text
stringlengths 3
16.2k
|
---|
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
Tags |
You can share this post! |
Previous article |
Samidoh ang’aa Murang’a akitishia kuzima nyota ya... |
Next article |
UDAKU: Jua Cali adai Tanzania haina pesa mastaa wakifurika... |
T L |
You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MUNGUTI MASKWOTA wapatao 10,000 wamewasilisha upya kesi katika Mahakama ya Upeo wakiomba ibatilishe uamuzi kwamba wafukuzwe kutoka kwa shamba la ukubwa wa ekari 25,000 wanalong’ang’ania umiliki wake na familia ya mwanasiasa marehemu Mark Too. Maskwota hao wanaodai mababu zao ndio waliotimuliwa kutoka kwa shamba hilo enzi za ukoloni, wanasema walipewa shamba hilo rasmi na aliyekuwa Rais hayati Daniel arap Moi, kisha Kamishna wa Ardhi M Okundu akaratibisha uamuzi huo mwaka 2007. Katika ombi lililowasilishwa na wakili William Arusei chini ya sheria za dharura, kikundi cha maskwota hao–Sirikiwa Squatters Group–kimeomba mahakama ibatilishe uamuzi huo kwa vile ilitegemea ushahidi ambao haukuwa umewasilishwa katika kesi waliyoshtaki katika Mahakama ya kuamua kesi za mashamba (ELC), Eldoret, Kaunti ya Uasin Gishu. Pia wameeleza bayana Jaji Mkuu Martha Koome, Naibu Jaji Mkuu Philomena Mwilu, majaji Mohammed Ibrahim, Smokin Wanjala, Njoki Ndung’u, Isaack Lenaola, na William Ouko walitegemea ushahidi wa Afisa wa Ugavi wa Mashamba R J Simiyu kutoa uamuzi wang’atuke shambani. Maskwota hao wamesema ushahidi wa Bw Simiyu uliowasilishwa mbele majaji hao saba kwa njia ya afidaviti ni mpya na kamwe “haukuwasilishwa mbele ya Jaji Antony Ombwayo aliposikiliza na kuamua kesi hiyo 2017.” Pia wanasema ushahidi huo haukuwasilishwa Mahakama ya Rufaa iliyosikiliza rufaa iliyowasilishwa na kampuni ya Fanikiwa, familia ya marehemu Mark Too, kampuni ya Lonrho Agribusiness (EA) Ltd, na Bw David K Korir. Hivyo basi, maskwota hao wanaeleza mahakama hii ya upeo kwamba ni kinyume cha sheria kutegemea ushahidi mpya kutoa uamuzi wa kesi hii iliyo na umuhimu mkubwa kwa umma. “Uamuzi huu wa Mahakama ya Juu wa Desemba 15, 2023, hauna mashiko kisheria na kamwe hauna nguvu kisheria kuwatimua maskwota hawa kutoka kwa shamba lao,” asema Bw Arusei. Pia maskwota hawa wanadai kwamba badala ya Mahakama ya Juu kujadili masuala ya kikatiba jinsi ilivyo jukumu lake, majaji hao walianza kufafanua na kutafsiri ushahidi wa watu binafsi na kuelezea maana ya ‘skwota’. Mahakama hii imeombwa ikague upya uamuzi iliyotoa kwa vile ilidanganywa na walalamishi na pia kutendewa ujanja. Akinukuu maamuzi ya majaji wastahiki kama vile Lord Dening, Bw Arusei amesema, mahakama ikigundua ilipotoshwa au kudanganywa na upande mmoja, iko na mamlaka na uwezo wa kufutilia mbali uamuzi iliyotoa na kuandika mwingine. Maskwota hao wanaomba Mahakama ya Juu iwarudishe shambani kama ilivyokuwa imeamuliwa na Jaji Ombwayo na Mahakama ya Rufaa. Vile vile mahakama hiyo imekosolewa kwa kumshambulia hayati Moi katika uamuzi huo pasi kutoa agizo wasimamizi wa mali yake wafike mbele yao kutoa mwanga kuhusu suala la umiliki wa shamba hili lililorudishwa kwa serikali na kampuni iliyokuwa inakuza miti inayotumika katika viwanda vya ngozi. Naibu msajili wa Mahakama ya Juu Nelly Kariuki aliwaamuru maskwota hao wawakabidhi nakala za kesi hii yao mpya wahusika wote kabla ya Januari 31, 2024, kesi itakapotajwa tena kwa maagizo zaidi. Jaji aliyesikiliza kesi hii mpya hakuiratibisha kuwa ya dharura ila aliamuru pande zote ziwasilishe ushahidi katika muda wa siku 14 kuanzia Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA RICHARD MAOSI WAMILIKI wa nyumba za wapangaji mtaani Kayole wameamua kulala mchana na kukaa macho usiku ili kupambana na wahalifu ambao wametawala ploti zao. Aidha wapangaji wanapoendelea kufurahia sikukuu wakiwa mashambani, wezi kwa upande mwingine wanavunja nyumba na kuiba bidhaa kutoka ploti moja hadi nyingine. Mbali na Kayole, maeneo mengine ambapo wizi umeripotiwa ni Kangemi, Korogocho, Githurai, Umoja, Kariobangi, Starehe, Syokimau, na Buruburu. Wanavunja nyumba na kuiba vyombo, fanicha, mitungi ya gesi ya kupikia, televisheni, na redio, huku hatimaye bidhaa hizo zikiuzwa kwa bei ya kutupa mtaani. Bw Gilbert Ambani ambaye ni mlinzi katika mojawapo ya ploti eneo la Syokimau, anasema wezi wengi huko katika msimu huu wa shamrashamra wanalenga vyuma chakavu kwa sababu huwapatia hela za haraka. “Baadhi ya wezi wanabomoa lango kuu na kuchukua vyuma huku wengine wakivunja mifereji,” Bw Ambani akaambia Taifa Leo. Naye Amon Andika ambaye ni landilodi mtaani Kayole, alisema kwamba imemlazimu kufanya kazi ya ziada ya kulinda nyumba za wapangaji wake ambao wengi walienda mashambani almaarufu ‘ushago’. Anasema mwaka 2023 ameamua kufanya kazi ya usoja kama wengi wanavyoiita, baada ya kubaini kuwa baadhi walinzi wake wa awali walikuwa wakishirikiana na wezi kutekeleza wizi. Bw Andika ameingia gharama ya kuwekeza upya kwenye mradi wa maji baada ya wezi kuvunja mfereji wake usiku wa Desemba 24, 2023, na kutoweka na paipu ya thamani ya Sh70,000. Anasema kwa sababu ya hali ngumu ya kiuchumi, hana uwezo wa kuajiri soja wa usiku. Ndiposa imemlazimu kuhatarisha maisha yake kwa kulinda mali mpaka ifikapo Mwaka Mpya 2024. Anasema ni desturi yake kila mwaka wapangaji wanapokuwa wameelekea ‘ushago’ kufurahia sikukuu, yeye anadumisha usalama. Mnamo Desemba 27, 2023, washukiwa 34 wa wizi walikamatwa katika eneobunge la Starehe katika operesheni iliyoongozwa na chifu na maafisa wa polisi. Hali ni kinyume na baina ya mwaka wa 2020 na 2021 ambapo wakazi wengi wa jiji waliamua kutosafiri kwa sababu ya mlipuko wa janga la Covid-19. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA CHARLES WASONGA KIONGOZI wa Narc-Kenya Martha Karua amesema kuwa muungano wa Azimio La Umoja-One Kenya ulitoka mikono mitupu katika mazungumzo kati yake na mrengo wa Kenya Kwanza (KKA). Kwenye mahojiano na runinga ya Citizen mnamo Alhamisi usiku, Bi Karua alidai wanachama wa Azimio katika Kamati ya Kitaifa ya Mazungumzo (Nadco) walisaidia KKA kuendeleza ajenda zao. “Kwa mtazamo wangu, mazungumzo hayo hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu hakuna muafaka uliofikiwa kuhusu ajenda zetu tatu kuu ambazo ni gharama ya maisha, haki katika uchaguzi, na heshima kwa demokrasia ya vyama vingi,” akasema Bi Karua. Akaongeza: “Muafaka ulipatikana kuhusu ajenda za Kenya Kwanza kama vile kuundwa kwa afisi ya kiongozi rasmi wa upinzani, na kuhalalishwa kwa afisi ya Mkuu wa Mawaziri, ambazo tayari Ruto alikwisha kuwasilisha bungeni.” Kiongozi huyo wa Narc Kenya alieleza kuwa vikao vya kamati ya Nadco vilivyodumu kwa miezi minane vilikuwa ni vya kuwapotezea Wakenya hela na muda kwa sababu serikali