_id
stringlengths
15
22
url
stringlengths
31
150
title
stringlengths
1
86
text
stringlengths
100
23.8k
20231101.sw_904_151
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Hickman, Hoyt L. and others. Handbook of the Christian Year. Abingdon Press (1986). ISBN 0-687-16575-X
20231101.sw_904_152
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Hitchcock, Susan Tyler. Geography of Religion. National Geographic Society (2004) ISBN 0-7922-7313-3
20231101.sw_904_153
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Letham, Robert. The Holy Trinity in Scripture, History, Theology, and Worship. P & R Publishing (2005). ISBN 0-87552-000-6.
20231101.sw_904_154
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Lorenzen, Thorwald. Resurrection, Discipleship, Justice: Affirming the Resurrection Jesus Christ Today. Smyth & Helwys (2003). ISBN 1-57312-399-4.
20231101.sw_904_155
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
McLaughlin, R. Emmet, Caspar Schwenckfeld, reluctant radical: his life to 1540, New Haven: Yale University Press (1986). ISBN 0-300-03367-2.
20231101.sw_904_156
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
MacCulloch, Diarmaid, A History of Christianity: The First Three Thousand Years. London, Allen Lane. 2009. ISBN 978-0-7139-9869-6
20231101.sw_904_157
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Marber, Peter. Money Changes Everything: How Global Prosperity Is Reshaping Our Needs, Values and Lifestyles. FT Press (2003). ISBN 0-13-065480-9
20231101.sw_904_158
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Marthaler, Berard. Introducing the Catechism of the Catholic Church, Traditional Themes and Contemporary Issues. Paulist Press (1994). ISBN 0-8091-3495-0
20231101.sw_904_159
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
McClintock, John, Cyclopaedia of Biblical, Theological, and Ecclesiastical Literature. Harper &Brothers, original from Harvard University (1889)
20231101.sw_904_160
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
McManners, John. Oxford Illustrated History of Christianity. Oxford University Press (1990). ISBN 0-19-822928-3.
20231101.sw_904_161
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Meconi, David Vincent. "Pagan Monotheism in Late Antiquity", in: Journal of Early Christian Studies.
20231101.sw_904_162
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Metzger, Bruce M., Michael Coogan (ed.). Oxford Companion to the Bible. Oxford University Press (1993). ISBN 0-19-504645-5.
20231101.sw_904_163
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Norman, Edward. The Roman Catholic Church, An Illustrated History. University of California (2007) ISBN 978-0-520-25251-6
20231101.sw_904_164
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Orlandis, Jose, A Short History of the Catholic Church. Scepter Publishers (1993) ISBN 1-85182-125-2
20231101.sw_904_165
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Otten, Herman J. Baal or God? Liberalism or Christianity, Fantasy vs. Truth: Beliefs and Practices of the Churches of the World Today.... Second ed. New Haven, Mo.: Lutheran News, 1988.
20231101.sw_904_166
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Pelikan, Jaroslav; Hotchkiss, Valerie (ed.) Creeds and Confessions of Faith in the Christian Tradition. Yale University Press (2003). ISBN 0-300-09389-6.
20231101.sw_904_167
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Putnam, Robert D. Democracies in Flux: The Evolution of Social Capital in Contemporary Society. Oxford University Press (2002).
20231101.sw_904_168
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Riley-Smith, Jonathan. The Oxford History of the Crusades. New York: Oxford University Press, (1999).
20231101.sw_904_169
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Robinson, George. Essential Judaism: A Complete Guide to Beliefs, Customs and Rituals. New York: Pocket Books (2000).
20231101.sw_904_170
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Sykes, Stephen; Booty, John; Knight, Jonathan. The Study of Anglicanism. Augsburg Fortress Publishers (1998). ISBN 0-8006-3151-X.
20231101.sw_904_171
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Ustorf, Werner. "A missiological postscript", in: McLeod, Hugh; Ustorf, Werner (ed.). The Decline of Christendom in Western Europe, 1750–2000. Cambridge University Press (2003).
20231101.sw_904_172
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Walsh, Chad. Campus Gods on Trial. Rev. and enl. ed. New York: Macmillan Co., 1962, t.p. 1964. xiv, [4], 154 p.
