_id
stringlengths 15
22
| url
stringlengths 31
150
| title
stringlengths 1
86
| text
stringlengths 100
23.8k
|
---|---|---|---|
20231101.sw_1191_24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ilitoa Mpango wa Kitaifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (NAPAs) mwaka 2007 kama ilivyoagizwa na Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi. Mwaka 2012, Tanzania ilitoa Mkakati wa Kitaifa wa Mabadiliko ya Tabianchi ili kukabiliana na wasiwasi unaoongezeka wa athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi katika mazingira ya kijamii na kiuchumi. |
20231101.sw_1191_25 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ina takriban 20% ya spishi za wanyama wengi wa Afrika wenye damu moto, wanapatikana kwenye mbuga zake za Taifa, hifadhi na bahari. Hifadhi za Taifa na mbuga za wanyama zimeenea katika eneo la zaidi ya kilomita za mraba 42,000 (sq. mi 16,000) na kuunda karibu 38% ya eneo la nchi. Tanzania ina mbuga 21 za taifa, pamoja na hifadhi mbalimbali za wanyamapori na misitu, ikijumuisha Hifadhi ya Ngorongoro. Magharibi mwa Tanzania, Hifadhi ya Taifa ya Gombe ni kitovu ya uchunguzi unaoendelea wa Jane Goodall wa tabia ya sokwe, ambao ulianza mwaka wa 1960. |
20231101.sw_1191_26 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ina bioanuwai nyingi na ina aina mbalimbali za makazi ya wanyama. Katika uwanda wa Serengeti nchini Tanzania, nyumbu (Connochaetes taurinus mearnsi), "bovids" wengine na pundamilia hushiriki katika uhamaji mkubwa wa kila mwaka. Tanzania ni nyumbani kwa takriban spishi 130 za amfibia na zaidi ya spishi 275 za wanyama watambaao, wengi wao wanapatikana Tanzania tu na wamejumuishwa katika orodha ya International Union for Conservation of Nature. Tanzania ina idadi kubwa ya simba Duniani. |
20231101.sw_1191_27 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ilikuwa na alama 7.13/10 kwenye Forest Landscape Integrity Index mwaka 2019, ilishika nafasi ya 54 duniani kati ya nchi 172. |
20231101.sw_1191_28 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Zanzibar (visiwa vya Unguja na Pemba) ina serikali na bunge lake vinavyoratibu mambo yasiyo ya muungano. |
20231101.sw_1191_29 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Muundo wa uongozi na utawala katika kipindi cha ukoloni ulizingatia mgawanyo wa madaraka baina ya mihimili mitatu ya dola yaani serikali, bunge na mahakama. |
20231101.sw_1191_30 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tangu uhuru, mgawanyo wa madaraka na uhusiano miongoni mwa mihimili hiyo uliimarishwa kwa kuzingatia wakati, mahitaji ya demokrasia na misingi ya utawala bora na umeainishwa pia katika katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 4 (1). |
20231101.sw_1191_31 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kuwepo kwa mfumo wa vyama vingi pia kulikuwa hatua ya kuendelea kuimarisha utawala wa ushiriki wa wananchi kadiri mahitaji ya upanuzi wa maono na falsafa duniani. |
20231101.sw_1191_32 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Ugatuzi, yaani mgawanyo wa kiutawala, unafuata Katiba ya nchi I 2.2. Tanzania imegawiwa kwa mikoa 31. Kila mkoa huwa na wilaya ndani yake. Jumla ya wilaya ni 169, ambazo kati yake 34 ni miji. |
20231101.sw_1191_33 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Watu wa Tanzania hawaenei sawasawa. Katika maeneo makavu sana, kwa wastani kuna mtu mmoja tu kwa kilomita ya mraba (1/km²), lakini sehemu zenye rutuba za bara, kuna watu 51 kwa kila kilomita ya mraba. Hatimaye huku Unguja kuna watu 134 kwa kilomita ya mraba na katika Mkoa wa Dar es Salaam ni 3,133 kwa kilomita ya mraba. |
20231101.sw_1191_34 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Nyingi katika jamii zilizohamia sehemu hii ziliingia katika makundi madogomadogo kwa amani, ingawa ziko zilizoingia kwa njia ya uvamizi na vita. Baadhi ya jamii zilizovamiwa zilijihami na kuwazuia wahamiaji wasiendelee kuteka maeneo mengine. |
20231101.sw_1191_35 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kufikia mwaka 1884, wakati Wajerumani walipoanza harakati za kufanya sehemu hii ya Afrika kuwa koloni lao, kulikuwa na makabila zaidi ya 120 katika eneo la Tanzania bara. |
