_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1175_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Uhai unapatikana kwa spishi milioni 10-14 za viumbe hai pamoja na wanadamu waliokadiriwa kuwa sasa bilioni 7.2. |
20231101.sw_1175_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Umbo la dunia linafanana na tufe au mpira unaozunguka kwenye mhimili wake. "Mhimili wa dunia" ni mstari kati ya ncha zake. |
20231101.sw_1175_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Lakini si tufe kamili. Ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta; ilhali umbali kati ya ncha mbili ni kilomita 12,713 lakini umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaani kipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha. Tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia. Kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali duniani palipo karibu zaidi na anga-nje si Mlima Everest kwenye Himalaya bali mlima Chimborazo nchini Ekuador. |
20231101.sw_1175_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili. Nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani nchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii. Kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia 11 pekee za maeneo yake. |
20231101.sw_1175_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Kwa jumla dunia ni sayari pekee katika mfumo wa jua yenye maji katika hali ya kiowevu usoni mwake. Bahari kuu ya dunia inashika asilimia 96.5 ya maji yote yaliyopo duniani. Maji ya bahari huwa na asilimia 3.5 chumvi ndani yake. |
20231101.sw_1175_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 za Asia, Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antarktika, Ulaya na Australia. (Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikiwa kama rasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama bara na Greenland kama kisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima). |
20231101.sw_1175_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Maeneo ya bahari kuu ya dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 za Pasifiki, Atlantiki na Bahari Hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenye Mfereji wa Mariana katika Pasifiki (mita 11,034 chini ya UB). Kwa wastani bahari huwa na kina cha mita 3,800. |
20231101.sw_1175_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Tumeona dunia ina umbo la mviringo au tufe. Tufe hilo si kipande kimoja kikubwa cha mwamba thabiti. Dunia ina muundo ndani yake. Muundo huo unafanana kiasi na kitunguu, yaani dunia yetu imefanyika kwa matabaka mbalimbali yanayofuatana kutoka nje kwenda ndani. Kila moja lina tabia yake. |
20231101.sw_1175_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Ganda la dunia ni sehemu imara na uhai wote tunaoujua unapatikana juu yake. Katikati hali ya koti na ya kiini ni ya joto kubwa sana na maada yake hupatikana katika hali ya giligili (si imara, kuyeyushwa). Kila ukiingia ndani dunia inazidi kuwa ya moto mpaka ukifika ndani kabisa daraja ya harara hufikia nyuzi 5000-6000 °C. |
20231101.sw_1175_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Matabaka hayo yanafanywa kwa elementi za kikemia ambazo ni feri (chuma) (32,1 %), oksijeni (30,1 %), silisi (15,1 %), magnesi (13,9 %), sulfuri (2,9 %), nikeli (1,8 %), kalsi (1,5 %) na alumini (1,4 %). Mabaki ya 1,2 % ni viwango vidogo vya elementi nyingine. Elementi hizo zinapatikana kwa hali safi au katika kampaundi za elementi. |
20231101.sw_1175_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Vipimo vimeonyesha ya kwamba matabaka mawili ya koti na kiini huwa tena na mgawanyiko ndani yake, hivyo matabaka yafuatayo yanaweza kutofautishwa. |
20231101.sw_1175_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Sehemu ya juu ya koti inafanana kikemia na ganda na sehemu hizo mbili zinaitwa tabakamwamba. Tabakamwamba ina unene wa kilomita 50 - 100. |
20231101.sw_1175_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Tabakamwamba imekatika katika vipande vinavyoitwa mabamba la gandunia. Vipande hivi vinaelea juu ya giligili ya koti la ndani. Ndiyo sababu bara lolote si la milele; kila bamba huwa na mwendo wake na ndiyo sababu katika historia ya dunia mabara yameachana na kuungana mara kadhaa. Kwa mfano imepimwa ya kwamba sehemu kubwa ya Afrika ya Mashariki ina mwendo wa kuachana na bara la Afrika na dalili yake ni bonde la ufa. |