haikuongozwa na nia njema iliposhiriki mazungumzo na upinzani. “Mazungumzo hayo yalilenga kutuchezea shere na kutuliza maandamano. Matokeo ya mazungumzo yetu na utawala wa KKA hayakuzaa matunda yoyote kwa sababu Wakenya bado wanaumizwa na kupanda kwa gharama ya maisha. Kwa mtazamo wangu, ripoti ya Nadco haina maana yoyote kwa Wakenya kwa sababu haishughulikii madhila yao,” Bi Karua, ambaye alikuwa ni mgombea mwenza wa Raila Odinga katika uchaguzi wa urais wa Agosti 9, 2022, akaongeza. Alielekeza lawama kwa utawala wa Kenya Kwanza kwa kile alichodai ni kufeli kufikiwa kwa malengo ya mazungumzo yake na upinzani. “Licha ya sisi kama upinzani na wananchi kuendelea kuushinikiza utawala huu upunguze gharama ya maisha, walipuuza na badala yake kuendelea kuongeza bei ya bidhaa za kimsingi na kuanzisha aina nyingine za ushuru,” akasema. Ili mazungumzo yoyote yafaulu, kulingana na Bi Karua, chama au mrengo ulioko mamlakani ni sharti kuonyesha nia njema kwa sababu wao ndio wanasukumwa kutimiza matakwa ya wananchi. Kiongozi huyo wa Narc-Kenya aliutaja utawala wa sasa kama ambao hauheshimu sheria na maamuzi ya mahakama. “Utawala huu unaendesha majukumu ya serikali kwa namna ambayo haijeshimu sheria na kudharau maoni ya wananchi ulivyofanya wakati wa ukusanyaji maoni ya umma kuhusu Sheria ya Fedha,” akasema. “Unapodharua Katiba na watu ambao walikupa mamlaka na matakwa ya wengi, unageuka serikali mbaya,” akaeleza alipoulizwa sababu yake ya kuirejelea serikali hivyo. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA FARHIYA HUSSEIN MWAKA 2023, unyama uliokuwa ukifanywa ndani ya wa Shakahola katika Kaunti ya Kilifi, ulifichuliwa ambapo zaidi ya watu 400 walipoteza maisha yao kwa itikadi kali za kidini. Mhubiri Paul Mackenzie ambaye alitajwa kuwa kiongozi wa wafuasi wake, anachunguzwa kwa madai ya kuwapotosha katika mafundisho ya kidini ambapo waumini walichanganyikiwa, wakiwemo watoto, wakaanza kufunga au kususia chakula hadi wakaanza kudhoofika na hatimaye kuanza kuaga dunia mmoja baada ya mwingine. Habari hizo zilipofahamika, idadi hii ya watu waliopoteza maisha ilikuwa nyingi sana, jambo liloshangazaa ulimwengu mzima. Walionusurika waliozungumza na Taifa Leo alisema waliokufa waliambiwa wafunge hadi kufa ili wakutane na ‘Yesu’. Miezi tisa baadaye, miili zaidi ya 400 inaendelea kuhifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha muda katika Kaunti ya Kilifi, ukumbusho wa kusikitisha kuashiria msimamo wao mkali wa kidini waliofuatilia. Watu hawa, ambao walitajwa na jamaa zao kuwa watu wachangamfu na maisha hapo awali walionekana kuishi maisha ya kudhoofisha na ya hali ya kusikitisha, maisha yao yalikatishwa na imani zile walizofuatilia kwa kina. Msitu huo ambao hapo awali ulikuwa sehemu nzuri ya mandhari ya kiasili, sasa umekuwa shahidi kwa ukatili uliofanywa huko ndani. Shakahola, kijiji katika Kaunti ya Kilifi, kilikuwa kimegubikwa na ukimya wa kutisha kwa miezi kadhaa. Makazi hayo ambayo wanakijiji walitaja zamani yalikuwa ya uchangamfu na yenye shughuli nyingi, sasa yalionekana yametawaliwa na ukimya mkuu. Katika msitu huo wa Shakahola, nyumba zilikuwa za udongo huku zikiezekwa kwa mapaa ya makuti. Njia zilizokuwa na watu wengi sasa zilikuwa kimya kwa kutisha, kana kwamba wanakijiji walikuwa wametoweka wakiacha nyuma vitu vya kibinafsi kama vile Biblia, ushahidi kuwa waliondoka ghafla. Sahani zilizotelekezwa zilizofunikwa ziliashiria ‘mlo wa mwisho’ wa wafuasi wa Kanisa la Good News International la Mchungaji Paul Mackenzie, ambalo inadaiwa lilichochea wao kuchukua mkondo hatari wa kufunga hadi kufa. Katika mazingira haya ya kutatanisha, ambapo ibada inayodhaniwa ilikuwa imezama katika unabii wa apocalyptic, cha kusikitisha ni kwamba baadhi yao hawakunusurika katika safari ya kuenda katika Hospitali Kuu ya Malindi. Wahanga walizikwa bila mpangilio makaburi yao yakiashiria kuzikwa kwao kwa haraka. Miezi kadhaa baadaye, miili yao ilifukuliwa. Watu hawa walionekana kutengwa na kusukumwa kwenye ukingo wa jamii, sauti zao zikiwa zimenyamazishwa na nguvu za itikadi kali. Maisha yao yalipochukuliwa kwa uchungu, heshima waliyostahili katika umauti wa iliondolewa pia. Ni wale tu walioaga dunia wangejua ikiwa kweli walikutana na Mungu wao. Miili yao ilizikwa kwa haraka msituni Shakahola, jambo lililodhihirishwa na jinsi makaburi hayo yalivyofukuliwa ambapo kwa kila mojawapo, miili zaidi ya mmoja ilipatikana ndani. Waumini hao hawakuzikwa na sanduku kama ilivyo kwa Wakristo bali walifunikwa na blanketi na nguzo nyinginezo. Miezi tisa baadaye, chumba cha kuhifadhia maiti cha muda bado kimesalia katika hopsitali ya Malindi, ukumbusho wa mkasa uliotokea mwaka 2023. Waathiriwa wamesalia katika hali ya kutatanisha, utambulisho wao bado haujathibitishwa, hadithi zao kubaini kiini cha kilichotokea ndani ya msitu wa Shakahola bado haijabainika. Hata katika kifo, ibada iliwanyima utambulisho wao, na kuacha miili hiyo ‘haijulikani’ kutokana na ukosefu wa nyaraka zozote. Ukweli uligundulika ni kwamba baadhi ya wanachama hao walitoka kaunti za mbali katika mikoa mingine nchini, jambo la kutatanisha katika kutambua na kudai miili hiyo. Mwezi Mei, serikali ilianzisha mpango wa DNA kulenga familia zinazoshuku kuwa jamaa zao waliopotea au walioaga wanaweza kuhusishwa na msitu wa Kilifi’ Shakahola. Takriban miezi saba imepita tangu kuzinduliwa kwake, lakini familia zinalalmikia kungoja matokeo ya DNA kwa hamu. Miongoni mwa walioathiriwa ni Bw Rodgers Mwibo, ambaye anatafuta mama yake, dada yake, na mpwa wake amabye alisema ni wafuasi waaminifu wa mhubiri Paul Mackenzie kutoka Kanisa la Good News International, waliohamia kwenye msitu huo mwaka mmoja uliopita. Akielezea masikitiko yake, Bw Mwibo alieleza kuwa kufuatia tangazo la serikali, alitoa sampuli zake za DNA kaunti za Nairobi na Malindi. “Badala ya kupata faraja, huku kusubiri kwa muda mrefu kunazidisha kiwewe changu. Kila nikiona picha ya mama yangu, natamani sana uwepo wake, hata kama ni kumuaga tu,” alilalamika Bw Mwibo huku akihoji ufanisi wa taratibu za DNA za serikali. Kulingana na Bw Mwibo, uhakikisho ulitolewa kwamba matokeo yatatolewa mara moja baada ya ukusanyaji wa DNA. Hata hivyo, kile kilichoahidiwa kuwa kipindi kifupi kimeongezeka hadi mwaka mmoja, na kumuacha yeye na wengine katika hali ya huzuni ya kihisia moyo. “Ni katika nchi gani miili hubaki kuhifadhiwa kwenye friji huku familia zikistahimili uchungu huu?” aliuliza Bw Mwibo. Jamaa mwingine, Bi Mary Mwikali anabainisha kuwa hatajua iwapo dadake na mpwa wake ni miongoni mwa waliofukuliwa kutoka msitu wa Shakahola au la. Kusubiri kwa hamu kunaendelea, na kuwaacha wakihangaika na sintofahamu ikiwa wapendwa wao bado wako hai au ni miongoni mwa watu 400 na zaidi wakiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Malindi. Afisa wa Masuala ya Dharura katika Shirika la Haki Africa, Bw Mathias Shipeta, alisema wasiwasi wake ni kwamba serikali imechukua muda mrefu unaohitajika ili kulinganisha na kulinganua DNA. “Inachukua muda gani hadi ulinganishaji wa DNA ukamilike? Familia zinamaliza mwaka bila kujua jamaa zao waliko. Haijafahamika wazi kama wameaga dunia au wapo hai. Ili kulifunga suala hili, ulinganishaji wa DNA lazima ukamilike na kukamilika kwa wakati kabla ya mwisho wa mwaka,” Bw Shipeta alisisitiza. Mwezi Julai, sampuli 266 zilikusanywa kwa madhumuni ya utambulisho wa vinasaba DNA. Uchunguzi wa DNA ni ulinganifu wa kisayansi wa maelezo ya kinasaba ya watu wasiojulikana au waliokufa na yale ya watu waliotambuliwa (waliokufa au walio hai). Mchakato huo ni muhimu kwa sababu za kisheria na za kibinadamu. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MASHABIKI wa klabu ya Arsenal mjini Murang’a sasa wameonywa na wenzao wa Manchester United na Chelsea wajiandae kumpokea ndovu wao akianguka pasipo hiari kutoka juu ya mti kumaanisha kushuka katika jedwali la Ligi Kuu ya Uingereza (EPL). “Huku kulimwa ambako mmeanza kulimwa ni mwanzo tu wa namna ambavyo mambo yatakuwa magumu kwenu katika mzunguko wa pili,” akafoka Bw David Njuguna ambaye ni mshirikishi wa the Red Devils mjini humo. Cheo chake hakitambuliki rasmi na klabu ya Manchester United. Bw Njuguna alisema kwamba Arsenal kuwa juu ya jedwali hata kwa mwanya wa pointi 10 sio tishio kwa kuwa katika mkondo wa lala salama, wao huwa butu, wasio na maono na mwelekeo na lazima wajihujumu wao wenyewe kama ilivyokuwa msimu jana. Katika mechi ya usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, Arsenal walirambishwa magoli 2-0 na West Ham. “Hata hamna heshima na wawekezajj na mnatuchomea beti. Kwa kuwa sikuamini kabisa mngeshinda hicho kipute, nilikuwa nimebashiri timu zote mbili angalau zingejipa goli. Sasa ona hamkufunga hata la kukataliwa,” akafoka Stacy Keach, mfuasi wa Chelsea. Janga hilo kwa wanabunduki Arsenal limewaacha katika nafasi ya pili kwenye jedwali wakiwa na pointi 40 huku Liverpool ikibakia kidedea kwa pointi 42. Hii ina maana kwamba Man City ambayo iko na pointi 37 kwa sasa lakini ikiwa imecheza mechi 18 Arsenal ikiwa imecheza mara 19 itaifurusha kutoka nafasi hiyo ya pili iwapo itachapa Sheffield United hapo Jumamosi kwa ubora wa magoli. “Kuna uwezekano mkubwa kwamba Arsenal itaingia mwaka Mpya ikiwa nambari tano nyuma ya Liverpool, Man City, Aston Villa na Tottenham na kabla ya tufike mechi ya 27, hata West Ham, Man United… watakuwa mbele ya Arsenal,” akasema Junita Kasyoki ambaye anashabikia Man United. Ni usiku ambao wafuasi wa Arsenal hawakujibu mipigo, waliondoka polepole na kimyakimya kutoka kwa mkahawa wa Green Park ambapo wengi walikuwa wakifuatilia mtanange huo ulioanza saa tano na robo usiku. “Lakini hata hivyo kushindwa kwetu kulisaidia West Ham kuruka Man United katika jedwali. Tungeshinda mchuano huo Man U wangebakia nafasi ya sita lakini kung’atwa kwetu kulisaidia Mashetani Wekundu kuteremka hadi nafasi ya saba,” akajituliza Bw Simon Ngonjo. Kwa sasa, maombi ya Arsenal ni kuzuke mikosi ya kushindwa kwa timu zote zilizo katika kumi bora katika mechi ya 20 lakini wao washinde ndipo warejee juu ya jedwali na presha ya kutwaa ligi ipungue. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA MWANGI MUIRURI MWANAMUME mmoja wa umri wa miaka 33 aliuawa usiku wa kuamkia Desemba 29, 2023, kwa kupigwa na majirani wa wakwe zake baada ya kile kinadaiwa alijaribu kutekeleza mauaji katika boma hilo alimokuwa amelala na bibi yake. David Kimani alikuwa amesafiri kutoka kijiji cha Kiunyu kilichoko eneobunge la Gatanga kwa msingi kwamba alikuwa na nia ya kumuona mkewe waliyetengana, binti yake wa umri wa miaka sita na pia mama mkwe. Mwanamume huyo alikuwa ametengana na Bi Esther Nyawira, 28, kwa kipindi cha mwaka mmoja na nusu na katika shamrashamra za msimu huu wa sherehe, akafika kwa boma la wakwe Desemba 28, 2023, katika kijiji cha Mung’etho kilichoko eneobunge la Maragua, akisema alienda kuwajulia hali. Lakini hata baada ya giza kuingia, hakuonyesha nia ya kuondoka arejee kwao na ndipo akakubaliwa alale kwa nyumba ya mama mkwe akiwa na bibi huyo wake. Mwendo wa saa sita usiku, Kimani anasemwa kwamba aliamka na akatwaa kisu na akaanza kumshambulia bibi yake aliyekuwa amelala huku kwa sauti akiapa kumuua na kisha aue mama mkwe na pia mtoto. Kwa mujibu wa Kaimu Naibu Kamishna wa Murang’a Kusini Bw Joshua Okello, mwanamume huyo baada ya kujaribu mara kadha warejeane na bibi yake pasipo mafanikio, akaamua kufika katika boma hilo akijipamba kama malaika wa mauti. Aliongeza kwamba mshukiwa alimdunga mwanamke huyo visu vitano “mara moja umbavuni upande wa kulia na mara nne kwa mkono wa kulia, majeraha yote yakiwa matano”. Bw Okello aliongeza kwamba sauti za juu za mwanamume huyo zilimwamusha mama mkwe na alipiga nduru ambayo iliwavutia majirani waliofurika katika boma hilo huku mvamizi baada ya kuingiwa na taharuki akitimua mbio hadi nje ya nyumba na akaingia katika kichaka. “Huku mwaathiriwa akikimbizwa hadi hospitali ya Murang’a kutibiwa, majirani nao walizindua msako ulioishia kumnasa Bw Kimani akiwa amejikunyata ndani ya kichaka hicho na wakamuua kwa kumpiga kwa vifaa butu,” akasema Bw Okello. Afisa huyo aliongeza kwamba ndani ya mkoba ambao marehemu alikuwa nao kulikuwa na sumu ya kuua wadudu kwa mimea na pia waraka wa mauti unaoaminika ulikuwa umeandikwa na mwanamume huyo. “Alikuwa amefichua katika waraka huo kwamba alinuia kuua mama mkwe, bibi yake na mtoto wake wa kike aliyekuwa akiishi kwa wakwe hao na kisha yeye mwenyewe ajitoe uhai,” akasema. Mwanamume huyo alikuwa aidha ameteta kwamba mama mkwe ndiye alikuwa kizingiti cha ndoa yake kupata uthabiti na kwa kuwa hakuwa na nia ya kumpenda mwingine, akaafikia uamuzi wa kuwaua watatu hao na kisha naye ajitume kuzimu akome mahangaiko ya mapenzi. Bw Okello alisema kwamba “huu ni mkasa ambao ungeepukika iwapo mwanamume huyo ambaye alikuwa mfanyabiashara Jijini Nairobi angepata ushauri nasaha ili kuwajibika changamoto zake za kimapenzi ndani ya mashauriano”. Alisema kwamba “ndipo ifike kiwango hicho cha kupanga mauaji ni kumaanisha alikuwa akisaka mbinu ya kusuluhisha changamoto hiyo lakini akaamua kufuata ushawishi wa pepo mbaya kujipa afueni”. Huku akiwakemea waliomuua mwanamume huyo na kuahidi uchunguzi wa kunasa washukiwa, Bw Okello alisema “hata jamii inafaa kuwa macho kuwatambua wanaoonekana kusombwa na mawazo na usaidizi wa ushauri usakwe kabla ya vishawishi vya janga kuzuka”. Bw Okello alionya