20231101.sw_1191_36 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kuna makabila 125 hivi. Makabila yenye watu zaidi ya milioni moja ni Wasukuma, Wanyamwezi, Wachaga, Waha, Wagogo, Wahaya, Wajaluo na Wamakonde. |
20231101.sw_1191_37 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Jambo la pekee kuhusu jamii zilizoishi na zinazoendelea kuishi Tanzania ni kwamba wakazi asili wanawakilisha makundi yote makuu manne ya lugha barani Afrika. |
20231101.sw_1191_38 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | 3. Kundi lingine ni makabila ya Wakushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania; hao ni makabila ya Wairaqw, Wafiome, Wasi na Waburunge. |
20231101.sw_1191_39 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Hatimaye kuna Wahadzabe wachache ambao utafiti wa DNA umeonyesha hivi karibuni wana uhusiano wa asili na Watwa wa nchi za Afrika ya Kati. |
20231101.sw_1191_40 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Pia kuna asilimia ndogo ya watu wenye asili ya nje ya bara la Afrika, kwa mfano Wahindi, Waarabu, Waindochina, Wafarsi, Wachina, Wagiriki na Waingereza. Hii ilisababishwa na karne za mchanganyiko wa mahitaji ya biashara yaliyofanywa na mabara ya Ulaya na Asia hapo Afrika. |
20231101.sw_1191_41 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Nchini Tanzania kuna lugha za kikabila zaidi ya mia moja na ishirini, kwa kuwa kila kabila lina lugha yake. |
20231101.sw_1191_42 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kiswahili ndiyo lugha ya taifa na inazidi kuwa lugha mama kwa watoto wengi, hasa mijini. Walau asilimia 90 za wakazi wanakitumia walau kama lugha ya pili. Kiswahili ni mojawapo kati ya lugha za Kibantu: hii imesaidia sana kukubaliwa kwa Kiswahili nchini, kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania ni wasemaji wa lugha za Kibantu. Kiswahili kinatumika kama lugha baina ya watu wa makabila mbalimbali na kwa mambo rasmi; kwa hiyo ni lugha rasmi ya dhati. |
20231101.sw_1191_43 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Baada ya uhuru, Kiingereza (iliyokuwa lugha ya kikoloni kabla ya uhuru) iliendelea kutumika kwa mambo kadhaa rasmi na kwa elimu kuanzia sekondari ingawa sera mpya inataka Kiswahili kishike nafasi yake hadi chuo kikuu; kwa hiyo ilichukuliwa kama lugha rasmi ya dhati pamoja na Kiswahili. Lakini utumizi rasmi wa Kiingereza umepungua katika milongo iliyopita, na sasa utumizi huu karibu umekwisha. Kwa hiyo siku hizi ni kawaida zaidi kuchukulia Kiswahili kama lugha rasmi ya dhati pekee. |
20231101.sw_1191_44 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Sera mpya ya elimu inakusudia kufanya Kiswahili kuwa lugha ya kufundishia katika ngazi zote kufikia mwaka 2024. |
20231101.sw_1191_45 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Nchi haina dini rasmi na katiba ya Tanzania inatangaza uhuru wa dini kwa wote. Mara nyingi idadi ya wafuasi wa dini hutajwa kuwa theluthi moja Waislamu, theluthi moja Wakristo na theluthi moja wafuasi wa dini za jadi. Lakini tangu uhuru swali la dini ya wananchi halijaulizwa tena katika sensa, kwa hiyo kadirio la theluthi-theluthi inawezekana ni zaidi azimio la kisiasa. |
20231101.sw_1191_46 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Usafiri nchini Tanzania ni hasa kwa njia ya barabara. Nyingine ni reli na ndege. Kwenye maziwa makubwa na pwani ya Bahari Hindi kuna pia usafiri wa meli. |
20231101.sw_1191_47 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Hadi sasa idadi ya barabara za lami si kubwa. Kuna hasa njia nzuri kati ya Dar es Salaam, Mbeya katika kusini-magharibi, Dodoma katika kitovu cha nchi, Arusha / Tanga katika kaskazini-mashariki. Kusini-Mashariki na Magharibi ya nchi kwa jumla haina barabara nzuri na mawasiliano ni magumu. |
20231101.sw_1191_48 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mashirika mawili ya reli yanayohudumia Tanzania: ni TRC (Shirika ya Reli Tanzania - Tanzania Railways Corporation) na TAZARA (Tanzania-Zambia Railways Corporation). TRC imetawala reli ya kati kuanzia Dar es Salaam hadi Kigoma halafu reli ya Tanga kati ya Tanga na Arusha. Tazara imeunganisha Dar es Salaam na kusini ya nchi hadi Zambia. Zote hazikutunzwa vizuri na usafiri unakumbwa na huduma mbaya pamoja na ajali. |