20231101.sw_1175_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Dunia inazungukwa na uga sumaku yaani mistari ya nguvu ya kisumaku. Sababu yake ni kwamba kiini cha dunia kinafanywa na chuma chenye tabia kama sumaku kubwa. |
20231101.sw_1175_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Tabia hiyo inasababishwa na mwendo wa mikondo ya chuma cha moto kilichoyeyuka katika kiini cha nje cha dunia. Mistari ya nguvu ya sumaku inatoka nje kwenye ncha ya kusini na kurudi ndani ya dunia kwenye ncha ya kaskazini. Tabia hiyo ni msingi wa kazi ya dira ambamo sindano ya dira huvutwa daima na ncha sumaku ya dunia na kuelekea kaskazini muda wote. |
20231101.sw_1175_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Ugasumaku wa dunia ni kinga muhimu kwa uhai wote duniani. Dunia inapigwa muda wote na mnururisho kutoka jua kwa njia ya "upepo wa jua". Mnururisho huo ni nuru pamoja miale ya hatari. Ugasumaku unakengeusha sehemu kubwa ya mnururisho hatari hadi unapita kando ya dunia na kutofika kwenye uso wa dunia. |
20231101.sw_1175_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Dunia yetu ni sayari pekee inayojulikana mpaka sasa ambapo binadamu na viumbe vingine vinaweza kuishi. Wanasayansi bado wanafanya ufafiti kujua kama kuna kuna viumbe hai kwenye sayari nyingine. |
20231101.sw_1175_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | dunia yetu ina umbali na jua unaofaa kwa maisha kwa sababu sayari zilizoko karibu zaidi na jua (k.m. Zuhura) zina joto kubwa mno na sayari zilizoko mbali zaidi kama Mrihi ni baridi mno. |
20231101.sw_1175_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | dunia yetu ina angahewa yenye asilimia 78 ya naitrojini, asilimia 21 ya oksijini na asilimia 1 ya aina nyinginezo za hewa, na kwa sababu hii uhai na maisha yanamakinika katika ardhi, kinyume na sayari nyinginezo. |
20231101.sw_1175_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Sehemu kubwa kabisa ya dunia inafunikwa na bahari, kwani takriban asilimia 70 ya uso wake unafunikwa na maji ya bahari na kutokana na maji yote yaliyokuwepo ardhini, asilimia 97 ni maji ya bahari, na asilimia 3 ni maji matamu. Theluthi inayobaki ni nchi kavu kwenye mabara mbalimali na visiwa vingi. |
20231101.sw_1175_24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Sura ya dunia ni kilomita mraba 510,000,000, ikiwa nchi kavu imechukua eneo la kilomita mraba 149,430,000 na maji yamechukua eneo la kilomita mraba 360,570,000. |
20231101.sw_1175_25 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Mabara makubwa ni Asia, Afrika, Amerika Kusini na Amerika Kaskazini, Australia na Ulaya. Asia na Ulaya mara nyingi hutazamiwa wakati mwingine kama bara moja ya Eurasia. |
20231101.sw_1175_26 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Hewa iliyoko juu ya ardhi vile vile ina matabaka mbalimbali, na kila tabaka lina kazi yake. Hewa kwa jumla ina masafa ya kiasi cha kilomita 560 au maili 348 kuendea juu, na baada ya hapo unaingia kwenye anga-nje. Hewa hiyo ndiyo inayokinga viumbehai na madhara ya Jua na mnururisho wa angani ambao unaingia anga ya dunia na kuteremka chini. |
20231101.sw_1175_27 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Cesare Emilliani: Planet Earth. Cosmology, Geology, and the Evolution of Live and Environment. Cambridge University Press 1992, ISBN 0-521-40949-7 |
20231101.sw_1175_28 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Dunia | Dunia | Comins, Neil F. (2001). Discovering the Essential Universe (2nd ed.). W. H. Freeman. Bibcode:2003deu..book.....C. ISBN 0-7167-5804-0. |
20231101.sw_1178_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia | Asia | Asia ni bara kubwa kabisa kuliko mabara yote mengine ya dunia. Bara hili lina eneo la kilomita za mraba 44,579,000 (maili za mraba 17,212,000), ambalo ni sawa na asilimia 30% ya ardhi yote. Wakazi wa bara la Asia ni 3,701,000,000 kwa mujibu wa makisio 2003. |
20231101.sw_1178_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia | Asia | Bara la Asia lina nchi 44 na visiwa mbali mbali vya madola mbalimbali. Mlima mrefu kabisa ulimwenguni ambao ni mlima wa Everesti wenye urefu wa mita 8,850 (futi 29,035) ulioko Nepal pia uko kwenye bara hili. Kadhalika, nchi zenye wakazi wengi zaidi ulimwenguni China na India pia ziko kwenye bara hili. |