20231101.sw_904_173
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
MacCulloch, Diarmaid. Christianity: The First Three Thousand Years (Viking; 2010) 1,161 pages; survey by leading historian
20231101.sw_904_174
https://sw.wikipedia.org/wiki/Ukristo
Ukristo
Roper, J.C., Bp. (1923), et al.. Faith in God, in series, Layman's Library of Practical Religion, Church of England in Canada, vol. 2. Toronto, Ont.: Musson Book Co. N.B.: The series statement is given in the more extended form which appears on the book's front cover.
20231101.sw_921_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza ni lugha ya jamii ya Kigermanik cha Magharibi iliyokua nchini Uingereza kwa muda wa miaka 1,400.
20231101.sw_921_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Leo, zaidi ya wasemaji milioni mia nne duniani wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya kwanza. Watu wengi zaidi wanazumgumza Kiingereza kama lugha ya pili, kwa sababu ni muhimu sana kwenye nyanja za mawasiliano, sayansi na uchumi wa kimataifa.
20231101.sw_921_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Lugha ya Kiingereza ilianzia huko Uingereza kutokana na kuingiliana kwa lugha mbalimbali, hasa lugha za kale za Ujerumani, Denmark na Ufaransa.
20231101.sw_921_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Sehemu ya kusini ya kisiwa cha Britania ilikuwa ndani ya Dola la Roma hadi mwanzo wa karne ya 5. Wenyeji walitumia lugha ya Kikelti pamoja na Kilatini cha Waroma, hasa mjini.
20231101.sw_921_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Baada ya Waroma makabila kutoka Ujerumani ya kaskazini na Denmark walianza kuvamia kisiwa hicho. Katika mwendo wa karne mbili waliteka sehemu kubwa ya Uingereza ya leo isipokuwa sehemu za magharibi kama vile Cornwall na Wales na sehemu za kaskazini walipoishi Waskoti.
20231101.sw_921_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Wavamizi walileta lugha zao za Kisaksoni na Kianglia (Ujerumani ya Kaskazini) zilizounganika kuwa lugha ya Kiingereza cha Kale ambacho kilikuwa karibu sana na Kijerumani cha Kale. Inaonekana ya kwamba wenyeji Wakelti walio wengi walianza polepole kutumia lugha ya watawala wapya, wengine waliuawa au walihamia sehemu zisizo chini ya Waanglia-Saksoni.
20231101.sw_921_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Lugha hii iliathiriwa mara mbili. Kwanza Wadenmark ndio waliojaribu kujenga ufalme wao kisiwani. Waliteka sehemu za Uingereza ya Magharibi. Kiasi cha maneno kutoka lugha yao kimeingia Kiingereza cha kale kama Wales.
20231101.sw_921_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Mwaka 1066 jeshi la Wanormani kutoka Ufaransa ya Kaskazini walivamia na kuteka Uingereza. Wanormani walikuwa wa asili ya Skandinavia lakini walikuwa wameshaanza kutumia lugha ya Kifaransa cha kale. Wanajeshi hao walikuwa mabwana wapya wa Uingereza wakitumia Kifaransa chao.
20231101.sw_921_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kwa karne kadhaa lugha mbili zilitumika kandokando: Kiingereza cha Kianglia-Saksoni cha watu wa kawaida na kile Kifaransa cha Kinormandy cha tabaka la watawala. Kwa jumla watawala walianza kutumia lugha ya raia lakini lugha hii ilibadilika pia kwa kupokea maneno mengi kutoka Kifaransa. Kuna makadirio ya kwamba zaidi ya theluthi moja ya maneno yote ya Kiingereza yana asili ya Kifaransa.
20231101.sw_921_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kipindi hiki cha kuingiliana kati ya Kifaransa cha mabwana na lugha ya kawaida kilileta Kiingereza cha Kati. Hadi leo asili ya maneno kutoka Kijerumani na Kifaransa ni wazi kabisa.