watu wa kijiji hicho cha Mung’etho kwamba “kwa sasa mnaweza kuwa mnasherehekea mkisema eti ni umati wa raia uliotekeleza mauaji hayo lakini wakati kutajitokeza shahidi aseme alikuona wewe ukishiriki mauaji hayo ndipo utajua ni watu binafsi wala si kundi ambalo huvunja sheria”. “Mchango wa raia katika kuimarisha usalama ni kupitia kutupasha habari kuhusu washukiwa na visa na wakimnasa mshukiwa, kazi yao inafaa tu kutuita tumtie mbaroni au wamwasilishe katika kituo cha polisi kilicho karibu,” akasema Bw Okello. Mwili wa marehemu ulipelekwa hadi mochari ya Murang’a. [email protected] You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA WANDERI KAMAU MUSTAKABALI wa Kanisa Katoliki uko kwenye njia panda barani Afrika, kufuatia agizo la Papa Francis kwa mapadre katika kanisa hilo kubariki wapenzi wa jinsia moja. Ingawa lengo kuu la agizo hilo linaonekana kama njia ya kuwavutia washiriki zaidi na kutowabagua watu hao, wachambuzi na wasomi wa masuala ya dini wanasema huenda agizo hilo lilitolewa bila Papa kupewa ushauri wa kina na uongozi wa kanisa hilo. Kanisa Katoliki lina mamilioni ya washiriki hapa Kenya na barani Afrika kwa jumla. Kulingana na takwimu kutoka kwa serikali, kanisa hilo ndilo linaloongoza kwa kuwa na washiriki wengi nchini, huku likifuatwa na makanisa ya Kiprotestanti. Tangu Papa Francis alipotoa agizo hilo, viongozi tofauti wa kanisa wameeleza na kutoa hisia tofauti, baadhi wakijitokeza wazi kulipinga. Baadhi ya viongozi wakuu ambao wamejitokeza kulipinga ni kiongozi wa kanisa hilo nchini, Askofu Philip Anyolo, ambaye pia ndiye Askofu Mkuu katika Dayosisi ya Nairobi. Kulingana na askofu huyo, agizo hilo linakinzana vikali na tamaduni za Kiafrika, hivyo hawataliruhusu. “Kiafrika, ndoa za jinsia moja hazikubaliki hata kidogo. Ndoa hizo pia zinaenda kinyume na mafunzo ya Biblia,” akasema Askofu Anyolo. Maaskofu wengine ambao wamejitokeza wazi kupinga agizo hilo ni Cornelius Odiwa wa Homa Bay na mwenzake wa dayosisi ya Eldoret, Askofu Dominic Kimengich. Askofu Odiwa alisema watafuata msimamo wa Askofu Anyolo, kwani ndiye kiongozi wa kanisa hilo nchini. Pia, alisema ndoa hizo hazikubaliki kabisa Kiafrika. Kando na viongozi wa Kanisa Katoliki, watu kutoka dini nyingine pia wameunga mkono pingamizi hizo. Baadhi yao ni Bw Samuel Kamitha, ambaye ni mwanahistoria na msomi wa masuala ya dini. Bw Kamitha pia ni mmoja wa waandalizi wakuu wa maombi maalum ambayo hufanyika Desemba 27 kila mwaka karibu na Mlima Kenya. Mnamo Jumatano, wakati wa maombi hayo, Bw Kamitha alisema hawatakubali hata kidogo tamaduni za kigeni kutumika kuharibu desturi asilia za Kiafrika. “Tunasimama kidete kupinga uhalalishaji wa ndoa za jinsia moja nchini. Hilo ni jambo linalokinzana kabisa na tamaduni zetu,” akasema. Maombi hayo yalihudhuriwa na Wakristo, Waislamu, watu wanaofuata dini za kitamaduni kati ya madhehebu mengine. Kutokana na hisia hizo, wasomi wa masuala ya dini wanasema kuwa mwelekeo huo mpya unafaa kuufungua macho uongozi wa Kanisa Katoliki kuhusu mustakabali wake barani Afrika. “Kikawaida, maagizo yote kutoka Vatican (makao makuu ya Kanisa Katoliki) huwa hayapingwi hata kidogo. Ni vigumu kusikia usemi au agizo la Papa likikosolewa au kupingwa. Hata hivyo, viongozi kadhaa wanapojitokeza wazi kupinga agizo lake, basi hiyo ni ishara wazi kuwa kuna tatizo kubwa ambalo lazima litatuliwe,” asema Dkt Rita Khamisi, ambaye ni msomi wa historia ya dini. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Fans Follow Us Subscriber © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
NA BARNABAS BII RAIS William Ruto Ijumaa, Desemba 22, 2023 alisema nafasi aliyopata ya kuliongoza taifa hili ni sehemu ya utabiri wa wazee wa jamii ya Wakalenjin kuhusu ufanisi wa kundi la rika lake la Kaplelach, “atakapotwaa uongozi wa taifa hili”. Akiongea nyumbani kwaka katika eneo la Sugoi, Turbo, Kaunti ya Uasin Gishu, Dkt Ruto alieleza kuwa sasa ni wajibu wake kuiwezesha nchi hii kupata ufanisi au iangamie. “Mimi ni mmoja wa wanachama wa rika la Kaplelach na ni fahari yangu kujitambulisha nao na kuchangia kutimia kwa utabiri wa wazee kwamba mmoja wetu ama atastawisha Kenya au ataiporomosha,” Dkt Ruto akaambia umati mkubwa wa watu waliokongamana nyumbani kwake eneobunge la Turbo. Alisema hayo jana, Ijumaa alipoandaa dhifa ya Krismasi kwa wakazi wa Uasin Gishu nyumbani kwake Sugoi. Dkt Ruto alitumia fursa hiyo kumshambulia mtangulizi wake Uhuru Kenyatta akisema rais huyo mstaafu alimrithisha hazina ya serikali isiyo na pesa zozote, akiilinganisha na ghala ambalo limetorokwa hata na panya. Alisema kwa muda wa miezi 15 ambayo ameshikilia wadhifa huo, amefaulu kurejesha imani ya wawekezaji, hali ambayo imefufua uchumi na kuboresha maisha ya wananchi. “Mnajua yale ambayo reggae na watu wa BBI walifanya kwa uchumi wetu. Nilipoingia afisini hakukuwa na chochote kwenye ghala, hata panya walikuwa wamelitoroka. “Tangu wakati huo nimefaulu kushawishi washirika wetu wa kimaendeleo na tumefufua uchumi licha ya kukosolewa na wapinzani wetu,” akasema Dkt Ruto. Mpango wa mageuzi ya katiba kupitia mchakato wa maridhiano (BBI) uliungwa mkono na Bw Kenyatta na kiongozi wa Azimio, Raila Odinga. Mahakama, hata hivyo, iliupiga breki. Hatua hiyo ilimfaidi pakubwa Dkt Ruto aliyetumia uamuzi huo kujipigia kura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa 2022. Rais Ruto aliambia wakazi wa Uasin Gishu kuwa yu katika tapo la viongozi ambao nia yao kuu ni kustawisha taifa hili. Rais ambaye alikuwa ameandamana na Mkewe Rachel Ruto, alisambaza zawadi mbalimbali kwa wakazi hao. Miongoni mwa zawadi hizo ilikuwa; unga wa mahindi, unga wa ngano, mchele, sukari, mafuta ya kupikia miongoni mwa bidha nyinginezo. Bidhaa hizo zilikuwa ni zawadi ya Krismasi kwa wakazi hao. Dkt Ruto aidha, alitumia nafasi hiyo kukariri kujitolea kwa serikali yake kupunguza gharama ya matibabu kupitia Sheria za kufanikisha Mpango wa Afya kwa Wote (UHC). “Chini ya sheria hii wale raia wasio na ajira ambao wamekuwa wakilipa ada ya Sh500 kwa mwezi kama mchango wa Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) sasa watalipa Sh300 pekee na kutibiwa maradhi yote yakiwemo Kansa,” Rais akaahidi. Dkt Ruto alisema ni makosa kwa watu fulani kuwenda kortini kusitisha miradi inayolenga kuimarisha maisha ya Wakenya kama vile mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. “Chini ya mpango wa ujenzi wa nyumba, nyumba 200,000 zitajengwa kila mwaka. Kufikia sasa zaidi ya watu 12,000 wameajiriwa katika maeneo 31 kunakojengwa nyumba hizo,” akasema Rais Ruto. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