20231101.sw_1178_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Asia | Asia | Ziwa kubwa kabisa ulimwenguni, bahari ya Kazwini (Caspian Sea) lenye eneo la kilomita za mraba 394,299 (maili za mraba 152,239) vile vile liko Asia kati ya ya nchi hizi: Azerbaijan, Urusi, Kazakhstan, Turkmenistan, na Uajemi. |
20231101.sw_1182_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Isa ni umbo la jina Yesu katika Qurani na pia katika lugha mbalimbali zilizoathiriwa na Uislamu. Ukurasa huu unahusu imani ya Uislamu kumhusu Yesu kadiri ya Kurani. |
20231101.sw_1182_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Kitabu hicho kilichoandikwa miaka 600 hivi baada ya Kristo kina aya 93 zinazomhusu, lakini hakileti mfululizo wa habari za maisha yake wala za mafundisho yake maalumu. |
20231101.sw_1182_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Ingawa Waislamu wanakiri pia vitabu vitakatifu vya Torati, Zaburi na Injili, katika ibada wanatumia Kurani tu na kwa kawaida ndiyo chanzo chao cha habari juu ya watu na matukio ya kabla yake. |
20231101.sw_1182_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Kwao nabii Isa ni mtume anayeaminiwa kuwa mmojawapo wa mfululizo wa mitume na manabii watukufu 124,000 wa Mwenyezi Mungu walioletwa ulimwenguni kuwapasha wanadamu ujumbe wa umoja wake, ili wamuabudu Yeye peke yake akiwa ndiye Muumba na Mruzuku wao hapa duniani. |
20231101.sw_1182_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Mitume na Manabii hao wameletwa katika zama mbalimbali na kwa watu, kaumu na umma mbalimbali, na mfululizo huu ulianza na Adamu, baba wa wanadamu wote, hadi Mtume Muhammad akiwa ndiye wa mwisho. |
20231101.sw_1182_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Isa ni miongoni mwa mitume wakubwa ambao Mwenyezi Mungu amewasifu kwa subira yao na ustahimilivu wao mkubwa: Manabii Nuhu na Ibrahimu na Musa na Isa na Muhammad. Tena ni miongoni mwa Mitume waliopewa Kitabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu kiitwacho Injili. "Masihi Isa bin Mariamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu na Neno lake tu alilompelekea Mariamu, na ni Roho iliyotoka kwake" (sura ya 4 aya 171). Wakristo wanamuita kwa kawaida Yesu Kristo. |
20231101.sw_1182_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Nabii Isa alizaliwa na bibi Maryam kimuujiza, kwani alizaliwa bila ya baba kwa amri ya Mola wake ambaye alimtuma malaika Jibril kumtangazia kupata kwa mtoto mtukufu. |
20231101.sw_1182_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Baada ya kuzaliwa, Nabii Isa, alisema utotoni mwake akiwa bado mchanga, ukiwa ni muujiza mwingine kwa watu ili kuwaonyesha kuwa yeye si mtoto wa kawaida, na kuwa mama yake hana dhambi ya kuja kwake bila ya baba. |
20231101.sw_1182_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Huo ni mfano mmoja katika mifano minne ya uumbaji aliyotuonyesha Mwenyezi Mungu, kwani Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu bila ya baba wala mama, na akamuumba Hawa bila ya mama, na akamuumba Isa bila ya baba, na akaumba wanadamu wote waliobakia kutokana na baba na mama. |
20231101.sw_1182_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Habari za kuzaliwa kwake Nabii Isa zinapatikana katika Kurani, surat "Maryamu" (19) kuanzia aya 16 - 35. |
20231101.sw_1182_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipojitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki. Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mcha Mungu. (Malaika) Akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako ili nikubashirie tunu ya mwana aliyetakasika. Akasema: Nitampataje mwana hali mwanamume yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba? (Malaika) akasema: Ni kama hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lililokwishaamuliwa. Basi akachukua mimba yake, na akaondoka nayo mpaka mahali pa mbali. Kisha uchungu ukampeleka kwenye shina la mtende; akasema: Laiti ningelikufa kabla ya haya, na nikawa niliye sahaulika kabisa! Pakatangazwa kutoka chini yake: Usihuzunike! Hakika Mola wako amejaalia chini yako kijito kidogo cha maji! Na litikise kwako hilo shina la mtende, utakuangushia tende nzuri zilizo mbivu. Basi kula, na kunywa, na litue jicho lako. Na pindi ukimwona mtu yeyote basi sema: Hakika mimi nimeweka nadhiri kwa Mwenyezi Mungu ya kufunga; kwa hivyo leo sitasema na mtu. Akenda naye (mwanawe) kwa jamaa zake amembeba. Wakasema: Ewe Maryamu! Hakika umeleta kitu cha ajabu! Ewe dada yake Harun! Baba yako hakuwa mtu muovu, wala mama yako hakuwa kahaba. |