20231101.sw_921_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Mfano mzuri ni maneno tofauti kwa wanyama kadhaa na nyama yao: ng'ombe huitwa "cow" (sawa na Kijerumani wa Kaskazini "Kau") lakini nyama yake ni "beef" (kutokana na neno la Kifaransa kwa ng'ombe "boeuf"); vilevile "sheep" kwa mnyama kondoo na "mutton" kwa nyama yake (Kijerumani ya Kaskazini: "Schaap" - Kifaransa: "mutton"), vilevile swine=mnyama – pork=nyama (nguruwe) na calf=mnyama – veal=nyama (ndama).
20231101.sw_921_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Wakulima wafugaji walitumia lugha yao kwa mnyama - mabwana wasiogusa mnyama lakini hula nyama yake waliendelea kutumia neno la Kifaransa kwa ajili ya mnyama yuleyule. Maneno yote mawili yaliingia katika Kiingereza cha Kisasa lakini kwa mambo mawili tofauti.
20231101.sw_921_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza cha Kisasa kimeanza na tafsiri ya Biblia ya William Tyndale; baadaye na washairi muhimu kama William Shakespeare.
20231101.sw_921_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Teknolojia ya uchapaji vitabu ilisambaza lugha hii nchini kote na kupunguza athira ya lahaja mbalimbali.
20231101.sw_921_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Wakati ule Kiingereza kilipokea pia maneno mengi kutoka lugha za Kilatini na Kigiriki zilizokuwa lugha za taaluma na sayansi hadi karne ya 18 kote Ulaya.
20231101.sw_921_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza cha Kisasa kimeendelea kurahisisha lugha. Lakini urekebisho wa tahajia umeshindikana hadi leo hata kama kulikuwa na majaribio mbalimbali. Kutokana na historia yake Kiingereza kimebaki na tahajia isiyolingana na matamshi ya maneno.
20231101.sw_921_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Mwandishi George Bernhard Shaw alionyesha tatizo hilo kwa pendekezo la dhihaka kwamba neno "fish" (samaki) liandikwe "ghoti": gh kama sauti ya "f" katika "cough", o kama sauti ya "i" katika "women", na ti kama sauti ya "sh" katika "nation".
20231101.sw_921_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Pamoja na hayo, lahaja za Kiingereza zinazidi kutofautiana, zile muhimu zaidi zikiwa zile za Britania na Marekani.
20231101.sw_921_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Tangu karne ya 19 idadi kubwa ya wasemaji wa Kiingereza hawaishi tena Uingerezea bali Marekani. Katika karne ileile Kiingereza kilikuwa lugha ya utawala katika maeneo makubwa ya makoloni ya Dola la Uingereza.
20231101.sw_921_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kutokana na matukio hayo yote, na Marekani kujitokeza katikati ya karne ya 20 kama nchi tawala kisiasa, kiuchumi na kiteknolojia, Kiingereza kimekuwa leo lugha ya kwanza ya mawasiliano duniani hata kama si lugha yenye wasemaji wengi wa lugha ya kwanza.
20231101.sw_921_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza ni lugha rasmi pekee katika nchi za Uingereza, Marekani, Australia, Nyuzilandi, Jamaica, na nchi nyingine.
20231101.sw_921_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Kiingereza ni lugha rasmi pamoja na lugha nyingine katika nchi nyingi, kwa mfano Kanada (pamoja na Kifaransa), India (pamoja na Kihindi na lugha za majimbo), Ireland (pamoja na Kigaelik), Philippines (pamoja na Kitagalog).
20231101.sw_921_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Nchi nyingi za Afrika zinatumia Kiingereza kama lugha rasmi, lakini ni Waafrika wachache (isipokuwa Waafrika Kusini) wanaoitaja kuwa lugha ya kwanza kwao. Nchi hizo ni Afrika Kusini, Eswatini, Ghana, Kamerun, Kenya, Lesotho, Liberia, Namibia, Nigeria, Sierra Leone, Zambia na Zimbabwe.
20231101.sw_921_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kiingereza
Kiingereza
Lugha nyingi za Afrika zimekopa maneno ya Kiingereza. Maneno hayo yamerekebishwa kulingana na sauti ya lugha nyingine, kwa mfano: Kiingereza: train --> Kiswahili: treni.
20231101.sw_923_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Afrika ni bara la pili duniani kwa ukubwa, likiwa na eneo la kilometa za mraba zipatazo 30,370,000 na kwa idadi ya wakazi, hao wakiwa 1,225,080,510 (mwaka 2016). Asia ndiyo bara kubwa pekee zaidi ya Afrika.
20231101.sw_923_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Neno "Afrika" limetokana na lugha ya Kilatini ya Roma ya Kale. kwa jina hilo Waroma wa Kale walitaja eneo katika Tunisia ya leo, hawakumaanisha bara lote.
20231101.sw_923_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Inasemekana asili yake ni kabila la "Afrig" lililoishi sehemu zile,lakini kuna pia maelezo mengine tofautitofauti.
20231101.sw_923_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Wakati huo Wagiriki wa Kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi kusini kwa Bahari ya Mediteranea, upande wa magharibi wa Misri.
20231101.sw_923_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yaliitwa kwa jina la "Ethiopia" linalomaanisha nchi ya watu weusiweusi (kwa Kigiriki "aithiops": aliyechomwa na jua).
20231101.sw_923_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Katika ramani za kale kutoka Ulaya maneno yote matatu ya "Afrika", "Lybia" na "Ethiopia" yanapatikana yakitumika kama jina la bara zima. Jina la "Afrika" limekuwa la kawaida kuanzia karne ya 16 BK.
20231101.sw_923_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Afrika imezungukwa na bahari karibu pande zote. Kuna kiungo chembamba cha nchi kavu upande wa kaskazini mashariki na bara la Asia kwenye rasi ya Sinai .
20231101.sw_923_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Upande wa kaskazini iko Bahari ya Mediteranea, upande wa mashariki kuna Bahari Hindi pamoja na Bahari ya Shamu na upande wa magharibi iko Bahari Atlantiki.
20231101.sw_923_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Barani kuna nchi huru 54 zinazotambuliwa na Umoja wa Mataifa, maeneo 9 yenye hali ya pekee na madola mawili ambayo yanajitawala bila kutambuliwa kimataifa.
20231101.sw_923_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Kuna umbali wa kilomita 8,000 kutoka Ras ben Sakka nchini Tunisia (37°21' N, sehemu ya kaskazini kabisa) hadi rasi ya Cape Agulhas nchini Afrika Kusini (34°51'15" S, sehemu ya kusini kabisa).
20231101.sw_923_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Umbali ni km 7,400 kutoka upande wa magharibi (rasi ya Cape Verde, 17°33'22" W) hadi mashariki (Ras Hafun nchini Somalia, 51°27'52" E).
20231101.sw_923_11
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Nchi kubwa ya Afrika ni Algeria na nchi ndogo ni funguvisiwa la Shelisheli katika Bahari Hindi. Nchi ndogo Afrika bara ni Gambia.
20231101.sw_923_12
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Kijiolojia Afrika iko kwenye bamba la Afrika. Lile bamba la gandunia la Afrika linaenea mbali zaidi kuliko maeneo tunayotazama kuwa Afrika kijiografia, ni pamoja na maeneo chini ya bahari linapopakana na mabamba ya Ulaya-Asia, Uarabuni, Uhindi na Australia, Antaktika, Amerika ya Kusini na Kaskazini. Upande wa mashariki wa bamba la Afrika kuna ufa unaozidi kupanuka ikielekea kujitenga kutoka Afrika kama bamba la Somalia.
20231101.sw_923_13
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Tabianchi ya Afrika ni pana, kuanzia kanda za tropiki hadi kufikia maeneo ya nusu-aktiki (baridi) kwenye ncha za milima mirefu.
20231101.sw_923_14
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Nusu ya kaskazini ya bara ni jangwa au angalau yabisi. Sehemu za kati na za kusini zina maeneo ya savanna na kanda za msitu wa mvua.
20231101.sw_923_15
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Mwaka 2010 idadi ya wakazi wa nchi zote za Afrika ilipita bilioni 1. Ni kwamba idadi yao imeongezeka sana katika miaka 40 iliyopita, ikipiku zile za Ulaya na Amerika.
20231101.sw_923_16
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Ilhali mwaka 1950 walikuwepo Waafrika milioni 229 pekee, idadi iliongezeka kuwa milioni 630 mwaka 1990 na milioni 1200 mnamo 2014.