JURGEN NAMBEKA, KEVIN CHERUIYOT na MERCY SIMIYU MAELFU ya watu kutoka sehemu tofauti nchini wanasafiri kuelekea maeneo mbalimbali kufurahia msimu huu wa sherehe, na kuuaga mwaka ambao umekuwa mgumu kiuchumi. Wakionekana kutotishika, wengi wao wako tayari kuukumbatia msimu wa Krismasi na Mwaka Mpya ili kujenga kumbukumbu za kudumu maishani mwao. Uchunguzi wa Taifa Leo Dijitali katika miji mingi mikubwa nchini, ulibaini kuwa kuna ongezeko la shughuli nyingi katika sekta ya uchukuzi kwa njia kama reli, barabara au hata anga. Katika eneo la Pwani kwa mfano, mikahawa mingi imejaa wageni hasa jijini Mombasa na Diani kutokana na idadi kubwa ya watu waliofika kwa sherehe hizo. Wenye vyumba vya malazi, maarufu kama Airbnb, wameongeza ada zao kwa hadi mara mbili. Jaribio la wanahabari wa Taifa Leo Dijitali kukata tiketi kwenye kampuni kubwa za mabasi, mashirika ya ndege na gari la moshi la Madaraka (SGR), liligonga mwamba, kwani zimejaa hadi Siku ya Krismasi. Hakuna nafasi yoyote iliyobaki hadi mwishoni mwa mwezi huu. Kwa mfano, mabasi ya kampuni ya Easy Coach kutoka Nairobi hadi Kisumu yamejaa hadi Desemba 24, huku yale ya kampuni ya Mash kutoka Nairobi hadi Kisumu, na Mombasa hadi Kisumu pia yalijaa kabisa hadi kesho, Jumapili, Desemba 24. Kampuni ya Easy Coach imeimarisha huduma zake za uchukuzi kwa kuongeza mabasi mengine 12 zaidi. Kampuni hiyo, ambayo huhudumu kati ya Nairobi hadi Magharibi mwa Kenya na Nyanza iliongeza nauli zake kwa Sh100. “Uamuzi wetu wa kuongeza nauli zetu kwa kiwango kidogo unalenga kuhakikisha hatuwafinyilii sana wateja wetu. Maeneo tunayohudumu kwa wingi ni Nyanza ya Kati, Magharibi na Nyanza Kusini. Tunahakikisha kuwa madereva wetu wanazingatia kikamilifu sheria na kanuni za barabarani. Watahudumu tu kwa hadi saa kumi ili kuhakikisha wanazingatia usalama barabarani,” akasema Bw Dennis Ouma, ambaye ndiye Meneja Mkuu wa Kituo cha Mabasi cha Easy Coach. Reli ya SGR, ambayo Wakenya wengi hupenda sana kuitumia kama njia ya haraka na nafuu ya usafiri, pia imejaa. Nafasi za usafiri kati ya Nairobi na Mombasa zitaanza kupatikana Desemba 30. Mashirika ya ndege pia yanavuna pakubwa msimu huu wa sherehe kutokana na idadi kubwa ya watu ambao wanasafiri. Katika shirika la ndege la Jambojet, juhudi za kikosi cha shirika la habari la Nation kukata tiketi za kusafiri kutoka Kisumu hadi Mombasa hazikufua dafu, baada yao kubaini kuwa nafasi zote za usafiri zimejaa hadi Desemba 30. Ni nafasi chache tu zilizopo za watu wanaosafiri kutoka Nairobi hadi Mombasa, kwani Sikukuu ya Krismasi 2023 inaendelea kukaribia. Vivyo hivyo, huduma za usafiri katika shirika la ndege la Skyward pia zinatafutwa na watu wengi. Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ) lililazimika kuongeza ndege moja zaidi ili kushughulikia idadi kubwa ya wasafiri katika msimu huu wa sherehe. Shirika hilo lilisema kuwa lilikodisha ndege aina ya A330 Airbus kutoka shirika la Hi Fly kutoka nchini Ureno. Ndege hiyo ina uwezo kubeba abiria 229. “Kutokana na ongezeko kubwa la wasafiri, tumelazimika kuongeza ndege moja zaidi ili kukidhi mahitaji yao ya usafiri.Kutokana na uwepo wa ndege hiyo, tunatarajia kuimarika kwa huduma za usafiri miongoni mwa abiria wetu,” akasema Afisa Mkuu Mtendaji wa shirika hilo, Bw Allan Kilavuka, kupiitia taarifa. Mabasi yanayosafiri kutoka Nairobi hadi Kisumu, Kitale, Bungoma, Eldoret na Busia, yanatoza abiria nauli ya Sh2, 000 kutoka Sh1, 700 huku wale wanaoelekea Kisii wakitozwa Sh1, 600. Katika nyakati za kawaida, abiria wanaosafiri hadi Kisunu, Eldotet na Kitale huwa wanatozwa kati ya Sh1, 000 na Sh1, 400. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA DAILY MONITOR MAMIA ya raia wa Uganda wanavuka mpaka wa Busia kuingia nchini Kenya ili kununua bidhaa kama vile vitambaa na mavazi kwa bei nafuu kabla ya sikukuu ya Krismasi. Bw David Basalirwa, ambaye ni mfanyabiashara na mkazi wa Wilaya ya Bugiri Mashariki nchini Uganda, anasema yeye hupendelea kununua mavazi kutoka Kenya. Bw Basalirwa anaeleza kuwa bei ni nafuu ikilinganishwa na masoko yaliyo karibu naye katika wilaya ya Iganga na miji mingine ya Uganda. “Huwa ninanunua nguo nyingi Kenya kwa Sh1,000 (sawa na Sh24,000 za Uganda), lakini kwa pesa hizi hapa Uganda mimi hununua nguo moja pekee,” Bw Basalirwa akasema akiongeza kuwa unafuu wa bei ya mavazi Kenya unampa ‘faida nzuri’ akiyauza kwao Uganda. Haya ni mabadiliko ya ghafla ikilinganishwa na awali kwani Wakenya wamekuwa wakifurika nchini Uganda kununua mavazi. Hali hii tofauti imechangiwa kwa kiasi fulani na kudororoa kwa thamani ya shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu ya Dola ya Marekani ambapo pia sarafu za mataifa ya kigeni zimeanza kupata nguvu. Mwaka 2022 Sh1 ya Kenya ilikuwa sawa na Sh35 za Uganda. Lakini sasa imeshuka thamani ambapo Sh1 ni sawa na Sh24.5 za Uganda katika kipindi cha zaidi ya mwaka mmoja. Bi Debora Babirye, aliyesafiri kutoka Wilaya ya Namayingo hadi mjini Busia mpakani mnamo Jumatatu kununua mapazia Kenya, anasema bei hizi nzuri zinasukuma wafanyabiashara kufurika Kenya kununua nguo ili wapate ‘faida nzuri’ katika msimu wa sherehe. Bi Babirye anasema alinunua jozi mbili za pazia kwa Sh400 (sawa na Sh9,000 za Uganda) na anatarajia kuuza kwa bei ya juu. Naye Bw Ivan Wandera, mkazi wa Busime katika wilaya ya Busia anadokeza kuwa alivuka mpaka kununua suruali kwa bei ya chini. “Nilinunua kila jozi ya suruali kwa Sh250 (sawa na Sh6,000 za Uganda). Bidhaa hizo huku zingenigharimu angalau Sh15,000 za Uganda hapa nyumbani (Uganda),” anaeleza. Mfanyabiashara wa Kenya katika Wadi ya Burumba Busia-Kenya Bw James Wanjala, anasema kuwa ‘ameshangazwa’ na idadi kubwa ya raia wa Uganda wanaoingia nchini Kenya kununua bidhaa, akiongeza kuwa hajawahi kuwaona wakijaa katika maduka ya Kenya. “Uchumi wa Uganda ni bora kuliko wa Kenya na raia wa Uganda wana pesa za kununua kwa bei yoyote,” akasema Bw Wanjala. “Tuna chini ya juma moja kufika Krismasi na bado sijanunua chakula na nguo za watoto na mke wangu,” akaongeza. Bw Baker Ssebanakitta, raia wa Uganda mkazi wa mpakani, anaeleza kuwa ameona Wakenya wakivuka mpaka kwenda Uganda kununua chakula na mavazi lakini raia wa Uganda aghalabu hununua mavazi. Mkazi wa Busia-Kenya Bw Eddy Juma naye akasema alikuwa Uganda kununua “mavazi bora” licha ya bei ya juu. Kwa moto uo huo Mkenya Bi Christine kutoka Kakamega anadokeza kuwa hupendelea kununua kitenge cha rangi tofauti na usanifu ambacho huvaliwa na wanawake wa Uganda kwa sababu ya “thamani yake nzuri.” Mfanyabiashara wa malimali Uganda mpakani, Bw Ibrahim Wairagala, anaeleza kuwa mauzo yake yako chini yakilinganishwa na miaka iliyopita. “Awali, Wakenya wangefurika madukani mwetu wakati wa Krismasi, lakini Krismasi hii, idadi iko chini,” alisema Bw