20231101.sw_1182_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Akawaashiria (mtoto). Wakasema: Vipi tumsemeze aliye bado mdogo yumo katika mlezi? (Mtoto) akasema: Hakika mimi ni mtumwa wa Mwenyezi Mungu. Amenipa Kitabu, na amenifanya Nabii. Na amenijaalia ni mwenye kubarikiwa popote pale niwapo. Na ameniusia Sala na Zaka maadamu ni hai, Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu. Na amani iko juu yangu siku niliyo zaliwa, na siku nitakayo kufa, na siku nitakayo fufuliwa kuwa hai. Huyo ndiye Isa mwana wa Maryamu. Ndiyo kauli ya haki ambayo wanaifanyia shaka. Haiwi kwa Mwenyezi Mungu kuwa na mwana, Subhanahu, Yeye ametakasika! Anapolihukumia jambo basi huliambia tu: Kuwa! Likawa. |
20231101.sw_1182_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Nabii Isa aliletwa kwa wanadamu kufikisha ujumbe kwao wa kuwafahamisha kuwa Mwenyezi Mungu ni Mmoja, hana mwenzake, na kuwa Yeye pekee ndiye mwenye kustahili kuabudiwa kwa haki. Ujumbe huu ndio ujumbe uleule uliotumwa kwa Mitume na Manabii wote kwa wanadamu ili kuwaongoza, naye alikuja kutilia mkazo na kusisitiza jambo hili na kuzipa nguvu tume za Mitume na Manabii waliopita. |
20231101.sw_1182_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Kadiri ya sura ya 3 aya ya 50 alisema ni "msadikishaji wa yale yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na ili niwahalalishieni baadhi ya yale mliyoharimishiwa, na nimewajieni na Ishara kutoka kwa Mola wenu, kwa hiyo mcheni Mwenyezi Mungu na mnitii". |
20231101.sw_1182_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Alitabiri kuwa baada yake atakuja Mmoja ambaye atawafundisha wanadamu ukweli wote na kuwaongoza kwenye haki na kuwaeleza kila wanalolihitaji katika maisha yao. Ujumbe wake ulikuwa ni wa mwisho kabla ya ule wa Mtume Muhammad ambao ndio wa mwisho kabisa kwa wanadamu wote. |
20231101.sw_1182_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Mwenyezi Mungu ameleta Mitume na Manabii wengi ulimwenguni, lakini alichagua baadhi yao na kuwateremshia vitabu vya uongozi na sharia na hekima kwa wafuasi wao. Katika vitabu vilivyoteremshwa kwa Manabii mbalimbali ni Taurati kwa Nabii Musa, Zaburi kwa Nabii Daudi, Injili kwa Nabii Isa, na Qurani kwa Nabii Muhammad. Kitabu cha Nabii Isa kiliteremshiwa Wayahudi ambao ndio walengwa wake wa kwanza wa Nabii Isa, kama ilivyothibitishwa na Qurani wakati aliposema: |
20231101.sw_1182_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Enyi Wana wa Israili! Hakika mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenu, ninayethibitisha yaliyokuwa kabla yangu katika Taurati, na mwenye kubashiria Mtume atakayekuja baada yangu jina lake ni Ahmad! Lakini alipowaletea hoja zilizo wazi, walisema: Huu ni uchawi ulio wazi! |
20231101.sw_1182_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Nabii Isa alipewa na Mwenyezi Mungu miujiza mbalimbali kumsaidia katika kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu, kwani ilikuwa kawaida kwa Mtume au Nabii kuonyesha miujiza kwa watu au kaumu yake ili awathibitishie kuwa yeye kweli ni mjumbe aliyeletwa na Mola wa ulimwengu huu. Mitume waliotangulia kabla ya Nabii Isa, kama Nuhu na Ibrahim na Musa na wengineo wote walikuja na miujiza mbalimbali. |
20231101.sw_1182_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Baadhi ya miujiza ya Nabii Isa kwa idhini ya Mwenyezi Mungu ni kuumba ndege kutokana na udongo, kuponyesha vipofu wakaweza kuona, na kuwaondoshea ukoma wale wenye ukoma, na kuhuisha mtu aliyekufa, na kuwateremshia wafuasi wake chakula kutoka mbinguni ili iwe ni dalili kwao wote. |
20231101.sw_1182_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Muhammad alikuta Wakristo au Manasara wakiwa wamehitilifiana katika imani yao kuhusu Nabii Isa, kwani wote walimkiri kuwa Mwana wa Mungu, lakini kwa wengi hii ilikuwa na maana kuwa yeye ni Mungu aliyejifanya mtu, isipokuwa wachache walitafsiri tofauti. |
20231101.sw_1182_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Makundi ya namna hiyo yalitengana baada ya Nabii Isa kuondoka ulimwenguni na kuwaachia wafuasi wake waendeleze kazi yake ya kutangaza dini ya Mwenyezi Mungu. Wafuasi waliokuja baada ya wale kumi na mbili waliokuwa pamoja naye, walitoa fikra na mawazo yao kuhusu Isa, hivyo baada ya muda waligawanyika makundi mbalimbali. |