20231101.sw_1191_49 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Huduma kwa ndege zinatumia hasa viwanja vya ndege 11 vyenye barabara ya lami kwa ajili ya ndege, hasa Julius Nyerere/Dar es Salaam, Kilimanjaro/Arusha-Moshi na Zanzibar-Kisauni. Pia kuna viwanja vingine vya ndege kama vile uwanja wa ndege wa Mwanza, Bukoba na Kigoma. |
20231101.sw_1191_50 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Usafiri wa majini pia unafanyika hasa katika bahari ya Hindi, ingawa hakuna meli ya serikali hapo na mashirika binafsi hutoa huduma. Usafiri wa majini hufanyika pia katika maziwa ya Viktoria, Tanganyika na Nyasa. Miongoni mwa meli ni MV Bukoba iliyozama tarehe 21 Mei 1996 pamoja na abiria karibu 1,000 na MV Nyerere iliyozama tarehe 20 Septemba 2018 pamoja na abiria zaidi ya 200. |
20231101.sw_1191_51 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Katika ziwa Tanganyika ipo meli ya Mv Liemba ambayo ilianza kutumika tangia kipindi cha ukoloni wa Wajerumani: inatoa huduma kati ya miji ya mwambao wa ziwa Tanganyika na nchi jirani. |
20231101.sw_1191_52 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mwaka 2017 ulianza ujenzi wa awamu ya kwanza ya njia ya geji sanifu nchini Tanzania inayolenga kuunganisha Dar es Salaam na Morogoro. Njia hii inatarajiwa kuendelea hadi Mwanza na hatimaye hadi Burundi. |
20231101.sw_1191_53 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mahali pafuatapo katika Tanzania pamepokewa katika orodha ya UNESCO ya "Urithi wa Dunia" (mwaka wa kukubaliwa – jina la mahali) |
20231101.sw_1191_54 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kuna aina zaidi ya tano za muziki nchini Tanzania, kama zilivyofafanuliwa na BASATA ni pamoja na ngoma (ngoma za asili), dansi, kwaya (muziki wa injili), taarab, na bongo flava (pop/hip hop). ). Ngoma ni muziki wa dansi wa kitamaduni, ngoma hutofautiana kati ya kabila na kabila. Dansi ni muziki wa bendi unatokana na muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (au "rumba ya kikongo"). Taarab ni muziki wa Waafrika wa pwani uliopokea athira kutoka tamaduni nyingi, hasa muziki wa Waarabu na Wahindi. Kimsingi ni uimbaji wa mashairi unaofuata muziki wa bendi. Kwaya ni muziki ambao asili yake ni kanisani. Bongo flava ni muziki wa pop wa Tanzania uliozaliwa na muziki wa kizazi kipya, unajumuisha reggae, RnB, na hip hop, uliochanganywa na vionjo vya asili (flava) lakini tangu wakati huo umekua na kuwa muziki wa kipekee wa maeneo ya Maziwa Makuu. Asili mbalimbali za ushawishi zimesaidia kufanya bongo flava kuwa muziki maarufu zaidi Afrika Mashariki, na muziki mmojawapo kati ya ile maarufu zaidi katika bara la Afrika. |
20231101.sw_1191_55 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tangu kuundwa kwa Tanzania hadi 1993, kurekodi na usambazaji wote wa muziki ulisimamiwa kikamilifu na BASATA, hasa kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD). Ni aina 4 tu za muziki za Kitanzania zilizoruhusiwa kurekodiwa au kutangazwa, ambazo wakati huo zilikuwa ngoma, taarab, kwaya na dansi. Sheria ya Huduma za Utangazaji ya 1993 iliruhusu mitandao ya kibinafsi ya matangazo na studio za kurekodi. Haya ni mojawapo ya mabadiliko muhimu zaidi katika tasnia ya muziki ya Tanzania tangu kuanzishwa kwa nchi miaka 30 kabla. Miaka michache kabla ya Act ya 1993, muziki wa hip hop ulikuwa umeanza kuimarika katika miji ya Dar es Salaam, Mbeya, Arusha na Mwanza. Ilikuwa ikianza mageuzi kutoka kwenye hip hop ya Kiingereza huko Uzunguni, maeneo tajiri kama Oysterbay na Masaki pamoja na shule za kimataifa, hadi kizazi kipya Uswahilini, vitongoji maskini na kutumia Kiswahili. Mara tu baada ya kufunguliwa kwa mawimbi ya redio, bongo flava ilizaliwa ikienea kwa haraka kote nchini, na katika Maziwa Makuu. |
20231101.sw_1191_56 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Utamaduni wa kifasihi wa Tanzania kimsingi ni wa simulizi. Tanzu na vipera maaarufu vya fasihi simulizi ni pamoja na ngano, mashairi, mafumbo, methali na nyimbo. Sehemu kubwa zaidi ya fasihi simulizi iliyorekodiwa Tanzania ni ya Kiswahili, ingawa lugha za makabila ya Tanzania zina mapokeo yake ya simulizi. Fasihi simulizi ya nchi imekuwa ikipungua kwa sababu ya mabadiliko ya muundo wa jamii, na kufanya uwasilishaji wa fasihi simulizi kuwa mgumu zaidi, pia teknolojia za kisasa zinachangia kushushwa kwa thamani ya fasihi simulizi. |