Wairagara. Mjasiriamali wa vitambaa, Bw Francis Magambo, analaumu kufifia kwa nguvu ya shilingi ya Kenya dhidi ya sarafu nyingine kwamba kumeshusha biashara. TAFSIRI NA LABAAN SHABAAN You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MAOSI WAFUGAJI wadogowadogo kutoka Ongata Rongai katika Kaunti ya Kajiado na jijini Nakuru wamelalamika kuwa visa vya wizi wa kuku na bata vimeongezeka sikukuu za Krismasi na Mwaka Mpya zikibisha hodi. Wafugaji waliozungumza na Taifa Leo walisema wezi wamekuwa wakijifanya ni wateja ambao hufika kwa maboma yao kukagua kuku na bata, lakini wanaishia kuwavamia na kuiba ndege hao. Kwa kawaida soko huwa zuri msimu wa sherehe kwa sababu watu hupenda kuchinja kuku na bata pamoja na ng’ombe, mbuzi na kondoo kuandaa nyama kwa ajili ya sherehe. Bi Agnes Warui ambaye ni mfugaji kutoka mtaa wa Mafuta Taa, anasema eneo hilo si salama kuendesha shughuli za ufugaji na kilimo. “Hii ni kwa sababu vijana waliopotoka kimaadili wanategemea uhalifu kujikimu kimaisha,” akasema Bi Warui. Bi Warui anasema aliachana kabisa na shughuli ya kufuga baada ya wahalifu kumvamia mnamo Desemba 2022 na kuiba kuku wake wote, jambo ambalo lilimkatisha tamaa. Hakika anasema biashara ya kuku na bata ni nzuri hususan msimu huu wa sherehe za mwisho wa mwaka. Hali ni kama hiyo katika mtaa wa Rhonda, Kaunti ya Nakuru ambako ndiko unyakaji wa kuku umeongezeka sana. Mitaa mingine ambayo imeripoti wizi wa kuku na bata ni Kaptembwo, Kiamunyeki, Machanga, Freearea, na Murogi. Kwa sababu hiyo, wakazi wameamua kutengeneza makundi kwenye mitandao ya kijamii wakitafuta kuku na mifugo yao ambayo imepotea Taifa Leo imebaini kuwa bei ya kuku imepanda kutoka Sh500 na sasa wanauzwa kwa hadi Sh1,200 mmoja. Kamishna wa Kaunti ya Nakuru Loyford Kibaara amewahakikishia usalama wakazi wa Nakuru msimu huu wa sikukuu ya Krismasi na sherehe za kupisha na kukaribisha Mwaka Mpya. Katika hafla ya hapo awali aliwahakikishia wakazi kuwa watafurahia Krismasi katika mazingira salama huku akiwaomba maafisa wa polisi, machifu, na wazee wa Nyumba Kumi kuwa macho. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA LABAAN SHABAAN RAIS William Ruto amemteua James Kipsiele Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Huduma ya Vijana kwa Taifa (NYS) kwa kipindi cha miaka mitatu kuanzia Desemba 20, 2023. Haya ni kwa mujibu wa Gazeti Rasmi la Serikali ambapo Rais alisema: “Nikitekeleza mamlaka niliyopewa na sehemu ya 16 (1) ya Sheria ya 1 ya NYS, William Samoei Ruto, Rais wa Jamhuri ya Kenya na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, ninamteua James Kipsiele Tembur kuwa Mkurugenzi Mkuu wa NYS kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia Desemba 20, 2023.” Bw Tembur aliwabwaga Mbw Njiri Nelson Mugweru, Anjere Alfred Tom, Nakitari Humphrey Okuku, na Mbaruku Moses Njeru na kutwaa nafasi hiyo. Waliomezea mate kiti hicho walifanyiwa usaili wa kazi mnamo Desemba 4, 2023, katika makao makuu ya NYS Nairobi. Bw Tembur amekuwa akihudumu wadhifa huu akiwa kaimu baada ya kupokezwa mikoba ya uongozi na Bi Matilda Sakwa aliyekamilisha kipindi chake cha kuhudumu mnamo Aprili 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA ALEX KALAMA MAHAKAMA Kuu ya Malindi mnamo Ijumaa imemuachilia kwa dhamana aliyekuwa Waziri wa Utalii Najib Balala pamoja na wenzake wawili ambao walikuwa wameshtakiwa pamoja katika kesi ya ufujaji wa Sh8.5 bilioni za ujenzi wa Chuo cha Utalii cha Ronald Ngala kilichoko eneo la Vipingo katika Kaunti ya Kilifi. Wakiwa mbele ya hakimu mkuu James Mwaniki katika mahakama hiyo ya Malindi, watatu hao walikanusha mashtaka yanayowakabili. Hakimu hiyo amemuachilia Bw Balala kwa bondi ya Sh5 milioni na mdhamini wa kiasi sawa na hicho au pesa taslimu Sh1 milioni. Pia katibu Leah Adda Gwiyo ameachiliwa kwa dhamana inayofanana na ya Bw Balala. Naye mhandisi Joseph Odero ameachiliwa kwa bondi ya Sh3 milioni au pesa taslimu Sh800,000. Upande wa washtakiwa umewakilishwa na mawakili watatu ambao ni Bw Mohammed Balala, Bw Maurice Kilonzo, na Bi Lucky Mnyazi. Upande wa mashtaka umewakilishwa na Joseph Mwangi. Afisa wa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) aliyeiwakilisha ni Bi Gicheru. Kesi hiyo itatajwa tena Desemba 28, 2023. Hakimu Mwaniki amesema kuwa atatoa mwelekeo zaidi siku hiyo ya kutajwa tena kwa kesi hiyo. Bw Balala alizaliwa mnamo Septemba 20, 1967. Aliwahi kuwa mbunge wa eneobunge la Mvita katika Kaunti ya Mombasa. Vile vile, alikuwa kinara wa chama cha Republican Congress Party of Kenya (RC) ambacho kilikuwa sehemu ya vyama vilivyotengeneza muungano wa Jubilee. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA CHARLES WASONGA RAIS wa Tanzania Samia Suluhu Hassan alichukua hatua ya kijasiri zaidi kwa kuvunja bodi ya Kampuni ya Usambazaji Umeme Tanzania (Tanesco), kutokana na ongezeko la visa vya kupotea kwa umeme. Juzi, Tanzania, sawa na Kenya, ilikumbwa na hitilafu ya kupotea kwa umeme kote nchini humo. Nchi hiyo imekuwa ikikumbwa na tatizo hilo kutokana na kiwango cha chini cha umeme unaozalishwa, hali ambayo imechangia kuanzishwa kwa mpango wa utoaji kawi hiyo kwa vipimo. Hata hivyo, nchini Kenya, kupotea kwa umeme kote nchini kumechangiwa na hitilafu zinazokumba nyaya za kusambaza kawi hiyo wala sio upungufu katika uzalishaji. Hata hivyo, Kenya na Tanzania zimeshughulikia changamoto hiyo kwa njia tofauti. Serikali ya Kenya imependekeza kutenganishwa kwa nyaya za kusambaza umeme na hamna afisa yeyote aliyechukuliwa hatua kutokana na hitilafu ya kupotea kwa kawi hii. Lakini nchini Tanzania, Rais Suluhu amevunja bodi ya kampuni ya Tanesco huku akimteua mwenyekiti wake Paule Kisesa Simuli kuwa balozi mpya wa nchi hiyo nchini Uganda. Nafasi ya Simuli amekabidhiwa Dkt Rhimo Nyanzaho, mkurugenzi wa kitengo cha biashara katika Benki ya Azania. Visa vya kupotea kwa umeme nchini Tanzania vinachangiwa na kupungua kwa maji katika mabwawa na ukarabati wa nyaya na nguzo za umeme unaoendelea. Kenya imekumbwa na visa vya kupotea kwa umeme kote nchini mara tatu ndani ya miezi sita huku kisa cha hivi punde kikitokea mnamo Desemba 10, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

