa zoezi la siku mbili la ukaguzi wa magari, lililoendeshwa kwa pamoja na IFIU na AKI, Ogwango alisema waligundua magari kadhaa yalikuwa yakitumia vyeti ghushi vya bima. Bw Ogwango, ambaye ni kamishna wa polisi, alibainisha kuwa baadhi ya madereva wa magari hawakujua kuwa bima walizokuwa wakitumia ni ghushi ama kutoka kwa kampuni za bima zilizosajiliwa au kampuni ambazo hazipo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved

NA MHARIRI
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini.
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na BENSON MATHEKA
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na MASHIRIKA
LONDON, Uingereza
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved
Na KINYUA BIN KINGORI
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili.
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA