_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_889_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Uhamisho huu unaitwa hijra na tangu khalifa wa pili Umar ibn al-Khattab huhesabiwa kuwa ni chanzo cha kalenda ya Kiislamu. |
20231101.sw_889_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Mjini Yathrib mtume aliendelea kuwa kiongozi wa kisiasa na wa kijeshi. Alifanya mapatano na watu wa Yathrib iliyoitwa baadaye "madinat an-nabi"" ikajulikana kwa kifupi kama Madina. |
20231101.sw_889_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kutoka Madina mtume alianza kushambulia misafara ya watu wa Maka akawashinda mara kadhaa. Wakati huohuo aliwafukuza Wayahudi wa Yathrib. |
20231101.sw_889_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Mwaka 628 viongozi wa Maka walilazimishwa kufanya mapatano na Waislamu na mwaka 630 jeshi la Waislamu liliingia mjini Maka. |
20231101.sw_889_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Uislamu unawafunza wafuasi wake mambo mengi yanayohusiana na maisha, ikiwa yale yanayohusu ibada kama Sala, Zakat, Saumu na Hija; ambazo pamoja na kauli ya Shahada ("Nakiri kwa moyo na kubaini kwa ulimi kwamba hakuna Mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na Muhammad ni Mtume wake") huitwa nguzo za Uislamu au yale yanayohusu maingiliano baina ya wanadamu, yakiwa maingiliano ya kijamii kama ndoa na talaka na ujirani mwema, au ya kiuchumi kama biashara, au ya kisiasa kama kawaida za kumchagua kiongozi wa dola, au ya uhusiano baina ya mataifa mbali mbali ulimwenguni. |
20231101.sw_889_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Uislamu unatazamwa kuwa mfumo kamili wa maisha ya binadamu, kiimani, kimaisha, kisiasa, kijamii na kiuchumi. |
20231101.sw_889_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Ibada katika Uislamu ni vile vitendo ambavyo Muislamu anamfanyia Mwenyezi Mungu peke yake, kwani ibada yoyote haitakikani iwe na ushirikina ndani yake, na wakati itakapokuweko aina yoyote ya shirki basi ibada ile inakuwa haina maana wala thawabu wala ujira wowote, ni kazi ya bure. |
20231101.sw_889_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kwa hiyo, kila Muislamu anatakikana wakati anapofanya ibada yake afanye kwa ajili ya Mola wake aliyemuumba akampa kila aina ya neema na kumtukuza kuliko viumbe vingine vyovyote, kwa kumpa akili, fahamu na elimu.Nguzo zauislamu :(Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani) [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]. |
20231101.sw_889_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kuna matendo kadhaa ambazo zinaitwa "Nguzo za Uislamu". Kwa kawaida ni tano zinazofundishwa katika madhehebu ya Wasunni jinsi inavyoonyeshwa hapo chini. |
20231101.sw_889_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Washia hawahesabu shahada kati ya nguzo tano wakiona shahada pamoja na imani ya Kiislamu ni msingi kwa nguzo tano halafu wanaongeza "wilayat" yaani kukubali uongozi wa Maimamu kama nguzo ya tano . |
20231101.sw_889_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Shahada: (Kiarabu: الشهادة) Nguzo ya kwanza katika Uislamu hujumuisha kutoa kauli mbili: Hakuna Mola apasaye Kuabudiwa ila Allah na Muhammad ni Mtume wake. Kauli hizo hutolewa pale mwanadamu anapoingia Uislamu. |
20231101.sw_889_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Salat: (Kiarabu: صلاة) ni sala inayofuata utaratibu maalumu mara tano kila siku: Asubuhi, mchana, alasiri, jioni na usiku. Kabla ya kuingia katika ibada hii Mwislamu anapaswa kufanya wudhu ambayo ni tendo la kutakasa mwili kwa maji au -kama hakuna- kwa kutumia vumbi badala yake. Salat ina maneno yake na pia namna ya kusimama au kujinama. Salat hii ni tofauti na dua (دعاء) au sala ya kuomba kwa hiari. |
20231101.sw_889_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Zakat: (Kiarabu: زكاة) Nguzo ya tatu ya Uislamu nayo ni ibada inayomuelekeza Mwislamu kuwaangalia Waislamu wenzake kwa hali na mali, na kushughulikia mahitaji yao ya maisha, kwa kutoa fungu la mali yake asilimia 2.5 kila mwaka kwa mwenye uwezo na kuwapa wale walio maskini na wasiojiweza ili nao waweze kuishi vizuri. |
20231101.sw_889_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Funga/Saumu: (Kiarabu: صوم) Wakati wa mwezi Ramadani kila Mwislamu anapaswa kufunga chakula na kinywaji chote kuanzia asubuhi hadi jioni. Watoto na wagonjwa hawapaswi kutekeleza wajibu huu. Waislamu wanaona maana ya ibada hii kumkurubisha Mwislamu na Mola wake na kumfanya amche na kumuogopa zaidi, kwani saumu humsaidia Mwislamu kufahamu shida na taabu ambazo wale wasiokuwa na uwezo wanazipata wakiwa na njaa na hawana cha kukila, na kwa hivyo, huingiwa na huruma na kuwa na moyo wa kutaka kuwasaidia na kuwaondoshea shida hizo. |
20231101.sw_889_24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Hajj (Kiarabu: الحجّ alhajj): Kila Mwislamu mwenye uwezo anatakiwa kwenda hijja Maka mara moja katika maisha yake wakati wa mwezi Dhul-Hija. Nguzo hii inawapa fursa Waislamu ulimwenguni kukutana na wenzao na kujua hali zao na kupata nafasi ya kuomba maghfira na msamaha kwa madhambi yao katika mkutano mkubwa kabisa wa wanadamu ulimwenguni. |
20231101.sw_889_25 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Uislamu umeweka kawaida mbali mbali katika maisha wakati watu wanataka kuweka uhusiano fulani baina yao ili mambo yaende vizuri na uhusiano uzidi kuwa mwema baina yao. Katika maingiliano yaliyowekewa kawaida na nidhamu katika Uislamu ni mambo yanayohusu: |
20231101.sw_889_26 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kuna mielekeo mikubwa miwili ndani ya Uislamu ambayo ni vikundi vya Wasunni 85-90% na Washia 10-15%. |
20231101.sw_889_27 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kundi kubwa ni Wasunni waliopata jina kutokana na Sunna ("kawaida") ya mtume; takriban asilimia 85-90 ya Waislamu wote huhesabiwa humo. Kati yao kuna madhehebu 4 ambao ni Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafii. Tofauti katika mafundisho si kubwa, zinahusu hasa sharia na fikh. |
20231101.sw_889_28 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uislamu | Uislamu | Kundi dogo zaidi ni Washia ambao wamegawanyika kati yao katika vikundi vingi. Washia walijitenga na Wasunni baada ya makhalifa wanne wa kwanza kuhusu swali ni nani anayefaa kuongoza Waislamu. Washia ni wale waliosisitiza sharti awe mtu kutoka ukoo wa Muhammad kupitia binti yake Fatima. Vikundi vya Washia vinatofautiana juu ya viongozi hawa. Jumuiya kubwa ya Washia ni Ithnashara walio wengi huko Uajemi, Irak na Lebanoni. |
20231101.sw_890_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kurani (kwa Kiarabu: القرآن, Qur'an) ni kitabu kitukufu cha Uislamu ambacho kinaaminiwa na Waislamu kuwa ni "Neno la Allah (Mwenyezi Mungu)". Kitabu hicho kwao ni tofauti kabisa na maandiko ya dini nyingine kwa maana hicho kinaaminika kwamba kimeandikwa moja kwa moja na Mwenyezi Mungu, kupitia mtume wake wa mwisho, Muhammad. |
20231101.sw_890_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kadiri ya Qurani (42:8), Mungu alimuambia Muhammad: "Na namna hivi tumekufunulia Qurani kwa Kiarabu ili uwaonye watu wa Makka na walio pembeni mwake" |
20231101.sw_890_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Lakini, kwa vile leo Waislamu walio wengi ulimwenguni hawajui Kiarabu, maana halisi ya Qur'an hutolewa kwa lugha nyingine, hivyo kupelekea wasomaji kuelewa vyema yale maneno ya Kiarabu kwenye Qur'an yana maana gani. Vitabu hivyo ni kama kamusi kwa ajili ya Qur'an - hawavisomi hivi kama moja ya sehemu ya Quran na Waislamu, ili kuwa badala ya Quran ya Kiarabu. |
20231101.sw_890_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Waislamu wengi wanaamini kwamba tafsiri ile si ya Qur'an tukufu wala si ya kweli; ni nakala ya Kiarabu tu iliyotolewa kwenye Qur'an ya kweli. |
20231101.sw_890_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Waarabu wa kabla ya Uislamu waliunda hadithi na hadithi juu ya miti, visima na milima, na waliunda ibada zinazohusiana na miamba na milima huko Safa, Marwa, Abu Kubeys, Arafat, Mina na Muzdalifah. Ingawa Qur'ani ilifuta ibada nyingine, haikupingana na maandiko ya Kiarabu yenye mizizi, badala yake, iliendeleza sana ibada hizo. Wakati mwingine inakuwa vigumu kuelewa Qur'ani bila kujua mazoea ya zamani; kihistoria, wanadamu hawakutumia kipimo cha wakati kikubwa kuliko mwezi. Hivyo, mtu ambaye alisema, "Nina umri wa miaka 200." alikuwa akihesabu miezi, sio miaka. Kwa kweli alikuwa na umri wa miaka 16. "Tulimpeleka Nuhu kwa watu wake na akakaa kati yao kwa miaka elfu, isipokuwa miaka hamsini." (Ankebut: 14) |