20231101.sw_1191_57 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Utamaduni wa kuandika na kusoma vitabu umeenea nchini Tanzania. Fasihi andishi nyingi za Kitanzania ni za Kiswahili au Kiingereza. Watu mashuhuri katika fasihi andishi ya Tanzania ni pamoja na Shaaban Robert (anatambulika kama baba wa fasihi ya Kiswahili), Muhammed Saley Farsy, Faraji Katalambulla, Adam Shafi Adam, Muhammed Said Abdalla, Said Ahmed Mohammed Khamis, Mohamed Suleiman Mohamed, Euphrase Kezilahabi, Gabriel Ruhumbika, Ebrahim Hussein, May Materru Balisidya, Fadhy Mtanga, Abdulrazak Gurnah, na Penina O. Mlama. |
20231101.sw_1191_58 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mitindo miwili ya sanaa ya Tanzania imepata kutambuliwa kimataifa. . Uchoraji wa Tingatinga umejulikana tangu miaka ya 1970. Mtindo huo umepewa jina la mwanzilishi wake, mchoraji wa Kitanzania Edward Said Tingatinga. Kwa ujumla michoro ya Tingatinga inayoonyesha watu, wanyama, au maisha ya kila siku. |
20231101.sw_1191_59 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Baada ya kifo cha Tingatinga mwaka wa 1972, wasanii wengine walikubali na kuendeleza mtindo wake, na aina hiyo sasa ndiyo mtindo muhimu zaidi unaolenga utalii katika maeneo ya Afrika Mashariki.: |
20231101.sw_1191_60 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Uchongaji wa mabombwe ya Kimakonde yamesifiwa tangu mwanzo wa karne ya 20. Wamakonde wengi wamehamia Dar es salaam au Arusha wanapohudumia soko la watalii na soko la nje. |
20231101.sw_1191_61 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Mchezo maarufu nchini Tanzania ni mpira wa miguu. Ingawa mpira wa miguu (kandanda) unaongoza kwa ufuasi mkubwa miongoni mwa vijana, michezo mingine kama vile mpira wa kikapu, mchezo wa ngumi na riadha inazidi kuwa maarufu miongoni mwa watu. Baraza la Michezo la Taifa ndicho chombo kinachosimamia michezo nchini chini ya Wizara ya Habari, Vijana, Michezo na Utamaduni. |
20231101.sw_1191_62 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ni chombo kinachosimamia mpira wa miguu nchini. Vilabu maarufu vya soka la kulipwa jijini Dar es Salaam ni Young Africans F.C. na Simba S.C. Wachezaji wa kandanda ambao wamechezea klabu kubwa za kigeni ni pamoja na Mbwana Samatta, Kelvin John, na Morice Abraham. Tanzania iliandaa Kombe la Mataifa ya Afrika U-17 2019. |
20231101.sw_1191_63 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Soka la wanawake ni mchezo unaokuwa kwa kasi zaidi Tanzania. Utamaduni wa wanawake kucheza mpira wa miguu umeanza kueleweka kwa wengie. Timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania, Taifa Queens ni bingwa wa Michuano ya CECAFA kwa Wanawake kwa mwaka 2016 na mwaka 2018. Michuano hii huandaliwa na Shirikisho la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA). Timu ya taifa ya wanawake chini ya miaka 17 'Serengeti Girls' ilifuzu kucheza Michuano ya Kombe la Dunia la Wanawake nchini India mwaka 2022. |
20231101.sw_1191_64 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Hasheem Thabeet ni Mtanzania wa kwanza kucheza Ligi ya Mpira wa Kikapu ya Marekani (NBA).Mwanariadha wa zamani wa Tanzania wa mbio za kati, Filbert Bayi Sanka mwaka 1974 aliboresha rekodi ya mbio ya mita 1500, na mwaka wa 1975 aliboresha rekodi ya mbio ya maili moja. Bado anashikilia rekodi ya Michezo ya Jumuiya ya Madola ya mita 1500. |
20231101.sw_1191_65 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Tanzania ina tasnia maarufu ya filamu inayojulikana kwa jina la "Bongo Movie". Studio nyingi za utayarishaji filamu za Kitanzania ziko Dar es Salaam. |
20231101.sw_1191_66 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Tanzania | Tanzania | Kabla ya uhuru wa Tanzania mwaka 1961, baadhi ya sinema za kigeni zilirekodiwa Tanganyika na Zanzibar. Tamasha la Kimataifa la Filamu la Zanzibar huandaa maonyesho ya filamu, warsha, muziki pamoja na sanaa zingine za maigizo. |
20231101.sw_1201_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Uhindi (pia: India) ni nchi kubwa ya bara la Asia, upande wa kusini, ikienea hasa katika rasi kubwa ya Bahari ya Hindi. |