PCS na CHARLES WASONGA RAIS William Ruto na Mama wa Taifa Rachel Ruto mnamo Ijumaa walisambaza zawadi za Krismasi kwa wakazi wa eneobunge la Turbo huku wakiwatakia Wakenya Krismasi njema na Mwaka Mpya wa fanaka. Wawili hao walisambaza vyakula mbalimbali ikiwemo unga wa mahindi, mafuta ya kupikia, unga wa ngano, mchele, sukari miongoni mwa vingine. Wakati huo huo, Rais Ruto alikariri kujitolea kwa serikali yake kupunguza gharama ya matibabu kupitia sheria za kufanikisha Mpango wa Afya kwa Wote (UHC). “Chini ya sheria hii, wale raia wasio na ajira ambao wamekuwa wakilipa ada ya Sh500 kwa mwezi kama mchango wa Bima ya Kitaifa ya Afya (NHIF) sasa watalipa Sh300 pekee na kutibiwa maradhi yote ikiwemo kansa,” Rais akaeleza. Rais alisema ni makosa kwa watu fulani kuenda kortini kusitisha miradi inayolenga kuimarisha maisha ya Wakenya kama vile mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu. “Chini ya mpango wa ujenzi wa nyumba, nyumba 200,000 zitajengwa kila mwaka. Kufikia sasa, zaidi ya watu 12,000 wameajiriwa katika maeneo 31 kunakojengwa nyumba hizo,” akasema Rais Ruto. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA PHILIP MUYANGA ALIYEKUWA Waziri wa Utalii Najib Balala na Katibu Leah Gwiyo wameshtakiwa Ijumaa katika Mahakama ya Malindi kwa matumizi mabaya ya ofisi. Wamefikishwa mbele ya hakimu mkuu wa Malindi James Mwaniki ambapo wamekanusha mashtaka. Kwa mujibu wa nakala ya mashtaka, wanadaiwa kutumia vibaya mamlaka yao kwa kuzipa kandarasi kampuni za Baseline Architects Ltd, Ujenzi Consultants, Armitech Consulting Engineering, na West Consult Consultant Engineers. Hatua hiyo ilikiuka uamuzi wa Baraza la Mawaziri wakati huo ambapo wawili hao wanadaiwa kupuuza na kutafuta huduma kutoka sekta ya kibinafsi ambapo malipo yasiyofaa ya Sh3.3 bilioni yalielekezwa kwa kampuni hizo kwa huduma za mchoro wa mradi, kuandaa stakabadhi, kusimamia na kuendeleza mradi wa chuo cha Utalii cha Ronald Ngala. Mshtakiwa mwingine ambaye ni Bw Joseph Odero akifanya kazi kama Westconsult Engineers amekanusha shtaka la kupokea kiharamu malipo ya Sh292.4 milioni kutoka kwa mfuko wa Tourism Fund ambayo awali ilifahamika kama Catering and Tourism Development Levy Trustees. Mahakama inatarajiwa kutoa uamuzi wake kuhusu kuachiliwa ama kwa bondi au dhamana ya pesa taslimu ifikapo saa tisa alasiri. Upande wa mashtaka haukupinga washtakiwa wakiachiliwa kwa dhamana. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA ALEX KALAMA ALIYEKUWA Waziri wa Utalii katika serikali ya utawala wa Jubilee Bw Najib Balala amefikishwa katika Mahakama Kuu ya mji wa Malindi akisubiri kujua hatima yake kuhusu kesi ya ufisadi inayomkabili ya ubadhirifu wa fedha za umma takriban Sh8.5 bilioni za ujenzi wa chuo cha utalii cha Ronald Ngala kilichoko eneo la Vipingo katika Kaunti ya Kilifi. Bw Balala na aliyekuwa Katibu wa wizara Leah Adda Gwiyo pamoja na Joseph Odero, wanakabiliwa na mashtaka 10 ikiwemo ufujaji wa fedha hizo zilitolewa katika hazina ya Tourism Fund kwa minajili ya ujenzi wa chuo hicho. Bw Odero ni mhandisi wa West Consult Engineers. Msemaji wa Tume ya Maadili na Kukabiliana na Ufisadi (EACC) Bw Eric Ngumbi alisema Bw Balala alikamatwa jijini Nairobi na ambapo baadaye akasafirishwa kwa ndege hadi Mombasa kabla ya kupelekwa katika mahakama ya Malindi kukabiliwa na mashtaka. “Wamekamatwa baada ya Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (ODPP) kuidhinisha mashtaka,” amesema Bw Ngumbi. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA RICHARD MAOSI MSONGAMANO mkubwa wa magari unaendelea kushuhudiwa katika barabara ya Nairobi-Nakuru, Wakenya wakielekea mashambani almaarufu ‘ushago’ kusherehekea sikukuu ya Krismasi na kuukaribisha Mwaka Mpya wakiwa na jamaa zao. Mnamo Ijumaa, barabara za kuingia na kutoka jijini pia zimefungika hasa maeneo ya Kimende, Kijabe na Flyover. Aidha nauli zimepanda baadhi ya walionuia kusafiri wakilazimika kusalia jijini kuendelea na shughuli zao. Bw David Omungala ambaye ni mkazi wa Freehold Nakuru, anasema nauli baina ya Nakuru hadi Luanda ni Sh2,000 ila tatizo ni uhaba wa magari. “Wasafiri wengi wanatatizika maana inabidi wakae steji hadi saa 10 usiku wakisubiri magari ya usafiri wa umma,” amesema Bw Omungala. Hata hivyo kwa sababu yeye ni mwendeshaji pikipiki, ameamua mwaka huu atasafiri mashambani kwa kutumia pikipiki yake, takriban mwendo wa zaidi ya kilomita 250. Bw Omungala anasema mwaka huu hakutarajia kwamba wasafiri watakuwa wengi ikizingatiwa kuwa gharama ya maisha imewabana wananchi. Taifa Leo pia ilizuru baadhi ya steji katikati mwa jiji la Nairobi ambapo nauli kati ya Nairobi na Kisumu ilikuwa si chini ya Sh2,500. Katika kituo cha magari ya uchukuzi wa umma cha Odeon, madereva wa magari ya kibinafsi wanatoza hadi Sh3,000, na hali itaendelea kuwa mbaya endapo wasafiri watazidi kuongezeka. Ifahamike kwamba Waziri wa Uchukuzi Kipchumba Murkomen alionya mtindo huo wa wenye magari ya kibinafsi kutumia kipindi cha shamrashamra kusafirisha abiria, akitishia kwamba serikali itawachukulia hatua kali kisheria. Katika Kituo cha Prestige Shuttle, nauli kati Nairobi na Nakuru ni Sh1,000 kinyume na nauli ya awali ya Sh600. Kwa sababu ya matatu kuwa chache magari ya kibinafsi yanatoza wasafiri Sh2,500 kati ya Nairobi na Eldoret, hii pia ikiwa na hatari zake kwa mujibu wa waziri. Hili linajiri siku chache tu baada ya vyuo na taasisi kufungwa wakati mmoja na sikukuu za mwisho wa mwaka. Magari mengi yalikuwa yamekodishwa kwa ajili ya sherehe za mahafala, Chuo Kikuu Cha Moi kikiwa ni cha punde zaidi kuendesha zoezi la kufuzu kwa mahafala mnamo Alhamisi, Desemba 21, 2023. You can share this post! Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |

NA MHARIRI |
BAADHI ya shule nchini zimejitokeza na kupinga matokeo ya Mtihani ya Darasa la Nane (KCPE) yaliyotangazwa Jumatano na Waziri... NA MHARIRI |
SERIKALI za kaunti zitalazimika kutafuta mbinu za usimamizi wa fedha iwapo magavana wanataka kujitolea kutimiza ahadi zao kwa... NA MHARIRI |
KILA Juni 14, ulimwengu huadhimisha Siku ya watu kuchangia damu duniani. Mwaka huu, kaulimbiu ilikuwa “Utoaji damu ni suala... NA MHARIRI |
UCHAGUZI mkuu wa Agosti 9 ulikuwa wa kipekee kwa jinsi ulivyokuwa na ushindani mkali kuliko mwingineo wowote ambao umewahi... NA MHARIRI |
MNAMO Ijumaa Rais William Ruto alipozuru eneo la Magharibi mwa Kenya, alisisitiza ahadi yake ya kuhakikisha kuwa viwanda vya... NA MHARIRI |
TANGAZO la Benki Kuu ya Kenya (CBK) kwamba wateja wataanza kutozwa ada ya kutoa pesa kutoka kwa benki hadi simu zao linajiri... NA MHARIRI |
RIPOTI ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali inayoonyesha kuwa mabunge ya kaunti yanapitisha bajeti kiholela bila kuhusisha... NA MHARIRI |
MKOPO wa Hustler Fund ulioanza kutolewa kwa wananchi wenye uwezo mdogo kimapato mnamo Jumatano huenda usiwafaidi raia jinsi... NA MHARIRI |
UZINDUZI wa Hazina ya Hustler jana Jumatano sasa unawapa matumaini mamia ya mama mboga, wanabodaboda na wafanyibiashara ndogo... NA MHARIRI |
HATUA ya serikali kuondoa marufuku dhidi ya mahindi ya GMO imezua mjadala mkali nchini. |
Suala la GMO limetekwa nyara na... NA MHARIRI |
KWA wiki chache sasa, kumekuwa na wasiwasi katika baadhi ya sehemu za nchi kuhusu homa ambayo inaonekana kuenea kwa... NA MHARIRI |