20231101.sw_890_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kwa kuongezea vyanzo vilivyoandikwa, masomo mengi na mashujaa, ambayo mengine ni tu katika utamaduni wa hadithi za Kiarabu, yamefunikwa kwa kifupi katika lugha ya Kurani, na marejeo madogo yanafanywa. Hadithi za Yusuf na Züleyha, İsa, Musa, İskender / Zülkarneyn ni hadithi ndefu zaidi. Hadithi za uumbaji na mafuriko, ibada ya Ibrahimu na Dhabihu, hadithi za manabii wa Kiebrania, imani ya Kiyahudi na historia, kama vile kutoka kwa Waisraeli kutoka Misri, zinachukua nafasi kubwa katika Kurani. |
20231101.sw_890_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Waislamu wanaamini kwamba Qur'an mtume Muhammad alipewa na malaika Jibrīl kwenye pango la mlima Hira, kwa kipindi cha zaidi ya miaka ishirini na tatu hadi mauti yake ilipomfikia. |
20231101.sw_890_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Qur'an haikuwa kitabu cha maandiko wakati wa uhai wa mtume Muhammad; iliwekwa kwa mawasiliano ya kimdomo tu. Bimaana, watu walihifadhi kichwani. |
20231101.sw_890_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Mtume labda hakuwa anajua kusoma wala kuandika, lakini kwa mujibu wa Waislamu, swahaba wake Abu Bekr alikuwa akiandika maandiko yale juu ya kitu fulani wakati huo mtume Muhammad yu hai. Pale Abu Bekr alipokuja kuwa khalifa, ameileta Qur'an na kuwa kitabu kitakatifu. |
20231101.sw_890_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Uthman, ambaye ni khalifa wa tatu, ameondoa vipengele ambavyo vilikuwa havihusiani na Qur'an tukufu. |
20231101.sw_890_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kuna sehemu 30 katika Qur'an, ambayo inafanya kuwa na sura 114. Kila sura ina namba tofauti ya mistari. |
20231101.sw_890_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kwa mujibu wa mafunzo ya Kiislam, sura 86 kati ya hizi zimeshuka mjini Makka, sura 24 kati ya hizi zimeshuka mjini Madina. |
20231101.sw_890_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Miongoni mwa sura zilizoshushwa mjini Medina ni pamoja na Al-Baqara, Al Imran, Al-Anfal, Al-Ahzab, Al-Ma'ida, An-Nisa, Al-Mumtahina, Az-Zalzala, Al-Hadid, Muhammad , Ar-Ra'd, Ar-Rahman, At-Talaq, Al-Bayyina, Al-Hashr, An-Nasr, An-Nur, Al-Hajj, Al-Munafiqun, Al-Mujadila, Al-Hujraat, At-Tahrim, At-Taghabun, Al-Jumua, As-Saff, Al-Fath, At-Tawba, Al-Insan. |
20231101.sw_890_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Katika Qu'ran , inasomwa kwamba Wayahudi na Wakristo pia huamini Mungu wa kweli. Dini hizo pamoja na Uislamu huitwa Dini za Abrahamu kwa sababu ya mahusiano hayo. |
20231101.sw_890_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Kuna baadhi ya kurasa za Qu'ran zinazoelezea habari za mambo ya watu wa katika Biblia. Kwa mfano watu wa katika Biblia waliotajwa kwenye Qu'ran ni pamoja na Adamu, Nuhu, Abrahamu, Lutu, Ismaili, Yakobo, Yosefu, Haruni, Musa, mfalme Daudi, Solomoni, Elisha, Yona, Ayubu, Zekaria, Yohane Mbatizaji, Bikira Maria na Yesu. |
20231101.sw_890_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Hata hivyo, kuna tofauti za muhimu kabisa baina ya Uislamu na toleo la Biblia katika kuelezea habari za aina moja. Kwa mfano, Qu'ran inaelezea kwamba Yesu Kristo si Mwana wa Mungu, kama jinsi Wakristo wanavyoamini; kwa Waislamu, alikuwa nabii tu, anayeheshimiwa kwa jina la Isa bin Mariamu. |
20231101.sw_890_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Uislamu unafundisha kwamba haya yanatokea kwa sababu maandiko ya awali ya Biblia yamepotea na hivyo kuna baadhi ya watu wameyabadilisha. Lakini nje ya Qu'ran hakuna uthibitisho wa fundisho hilo. |
20231101.sw_890_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Kurani | Kurani | Sheria zinazotegemea matamshi na ufafanuzi wa Kurani ni shida leo kuzilinganisha na haki za binadamu, usawa wa kijinsia na dini ya binafsi na uhuru wa kusema. |
20231101.sw_891_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi au Sunnah ni maneno na vitendo ambavyo Mtume Muhammad alikuwa akisema au akifanya katika kipindi chake cha utume. Hadithi hizi ni mmoja kati ya miongozo ya imani kwa Waislamu. |