20231101.sw_1201_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kwa eneo ina nafasi ya saba duniani, lakini kwa idadi ya wakazi (1,352,642,280 mwaka 2018) ni nchi ya pili baada ya China. Kati ya nchi za kidemokrasia ndiyo yenye watu wengi zaidi duniani. Tena inakadiriwa kwamba miaka ya hivi karibuni itapiku China. |
20231101.sw_1201_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kiutawala Uhindi ni shirikisho la jamhuri lenye majimbo ya kujitawala 29 pamoja na maeneo ya shirikisho 7. |
20231101.sw_1201_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Binadamu walifika India kutoka Afrika kabla ya miaka 55,000 iliyopita. Uwepo wao wa muda mrefu, kwanza kama wawindaji-wakusanyaji waliozagaa barani, umefanya watu wa eneo hilo wawe na tofauti kubwa kati yao upande wa urithi wa kibiolojia, ambayo inapitwa na Waafrika tu. |
20231101.sw_1201_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Makazi ya kudumu yalianza magharibi, katika beseni la mto Indus, miaka 9,000 iliyopita, hata kuzaa ustaarabu maalumu (Indus Valley Civilisation) katika milenia ya 3 KK. |
20231101.sw_1201_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kufikia mwaka 1200 KK, Kisanskrit cha Kale, mojawapo kati ya lugha za Kihindi-Kiulaya, kilikuwa kimeenea India kutoka Kaskazini-Magharibi, kikawa lugha ya Rigveda, mwanzoni mwa dini ya Uhindu. Hivyo lugha za Kidravidi zikakoma kaskazini. |
20231101.sw_1201_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kufikia mwaka 400 KK, matabaka ya kudumu katika jamii yalikuwa yamejitokeza katika Uhindu. Hapo dini za Ubuddha na Ujaini zilitokea, zikipinga taratibu hizo za kibaguzi. Katika bonde la mto Gange yalianza madola ya Maurya na Gupta. Ndani yake hadhi ya wanawake ilirudi nyuma, na mtazamo wa kwamba baadhi ya watu hawatakiwi hata kuguswa ukaimarika. Huko India Kusini, Falme za Kati zilieneza maandishi na tamaduni vya lugha za Kidravidi kwa falme za Asia Kusini Mashariki. |
20231101.sw_1201_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kati karne za kwanza baada ya Kristo, dini za Ukristo, Uislamu, Uyahudi na Uzoroastro pia zilitia mizizi katika pwani za Kusini. |
20231101.sw_1201_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Majeshi kutoka Asia ya Kati yalivamia kwa kwikwi mabonde ya India, hata kuunda usultani wa Delhi na kuingiza India Kaskazini katika umma wa Kiislamu. |
20231101.sw_1201_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Katika karne ya 15 BK, Dola la Vijayanagara liliunda utamaduni wa kudumu wa Kihindu kusini mwa India. Katika Punjab, Usikh ulianzishwa, ukipinga dini rasmi. |
20231101.sw_1201_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Dola la Mughal, mwaka 1526, liliwezesha karne mbili za amani na kuacha urithi wa usanifu majengo bora. |
20231101.sw_1201_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Uhindi wa Kiingereza ni kipindi cha historia ambapo nchi za Bara Hindi ama zilitawaliwa na Uingereza moja kwa moja ama zilikuwa chini ya usimamizi wa Uingereza kama nchi lindwa. |
20231101.sw_1201_12 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Utawala huo ulienea juu ya Uhindi wa leo pamoja na Pakistan, Bangladesh, Nepal na kwa muda pia juu ya Burma (Myanmar). |
20231101.sw_1201_13 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Tarehe 31 Desemba 1600 malkia Elizabeth I alitoa hati ya ulinzi wa kifalme kwa biashara kati ya Uingereza na "Uhindi wa Mashariki". |
20231101.sw_1201_14 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kampuni iliyopokea hati hii ilikuwa kundi la wafanyabiashara na matajiri wa London waliovutwa na utajiri wa nchi za mashariki na hasa na faida kubwa mikononi mwa wafanyabiashara Wareno na Waholanzi waliotangulia katika biashara kati ya Ulaya na nchi za Asia ya Kusini. |
20231101.sw_1201_15 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kampuni ilishindana kibiashara na kivita na wafanyabiashara wa Ureno, wa Uholanzi na wa Ufaransa. Iliweza kununua au kuvamia vituo vya biashara na kujenga maboma yake kuanzia mwaka 1644 huko Bombay, Madras na penginepo. |
20231101.sw_1201_16 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Mwaka 1717 kampuni ilipata kibali cha mtawala wa Moghul cha kusamehewa kodi kwa biashara katika Ubengali. |
20231101.sw_1201_17 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Tangu mwaka 1680 kampuni ilianzisha jeshi lake la maaskari Wahindi na kuwa mshiriki katika siasa ya Uhindi. |