20231101.sw_923_17
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Hivyo asilimia ya watoto na vijana ni kubwa. Kuna nchi kadhaa ambako zaidi ya nusu ya wananchi wako chini ya umri wa miaka 25. Wakazi wa Afrika ni vijana kuliko wale wa mabara mengine yote; mwaka 2012 umri wa wastani ulikuwa miaka 19.7, wakati kidunia ulikuwa 30.4.
20231101.sw_923_18
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Kusini mwa Afrika, Afrika Mashariki na ya Kati watu wengi ni wasemaji wa lugha za Kibantu (kwa mfano Kiswahili). Asili yao ilikuwa pande za kusini za kanda ya Sahel na kutoka kule walienea katika sehemu nyingi za Afrika upande wa kusini kwa Sahara.
20231101.sw_923_19
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Wakazi asilia siku hizi wako wachache, wakionekana kama wasemaji wa lugha za Khoisan au za Wabilikimo.
20231101.sw_923_20
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Watu wa Afrika Magharibi husema zaidi Lugha za Kiniger-Kongo hasa zisizo za Kibantu, pamoja na wasemaji wa lugha za Kinilo-Sahara.
20231101.sw_923_21
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Waarabu waliovamia eneo hilo lote tangu karne ya 7 BK wameleta lugha yao pamoja na dini ya Uislamu. Lugha yao imekuwa lugha ya watu wengi siku hizi. Wasemaji wa Kiberber bado wako wengi kidogo Moroko na Algeria na wachache katika sehemu za Tunisia na Libya.
20231101.sw_923_22
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Kutokana na ukoloni, lugha za Kihindi-Kiulaya zinazumgumzwa pia, hasa Kiingereza, Kifaransa na Kireno.
20231101.sw_923_23
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Katika kisiwa cha Madagaska kwenye Bahari ya Hindi, inatumika lugha ya Kimalagasy, ambayo ni kati ya lugha za Austronesia.
20231101.sw_923_24
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Waafrika wana imani za dini nyingi tofauti, lakini takwimu zinazotolewa hazina hakika, pia kwa sababu suala hilo ni nyeti kisiasa kwa serikali zenye mchanganyiko mkubwa wa watu, kama vile Nigeria, Ethiopia na Tanzania.
20231101.sw_923_25
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Kadiri ya World Book Encyclopedia, Islam ndiyo inayoongoza, ikifuatwa na Ukristo. Kumbe kadiri ya Encyclopedia Britannica, 45% za wakazi ni Wakristo, 40% ni Waislamu na 10% wanafuata dini asilia za Kiafrika. Wachache tu ni Wahindu, Wabuddha, Wabaha'i au hawana dini yoyote.
20231101.sw_923_26
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Moore, Clark D., and Ann Dunbar (1968). Africa Yesterday and Today, in series, The George School Readings on Developing Lands. New York: Praeger Publishers.
20231101.sw_923_27
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Naipaul, V. S.. The Masque of Africa: Glimpses of African Belief. Picador, 2010. ISBN 978-0-330-47205-0
20231101.sw_923_28
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Besenyő, János. Western Sahara (2009), free online PDF book, Publikon Publishers, Pécs, ISBN 978-963-88332-0-4, 2009
20231101.sw_923_29
https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika
Afrika
Wade, Lizzie. Drones and satellites spot lost civilizations in unlikely places, Science (American Association for the Advancement of Science), DOI: 10.1126/science.aaa7864, 2015
20231101.sw_1163_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kuki
Kuki
Kuki ni tafsiri ya muda ya neno la Kiingereza cookie, ambalo maana yake asili ni biskuti au keki ndogo, lakini katika utarakilishi linatumika ili kompyuta yenye kurasa za tovuti iweze kuwasaliana na watazamaji.
20231101.sw_1163_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Kuki
Kuki
Programu za tovuti hizi zinahifadhi habari kadhaa za mtazamaji au mtumiaji (k.m. jina la mtumiaji, neno la siri, ruhusa, mapendekezo) kwenye kompyuta ya mtazamaji mwenyewe. Hivi mtazamaji anatambuliwa kila wakati anaingia kwenye tovuti hii.