20231101.sw_1182_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Waislamu pamoja na Wakristo wanaamini kuwa Isa atarudi tena ulimwenguni kukamilisha kazi yake aliyoiacha baada ya kupaa kwenda kwa Mola wake, na haya yanaelezwa katika vitabu vya dini vya Kiislamu na vya Kikristo, lakini wanahitilifiana kuhusu namna na njia aliyoondokea ulimwenguni. |
20231101.sw_1182_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Waislamu wanasema kuwa Isa alichukuliwa na Mola wake na kupandishwa kwake mbinguni baada ya Wayahudi kutaka kumuua, na kwa hivyo hawakuweza kumuua wala kumsulubu. Wakristo kwa upande mwingine, wanaamini kuwa aliwahi kusulubiwa na kuzikwa kisha akafufuka siku ya tatu. Muhimu hapa ni kujua kuwa atarudi tena duniani kukamilisha kazi aliyopewa na Mwenyezi Mungu. |
20231101.sw_1182_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Isa | Isa | Hivyo ni kweli kwamba imani kwa nabii Isa na kwa Yesu Kristo ni tofauti sana katika Ukristo na Uislamu. |
20231101.sw_1183_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Bara (au kontinenti) ni pande kubwa la nchi kavu la Dunia linalozungukwa na bahari. Kwa kawaida tunatofautisha mabara 7 ya Afrika, Amerika Kaskazini, Amerika Kusini, Antaktiki, Asia, Australia, na Ulaya. |
20231101.sw_1183_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Neno "bara" lamaanisha pande kubwa la nchi kavu , tofauti na bahari au visiwa vidogo karibu na pwani ya nchi kavu kubwa zaidi. Neno "kontinenti" latokana na Kilatini "terra continens" yaani "nchi (kavu) mfululizo". |
20231101.sw_1183_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa hiyo elezo la neno bara / kontinenti katika sayansi ya jiografia ni "masi kubwa na mfululizo za nchi kavu zinazotengwa kwa maeneo makubwa ya maji" Lakini hali halisi sehemu kubwa ya mabara saba yanayokubaliwa kwa kawaida hayatengwi kabisa kati yake kwa maji. Kwa mfano Ulaya na Asia hayatengwi kabisa na tofauti yake ni kihistoria na kiutamaduni, si kijiografia. Pia neno "masi kubwa" halieleweki waziwazi kabisa. Kwa nini Greenland yenye eneo la kilomita za mraba 2,166,086 inaitwa "kisiwa" lakini Australia yenye eneo la 7,617,930 huitwa bara? |
20231101.sw_1183_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mabara yote ya Dunia yetu huwa na pwani kwenye bahari kuu ambayo ni moja tu ikigawiwa kwa sehemu mbalimbali na mabara vigezo vingine. |
20231101.sw_1183_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa lugha ya kawaida “bara” ni eneo mfululizo wa nchi kavu. Kwa maana hii “Tanzania bara” ni eneo lote la Tanzania isipokuwa visiwa ambavyo ni sehemu ya nchi ya Tanzania bila visiwa vya Unguja, Pemba, Mafia na kadhalika. |
20231101.sw_1183_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa macho ya jiolojia “bara” ni pana kuliko nchi kavu tu. Tunaangalia eneo lote la miamba inayounda bara. Siku hizi tunajua kwamba kila bara linalingana na kipande cha ganda la dunia tunachoita bamba la bara (continental plate). Kipande hiki kinaendelea pia chini ya uso wa bahari katika tako la bara (continental shelf) katika maji yasiyo na kina kikubwa pamoja na visiwa vya sehemu hizi. Kwa mtazamo huu visiwa vya Britania na Eire ni sehemu za Ulaya na vivyo hivyo Autralia na Guinea Mpya ni bara moja. |
20231101.sw_1183_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa maana ya utamaduni wazo la bara linaweza kujumlisha pia visiwa vya mbali kama vile Iceland huhesabiwa sehemu ya Ulaya au hata mikoa ya Ufaransa katika Bahari Hindi kuhesabiwa kisiasa katika Ulaya. |
20231101.sw_1183_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwenye ramani zinazotumia lugha ya Kiingereza kawaida huhesabiwa mabara saba duniani, mengine yakiwa makubwa na mengine madogo. |
20231101.sw_1183_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | [[File:Continental models-Australia.gif|thumb|450px|Ramani inayoonyesha njia mbalimbali za kugawa dunia kwa mabara. Kutegemeana na mawazo ya wataalamu mabara huweza kuhesabiwa kwa namna tofauti. Kwa mfano Eurasia kwa kawaida huhesabiwa kuwa mabara 2 Ulaya na Asia (nyekundu). Wengine hujumlisha pia Eurasia pamoja na Afrika kuwa bara 1. Amerika ya Kaskazini na Amerika ya Kusini wakati mwingine hutazamiwa kuwa bara moja ya Amerika. |