20231101.sw_891_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi hizi zinajumuisha pia mambo aliyoyaona au kuyasikia katika muda wa utume wake akalinyamazia kimya au akawa hakulipinga na akalikubali. |
20231101.sw_891_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Kisha Mwenyezi Mungu akamletea mjumbe kutoka kwake aitwaye malaika Jibrili anayeaminiwa na Waislamu kuwa ndiye aliyempa aya zilizoko katika msahafu wa Waislamu, Kurani. |
20231101.sw_891_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Inaelezwa kuwa Jibrili alimpa Muhammad aya hizo kwa muda wa miaka ishirini na mitatu mpaka alipofariki dunia akiwa na umri wa miaka 63. |
20231101.sw_891_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad zimekusanywa katika vitabu vingi sana na wanazuoni mbalimbali wa Hadithi, lakini vitabu vya hadithi ambavyo ni muhimu na vinategemewa na wengi katika Uislamu ni hivi vifuatavyo: |
20231101.sw_891_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Mtume Muhammad alikuwa hapendelei Hadithi zake ziandikwe wakati mmoja na Kurani, yasije yakachanganyika maneno yake na yale ya Mwenyezi Mungu. Kwa hiyo Hadithi zilichelewa kuandikwa mpaka baada ya kufariki kwake dunia kwa muda mkubwa kidogo, na kwa sababu hiyo Hadithi zikatawanyika sehemu mbalimbali kulingana na usahihi wake au udhaifu wake au uwongo wake. |
20231101.sw_891_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hivyo kuna Hadithi aina nne kulingana na fahamu na kutegemewa kwa msimulizi wa hiyo Hadithi: Hadithi Sahihi, Hadithi Hasan (Nzuri), Hadithi Dhaifu na Hadithi Maudhu'u (Hadithi ya Uwongo). |
20231101.sw_891_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Vile vile, kuna aina nyingine za Hadithi zilizogawanyika kwa mujibu wa mambo mengine kama vile: kwa mujibu wa wapokezi, au mfululizo wa wasimulizi, au idadi ya wasimulizi katika kila sehemu ya mfululizo, au kwa mujibu wa simulizi lenyewe na msimulizi wake. |
20231101.sw_891_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi Sahihi huwa imesimuliwa kutegemewa ukweli wake na dini yake na mtu ambaye anafahamu nini anasimulia, na kuieleza hadithi kama alivyoipokea kutoka kwa Mtume Muhammad. |
20231101.sw_891_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi Dhaifu huwa ile isiyofikia daraja ya Hasan, kwa sababu ya upungufu wa mmoja katika wasimulizi, au mfululizo wa wasimulizi haufikii mpaka kwa Mtume unakatika kwa mojawapo ya Masahaba, au mmoja katika wasimulizi si wa kutegemewa, na kuna kasoro fulani katika mambo haya. |
20231101.sw_891_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi Maudhu'u (ya Uwongo) ni ile hadithi iliyobuniwa ikatiwa katika Hadithi za Mtume, na huwa kawaida inakwenda kinyume na Qurani au Hadithi nyinginezo Sahihi au Hasan, au kutonasibiana na maneno yake Mtume au kuwa msimulizi wa Hadithi hii ni mwongo, au kuwa msimulizi hakukutana na yule ambaye amesema amepokea kwake katika mfululizo wa wasimulizi waliotajwa, au kuweko kasoro fulani katika maelezo au matukio yaliyotajwa ndani ya Hadithi hio. |
20231101.sw_891_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Hadithi%20za%20Mtume%20Muhammad | Hadithi za Mtume Muhammad | Hadithi Mauquf ni ile hadithi iliyosimuliwa na masahaba lakini wasiseme kuwa wameipokea kutoka kwa Mtume mwenyewe. |
20231101.sw_904_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Ukristo (kutoka neno la Kigiriki Χριστός, Khristos, ambalo linatafsiri lile la Kiebrania מָשִׁיחַ, Māšîăḥ, linalomaanisha "Mpakwamafuta" ) ni dini inayomwamini Mungu pekee kama alivyofunuliwa kwa Waisraeli katika historia ya wokovu ya Agano la Kale na hasa Yesu Kristo katika Agano Jipya ambaye ni mwanzilishi wake katika karne ya 1. |
20231101.sw_904_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Dini hiyo, iliyotokana na ile ya Wayahudi, inalenga kuenea kwa binadamu wote, na kwa sasa ni kubwa kuliko zote duniani, ikiwa na wafuasi 2,400,000,000 (33% kati ya watu 7.274 bilioni), ambao nusu ni waamini wa Kanisa Katoliki na nusu ya pili wamegawanyika kati ya Waorthodoksi (11.9%) na Waprotestanti (38%) wa madhehebu mengi sana. |
20231101.sw_904_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Karibu wote wanakubali Utatu Mtakatifu, yaani kwamba milele yote Mungu ni nafsi tatu zenye umoja kamili: Baba, Mwana na Roho Mtakatifu. Ni kwa jina lao kwamba mataifa yote wanahimizwa kubatizwa kwa maji, ili kuzaliwa upya, kadiri ya agizo la Yesu ili kuingizwa katika fumbo la Mungu pekee kupitia fumbo la kifo na ufufuko wake mwenyewe. |