20231101.sw_1201_18 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kati ya miaka 1756 na 1763 Uingereza pamoja na mataifa mengine ya Ulaya ilishiriki katika Vita vya miaka saba viliyokuwa vita vya kwanza vya kimabara. Waingereza walipigana pamoja na Prussia dhidi ya Austria, Ufaransa, Urusi na Uswidi. Jeshi la kampuni liliendesha vita hivyo dhidi ya maeneo ya Ufaransa katika Uhindi. Wafaransa walishindwa wakabaki na vituo vidogo tu katika miji kama Pondicherry na Mahe lakini kampuni iliongeza maeneo yake katika Uhindi. |
20231101.sw_1201_19 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Baada ya mwaka 1757 Kampuni ya Kiingereza ilikuwa enzi muhimu, iliweza kushindana hata na nguvu ya Moghul. Ilianza kutawala sehemu kubwa za Uhindi wa Kusini pamoja na Ubengali. |
20231101.sw_1201_20 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | mikataba na madola ya watawala wa Kihindi waliokubali kupokea mabalozi wa kampuni kwao waliokuwa kama washauri wakuu wa Maharaja au Nawab wa eneo; siasa ya nje na mambo ya jeshi ziliwekwa chini ya kampuni |
20231101.sw_1201_21 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Mafaniko makubwa ya kampuni yalisababisha mgogoro huko Uingereza na sheria mbalimbali za bunge la Uingereza zililenga kuongeza athira ya serikali ya Uingereza juu ya shughuli za kampuni. |
20231101.sw_1201_22 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Katika karne ya 19 kampuni ikawa mtawala wa sehemu kubwa za Uhindi, ama kwa njia ya mikataba na watawala wa kienyeji au kwa utawala wa moja kwa moja. Kampuni ilianza kubadilisha uso wa India kujenga reli na kuanzisha mawasiliano wa kisiasa kwa huduma ya posta na pia simu za telegrafi. |
20231101.sw_1201_23 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Mwaka 1857 ilitokea uasi wa wanajeshi Wahindi wa jeshi la kampuni uliosababisha na mkasi wa mabadiliko na dharau ya viongozi Waingereza kwa utamaduni wa wenyeji. Utawala wa kampuni ulianza kuporomoka; uliokolewa tu kwa kupeleka Uhindi wanajeshi kutoka Uingereza. Uasi ulikomeshwa kwa mabavu. |
20231101.sw_1201_24 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Lakini kuingilia kati kwa serikali ya Uingereza kulikuwa mwisho wa utawala wa kampuni. Mwaka 1858 serikali ya London ilichukua madaraka yote ya kampuni ikafanya Uhindi kuwa koloni la taji la Uingereza. |
20231101.sw_1201_25 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Kuanzia mwaka 1858 Uhindi ulitawaliwa kama koloni la Uingereza. Kaisari wa mwisho wa Moghul Bahadur Shah Zafar II aliondolewa nchini. Malkia Viktoria wa Uingereza alichukua cheo chake akaitwa "Kaisari wa Uhindi" (kwa Kiingereza: "Empress of India"; kwa Kihindi: "Padishah-e-Hind") akamuachia utawala gavana wake aliyepewa cheo cha "makamu wa mfalme" (Vice-Roy). |
20231101.sw_1201_26 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Muundo wa utawala uliendelea: maeneo ya kampuni yalikuwa makoloni ya Uingereza. Maeneo ya watawala Wahindi yalibaki yalivyo lakini kila Maharaja au Nawab alipaswa kula kiapo cha utii kwa malkia kama Kaisari au malkia mkuu wa Uhindi na kumkubali mshauri Mwingereza katika jumba lake kama mwakilishi wa Uingereza. |
20231101.sw_1201_27 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Mwisho wa karne ya 19 harakati za kutafuta uhuru zilianza upya. Mwaka 1885 chama cha INC (Indian National Congress) kiliundwa na Wahindu na Waislamu pamoja waliodai uhuru. Mwaka 1906 viongozi Waislamu walitoka katika INC na kuunda "Shirikisho la Waislamu". |
20231101.sw_1201_28 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Mwaka 1917 Uingereza ulitamka ya kwamba ulitaka kuelekea polepole hali ya kujitawala kwa Wahindi. Viongozi wa wenyeji hawakuridhika na mkasi wa mabadiliko. Chini ya uongozi wa Mahatma Ghandi mwendo wa kupigania uhuru bila mabavu ulipata nguvu. Ghandi alipigania hasa umoja wa Wahindu na Waislamu lakini alipingwa na viongozi wenye itikadi kali wa pande zote mbili. |
20231101.sw_1201_29 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia Waingereza walikubali kujiondoa katika Uhindi. Swali kubwa lilikuwa kama nchi itabaki kama nchi moja au kama maeneo ya Waislamu yatajitenga. |