20231101.sw_1183_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kutokana na elezo kuu kuwa bara ni masi ya nchi kavu iliyotengwa na bara nyingine kwa maji kuna mawazo tofauti kuhusu idadi ya mabara. |
20231101.sw_1183_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Ulaya na Asia kwa pamoja ni masi moja kubwa ya nchi kavu na kijiografia hakuna tofauti. Sababu za kuzihesabu kuwa mabara mawili ni kiutamaduni na kihistoria tu. Kwa hiyo mara kwa mara kuna pendekezo kuzijumlisha kwa jina "Euroasia" au "Eurasia". |
20231101.sw_1183_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Amerika Kusini na Amerika Kaskazini zinaunganishwa kwa shingo ya nchi ya Panama na hata hapo mara nyingi hujumlishwa kama "bara pacha" |
20231101.sw_1183_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mfumo wa mabara saba hufundishwa kule China, India, Pakistan, Ufilipino, sehemu za Ulaya na katika nchi nyingi zinazotumia lugha ya Kiingereza pamoja na Australia and England |
20231101.sw_1183_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Eurasia bara moja) hutumiwa zaidi pale Urusi, Ulaya ya Mashariki na Japani |
20231101.sw_1183_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mfumo wa mabara sita (kwa kuhesabu Amerika kuwa bara moja) hutumiwa Ufaransa na nchi zilizokuwa koloni zake na Italia, Urenol, Hispania, Romania, Amerika Kusini Ugiriki, na nchi kadhaa nyingine za Ulaya. |
20231101.sw_1183_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kuna pia mfumo wa kuhesabu mabara matano kwa kuacha Antaktika isiyo wa wakazi kwenye msingi wa mabara sita. Huu unatumiwa katika nembo na katiba ya harakati ya Michezo ya Olimpiki. |
20231101.sw_1183_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mabara jinsi yalivyo leo hayakuwepo tangu mwanzo wala hayakai vile. Ilhali kila bara linalingana na bamba 1 au mabamba ya gandunia ina pia mwendo pamoja na bamba lake. Wanajiolojia huamini ya kwamba miaka mamilioni iliyopita mabara yote yaliwahi kukaa pamoja kama bara 1 kubwa sana lililoendelea kupasuliwa baadaye. Vipande huelea juu ya koti ya dunia ambayo ni kiowevo na moto. Mwendo wa mabamba umepimiwa kuwa sentimita kadhaa kila mwake. Uhindi zamani haikuwepo sehemu ya Asia, na sasa hivi Afrika inaelekea kupasuliwa kwenye mstari wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki. |
20231101.sw_1183_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Eneo la dunia yote kwa jumla ni [510,066,000 kilomita mraba], ikiwa nchi kavu imechukuwa eneo la [148,647,000 kilomita mraba] na maji yamechukuwa eneo la [361,419,000 kilomita mraba]. Eneo la maji kulingana na eneo la nchi kavu ni asilimia 70.9, na nchi kavu [148,647,000 kilomita mraba] ni asilimia 29.1. Maji ya bahari yamechukuwa eneo la [335,258,000 kilomita mraba]ambalo ni asilimia 97, na maji yaliyobakia matamu ni asilimia 3 tu. |
20231101.sw_1183_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mabara jinsi yanavyoonekana hukaa juu ya mabamba ya gandunia ambayo ni vipande vikubwa vya mwamba vinavyounda uso wa dunia. Mabara tunavyoyajua yanalingana kila moja na bamba lake na kila bamba ina mwendo wake wa polepole. Hii ni sababu ya kwamba baada ya miaka mingi uso wa dunia utaonekana tofauti kuliko leo. |
20231101.sw_1183_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kijiolojia bara haliishi kwenye pwani pale bahari inapoanza. Bara linaendelea chini ya uso wa bahari kama tako la bara. |
20231101.sw_1183_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Mabara na mabamba yao ni kama ifuatayo: Afrika (Bamba la Afrika), Antaktika (Bamba la Antaktika), Australia (Bamba la Australia), Ulaya na sehemu kubwa ya Asia (Bamba la Ulaya-Asia), Amerika Kaskazini pamoja na Siberia (Bamba la Amerika ya Kaskazini) na Amerika Kusini (Bamba la Amerika ya Kusini). Mabamba madogo yamejitenga ingawa nchi juu yao inaonekana kuwa sehemu ya bara lingine. Mfano wake ni Bara Hindi iliyokuwa kama bara ndogo au kisiwa kikubwa zamani lakini tangu miaka milioni 10 imejisukuma chini ya bamba la Asia-Ulaya na kuikunja hadi kutokea kwa milima ya Himalaya. |
20231101.sw_1183_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa jumla miamba ya sehemu za mabara ni mipesi kushinda miamba ya chini na hii ni sababu ziko juu ya miamba mingine. |