20231101.sw_904_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kitabu kitakatifu cha Ukristo kinajulikana kama Biblia. Ndani yake inategemea hasa Injili na vitabu vingine vya Agano Jipya. |
20231101.sw_904_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Wakati wa Mababu wa Kanisa misingi ya imani ya Ukristo ilifafanuliwa na Mitaguso ya kiekumeni namna inayokubaliwa na wengi kabisa kati ya Wakristo wa leo. Maungamo yao yanakiri kwamba Yesu ni Mwana wa Mungu aliyefanyika mtu ili kuwaokoa binadamu. Baada ya kuteswa na kuuawa msalabani alizikwa ila akafufuka, siku ya tatu akapaa kwa Mungu akishiriki mamlaka ya Baba hadi atakaporudi kuhukumu waadilifu na wasiotubu, akiwapa tuzo au adhabu ya milele kadiri ya imani na matendo yao. |
20231101.sw_904_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Hivyo, kati ya madhehebu ya Ukristo, karibu yote yanamkiri Yesu kuwa kwa pamoja Mungu kweli na mtu kweli: katika umoja na nafsi yake ya Kimungu zinapatikana sasa hali hizo zote mbili. |
20231101.sw_904_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Yote yanamkiri kuwa Mwokozi wa watu wote, na kuwa ndiye atakayerudi mwishoni mwa dunia kwa hukumu ya wote, ingawa maelezo kuhusu jambo hilo yanatofautiana. |
20231101.sw_904_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Vilevile yote yanamchukua kama kielelezo cha utakatifu ambacho - kwa msaada wa Roho Mtakatifu na wa sakramenti zilizowekwa na Yesu mwenyewe, kuanzia ile ya ubatizo - kiwaongoze ndani ya Kanisa katika maadili yao maalumu, kuanzia unyenyekevu na upole hadi upendo unaowaenea wote, bila kumbagua yeyote, hata adui. |
20231101.sw_904_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Chimbuko la Ukristo ni mtu huyo aliyezaliwa takriban miaka 2000 iliyopita huko Mashariki ya Kati, katika kijiji cha Bethlehemu kilichopo hadi hivi leo kwenye mipaka ya Palestina; alikuwa akiitwa Yesu wa Nazareti (kijiji alikokulia) au mwana wa Yosefu mchonga samani,mama yake akifahamika kwa jina la Bikira Maria. |
20231101.sw_904_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kwa kumuita pia Kristo, wafuasi wake walikiri kwamba ndiye aliyetimiza utabiri wa manabii wa kale, kama unavyopatikana katika vitabu vya Biblia ya Kiebrania na Deuterokanoni. |
20231101.sw_904_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Habari za maisha na mafundisho yake zinapatikana kirefu zaidi katika Injili nne zilizokubalika, katika Agano Jipya kwa jumla, lakini pia ziliandaliwa na kutabiriwa na Agano la Kale. |
20231101.sw_904_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Ukristo ni matokeo ya utume wa Yesu, uliopokewa na waliomwamini kuwa ndiye Masiya, yaani mkombozi aliyetimiliza ahadi za Mungu kwa binadamu. |
20231101.sw_904_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika kitabu cha Mwanzo tunasoma utabiri wa kuja kwake ulianzia katika bustani ya Edeni pale Mungu alipomwambia nyoka, yaani shetani, kuhusu mwanamke kwamba "uzao wake utakuponda kichwa" (Mwa 3:15). |
20231101.sw_904_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Baadaye Abrahamu, babu wa taifa la Israeli, kwa imani na utiifu wake kwa Mungu, aliahidiwa kwamba katika uzao wake mataifa yote yatabarikiwa. |
20231101.sw_904_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Musa, mwanaharakati aliyewakomboa watu wa Israeli kutoka utumwani Misri takribani miaka 1250 KK (kabla ya kuzaliwa kwa Yesu), ndiye nabii wa kwanza kutabiri wazi kwa niaba ya Mungu ujio wa Masiya au Kristo (Kumb 18:15-22, hususan mstari 18: "Nitawainulia nabii kama wewe kutoka miongoni mwa ndugu zenu; na nitatia neno langu kinywani mwake na atasema nao yote niliyomwamuru." |
20231101.sw_904_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kuja kwake kulitimia katika Agano Jipya, ambalo ni ukamilifu wa yote yaliyotabiriwa katika Agano la Kale. Kwani Musa alitumwa kuanzisha Agano la Kale kama maandalizi ya Agano Jipya, akikabidhi mifumo mingi ya nje na ndani kwa watawala na waamuzi waliomfuatia watakaoshikilia Agano la kusubiri Masiya wakishirikiana na manabii na makuhani. |