RIPOTI kwamba wabunge, kupitia Tume ya Huduma ya Bunge (PSC), wanataka kushinikiza Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC)... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na BENSON MATHEKA |
NAIBU wa Rais William Ruto atatumia muungano ‘ulioundwa’ mwaka 2021 na kiongozi wa Amani National Congress (ANC)... Na WANDERI KAMAU |
Naibu Rais William Ruto na waandani wake wameapa kufanya kila wawezalo kulemaza juhudi za Kiongozi wa ODM, Raila Odinga... Na CHARLES WASONGA |
WABUNGE wandani wa Naibu Rais William Ruto jana walifaulu kuzuia kupitishwa kwa Mswada tata wa marekebisho ya Sheria... BRIAN OCHARO na VALENTINE OBARA |
UBABE wa kisiasa kati ya Kiongozi wa ODM, Bw Raila Odinga, na Naibu Rais William Ruto katika Kaunti ya... Na CHARLES WASONGA |
HATUA ya Naibu Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga kushikilia kuwa wawaniaji wanaounga azma zao za... Na WANDERI KAMAU |
SUALA lililozua gumzo wiki hii ni majibizano yaliyozuka kati ya mrengo wa Naibu Rais William Ruto na mwanasiasa Maina... Na JUSTUS WANGA |
GAVANA wa Meru Kiraitu Murungi amekiri kwamba umaarufu wa Naibu Rais William Ruto umekita mizizi zaidi katika eneo la... Na CECIL ODONGO |
INASIKITISHA kuwa Naibu Rais Dkt William Ruto na Seneta wa Baringo Gideon Moi sasa wanalitumia suala la msitu wa Mau kwa... Na WYCLIFFE NYABERI |
NAIBU Rais Dkt William Ruto amemshambulia Rais Uhuru Kenyatta huku akisema ataondoka mamlakani bila kulipa deni la... Na CHARLES WASONGA |
NAIBU Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila Odinga wanaonekana kuendeleza mbinu za kampeni za kulambana visigino... Na IAN BYRON |
HATUA ya Gavana Okoth Obado kujihusisha na siasa za chama cha United Democratic Alliance (UDA) cha Naibu Rais, Dkt William... BENSON MATHEKA NA CHARLES WASONGA |
?WASHIRIKA wa Naibu Rais William Ruto wamegeuka kupe kwa ‘ kufyoza mamilioni ya fedha anazoyapa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na MASHIRIKA |
LONDON, Uingereza |
WAZIRI Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, jana alitangaza masharti makali kudhibiti maambukizi ya... Na ELIZABETH MERAB |
WANASAYANSI wanachunguza kuhusu mchipuko wa virusi vipya vya corona aina ya Delta, katika nchi za Amerika, Uingereza,... Na MAUREEN ONGALA |
MASAIBU ambayo wagonjwa wa Covid-19 hupitia katika kaunti za Pwani, yameanikwa wazi baada ya kifo cha afisa mkuu wa... SIAGO CECE na ANTHONY KITIMO |
UFISADI miongoni mwa baadhi ya maafisa wa serikali katika mpaka wa Kenya na Tanzania, umezidi kuwaweka... Na WAANDISHI WETU |
WINGU la maangamizi limetanda kote nchini huku aina mpya ya corona maarufu kama 'Delta' ikiua watu kwa... Na WINNIE ONYANDO |
HUENDA visa vya wasafiri kulazimishwa kupima upya corona mpakani mwa Kenya na Tanzania vikakoma baada ya serikali hizo... NA WANGU KANURI |
AGIZO la serikali la kudhibiti mkurupuko wa ugonjwa wa corona mwaka jana limewashurutisha Wakenya wengi kufanyia kazi... Na Titus Ominde |
VIONGOZI wa kidini Kaskazini mwa Rift Valley (North Rift) wameshutumu wanasiasa kwa kupepeta usambazaji wa virusi vya... Na WANTO WARUI |
Huku wanafunzi wa kidato cha kwanza wakiripoti katika shule zao mpya za sekondari hii leo, kuna uwezekano wa maambukizi... Na CHARLES WASONGA |
NAKUBALIANA na kauli ya maafisa wa afya katika kaunti ya Nairobi kwamba wanasiasa ndio wanachochea ongezeko la visa... Na SAMMY WAWERU |
DICKSON Muceri amekuwa mkazi wa Nairobi kwa muda wa miaka kadhaa ila sasa kitovu hicho cha jiji kuu la nchi hakikaliki... Na MARY WANGARI |
WANASAYANSI wamethibitisha kuwa kuchelewesha upokeaji dozi ya pili ya chanjo ya Covid-19 kwa kiasi cha miezi 10 baada ya... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Na KINYUA BIN KINGORI |
WAKATI huu viongozi wa kisiasa wameanza mapema kampeni zao kwa kuzuru maeneo mbalimbali nchini, ili kushawishi... Na WANDERI KAMAU |
KULINGANA na Ripoti ya Jaji Mstaafu Akilano Akiwumi (1997) kuhusu chimbuko la ghasia za kikabila nchini, wanasiasa ndio... Na WANTO WARUI |
KWA mara nyingine tena tuzo inayoenziwa sana kote ulimwenguni imerudi katika eneo letu la Afrika Mashariki mara hii... Na DOUGLAS MUTUA |
MWAFRIKA akiwajibishwa na Mzungu hupiga kamsa na kudai anaonewa, ati msingi wa maonevu ni ubaguzi wa rangi... Na WANDERI KAMAU |
MOJA ya changamoto kuu zinazokikumba kizazi cha sasa nchini ni ukosefu wa ufahamu wa lugha zao asili. |
Ingawa lugha... Na KINYUA BIN KINGORI |
JUHUDI za kuhakikisha taifa limefanikiwa kupiga vita ufisadi lazima ziendeshwe kuambatana na Katiba, bila njama... Na WANDERI KAMAU |
UFICHUZI wa sakata ambapo watu maarufu duniani wamekuwa wakificha mabilioni ya fedha katika akaunti za siri ng’ambo... Na FAUSTINE NGILA |
NINA imani kuwa iwapo kufikia sasa hujawahi kuelewa teknolojia ya blokcheni, leo utaelewa kwa kuwa jana uliathirika... Na CHARLES WASONGA |
NI jambo la kusikitisha kuwa ni wakati kama huu ambapo uchaguzi mkuu unakaribia ndipo wanasiasa wametambua umuhimu wa... Na MARY WANGARI |
IDADI ya watu wanaoandaa hafla za uchangishaji pesa za kugharamia matibabu imeongezeka pakubwa katika siku za hivi... Na CECIL ODONGO |
CHAMA cha Kanu bado kina safari ndefu kurejelea umaarufu wake wa enzi za utawala wa chama kimoja na miaka ya 90 hata... Na CHARLES WASONGA |
UTEUZI wa waliokuwa maafisa wanne wa ngazi za juu katika Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) kushikilia nyadhifa... Be our fan Follow us Join us Subscribe our newsletter to stay updated © Copryright 2023 Taifa Leo. All Rights Reserved |
Naomi Wamboi, 21, ndiye anatupambia yeye ni mwanamitindo aliyewahi kushinda tuzo za Miss Nakuru. Akipata muda anapenda kusafiri na... Winnie Miriam Nechesa 21, ni mwanafunzi kutoka Chuo Kikuu Cha Maasai Mara kaunti ya Narok.Anapenda kuchora, na kujumuika na... Lilian Njeri mwenye umri wa miaka 21 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mwanamitindo na mkaazi wa Narok.Uraibu wake ni kusafiri na... Mary Njeri mwenye umri wa miaka 21 ni mkaazi wa mtaa wa Langalanga kaunti ya Nakuru.Yeye ni mwanafasheni wa mapambo na vipodozi.Uraibu wake... Marylene Watiri mwenye umri wa miaka 22 ni mtaalam wa Beauty Therapy jijini Nairobi, aidha yeye ni mwanamitindo na mlimbwende.Uraibu wake... Zaweria Njoki mwenye umri wa miaka 21 ni Video Vixen kutoka kaunti ya Nakuru.Uraibu wake ni kuandika makala ya kitaaluma na kujumuika na... |
Malkia wetu leo ni Babra Ingasiani mwenye umri wa miaka 21, yeye ni mzaliwa wa kaunti ya Kakamega.Uraibu wake ni kusakata densi ya... Pauline Kimani mwenye umri wa miaka 23 ndiye anatupambia jarida letu leo.Yeye ni mkaazi wa eneo la Lanet na mfanyikazi mjini Nakuru.Uraibu... |