20231101.sw_1201_30 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Tarehe 14/15 Agosti 1947 utawala wa Uingereza ulikwisha. Bara Hindi iligawanywa katika nchi mbili za Uhindi na Pakistan. Mgawanyo ulikuja na vita na kumwaga kwa damu nyingi. |
20231101.sw_1201_31 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Tarehe 30 Januari 1948 Ghandi mwenyewe aliuawa na Hindu mkali aliyemchukia kwa sababu alitaka usawa wa Waislamu na Wahindu. |
20231101.sw_1201_32 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Lugha ya taifa ni Kihindi, ambacho ni lugha ya Kihindi-Kiulaya, pamoja na Kiingereza ambacho pia ni lugha rasmi. Kuna lugha 21 kubwa na lugha nyingi zisizo na wasemaji wengi sana. |
20231101.sw_1201_33 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Lugha ndogo chache ambazo si lugha za Kihindi-Kiulaya (74 %) wala za Kidravidi (24 %) ni lugha za Kisino-Tibeti, lugha za Kiaustro-Asiatiki na lugha za Kitai-Kadai. Visiwani mwa Andaman, kulikuwa na lugha za Kiandamani lakini nyingi zao zimeshatoweka kabisa. |
20231101.sw_1201_34 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Wakazi walio wengi (79.8 %) hufuata dini ya Uhindu. Takriban 14.2 % ni Waislamu; hivyo Waislamu wa Uhindi ni jumuiya ya tatu katika umma wa Kiislamu duniani baada ya Waislamu wa Indonesia na Pakistan. |
20231101.sw_1201_35 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Uhindi | Uhindi | Dini nyingine ni Ukristo (2.3 %), Usikh (1,7 %), Ubuddha (0.7 %), Ujain (0.4 %), Uzoroastro na Bahai. |
20231101.sw_1203_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Afrika ya Mashariki ni sehemu ya bara la Afrika ambayo iko upande wa mashariki, ikipakana na Bahari ya Kihindi. |
20231101.sw_1203_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Mayotte na Réunion, zilizokuwa makoloni na sasa ni mikoa ya Ufaransa, zinahesabiwa pia katika orodha hii. |
20231101.sw_1203_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Malawi, Zambia na Zimbabwe wakati mwingine zinehesabiwa kuwa sehemu ya Afrika ya Kusini (zamani zilikuwa pamoja kama Rhodesia ya Kusini, Rhodesia ya Kaskazini na Unyasa katika Shirikisho la Afrika ya Kati) |
20231101.sw_1203_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Komori, Morisi, Shelisheli, Mayotte na Réunion ni visiwa vidogo vya Bahari Hindi vinavyohesabiwa kuwa sehemu za Afrika ya Mashariki. |
20231101.sw_1203_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Majina ya miji ya Afrika ya Mashariki imetajwa mara ya kwanza katika Periplus ya Bahari ya Eritrea (karne ya 1 B.K.). |
20231101.sw_1203_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Tangu uenezaji wa ukoloni wa Kizungu upande wa Mashariki wa bara ulianza kuitwa Afrika ya Mashariki. Somalia, Eritrea na Ethiopia za leo zilitawaliwa na Italia kama "Afrika ya Mashariki ya Kiitalia" (Africa Orientale Italiana) katika miaka ya 1936 hadi 1941, Kenya ilitwaliwa na Uingereza kwa jina la "Afrika ya Mashariki ya Kiingereza" (East Africa Protectorate au pia British East Africa) hadi 1920, Tanganyika pamoja na Rwanda na Burundi zilijulikana kama "Afrika ya Mashariki ya Kijerumani" (Deutsch Ostafrika) hadi 1919 na Msumbiji iliitwa mara nyingi "Afrika ya Mashariki ya Kireno" (África Oriental Portuguesa) hadi uhuru. |
20231101.sw_1203_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Wakazi wengi wa Afrika ya Mashariki ni wasemaji wa lugha za Kibantu; sehemu ya kaskazini wasemaji wa lugha za Kihamiti ni wengi (Waoromo, Wasomalia). Katika Ethiopia kuna wasemaji wengi wa lugha za Kisemiti. Pia kuna wasemaji wa lugha za Kiniloti na lugha za Khoisan. |
20231101.sw_1203_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Nchi mashuhuri zaidi katika sehemu hii ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda na Burundi kwa sababu ya kutumia lugha moja katika mawasiliano baina ya wananchi wa sehemu hii, yaani Kiswahili. |
20231101.sw_1203_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Aghalabu nchi za Afrika ya Mashariki zinazungumza lugha ya Kiswahili kama lugha ya mawasiliano kati yao, kwani katika nchi hizi kuna makabila mengi sana na kila kabila lina lugha yake ambayo kawaida inatumika nyumbani baina ya watu wa kabila moja, lakini wakitaka kuwasiliana na makabila mengine, mara nyingi hutumia lugha ya Kiswahili, na hii ni kwa sababu lugha hii ndiyo iliyoenea zaidi na kufahamika zaidi katika eneo hili la dunia. |