20231101.sw_904_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Yesu alizaliwa miaka kama 1800 baada ya Abrahamu. Vitabu vya Injili vinaeleza matukio na mafundisho ya Yesu ambayo ndiyo mwongozo wa imani hiyo. Maisha na kazi ya Yesu vimeibua mambo mengi katika historia. Ndiyo sababu kalenda iliyoenea duniani huhesabu miaka kutoka ujio wake; huu ni mchango mmojawapo wa Ukristo katika ustaarabu. |
20231101.sw_904_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Nikodemu, mshiriki mmojawapo wa baraza la Sanhedrini, ambalo lilikuwa pia mahakama kuu ya Wayahudi, alivutiwa na kutaka kujua zaidi kuhusu siri ya miujiza hiyo na ujumbe kutoka kwa Mungu; kwani yeye alihamasika kuona ishara zile kutoka kwa Mungu. |
20231101.sw_904_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Yesu akamjibu kwamba hakika mtu hawezi kuingia ufalme wa Mungu asipozaliwa mara ya pili kwa maji na Roho Mtakatifu. |
20231101.sw_904_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Pia akajieleza kuwa mpatanishi wa ulimwengu wa dhambi na Mungu na kwamba kila anayemgeukia kwa imani hatapotea, bali atarithi uzima wa milele: alisema mwenyewe ni mfano wa nyoka wa shaba aliyetengenezwa na Musa. (Yoh 2:23-3:21; Hes 21:9). |
20231101.sw_904_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Akiwa kando ya Ziwa la Galilaya, Yesu alikuta umati wa watu umekusanyika. Basi akapanda mashuani na kuenda mbali kidogo na ufuoni, akaanza kuwafundisha kuhusu Ufalme wa mbinguni kupitia mfululizo wa mifano. |
20231101.sw_904_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Mmojawapo ni huu ufuatao: "Ufalme wa mbinguni ni kama punje ya haradali ambayo mtu anaipanda. Ingawa ni mbegu ndogo sana inakua na kuwa mti wa mboga mkubwa kuliko yote. Inakuwa mti ambao ndege wanauendea, wakipata makao katika matawi yake". (Math 13:1-52; Mk 4:1-34; Lk 8:4-18; Zab 78:2; Isa 6:9,10). |
20231101.sw_904_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Jumuia ya Wakristo inaitwa Kanisa, yaani "mkusanyiko" kama lilivyotajwa na Yesu mwenyewe hasa katika Injili ya Mathayo 16:18: "Wewe ndiwe Petro na juu ya mwamba huu, nitalijenga kanisa langu. Wala milango ya kuzimu haitalishinda". |
20231101.sw_904_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Yesu aliita wengine 11 pamoja na Petro kuunda kundi la mitume wake. Idadi yao ilipangwa kwa kusudi la kudokeza kwamba ndiyo mwanzo mpya wa taifa la Mungu, kama vile watoto 12 wa Yakobo Israeli walivyokuwa mwanzo wa taifa lake la kale. |
20231101.sw_904_24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Yesu na wanafunzi wake wa kwanza walikuwa Wayahudi. Yaani walizaliwa katika uzazi wa Abrahamu wakiwa watoto wa Agano lililofanywa kati ya Mungu na taifa lake la Israeli zamani za Musa. |
20231101.sw_904_25 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Wakati wa Yesu Waisraeli hao waliitwa "Wayahudi". Walio wengi waliishi nje ya nchi ya Israeli/Palestina, kutokana na vita vingi vya zamani vilivyosababisha wakimbizi kuhamia nchi zenye usalama zaidi. Jumuiya za Wayahudi zilipatikana katika miji yote mikubwa ya Afrika Kaskazini (hasa Misri na Libia), Ulaya Kusini na Asia Magharibi mpaka Uajemi. |
20231101.sw_904_26 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kwa upande mmoja Wayahudi walitoka katika ukoo wa Ibrahimu, hasa waliokaa Israeli/Palestina. Lakini watu wengine wenye asili ya mataifa tofauti waliwahi kujiunga na imani ya Wayahudi na kuchukua hatua ya kuongoka na kutahiriwa. |
20231101.sw_904_27 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika mazingira yao Wayahudi walikuwa watu wa pekee waliomshuhudia Mungu mmoja tu. Walikuwa tofauti na wengine kwani hawakushiriki katika ibada ya miungu ya serikali, tena walitunza utaratibu wa sabato yaani kutotenda kazi siku ya saba. |
20231101.sw_904_28 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Mitume wa Yesu walizunguka awali hasa katika jumuiya za Wayahudi kila mahali walipokwenda. Mwanzoni Kanisa lilionekana kama dhehebu la Kiyahudi tu. Baada ya kupokea watu kutoka mataifa bila kuwatahiri hali ilibadilika: Kanisa likawa taifa la Mungu kutoka kwa Wayahudi na kwa Mataifa. |