20231101.sw_1165_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Panzi ni aina za wadudu wanaokula mimea. Wameainishwa katika nusuoda Caelifera ya oda Orthoptera. Takriban spishi zote huchupa mbali kwa kutumia miguu yao ya nyuma ambayo ina nguvu sana. Nyingi zinaweza kuruka angani. Panzi wana vipapasio vifupi kuliko mwili wao. Panzi wakubwa ambao wanajikusanya kwenye makundi makubwa huitwa nzige. Kuna panzi wakubwa wengine wenye miiba mikubwa kwenye miguu ya nyuma lakini wasiojikusanya katika makundi. Panzi hao hufanana na ndege wadogo wakiruka juu na huitwa parare.
20231101.sw_1165_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Panzi majike wana vali mwichoni kwa fumbatio zinazowawezesha kuchimba ndani ya ardhi na kutaga mayai yao katika vibumba. Vibumba vya mayai huweza kuwa na mayai kumi na tano hadi zaidi ya mia moja. Mayai ya spishi nyingi za panzi huingia kwa diaposi kupitia majira ya baridi au kiangazi. Hali ya hewa ikiwa nzuri mayai yaendelea kupevuka halafu tunutu wanatoka. Tunutu (panzi wachanga bila mabawa) hubambua ngozi yao mara tano hadi mara saba kufuatana na spishi. Kila hatua ya ukuaji ni ndefu kuliko ile iliyotangulia. Wakati wa ubambuaji wa mwisho panzi wenye mabawa anatoka na kuwa mpevu ndani ya siku au wiki chache.
20231101.sw_1165_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Kuna wadudu ambao wanafanana na panzi lakini wana vipapasio virefu kuliko mwili wao. Hawa ni wana wa nusuoda Ensifera. Spishi moja kati yao anaitwa senene na huliwa na watu. Jike ana mrija wa kutaga unaofanana na kitara. Anataga mayai juu ya au ndani ya mimea.
20231101.sw_1165_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Panzi huliwa sehemu nyingi duniani kwa sababu wana virutubishi vya (protini) vingi. Wanajeshi huambiwa wakamate panzi na kuwala wakipungukiwa chakula.
20231101.sw_1165_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Panzi
Panzi
Kuna familia nyingi za panzi, lakini takriban spishi zote za Afrika ya Mashariki ni wanafamilia wa Acrididae na Pyrgomorphidae. Mwainisho wa sikuhizi ni kama ufuatao (familia zote hazionyeshwi):
20231101.sw_1166_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nzige
Nzige
Nzige ni jamii ya panzi wenye uwezo wa kujikusanya kwenye makundi makubwa na kuruka umbali mrefu kwa pamoja. Wanao huitwa tunutu. Nzige wanapokuwa wametawanyika mmojammoja huishi kama panzi wa kawaida. Wanapozaliana na kuongezeka idadi hujikusanya katika makundi. Makundi ya tunutu husafiri kuelekea upande mmoja na kula majani wanakopitia. Makundi ya nzige waliokomaa huweza kufikia idadi ya zaidi ya bilioni na huruka umbali mrefu na kuharibu mazao wanakotua.
20231101.sw_1166_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nzige
Nzige
Nzige hudhibitiwa kwa dawa za kikemikali. Ni vema nzige wadhibitiwe wanapokuwa wadogo au tunutu kabla hawajaingia mashamba na kuharibu mazao. Tunutu wanaweza kudhibitiwa kwa mashine zinazobebwa mikononi au mgongoni, au zilizopachikwa juu ya gari la pickup. Makundi ya nzige waliokomaa ni lazima yadhibitiwe kwa ndege.
20231101.sw_1166_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nzige
Nzige
Hivi karibuni dawa ya kibiolojia imeendelezwa na mradi wa kimataifa LUBILOSA. Dawa hiyo ina spora za kuvu Metarhizium acridum ndani yake. Siku hizi kuna vifundiro vya kibiashara vitatu sokoni: "Green Muscle" na "Green Guard" vya kampuni BASF na "NOVACRID" cha kampuni ÉLÉPHANT VERT. Vifundiro hivi vinaweza kupulizwa katika mafuta ya diseli kwa mashine za kiwango kidogo sana (g 50 katika L 0.5-2 kwa ha).