20231101.sw_1183_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Bara la Antaktika halina wakazi wa kudumu wala nchi huru hata moja ijapokuwa nchi kama 7 zinadai kumiliki sehemu fulani za bara hili. |
20231101.sw_1183_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Bara | Bara | Kwa hivyo, kwa ujumla, kuna madola 192 katika mabara yote ya ulimwengu, mara huzidi kukitokea na mgawanyiko wa nchi au hupungua kukitokea umoja au muungano wa nchi. |
20231101.sw_1191_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania (jina rasmi: Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi iliyoko Afrika ya Mashariki ndani ya ukanda wa maziwa makuu ya Afrika. Imepakana na Uganda na Kenya upande wa kaskazini, Bahari Hindi upande wa mashariki, Msumbiji, Malawi na Zambia upande wa kusini, Kongo, Burundi na Rwanda upande wa magharibi. |
20231101.sw_1191_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Eneo lina kilometa za mraba 947,303 (nchi ya 31 duniani); maji ya ndani yanachukua asilimia 6.2. Mlima Kilimanjaro, mlima mrefu zaidi barani Afrika, upo kaskazini-mashariki mwa Tanzania. |
20231101.sw_1191_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2022 ilikuwa 61,741,120 (nchi ya 24 duniani) kutoka 44,928,923 waliohesabiwa katika sensa ya mwaka 2012, likiwa ongezeko la 3.2% kwa mwaka. |
20231101.sw_1191_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mji mkuu ni Dodoma (wenye wakazi 410,956), lakini Dar es Salaam ndilo jiji kubwa zaidi, lenye watu 4,364,541. |
20231101.sw_1191_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Miji mingine ni kama vile Mwanza (706,543), Arusha (416,442), Mbeya (385,279), Morogoro (315,866), Tanga (273,332), Kahama (242,208), Tabora (226,999) na Zanzibar (223,033). |
20231101.sw_1191_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Jina "Tanzania" liliundwa kama mkusanyiko wa majina ya maeneo mawili yaliyoungana kuunda nchi: Tanganyika na Zanzibar. Jina lilipatikana kwa mashindano yaliyotangazwa mwaka 1964 na serikali kutafuta jina fupi zaidi kuliko "Republic of Tanganyika and Zanzibar". |
20231101.sw_1191_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mshindi alikuwa mwenyeji wa Dar es Salaam aliyeitwa Mohamed Iqbal Dar. Alipendekeza kuunganisha herufi tatu za kwanza za TANganyika na ZANzibar akafikia "Tanzan". Hakuridhika bado, akaona nchi nyingi za Afrika zina majina yanayoishia na "ia" akaongeza herufi hizi. Mwenyewe alieleza baadaye chaguo lake kwamba aliamua kutumia "I" ya jina lake Iqbal na "A" ya jina la dhehebu lake analolifuata katika Uislamu la Ahmadiyya. |
20231101.sw_1191_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Jina "Tanganyika" linatokana na maneno ya Kiswahili tanga (kwa kiingereza "sail") na nyika (kwa kiingereza "uninhabited plain", "wilderness"), yakiunda msemo "tanga nyikani". Wakati fulani inaelezwa kama marejeleo ya Ziwa Tanganyika. Jina la Zanzibar linatokana na "zenji", jina la watu wa eneo hilo (inadaiwa lina maana ya "nyeusi"), na neno la Kiarabu "barr", ambalo linamaanisha pwani au ufukwe. |
20231101.sw_1191_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | (Kuhusu historia ya maeneo ya Tanzania kabla ya 1964 angalia makala za Tanganyika, Zanzibar na Afrika ya Mashariki ya Kijerumani) |
20231101.sw_1191_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kabla ya uhuru nchi zote mbili, Tanganyika na Zanzibar, zilikuwa chini ya utawala wa Uingereza lakini hazikuwa makoloni ya kawaida. |
20231101.sw_1191_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Zanzibar ilikuwa na hali ya nchi lindwa kutokana na mikataba kati ya masultani wa Zanzibar na Ufalme wa Muungano (Uingereza). |
20231101.sw_1191_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanganyika iliwahi kuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani hadi Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia halafu ikawa chini ya Uingereza kama eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa lililoweka Tanganyika katika ngazi "B" ya maeneo ya kudhaminiwa. |
20231101.sw_1191_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanganyika na Zanzibar zilikuwa nchi mbili tofauti hadi 1964, zilipoungana na kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Hapo kiongozi wa Tanganyika Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alipata kuwa Rais wa kwanza na kiongozi wa mapinduzi ya Zanzibar Abedi Amani Karume akawa Makamu wa Kwanza wa Rais. |