20231101.sw_904_29 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Mara baada ya Yesu kwenda zake katika tukio linalotajwa kupaa kwake mbinguni, wafuasi wake wakarudi Yerusalemu, yapata mwendo wa sabato, na walipoingia huko, wakapanda ghorofani walipokuwa wakikaa Mtume Petro na wenzake. |
20231101.sw_904_30 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Hata ilipotimia siku ya Pentekoste walikuwapo wote mahali pamoja. Ukaja upepo toka juu kama upepo wa nguvu ukienda kasi, ukaijaza nyumba yote waliyokuwa wameketi. Kukatokea na ndimi zilizogawanyikana, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao. Wote wakajazwa na Roho Mtakatifu, wakaanza kusema kwa lugha nyingine, kama Roho alivyowajalia. (Mdo 1:12-14, 2:1-4). |
20231101.sw_904_31 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Hii ilifuatiwa na Petro na wenzake kuanza kuhubiri ufufuko wa Bwana Yesu na hatimaye kugusa watu 3,000 waliokubali kubatizwa siku hiyo. (Mdo 2: 37-40). |
20231101.sw_904_32 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Watu walipokuwa wakidumu katika fundisho la mitume, sala, kumega mkate na katika ushirika, wengi wakaona ishara zao nyingi basi nao wakauza mali zao, na vitu walivyokuwanavyo, na kugawia watu wote kama kila mtu alivyokuwa na haja. |
20231101.sw_904_33 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Basi, siku zote kwa moyo mmoja walidumu ndani ya hekalu, wakila pamoja na kushiriki kwa moyo mweupe. |
20231101.sw_904_34 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kukutanika na kushiriki mafumbo makuu, kushukuru na kusifu, pamoja na uwepo wa vipaji na karama za Roho Mtakatifu, hufanya Kanisa liwe hai. |
20231101.sw_904_35 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Ujumbe wa Yesu ulienea haraka toka Yerusalemu hata Lida, Yafa, Kaisaria, Samaria, Damasko n.k. na kuanzisha jumuia nyingi. |
20231101.sw_904_36 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Nazo jumuia kwa bidii za waamini wa mwanzo zikafika Foinike, Kipro, Antiokia, ambako waliitwa Wakristo kwa mara ya kwanza, kutokana na waamini wa mataifa mengine kuwazidi wale wenye asili ya Kiyahudi (Mdo 11:1-23). |
20231101.sw_904_37 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Imani na desturi za mikusanyiko hiyo zenye asili ya Kiyahudi zilitapakaa na hivyo kuanza kusuguana na mapokeo ya jamii mbalimbali zilipopenya. Hii inatokana na ukweli kwamba watu wengi wa siku zile tayari walikuwa na imani zao walizokuwa wakizitunza. |
20231101.sw_904_38 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Basi ukaja wakati ambao Wakristo wakaanza kukosoana kuhusu dhamiri zao na huduma. Ndiyo asili ya nyaraka mbalimbali ambazo zinaunda sehemu muhimu wa Agano Jipya. |
20231101.sw_904_39 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kila jumuiya inatumia mbinu zake za uongozi. Mkuu wa jumuiya ya wanafunzi tangu mwanzo ni Bwana Yesu. Lakini kama kundi ni kubwa kazi ya uongozi ni tofauti. Haiwezekani kufanya kila kitu pamoja watu wakiwa wengi. Ipo lazima ya kugawana kazi na madaraka. |
20231101.sw_904_40 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Suala hili limekuwa muhimu sana katika historia ya Ukristo. Njia mbalimbali za uongozi ambazo zilitafutwa na kujaribiwa zinaonyesha tofauti muhimu kati ya madhehebu mbalimbali. Kwa jumla njia hizo zote zinajaribu kuiga mifano ya ushirika wa kwanza inayopatikana katika Biblia. Vyeo na shughuli maalumu zilizopo katika Ukristo leo, vina asili na mwanzo katika ugawaji wa madaraka ulivyokuwa wakati wa mitume. |
20231101.sw_904_41 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika nyaraka za Paulo (ambazo ni maandiko ya kwanza katika Agano Jipya) tunaona hali ya Ukristo mwanzoni kabisa. Paulo anataja mitume, manabii, walimu, wenye vipawa mbalimbali (1Kor 12,28 n.k.), au maaskofu na mashemasi, pia wazee. Kwa jumla hakuna picha kamili ya utaratibu mmoja uliokuwepo kila mahali. |
20231101.sw_904_42 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika ushirika wa kwanza kule Yerusalemu Mitume, yaani marafiki wa Yesu wa karibu waliotumwa naye na kupewa kazi ya kueneza Habari Njema, ndio waliokuwa viongozi. Lakini baada ya muda mfupi kazi zilikuwa nyingi, hivyo wakaongeza "Wasaidizi saba". Hao saba walishughulikia hasa huduma za upendo, yaani kuwagawia wajane na wazee misaada. |