20231101.sw_1203_9 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Nchi za Afrika ya Mashariki, hasa Kenya, Uganda na Tanzania ni nchi ambazo ni karibu tangu zamani. Zimeshirikiana historia, zote zimekaliwa hasa na makabila yanayotumia lugha za Kibantu (Kenya na Uganda wana pia idadi muhimu ya wakazi wasiotumia lugha za Wabantu). Katika nchi zote tatu lugha ya Kiswahili imekuwa lugha muhimu ingawa kwa daraja mbalimbali. Wakati wa ukoloni zilitawaliwa na Uingereza iliyoacha taasisi na taratibu mbalimbali zilizosaidia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki wakati wa uhuru. |
20231101.sw_1203_10 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Tanzania, Kenya na Uganda zina ukubwa wa eneo la maili za mraba; Tanzania 360,000 ikifuatiwa na Kenya 224,960 na Uganda 93,980 upande wa mashariki nchi hizi zimepakana na bahari ya Hindi na upande wa kaskazini mashariki zimepakana na Somalia, upande wa kaskazini zimepakana na Ethiopia na Sudan Kusini upande wa magharibi ni Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na jamuhuri ya Rwanda na Burundi, kusini ni Zambia, Malawi na Msumbiji. |
20231101.sw_1203_11 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Afrika%20ya%20Mashariki | Afrika ya Mashariki | Nchi hizi zimepitiwa na mstari wa ikweta, umepita Kenya na kusini mwa Uganda. Kenya na Tanzania zina ukanda wa pwani wenye bandari za Mombasa; Tanga; Bagamoyo; Dar es Salaam; Zanzibar; Kilwa na Mtwara. |
20231101.sw_1204_0 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Simu (kutoka Kiarabu سیم, sim, inayomaanisha "waya") ni chombo cha mawasilianoanga kinachotumia umeme. |
20231101.sw_1204_1 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Awali simu ilihitaji iunganishwe na nyaya, lakini leo hii inaweza kutumia redio. Hiyo inaitwa nyayatupu, siwaya au simu bila waya. |
20231101.sw_1204_2 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Watu wengi wanaamini kuwa simu iligunduliwa mnamo 1876 na Alexander Graham Bell, Mskoti mwenye umri wa miaka 29 aliyeishi nchini Marekani. Lakini Mwitalia Antonio Meucci alianzisha matumizi ya simu toka mwaka wa 1871 hukohuko Marekani. |
20231101.sw_1204_3 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Tangu mwishoni mwa karne ya 20 kuna aina mpya ya simu iliyoenea ambayo ni simu ya mkononi. Ingawa haistahili kweli kuitwa tena "simu" kwa maana asilia kwa sababu hakuna simu, ni aina ya mtambo wa mawasiliano uliosambaa haraka sana. |
20231101.sw_1204_4 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Katika nchi nyingi za Afrika simu hizi zina faida ya pekee kwa sababu zinaruhusu mawasiliano hata pale ambako nyaya za Posta hazifiki. |
20231101.sw_1204_5 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Kila simu inapaswa kuwa na namba ya pekee ikiunganishwa katika mtandao wa simu. Isipokuwa ofisi au kampuni inaweza kuwa na namba moja kwa simu zake zote halafu maungio ya simu ya ndani ambako ama mtu au mtambo unaunganisha simu za ndani na mtandao wa nje. |
20231101.sw_1204_6 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Kwa kawaida mtandao wa simu ndani ya nchi inagawiwa kwa maeneo. Maeneo haya yanaweza kugawiwa tena hadi ngazi ya mtandao wa mahali. Kila eneo linafikiwa kupitia namba ya eneo; ndani ya eneo inatosha kutumia namba ya simu yenyewe. |
20231101.sw_1204_7 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Mfano: simu ya namba 556677 iko mjini Dar es Salaam. Namba ya eneo la Dar es Salaam ni 022. Kufikia simu hii ndani ya eneo la Dar es Salaam inatosha kupiga 556677. Mtu anayetaka kuipigia kutoka Dodoma au Arusha anatangulia namba ya eneo na kupiga 022-556677. |
20231101.sw_1204_8 | https://sw.wikipedia.org/wiki/Simu | Simu | Simu za mkononi huunganishwa katika mtandao mkubwa wa kitaifa kufuatana na kampuni inayotoa huduma kama vile Airtel, TIGO au TTC yenye mtandao wake wa pekee. Kwa teknolojia bila waya hakuna haja ya ugawaji wa kieneo. Lakini kwenye simu hizi ni lazima kutumia pia namba ya mtandao muda wote. Kwa kupiga simu ya kawaida kutoka simu ya mkononi ni lazima kutumia muda wote namba ya kieneo hata kama mwenye kupiga yuko mji uleule maana mitandao ni tofauti. |