20231101.sw_1191_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania, chini ya Rais wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (1985–1995) iliruhusu mfumo wa vyama vingi vya siasa Tanzania na kuanza mpango wa kurekebisha uchumi kuendana na masharti ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani. |
20231101.sw_1191_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Rais wa awamu ya tatu, Benjamin Mkapa (1995–2005) aliendeleza mfumo wa uchumi wa soko huria ambapo mashirika ya umma yanabinafsishwa. |
20231101.sw_1191_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tarehe 21 Desemba 2005 Jakaya Kikwete aliapishwa kuwa Rais wa nne wa taifa (2005–2015), naye aliendeleza sera za watangulizi wake akitokea chama hichohicho cha CCM. |
20231101.sw_1191_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kufuatana na kifo chake tarehe 17 Machi 2021, makamu wake, Samia Suluhu Hassan, aliapishwa kuwa rais wa awamu ya sita. |
20231101.sw_1191_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Ikiwa na eneo la kilomita za mraba 947,303 (365,756 sq mi), Tanzania ni nchi ya 13 kwa ukubwa barani Afrika na ya 31 kwa ukubwa duniani. Inapakana na Kenya na Uganda upande wa kaskazini; Rwanda, Burundi, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo upande wa magharibi; na Zambia, Malawi, na Msumbiji upande wa kusini. |
20231101.sw_1191_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania iko kwenye pwani ya mashariki ya Afrika na ina ufuo wa Bahari ya Hindi takriban kilomita 424 (885 mi). Pia inajumuisha visiwa kadhaa vya pwani, vikiwemo Unguja (Zanzibar), Pemba, na Mafia. Tanzania ni nchi yenye sehemu za juu na za chini kabisa barani Afrika: Mlima Kilimanjaro, wenye urefu wa mita 5,895 (futi 19,341) juu ya usawa wa bahari, na kina cha Ziwa Tanganyika, katika mita 1,471 (futi 4,826) chini ya usawa wa bahari kwa mtiririko huo. |
20231101.sw_1191_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ina milima na misitu minene kaskazini-mashariki, ambako kuna Mlima Kilimanjaro. Nchi iko katika eneo la Maziwa makubwa ya Afrika, hivyo maziwa yanafunika km2 61,500, yaani 6% za eneo lote la nchi. Upande wa kaskazini na magharibi kuna Ziwa Victoria, ziwa kubwa zaidi barani Afrika, na Ziwa Tanganyika, ziwa lenye kina kirefu zaidi barani humo, linalojulikana kwa aina yake ya kipekee ya samaki. Upande wa kusini magharibi kuna Ziwa Nyasa. Eneo la katikati mwa Tanzania ni uwanda mkubwa, wenye tambarare na ardhi ya kilimo. Ukanda wa mashariki una joto na unyevunyevu, huku Visiwa vya Zanzibar vikiwa karibu. Maporomoko ya maji ya Kalambo katika mkoa wa kusini-magharibi mwa Rukwa ni maporomoko ya pili kwa urefu barani Afrika, na yanapatikana karibu na ufuo wa kusini-mashariki wa Ziwa Tanganyika kwenye mpaka na Zambia. Eneo la Hifadhi ya Menai Bay visiwani Zanzbar ndilo eneo kubwa zaidi la bahari lililohifadhiwa. |
20231101.sw_1191_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Hali ya hewa inatofautiana sana ndani ya Tanzania. Katika nyanda za juu, halijoto huanzia 10 hadi 20 °C (50 na 68 °F) wakati wa msimu wa baridi na joto kwa mtiririko huo. |
20231101.sw_1191_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania hupata majira ya joto katika miezi ya Desemba, Januari na Februari (25–31 °C au 77.0–87.8 °F) huku kipindi cha baridi zaidi kikitokea kati ya Mei na Agosti (15–20 °C au 59–68 °F). Halijoto ya kila mwaka ni 20 °C (68.0 °F). |
20231101.sw_1191_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Hali ya hewa ni baridi katika maeneo ya milima mirefu. Tanzania ina vipindi viwili vikuu vya mvua: Mvua za vuli hunyesha katika miezi ya Oktoba, Novemba na Desemba na mvua za masika hunyesha katika miezi ya Machi, Aprili na Mei ingawa zipo tofauti ndogo kati ya sehemu mbalimbali. Kiasi cha mvua na halijoto husababisha tofauti za aina ya uoto wa asili, udongo na aina ya mazao yanayolimwa. |
20231101.sw_1191_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mabadiliko ya hali ya hewa nchini Tanzania yanasababisha kuongezeka kwa joto na uwezekano mkubwa wa matukio ya mvua kubwa (kusababisha mafuriko) na vipindi vya ukame. Mabadiliko ya hali ya hewa tayari yanaathiri sekta za kilimo, rasilimali za maji, afya na nishati nchini Tanzania. Kupanda kwa kina cha bahari na mabadiliko ya ubora wa maji kunatarajiwa kuathiri uvuvi na ufugaji wa samaki. |