20231101.sw_1166_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Nzige
Nzige
Nzige wanatajwa mara nyingi katika Biblia kati ya vitisho vikubwa kwa binadamu kutokana na njaa wanayoweza kusababisha.
20231101.sw_1169_0
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Muhammad (kwa Kiarabu "Mwenye kusifika sana"; jina kamili kwa kirefu ni محمد بن عبد الله بن عبد ﺍﻟﻤﻄﻠﺐ ﺍﻟﻬﺎﺷﻤﻲ Muhammad bin 'Abd Allāh bin 'Abd al-Muţţalib al-Hāshimī) anaaminika katika dini ya Uislamu kuwa ni mtume wa mwisho wa Mungu (Allah) kwa binadamu.
20231101.sw_1169_1
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Muhammad alizaliwa yatima kwani baba yake alifariki kabla yeye hajazaliwa. Hakuishi sana na mama yake (Amina), kwa kuwa naye alifariki dunia Muhammad akiwa na umri wa miaka sita.
20231101.sw_1169_2
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Baadaye akachukuliwa na babu yake Abdul Muttalib na kuishi naye kwa muda wa miaka miwili, kisha babu yake naye akafariki.
20231101.sw_1169_3
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Kazi ya kumlea Muhammad ilimwangukia ami yake Abu Talib ambaye ndiye aliyeishi naye mpaka ukubwa na kumuoza na kumpa himaya wakati alipoanza kazi ya kufikisha ujumbe wa Mwenyezi Mungu kwa watu.
20231101.sw_1169_4
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Kadiri ya hadithi za Kiislamu, ilipokua karibu atadhihiri Mtume mapadri wa Kinasara na makuhani wa Kiyahudi waliokuwa wakikaa Bara Arabu walikuwa wakiwatahayarisha majirani wao wa Kiarabu waliokuwa wakiabudu sanamu, wakiwaambia: “Karibu ataletwa Mtume katika nchi yenu hii, abatilishe hii ibada yenu mbovu ya sanamu”. Walipoambiwa hivi wale Waarabu waliwauliza jina la Mtume huyo, wakawajibu kuwa jina lake litakuwa Muhammad. Kwa hivyo kila mwenye kusadiki hayo alimwita mwanawe Muhammad.
20231101.sw_1169_5
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Lakini hayakusikilizana majina haya ila kwa baadhi ya Waarabu waliokua wakikaa Shamu tu na Najran (Yaman) ambako mapadri wengi walikaa, na vilevile katika Madina ambayo nusu ya wakazi wake walikuwa Wayahudi.
20231101.sw_1169_6
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Hata lilipoanza kutangaa jina la Mtume, waliokuwa wamekwisha kuitwa kwa jina hilo walikuwa wachache tu Bara Arabu nzima.
20231101.sw_1169_7
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Inasemekana Mtume aliinukia tangu utotoni kwake juu ya sifa zake nzuri na ukomavu wa akili ya kiutu uzima, hakupata kufanya vitendo vya utoto umri wake, wala kuazimia kuvifanya ila mara mbili tu, ambazo mara mbili zote hizo Mwenyezi Mungu alimhifadhi navyo.
20231101.sw_1169_8
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Kitendo chenyewe alichokiazimia kukifanya mara mbili zote hizo na Mwenyezi Mungu akamhifadhi nacho ni kutaka kwenda kukesha katika ngoma za arusi mbili za marafiki wake waliooa katika mji wa Makka.
20231101.sw_1169_9
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Lakini Mungu alimpa usingizi mkubwa katika masiku yote hayo mawili hata hakuweza kufumbua jicho, wala kunyanyua miguu kwenda mahali. Hajapata kuhudhuria hata mara moja katika ibada za kuabudu sanamu wala kula chakula kilichochinjwa kwa ajili yao. Moyo wake ulichukizwa na hayo na mambo mengine yaliyo mabaya.
20231101.sw_1169_10
https://sw.wikipedia.org/wiki/Muhammad
Muhammad
Tangu udogo wake Mtume aliondokea na sifa nzuri ambazo hapana hata mmoja katika hirimu zake aliyekuwa nazo zote. Kila sifa zinazohesabiwa kuwa ni njema na Waislamu ndizo alizokuwa nazo tangu utoto wake.