20231101.sw_904_43 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Mwishoni mwa karne ya 1 cheo cha "Askofu" kiliimarika sana, lakini pia vikundi vya Wakristo wenye vyeo maalumu vya utumishi vilianza kutokea. Pamoja na Askofu vyeo vya Kasisi na Shemasi vilikuwa kawaida. Mashemasi wa kike walipatikana pia mwanzoni, lakini walipotea baadaye, kutokana na utamaduni uliokazia kipaumbele cha wanaume. |
20231101.sw_904_44 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Kuanzia mwaka 100 hivi Kanisa likaitwa "katoliki" maana yake Kanisa moja kwa ajili ya nchi zote na watu wote, tofauti na vikundi vilivyojitenga nalo. Kila mji ulikuwa na askofu wake aliyeongoza kanisa. Maaskofu wa eneo au mkoa mmoja walikuwa chini ya Askofu Mkuu. Maaskofu wa Roma (Ulaya hadi Afrika Kaskazini-Magharibi), Aleksandria (Afrika) na Antiokia (Asia), waliheshimiwa kuliko maaskofu wengine wote wakaitwa "Papa" na "Patriarki". Cheo cha Patriarki kilipatikana pia kwa Askofu wa Bizanti (leo nchini Uturuki) baada ya makaisari wa Roma kuhamia kule, na vilevile kwa Askofu wa Yerusalemu. |
20231101.sw_904_45 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika karne za baadaye vikundi mbalimbali vilianza kupinga kuwapo kwa vyeo maalumu vya utumishi. Walisisitiza zaidi "ukuhani wa Wakristo wote" maana yake kila Mkristo hushiriki utumishi ulio mmoja tu katika Kanisa. Madhehebu mengine ya Kiprotestanti, yakikumbuka sana matatizo ya utaratibu wa kiaskofu wakati wa karne za kati, yaliona afadhali kuendelea bila cheo hicho. Wakatoliki, Waorthodoksi, Waorthodoksi wa Mashariki pamoja na Wamoravian na Waanglikana wamehifadhi ngazi za kale yaani Uaskofu, Ukasisi na Ushemasi. Nchini Tanzania Walutheri pia Wabatisti wa aina ya A.I.C. wanaheshimu cheo cha Uaskofu. Lakini kimataifa sehemu kubwa ya Walutheri, na hasa Wapresbiteriani (Reformed) na Wabatisti hawana Askofu, wakisisitiza zaidi uwezo na haki ya kila Mkristo kushiriki katika shughuli zote za utumishi akichaguliwa. |
20231101.sw_904_46 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Imani ya Ukristo ni juu ya Yesu. Alikuja kwelikweli hapa duniani. Alichagua kuja katika nchi ile ya Israeli miaka 2000 iliyopita. Akawachagua wanafunzi wake ambao tunawaita "mitume". Hakika alikuwa na maana kufanya hivyo. Mitume ndio waliotekeleza maagizo ya Yesu, "Basi enendeni, mkawafanye mataifa yote kuwa wanafunzi, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na Mwana, na Roho Mtakatifu; na kuwafundisha kuyashika yote niliyoamuru ninyi; na tazama, mimi nipo pamoja nanyi siku zote, hata ukamilifu wa dhahari" (Math 28:19-20). Biblia inatupa habari za aina hii: wale Mitume ni mifano ya Ukristo wetu katika nguvu au karama zao, lakini pia katika udhaifu wao. |
20231101.sw_904_47 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Petro ni jina lenye maana ya "mwamba". Alikutana na Yesu akiwa mvuvi, akaendelea kuwa rafiki yake wa karibu sana. Yesu alipokamatwa, Petro alitaka kutumia upanga wake ili amtetee. Lakini alipoulizwa baadaye kama yeye ni rafiki wa Yesu aliogopa akasema hamjui. |
20231101.sw_904_48 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Katika ushirika wa Yerusalemu alikuwa kiongozi muhimu. Alikuwa Mtume wa kwanza kumpokea katika Kanisa watu wasio Wayahudi bila kudai watahiriwe kwanza. Baadaye akawa katika mji mkubwa wa Antiokia. Katika taarifa ya Luka tunamwona tena Yerusalemu alipokutana na Paulo na kushauriana juu ya kupokea Wapagani katika Ukristo. |
20231101.sw_904_49 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Agano Jipya ina nyaraka mbili zilizoandikwa kwa jina lake. Kumbukumbu ya kale inasema alifika mpaka Roma. Hapo aliuawa pamoja na Paulo katika mateso ya kwanza ya Wakristo chini ya serikali. |
20231101.sw_904_50 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo | Ukristo | Petro ni mfano mzuri wa nguvu na udhaifu katika maisha ya Kikristo. Alikuwa na moyo mkuu kumtetea Yesu kwa upanga asikamatwe - lakini mpaka siku ile hakuelewa kwamba njia ya Yesu si njia ya silaha. Alitaka kuwa karibu na Yesu - lakini kwa hofu akamkana. Alimwingiza katika Kanisa jemadari Mpagani - lakini baadaye akawaogopa waliosema kwamba Mpagani asiingie katika ushirika mpaka awe ametahiriwa na kuwa Myahudi kwanza. Mwishoni mwa maisha yake Petro akawa shahidi wa damu kwa Bwana wake kule Roma akafa msalabani kama Yesu. |